RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

Huu ulikua Wakati mgumu kwa Tanzania Wakati Amri Jeshi mkuu akitafakari nini cha kufanya kwa Mstakabali wa Taifa!!! Mpaka Kifimbo kinaonekana nusu!!! Usifananishe jeshi na vitu vya kipuuzi!!!
images (6).jpeg
 
Tena acha uongo kabisa, sio kama siwapendi, vitaje hivyo vyuo vya polisi vinavyoendesha kozi ya uongozi mdogo (Jnr) na kozi ya uongozi mkubwa (Snr)
Nimekulia kota za polisi sio kama nabuni.
Haaaaaahaaaaa tusome hata mitandaoni tu si lazima tubishane Sana hata mm nilio mbali na tz yenu naelewa hayo mambo ya majeshi yenu kwa kuyafuatilia shughuri zake

Unaposema polis na magereza hawaend koz yoyote ya uongozi utachekwa mzee baba hebu fuatilia kwanza ndio uandike kuishi karibu na mahakama si kujua Sheria.kuanzia cpl, Sgt,ssgt,rsm,nyota vyote huenda course kuanzia kiez mitatu had minne ya pili hupewa ya tatu huenda kozi kuanzia vyeo vya hapo juu wanapewa kwa mujibu wa sheria ya rais wa jamhuri ya muungano wa tz

Na kwa taarifa yako hyo 2007 hakuna polis Alie kimbia hata mmoja na hakuna alienda smi kilichokuwa kinafanyika Ni utaratibu kuwa majeshi yote kuanzia nyota wapige koz sehemu moja ila muafaka haukupatikana.

Na hata hao jwtz huwa wanakwenda pale ccp Moshi kupata mafunzo ya upolisi MP na wanajua shughuri yake ya kile chuo Nina jamaa zangu kibao wako Katika majeshi haya wanatoa data Kama kawa.na nchi mbali mbali hupeleka polis wao kupata mafunzo pale ccp na Ni chuo Bora kwa mafunzo.
 
