Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

Mimi ni Muislamu LAKINI amini nakwambia achana kabisa na huyo mtu aitwae Yesu. He is something else.
Yesu atabaki kuwa Yesu.

Kuhusu Wayahudi kutokumkubali isikuchanganye SANA mkuu, hata Yesu mwenyewe alisha sema Nabii hakubaliki kwao.

Hapa tunachojadili ni hoja za Wayahudi wenyewe.
Yesu he is something else Kwa sababu umeshamezeshwa hivyo.
 
UNA UHAKIKA ZAMANI WALIKUWA WANAZALIWA BILA DHAMIRI KWAMBA KUNA MUUMBAJI NA SASA NDO WANA DHAMIRI YA KUMJUA MUNGU???
Bila shaka... Ndiyo maana katika kuongea nao Mungu alikuwa anaanza kwa kujitambulisha

Mimi ni MUNGU wa.... Niliye ku...

Lakini baada ya Yesu kila mtu anamjua Mungu wala haina haja ya kukaa ukafundishwa labda uamue kuviolate dhamiri yako njema mwenyewe.
Ila ki uhalisia UPENDO wa MUNGu tunazaliwa nao
 
Sema wayahudi/israel tuwape heshima yao Aisee...Ni kataifa kadogo sana na wala hakajawahi kutawala dunia, sanasana kenyewe ndiyo kalikuwa kanaonewa na kutawaliwa.
Lakini pamoja na hayo bado kamefanikiwa kutengeneza dini kuu 3 ambazo zinatawala dunia sasa (Uyahudi,Ukristo na Uislam)
Hivyo influence ya hako kataifa kadogo itadumu kuliko mataifa makubwa yaliyotawala dunia kama Ugiriki,Uyunani,Uajemi,Rumi,Uingereza,Ujerumani,USA nk. nk.

Ni kweli Kabisa.

Unakuta MTU anawachukia Wayahudi alafu ndani ya wiki akienda kuabudu lazima atajiwe Myahudi mmoja katika nyumba ya ibada anayoabudia
 
hoja zao zote ni za kijinga sana.

a) kwamba hakushusha utawala wa Mungu,hapa walirenga nini wakati Yesu amekuja kama Mungu akakaa kwetu,tukauona utukufu wa Mungu??walitaka Mungu ashushe malaika wawe wanajaeshi ama??

b)hakutokana na ukoo wa daudi lakini mama yake ni wa ukoo huo mariam,hawa wavuta bangi walitaka azaliwe masihi kutokana na wao halafu ashushe utawala wa Mungu,bangi ni janga.

c) masihi lazima warudishe waisrael wote waliotawanyika,hapa wanajipa umuhimu zaidi ya mataifa mengine mbele za Mungu,hata hapo walipo wamerudishwa kibabe aliyewarudisha ndiye masihi wao???ni nani??

d) magonjwa na taabu-hapa sio paradiso ni duniani magonjwa na taabu ziko pale pale,na kama hawatampokea hata huko paradiso watapasikia kwenye simu.
 
Sio kweli.wapo Watu hawaamini na hawajui kuwa kuna MUNGU.
Yaani hata hiyo dhana tuu ya Mungu hawajawahi hata kuisikia. Watu wa hivyo wapo.

Watu wangekuwa wanamjua Mungu tangu wakiwa wadogo zisingekuwepo Dini
Labda tunatofautiana kwenye dhana ya kumjua MUNGU ndio maana unadiriki kusema kuna watu wanazaliwa wakiwa hawamjui MUNGu, lakini ukweli ni kuwa kila mtu anamjua MUNGU hata bila kusikia habari zake.
Kumjua Mungu ni ile hali ya kuuishi upendo wa kristo katika maisha yetu. Maana nyepesi ni kufanya matendo yale unayopenda kufanyiwa.

Sasa hebu jiulize kama kuna mtu anazaliwa anapenda kuibiwa, kuchapiwa mke, mtoto wake kufanyiwa mapenzi kinyume na maumbile pamoja na maovu yote; Bila shaka hayupo.
Na kwa wale wanao fanya huo uovu wanafanya kwa kuenda kinyume na dhamiri za roho zao yani wanafanya huku wakijua kuwa wanafanya jambo lisilostahili kufanywa.

Kwa maana hiyo ya kumjua MUNGU basi kila mtu anazaliwa akiwa anamjua, bila kujali ataingia kanisani au la
 
Hapo unazungumzia Silika na hulka ambavyo having uhusiano wowote na mambo ya Kujua au kutokuijua(Akili au utashi)
Unaposema kujua, kufahamu au kuelewa unazungumzia AKILI.

