Samia akicheka na nyani atavuna mabua.
Samia asipende sifa za kijinga kutoka kwa watu hasa wapinzani.
Wapinzani wengi kama sio wote nchi hii ni makuwadi/madalali wa watu. Wanafanya siasa kwa mwamvuli wa watu wengine walioko nyuma yao.
Naona wajinga wanampaka mama mafuta kwa mgongo wa chupa eti fungua nchi, afungue nchi kwani ilikua imefungwa?
Naona mama anataka kuingiingiza TPDC kwenye deni lingine kama lile la JK TPDC inadaiwa Trillioni 3.5 hadi mwaka jana June kwa taarifa ya CAG. Kujenga bomba lingine hadi Mombasa ni deal ya watu hiyo maana itahitajika mkopo tena wa zaidi ya Trillioni 4 ama Dollar Billion 2 za Marekani.
Tulikopa kujenga bomba toka Mtwara Dar, linatumika kwa 4% huku 96% haitumiki. Sasa tunataka kukopa tena tupeleke gas Mombasa.
Tusubiri tuone.