Rwanda ifikapo 2026 watakuwa na umeme wa nyuklia wa bei nafuu na uhakika. Sisi tunashindwa nini wakati madini ya nyuklia tunayo kibao?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,954
4,327
Jirani zetu Rwanda wameanza ujenzi wa vinu vya kisasa vya nuclear ambavyo ifikapo mwaka 2026 vitakuwa vinazalisha umeme wa uhakika wa bei nafuu. Vinu hivi vitazalisha pia mafuta na bidhaa nyingine. Vitaiwezesha Rwanda kuwauzia umeme nchi jirani kama Tanzania.

Sisi tuna madini ya nuclear kibao. Tunashindwa nini kuzalisha umeme wa nuclear na badala yake kuhangaika na vimiradi vya umeme wa jua, upepo na joto ardhi ambavyo haviwezi kuzalisha umeme mwingi na ujenzi wake una gharama kubwa na hivyo kufanya umeme utokanavyo na vyanzo hivyo kuwa wa bei kubwa sana.

Hili Naibu Waziri Mkuu alale nalo mbele ili Raisi wetu aache legacy yake, SSH Nuclear Plants.
 
Sisi miongozi yetu mijizi, haina vision ya maendeleo zaidi ya kuiba..

Yote 9, 10 hivyo vinu watawekana mtoto wa mjomba na shangazi bila kujali UJUZI matokeo yake ni ajari kubwa mnooo, nuclear si mchezo.
 
Sina imani kama Rwanda wanaweza fanikisha azimio hili mwaka 2026. Nuclear reactor ya gharama nafuu inahitaji zaidi ya trilioni 2.5 za kibongo na unazalisha around 300MW ambazo zitaitosheleza kabisa Rwanda maana kwa sasa hawafikishi 350MW.

Miaka fulani lengo lao lilikuwa kuwa na karibia 600MW kabla ya 2025 nadhani ndio katika harakati za kufikia malengo hayo.

Na hizo gharama zinaweza zidi sababu hawana miundombinu wezeshi ndio kwanza waanzisha sekta ya nyuklia. Sasa kwa bajeti yao ni mradi mzito kidogo kwa miaka michache hii.
 
Acha uwongo, mura! A typical nuclear reactor plant (kinu kimoja cha nyukilia) produces 1 gigawatt (GW) of electricity. Na kwa kuwa uranium ni ya kwetu, hatuinuni, bei ya kujenga kinu kimoja siyo kivile. Ni rahisi kuliko ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere.

Kama Rwanda ambao hawana madini ya nyukilia wameweza, kwa nini sisi tuliyo na madini haya tushindwe?

Tulipaswa hadi sasa kuwa na vinu visivyopungua 10, kila kimoja kikizalisha 1 GW za umeme wenye very low maintenance cost, usiochafua mazingira na wa uhakika (very reliable).
 
hv kwa akili yako broo unajua wezi wapo nishati tu...?? yani sasa hv ni chukua chako mapema kula ila usivembewe
Hao wengine ni wadokozi tu na ni rahisi kuwadhibiti. Wezi hawawezi kuisha hapa duniani. Walianza Adamu na Eva walipoiba lile tunda la mti wa kati kwenye ile bustani ya Adeni.
 
N
Acha uwongo, mura! A typical nuclear reactor plant (kinu kimoja cha nyukilia) produces 1 gigawatt (GW) of electricity. Na kwa kuwa uranium ni ya kwetu, hatuinuni, bei ya kujenga kinu kimoja siyo kivile. Ni rahisi kuliko ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere. Kama Rwanda ambao hawana madini ya nyukilia wameweza, kwa nini sisi tuliyo na madini haya tushindwe? Tulipaswa hadi sasa kuwa na vinu visivyopungua 10, kila kimoja kikizalisha 1 GW za umeme wenye very low maintenance cost, usiochafua mazingira na wa uhakika (very reliable).
Ni type gani ya nuclear reactor inayotoa 1GW inakuwa ya gharama nafuu, na hiyo gharama nafuu ndio kitu gani in numbers.

Nimekutajia small modular rector au mini reactor ambayo range yake ni hapo 300MW. Ziliwahi kuwepo za chini ya hapo hata 20MW ila kiuchumi angalau 300MW ndio viable. Wewe unataka 1GW ambayo Rwanda hawana uwezo wa kujenga hata washinde njaa miaka mitatu.

AP300 ya Marekani inagharimu $1 billion ni ya 300MW.
BWRX-300 ya Hitachi na General Electric gharama ni $1.5 billion na inatoa 300MW.

Ukitaka mambo makubwa ya 1GW tafuta mfano wa deal la Russia na South Africa ambapo mradi wa SA ni dola bilioni 50 tena hapo ni Russia ambao reactors zake ni za bei nafuu kidogo. Unadhani nishati ya nyukilia ni matako kwamba kila mtu anayo.
Hao Rwanda wanajenga 1GW reactor ya nini wakati lengo lao wafike 600MW kasoro na sasa wana zaidi ya 300MW.
 
Tofauti ya Wanyarwanda na sisi ni kwamba Wanyarwanda wana akili sisi ni mazuzu ambayo viongozi wake yanayowaza kuwalipa posho wake/waume wao badala ya kutumia pesa hizo kwenye mambo ya msingi ya kusaidia umma.

Usimlinganishe mtu mwenye akili kama Kagame na hawa mbumbumbu wa CCM
 
Jirani zetu Rwanda wameanza ujenzi wa vinu vya kisasa vya nuclear ambavyo ifikapo mwaka 2026 vitakuwa vinazalisha umeme wa uhakika wa bei nafuu. Vinu hivi vitazalisha pia mafuta na bidhaa nyingine. Vitaiwezesha Rwanda kuwauzia umeme nchi jirani kama Tanzania.

Sisi tuna madini ya nuclear kibao. Tunashindwa nini kuzalisha umeme wa nuclear na badala yake kuhangaika na vimiradi vya umeme wa jua, upepo na joto ardhi ambavyo haviwezi kuzalisha umeme mwingi na ujenzi wake una gharama kubwa na hivyo kufanya umeme utokanavyo na vyanzo hivyo kuwa wa bei kubwa sana.

Hili Naibu Waziri Mkuu alale nalo mbele ili Raisi wetu aache legacy yake, SSH Nuclear Plants.
Bullshit.
 
Kagame ni Rais mwenye maono,uthubu na akili nyingi.
Marehemu Magufuli alilijua hilo, akafanya naye urafiki mara tu alipochaguliwa kuwa rais na akajifunza kwake. Safari yake ya kwanza nje ya nchi ilikuwa Rwanda. Baada ya muda mfupi alibobea hadi kumpita mwalimu wake (Kagame). Staili ya utawala wao ulikuwa unafanana sana na wote wawili walikuwa hawampendi Kikwete.
 
Back
Top Bottom