Hali ya upatikanaji wali na nyama shule niliyosoma

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,626
46,270
Katika shule ya sekondari ya Advance niliyosima tulikuwa tunakula wali mara mbili tu kwa wiki, Jumatano mchana na Jumapili mchana. Nyama pia tulikuwa tunakula mara mbili tu kwa siku. Siku nyingine zote ilikuwa ugali na maharage. Asubuhi tulikuwa tunakunywa uji mweupe na sukari tu, sina uhakika kama unga wa uji na ugali ulikuwea umeongezewa virutubisho.

Siku wali au nyama vikipikwa kulikuwa na msongamano na purukushani kubwa sana maeneo ya jikoni na dining, haikuwa rahisi kupata ubwabwa au nyama. Hata mabishoo ambao walikuwa hawali chakula cha shule huwezi kuwakosa maeneo ya jikoni siko hizo za ubwabwa na nyama.

Kuna wanafunzi wengi walikuwa wanakosa ubwabwa kwa sababu umepikiwa kidogo au watu wamerudia na kuficha wali mwingine au nyama wale usiku, wanaochelewa au kukosa walikuwa wanaishia kupewa ugali wa jioni na wengine siku ya nyama walikuwa wanakosa nyama na kuishia kupewa mchuzi wa nyama na maharage.

Kwa upande wa nyama mara nyingi ilikuwa ni ukiwahi unapata vipande viwili vidogo tu kipande kimoja, na pia inaweza kuwa bahati yako mbaya ukaangukia kupata mfupa.

Siku ya ubwabwa au nyama vipindi vya masomo kuelekea chakula cha mchana au baada ya chakula cha mchana vilikuwa vinavurigika sana.

Ninapoona watu wanafanya mzaha na kusagia kunguni mchele wa Wamarekani tena ambao umeongezwa virutubisho kwa ajili ya watoto wa shule ili uondolewe wasile mashuleni au washindie suti ya ugali maharage tu natamani kuwachapa hata makofi, hawa ni watu wasiojua chochote kuhusu maisha ya wanafunzi kutoka familia masikini, wanahitaji kupuuzwa.
 
Waafrika tuna upumbavu wa milele, tumeshindwa kulisha watoto mashuleni na bado misaada hatutaki!
Kulisha watoto vyakula vibovu sio sifa!
 
Advance shuleni wali ilikua Kila siku jioni, ugali beans Kila siku mchana
 
Back
Top Bottom