Safari ya Rais Samia Suluhu Hassan Jijini New York ni ya muhimu kiuchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
KWANINI SAFARI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NEW YORK NI YA MUHIMU KIUCHUMI.

BILA shaka aliposema “Ili ufike haraka nenda peke yako, ili ufike mbali nenda na wenzako,” alimaanisha. Rais Samia ameanza safari kuelekea New York Marekani kuhudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na baadae kuhudhuria mikutano ya kujadili mabadiliko ya tabia ya nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Safari hii ni muhimu sana kwa sababu masuala yote yanayojadiliwa yana umuhimu wa kipekee kwetu kama taifa, tunaathirika kwa namna chanya na hasi na masuala hayo, kama sehehmu ya dunia ni muhimu sisi pia kuwa sehemu ya mchakato wa majadiliano wa namna ya kukabiliana na changamoto hizo au kutumia fursa zinazopatikana kutokana na maazimio ya utekelezaji wa mipango inayotokana na majadiliano yanayohusu masuala hayo.


Tangu uhuru Tanzania imekuwa na nafasi ya kipekee katika diplomasi ya kimataifa, misingi imara ya msimamo wa taifa letu iliyowekwa na waasisi wetu wakiogozwa na mwanadiplomasia namba moja Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere iliipa Tanzania heshima kubwa katika masuala ya utetezi wa haki na kupinga uonevu wa aina zote popote duniani, umoja kama ule wa nchi zisizofungamana na upande wowote, kuwa mwenyekiti na makao makuu ya Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika na msimamo dhidi udhalimu duniani ulijenga heshima kubwa wa Tanzania kimataifa.
Wakati huu Taifa linapombana kujikomboa kiuchumi na kuwa na uchumi mkubwa na imara, ni nafasi ya kujenga juu ya msingi hiyo ili kuimarisha diplomasia ya kimataifa.

Ukweli ulio bayana ni kwamba huwezi ukajenga uchumi imara bila kushirikiana na wenzako duniani, mifumo ya dunia ya sasa ilivyoumbwa hata kama ina viashiria vya mataifa makubwa kuwanyonya wadogo, namna nzuri ya kuepuka ukandamizaji huo siyo kujitenga, isipokuwa ni kujifunza kuogelea kwenye mto wenye mamba. Na ndivyo tulivyofanya awali hasa wakati wa vita baridi, tuliweza kusimama katikati na kuwa na marafiki pande zote za mvutano huo mkubwa wa dunia.

Ziara ya Rais Samia katika Umoja wa Mataifa na nyingine zinazofuata ni sehemu muhimu sana ya harakati za ujenzi wa haiba ya Tanzania katika uga wa kimataifa na kwa namna hiyo anaongeza matofali zaidi juu ya msingi wa diplomaisia ya Tanzania, ili kulipa taifa heshima na hadhi inayostahili kimataifa.

Kama tunataka kuwa sehemu muhimu ya dunia na sisi kuweza kupenyeza ajenda zetu, ni lazima na muhimu sana kiti cha Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa kikaliwe na kiongozi mkuu wa nchi katika matukio muhimu na mikutano mikubwa kama huu wa Septemba.

Tanzania kimataifa
Diplomasia ya Uchumi

IMG-20210920-WA0155.jpg
 
Safari yoyote wa Kiongozi inakuwa na manufaa kama Safari hio itatumiwa kufanya kile kinachotakiwa...

Moja sio kwenda na watu lukuki ambao wanakwenda shopping na sio kufanya kazi iliyowapeleka (in this day and age mengine yanaweza kufanyika through technology) wachache decision makers ndio wanakwenda...

Mbili kuna kusafiri kikazi na kuna kusafiri kiutalii (inategemea kama watakwenda kikazi kweli na sio kutalii kwa jina la kwamba wapo kazini)
 
Stephano mdenganyi kwa haraka haraka baada ya kusoma kichwa cha habari, nikasoma jina la mleta uzi wwaa kumpamba bi mkubwa, badala ya stephano mdenganyi ikaja STEFANO MDANGAJI,

Samehe macho yangu mkuu
 
Back
Top Bottom