Dereva wa Magari ya Watalii, Omari Msamo adaiwa kuuawa na askari wa jeshi la Polisi

Zombieboss

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
727
741
1000014912.jpg

Mwananchi mwenzetu na aliyekuwa dereva wa magari ya watalii, Omari Msamo ameuawa na askari wa Jeshi la Polisi, Wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha.

Omari Msamo ameuawa baada ya kusimamishwa na kushushiwa kipigo kizito kilichopelekea kutoa uhai wake na polisi wa usalama barabarani baada kutuhumiwa kuendesha gari akiwa ametumia kilevi.

Jeshi la Polisi linatumia kila jitihada kuzuia vyombo vya habari kuripoti tukio hili Kama njia ya kuficha na kuwanusuru askari wake dhidi ya mkono wa sheria.

====

UPDATE 1

JamiiForums imefanya jitihada za kutafuta upande wa Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo ambaye simu yake haikupokelewa.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na familia ya marehemu zimeeleza kuwa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Tamko la Hospitali
Akielezea kinachoendelea Mganga Mfawidhi Wa Hospitali ya Mount Meru, Dkt. Alex Ernest amesema:

Mwili upo hapa hospitali, taratibu nyingine zinazoendelea ni masuala ya Kipolisi, Hospitali haina mamlaka ya kuutoa mwili ambao una kesi Polisi.

“Hapa uliletwa mwili ambao tayari ulishakufa, bado hatujafanya toxicology study ambayo inaweza kukupa majinu ya mtu amekufaje kama ni sumu au ulevi au sumu nyingine yoyote iliyohusika, siwezi kusema chochote na hatujatoa tamko lolote ‘public’.

“Mwili uliletwa na ndugu zake nadhani juzi (Machi 18, 2024), sikuwepo eneo la tukio lakini nilitewa ripoti kama kiongozi.

“Sijaenda kwenda details ya suala hilo lakini ripoti niliyonayo ni kuwa mwili upo, uchunguzi wa kidaktari unaendelea na tukikamilisha tutatoa ripoti ya kitaalam kuhusu tulichobaini kwenye mwili lakini suala kwamba chanzo cha kifo au nini kilitokea huko alipokuwa ni suala la Polisi.”

=====

UPDATE 2: Taarifa ya Jeshi la Polisi

Tukio la kifo cha Omar Saimon Msami ambaye taarifa zake zimeonekana kusambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii lililotokea Karatu Mkoani Arusha lilianza kufanyiwa uchunguzi tangu liliporipotiwa kutokea Machi 16, 2024.

Kutokana na mazingira ya tukio hilo, Jeshi la Polisi liliona umuhimu wa kushirikisha wataalamu mbalimbali hasa wanaochunguza matukio ya vifo na baadhi ya wanandugu kulingana na uhitaji wa uchunguzi

Imebidi kufanya hivyo kutokana na mtitiriko wa maeneo aliyotembelea baada ya kuwarudisha wageni wake maeneo waliotakiwa kulala jioni ya Machi 15, 2024.

Uchunguzi unaofanywa na wataalamu utakapokamilika na ushahidi ukibainisha kifo kimesababishwa na mtu yeyote yule hatua za kisheria zitachukuliwa bila kujali cheo chake na nafasi yake katika jamii.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

GJHJ2DiXsAArrLk.jpg
 
Je, ipi ni Taarifa kamili kuhusiana na suala hili? Marehemu tayari alishazikwa so bado??
 
Wadau wa utalii wamo humu huko Karatu...

Unapiga Namibia zako Redstone mtu anakutumbulia macho.....hajuwi huko shamba kubwa Ndutu ni balaa ukitoboa unasema thankyou God
 
Back
Top Bottom