Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?.

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,653
2,000
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kidogo, kuendelea na zile makala zangu za kwa maslahi ya Taifa. hii ni mada ya swali
Jee Wajua Kuwa Mazungumzo Yetu na Barrick Ni Mazungumzo Tuu? Mwenye Uamuzi wa Mwisho ni Acacia!, Kwa Nini Acacia Hawakushirikishwa?!. Jee Tutalipwa?.

Kwanza its sad kwa sisi Watanzania kupata update ya hatima ya rasilimali zetu, kutoka huko huko kwa hawa hawa mabwana wezi wa rasilimali zetu!. Mazungumzo yanafanyikia Dar es Salaam ndani ya Ikulu yetu, na tangu mwanzo ilielezwa msingi mkuu wa mazungumzo hayo ni trust, truthfulness na transparency, kwa nini sisi wenye rasilimali hizi hatupewi updates za kinachoendelea kwenye mazungumzo hayo?!, lakini wenzetu wako ulaya ndio wanatoa updates huko kwao kwenye tovuti zao!, what sort of transparency is this?!. Mazungumzo, Tanzania, updates Canada na London!, yaani sisi Watanzania ndio wenye rasilimali hizi, mazungumzo yanafanyikia ndani kwetu, lakini taarifa ya kinachoendelea ni mpaka tukakipate kwa wezi wetu?!. There is something wrong, somewhere kwa upande wetu!.

Umuhimu wa Tanzanian Updates.
Kwa vile mazungumzo haya ni kuhusu rasilimali zetu, mmiliki wa rasilimali hizi, yaani mwenye mali ni Mtanzania. Serikali yetu inafanya yote kwa niaba ya mwenye mali, Watanzania, hivyo ni muhimu kwa Watanzania tukapatiwa updates za kinachoendelea kutoka serikali yetu na sio kupokea updates za kutoka upande wa pili ili Watanzania tuwe well informed what's is going on to avoid surprises mwisho wa mazungumzo.

Lengo la Local Updates.
Lengo kuu la Watanzania kupatiwa local updates sambamba na hizo updates zao ni ili kujiridhisha, kinachoendelea kwenye mazungumzo hayo kinachoripotiwa na wazungu hawa ni cha kweli ndicho kilichokubaliwa na serikali yetu?, yaani we have to speak one language na sio sisi tunaelezwa hivi, halafu wao wanaeleza vile!.

Mkanganyiko Tangu Taarifa ya Mwanzo ya Makubaliano.
Kama mtakumbuka mara tuu baada ya makubaliano ya msingi, Watanzania tulitangaziwa na rais wetu na rais wa Barrick Gold, kilichokubaliwa. Rais wetu akitangaza kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuwa wamekubali watatulipa ila kiwango kitaamuliwa, lakini ili kuonyesha goodwill ya kutulipa, kwanza watatupatia Dola milioni 300 za nia njema, na rais akaonyesha furaha yake na kueleza jinsi tunavyozisubiri kwa hamu na shauku kubwa. Pia akaeleza wamekubali tutagawana faida pasu kwa pasu. Itaundwa kampuni mpya ambayo serikali itamiliki hisa za asilimia 16%. Waziri wa sheria Prof. Kabudi akafafanua jinsi tutakavyo faidika kwa 50/50 ya net profits baada ya kutoa kodi zote za serikali.
[/CENTER]
Lakini Rais wa Barrick alisema wamekubaliana tutagawana 50/50 ya economic benefits. Hii maana yake ni kwanza unaondoa operating costs, kisha tutagawana ile gross, hivyo ile 16% ya shares ukijumlisha kodi zote, kufikia 50%. Hii maana yake sisi tumeambiwa tunagawana faida, 50/50, mzungu anasema tunagawana economic benefits 50/50, ndani ya economic benefits, kodi zote na ile 16% ya free carried shares ni inclusive. Wote Barrick na Acacia wao wakapost kwenye website zao makubaliano hayo yakionyesha mgawo wa 50/50 ni economic benefits na sio net profits kama tulivyo elezwa. Huu tayari ni mkanganyiko, siku ya siku itambidi Prof. ameze maneno yake ya 50/50 net profits!. Hivyo ni muhimu kila kinachosemwa na wazungu hawa, kisemwe na viongozi wetu ili sote tujiridhishe kinachosemwa na wazungu hawa ndicho kinachoendelea, sio wenzetu wanatoa updates, sisi wenye mali kimya!.

Hata kwenye kushika uchumba cha dola milioni 300, boss wa Barrick kasema ni utanguluzi wa goodwill, Acacia kagoma na kusema watatulipa hiyo pesa baada ya kutoa madeni yote ya Vat refund wanaotudai!. Kama ni hivyo mnadani hapo kuna kitu tena?!. Tumeelezwa malipo yatakuwa siri!, siri for what wakati tulielezwa wazi kuwa tutalipwa!. Kishika uchumba hakiwezi kufanywa siri, lazima mwana mwali ajue na nduguze wajue ndipo wapange harusi.

Updates za mazungumzo.
Leo nimepata muda kufuatilia hatima ya mazungumzo kati ya serikali yetu ya Tanzania na Kampuni ya Barrick kuhusu hatma ya makinikia ya Acacia yaliyozuliwa, kupitia taarifa kwenye tovuti ya Barrick, mazungumzo yameelezwa kuwa yanaendele vizuri
Barrick Gold Corporation - Update on Discussions with Government of Tanzania

Acacia nao kwenye tovuti yao nao wameeleza kitu kile kile kilichoelezwa na Barrick
Press Release Item

Jambo la kwanza la maendeleo ya mazungumzo haya, ni mazungumzo yasiyo na time frame, yaani hayana muda maalum wa kumalizika na kufikiwa makubaliano!, mazungumzo ya aina hii ni mazungumzo gani yasiyo na SMART Objectives yanaendelea tuu na yanaweza yakaendelea tuu bila mwisho?!.

Barrick wametoa statement fupi ya page 1 yenye para 3 zenye lines 15 na maneno 146 lakini wakaweka angalizo lenye page 2, para 4 zenye lines 69 na maneno 775!. One has to be good kusoma hiyo statement together with angalizo kuelewa the motive behind.

Tukija kwa Acacia, wao wametoa tuu statement ya Barrick bila kuweka angalizo la pembeni ila wao wameweka msimamo wao wazi kuwa "The Company has been supporting Barrick in its discussions with the GoT, but has not been directly involved in those discussions to date. Any proposal received by the Company in the future that might be agreed in principle between Barrick and the GoT as a result of those discussions will be subject to review by the Independent Committee of the Acacia Board of Directors". Wanaunga mkono mazungumzo hayo lakini wao sio sehemu ya mazungumzo hayo na kwanza hawajahusishwa popote hadi leo, hivyo chochote kitakachofikiwa na mazunguzo hayo kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania, ni lazima kiridhiwe na kamati yao maalum!. Hii maana yake maafikiano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali yetu na Barrick sio final and conclusive, mwennye uamuzi wa mwisho ni Acacia!. Kama hali ni hii, kwa nini wanasheria wetu nguli na makini hawakuwahusisha Acacia kwenye mazungumzo haya ambao ndio the determinant ya utekelezaji wa makubaliano yoyote?. Jee mnatambua kuwa chochote ambacho serikali yetu itakubaliana na Barrick, hala Acacia wakakataa kutekeleza, hakuna kitu chochote ambacho tunaweza kuwafanya?.

Wakati mazungumzo yetu na Barrick yako kwenye dilly dallying, wenzetu Barrick wameelekeza macho na masikio yao China!,
"Barrick’s focus on China is real and deliberate.
Barrick’s focus on China is real and deliberate. In 2014, we created the position of President for Barrick China to manage our interests there. In 2015, we sold half of our ownership in the Porgera gold mine in Papua New Guinea and began joint operations with the buyer, Zijin, one of China’s big three gold miners. In 2017, we formed a 50-50 joint venture with Shandong Gold, another one of the big three, at the Veladero mine in Argentina. In addition, two of China’s largest banks—ICBC and China Construction Bank—have joined Barrick’s revolving credit facility, the first time either has forged such a relationship with a Western mining firm".

Hivyo mkisikia Barrick imeuza interest zao za Acacia kwa Wachina, naowaomba msishangae!, naamini wale "jamaa zetu" pia ni mingoni mwa watumishi wazelendo wa Acacia, hivyo wakiona ziara za makundi ya watu kutoka China huku wakiandamana na mabosi wa Barrick, waripoti haraka sana maana usikute ni ngombe wetu wa maziwa yuko mnadani!. Wazungu ambao ni watu wako very much time conscious, ukiona wanazungumza na wewe mazungumzo yasiyoisha bila kuonyesha time concern, kama wewe ni mtu unaejua kutazama mbali, ni lazima uogope!.

Swali la Msingi ni Jee Tutalipwa?.
Kwa mazungumzo ni siri, hakuna ajuaye ni nini kimekubaliwa na nini hakijakubaliwa, my honest opinion ni kuwa hatutalipwa!, hata kile kishika uchumba cha dola milioni 300, I doubt kama tutalipwa, kwa sababu the bone of contention, ni Tanzania kuibiwa kwenye makinikia kwa vile hatujui kilichomo!. Ili tujue kilichomo ni kama tuu tutayachenjua makinikia sisi wenyewe!. Sijawahi kusikia lolote kuhusu uchenjuaji wa makinikia yale, hivyo hata zile fedha za Noah zetu, zijui kama hata robo zitalipwa!.
A Way Forward.
Serikali yetu itoe updates za maendeleo ya mazungumzo na sio kuwaachia wazungu pekee ndio watoe updates zao.
na pili tuwe makini sana na wazungu hawa katika kutoa taarifa tumekubaliana nini, na sio mezani mnakubaliana hivi, wananchi wanatangaziwa, kisha mzungu analeta statement ya kitu tofauti, tumeelezwa tutagawana faida 50/50 wao wanaeleza tutagawana 50/50 za economic benefits.

Mpaka sasa Watanzania wanaamini hiki alichosema rais wetu, na ufafanuzi wa Waziri Prof. Kabudi, japo ni tofauti kabisa na kinachoandikwa na wazungu hawa, hivyo sisi kama Watanzania, tunamwaminia rais wetu, na kilichosemwa na Prof. Kabudi, sasa kama hawa wazungu wanasema tofauti, hayo ni yao.

Mazungumzo ni kati ya rais wa nchi yetu ambaye ndie mamlaka kuu kuliko zote nchini kwetu na Mwenyekiti wa Barrick Gold ambao ndio wamiliki wa Acacia. Waziri Kabudi na timu yake wako pale kwa niaba ya rais wetu, hivyo makubaliano yatakayo fikiwa yanapaswa kuwa final and conclusive!, iweje leo wazungu hawa wanasema chochote kitakachokubaliwa kati ya serikali yetu na Barrick ni subject to approval ya an independent board ya Acacia!. Who is Acacia ambaye is not part ya mazungumzo, ndie atakuja kuamua kutekeleza makubaliano hayo?!. Huku ni kumu undermine rais wetu!. Kama Acacia ndio determinant ya utekelezaji wa mazungumzo haya, namshauri rais wetu na Prof. Kabudi na team yake, wasikubaliane kwanza chochote mpaka wamwite Acacia mezani, akubali ndipo tutangaziwe, it's not too late, na kwa sababu mazungumzo haya hayana time frame, mwiteni Acacia hili jambo liishe kwa amani.

Lets hope for the best!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Rejea kuhusu makinikia

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300 - JamiiForums

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums"]

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!". - JamiiForums

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli? - JamiiForums

Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu. - JamiiForums

Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?. - JamiiForums

Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
 
Jurrasic Park

Jurrasic Park

JF-Expert Member
3,774
2,000
Alafu naskia makinikia yashaondoka cc Tundu Lissu

Huwezi kupambana na bepari maana kila hatua anayopiga ana utaalamu wa karne. Angalia mkonge baada ya nyerere kuleta za kuleta mkongo ukamuozea mpaka Jomo Kenyatta akasema kwamba anaongoza maiti.
 
K

KIBST

JF-Expert Member
517
1,000
Ishu si kulipwa TU...Ishu ni kwamba atleast tumeonyesha kuthamini RASILIMALI ZETU....tatzo sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana Tunakaa kusubiri kuona mambo yakiharibika tu tupate sehemu ya kusemea PUMBA zetu LAKINI hatutaki kabsa kupongeza hatua zilizo chukuliwa kuzuia KUIBIWA RASILIMALI ZETU na hawa mabwana wakubwa....Tumpongeze JPM kwenye hili jamani
Hata kama BARRICK anaenda kuuza hisa zake kwa hao WACHINA hii ni kwa sababu tu MIANYA YAO YA KIJINGA KUTUPIGA SISI WATANZANIA IMESHTUKIWA angethubutu vipi kuuza HISA ZAKE kama tusingemshtukia????Hata huyo mchina atakaekuja LAZIMA tuanze nae VIZURI
 
Slim5

Slim5

JF-Expert Member
25,064
2,000
Taarifa kwamba sintapata Noah, zimeniuma sana! Ndoto zangu zimeyeyuka! Najua ningepata Noah 4! Yangu, ya wife na za watoto wawili! Ningahamia Sanya Juu fasta! Mjini tena basi!
 
M

Massanda OMtima Massanda

JF-Expert Member
1,059
2,000
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kidogo, kuendelea na zile makala zangu za kwa maslahi ya Taifa. hii ni mada ya swali
Jee Wajua Kuwa Mazungumzo Yetu na Barrick Ni Mazungumzo Tuu? Mwenye Uamuzi wa Mwisho ni Acacia!, Kwa Nini Hakushirikishwa?!. Jee Tutalipwa?.

Kwanza its sad kwa sisi Watanzania kupata update ya hatima ya rasilimali zetu, ni kutoka huko huko kwa hawa mabwana wa rasilimali zetu, au wezi wetu!.

Leo nimepata muda kufuatilia hatima ya mazungumzo kati ya serikali yetu ya Tanzania na Kampuni ya Barrick kuhusu hatma ya makinikia ya Acacia yaliyozuliwa, kupitia taarifa kwenye tovuti ya Barrick, mazungumzo yameelezwa kuwa yanaendele vizuri
Barrick Gold Corporation - Update on Discussions with Government of Tanzania

Acacia nao kwenye tovuti yao nao wameeleza kitu kile kile kilichoelezwa na Barrick
Press Release Item

Jambo la kwanza la maendeleo ya mazungumzo haya, ni mazungumzo yasiyo na time frame, yaani hayana muda maalum wa kumalizika na kufikiwa makubaliano!, mazungumzo ya aina hii ni mazungumzo gani yasiyo na SMART Objectives yanaendelea tuu na yanaweza yakaendelea tuu bila mwisho?!.

Barrick wametoa statement fupi ya page 1 yenye para 3 zenye lines 15 na maneno 146 lakini wakaweka angalizo lenye page 2, para 4 zenye lines 69 na maneno 775!. One has to be good kusoma hiyo statement together with angalizo kuelewa the motive behind.

Tukija kwa Acacia, wao wametoa tuu statement ya Barrick bila kuweka angalizo la pembeni ila wao wameweka msimamo wao wazi kuwa "The Company has been supporting Barrick in its discussions with the GoT, but has not been directly involved in those discussions to date. Any proposal received by the Company in the future that might be agreed in principle between Barrick and the GoT as a result of those discussions will be subject to review by the Independent Committee of the Acacia Board of Directors". Wanaunga mkono mazungumzo hayo lakini wao sio sehemu ya mazungumzo hayo na kwanza hawajahusishwa popote hadi leo, hivyo chochote kitakachofikiwa na mazunguzo hayo kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania, ni lazima kiridhiwe na kamati yao maalum!. Hii maana yake maafikiano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali yetu na Barrick sio final and conclusive, mwennye uamuzi wa mwisho ni Acacia!. Kama hali ni hii, kwa nini wanasheria wetu nguli na makini hawakuwahusisha Acacia kwenye mazungumzo haya ambao ndio the determinant ya utekelezaji wa makubaliano yoyote?. Jee mnatambua kuwa chochote ambacho serikali yetu itakubaliana na Barrick, hala Acacia wakakataa kutekeleza, hakuna kitu chochote ambacho tunaweza kuwafanya?.

