SoC03 Wahitimu wa shahada ya sheria na shule kuu ya sheria Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

hassan yahaya

Member
Aug 27, 2022
32
34
Kuna kauli imezoeleka sana ya "jicho la tatu". Kuangalia au kufikiria jambo kwa jicho la tatu ndio jambo nalotaka kulifikisha mahala husika. Kauli hii inamaana ya kufikiria jambo kwa undani na umakini mkubwa na kuangalia athari zake na hasara zake.

Mada yangu inalenga sekta ya elimu hususani elimu ya juu yaani elimu ya chuo kikuu. Kila mtu anayesoma anatamani afike elimu hii ya juu ili impatie matunda kwa kile anachokisoma. Lakini sote tunajua safari ya kusoma ni ngumu sana inachangamoto nyingi sana. Lakini pia mtoto anaposoma wazazi wanajinyima kula vizuri, kuvaa vizuri, kujenga nyumba nzuri na kuishi maisha mazuri kijumla. Lakini wazazi hawa hutenguka nguvu pale wanapoona kile walichokitarajia hawawezi kukipata tena kutokana na mifumo iliyowekwa na hujilaumu sana na kuwakatia tamas vijana wao.

Nataka nizungumzie suala la wahitimu wa shahada ya sheria ambao wanataka kwenda kujiunga shule kuu ya sheria. Hili ni wazo la kila anayesoma sheria kwamba baada ya kumalizika shahada yake basi aende ili aweze kuajiriwa au kujiajiri kama vile kuwa wakili. Lakini suala lililopo ni tofauti na hamkatisha tamas kabisa yule anayesoma na kuona kama anapoteza muda.

Sheria ni kitu muhimu sana kwani hatuwezi kuishi bila sheria. Kwa wale waumini wa dini maandiko ya vitabu vitukufu yana tuonyesha kuwa hata mungu baada ya kuumba viumbe vyote akaweka sheria ili viweze kuishi vizuri. Lakini kwasababu tunatofautiana kidini na kiimani utawala wa maisha ya hapa duniani yamewekewa sheria ambazo wasomi mbalimbali wamekaa kuzijadili na kuona kuwa zinafaa kulinda na kuipa mwongozo jamii na kuzipitisha sheria kadha wa kadha.

Lakini kwa masikitiko makubwa leo hii vijana wetu wanahitimi chuo kikuu katika shahada ya sheria wanaishia mtaani bila mwendelezo wowote na bila msaada wowote kwasababu wanadhindwa kugharamia ili kukidhi mahitaji ya kwenda shule kuu ya sheria ili na wao wawe na hadhi fulani, ili watambulike na waweze kusaidia katika kutoa elimi ya sheria na kusimamia haki za kila raia.

Gharama za kwenda kusoma shule kuu ya sheriw ni zaidi ya milioni tano. Lakini serikali inafahamu kwamba kunawatu wametoka familia duni chuo kikuu walisoma kwa mkopo je kwanini wasipunguze hizi gharama na kuwapa mikopo ili baada ya kupata ajira vijana hao waweze kurejesha hiyo mikopo kiurahisi na sio kuishi na madeni miaka yake yote ya kazi. Huzi gharama ni kubwa sana na wapo watu hawaziwezi kukidhi wanapaswa wasaidiwe kwani walisimeshwa ili waje kuwakomboa wengine, wanavyoshindwa kwenda wao basi hata baadhi ya watu waliokuwa wakiwategemea wananyong'onyea kabisa. Gharama hizi zikipungua itakuwa rahisi sana kwa hawa wahitimu kwenda kusoma ili waweze hata kujiajiri. Lakini kama suala la gharama kupunguzwa ni gumu basi serikali itoe ajira kwa hawa wahitimu ili waweze kupata hiyo pesa nao waende wakasome.

Tkiachana na suala hili la gharama lakini pia lipo suala la matokeo ya wanaoenda kusoma hii shule kuu ya sheria. Matokeo yamekuwa mabaya sana na yanakatisha hata tamaa kwa wale waliokuwa wanataka kusoma. Matokeo ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa kati ya wanafunzi 633 wanafunzi 26 ndio waliofalu na waliobaki 607 hawajafaulu. Matokeo haya yanasikitisha sana na yanakatisha tamaa hata mtu aliyesoma kwa mara ya kwanza atadhani kwamba amesoma vibaya kakini ndio ukweli ulivyo. Asilimia ya waliofaulu ni 4.11% kwa nasna ya kwamba hata robo ya walio faulu haijafika. Inamaana hawa wanafunzi 607 warudishe taarifa kuwa hawajafaulu.

Lakini majibu yaliyotoka ni kuwa tatizo lipo kwa wanafunzi wenyewe, inawezekana kuwa ni kweli au si kweli kwasababu tathmini hii wameifanya wenyewe na wao ndio walitoa majibu je, tutawaamini vipi?. Sawa tuchukue majibu ya kuwa wanafunzi ndio hawana uelewa mzuri lakini kabla ya kumhukumu mwanafunzi hebu tuangalie mazingira aliyosoma unakuta kasoma chuo kinatambulika na serikali na walio wanaofundisha wanavigezo vya kufundisha, je, ni kweli kwamba kati ya wanafunzi 633 wanafunzi 607 hawajui?

TUFANYEJE ?
Kwa mtazamo wangu naona kwamba mamlaka z
husika zikae zipitie upya juu ya utolewaji wa shahada hizi za sheria na kukagua walimu wanaofundisha kama kweli wanapaswa kufundisha au laa!

Kakini pia wanafunzi wa sheria wanapaswa kuhudhuria mafunzo kwa vitendo angalau mara mbili na sio mara moja kama unavyodanyika ba vyuo vingi hapa nchini.

Wahusika kutoka shule kuu ya sheria wanapaswa kutembelea vyuoni ili kutoa hamasa na elimu kuhusu shule kuu ya sheria ili kila mwanafunzi aweze kufahamu na aweze kujipanga vyema ba sio kwenda tu bila kujua kama kurusha mishale gizani.

Walimu wanaofundisha wanafunzi wawe waadilifu waache upendeleo kuwasaidia wanafunzi kwani hawawasaidii bali wanawapotosha na kudidimiza malengo yao.

Gharama za kwenda kusoma shule kuu ya sheria ipunguzwe ili wanafunzi waweze kuilipa.
Vigezo vya udahili wa wanafunzi wanaotaka kusoma shahada ya sheria vipandishwe ili watakaosoma wawe wenye uelewa mzuri hii itasaidia katika kufaulu kwa wanafunzi.

TAKUKURU iweke mfumo mzuri wa kufuatilia rushea vyuoni kwani rushwa ni nyingi, wapo wanaotoa rushwa za pesa na wengine rushwa za ngono ili wapate GPA nzuri lakini kichwani hamna kitu.
ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA, MSHIKE SANA ELIMU USIMUACHE AENDE ZAKE.
 
Back
Top Bottom