Usiku wa Jumanne ya kuamkia Novemba 15, 1978, kikosi cha kwanza cha askari wa Tanzania, kikiwa chini ya Luteni Kanali Benjamin Noah Msuya, kilivuka Mto Kagera kwa mashua ndogo na kuingia ng’ambo ya pili.
Hadi kufikia wakati huo (wa kuvuka mto), zaidi ya Watanzania 1,000 walikuwa wameuawa, alisema Msuya katika mahojiano na gazeti The Monitor la Uganda la Jumamosi ya Mei 3, 2014 nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam.
Msuya aliongoza batalioni ya 19 ya JWTZ iliyokuwa chini ya Brigedi ya 208 iliyoongozwa na Brigedia Jenerali Mwita Marwa. Kazi yake ilikuwa ni kuivamia na kuitwaa Kampala, lengo ambalo hatimaye lilifikiwa Jumanne ya Aprili 10, 1979.
Baada ya kufanikiwa, Luteni Kanali Msuya akaitawala Kampala kama meya wake na pia kama rais wa Uganda kwa siku tatu hadi nchi hiyo ilipompata Yusuf Kironde Lule kuwa rais.
Alfajiri ya Jumapili ya Novemba 19, Luteni Kanali Msuya alituma kikosi kingine cha askari kwenda ng’ambo ya Mto Kagera, kikitumia mashua nyingine ndogo. Huko walishangazwa sana kuona uporaji na mauaji yaliyofanywa na askari
Miili ya Watanzania waliouawa na majeshi ya uvamizi ilikuwa imeshaanza kuoza. Kikosi hicho kiligundua kuwa miili mingine ilikuwa imekatwa viungo, ishara kwamba wengi wao waliteswa kabla ya kuuawa.
Serikali ya Tanzania ilisema kiasi cha wakazi 40,000 walivuka Mto Kagera kukimbia majeshi ya Uganda, wakiacha kiasi cha raia kati ya 5,000 na 10,000 wakihofiwa kuuawa.
Miongoni mwao, kwa mujibu wa gazeti la Serikali la Daily News, walikuwako Watanzania 485 waliopelekwa gereza la Mutukula upande wa Uganda, ambako waliuawa kwa kulipuliwa kwa baruti.
Habari iliyoandikwa na John Darntonnov kwenye gazeti The New York Times la Alhamisi ya Novemba 23, 1978 inasema katika maeneo yaliyovamiwa na majeshi ya Idi Amin, hasa ya biashara, “kitu pekee chenye uhai kilichoonekana (baada ya uvamizi) ni mbwa mweusi aliyekonda” baada ya raia Watanzania wengi kuyakimbia majeshi ya Idi Amin.
Maduka yote, kwa mujibu wa The New York Times, yaliporwa.
“Katika duka moja lililoporwa, kilichokuwa kimesalia dukani hapo ni picha ya harusi ya mmiliki wa duka, Zaharan Salum na bibi harusi wake, ambayo ilikuwa inaning’inia ukutani,” liliandika gazeti hilo.
Kati ya ng’ombe 12,000 waliokuwa ranchi ya Narco, ni ng’ombe 100 tu walisalia baada ya wengine kuporwa. Wamiliki wa ranchi hiyo, ambao ni raia wa Australia, hawakuonekana baada ya uporaji huo na ilihofiwa kuwa nao waliuawa. Kiwanda ha sukari cha Kagera na shamba la miwa, viliteketezwa.
Doria ya Luteni Kanali Msuya ilifika hadi mpakani mwa Uganda Jumatano ya Novemba 22. Kwa wakati wote huo askari wa Amin hawakuonekana. Lakini doria hiyo ilipofika eneo la Minziro, iliona kiasi cha askari 30 wa Amin na vifaru viwili vikiwa eneo la kanisa. Askari hao wa doria hawakufanya shambulio lolote bali walirudi hadi Kyaka.
Ijumaa ya Novemba 24, vikosi kadhaa vya JWTZ, vikiongozwa na mabrigedia watatu; James Luhanga, Mwita Chacha Marwa na Silas Mayunga vikawa vimetanda kuzingira maeneo yaliyotekwa.
Siku hiyo hiyo daraja la dharura la Mto Kagera likaanza kujengwa kwa ajili ya kuvusha vifaru na zana nyingine za kivita. Kazi hiyo ilikamilika na siku iliyofuata na zana za kivita zikaanza kuvushwa.
Wakati daraja la dharura likijengwa, Rais Nyerere alizuru eneo hilo. Ingawa awali makamanda wa JWTZ walitaka kumzuia. Akiwa uwanja wa vita, alitumia darubini kutazama wapiganaji wa Amin wakiwa vilimani, umbali wa kilometa kumi kutoka mpakani, tayari kuishambulia Tanzania.
Ziara hiyo ya Nyerere ilimshawishi kukubaliana na makamanda wa JWTZ kuwa eneo la Kagera haliko salama na kwamba ili usalama uwepo, ilikuwa ni lazima jeshi la Tanzania livuke mpaka.
Usiku wa Jumapili ya Novemba 21, 1971 askari wa Tanzania walivuka mpaka na kuingia Uganda. Kikosi cha kwanza kilisaidiwa na vifaru na kiliongozwa na Luteni Kanali Salim Hassan Boma.
Vikosi kadhaa vilijizatiti maeneo ya misitu kuzunguka mji wa Mutukula. Kabla ya kupambazuka, kikosi kimojawapo kilichoongozwa na Luteni Kanali Salim Hassan Boma, kikisaidiwa na vifaru, kilitembea katika barabara kuu ya kuelekea Mutukula. Hii ilikuwa ni mbinu ya kuwavuta adui na ilifanikiwa.
Wakati majeshi ya Idi Amin yakifuatilia nyendo za kikosi cha Luteni Kanali Boma kilichokuwa mbele yao, yalishtukiwa yakishambuliwa na kikosi kingine cha JWTZ kutoka nyuma yao. Kwa jinsi askari wa Idi Amin walivyopagawa, walilazimika kukimbia na kutelekeza silaha zao.
Kwa njia hiyo JWTZ ikajipatia silaha mbalimbali kuanzia vifaru hadi bunduki za kawaida. Katika mapambano hayo, kikosi cha Luteni Kanali Boma kilipoteza wanajeshi watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa. Hata hivyo, bila ujasiri huo ilikuwa ni vigumu kuvunja ngome ya jeshi la Uganda katika vilima vya eneo hilo.
Kwenye mapigano ya Mutukula, idadi kubwa ya raia waliuawa.
“Kila kitu kiliharibiwa na kila kilichokuwa na uhai kiliuawa,” imeandikwa katika kitabu cha War in Uganda.
“Mabuldoza yalifukia nyumba zote za udongo. Vikongwe ambao hawakuweza kukimbia waliuawa kwa kupigwa risasi. Kufikia mchana (Jumatano ya Novemba 22, 1978) Mutukula haikuwapo tena isipokuwa kwenye ramani.”
Jeshi la Tanzania “lilianza kulipiza kisasi kwa namna isiyotofautiana na ile ya Idi Amin” wakati akiteka eneo la Kagera.
Habari za ushindi wa kuitwaa Kagera zilimfariji Mwalimu Nyerere, lakini inasemekana, hakufurahishwa na habari za mauaji yaliyofanywa na jeshi lake.
Baadaye Nyerere alitoa amri ya maandishi kwa jeshi lake litofautishe jeshi na raia na mali zao. Vyovyote iwavyo, ushindi wa kwanza ukawa umepatikana kwa kuikomboa Mutukula.
 
