Liz Senior
JF-Expert Member
- Apr 19, 2007
- 483
- 53
Hawajakutana Maaskofu wowote. Wanaozungumza sasa ni Mtikila na wenzake. Mchungaji amekwepa waandishi anasema yuko LIKIZO.... inawezekana anaweza kachukuliwa hatua.
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?
Kwa kadri nijuavyo "rituals" za kanisa, sadaka huwa hairudi na kanisa wanaamini wanaweza kuzigueza hela chafu kuwa safi kwa kufanya kazi takatifu ya bwana kwi..kwi..kwi.. acha nicheke mie, dunia hii ina mambo! Heri waliojiamulia kuwa atheists!
Mtikila anasema, wamelinajisi kanisa
Mtikila anasema, wamelinajisi kanisa
Hongera sana kwa Kanisa kumualika huyo FISADI na tumeweza kuyapata yaliyokuwa MOYONI mwake. Bila mwaliko huo tungejua yote hayo> Huyu Rostam aliongea kama vile watoto wanavyotoa siri kwa Baba mara anaporudi safari. NIMEMSHANGAA SANA LAKINI NIMEFURAHI.
Lakini hebu twendeni nyuma na mbele, tusilikuze sana hili jambo. Kuna waumini kibao wanaotoa sadaka zao makanisani na misikini ambazo wamechota kutoka fungu walilolipata kwa njia ya kifasadi au nyingine. Hapa tusibadilishe mada ya ufisadi, kama Rostam ni fisadi hawezi kuwa Omega na Alfa, atakuwa sehemu ya huo mfumo wa ufisadi na zaidi ya yote atakuwa ni uzao wa huo mfumo wa ufisadi.
Watetezi wa mchungaji aliyemwalika Rostam kanisani wanaweza wakaja na hoja kama hizi:
Kanisa halipaswi kuwakataa wale wanaoamua kuingia nyumbani kwa Bwana. Kwa hiyo ukiangalia kwa jicho lingine ni kwamba kanisa lilipata nafasi nadra ya kufanikiwa kumleta mbele za bwana moja ya waliopotea. Sasa cha kujiuliza Rostam alipata nafasi ya kukiri, kutubu na kumrudia bwana? Hili ndio swali la msingi la kujadiliwa na hao maaskofu. Maaskofu wasiongozwe na siasa kwenye mjadala muhumu kama huu bali roho ya Bwana tu!
Sasa kama hao maaskofu watamsuta mchungaji au kiongozi wa kanisa aliyemwalika Rostam, watajuaje kama aliongozwa na roho ya Bwana katika kumwalika huko? Na je, wanajuaje kama Rostam aliongozwa na Bwana kusema maneno aliyoyasema na kutoa sadaka aliyotoa mbele za madhahabu ya Bwana wa Majeshi? Mtikila anaweza kutusaidi kujibu haya maswali?
hakuna mwenye ujanja wa kurudisha pesa ya Rostam.nachojua ni kuwa makanisa yanapokea mpaka pesa za mashoga duniani na kuziombea ije kuwa pesa safi kama ya rostam eti kwa kuwa ana allegation ambazo hazijathibitishwa bado.
Ufisadi upo hata nadani yamakanisa kadhaa. Viongozi wa makanisa wanaweka pesa mbele, hasa kkkt, ndio maana utaona watu kama akina Mengi wanaalikwa kuwa wageni rasmi kwa shughuli za kikanisa japokuwa yeye (Mengi) ndoa yake imeshindikana. Hana imani ila ana pesa yake!
sadaka ni sadaka tu cha muhimu kuiombea ili kuvunja hiyo nguvu iliyoko nyuma ya hiyo sadaka inayotolewa