Sababu ya mwitikio wa watu kusoma shahada ya Umahiri (Master's dgree) kupungua?

Mtambachuo

Senior Member
May 6, 2023
197
293
Habari ya muda wanajamvi. Nimejaribu kufuatilia udahili wa vyuo vikuu kwa miaka mitano nikagundua hamasa ya watu kusoma master's degree imepungua sana.

Hata mtaani ni wachache sana utasikia wanasema wanataka kusoma Master, ukilinganisha na miaka 10 iliyopita hasa 2010 hadi 2015 hamasa ilikuwa juu sana mpaka hata nje ya nchi watu walikuwa wanaenda kwa wingi kusoma.

Hii ipo wazi kwani baadhi ya matangazo ya kazi za wahadhiri zinarudiwa kutangazwa mara mbili mbili na bado zinakosa watu wenye sifa hizo ambayo mara nyingi ni Master's degree au PhD lakini GPA kubwa inazingatiwa pia.

Nini inaweza kuwa sababu, ni kukosa ajira na fedha, watu hawapendi kusoma, shida ni vyuo au sababu ni nini hasa wakuu..
 
Mimi nikishapata haka kadiploma ndo baaas

Na ninakasotea balaa yaani

diploma na/au bachelor vinatosha kwa sasa, lengo la kusoma sasa hivi no kuongeza lifetime earnings(kipato chako maisha yako yote) na sio kupata jina kama zamani

ukiwa na diploma/bachelor ama vyote una qualify kwa viiiingi, masters unakua overqualified kaichukue kukiwa na ulazima
 
Wenye mastaz wamenyonyoka mwili mzima wakinuka madeni huku wenye diploma wakila mema ya uchawa.

Masters za education, utawala, nk ni mbwembwe tu.

Wanaokula mema ya mastaz na wahadhiri wa vyuo, watafiti na watu wa afya.

Kasome mastaz kama una ndugu kigogo, hata kupata uchawa ukiwa na mastaz ni vigumu sana.
 
Nakumbuka mkuu na ulisema kana kukosesha mood yakusoma kabisa. Kikubwa ni uwe skills kwenye ulichosoma.
 
Habari ya muda wanajamvi. Nimejaribu kufuatilia udahili wa vyuo vikuu kwa miaka mitano nikagundua hamasa ya watu kusoma master's degree imepungua sana.

Hata mtaani ni wachache sana utasikia wanasema wanataka kusoma Master, ukilinganisha na miaka 10 iliyopita hasa 2010 hadi 2015 hamasa ilikuwa juu sana mpaka hata nje ya nchi watu walikuwa wanaenda kwa wingi kusoma.

Hii ipo wazi kwani baadhi ya matangazo ya kazi za wahadhiri zinarudiwa kutangazwa mara mbili mbili na bado zinakosa watu wenye sifa hizo ambayo mara nyingi ni Master's degree au PhD lakini GPA kubwa inazingatiwa pia.

Nini inaweza kuwa sababu, ni kukosa ajira na fedha, watu hawapendi kusoma, shida ni vyuo au sababu ni nini hasa wakuu..
Mimi ni mmoja WAPO.
Nilidahiliwa kusoma PhD online na chuo kimoja hivi kipo huko nje.
Mwaka juzi wakati na-apply nilikua na mzuka sanaaaa.
Ila mwaka jana nikapiga chini masomo yenyewe.
Nimeona napoteza muda, Bora nitafute pesa tuuuu.

#YNWA
 
Wenye mastaz wamenyonyoka mwili mzima wakinuka madeni huku wenye diploma wakila mema ya uchawa.

Masters za education, utawala, nk ni mbwembwe tu.

Wanaokula mema ya mastaz na wahadhiri wa vyuo, watafiti na watu wa afya.

Kasome mastaz kama una ndugu kigogo, hata kupata uchawa ukiwa na mastaz ni vigumu sana.
Dah ni kweli kama hizo master za education na utawaka ni nyingi sana. Hata uchawa hupati dah hii noma
 
Mimi ni mmoja WAPO.
Nilidahiliwa kusoma PhD online na chuo kimoja hivi kipo huko nje.
Mwaka juzi wakati na-apply nilikua na mzuka sanaaaa.
Ila mwaka jana nikapiga chini masomo yenyewe.
Nimeona napoteza muda, Bora nitafute pesa tuuuu.

#YNWA
Ilikuaje mkuu hawakukupa support au ndio hiyo kupoteza muda badala ya kusaka pesa.
 
Back
Top Bottom