Barrick Yaitangaza Vibaya Tanzania “Considered a higher risk",na "Acacia Mining reflects Tanzania risk". Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli Tukanushe Au?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali, hawa Barrick wanaitangaza vibaya Tanzania kwa kusema kuwa Tanzania is Considered a higher risk",na kuwa mgogoro wa "Acacia Mining reflects Tanzania risk". Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli jee tukanushe kwa kuusema ukweli au tuendelee kujinyamazia na kumuachia Mungu?.

Uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, sio tuu unaweza kuonekana kama ndio ukweli, bali unaweza kabisa kugeuka kuwa ukweli kwa sababu baadhi ya kauli huumba!.

Maneno haya ni matamshi wa Bosi wa Barrick kwenye interview na shirika la habari za Uingereza Reuters kuhusu mgogoro wa Acacia ambapo siku ya Jumapili iliyopita, licha ya kuwa sio siku ya kazi, lakini siku hiyo, inasemekana serikali yetu iliziandikia barua migodi mitatu ya Acacia nchini kuiambia kuwa serikali haaitambui Acacia, hali iliyoilazimu kampuni mama ya Barrick, kutoa offer ya kununua hisa zote za Acacia, hivyo kuifungisha virago, na kutekeleza yale makubaliano na serikali yetu.

Kabla sijaendelea, naomba kukiri nimekuwa inspired na bandiko hili
UPDATE 1-Barrick's offer for Acacia Mining reflects Tanzania risk -CEO
Mkuu Winnerian, asante kwa taarifa hii.
Kiukweli sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana!, huyu mtu anatutangaza vibaya hivi kimataifa kuwa Tanzania ni higher risk nation for investors, halafu watu humu wanashangilia!.

Taarifa hii kaitolea Reuters na sio kwenye haya magazeti yetu ya kufungia maandazi.
What does this tell about our nation to the rest of the world as far as investment climate is concerned?.

Hoja kuu ya bandiko hili, hawa jamaa wanasema vibaya, wanatungaza vibaya ulimwenguni, jee ni kweli sisi Tanzania tuko Considered a higher risk kwenye investments?. Kauli hii ina maana gani kwa investors?.
Jee ni kweli the situation ya Acacia Mining in reflects Tanzania risks?

Naomba kuziweka hoja zangu in number formats ili iwe rahisi kueleweka, na mtu ukiuliza, uweze kuuliza kuhusu specific kipengele.
  1. Tangu kuibuka kwa mgogoro wa makinikia ya Acacia, ulioanza kwa kuzuiliwa kwa mchanga wa makinikia ya Acacia, tukaunda tume, tukagundua kumbe tulikuwa tunaibiwa, tukaja na deni la dola bilioni 190, Acacia akataa kuwa haibi na halipi. Ndipo baba mtu Barrick akaingilia kati kwa kuja nchini kubembeleza, hatimaye mazungumzo yakaanza. Kuna mengi yametokea mengine mazuri, mengine mabaya, hatimaye tukafanya mazungumzo ambayo yamefikia tamati, kukatolewa mapendekezo ikabaki hatua ya mwisho ya kuyakubali mapendekezo hayo, makubaliano yasainiwe utekelezaji uanze.
  2. Mazungumzo hayo yaliweka falsafa tatu kuu za kufuatwa ambazo ni T.T.T, Trust, Truthfulness na Transparency, kwa lugha yetu adhimu ni Kuaminiana, Kuwa Wakweli na Kuwa Wawazi. Naomba nisizungumzie la Kuaminiana, na Kuwa Wakweli, lakini kwenye hili uwazi, wenzetu wazungu wamekuwa wawazi zaidi.
  3. Tangu kuanza kwa mazungumzo, sisi Tanzania tumetoa taarifa mbili tuu,na zote zimetolewa Ikulu, taarifa ya kwanza ni ile ya kufikia makubaliano kuwa itaundwa kampuni mpya ambayo tutagawana faida, profits, pasu kwa pasu, na kuahidiwa kile kishika uchumba cha dola milioni 300 za nia njema kuonyeshea nia ya kulipa ile mahari kamili ya dola bilioni 190 baada ya kupigiana hesabu. Baada tuu ya taarifa hiyo ya ikulu, sisi Tanzania tuliishia hapo, wenzetu siku hiyo hiyo waliweka kwenye websites zao tulichokubaliana kugawana 50/50 ni economic benefts za sio faida. Ikulu yetu never bothered to correct.
  4. Taarifa ya pili ni ile ya kutangaza maafikiano ya mwisho kuwa sasa tumewasamehe lile deni lote la dola bilioni 190, na badala yake tutapewa kifuta machozi cha kile kishika uchumba cha dola milioni 300, Acacia itavunjwa na kuundwa kampuni mpya ambapo tutapewa hisa za asilimia 16% tutagawa faida za kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.
  5. Wakati wote huu, wenzetu walikuwa wakitoa updates za kinachoendelea, hivyo sisi huku kukipata kupitia kwenye websites zao. Dhahabu ni yetu, mazungumzo yanafanyikia ikulu yetu, lakini updates za kinachoendelea, tunakwenda kukipatia Toronto ilipo Barrick, au London ilipo Acacia, why not Dar es Salaam kwa mwenye mali na ndiko lilipo tatizo?.
  6. Mgogoro wa sasa wa Barrick kununua hisa zote za Acacia na kuifuta, pia originating ni Dar es Salaam, Watanzania tunapokea taarifa kuwa Siku ya Jumapili, tarehe 19th May 2019, serikali yetu, licha ya kuwa ni Jumapili, sio siku ya kazi, huwezi kuandika barua za kiserikali siku ya Jumapili, lakini kwa serikali ya Magufuli ya Hapa Kazi Tuu, hakuna cha Jumapili wala sikukuu, ni kazi tuu, ikitokea kazi ya urgency kama hizi barua za kutoitambua Acacia, serikali yetu inaingia kazini, Jumapili ya wiki iliyopita, serikali imeingia kazini, imeziandikia barua migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, kuwaeleza kuwa hawaitambui Acacia, hali iliyoilazimu Barrick kutoa offer ya hostile take over kwa Acacia kuzinunua hisa zote za Acacia, ambazo hazimilikiwa na Barrick, itake isitake, hivyo kuimeza rasmi Acacia kuwa sehemu ya Barrick. na wana hisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa wa Barrick. Kwa Tanzania Hostile take over iliwahi kutokea kwa kiwanda cha Bia cha Kibo kule Moshi. Tofauti ya hostile take over ile na hii, migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, itaendelea kuwepo, hakuna atakayepoteza kazi na uzalishaji unaendelea, kitakachokufa ni Acacia tuu, nafasi yake inavhukuliwa na Barrick, everything else stays the same.
  7. Kitendo hiki kilichofanywa na serikali yetu kui disown Acacia ni kitendo cha kishujaa sana na huu ndio uanamme. Haiwezekani madini yetu, mtu anayetambulika nchini kama ni mmiliki ni Barrick kupitia Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, huyu Acacia ni mtu wa kuja tuu, hatambuliwi halafu analeta nyodo kibao.
    Barua hizo za serikali, zimepelekea leo Acacia na Barrick kutoa press release hizi
    .
  8. Hii ya serikali yetu kuandikia barua migodi siku ya Jumapili ambayo sio siku ya kazi, kuileza hiyo migodi kuwa serikali haitambui Acacia, hivyo Bariick kulazimika kuinunua. Yaani barua ziandikwe Dar es Salaam, zisambazwe Dar es Salaam, lakini Watanzania tujue kupitia websites za wazungu, what sort of transparency is this?
  9. Huku kwa Tanzania kutangazwa vibaya na Barrick, kunafuati serikali yetu kuandika barua hizo. Swali ni jee ni kweli serikali yetu imeandika barua kwa migodi kutangaza hawaitambua Acacia?. Maana wanaosema haya mpaka sasa ni hawa wazungu, sijasisikia serikali yetu ikijibu chochote, kama huu ni uongo, tusiunyamazie uongo kama huu ambao unatuchafua, tukinyamaza dunia itaamini anachosema bosi wa Barrick kuhusu Tanzania ni kweli. Jee ukweli ni upi?.
  10. Baada ya kusikia serikali yetu imewatosa Acacia, niliipongeza https://www.jamiiforums.com/threads...tile-take-over-soon-itakuwa-kwishney.1587164/, bila kujua kuwa kumbe kuwatosa huku kutapelekea Tanzania kuzidi kuchafuliwa kimataifa as far as investment climate is concerned.
  11. Hongera sana kwa Serikali Yetu, Kuwatosa rasmi Acacia Kwa kuandika barua rasmi za kutowatambua, kutakakopelekea kifo rasmi cha Acacia, Huu Ndio Uanaume!. Haiwezekani madini yetu, Tanzania inazungumza na Baba Mtu, Barrick, halafu wewe mtoto tuu, Acacia kila siku ni kuleta nyodo. Sasa Acacia Itakula Jeuri Yake, it Faces a Hostile Take Over from Barrick, and Soon Itakuwa Kwishney!. A thing of the past, a history!. Ila haya sisi Watanzania tulipaswa kuelezwa na serikali yetu tangu kuhusu hizo barua na sio sisi tuzisikie kwa wazungu hawa.
  12. Tangu kutokea mgogoro wa makinikia ya Acacia, kwanza tulipongeza hatua ya rais Magufuli kuuzuia mchanga wa makinikia Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie
  13. Baada ya kuzuiliwa kwa mchanga, Rais Magufuli akaunda Tume zake mbili, zikamletea ripoti zake mbili, baada ya kushuhudia live presentation ya tume ya pili, nilitoa opinion yangu Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika?
  14. Ripoti za tume hizo zikaosnyesha kuwa siku zote, tumekuwa tukiibiwa, TRA wakaja na bili ya ajabu ya deni ya Dola Bilioni 190 US $ sawa na TZS 424 trilioni kwa fedha za madafu, kuhusu deni hili, sisi wachumi wa Sultani Mangungo wa Msovero ya JF, tukamweleza rais wetu kuwa anadanganywa na kumsihi asidanganyike.
    Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli
    Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye
  15. Acacia kwanza akatoa taarifa kuwa hayatambui makubaliano hayo kwa vile hakushirikishwa, Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto ...lakini siku chache baadae akatoa taarifa ya kukubali kila kitu.
    Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa ...
  16. Sisi wahojaji tukaendelea kuhoji sio tuu uwezo wa Acacia kulipa deni letu la dola bilioni 190, bali hata uwezo Acacia kulipa tuu hata hizo dola milioni 300 za goodwill. Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia ...
  17. Pia tukahoji, kama Acacia ndio determinant wa kutulipa, kwa nini hakushirikishwa kwenye mazungumzo?. Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye ...
  18. Mapendekezo ya makubaliano ya mwisho yalitolewa na Barrick kuwa sasa Acacia watalipa ile dola milioni 300 tuu na deni lote la dola bilioni 190, tukasamehe, Acacia akaibuka na kuikana Barick kuwa wao hawajui chochote kwa vile hawakushirikishwa, hivyo wanasubiri taarifa rami ya Barrick ndipo watangaze uamuzi. Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na ...
  19. Acacia wakaibuka tena kuwa bado hawajapewa makubaliano. Kwanini Mapendekezo ya Makubaliano yetu na Barrick bado hayajafika
  20. Japo Acacia ni mtoto wa Barrick, huyu ni mwana mkaidi, kama kawaida ya mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi, hivyo siku ya Iddi ya Acacia imewadia. Funzo tunalolipata hapa ni siku zote
    kiburi sii maungwana. Acacia alikuwa jeuri, sasa anakula jeuri yake, soon Acacia itabaki kuwa ni historia, kwishney
  1. Ila naomba kutoa angalizo muhimu kwa serikali yetu, hii saga yote ya Acacia na Barrick, mara kimepanda, mara kimeshuka, to me it looks like a game that people plays. Hawa ni baba na mwana, na huu ni mchezo tunachezewa, the bottom line ni lile deni letu la kodi kutoka US$190 bilioni hadi just $300milioni, this is peanut, ila tukiamua kuiita ndio a win win situation for the sake ya uzalendo kwa uwezo wa viongozi wetu ku negotiate, then Watanzania tutawakubalia, na kujifunza somo kuwa na wanasheria nguli tuu peke yake bila watu ambao ni negotiators, hakutoshi. Japo tutapata 16% na kugawana 50/50 za economic benefits, mimi naona kama hapa tunapigwa mchana kweupe huku tunajiangalia.
  2. Kama sasa tunaanza kuchafuliwa na huku makubaliano ya mwisho hayajasainiwa, naona kama vile tunanyanyaswa, kusimangwa na kunyanyapaliwa wakati dhahabu ni yetu, sisi wenye mali tuko kimya tunafanya mambo kimya kimya, halafu wavunaji wa rasilimali zetu wao ndio kila siku press release, na press conferences Toronto na London, hiki kimya chetu kinaashiria nini?.
  3. Msingi mkuu wa yote haya ni mgogoro wa makinikia. Tulizuia makontena ya mchanga, kwa sababu tulihisi tunaibiwa kwa kutokujua kilichomo ndani ya mchanga ule, tukaunda tume mbili kuchunguza, tukajiridhisha kuwa ni kweli tunaibiwa na TRA wakaja na figure ya dola bilioni 190. Ili tuthibitishe madai yetu ya tunaibiwa nini, ilibidi ule mchanga uchenjuliwe ndipo tupigiane hesabu za kweli. Kitendo cha kusamehe deni la dola bilioni 190, kwa kifuta jasho cha dola milioni 300, kinaeleweka kwa wenye akili wote kuwa kule kwenye majadiliano, tumeshindwa kuthibitisha hicho kiwango cha dhahabu. Maadam makinikia bado yapo, tunashindwa nini kuyachenjua na kuwathibishia?. Mpaka sasa, sijasikia tena kuhusu ununuzi wa kichenjulio, kiukweli mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, sio tuu nitashangaa bali, bali kiukweli kabisa nitaamini sisi Watanzania .... naomba nisimalizie
  4. Hitimisho.
    Watanzania wote wazalendo wa kweli wa taifa hili, tumuunge mkono rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli katika vita vya kulinda rasilimali zetu dhidi ya mabeberu, na kama una jicho la tatu la kuangazia visivyoonekana na wenye macho mawili tuu, then share what you see which others don't see so that we can all see, kwenye hili, la mgogoro wa makinikia, kuumaliza bila mchanga ule kuchenjuliwa tukajua kilichomo, hili ni kosa kubwa tutafanya kwa sababu, tuliuzuia mchanga kwa kuhisi tunaibiwa kwa sababu hatujui kilichomo, tukiumaliza huu mgogoro bila kujua kilichomo, tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwa sababu tutaendelea kuibiwa.
  5. Mwisho. Kwangu mimi kwenye hili, I feel there is either something fishy or there is something wrong with us somewhere somehow katika uelewa wa haya mambo, dawa pekee ni kwa pande zote lets come clean, honest, truthfully, na very transparent ili ku establish trust kwa pande zote ikiwemo kwa sisi Watanzania kuamini serikali yetu kuwa its doing the best kwa nchi yetu Tanzania na kwa Watanzania, hivyo namaliza kwa kuuliza tena hili swali, huku kwa Baarick kututangaza vibaya, Jee ni kweli?. Kama ni kweli, hatuna jinsi tujikalie kimya, lakini kama sii kweli jee Tanzania tuendelee kujinyamazia kimya huku nchi yetu ikichafulia kimataifa kwa upande wa uwekezaji kwa kuwachia Mungu, au tukanushe kwa kuusema ukweli ili dunia iujue ukweli kuhusu nchi yetu.

    Mungu Ibariki Tanzania,
    Jumatatu Njema.
    Paskali
 
Risk is measured in terms of impact x likelihood
Kila organisation imeset risk "appetite" meaning the level of risk an organisation can tolerate,what is higher risk to Barrick could be insignificant risk to GGM...
Hapa sijui kama nzi wa lumumba watanielewa
 
Haloo umeibua mjadala ambao hata mimi nilikuwa sijauona. Very hidden mkuu bila kuwa na ugreat thinker hapa tusingeweza kuliona hili nakupongeza sana katika hili japo nahuzunika kusema sio kwamba wanatuzushia hili linatokana ukweli kwamba katika Taifa lolote liwe Taifa tajiri au maskini kunapokuwepo na "Political instability" ni dhahiri shahiri kwamba eneo hilo linakosa mvuto wa kiuwekezaji. Kwanini nasema hivi: "Political instability" sio vita ya CCM na upinzani la hasha ni consistency ya Nchi kama Nchi kufuata utawala wa kisheria na wa kihaki. Mfano mzuri kuna minong'ono ilishawahi kutokea kwamba wafanyabiashara wanawindwa chinichini na rumours nyingine nyingi ambazo zinajidhihirisha katika uhalisia wa mambo yanavyotokea pamoja na matamshi ya viongozi wazito na wenye mamlaka. Labda nitaje maeneo ambayo ni mazuri kwa wawekezaji na uone mwenyewe kwanini
1. Honkong
2. UK
3. Singapore
4. Malaysia
5. Poland
6. USA
7. Germany
8. Philippines
9. n.k.

Haya mataifa na mengine mengi yanalinda sana utawala wa sheria na haki. Wakati mwingine kura zinapigwa mpaka kwenye public transport kusiwe na shaka wala wizi wa kura.

Bila shaka Taifa letu la Tanzania linayo nafasi ya kubadilika na kuelekea zaidi kwenye utawala wa haki na sheria. Katiba nzuri, sheria nzuri zisizo na maslai ya wachache bali wengi, kuheshimu democrasia n.k
 
....
Haya mataifa na mengine mengi yanalinda sana utawala wa sheria na haki. Wakati mwingine kura zinapigwa mpaka kwenye public transport kusiwe na shaka wala wizi wa kura.

Bila shaka Taifa letu la Tanzania linayo nafasi ya kubadilika na kuelekea zaidi kwenye utawala wa haki na sheria. Katiba nzuri, sheria nzuri zisizo na maslai ya wachache bali wengi, kuheshimu democrasia n.k
... umenikumbusha uzi ulioletwa juzi kati humu kuhusu Chama kuvamia uchaguzi wa DARUSO huko UDSM ili kupenyeza mamluki wao kwenye nafasi mbalimbali za uongozi! Shithole!
 
Hapa hakuna MALIPO jamani ifike kipindi tuongee ukweli na tuache siasa Kwa ushahidi ambao mayalla umetuwekea bilashaka Tanzania itaambulia mabua Tu..

Hawa wazungu sio mafal* kiasi hicho mpaka watoe hizo pesa zote sikuzote ukiingia kichwakichwa Kwenye mikataba ya ovyo matokeo yake huwa hivi, Tanzania tulijichanganya tokea enzi zile za akina mkapa na kikwete
 
Hakuna vita ngumu Duniani kama kama vita ua Kiuchumi,Serikali inawajibu wa kujibu mapotoshi haya haraka sana.Rais wetu azidi kuweka msimamo ule ule wa win win situation na kama haiwezekani hii migodi ibaki tu..Zama za Tanzania kufanywa mazuzu itoshe kusema ikome
 
Back
Top Bottom