Story ya Kagera War- Tz

Tarehe 28-10-1978 nilikuwa kambini LUGARO kikosi cha MMJ nilikuwa nimejipumzisha ghafla likapigwa Baragumu na tulipoenda kusikiliza tuliambiwa kuwa kuwa Idd-Amin kavamia huko Kagera tukaamliwa kuchukua vitu vyetu na kuvipeleka kwa STORE-KEEP vikiwa na majina mimi nilichukua bage langu na kuliandika jina langu na kulikabidhi kwa STORE-KEEPER.Na hapo hapo tulianza kuchukua vifaa vya kivita kama vile Combat mpya Bunduki SMG ya kwangu ilikuwa NHN 66482612.

Jioni hiyo ya 28-10-1978 Tulichukuliwa na magari ya Jeshi kwenda station ya Railway huko Dar-es-salaam na tuliondoka usiku huo huo kuelekea station ya ISAKA-Kahama.

Tulifika Station ya Railway ya Isaka 01-01-11-1978 Mchana tulikuta mabasi mengi sana ya kiraia yametusubiri kwenda Vitani mimi na wenzangu tulipanda Basi moja lilikuwa limeandikwa LUPONDIJE lilikuwa na namba MZA 234 Tuliondoka hapo isaka saa 9 mchana kuelekea Kahama mjini bahati mbaya sana Basi letu lilipofika tu pale stand ya Kahama Msafara wa magari yote ndo ulipoanza kuondoka na sisi ilibidi tupitilize tu bila kupata chakula hapo na kwa kufupisha habari nilifika kwenye uwanja wa Mapambano 03-11-1978 Mchana

Nilipofika wakati nateremka Kwenye Basi mimi niliitwa na Major mmoja kuwa nichukue askari wanne niende kwenye Landrover ya Jeshi ilikuwa imefunikwa na turubai na nilifanya hivyo nilipofungua nilikutana na Maiti za askari wetu watatu waliolipuliwa na Bomu la kutupwa ilibidi tuzishushe Maiti hizo na mimi ilikuwa mara yangu ya kwanza kubeba Maiti katika Maisha yangu Kwangu mimi niliona kama ni Uchuro kwangu kufika tu Mstari wa mbele na kukutana na Maiti kwangu mimi ilinipa taabu sana.

