Hapa nazungumzia wale ambao hawali nyama kiimani na si wale ambao hawali kwasababu za kiafya tofauti na ukristo na uislam, dini kama buddhism, krishna nk wanaamini sana katika karma ya kila kiumbe na uwepo wake katika uso wa dunia, kwamba bata, mbuzi, samaki, punda na chochote chenye uhai kuna sababu maalum ya kuwa hivyo kilivyo.
Kwahiyo huwezi kutoa uhai wake kwa ajili ya shibe yako, utakuwa unajitengenezea karma mbaya, yani leo ukimuu mnyama ukala nyama yake next reincarnation yeye atazaliwa binadamu na wewe mnyama halafu atatenda kama wewe ulivyotenda imani hii imezama mno mioyoni mwao kiasi kwamba ni ngumu mno kuwakuta wanakula nyama. Kuna mazingira ambayo yanaweza kuwafanya wale nyama nayo ni
1.hawakushuhudia mnyama akichinjwa/akiuliwa
2. Hakuchinjwa kwa ajili yao
3. Isiwe ni nyama kwa ajili ya biashara, hapo anaweza kula na karma isimdhuru kila imani ina uchizi wake, kuna mavegetarian ambao kwa compassion kwa viumbe hufagia kabla ya kukanyaga ili wasiwadhuru viumbe
Mimi ni Vijitari (miaka takriban 20 sasa), ila ninakula maziwa na mayai.
Kutokula miili ya viumbe wenye nasibu ya damu yaweza kufanyika ni jambo na hali ya kawaida kulingana na 'ukomavu' wa kiroho wa mtu.
Kwa mfano mimi hupenda kupima chochote ninachotaka kukila ikiwa tumbo langu linaona kufaa ama laa; siku zote tumbo langu huniambia hapana halihitaji kwa vitu kama nyama... Nidhamu ya kushirikisha tumbo kwangu ndiyo yenye manufaa. Haikunichukua miye muda kuzoea kutokula nyama n.k -- unaweza kusema miongoni mwetu, maisha ya kutokula nyama huwenda tumetoka nayo mahala; kama wewe unakubaliana na nadharia ya kurudia upya mwili, utwaaji upya mwili basi katika hili unaloshauri kufuatilia kweli yake.
Ndiyo, kutokula nyama kuna maana hasa ikiwa maisha na nidhamu ya namna hii yafungamana na nadhiri za kiimani.
Unaweza kuleta mashauri mengi juu ya huruma na mapenzi kwa uhai lakini haya ni sehemu ya ukweli wa jambo lenyewe zima. Hata mashauri ya kiafya -- waweza kufungamanisha afya bora ya mwili na akili kwa nidhamu ya mtu asiyeishi kwa kula vinavyodhuriwa ila ukweli hasa wa jambo lenyewe usiwe ni kwa ajili ya 'mazuri' yake...
Ndiyo, usafi wa dhamira na nia unahusika katika kudumisha nidhamu ya kutokula viumbe hai wengine wenye namna ya karibu ya akili, damu, hisia na hamu ya kuishi na kustawi kama wewe mwenyewe ulivyo.
Na basi, katika mawaidha na mashauri ya waliofika wongofu, uvijitari huwa ni njia na mwongozo kwa mtu anayetamania ama mwenye kuwa na hamu ya kutaamulika -- kupata wongofu--japo kama Buddha inavyotaarifika kupata kusema : wongofu hautamaniwi bali 'Njia ya Kati' inaweza kufuatwa ili kuja kumfikisha yeye katika wongofu.
Kwa hiyo kuishi kama vijitari ni jambo moja miongoni mwa mwengine yanayofanya 'Njia ya Kati'... Haya husaidia kumtakasa mtu na kumweka yeye katika hali ya kuweza mwepesi 'kukumbuka' neema na rehema za uzima wote. Kwa mfano, kulingana na mafundisho ya Buddha, kiini cha ukweli wa maisha ya mtu masumbuko -- kutokana na mtu mwenyewe kufangamana mno na mambo ya ulimwengu na hata kusahau asili ya Kibuddha ndani yake... Kufanyika Buddha ni kuurudia wongofu wa nuru ya uzima wako... Na ndiyo maana Buddha aliianza msingi wa mafundisho yake kuelekeza kuhusu Unne wa Ukweli Bora -- maisha yote ni masumbuko.... kuishia kwenye mwongozo wa Gurudumu la Dhamma -- alama ya mwanzo ya ubuddha yenye kuwasilishwa kwa wafuasi wa Ubuddha kama gurudumu lenye midenge minane, Dhamma Chakra...
Safari ya mtu kuelekea kwenye wongofu husonga kwa gurudumu la dhamma -- kuifuatisha njia ya Buddha (Dhammapada). Uvijitari ni sehemu ya kutekeleza kusudi na mapenzi ya 'Njia ya Kati' ya Buddha kama mwalimu na Mkuu kwa kusudio la kiimani.
Hufundishwa matatu kuhusu 'Umbile' la Buddha -- hulka na mwonekano... Kwamba kweli ya Buddha ni mbegu ndani ya namna tatu za mwili katika moja (1) Mwili Dharma (Dharma kaya) (2) Mwili Sambogha (Sambhoga kaya) (3) Mwili Nirmana (Nirmana Kaya) ... Haya matatu yanahusika sifa na hulka zake kwa yeyote mwenye kukomaa katika njia ya kati ya Buddha... Na haya ndiyo hasa hufutika ndani yake (i) huruma/upendo/utumikishi wa kweli, (ii) Sababu na hali za madhahiriko yote, kwamba kila kitu kina namna ya kuingiliana ama kufungamana na kingine na (iii) Nuru yenye kufunua yote--yenye kuwezesha kufunua ukweli wa yote... Na basi wongofu una msingi wa haya matatu kukamilika katika mtu na basi mtu huyo kuwa 'Kataamulika' na mwenye wongofu...
Kwa hiyo ni sehemu ya Nirmana Kaya inayofanya Ma-buddha kuhubiri wongofu; ni sehemu ya Sambhoga kaya inayowafanya Ma-Buddha na wafuasi wa Buddha kuhubiri injili ya kuepuka kudhuru kiumbe kingine kwa kuwa ukosefu wa nuru sahihi ndani yako wakufanya kipofu wa matendo yako na hatima yake kutoka hali moja hadi ingine; ni sehemu ya Dharma Kaya ndiyo inayosukuma Ma-Buddha kufundisha kuhusu matendo ya kujali -- kwamba hatma ya kimoja yaweza kuwa ndani ya kingine, mpango mmoja kuwa ndani ya mwingine -- basi ni vema kuwa na rehema, kuepuka dhulma na machukizo mengine ili kufanya wepesi wa wewe mwenyewe nyote yako kujibayanisha miongoni mwa mengine yote kuchukua nafasi na kudumu na kupita katika ulimwengu wa maumbo na viumbe.
Dharma ni namna ingine ya asili ya kile ambacho Yesu alikuja alifundisha kuhusu 'Kristu' na 'Njia Nyembamba' ya kwenda uzimani. Kanuni ya matendo na dhamira safi kuhusu kutendea mwingine kama ambavyo wewe ungependa kutendewa ni usanisi wa yote mawili Dharma kaya na Sambhoga kaya. Yesu kufundisha kuhusu Nuru ya Milele ni muktadha wa Nirmana Kaya... Lakini Yesu ni Mtekinokrasia, Ni Mkuu aliyependa kufundisha hasa juu ya 'Neema' ya kuitumia Dharma na Kheri zake; na ndiyo maana alifundisha zaidi kuhusu 'Ufalme wa Mbingu', Nuru na Chumvi... Buddha ni Mmeritokrasia, yeye Dharma ni hali moja, Nuru yafunua hata hatma ya Dharma yenyewe -- hakuna cha zaidi ila Utupu, kuwa huru kabisa na hata yote yaliyo ndani ya wakati...
Na ndivyo Basi, wakati kwa Yesu, vitu kama mtu, nafsi na Mungu hutajwa ila kwa Buddha hakuna nafsi -- hakuna Mungu...
Ila mwenye hekima kwake yawa bayana : 'Njia ya Kati' ya Buddha yanasibu kweli ya namna ingine ya mtu kuutafuta ukweli wa ufalme wa Mungu na haki yake yote -- na mengine kuja kuzidishiwa katika mtu. Kutamani wongofu ni kosa la kiufundi kama vile mtu kudhani kujua ya ulimwengu dhahiri peke yake yatamkirimu yeye fahari na faraja...
Kujua ya Yesu vizuri na ya Buddha vizuri yanaweza kumuongoza Mfuasi kung'amua siri na mafumbo ya uzima katika kile Mafundisho ya Buddha hutajwa kama mashauri ya Sambhoga Kaya... Kuishi ndani ya wakati na kutoka nje yake. Kutawala mambo ya sasa, mbele na nyuma ya wakati na hata kupitilizia mbali hayo yote.