Rostam aibukia kanisani!

connecting to the dot....Kwani Askofu Laizer ni wa Kanisa gani??Huyu si ndiye aliongoza mapokezi ya Lowassa?
 

Kwani Mtikila hajawahi kula noti ya Rostam?!?
 
Kwani Mtikila hajawahi kula noti ya Rostam?!?

Vipi Mpita njia, kwani una clue yoyte ya Mtikila naye kupata chochote toka kwa RA? mwaga data mkuu, we talk openly here.

Kuhusiana na Kanisa la KKT, I know Malasusa in person, he is a strong man, hope he will do something on this immediately! unless nguvu ya mafisadi iwe imemtembelea na kumdhoofu hasa kupitia kwa Lowassa!
 

Niongezee hapo,Mchungaji ndio mwenyekiti wa baraza la wazee ktk usharika.
Lakini sioni sababu ya kulihukumu kanisa kwa jambo hili,viongozi wote walituhumiwa na ufisadi wamekuwa wakizungumza na kujisafisha kila sehemu kwa kusaidiwa na serikali.
Je sisi kama wanajamii tumejitahidi kwa kiasi gani kupigavita huu ufisadi,kama sio kujahapa na kulalamika kisha tunazima kompyuta zetu na kwenda kulala.
Kama kweli tunataka kuupigavita ufisadi kwa vitendo basi tuwapeleke hawa watuhumiwa mahakamani ili sheria ikachukue mkondo wake.
Kwa mimi ninavyojua kuhusu hivi vikundi vya makanisa wao watamwalika mtu ili wao wapate kile wanachokitaka na sio maneno matamu kama asali.
kwaya ilihitaji pesa kwa ajili ya kujiendesha ktk kumtumikia mungu,hivyo wamepata wao na azizi mkataba wao uliishia hapo.
 
Lakini RA alisema maneno "mazito" tu hapo Kanisani. Alisema Nchi inaelekea kubaya kwa sasa yakiwemo:
1.NDOA nyingi zinavunjika;
2.WATOTO wanaongezeka MITAANI;
3.CHUKI zimezidi miongoni mwa JAMII hadi kuombeana VIFO.
Pengine alisahau kusema kuwa UFISADI una MCHANGO wa AINA YAKE katika yote hayo.
 

Ukiangalia kwa makini lengo la RA halikuwa tu kutoa huo mchango wa pesa aliona ni mahali sahihi kwake kucheza ule Mchezo wa Karata uitwao "MAPIKU"

"Nadhani nianze kwa kuwapongeza pamoja na maneno mengi ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi
yangu hamkuyajali na kwa maana nyingine mmeyaona kuwa ya kizushi, kijiweni na yenye wivu," alisema Bw. Aziz.
Aliwashukuru waumini hao na kusema wao si wazushi na hawana wivu dhidi ya mtu yeyote bali ni watu wanaopenda haki kama Mwenyezi Mungu anavyotaka.

Naye Mchungaji wa kanisa hilo, Bw. Joseph Masage alimtaka, Bw. Aziz kutokata tamaa na mambo mbalimbali yanayomwandama kwani alisema Mungu ndiye anayejua huduma anayoifanya hapa duniani.



"Kweli yanaweza kuwepo maneno mengi lakini yote hayo ni mapito endelea kufanya huduma ambazo unaona ni nzuri
katika jamii na Mungu atazidi kukubariki," alisema Mchungaji Masage.(majira)
 
Tuliposema wamelala kitanda kimoja na wezi na kujifunika blanketi na mafisadi, si Kanisa walidhani tunawalaumu bure? Sasa leo wamekutana wakifanya unajisi wao hadharani, wataweza kujiweka tena wakfu?
 



I love Mtikila...akiona chungwa anasema chungwa.

Huyu mtu anatufaa sana sehemu fulani fulani lakini sio Ikulu.

Pamoja na mtikila kuanza kupiga kelele (pengine ana malengo yake binafsi) lakini itakuwa vema iwapo KKKT itasimama na kutoa tamko kuhusiana na hii public outcry iliyotokana na kitendo chao
 

You are probably missing the point too! Kwani nani amesema aliyoyasema Rostam yanawakilisha kanisa? Kila mtu anajua kwamba Rostam sio kiongozi wa kanisa na wala hakutumwa na kanisa kusema alichosema, ametoa feelings zake! Kwa hiyo sioni hoja wala haja ya mchungaji wa kanisa kusawazisha kile alichosema Rostam.