VITA VILIPOANZA
Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Msimamo wa vita ulikuwa umepangwa vizuri sana na ulikuwa na MAKAMANDA wafuatao-
1. Brigadier Marwa waliingia Uganda kwa kupitia mpaka na Rwanda na Zaire.
2. Brigadier Kiwelu alielekea Mbarara,
3. Brigadier Marwa alielekea Masaka
4. Brigadier Walden aliingia Uganda pia kwa kupitia Rwanda na kuelekea Kasese
5. Brigadier Mayunga yeye alibaki upande wa Tanzania ambapo brigade yake iligawanya katika makundi mawili, kundi moja liingia maeneo ya Mtukula kutokea Rwanda, , wakati kundi jingine lilibaki pale pale mto Kagera lakini likiwa na mizinga mizito (BM-40) kiasi cha kuweza kurushia makombora hayo moja kwa moja hadi askari wa Amini waliokuwa pale Mutukula. Ilichukua muda wa karibu wiki tatu kwa plani ya vita kukamilika na majeshi yetu kujipanga vile.

KIPIGO TOKA MAJESHI YA AMIN

Baada ya majeshi ya Amin kuchukua eneo la Mutukula, walipandisha bendera ya Uganda na kubomoa lile daraja la mto Kagera. Brigadier Yusuf Himid ambaye alikuwa Brigade Commander wa Kanda ya Magharibi wakati huo alituma Battalion moja kujaribu kuvuka mto ule kwa kutumia mitumbwi wakati wa usiku kusudi wakapambane na wavamizi wale. Hata hivyo wakati platoon za kwanza kwanza zinaanza kutekeleza amri hiyo, wakaonekana na majeshi ya Amin ambayo yalikuwa yamejikita kilimani; Askari wetu wale walimiminiwa mizinga ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa askari. ..bahati mbaya sana tulipigwa sana na majeshi ya amin na kupelekea Majeshi yetu kurudi nyuma kujijenga upya na kupelekea lile daraja kuvunjwa conteravertially Bahati nzuri mimi na wenzangu tulikuwa tumewahi kuvuka kwenye hilo Daraja na Tulipojijenga upya kazi ilianza na ilikuwa ngumu sana maana ilikuwa ni masika Mvua zilikuwa zinanyesha sana sana kwa sababu mimi na wenzangu tulikuwa askari wa Miguu Infrantry haikutupa taabu tuliendelea kusonga mbele kitendo hicho cha kurudishwa nyuma kilisababisha Brigedier Yusuph Hamid kuondolewa mstari wa mbele hivyo Brigade ya magharibi ikawekwa mikononi mwa Colonel (wakati huo) Kotta ambaye legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa afrika ..kama mnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.....

Baada ya kile kipigo bregedia Yusuph Hamid aliondolewa from front line kama ilivyokawaida ya war plans...maana kamanda aliyepigwa hulazimika kupumzishwa kwanza ili atafakari wapi wapi alikosea.

Pale Ngome, kamanda aliyepanga vita ile yote alikuwa ni Colonel Lupogo Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Kipindi hicho mimi nilikuwa na ki-radio kidogo cha mfukoni niliweza kusikiliza Radio Ujeruman na Radio nyingi tu kila zilipokuwa zinatangaza kutadhimini uwezo wetu wa kivita na uwezo wa Majeshi ya Amini ilionekana wazi kuwa Maeshi ya Amini yalikuwa Bora na zana Bora kuliko zetu kwa upande wa vifaru sisi tulikuwa na T 34 vya kizamani sana na Uganda vifaru walikuwa navyo T 55 Kwa wakati huo walikuwa navyo Bora sana kuliko sisi.Pia Amini alisikika kwenye vyombo vya habari akishangilia kuwa jeshi lake limeweka rekodi kwa kuteka Mtukula kwa muda wa dakika 25 tu.

VITA VYAANZA RASMI FRONTLINE

Baada ya mejeshi yetu kujipanga ndipo filimbi ilipopigwa na Brigadier Kiwelu akarusha risasi ya kwanza dhidi ya Barracks moja ya Amin iliyokuwa pale Mbarara. Brigadier Marwa naye akawarushia risasi (ya kuwambia kuwa kazi imeanza) wale askari wa Amini walikuwa pale Mutukula.

Brigadier Mayunga naye akadonoa kidogo kutokea Magharibi, harafu akatumia ujumbe mwingine wa BM-40 kutokea Kagera. Askari hao wa Amin waliokuwa pale Mutukula (Simba Battalion) walipoona wanapata kipigo kutoka pande zote wakaomba msaada kutoka Mbarara, hata hivyo wakaambiwa kuwa ile Battalion ya Mbarara nayo ilikuwa imeelemewa na kipigo cha Kiwelu, ndipo wakaomba msaada utokee Entebbe. Ile Battalion iliyoletwa kutokea Entebbe ikakutana na kizingiti pale Masaka ambapo Brigadier Marwa alikuwa kajichimbia.

Wakati Amin bado anafikiria afanyeje kuhusu vipigo hivi vya Masaka, Mbarara na Mtukula, akapewa taarifa nyingine kuwa kulikuwa na kipigo kingine kimeanza kutokea Kasese kuelekea Kampala; hiki kilikuwa ni kipigo cha Brigadier Walden. Basi kuanzia hapo ndipo vita ile ilipoanza kupendeza kweli kweli kwa majeshi yetu,. Walianza kuwabomoa majeshi ya Amini yaliyokuwa miji hiyo huku yakiayaacha yale ya Mtukula pale pale na bendera yao ili wajifie wenyewe kwa kukosa supplies kwa vile walikuwa hawapati chakula wala msaada wowote kutoka ndani ya Uganda tena.

Baada ya kugundua kuwa kuwa alikuwa amezungukwa sana kwa vile majeshi yake mazito yalikuwa ndiyo yameshathibitiwa, Amini akaitangazia dunia kuwa amevamiwa na majeshi ya Tanzania (na kweli safari hii alikuwa amevamiwa kikwelikweli). Hata hivyo Nyerere naye akajibu kuwa jamaa huyu alituvamia akachukua sehemu ya Kagera, na kuitangazaia dunia. Ili kuionyesha dunia kuwa anasema kweli, Nyerere na Sokoine walikaribisha ujumbe wa OAU pale Kagera na kuwaomnyesha kuwa lie eneo la Mutukula bado lilikuwa linakaliwa na majeshi ya Amin na bendera yake bado inapepea. Kufanya hivyo kulifanya jumuia ya kimataifa isimwamini Amin katika kipindi ambacho alikuwa akipewa kipigo safi sana.

HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA

Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakiya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka wiliwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.

Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.

KIPIGO CHA LUKAYA

Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindii ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mshiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani

Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam Cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.

Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege nyingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zatu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.

Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.

BRIG GEN MOSES NNAUYE

huyu alishiriki kama muhamasishaji ..ni muhimu sana..akiwa ni vikosi vya bendi na burudani...[ie mwenge jazz,na kwaya ya luteni komba...hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu...na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...

Ma-CDF wetu kwa kadri niwezavyo.

WAKUU WA MAJESHI CDF

1.1964-1974: Sarakikya
2.1974-1980: Twalipo
3.1980-1988: Musuguri
4.1988-1994: Kiaro
5.1994-2001: Mboma
6.2001-2007: Waitara
7.2007-2016 Mwamunyange
8.2016-Venance Mabeyo-

CHANGAMOTO ZA VITANI

Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mble wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya KarumaKwa maajabu, Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe

2. Gen Msuguri alikuwa siyo msomi sana lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha. Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.

3. Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.

..kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.

Lt.Col.Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule.

..Lt.Col.Hassani Boma na Lt.Col.Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.

Maj.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.
luteni col ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.

..Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.

..baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

..Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.

..Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.

Every nation and every country has been blessed by great individuals. They have left footprints. Their lives and actions tells us the purpose of life and living. Maj. Gen Mwita Chacha Marwa a.k.a Kambale was never a scholar neither a good politicians but he is worth a role model to many of us. we can learn from him and make our lives beuatiful and worth living. God has decided to call him at the time when Tanzania may have wanted him more, we are in a critical time of struggle, struggle that can not be compared to theirs at that time. But it a struggle that pose danger to survival of this nation.
 
A
Haaaaaa.Haya maaskari sijui yakoje sijui yanawaza nini. Leo mlinzi was getini nawapa Elimu nyie mabregedia masacp na macopolo .Kwanza kaa kimya soma kwa makini sana.Majeshi yote ni Idara ndani ya Wizara zake Hivyo msijione bora sana bosi was mkuu wa majeshi ni katibu mkuu wa Wizara na Bosi wa IGP ni katibu Mkuu tu baada ya hapo Waziri halafu Rais sasa msijone miungu watu hapa nyie sawa tu wafanyakzi wengine wa umma acheni mbwembwe. Sasa nawafafanulia kuhusu vyeo vyenu ni kwamba kazi za mwenye nyota moja Jeshi la Wananchi ni sawa tu na Jeshi la Polisi tofauti ni utendaji tu anzieni kwenye paredi ni nani anakagua wachafu na wasafi ni nani anawakagua malindoni ni nani anaongoza platoon ni nani anaongoza mkoa kanda mpaka nchi utagundua alama zao kwenye mabega zinafanana. Twendeni kwenye Ushaidi sasa. Nini maana ya Jeshi,Mwanajeshi,kazi za vyeo vyao
Ibara ya 151:ya katiba ya Tz
Jeshi" maana yake ni lolote kati ya majeshi ya ulinzi na ni
pamoja na jeshi lolote jingine lililoundwa na Katiba hii au
kwa mujibu wa sheria na linalotawaliwa kwa amri ya51.-(1) Katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitaji
vinginevyo:
"amri ya Jeshi" maana yake ni sheria au amri
iliyotolewa kwa mujibu wa sheria, ya kusimamia nidhamu katika
jeshi;

"askari" likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni
pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya
jeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu;

Ibara ya 147 maana ya Mwanajeshi.
147(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa.

Twende kwenye majukumu
Sheria ya kanuni ya Adhabu

Kutoa tamko kwa
wafanya ghasia
kutawanyika
Sura ya 500 kif.
7; Sura 356 kif
11 (13) kifungu cha
77cha kanuni ya Adhabu kinasema Hakimu yeyote au, kama hayupo, afisa wa polisi wa au aliye juu ya
cheo cha mkaguzi(nyota moja na kuendele) au akida wa jeshi(Nyota moja na kuendelea/commissioned officer)la vita la Jamhuri ya Muungano,
atakayeona watu kumi na mbili au zaidi wamekusanyika kwa ajili ya
ghasia ana wasiwasi kuwa ghasia inataka kufanywa na watu kumi na mbili
au zaidi, au anaweza kutoa au kutolesha ilani kwa jina la Rais, kwa namna
atakayoona yafaa, kuwaamrisha wafanyaji ghasia hao au watu
waliokusanyika watawanyike kwa aman.
Mabano hayo nimeweka kwa ajili ya ufafanuzi tu kuonesha ulinganifu katika
Twendeni kwenye Uhalisia sasa
He unamkumbuka aliyekuwa kiongozi wa Operesheni tokomeza enzi za jk basi ni Simon Siro akiwa SACP wa Polisi aliongozi vikosi vya Jeshi la Polisi,Jeshi la Wananchi pamoja na Tanapa ndani ya vile vukokosi kulikuwa na majors wa kutosha na Makanali wote walpokea maelekezo kutoka kwake vipi apo mbona Hugo bado hakuwa kamishina kamili.Msichanganye mambo waungwana kamishina wa Polisi ni kamishina wa Polisi anaongoza commission Fulani kama vile fedha,utawala,mafunzo ,forensic na kadhalika sasa huku Jeshi la Wananchi commissioned Officer wanyota moja au mbili anaongoza commission gani? Mimi ninachojua anaongoza platoon tatu yaani company wakati kamishina msaidizi wa polisi anaongoza mkoa wenye watu askari pamoja na idara zote na ndiyo muongeaji hasa kwenye kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa kama alivyolinda Heshima ya Jwtz pale Arusha kwa kuwajibu waandishi wa habari.Narudia tena kuwa kamishina ndani ya Polisi ni cheo cha mwisho kabisa maana kinachofuata ni hisani ya Rais sasa wewe na kanyota chako ukajifananishe na Mambosasa aliyepewa V8 na walinzi Nyumba Kali eneo sawa na Mawaziri na makatibu wakuu wakati wewe umeja wako unatembelea defender mbovu na unalala nyumba Dirisha kama LA choo tens chafu hasa. Acheni kulishwa ujinga askari na mnakaririshwa kasumba dharau mwishowe mnaanza kupigana. Ebu fikiri kwa kina unafikiri Mkuu wa wilaya ya Arumeru anaweza kumuamrisha Shana ? Maana Shana ni Dcp bado kuwa kamishina kamili .na mkuu wa wilaya ni kamishina? Fikiri kwa kina sana acha kudanganywa na macoplol sugu yanakuambia yalikwenda vitani Uganda wakati walioenda vitani wote wameshastafu maana aliyeingia na miaka 18 kastafu mwaka Jana.. Pia mkumbuke kila taaluma inaumuhimu katika jamii .

