Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

Huwa najiuliza hivi biashara kubwa kubwa za Edo mpaka kuonekana ana utajiri wa wizi zilikuwa ni zipi hasa?
Mkuu, umesahau alikuwa mkurugenzi wa Arusha International Conference Centre, na Waziri kwa miaka mingi sana kabla ya kugombea uraisi 1995? Kuna watu wanapewa ukurugenzi au uwaziri miaka mitatu tu na wanabadilika kabisa katika hali yao ya kifedha. Kuna namna, sio lazima uibe hela ya serikali. Leo hii ukiambiwa tunakupa kazi utununulie magari 100 tu wizara ya kilimo tayari unaweza kuwa bilionea, au kivuko cha kigamboni.
 
Hivi ulimfahamu Nyerere wewe, yule ambae aliimbisha watu kiongozi asiwe na nyumba ya kupangisha, asiwe na mishahara miwili, ungetegemea aruhusu tajiri Lowasa awe raisi, na akijua utajiri wa Lowasa haukutokana na biashara? Kumbuka tunaongelea 1995, ambapo matajiri Tanzania walikuwa watu kama Lowasa
Alikuwa na roho mbaya huyo babu yenu
 
Hakuna niliposema kosa la Lowasa lawama kwa Samia. Nimelinganisha hali ya wakati huo na sasa, kwa sababu wapo wanaoona Lowasa wakati huo alionewa, kwa sababu tu wanai-reflect hali ya wakati huo chini ya influence ya Nyerere wakitumia context ya sasa chini ya influence ya Samia. Inabidi uolewe uandishi katika comparative contexts

Na pia uelewe kwamba wewe unachoona ni rushwa labda aliyofanya Lowasa wakati huo, kwa sasa ndio kile kimehalalishwa kuwa ni kula kwa urefu wa kamba yako, na hili limehalalishwa na mamlaka ya juu kabisa nchini - raisi, bila kutolewa ufafanuzi. So anything goes.
Mada yako ingekuwa na mantiki kama ungelinganisha na EL kukataliwa na CC ya CCM mwaka 2015. Habari ya Samia usingeiingiza hapa.
 
Huu msiba umetubless wale wa upande mwingine ihiiiiiiii,,,, naona JF sasa imetawaliwa na thread za machawa wa msoga na monduli,,,acha tupate burudani
 
...... Kwa hili samia alionyesha hafai kua rais wa jamhuri....... ......Heshima yake itakua kuhakikisha nchi inapata kiongozi aina ya jpm 2025.
Kama hafai kuwa Raisi kwa kuhalalisha watu kufanya ufisadi kwa vile yeye mwenyewe ni fisadi, ni kwa nini unaona anaweza "hakikisha nchi inapata kiongozi aina ya jpm 2025' ????

Halafu kwa nini unataka Rais anaeondoka madarakani ndio akuchagulie Rais ajaye ? Nini maana ya kufanya uchaguzi na kubadilsha viongozi kila baada vipindi fulani kama unataka akili za yule yule aliyekuwepo ndio akuchagulie mrithi? Hivi chui akizeeka anaweza kupendekeza Twiga amrithi madaraka yake mbugani ?

Watanzania tumepikwa tukaiva U-third world wa utawala wa ki-Chifu Chifu. Tumeiva tepe tepe! Mmedanganywa miaka nenda rudi mpaka mkaamini kwamba Rais ndio anapaswa kuchagua Rais, masikini ya Mungu ..... daaaaah.... inauma vibaya sana. Julius Nyerere alianzisha hii trend alipom handpick Ally Mwinyi, right, lakini kuna mambo Baba wa Taifa alikosea jamani, na akaseme kuna ya kijinga tukiyaona tusimfatishe, aliyaita ya kijinga, au hakusema hivyo jamaniii ?????
 
Mada yako ingekuwa na mantiki kama ungelinganisha na EL kukataliwa na CC ya CCM mwaka 2015. Habari ya Samia usingeiingiza hapa.
Mada yangu nimesema inahusu watu wa sasa kuona Lowasa alionewa tangu ile 1995 kwa tuhuma za ufisadi, na kisha na Kikwete 2015. Sasa kwa sababu lengo ilikuwa kujibu hoja ya kwamba alionewa kuwa fisadi na kukataliwa uraisi 1995, ndio maana nikasema mnapaswa muelewe context ya ufisadi ya 1995 chini ya inflence ya Nyerere na context ya sasa chini ya Samia. Na nikzidi kuwaelimisha watu kwamba msimsafishe Lowasa 1995 kwa kutumia context ya sasa ya Samia. In fact, kwa namna Samia alivyo, Nyerere angemkataa Samia kuwa raisi wa Tanzania zaidi ya alivyomkataa Lowasa
 
Nyerere aliongoza watu milioni 20 na sio zaidi Samia anaongoza watu milioni 63.

Wakati wa Mwalimu chuo kikuu kilikuwa kimoja tu na mtu akimaliza masomo anaikuta kazi inamsubiri wakati huu wa Samia akili kichwani mwako, usipokuwa mtundu na mbunifu utakula jeuri yako.
 
Mada yangu nimesema inahusu watu wa sasa kuona Lowasa alionewa tangu ile 1995 kwa tuhuma za ufisadi, na kisha na Kikwete 2015. Sasa kwa sababu lengo ilikuwa kujibu hoja ya kwamba alionewa kuwa fisadi na kukataliwa uraisi 1995, ndio maana nikasema mnapaswa muelewe context ya ufisadi ya 1995 chini ya inflence ya Nyerere na context ya sasa chini ya Samia. Na nikzidi kuwaelimisha watu kwamba msimsafishe Lowasa 1995 kwa kutumia context ya sasa ya Samia. In fact, kwa namna Samia alivyo, Nyerere angemkataa Samia kuwa raisi wa Tanzania zaidi ya alivyomkataa Lowasa
Nyerere angekuwepo leo angekuwa ni mzee wa miaka 102 asingekuwa na nguvu ya kuhudhuria vikao vya CCM achilia mbali kuwa na akili yenye uwezo wa kuichagulia TZ yenye watu milioni 63 nani aiongoze.

Mambo ya 1995 yameshapoteza kabisa mantiki leo hii 2024.
 
Juzi hapa niliweka thread JF iliyosema wengi wa matajiri wa Tanzania ni wanasiasa na sio wafanya biashara, nikiwa na maana kwamba utajiri wao haujatokana na kufanya biashara bali umetokana na nafasi zao za kisiasa au uongozi serikalini kujitajirisha - urefu wa kamba zao. Kwa wengi wetu huo ni ufisadi.

Sasa hili kiongozi wa kisiasa au serikali kujitajrisha kutokana na nafasi yake, Raisi Samia alilihalalisha pale aliposema mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. Kila mtu anajua kwamba urefu wa kamba aliousema Samia sio mashahara, basi ni nafasi mtu anazopata kutokana na nafasi yake.

Sasa, mara ya kwanza Lowasa alipotaka kugombea uraisi, mwaka 1995, alikuwa tayari ni mtu tajiri sana tu. Aliweza hata kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini kwa ndege ya kukodi. Na Lowasa hakuwahi kuwa mfanya biashara, na hivyo utajiri wake kwa kiasi kikubwa ulitokana na nafasi za uongozi alizokuwa amekuwa nazo hadi wakati huo - urefu wa kamba yake! Hilo lilimtatiza sana Nyerere, na hakuwa tayari kumruhusu mtu wa namna hiyo kuwa raisi wa Tanzania.

Hali siku hizi ni tofauti sana, hasa chini ya uongozi wa raisi Samia. Kimsingi Samia amehalalisha wanasiasa na viongozi wa serikali kutumia nafasi zao kujitajirisha, na wanapojitajirisha hauwaulizwi maswali yeyote! Katika hizi enzi, utajiri wa Lowasa kuwa ulitokana na nafasi za uongozi serikalini usingekuwa tatizo kwake kuwa raisi wa Tanzania! Hizi sio enzi za Nyerere tena.

Nyerere alijua wazi jambo moja ambalo labda Samia halielewi, kwamba katika nchi zote, watu wenye "kamba" za kuwaruhusu kula huwa si zaidi ya 10% ya raia wote nchini. Yaani wafanyakazi wa mshahara katika nchi huwa hawazidi 10% ya idadi ya raia nchini!

Samia alipotoa kauli ya mtu kula kwa urefu wa kamba yake, kuna watu niliwaambia kauli hiyo kimsingi ilitolewa ili kuhalalisha jambo ambalo Samia mwenyewe aliona anawezwa kusutwa nalo- yeye binafsi kula kwa urefu wa kamba yake ya urais, na hivyo akaona akisema kila mtu afanye hivyo basi hakuna atakaemshangaa yeye akifanya hivyo. Niliwaeleza watu kuwa, Samia anafanya hivi si kwa sababu yeye ni fisadi, bali ni jambo la kawaida katika tamaduni za kiarabu ambazo Samia ana asili nazo - kula kwa urefu wa kamba yako, na hata kuwalisha wanaokuzunguka!

Na of course, hilo pia watu wanapaswa kuelewa kwanini labda Wazanzibari kipindi hiki wamepata nafasi nyingi upande wa bara. Ni kawaida ya "nepotism" ambayo inatokana na tamaduni za kiarabu, kusaidia wale ambao unaona ni ndugu zako zaidi kuliko wengine. Sasa mindset zinazotokana na desturi za society, ni vigumu sana kumbadilisha mtu, na Watanzania wanapaswa kulielewa hilo, na kulivumilia kwa sasa.

Kwa mtu mwenye asili ya tamaduni za kiarabu, ukiwa na nafasi kama ya uraisi, basi utahakikisha watoto wako, wajomba, mashemeji, wakwe zako na ndugu zao, na hata rafiki za watoto wako, nk, wote wanafaidika na hata kutajirika na nafasi yako. "Nepotism" katika culture ya kiarabu, ambayo Samia inamhusu, ni jambo la kawaida, hawalionei aibu! Angalia katika serikali za kiarabu, uone nani wanapewa nafasi za uongozi wa nchi, nani ni matajiri - karibu wote wanakuwa ni wanaukoo!

Kwa mfano, ni rahisi sana kwa upande wa Zanzibar watoto wa maraisi waliopita nao pia kuja kuwa maraisi - na tumeliona hili tayari. Sintashangaa huko mbele mtu kutoka familia ya raisi Samia kuja kuwa raisi wa Zanzibar. Hii ni sehemu ya tamaduni za kiarabu, kurithishana au kupeana madaraka ndani ya ukoo. Nimeona baadhi ya Watanzania bara kuanza kuiga hii culture, kuwaandaa watoto wao kuja kuwa viongozi upande wa bara. Niwaonye mapema, huenda hili linakubalika upande wa Zanzibar kutokana na silka za kiarabu, lakini kwa bara litatuletea matatizo!
Kosa la Lowassa kuwa mlutheri tu......hizo zingine zote ni ngonjera
 
Alikuwa na roho mbaya huyo babu yenu
Babu yetu alikuwa na moyo safi sana. Amini nakuambia, kwa namna Samia alivyojionyesha, Nyerere asingekubali NEC imputishe 2025. Yaani hafikii hata points za Lowasa za 1995. Utasemaje vitu kama kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake na wewe ni raisi wa nchi? Unahalalisha ufisadi kwa wachache walio na nafasi?
 
Nyerere angekuwepo leo angekuwa ni mzee wa miaka 102 asingekuwa na nguvu ya kuhudhuria vikao vya CCM achilia mbali kuwa na akili yenye uwezo wa kuichagulia TZ yenye watu milioni 63 nani aiongoze.

Mambo ya 1995 yameshapoteza kabisa mantiki leo hii 2024.
Enyi watu wa kizazi hiki kiovu mnaoona kupewa kuongoza kitengo chenye mianya ya rushwa ni kuukata! Ipo siku ya mapinduzi inakuja mbele yenu, mtalia kilio cha mbwa koko aliepigwa!
 
Juzi hapa niliweka thread JF iliyosema wengi wa matajiri wa Tanzania ni wanasiasa na sio wafanya biashara, nikiwa na maana kwamba utajiri wao haujatokana na kufanya biashara bali umetokana na nafasi zao za kisiasa au uongozi serikalini kujitajirisha - urefu wa kamba zao. Kwa wengi wetu huo ni ufisadi.

Sasa hili kiongozi wa kisiasa au serikali kujitajrisha kutokana na nafasi yake, Raisi Samia alilihalalisha pale aliposema mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. Kila mtu anajua kwamba urefu wa kamba aliousema Samia sio mashahara, basi ni nafasi mtu anazopata kutokana na nafasi yake.

Sasa, mara ya kwanza Lowasa alipotaka kugombea uraisi, mwaka 1995, alikuwa tayari ni mtu tajiri sana tu. Aliweza hata kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini kwa ndege ya kukodi. Na Lowasa hakuwahi kuwa mfanya biashara, na hivyo utajiri wake kwa kiasi kikubwa ulitokana na nafasi za uongozi alizokuwa amekuwa nazo hadi wakati huo - urefu wa kamba yake! Hilo lilimtatiza sana Nyerere, na hakuwa tayari kumruhusu mtu wa namna hiyo kuwa raisi wa Tanzania.

