Ufumbuzi wa kudumu kuhusu changamoto ya nishati ya umeme hapa Tanzania

Nov 16, 2023
14
22
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Kuhusu changamoto ya Nishati Ya Umeme, Hapa nyumbani TANZANIA, na ufumbuzi wa kidumu, ili Tatizo hili liwe HISTORIA, NAOMBA KUSHAURI yafuatayo, kwa mpendwa wetu, Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kuwa;

1. Tuthubutu Sasa, Kutumia vyanzo vingine vya UZALISHAJI WA UMEME, kama; Gesi YETU Ya asilia inayovunwa Kusini mwa Tanzania, Nishati Jua, UPEPO, Joto ardhi, MAWIMBI YA BAHARI, MAKAA YA MAWE, Mvuke, Na Uranium....
Mikoa ya Rukwa na Katavi, imebarikiwa Sana Na uwepo wa madini Ya URANIUM, Ambayo Ni malighafi Bora Sana Duniani kwa UZALISHAJI wa UMEME, Ambao ; Ni Nafuu katika UZALISHAJI Na Uendeshaji.

Tutakapo zalisha Umeme kwa Kutumia Uranium, Bei Yake inakuwa NAFUU kwa; MLAJI, MTEJA au mwananchi wa Kawaida Na kuyafanya MAISHA kuwa Nafuu...

2. Tunaweza kuwaalika wawekezaji walio endelea Kiteknolojia, Hasa katika UZALISHAJI wa UMEME kwa Kutumia Uranium... Kama; CHINA, JAPAN, URUSI, UJERUMANI, MAREKANI, NA INDIA ili waje Kuwekeza na Kutujengea VINU Vya NYUKLIA VYA KUZALISHA UMEME. Hapa nyumbani TANZANIA.

3. VINU VYA KUZALISHA UMEME kwa Kutumia Joto Ardhi VIJENGWE MBEYA, eneo linalotoa Joto ardhi. Na Wachina ndiyo Wataalamu SAHIHI eneo Hili.

4. Kuhusu KUZALISHA wa UMEME kwa Kutumia; MAWIMBI YA BAHARI. Wataalamu wazuri na sahihi, eneo watakaofaa katika Kutujengea MIUNDOMBINU YA KUZALISHA UMEME, Juu Ya Uso wa bahari....... Surface of the deep. Ni WAJERUMANI..

5. KUHUSU VINU VYA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA GESI, Nashauri Kuwa; Wataalamu SAHIHI eneo Hili Ni Wachina.

Mheshimiwa Rais NAOMBA Kutoa hoja Hii kwako kua Tukitumia vyanzo hivyo HAPO Juu katika KUZALISHA UMEME... Tutakuwa na Umeme mwingi Sana, kuliko Nchi yoyote Afrika. TUTAUUZA UMEME HUO WA ZIADA AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI, Na Kuimarisha Sana Pato la Taifa. Hii itavutia wawekezaji WENGI Duniani, kuja kujenga VIWANDA, maana Bei Ya Umeme itakuwa Nafuu SANA!.

_______________________________
kazi iendelee.......
______________________________;
JORDAN TWARINDWA
0689496679
 
Back
Top Bottom