Nyongeza ya mawazo tu
Wote Nazi yetu kuu kutulinda sisi Wananchi na Mali zetu yanini mnaleta ligi na kufedheheshana kwa kujiona imara zaidi kiliko wengine.Nyie ni walinzi tu Nazi yenu kuu ni ulinzi .Amka kifikra askari acha ubabe wakishamba tafuta pesa uache kufungulia mageti wenzako.
Acha urongo mkuu,operesheni tokomeza iliongozwa na brigedier general wa jwtz,sirro akiwa sacp kipindi hicho alikuwa msaidizi wa operesheni
 
Ilo kamanda lina kadi ya chama ndoto yake kubwa ni kuwa IGP kwahyo linajitoa akili sana ili kufika lengo
 
Katiba siyo msahafu. Katiba nayo ina mapungufu. Neno Jeshi haliwezekani kutumika kwenye Magereza wala Polisi.

Mimi nakufafanulia kitaalamu. Istilahi neno Jeshi kwa Tz linavyotumika na maana yake ni tofauti kabisa. Tz Polisi kwa kingereza linaitwa Tanzania Police Force.

Neno Force ndipo lilipowachanganya kwa lugha ya Kiswahili, wao wametafsiri kama Jeshi. Force kwa police ni Enforcement of the law.

Kwa maana wanawafanya watu wafuate sheria kwa wale wanaovunja sheria, ndiyo maana wana deal na raia. Ndiyo maana inapotokea ghasia Police huwa wana restore order ili kuleta amani na usalama ndani ya nchi.

Ukija kwenye TPDF imeandikwa kabisa ni armed forces in Tanzania. Wakati ukiangalia Tanzania Police force huwezi kukuta imeelezewa kama armed forces.

Kwa nini iwe hivyo? Jawabu ni kutokana na majukumu yao. Kwa hiyo Police siyo Jeshi! Police ni idara tu inayoshughulika na usalama wa raia na mali za raia.

Ukibisha, Tuambie maana ya Jeshi ni nini?
Katiba ndiyo sheria kuu imeshatoa maana wewe unatoa wapi hyo maana.Katiba haipingwi na sheria yoyote ile na katiba hasa ni ile ya kiswahili na imetoa tafasiri.
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO YA MWAKA 1977
SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI

147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa.
Madaraka ya
Amiri Jeshi Mkuu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.49
148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
 
Nini maana ya Jeshi?
jeshi ni kundi la askari lililopitishwa na serikali ya nchi husika,kutumia nguvu na silaha katika utendaji wake.

1.ni lazima serikali iliunde au ilitambue,basi hakuna tatizo.ndio maana kuna waasi,wana kila nyenzo lakini hawapewi hadhi ya jeshi sababu serikali zao haziwatambui.
 
Tanzania kuna vyombo vya ulinzi na usalama, polisi, uhamiaji, magereza, zimamoto na uokoaji wote hao wako kwenye usalama. Wapo kwenye wizara moja (Wizara ya mambo ya ndani).
Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania pekee lipo kwenye wizara ya ulinzi. Na ndio jeshi kwa maana jeshi liwe limekamilika kwenye vifaa vyenye nguvu dhidi ya adui na kwa vile ulinzi wake ni kwa nchi dhidi ya maadui tofauti na polisi ambao wanaangalia usalama wa raia, uhamiaji ambao wanaangalia usalama wa raia pamoja na kuzuia wasio raia kuingia nchini kwa njia zisizo rasmi, magereza wanawalinda wenye makosa mbali mbali zimamoto na uokoaji wako tayari kwa ajili ya kuzuia/kudhibiti majanga mbali mbali. Wote mnaobishana hapa mnatakiwa mjue vitu vidogo kama hivi ili walau mbishane kwa kujua sio kichwa kichwa tu.
Polisi ni polisi popote pale duniani na sio jeshi la polisi, kwa vile halina silaha zenye nguvu kama majeshi rasmi.
kwahiyo ishu ni siraha sio!!

unawajua alshabaab,unajua kuna vyuma wanavyo havijawahi kushikwa na askari yeyote yule chini ya ardhi ya tz[emoji16][emoji16].

je kwa kigezo hicho wanapaswa kuitwa jeshi zaidi ya jwtz?
 
Hii chai
JWTZ ____polisi
Lt usu = assistance inspector
LT. = inspector
Captain =ASP
MEJA =SP
LT. COLONEL =SSP
COLONEL =ACP
BRIGEDIA GENERAL. =SACAP
MEJA GENERAL. =DCP
LT GENERAL =CP
GENERAL. =IGP

Note: wakikutana afisa wa jwtz na afisa wa polisi wanao lingana vyeo, afisa wa polisi atampigia saluti afisa wa jwtz kwa sababu JWTZ ndio jeshi SNR. But wakikutana mmoja anamzidi mwingine cheo, protoco za kijeshi lazima zifuatwe mdogo kumsalimia mkubwa.
 
Nimekuunga mkono Mkuu....Watu wanafikiri Brigdea Jeneral ni cheo kikubwa sana jeshini kumbe cha kawaida tu ..
Kama unadhani sio cheo kikubwa subiri vita ije ndio utajua maana yake.Hivi unajua brigade ukubwa wake?.
Vita vya Kagera Musuguri,Walden,Mayunga,Kiwelu wote walikuwa mabregedier lakini walimchachafya Amini.Walipandishwa vyeo vita vikiwa vinaendelea
 
Tanzania kuna vyombo vya ulinzi na usalama, polisi, uhamiaji, magereza, zimamoto na uokoaji wote hao wako kwenye usalama. Wapo kwenye wizara moja (Wizara ya mambo ya ndani).
Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania pekee lipo kwenye wizara ya ulinzi. Na ndio jeshi kwa maana jeshi liwe limekamilika kwenye vifaa vyenye nguvu dhidi ya adui na kwa vile ulinzi wake ni kwa nchi dhidi ya maadui tofauti na polisi ambao wanaangalia usalama wa raia, uhamiaji ambao wanaangalia usalama wa raia pamoja na kuzuia wasio raia kuingia nchini kwa njia zisizo rasmi, magereza wanawalinda wenye makosa mbali mbali zimamoto na uokoaji wako tayari kwa ajili ya kuzuia/kudhibiti majanga mbali mbali. Wote mnaobishana hapa mnatakiwa mjue vitu vidogo kama hivi ili walau mbishane kwa kujua sio kichwa kichwa tu.
Polisi ni polisi popote pale duniani na sio jeshi la polisi, kwa vile halina silaha zenye nguvu kama majeshi rasmi.
Wewe jamaa hapa umeongea pumba tupu.
Kama polisi hawana silaha zenye nguvu wanapambana vipi na majambazi au majangiri?
 
Hawawezi wameshazoea ubwanyenye! Mwaka 2007 walipelekwa pale SMI kwa ajili ya kozi ya uongozi, unaambiwa ndani ya wiki wote walikimbia [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
Na nahisi msongo wa mawazo unawasumbua kwa vile polisi kwao ni ngumu sana kupanda vyeo, unakuta mtu ana miaka zaidi ya 20 kazini eti ndio anakuwa Koplo. Wakati jeshini ni kozi na elimu yako tu vinakubeba. Jwtz ndio jeshi haya mengine ni vyombo vya usalama wa raia.
Hata nembo rasmi ya polisi inajieleza
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1202075
Kuwa usalama wa raia sio kigezo Cha kutokuwa jeshi bali huo ni mgawanyo tu wa majukumu.
Au wewe ulitaka majeshi yote yakalinde mipakani halafu huku mitaani Nani angetoa huduma?
 
Back
Top Bottom