Kwenye mapendekezo 21 ya ripoti ya Kamati ya Professor Osoro, yapi yana ukweli, yapi si ya kweli? Tumeshatekeleza mangapi? Makinikia ilikuwa usanii?

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,819
2,000
Wanajamvi, nadhani suala hili, halikuzungumziwa vya kutosha hata kidogo. Lissu yeye alishaumizwa na wengine walitishika kabisa kulizungumzia!

Hata hivyo, bado limezungumziwa sana na makada wa CCM hata humu ndani. Mfano kina Pasco! Lakini kwa namna ya uongo na propaganda nyingi.

Ripoti yenyewe imelalamika zaidi kuhusu kodi, na ikapendekeza uwepo uwajibikaji kwa watumishi mbali mbali wa ngazi tofauti za serikali kutokana na misamaha ya kodi kwa makampuni hayo!

Ya kuhusu makinikia, hapo hakukuwa na lolote! Hata kile ambacho kada maarufu wa chama humu Pascal Mayalla, alikuja na uongo mwingi sana humu kuhusu kile alichokiita “kishika uchumba”. Lakini ukifuatilia kwa makini, utagunduwa kuwa hata hicho kilicholipwa na Barick kwa niaba ya ACACIA, walilipa tu ili thamani ya hisa zao, isiendelee kushuka kwenye soko la dunia, pamoja na gharama zinazotokana na kuzuiwa kwa makontena hayo, habari kuwa yamezuiwa, ni mbaya zaidi kwa uchumi wa kampuni kuliko kuwndelea na kesi MIGA! Lakini hakuna nilichoona kwamba wamekubali kuwa wamefanya chochote kile kinyume na mkataba ambao ni CCM waliusaini.

Sitaki kuzungumza mengi, nitayaleta mapendekezo yote hapa, kisha tuyachambuwe, kwasababu uchaguzi umekaribia, sasa tujulishane ukweli ili tujuwe kama tuwape kura au tuwapumzishe.

Maana mojawapo ya mapendekezo, ni sisi kuifahamu mikataba, na wale walioisaini na kuipitisha, wawajibike, lakini naona usanii tu huku wapinzani wakisingiziwa na Lissu wa watu.

Pia kamati ilipendekeza kuwa “Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya waliokua mawaziri,wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba na makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya madini na watumishi wengine wote waliohusika katika kuingia mikataba ya madini.“

Hapo chini, ni kasehemu ka ripoti hiyo ambayo iliitwa “rubbish” ama takataka ya kiprofesa! Ukiisoma kiukweli ni uongo mtupu! Na ndiyo maana tukalipwa kile Pascal Mayalla alichokiita kuwa ni “kishika uchumba”, yani pesa ama gharama za kumzuilia “mwali”, ama mchumba pale bandarini! Ambapo hicho kishika uchumba cha usd 300m, kilitolewa na Barrick, siyo kwasababu eti wamekubaliana na hiyo ripoti, bali ni kwasababu wanaendelea kupata hasara, khasa kwenye thamani ya hisa zao, ambapo wote tunafahamu kuwa taarifa kama hizo huwa zinaathiri thamani yake kwenye soko la dunia! Lakini kama wangelazimishwa kulipa hicho kiasi kilichotajwa, basi ni kweli MIGA ingehusika! Na hapo ndipo point ya Tundu Lissu ilipokuwepo!

Hapo chini ni sehemu hiyo, nimepunguza vipengele vya madini waliyosema yamo ndani ya makinikia! Vipengele hivyo...

“4. Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu. Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki kukadiria mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato kwa nchi yetu.

5. Thamani zote za madini kwenye makinikia yaliyo ndani ya makontena zilizoainishwa hapo juu, zimepatikana kwa kutumia uzito wa wastani wa tani 20 za makinikia kwenye kila kontena. Hata hivyo, katika kupima uzito wa makinikia ndani ya makontena, kuna makontena kadhaa yaliyokuwa na uzito zaidi ya tani 20 za makinikia, kwa mfano makontena yenye namba CAIU 2461301, TCLU 0701267, MRKU 6880530 na MSKU 4280570 yalikuwa na makinikia yenye uzito wa tani 23.1; 22.9; 22.7 na 22.2, kwa mtiririko huo. Hivyo basi, ongezeko hili la uzito linaongeza thamani ya makinikia na hivyo kuongeza upotevu zaidi wa mapato ya Serikali.

