Sababu, kwanini Acacia hawataki kulipa $300m

Sababu, kwanini Acacia hawataki kulipa $300m

Mkuu,
Mbona wametumia neno “ability”.

Mkuu,
Mbona mnapenda kupindisha mambo. Kuna neno “Upfront”. Na content kuna neno “ability”!
Kama mmezoea kuingizwa mjini na wazungu hatuna msaada wowote.

"In future we will form a partnership, a 50/50 partnership" by Mwanaume, which future.
 
Tafadhali sana walipe haraka, nipate buku 14 yangu nataka kaitumia...
 
kwani nyie mazungumzo mmefanya ba Barick au AAccacia??
 
Huenda hawana uwezo maana biashara ilisimama tokea makinikia yazuiwe
Kwani si walisema makinikia hayakuwa na dhahabu nyingi na kuiponda ripoti kuwa ya uwongo na kama kweli madini yangekuwa kwa kiwango kilichotajwa na kamati basi Tanzania ingekuwa nchi ya kwanza kwa kuzalisha dhahabu duniani? Iweje leo waseme wamepata hasara kubwa kwenye mchanga usio na thamani karibu sawa na wa kujengea nyumba?
 
Dola
Acacia Mining takes further revenue hit as deal with Tanzania nears

"Barrick is equally aware of our balance sheet as we are, so we don’t have the ability to make an upfront $300m payment,” said Andrew Wray, adding that the form of the payment - for example, installments - would have to be worked out in further talks.

Walichosema ni kuwa kwa sasa hawana pesa ya kulipa mbele kwa sababu mgogoro umeathiri akaunti yao ya benki. Itabidi yafanyike mazungumzo kuwe na utaratibu wa kulipa kwa awamu.
milion 3 au milion 300?( Hapo kwenye heading).
 
Bosi wao kakubali walipe ili isaidie kutatua mgogoro wao wa deni la kodi.

Mkuu hivi hawa WaCanada inakuwaje sisi tunawabembeleza watulipe wakati wao wamekamata ndege yetu kwa kudaiwa? Kwanini tusikamate mitambo yao na kutaifisha migodio yote wanayomiliki ili wazungu wasituchezee?
 
Mi naomba niulize, ivi izo USD 300m zime kokotolewaje hadi kufikia hapo? Kwanini sio 500m? Yani kitu gani kilichowafikisha hapo kwenye 300m? Na je madai yetu ya trillion 190+ wao Barrick wanasemaje? Na zile ripoti walipewa wazisome? Walikubaliana na kile kilichoandikwa? Kama ndio walipe! Kama hapana wao wanaona wapi ripoti haipo sawa? Na je tunafikiaje muafaka?
Kabudi bado hajaeleweka kabisa!
 
Wao walisema hawawezi kulipa $300m, kama ni milioni $3m labda wanaweza.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Bw. Brad Gordon alisema tangu serikali ya Tanzania izuie kusafirisha makinikia nje ya nchi na kuyazuia makontena yake bandari ya DSM, kampuni yake imekuwa ikipata hasara ya dola za kimarekani 15m kila mwezi.

Makontena yamezuiliwa tangu mwezi wa tatu ni karibu miezi 8 sasa, kwa gharama hiyo Acacia wameshapata hasara ya takribani $120m.

Kwenye mazunguzo yaliyoisha juzi kati ya serikali na wawakilishi wa Acacia, Barrick wamekubaliana Acacia walipe $300m in good faith.

Je, kwenye makubaliano hayo wali consider hasara wanayopata Acacia hadi leo? au tuseme ndio sababu ya wao kugoma kulipa? na je, wakisema kwenye hiyo $300m watoe hasara ya $120m tupo tayari kuchukua $180m zilizobaki ili nasisi tuonyeshe uaminifu kwao au hatuwaamini tena, kama hatuwaamini kwanini tuendelee kufanya nao biashara.

Mawazo yako Tafadhali.
Hakuna tatizo kabisa, itafunguliwa account maalum pale BOT ambako mapato ya mauzo yao kila mwezi yatakua yanaingizwa pamoja na mapato ya mauzo ya hayo makinikia ya USD 120 mil.

Zitakapotimia USD 300 mil tutachukua chetu na account itafungwa na tutaendelea na utaratibu mwingine kama tulivyokubaliana na Barick.
 
Hakuna tatizo kabisa, itafunguliwa account maalum pale BOT ambako mapato ya mauzo yao kila mwezi yatakua yanaingizwa pamoja na mapato ya mauzo ya hayo makinikia ya USD 120 mil.

Zitakapotimia USD 300 mil tutachukua chetu na account itafungwa na tutaendelea na utaratibu mwingine kama tulivyokubaliana na Barick.
Unataka kuzalisha Escrow nyingine tena.
 
Kwani kuna mtu alikua anasema kwamba hawatalipa?

Wataachaje Kulipa wakati ni makubaliano na tumetiliana saini kama mkataba? Mitambo yao ipo na shughuli za uzalishaji zinaendelea alafu wakiuke mkataba? Si tunataifisha tu mali zao zote tena bila kwenda mahakama za nje
 
Back
Top Bottom