toroka uje mjini
JF-Expert Member
- Mar 29, 2017
- 1,584
- 2,116
Wewe usiige tu..wahenga walishasema ukijichamba saana mwishoe utakamata NNYAAAA,,Mimi pia ni mmoja katika ya watu ambao hawali nyama. Mwanzoni nilifanya kutokana na Imani Yangu, lakini kwa sasa naona umuhimu na faida yake hata kwa nje ya Imani.
Sio tu Buddhism, Hinduism, Rastafaris, Ethiopian Monks, Nazarenes(Jews), na ancient Egyptians hata ukristu kuna makundi yasiyokula nyama hasa ukristu wa kale ulielewa umuhimu wa vegetarianism.
Kihistoria, imani za kale zilianza kuuliza kwanini sisi wanadamu tupo hapa duniani? Nini kinachotutofautisha na wanyama na mimea? Hivyo watu waliokuwa ENLIGHTENED kama Krishna, Buddha, Waisraeli wa kale, waliona umuhimu wa kuishi kwa Amani. Sio kuishi tu kwa amani na mwanadamu mwenzako bali kwa viumbe vyote. Haina haja ya kumpiga mnyama bila sababu na baadaye wakaona hata kumpiga mnyama haitoshi, ili kuwa na amani na kuweza kuboost Third Eye, Karma, na kubalance Chakras zako, Ishi kwa kutoua mnyama kabisa. Kila kiumbe kina haki ya kuishi. Mimea ndio source ya kwanza ya chakula then Nyama ni Secondary source. Haina haja ya kumchinja mnyama na kumla wakati kuna vyakula vingi haviitaji kuua kiumbe. Tunapaswa kuishi kwa kuheshimu all aspects of life duniani. Kuna sababu nao wakaishi hivyo yanini niwaue, nao husikia maumivu, wanyama wanahisia ambazo hata sisi tunazo mfano upendo, huhisi maumivu, n.k lakini pia nao wanahaki kuhishi. Sisi wanadamu tuna akili ya kuwatunza na kuwajali kwani wote tumeumbwa pamoja.
Tatizo ni ego ya mwanadamu kuwa sisi ndio kila kitu na kila uhai wa kiumbe tunaweza kuutoa. Kuwa vegetarian kunakupa sio tu afya ya mwili hasa katika miaka ya vyakula vya madawa bali hata inatupa afya kiroho na kiakili. Ni vigumu kumuelezea mtu. Lakini ni kitu ambacho hakiitaji Kiongozi wa dini, wala kitabu cha dini, ni kitu kitokacho kwa hisia, hisia ya upendo tuliyozaliwa nayo sisi wanadamu kutoka aliyetuumba.
ati kwanini tuwapige au kua wanyama..
Sasa simba anavomvizia nyumbu na akamla nae anadhambi???
Sikia wewe MWENYEZI MUNGU MUUMBA AMEUMBA KILA KITU BINAADAMU WANYAMA NA VIUMBE HAI WOOTE NA KILA ALIEMUUMBA KAMPAGIA RIZIKI YAKE..
UKIAMINI HIVYO BASI..SIMBA CHUI FISI WASINGEKULA NYAMA.
TUANZIE KWAKO KWANZA WE ULIPOZALIWA KABLA YAKUITA MAMA ULIITA NYAMAAAA,,,LEO UMEBALEGHE USHAJIONA MJAAANJA WA KUTOFAUTISHA MAMBO..
SASA JIULIZE HAYO MENO YA MWISHO(MAGEGO)ULIWEKEWA KWA AJILI YAKUTAFUNA MIWA AU??