NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Hapa sisemei kwamba mtu ana phd / masters / degree ya udaktari, uhandisi, uhasibu, Sheria, masoko, IT. La Hasha !! Hizi taaluma ni kipengere kidogo kwenye elimu, mtu alieelimika huwa kajenga mazoea ya kusoma vitabu nje ya taaluma vyenye maarifa yanayogusia maisha, jamii, kustarabika, kuwa mtu bora, n.k. unaweza kuwa na phd ya Uhandisi lakini kama husomi vitabu nje ya IT utaonekana hujaelimika kawenye mambo ya kawaida kabisa katika maisha nje ya taaluma, Mbaya zaidi kwa hapa kwetu mtu akimaliza shule hata hivyo vitabu vya taaluma havigusi tena labda aende tena chuoni ama iwe ni kwajili ya kufanyia kazi, hii inaonyesha wazi kabisa kusoma vitabu sio kwa kupenda.
Hapa Nchini wasomi wengi sana wanamaliza vyuo hawavijui vitabu muhimu kama how to talk to win friends and influence people, 40 laws of power, The art of war, Rich dad poor dad, n.k.
Hii imepelekea wahitimu wengi nchini kutumia nguvu kubwa kujitambulisha wamesoma vyuoni kwasababu katika hali ya kawaida vitu wanavyofanya na kuongea watu huwa na mashaka hasa hawa ambao wameishia darasa la sabab na form 4 ambao nao wameaminishwa mtu akifika chuoni anakua kaelimika hivyo wanachokiona kwa wahitimu kinatia mashaka.
Dalili za wasomi wetu kutokuelimika ni hizi
Upeo Mdogo wa Maarifa: Watu ambao hawajazoea kusoma vitabu wanaweza kuwa na maarifa kidogo au wamejikita zaidi katika maarifa ya utaalamu wao pekee, Mbongo ukimwambia akupe elimu yeye ataanza kumwaga vitu alivyosomea kwenye taaluma yake, na hapa wengi katika mazungumzo ya kawaida tu ama maisha nje ya taaluma zao huwa wanaumbuka, mtu mara ya mwisho kuongea point hadi ufikirie.
Kutokuwa na Uwezo wa Kujieleza Vyema: Kusoma vitabu kunaweza kuimarisha ustadi wa lugha na uwezo wa kujieleza vizuri kwa facts. Watu ambao hawajazoea kusoma wanaweza kuwa na changamoto katika kuwasiliana kwa ufasaha.
Kutokuwa na Ujuzi wa Kuchambua: Kusoma vitabu kunaweza kukuza uwezo wa kuchambua mawazo na kujenga hoja. Watu ambao hawajazoea kusoma wanaweza kuwa na shida katika kuchanganua mambo kwa undani.
Ugumu wa Kujifunza Vitu Vipya: Kusoma vitabu kunaweza kufundisha jinsi ya kujifunza vitu vipya na kutafsiri habari mpya. Watu ambao hawajazoea kusoma wanaweza kuwa na ugumu katika kujifunza mambo mapya hasa kwa hapa nchini ambako elimu imelenga zaidi kusoma kwa kulazimisha kukariri definitions.
Kutojua Kusoma Kwa Furaha: Watu wanaojifunza kupitia kusoma vitabu mara nyingi hufurahia mchakato huo na wanaweza kuwa na uwezo wa kusoma kwa kujitolea hata nje ya mahitaji ya kitaaluma, Kwa hapa Tanzania mtu mwenye masters unaweza kumpa kitabu anaishia page ya 10 imetoka hio, atatalalamika kitabu kirefu kinamchosha ama atakwambia ashamaliza shule usimchoshe na mavitabu.
Kutokuwa na Mawazo na Mtazamo Mpana: Kusoma vitabu kutoka nyanja mbalimbali kunaweza kuongeza ufahamu na mtazamo mpana. Watu ambao hawajazoea kusoma wanaweza kukosa ufahamu wa mambo mbalimbali.