Uwezo na mpaka wa kanisa ulikuwa ni kumwalika kufika kanisani na kumpa nafasi ya kuongea, lakini kanisa halikuwa na halina uwezo wa ku-control kile ambacho Rostam angesema baada ya kumpa jukwaa. Pengine issue hapa iwe sasa je, ilikuwa sawa kanisa kumwalika Rostam kwenda kanisani? Kwa maoni yangu kanisa siku wameamua kujenga urafiki na kila mtu mwenye pesa kwa ajili ya kutunisha mifuko yao. Otherwise sioni kabisa sababu za msingi za kumwalika Rostam kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli ya kanisa.
 
''mamvi'' i like that.Huyo jamaa naye nuksi.kwenye hilo anahusika.
 
Tuliposema wamelala kitanda kimoja na wezi na kujifunika blanketi na mafisadi, si Kanisa walidhani tunawalaumu bure? Sasa leo wamekutana wakifanya unajisi wao hadharani, wataweza kujiweka tena wakfu?
Mwanakijiji iko wapi ule walaka wako kwa viongozi wa dini?
 
Kina Mtikila ndiyo wale wenye ile COALITION FOR FREEDOM AND JUSTICE!
Wao ndio watakaopelekeshana na MAFISADI kwa niaba ya Taifa!
Coalition hiyo ina Masheick,MAASKOFU,ccm safi,wapinzani safi,wanasheria,viongozi wa dini safi na wafuasi wao wenye mawazo HURU!
Navyoelewa...Hii ndio coalition itakayofunguwa kesi ya EPA kama kukiwa na Mizengwe!
Nani kasema ni KKKT wenyewe ndiyo wakutuamlia? Wajiunge na coalition na viongozi wakileta za kifisadi washarika watawatema...!
At least wale WAZALENDO!
 
Kwa taarifa yenu kati ya washirika prominent wa kkkt Kinondoni ni wazee wa kanisa Spika Samweli Sitta na mh.Mwambalaswa(MB),tafakari!
 
Kwa taarifa yenu kati ya washirika prominent wa kkkt Kinondoni ni wazee wa kanisa Spika Samweli Sitta na mh.Mwambalaswa(MB),tafakari!

Bishanga kama wewe ni Mzee Mzima wa Kipindi marufu cha "Mambo Hayo"..Karibu ukumbini mkuu.

Kama ni wewe basi pokea salam kutoka hapa USA.

NB:Vipi kuhusu msimamo wa Askofu wao Mkuu? Ni lazima waweke wazi kama mwaliko alipewa kwa baraka za nani ili waumini wajuwe pa kwenda na si kulishwa pilao na kushangilia MAFISADI kwa AMRI za wachungaji wenye mielekeo hiyo!

Walikuwa wapi wakati Kilaini aliposema Taifa liombewe na kuanzisha maombi hapo jangwani kama tulivyoomba hapa jf?
 
Ninachojua ni kuwa ni lazima kanisa litasema na kuweka mambo sawa laa sivyo linaweza kukumbwa na msukosuko wa kuanza kupambana na waumini wao ambao wanaupinga ufisadi ambao ndio wengi zaidi ya hao wenye vijisenti.

Wasiposimama wajue kuwa huu unaweza ukawa ndio mwanzo wa KKKT kupasuka na kuanzishwa kwa KKKT mbili .
 

Sema weye KIAZI..Miye MUHOGO Taab TUPU..!

Kwani Nikisema nitaambiwa nina MZIZI!

Niliwaambia toka mwanzo wataweza kusababisha MAPINDUZI MABAYA NA WAUMINI WAKAWAGEUKA!

Ni wazi KUNA WACHUNGAJI MAFISADI WASIOJALI UBINADAMU NA WENYE KUJALI PESA ZAIDI!

WAUMINI WATAWATAMBUWA TU!
 



Jeeezus Christ! Did the Mchungaji really said that?? TUMEKWISHA, in capital letters!!
 

Gwiji kuja mbele ya Bwana sivyo hivyo yakhe!!! Sio kufanya kama unavyoenda kilabuni.... Kwenda mbele ya Bwana ni kutubu makosa na kubadilika... kitu ambacho Rozi Azizi hakukifanya!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…