Kwenye somo la biology tumefundishwa kwamba mimea nayo ni viumbe hai,isipokuwa mawe sio hai,labda sasa tugeukie kula udongo na mawe,ili tusije tukaviua viumbe vyenzetu
ni mimea sio viumbe uhai wao na wetu una tofauti kubwa sana..!
Hata mimea Ina haki ya kuishi kwani ndio inayotupatia hewa ya oxygen, wasile kitu chochote wanywe maji tu.
Mimi pia ni mmoja katika ya watu ambao hawali nyama. Mwanzoni nilifanya kutokana na Imani Yangu, lakini kwa sasa naona umuhimu na faida yake hata kwa nje ya Imani.
Mi huwa naona hata mimea kuiua ni dhambi fulani hivi.
Yani inatia huruma unakuta maboga yameshanua yenyewe wewe unakata.
Ila ni imani nzuri . Mi naipenda ya kutoua wanyawa na wadudu na ndege pia. Kuna siku nilishuhudia ngombe akichinjwa nikisikia vibaya sana
Hapa nazungumzia wale ambao hawali nyama kiimani na si wale ambao hawali kwasababu za kiafya tofauti na ukristo na uislam, dini kama buddhism, krishna nk wanaamini sana katika karma ya kila kiumbe na uwepo wake katika uso wa dunia, kwamba bata, mbuzi, samaki, punda na chochote chenye uhai kuna sababu maalum ya kuwa hivyo kilivyo.kwahiyo huwezi kutoa uhai wake kwa ajili ya shibe yako, utakuwa unajitengenezea karma mbaya, yani leo ukimuu mnyama ukala nyama yake next reincarnation yeye atazaliwa binadamu na wewe mnyama halafu atatenda kama wewe ulivyotenda imani hii imezama mno mioyoni mwao kiasi kwamba ni ngumu mno kuwakuta wanakula nyama. Kuna mazingira ambayo yanaweza kuwafanya wale nyama nayo ni 1.hawakushuhudia mnyama akichinjwa/akiuliwa 2. Hakuchinjwa kwa ajili yao 3. Isiwe ni nyama kwa ajili ya biashara, hapo anaweza kula na karma isimdhuru kila imani ina uchizi wake, kuna mavegetarian ambao kwa compassion kwa viumbe hufagia kabla ya kukanyaga ili wasiwadhuru viumbe
hii imani inaenda mbali zaidi kwakuwa hata dawa za kuulia wadudu wao hawatumii kabisa, na kama wakiitumi wanatumia ile tu ya kulewesha na si kuondoa uhai, kwa vegetarians kuuwa kiumbe ni dhambi kubwa kuliko zote na karma yake ni mbaya sana