Hali siku hizi ni tofauti sana, hasa chini ya uongozi wa raisi Samia. Kimsingi Samia amehalalisha wanasiasa na viongozi wa serikali kutumia nafasi zao kujitajirisha, na wanapojitajirisha hauwaulizwi maswali yeyote! Katika hizi enzi, utajiri wa Lowasa kuwa ulitokana na nafasi za uongozi serikalini usingekuwa tatizo kwake kuwa raisi wa Tanzania! Hizi sio enzi za Nyerere tena.

Nyerere alijua wazi jambo moja ambalo labda Samia halielewi, kwamba katika nchi zote, watu wenye "kamba" za kuwaruhusu kula huwa si zaidi ya 10% ya raia wote nchini. Yaani wafanyakazi wa mshahara katika nchi huwa hawazidi 10% ya idadi ya raia nchini!

Samia alipotoa kauli ya mtu kula kwa urefu wa kamba yake, kuna watu niliwaambia kauli hiyo kimsingi ilitolewa ili kuhalalisha jambo ambalo Samia mwenyewe aliona anawezwa kusutwa nalo- yeye binafsi kula kwa urefu wa kamba yake ya urais, na hivyo akaona akisema kila mtu afanye hivyo basi hakuna atakaemshangaa yeye akifanya hivyo. Niliwaeleza watu kuwa, Samia anafanya hivi si kwa sababu yeye ni fisadi, bali ni jambo la kawaida katika tamaduni za kiarabu ambazo Samia ana asili nazo - kula kwa urefu wa kamba yako, na hata kuwalisha wanaokuzunguka!

Na of course, hilo pia watu wanapaswa kuelewa kwanini labda Wazanzibari kipindi hiki wamepata nafasi nyingi upande wa bara. Ni kawaida ya "nepotism" ambayo inatokana na tamaduni za kiarabu, kusaidia wale ambao unaona ni ndugu zako zaidi kuliko wengine. Sasa mindset zinazotokana na desturi za society, ni vigumu sana kumbadilisha mtu, na Watanzania wanapaswa kulielewa hilo, na kulivumilia kwa sasa.

Kwa mtu mwenye asili ya tamaduni za kiarabu, ukiwa na nafasi kama ya uraisi, basi utahakikisha watoto wako, wajomba, mashemeji, wakwe zako na ndugu zao, na hata rafiki za watoto wako, nk, wote wanafaidika na hata kutajirika na nafasi yako. "Nepotism" katika culture ya kiarabu, ambayo Samia inamhusu, ni jambo la kawaida, hawalionei aibu! Angalia katika serikali za kiarabu, uone nani wanapewa nafasi za uongozi wa nchi, nani ni matajiri - karibu wote wanakuwa ni wanaukoo!

Kwa mfano, ni rahisi sana kwa upande wa Zanzibar watoto wa maraisi waliopita nao pia kuja kuwa maraisi - na tumeliona hili tayari. Sintashangaa huko mbele mtu kutoka familia ya raisi Samia kuja kuwa raisi wa Zanzibar. Hii ni sehemu ya tamaduni za kiarabu, kurithishana au kupeana madaraka ndani ya ukoo. Nimeona baadhi ya Watanzania bara kuanza kuiga hii culture, kuwaandaa watoto wao kuja kuwa viongozi upande wa bara. Niwaonye mapema, huenda hili linakubalika upande wa Zanzibar kutokana na silka za kiarabu, lakini kwa bara litatuletea matatizo!
Umeandika ujinga mtupu. Jiulize yule Dudley alishafanya biashara wapi hadi kumiliki gazeti la Tanzania Daima na jumba Mikocheni? Hao tunaowaona malaika ndo mafisadi wa hatari. CHADEMA ikichukua nchi sio tutasikia Dudley ni shareholder wa migodi ya madini na mmiliki wa majengo city centre?
 
Enyi watu wa kizazi hiki kiovu mnaoona kupewa kuongoza kitengo chenye mianya ya rushwa ni kuukata! Ipo siku ya mapinduzi inakuja mbele yenu, mtalia kilio cha mbwa koko aliepigwa!
Mkuu hizo ni ndoto za mkosaji tu, Mbowe alikuwa mwnaharakati anatisha watu kwa makala zake za gazeti la Tanzania Daima miaka ya 2000 katikati leo hii anaitwa ikulu na analamba asali kama kawaida.
 
Kwa hiyo nyerere alikuwa anamuogopa Lowassa?
Alijuaje mtu kajitajirisha kwa wizi ampe adhabu ya kutogomea Urais badala ya kumfukuza CCM au ashawishi Serikali imuweke ndani. Kunauwezekano jamaa alikuwa a mpunga halali kitambo.
 
Back
Top Bottom