Ruling Kuhusu Kesi ya Lema ni Leo!!

Ruling Kuhusu Kesi ya Lema ni Leo!!

Kuna coaster kama tano hivi,zimeingia sasa hivi na watu kutoka Moshi.
Umejuaje kama zimetoka moshi?
Ziliondoka Moshi saa ngapi?
Je wewe ni Wakala wa CHADEMA kwenye masuala ya usafiri?
Kwani CHADEMA haina wafuasi hapa Dar es salaam?Majimbo ya UBUNGO na KAWE yapo chini ya chama gani?je hayana wapigakura wa kutosha wanaoipenda CHADEMA?
 
Leo ni hukumu ya kesi ya lema au ni hukumu ya pingamizi ya rufaa ya lema please nielewesheni.
 
"Non of your business"umechangia nauli ya kukodi hayo magari? Kupata haki ni gharama kubwa zaidi
ya kukodi magari,hata ingeahirishwa mara 1000 watu bado watakodi magari na kuja mahakamani mpaka
kieleweke"!!!!!!!

Msamehe bure mkuu hajui atendalo !
 
Mahakama zetu zina urasimu mwingi, yawezekana ni wa makusudi au mazingira ndiyo yanasababisha. Kwa yanayotokea Watanzania tunathibitisha ukweli wa kauli ya Mh. Tundu Lissu. Kesi inayogusa maslahi ya mnyonge huwa inapigwa danadana ili ikiwezekana mlalamikaji atoe hongo au akate tamaa hasa pale mshitakiwa akiwa na pesa au nafasi fulani ya utawala. Hii ni aibu kwa muhimili wa mahakama na mkuu wa nchi hasa kwa kuwa alihusishwa na hukumu hii ya Mh. G. Lema.
 
Kieleweke tu leo .Tunataka tuwe na mwakilishi wetu bungeni.Mungu Ibariki Arusha!
 
Hizi mahakama zetu za hovyo!!! Watakuja na mambo ya kijinga kabisa......tusubiri, hii yote kusubiria kutangaza majimbo ya sumbawanga na Igunga ni zuga tu....... !!!
 
Maana yake ni kutotenda haki,mbona imeeleweka vema tu!
kwani anayejua haki imetendeka au haijatendeka kwa mujibu wa utaratibu ni nani?mimi najua ni mahakama na huko ndiko ishu ya lema ilipo.sasa kwa nini unaanza kuwa biased na hukumu kabla haijatolewa?
 
....watarudi tena kuja kutuambia sasa wamerekebisha kasoro, halafu wataahirisha na kupanga siku ya kuanza kusikiliza mwakani Mungu akipenda! Hawa jamaa ni kama vile wanachezea mood zetu.

Hii mahakama inatuhujumu tu.Huko siyo kutenda haki kabisa!
 
Ruling tayari,mapingamizi 2 yametupwa,moja limekubaliwa,lakini kwambain 14 days kasoro irekebishwe na kesi ya msingi iendelee

Mkuu Yericko Nyerere tafadhali funguka vizuri zaidi. Tumeambiwa hapa kwamba kesi imeahirishwa kwa muda wa siku 14 ili mahakama ifanye marekebisho ya kasoro zilizojitokeza.

Sasa hapa tena unasema Ruling tayari, mapingamizi mawili yametupwa na moja limekubaliwa. Nimeshindwa kukupata vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Yericko Nyerere tafadhali funguka vizuri zaidi. Tumeambiwa hapa kwamba kesi imeahirishwa kwa muda wa siku 14 ili mahakama ifanye marekebisho ya kasoro zilizojitokeza.

Sasa hapa tena unasema Ruling tayari, mapingamizi mawili yametupwa na moja limekubaliwa. Nimeshindwa kukupata vizuri.
Huyu atafafanua, tusubiri.
 
Hizi mahakama za ajabu sana,yani wao hawakuona kasoro hizi kweli cku zote,any pamoja na kuichelewesha haki ya wana Arusha bado Magamba wanapoteza muda kwa swala zima la Mh Lema na Arusha
 


Leo ni hukumu ya pingamizi la kutupilia mbali rufaa lililotolewa na mawakili upande wa CCM, kama pingamizi litakubaliwa basi rufaa haitasikilizwa, kama pingamizi litakataliwa basi rufaa ya Lema itasikilizwa na kupangiwa tarehe nyingine ya hukumu.

Ahsante ufafanuz mzuri
 
mungu yuko pamoja nae ni lazima ashinde tuu... Na ubunge wake atarudishiwa.......

mwanangu na mpendwa mheshimiwa lema, siku zote mtu mwema anajaribiwa na shetani na wakati fulani mungu anaruhusu ili watu wengine wajue jinsi mungu anavyoweza kumlinda mtu anayedhulumiwa.

Umedhulumiwa wadhifa wako pasipo na sababu lakini sasa imetosha, mungu anakwenda kuingilia kati na utarudishiwa ubunge wako uliopewa na wananchi wa arusha
mungu akubariki asubuhi hii unaposubiri matokeo ya case yako
amina
 
hii hukumu imekua kama kitendawili,kwani tatizo ninini? Na sheria zinasemaje kuhusu hukumu kama hizi, mwenye kujua atujuze tf.
 
Huenda kilio cha Lissu kiko sahihi[/QUOTE

Kama hadi leo wewe ni miongoni mwa watu, ofcourse wachache, wasioelewa na kuona ukweli ktk hoja ya Tundu juu ya uteuzi wa majaji, tena kwa ushahidi mzito ambao hawajaweza kukanusha, basi kuna matatizo makubwa.
 
Back
Top Bottom