6. Pamoja na kuchunguza makinikia, Kamati pia ilichunguza shehena ya mbale za copper ndani ya makontena matano (5) yaliyozuiliwa bandarini. Sampuli za mbale hizo zilipatikana kuwa na viwango vya dhahabu hadi kufikia 38.3 g/t, viwango ambavyo havikuoneshwa kwenye ripoti ya upimaji wa kimaabara wa TMAA, na hivyo kutotumika katika kukokotoa malipo ya mrabaha Serikalini.”
Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini. (Ripoti ya Osoro na Mruma)

cc Nguruvi3
Pascal Mayalla said:
Mkuu J Mushi, kwanza naomba nikupe pole kwasababu hii hoja ya 50/50 ni complex issue ambayo
  1. Watanzania wengi hawaielewi kutokana na kutokuzoea biashara za hisa kwenye the corporate world. Sisi tumezoea simple business, this is corporate business.
  2. Sikulaumu wewe, kwasababu ile siku tunatangaziwa makubaliano haya pale Ikulu, hata chief negotiator wetu, Prof. Kabudi alikuwa hajui economic benefits, hivyo akatangaza kuwa tutagawa faida, profits na akamweleza rais Magufuli hivyo na rais Magufuli akalitangazia taifa, kuwa tutagawana faida 50/50.
  3. Faida ni profits inapatikana baada ya kutoa kodi zote, na gharama zote za uendeshaji. Faida hii inagawanywa kwa uwiano wa hisa, yaani shares ratio, hivyo kwenye mgawanyo wa faida, Barrick wenye 84% shares watapata 84% ya net profits na sisi Tanzania tutapata 16% ya net profits.
  4. Economic benefits ni manufaa ya kiuchumi, na sio CSR kama ulivyoeleza wewe, na huu ndio uthibitisho unajadili kitu usichokijua, sikuiti mjinga kwasababu kutojua kitu sio kosa, muhimu ni kama unajua kitu, muelimishe asie jua.
  5. CSR ni Community Social Responsibility ambayo wawekezaji wote, makampuni yote na wafanyabiashara wote wana wajibu wa kurejesha sehemu ya faida kwa jamii inayowazunguka. Hata mimi na kale kampuni kangu ka PPR, wakati wa maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane, huwa ninatengeneza faida kubwa, hivyo kurudisha kwenye jamii, huwa nafanya matangazo ya bure kwa wananchi wa kawaida ambayo yatalisaidia taifa.
  6. Economic benefits ni faida za kiuchumi zinazotokana na biashara husika. Hii inajumuisha faida zote ambazo Tanzania itapata kutokana na migodi hii, ambazo zinajuiisha kodi zote, royalties, CSR na ile 16% ya free carried shares zetu.
  7. Tunachogawana 50/50 ni economic benefits na sio net profits. Hivyo katika mgawanyo huo, namna ya kugawana ni kwanza kutoa gharama zote za uendeshaji na kodi zote za serikali. Kisha kutenga ile faida ya shares 84% ya Barrick na kuiweka pembeni.
  8. Unachukua ile faida ya shares zetu 16%, unajumlisha kodi zote, unajumlisha royalties, unajumlisha gharama zote za CSR, ukiisha pata unaweka pembeni.
  9. Kisha sasa unalinganisha kile kilichopatikana kwenye ile 84% ya shares za Barrick ambacho Canada anachukua, na kulinganisha na kile Tanzania tunachopata kwa ile 16% yetu, ukijumlisha na kodi zote za serikali, ukijumlisha na royalties, ukijumlisha na CSR.
  10. Ikitokea faida ya shares 84% ya Barrick ni kubwa kuliko Tanzania tulichopata, then inachukuliwa hesabu ya jumla ya faida yote ya ile 84% ya faida za shares za Barrick, unatoa mapato yote Tanzania tuliyofaidika nayo, kisha the difference ya mapato ya ziada ya Barrick, yanagawanywa pasu kwa pasu, 50/50, kati ya Tanzania na Barrick, kea Barrick kuimegea Tanzania kiasi za ziada ili kila mmoja awe amefaidika kwa 50/50.
NB. ili kuuelewa utaratibu huu, lazima uwe na kichwa chenye uelewa wa mahesabu ya kihivyo, bahati nzuri sana kwa Tanzania, rais Magufuli ni mtu mwenye kichwa cha uelewa huu, japo very unfortunately Mwalimu wangu Prof. Kabudi ambaye ni kichwa mbaya, GPA yake ya 4.9 pale UDSM bado inashikilia rekodi ya UDSM tangu kuanzishwa haijawahi kuvunjwa mpaka kesho, ila na yeye mwanzo hakujua tofauti ya economic benefits na profits, ila sisi wanafunzi wake tena wa PASS tuu, tulisaidia kupitia humu humu jf, na somo likaeleweka.
Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?.
https://www.jamiiforums.com/threads...da-ni-kweli-au-ni-changa-la-macho-tu.1472575/