Kitu ku-operate ndani ya mwili wako haimaanishi unakijua au kukifahamu kitu hicho.
Kwa mfano unaweza kuwa unaumwa Malaria lakini usijue kuwa ugonjwa unaokusumbua ni Malaria.

Mwanadamu amezaliwa akiwa na Akili ambayo haijui Jambo lolote lile, liwe jema au Baya.

Hata Adamu aliumbwa akiwa hajui jema na Mabaya.
Mbona useme kuwa Mwanadamu anazaliwa anamjua Mungu?
Ilhali Watu huzaliwa wakiwa hawajui Jambo lolote lile
 
Am.a muslim bro. Sijamezeshwa chochote na YOYOTE..I have experience.

Google uliza kwanini wasomi wa degree za juu kabisa za masonic wanamuita Yesu "Master Jesus*

Kutokana na Falsafa zake.
Lakini zaidi ya hapo hakuna ziada.
 
NITARUDI KUKUJIBU.

LAKINI WEWE MWEUPE SANA KWENYE BIBLE.

HUJASOMA VIZURI BIBLE, HUJASOMA DHAMBI, YANI KWA KIFUPI HUIJUI BIBLE.

Ila binafsi nimesoma sana sana sana Yesu.
Nimesoma Yesu kupita maelezo.

Yesu ni mwamba Mno.

Hakika nitarudi nijibu vi hoja vyako.
 
Sema wayahudi/israel tuwape heshima yao Aisee...Ni kataifa kadogo sana na wala hakajawahi kutawala dunia, sanasana kenyewe ndiyo kalikuwa kanaonewa na kutawaliwa.
Lakini pamoja na hayo bado kamefanikiwa kutengeneza dini kuu 3 ambazo zinatawala dunia sasa (Uyahudi,Ukristo na Uislam)
Hivyo influence ya hako kataifa kadogo itadumu kuliko mataifa makubwa yaliyotawala dunia kama Ugiriki,Uyunani,Uajemi,Rumi,Uingereza,Ujerumani,USA nk. nk.
Udhibitisho tafadhali
 
hoja zao zote ni za kijinga sana.

a) kwamba hakushusha utawala wa Mungu,hapa walirenga nini wakati Yesu amekuja kama Mungu akakaa kwetu,tukauona utukufu wa Mungu??walitaka Mungu ashushe malaika wawe wanajaeshi ama??

b)hakutokana na ukoo wa daudi lakini mama yake ni wa ukoo huo mariam,hawa wavuta bangi walitaka azaliwe masihi kutokana na wao halafu ashushe utawala wa Mungu,bangi ni janga.

c) masihi lazima warudishe waisrael wote waliotawanyika,hapa wanajipa umuhimu zaidi ya mataifa mengine mbele za Mungu,hata hapo walipo wamerudishwa kibabe aliyewarudisha ndiye masihi wao???ni nani??

d) magonjwa na taabu-hapa sio paradiso ni duniani magonjwa na taabu ziko pale pale,na kama hawatampokea hata huko paradiso watapasikia kwenye simu.

a) utawala wa MUNGU yupi ulishushwa na Yesu Mnazareth?
Unajua maana ya utawala wa MUNGU?
Achana na utawala wa Mungu, unaelewa maana ya utawala?

b) Kimaandiko na kinabii Ukoo hautoki Kwa Mwanamke/Mama Bali unatoka Kwa Mwanaume/Baba.
Hata hivyo hakuna ushahidi Mariam alitokea katika ukoo wa Daudi.

c) Wayahudi bado hawajarudi Israel, kuundwa Kwa taifa la Israel ni tofauti na kurudishwa Kwa waisrael katika nchi Yao.
Alafu usiseme wanajipa umuhimu kuliko mataifa mengine, sema Unabii ndio unawapa umuhimu kuliko mataifa mengine.

d) misheni ya Masihi ni kuondoa hayo magonjwa bila kujali ni paradiso au sio paradiso.

Hapa tunajadili Aya za Unabii sio porojo au maneno matupu.
 
NITARUDI KUKUJIBU.

LAKINI WEWE MWEUPE SANA KWENYE BIBLE.

HUJASOMA VIZURI BIBLE, HUJASOMA DHAMBI, YANI KWA KIFUPI HUIJUI BIBLE.

Ila binafsi nimesoma sana sana sana Yesu.
Nimesoma Yesu kupita maelezo.

Yesu ni mwamba Mno.

Hakika nitarudi nijibu vi hoja vyako.

Utamjua Yesu kuliko Wayahudi?
Utaijua Bible kuliko walioiandika na inayowazungumzia?

Hizo hoja niza Wayahudi, hivyo ukija ujibu hoja moja Baada ya nyingine.
Mimi nitakuwa upande wa Wayahudi katika Mjadala huu
 
Back
Top Bottom