Wakati mazungumzo yetu na Barrick yako kwenye dilly dallying, wenzetu Barrick wameelekeza macho na masikio yao China!,
"Barrick’s focus on China is real and deliberate.
Barrick’s focus on China is real and deliberate. In 2014, we created the position of President for Barrick China to manage our interests there. In 2015, we sold half of our ownership in the Porgera gold mine in Papua New Guinea and began joint operations with the buyer, Zijin, one of China’s big three gold miners. In 2017, we formed a 50-50 joint venture with Shandong Gold, another one of the big three, at the Veladero mine in Argentina. In addition, two of China’s largest banks—ICBC and China Construction Bank—have joined Barrick’s revolving credit facility, the first time either has forged such a relationship with a Western mining firm".

Hivyo mkisikia Barrick imeuza interest zao za Acacia kwa Wachina, naowaomba msishangae!, naamini wale "jamaa zetu" pia ni mingoni mwa watumishi wazelendo wa Acacia, hivyo wakiona ziara za makundi ya watu kutoka China huku wakiandamana na mabosi wa Barrick, waripoti haraka sana maana usikute ni ngombe wetu wa maziwa yuko mnadani!. Wazungu ambao ni watu wako very much time conscious, ukiona wanazungumza na wewe mazungumzo yasiyoisha bila kuonyesha time concern, kama wewe ni mtu unaejua kutazama mbali, ni lazima uogope!.

Swali la Msingi ni Jee Tutalipwa?.
Kwa mazungumzo ni siri, hakuna ajuaye ni nini kimekubaliwa na nini hakijakubaliwa, my honest opinion ni kuwa hatutalipwa!, hata kile kishika uchumba cha dola milioni 300, I doubt kama tutalipwa, kwa sababu the bone of contention, ni Tanzania kuibiwa kwenye makinikia kwa vile hatujui kilichomo!. Ili tujue kilichomo ni kama tuu tutayachenjua makinikia sisi wenyewe!. Sijawahi kusikia lolote kuhusu uchenjuaji wa makinikia yale, hivyo hata zile fedha za Noah zetu, zijui kama hata robo zitalipwa!.

Lets hope for the best!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Ni sahihi na muhimu kupata mrejesho wa ni nini kinaendelea. Aidha sina uhakika ni kwa nini Acacia haikuhusishwa japo ilisemekana kwamba serikali haikuwa inaitambua jambo ambalo lina maswali mengi kuliko majibu.
Hata hivyo, naamini kwamba ama Barrick au Acacia pamoja na serikali yetu, wote wamepoteza kwani Buzwagi na Bulyahulu vimefungwa na hivyo wote kupoteza mapato (japo serikali inao unafuu kwani madini hayaozi).
Swali ambalo nabaki nalo ni, je, maazimio au ahadi zile za Barrick kuilipa serikali yanaweza kutumika kuishitaki Barrick au Acacia (kwa maana nyingine) kwenye vyombo vya sheria?
 
K

kipumbwi

JF-Expert Member
2,319
2,000
Kuna mtu aliwaita Barrick ni wezi,walipokuja Tanzania kuzungumza akawaita kuwa ni wanaume haswaa,wakajifungia ndani mmoja tukiambiwa mwanaume haswaa, mwingine hatukuambiwa ni nani haswaa!!

Matarajio ni mimba tu na kichefu chef!!
 
Mahesabu

Mahesabu

JF-Expert Member
5,321
2,000
Pale Mwandishi Nguli na Mwanasheria msomi anapochagua kutofuata weledi.

1. Audi Alteram Pat.......

2. Negotiations terms Pascal unazijua?????

3. Pascal hao acacia "wako" toka awali walikuwa wakitoa matamko yao yenye kuwapendeza waliopenda kuyasikia....na bado mazungumzo yaliendelea.....

"WAO NI AKINA NANI LEO, WAMFANYE MSOMI PASCAL AHADAIKE"?????
 
Forum statistics

Threads
1,424,577

Messages
35,067,415

Members
538,026
Top Bottom