Update: 22/8/2020
Baada ya hotuba hii ya Lissu, sasa nime connect the dots kuwa yote niliyosema ni ya kweli.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,059
2,000
Lugha tamu toka serikalini na wapambe wao-report wamefungia makabatini under lock and key. Professorial rubbish itabaki kuwa professorial rubbish. Kama makinikia yameruhusiwa kwenda kwa nini hatuambiwi nini na kiasi gani kiko ndani halafu tulinganishe. Ile report ya uchumi ilibase kwenye report ya kwanza Mruma? Sasa kama report ya kwanza haieleweki kitalaam basi ya pili Osoro imejengwa kwenye msingi hewa. Kutoka 1.9B hadi 300M-tutafakari.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
51,451
2,000
Wanajamvi, nadhani suala hili, halikuzungumziwa vya kutosha hata kidogo. Lissu yeye alishaumizwa na wengine walitishika kabisa kulizungumzia!

Hata hivyo, bado limezungumziwa sana na makada wa CCM hata humu ndani. Mfano kina Pasco! Lakini kwa namna ya uongo na propaganda nyingi.

Ripoti yenyewe imelalamika zaidi kuhusu kodi, na ikapendekeza uwepo uwajibikaji kwa watumishi mbali mbali wa ngazi tofauti za serikali kutokana na misamaha ya kodi kwa makampuni hayo!

Ya kuhusu makinikia, hapo hakukuwa na lolote! Hata kile ambacho kada maarufu wa chama humu Pascal Mayalla, alikuja na uongo mwingi sana humu kuhusu kile alichokiita “kishika uchumba”. Lakini ukifuatilia kwa makini, utagunduwa kuwa hata hicho kilicholipwa na Barick kwa niaba ya ACACIA, walilipa tu ili thamani ya hisa zao, isiendelee kushuka kwenye soko la dunia, pamoja na gharama zinazotokana na kuzuiwa kwa makontena hayo, habari kuwa yamezuiwa, ni mbaya zaidi kwa uchumi wa kampuni kuliko kuwndelea na kesi MIGA! Lakini hakuna nilichoona kwamba wamekubali kuwa wamefanya chochote kile kinyume na mkataba ambao ni CCM waliusaini.

Sitaki kuzungumza mengi, nitayaleta mapendekezo yote hapa, kisha tuyachambuwe, kwasababu uchaguzi umekaribia, sasa tujulishane ukweli ili tujuwe kama tuwape kura au tuwapumzishe.

Maana mojawapo ya mapendekezo, ni sisi kuifahamu mikataba, na wale walioisaini na kuipitisha, wawajibike, lakini naona usanii tu huku wapinzani wakisingiziwa na Lissu wa watu.

Pia kamati ilipendekeza kuwa “Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya waliokua mawaziri,wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba na makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya madini na watumishi wengine wote waliohusika katika kuingia mikataba ya madini.“
Maigizo tupu, kashateuliwa sasahivi hata copy ya hiyo report hana
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
51,451
2,000
Lugha tamu toka serikalini na wapambe wao-report wamefungia makabatini under lock and key. Professorial rubbish itabaki kuwa professorial rubbish. Kama makinikia yameruhusiwa kwenda kwa nini hatuambiwi nini na kiasi gani kiko ndani halafu tulinganishe. Ile report ya uchumi ilibase kwenye report ya kwanza Mruma? Sasa kama report ya kwanza haieleweki kitalaam basi ya pili Osoro imejengwa kwenye msingi hewa. Kutoka 1.9B hadi 300M-tutafakari.
Ili kuwa chuki binafsi hakuna kilichofanyika hata kimoja
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,806
2,000
Pia kamati ilipendekeza kuwa “Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya waliokua mawaziri,wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba na makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya madini na watumishi wengine wote waliohusika katika kuingia mikataba ya madini.“
Serikali ilifanya uchunguzi wa kina, waliokutwa na hatia walishitakiwa, wakakiri makosa, wakahukumiwa.
P
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom