Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na Kumruka Barrick Kuwa Haijui Chochote Kuhusu Makubaliano Yoyote na Tanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,795
2,000
Wanabodi
Salaam.
Angalizo la Uzalendo.
Naomba kuanza bandiko hili na angalizo la uzalendo wa kweli wa nchi yako, ni pale unapo note nchi yako inataka kupigwa changa la macho, rais wako anataka kudanganywa mchana kweupe, unatoa angalizo ili kuwagutusha kabla, ili likija kutokea kuwa hakuna excuse kuwa viongozi wetu hawakujua.

Kuhusiana na sakata la Makinikia na Mazungumzo kati ya serikali yetu na Barrick huku mhusika Mkuu Acacia akiwekwa pembeni, leo yamefanyika mambo makubwa matatu.
Jambo la kwanza ni Barrick ambaye ndiye mmiliki wa Acacia, ametoa press release kwenye website yao kuhusu mazungumzo na Tanzania. taarifa hiyo ya Mark Bristow, President and CEO of Barrick. inapatikana hapa Barrick Gold Corporation - Barrick and Tanzanian Government Progress Discussions in Settlement of Acacia Disputes
Press release hiyo imesema hivi
Barrick and Tanzanian Government Progress Discussions in Settlement of Acacia Disputes
Press Release
(opens in new window) PDF

FEBRUARY 20, 2019
ALL AMOUNTS EXPRESSED IN U.S. DOLLARS

TORONTO — Barrick Gold Corporation (NYSE:GOLD)(TSX:ABX) (“Barrick” or the “Company”) today announced that the Company, in its capacity as a facilitator, and the Government of Tanzania have arrived at a proposal that sets forth the commercial terms to resolve outstanding disputes concerning Acacia Mining plc’s operations in Tanzania.
The Company will present this proposal to the Independent Directors of Acacia in the near future for their consideration.
The proposed framework is consistent with the agreement announced in October 2017 and includes the following elements:
 • The creation of a local operating company to manage Acacia’s operations in the country.
 • Economic benefits from Acacia’s operations to be shared on a 50/50 basis. The Government’s share of economic benefits would be in the form of royalties, taxes and a 16 percent free carry interest in the Tanzanian operations.
 • A payment of $300 million to the Government of Tanzania to resolve outstanding tax claims, to be paid over time on terms to be settled by the parties.
Mark Bristow, President and CEO of Barrick, said: “Significant amounts of real value have been destroyed by this dispute and, in Barrick`s view, this proposal will allow the business to focus on rebuilding its mining operations in partnership with their respective stakeholders, and most importantly long suffering investors, including Barrick”.
Work is underway to finalize the definitive agreements needed to give effect to the proposal. To become effective, the proposal and those agreements must be approved by Acacia and the Government of Tanzania, in keeping with applicable laws and regulations. Barrick holds a 63.9 percent equity interest in Acacia, a publicly traded company listed on the London Stock Exchange that is operated independently of Barrick.
Ufafanuzi mfupi wa taarifa ya Barrick inasema Barrick na Serikali ya Tanzania leo wamefikia mapendekezo ya kuumaliza rasmi mgogoro wa makinikia kati ya Acacia na serikali ya Tanzania. Taarifa hiyo imesema. wamekubaliana mambo matatu
 1. Itaundwa kampuni mpya kuimanage Acacia in Tanzania
 2. Tutagawa 50/50 za economic benefits ambapo ndani ya hiyo economic 5-% ya Tanzania itajumuisha zile 16% shares, royalties na taxes zote
 3. Watatulipa dola milioni 300 to resolve outstanding tax claims.
Taarifa hii ya Mark Bristow, President and CEO of Barrick, imesema proposal hiyo, itawasilishwa kwenye bodi ya Acacia in the near future (haikusemwa lini), lakini imesisitiza Bodi ya Acacia ndio yenye mamlaka ya mwisho kukubali au kukataa proposal hiyo.

Jambo la pili ni Baada ya taarifa hii, Acacia nao, wakatoa press release kwenye website yao,
Leo leo, Acacia wametoa Press Release kuwaruka Barrick
Jambo la tatu ni Bosi wa Barrick Afrika, leo katinga ikulu yetu kumuona rais wetu na Taarifa ya Ikulu ni hii kuhusu mazungumzo hayo

My Take.
Huu ni uchambuzi wangu kuhusu taarifa zote tatu naomba niuweke in points format ili ikitokea tunabishana mahali, tubishana kwa hoja kuhusu kifungu fulani.
 1. Taarifa ya kwanza ni habari njema kuwa hatimaye mazungumzo haya yamefikia mwisho, tamati na wamekubaliana mambo matatu ya msingi.
 2. Itaundwa kampuni mpya kuimanage Acacia in Tanzania, hili limekaa vizuri, hii maana yake Acacia itavunjwa na kuundwa kampuni mpya ambayo kwenye bodi yake sasa kutakuwa na Watanzania shauri ya ile 16% stake ya sheria mpya ya madini.
 3. Tutagawa 50/50 za economic benefits ambapo ndani ya hiyo economic 50% ya Tanzania itajumuisha zile 16% shares, royalties na taxes zote. Mwanzo tulielezwa tutagawana faida, kumbe sasa sio faida tena bali imekuwa ni Economic benefits. Aliyetutangazia tutagawa faida ni rais wetu na Waziri wetu Kabudi, alifafanua vizuri. Kwa vile haya sasa ndio makubaliano ya mwisho, hii maana yake ni ama rais wetu pale mwanzo alipotoshwa, na waziri alipotosha, taarifa walizotoa mwanzo zilikuwa ni za uongo au upotoshwaji, ukweli wenyewe sasa ndio huu, ama tangu mwanzo ilikuwa ni economic benefits tatizo ni lugha za watu. Hili mimi nililiulizia rasmi humu Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums
 4. Watatulipa dola milioni 300 to resolve outstanding tax claims. Deni tunalowadai ni dola bilioni 190, Ile dola milioni 300 ya goodwill iliahidiwa tuu kuonyesha nia njema, lakini sasa ndio pekee inatajwa kama settlement deal!. Hapa kuna changa la macho!, tusubiri hiyo settlement deal yenyewe maana hizi lugha za watu ni shida. Kama lile deni la Dola bilioni 190 ni deni la kweli. halafu unakubali ku settle kwa dola milioni 300!, wenye akili tumeishaelewa, kuna vitu vingine ukichemsha sio lazima usema, viondoe kimya kimya tuu watu wasijue!.
 5. Kule mwisho anaposema makubaliano yoyote lazima yaridhiwe na Acacia, hapa ndipo kwenye tatizo kubwa. Who is this Acacia kama mmiliki wa Acacia ni Barrick na mazungumzo hayo sio tuu ni serikali ya Tanzania na Barrick, nali ni makubaliano ya rais wa Tanzania na rais wa Barrick, baada ya kukubaliana then kuna mtu mkubwa zaidi yao ndiye ataamua kutekeleza au laa!. hii haijakaa vizuri na niliizungumzia hapa Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums
 6. Tukija kwenye taarifa ya Acacia, kiukweli kabisa haijakaa vizuri na hii sii dalili nzuri, wewe kama mwana jf, be the first to know from me, kuwa mapendekezo yoyote ya settlement kati ya Barrick na Tanzania, hata yakifikishwa kwenye Bodi ya Acacia, yatakataliwa!, Kitakachofuata ni baba Barrick ndiye ama atalipa fedha hizo kwa niaba ya mwanaye, kisha atamwadhibu mtoto wake jeuri huyu kwa kumchapa bakora za kisawasawa kwa kuivunjilia mbali Acacia na kuunda Kampuni mpya yenye bodi yenye Watanzania.
 7. Sababu za kusema hivi ni huyu Acacia ni mtoto tuu, baba ni Barrick, haiwezekani baba azungumze, na kutuma ujumbe kuja kuzungumza na rais wetu na atoe ahadi kwa rais, kisha atoe press release kuwa mambo yamemalizika na mtoto ataarifiwa tuu kwa ajili ya utekelezaji, halafu wewe mtoto, licha ya kusoma Press Release ya baba, halafu wewe mtoto unatoa press release yako kumkana baba yako kuwa bado hujaarifiwa!. Huu ni ujeuri wa aina gani au hiki ni kiburi cha aina gani?, kiafrika hapa mtoto unaweza hata kupata laana, lakini mambo haya kwa wenzetu wazungu tena jeuri hii ya mtoto huyu haikuanza leo na hapa niliwahi kuizungumza Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
 8. Nikija kwenye taarifa ya Ikulu taarifa ya Ikulu, inaonyesha sasa the settlement ni ile dola milioni 300 tuu, ambacho sasa kinaitwa kifuta machozi ya zile dola bilioni 190!. Niliwahi kutoa angalizo humu kuwa rais Mkapa alidanganywa akadanganyika, JK pia akadanganywa akadanganyika, nikasema naziona dalili za rais Magufuli kutaka kudangaywa, kama tume settle dola bilioni 190 kwa dola milioni 300, hapa kiukweli kabisa, Watanzania tutahitaji tuelimishwe labda tutaelewa na ikiwa jili deni la kodi ni deni fake, lets come clean kwa kuusema ukweli kuwa tuliwazushia tuu, hii maana yake TRA ni wazushi?. Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums
 9. Pia taarifa ya Ikulu imethibitisha mgawo sasa ni 50/50 ni wa economic benefits, na sio 50/50 ya faida. Hili linahitaji ufafanuzi tuu wa ziada kwa viongozi wetu kumuomba radhi rais wetu kwa kumpotosha na kutupotosha Watanzania, na kiukweli wakitoa sababu tuu kuwa ni hixi lugha za wenzetu, Watanzania tutawaelewa.
 10. Msingi mkuu wa yote haya ni mgogoro wa makinikia. Tulizuia makontena ya mchanga, kwa sababu tulihisi tunaibiwa kwa kutokujua kilichomo ndani ya mchanga ule, tukaunda tume mbili kuchunguza, tukajiridhisha kuwa ni kweli tunaibiwa na TRA wakaja na figure ya dola bilioni 190. Ili tuthibitishe madai yetu ya tunaibiwa nini, ilibidi ule mchanga uchenjuliwe ndipo tupigiane hesabu za kweli. Sijasikia tena kuhusu ununuzi wa kichenjulio, kiukweli mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, sio tuu nitashangaa bali, bali kiukweli kabisa nitaamini sisi Watanzania .... naomba nisimalizie
Hitimisho.
Watanzania wote wazalendo wa kweli wa taifa hili, tumuunge mkono rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli katika vita vya kulinda rasilimali zetu dhidi ya mabeberu, na kama una jicho la tatu la kuangazia visivyoonekana na wenye macho mawili tuu, then share what you see which others don't see so that we can all see, kwenye hili, la mgogoro wa makinikia, kuumaliza bila mchanga ule kuchenjuliwa tukajua kilichomo, hili ni kosa kubwa tutafanya kwa sababu, tuliuzuia mchanga kwa kuhisi tunaibiwa kwa sababu hatujui kilichomo, tukiumaliza huu mgogoro bila kujua kilichomo, tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwa sababu tutaendelea kuibiwa.

Pili there is something fishy and there is something wrong with us somewhere somehow katika uelewa wa haya mambo. Hizi dilly dalyings za Acacia na Barrick, mimi kwangu naziona kama its a game people play. Acacia na Barrick ni baba na mwana, wanajuana and they are one.

Nawatakia Jumatano njema
Paskali

Rejea kuhusu makinikia

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300 - JamiiForums

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums"]

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!". - JamiiForums

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli? - JamiiForums

Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu. - JamiiForums

Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?. - JamiiForums

Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Bosi wa Barrick, leo katinga ikulu yetu kumuona rais wetu na kutuletea habari njema kuwa wataheshimu makubaliano yote kati ya Barrick na serikali yetu na kuwa tayari wameisha yawasilisha Acacia kwa utekelezaji.

Leo leo, Acacia wametoa Press Release kuwaruka Barrick

2019

My Take.
Hii sii dalili nzuri, wewe kama mwana jf, be the first to know from me, kuwa mapendekezo yoyote ya settlement kati ya Barrick na Tanzania, tayakafikishwa kwenye Bodi ya Acacia, yatakataliwa!.

Acacia ni mtoto tuu, baba ni Barrick, haiwezekani baba aseme kitu fulani, atoe press release, azungumze hadi na Reuters na kutangazia dunia, halafu wewe mtoto unatoa press release kumkana baba!.

Paskali
Tutatumia jeshi wee waache tu
 

The Elephant

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
4,159
2,000
Pia ni tatizo la serikali kudanganya uma! Barrick wenyewe wanasema watapeleka mapendekezo yote kwenye bodi ya ACACIA kwa ajili ya approval lakini serikali inasema BARRICK wamekubali kila kitu walichojadili wakati approval bado kutoka ACACIA

Mwisho wa siku usishangae migodi ikifunguliwa bila mirejesho ya nini walikubaliana
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,123
2,000
Bosi wa Barrick, leo katinga ikulu yetu kumuona rais wetu na kutuletea habari njema kuwa wataheshimu makubaliano yote kati ya Barrick na serikali yetu na kuwa tayari wameisha yawasilisha Acacia kwa utekelezaji.

Leo leo, Acacia wametoa Press Release kuwaruka Barrick

2019

My Take.
Hii sii dalili nzuri, wewe kama mwana jf, be the first to know from me, kuwa mapendekezo yoyote ya settlement kati ya Barrick na Tanzania, tayakafikishwa kwenye Bodi ya Acacia, yatakataliwa!.

Acacia ni mtoto tuu, baba ni Barrick, haiwezekani baba aseme kitu fulani, atoe press release, azungumze hadi na Reuters na kutangazia dunia, halafu wewe mtoto unatoa press release kumkana baba!.

Paskali
Kwani sie mgodi tulimkabidhi nani kati ya hawa wawili?
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Pia ni tatizo la serikali kudanganya uma! Barrick wenyewe wanasema watapeleka mapendekezo yote kwenye bodi ya ACACIA kwa ajili ya approval lakini serikali inasema BARRICK wamekubali kila kitu walichojadili wakati approval bado kutoka ACACIA

Mwisho wa siku usishangae migodi ikifunguliwa bila mirejesho ya nini walikubaliana
Huu ndiyo ugomvi tunaoutaka sio ugomvi na Lissu au wapinzani
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,086
2,000
Bosi wa Barrick, leo katinga ikulu yetu kumuona rais wetu na kutuletea habari njema kuwa wataheshimu makubaliano yote kati ya Barrick na serikali yetu na kuwa tayari wameisha yawasilisha Acacia kwa utekelezaji.

Leo leo, Acacia wametoa Press Release kuwaruka Barrick

2019

My Take.
Hii sii dalili nzuri, wewe kama mwana jf, be the first to know from me, kuwa mapendekezo yoyote ya settlement kati ya Barrick na Tanzania, tayakafikishwa kwenye Bodi ya Acacia, yatakataliwa!.

Acacia ni mtoto tuu, baba ni Barrick, haiwezekani baba aseme kitu fulani, atoe press release, azungumze hadi na Reuters na kutangazia dunia, halafu wewe mtoto unatoa press release kumkana baba!.

Paskali
Abracadabra! Now you see it, now you don’t!😀
1550675036509.jpeg
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,256
2,000
Update on Discussions in Tanzania
20 Feb 2019

Acacia notes today’s announcement by Barrick Gold Corporation (“Barrick”), Acacia’s majority shareholder, regarding an update on the ongoing discussions with the Government of Tanzania (“GoT”)

Acacia has not yet received any proposal from Barrick regarding a comprehensive resolution of the Company’s disputes with the GoT. Any proposal received by Acacia will be subject to review by the Independent Committee of the Acacia Board of Directors.

A further update will be provided when appropriate.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Update on Discussions in Tanzania
20 Feb 2019

Acacia notes today’s announcement by Barrick Gold Corporation (“Barrick”), Acacia’s majority shareholder, regarding an update on the ongoing discussions with the Government of Tanzania (“GoT”)

Acacia has not yet received any proposal from Barrick regarding a comprehensive resolution of the Company’s disputes with the GoT. Any proposal received by Acacia will be subject to review by the Independent Committee of the Acacia Board of Directors.

A further update will be provided when appropriate.
Naanza kuingiwa na wasiwasi kuwa tunadanganywa na JPM
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,123
2,000
Swali gani ra ajabu hivi?. Wewe jua bariki ni mshenga wa mazungumuzo kati yaTz na acacia. Na hadi sasa mshenga hajafikisha report kwa muoaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali bado liko pale pale, tulimpa nani mgodi? Uliempangisha nyumba yako ndie unaetakiwa ukubaliane nae maswala mbali mbali kama vile kiwango cha kodi, aina ya ulipaji, etc.

Sio kaka, mjomba, binamu, mkwe wala nani yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom