Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Hilo ni suala binafsi kwani Mwanaasha na Ridhwani wamezaliwa na mama mmoja kwi! kwi! kwi! ahaaaaa!!!!!!

HAo ni watoto wa NDANI YA NDOA iliyo halali! hata angeamua kuzaa na wanawake wanne tofauti DINI YAKE INARUHUSU ! nikuulize wewe! hao walozaliwa na raisi wako DHAIFU WA NAFSI ni wa NDoa? usikurupuke mkuu, tunataka ujibu hoja!~ huyu hafai kuwa RAis narudia , atajaza mimba watoto wetu bure !
 
Huyu mzee hapo sasa ndo simwelewi kwani kuishi bila ya hivi viumbe hawezi umri wenyewe umesonga.Baba slaa tulizana hawa wanawake watakuvuruga tu
 
Siku si nyingi ukweli utaujuwa na utajutia posti yako hii.
Dr hakumuoa huyo Kamili, na wanao wajuwa wametanabaisha kuwa hawakuwahi hata kukaa pamoja.
Sasa hii ndoa mnayoilazimisha hapa ni ipi?
ETI Utajutia...upofu mwingine wala hauna maana hata kidogo na nakuona umekazana sana kujibu post mbalimbali...kazi unayo maana ake hadi unashindwa kabisa kufahamu nini kimeandikwa!! Ni wapi nimelazimisha hiyo unayoita ndoa?! Ni wapi nimesema Dr Slaa alimuoa huyo Rose?!!!!!

To cut story short; si wewe wala yeyote mwenye ubavu wa kumsafisha Dr. Slaa. Ni Dr Slaa mwenyewe ndie mwenye ubavu huo.
 
Hivi yule jamaa aliyefungua kesi ya kudai fidia ya kupokonywa mke aliishia wapi?

Haya yalikuwa maajabu ya uchaguzi wa 2010, CCM walikuwa wameshikwa pabaya na CDM, Jamaa wakawa wanatafuta kila mbinu ya kujikwamua. uchaguzi umepita na kila kiyu kimesahaulika.
 
Mkuu Buchanan Naomba uihamishie hii thread kwenye jukwaa la habari mchanganyiko au Mapenzi hii sio Siasa

Kweli kabisa Mkuu, hamna siasa hapa!
Kuna sheria, Mapenzi na ni kitimbi cha wanasiasa binafsi.....

Naunga mkono hoja kuwa itolewe huku kwenye jukwaa la siasa!
 
Nahisi kuna mtu anatafuta haki yake ya kutambuliwa kama Mke wa kwanza na hivyo kuwa 'First Lady' 2015! Serikali inatambua mke mmoja tu, tena wa kwanza basi. Na hiki ndicho kilimfanya hata Mama Anna Mkapa kurudiana na Mumewe William Mkapa mwaka 1995 licha ya kutokuwa na mawazo kabla kama angekuja kurudiana na mwenzi wake. Baada ya Urais wa Mkapa kuisha mwaka 2005 Mama Anna Mkapa akala kona. Leo hii William Mkapa anaishi mwenyewe Lushoto!

TUMBIRI (PhD, HULL University - United Kingdom),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Sina uhakika sana na maisha ya ndoa ya Rose na Slaa yalivokuwa ila kama kweli walifunga ndoa kanisa katoliki inakuwaje Slaa anataka kufunga ndoa nyingine huku akielewa wazi kanisa katoliki haliruhusu ndoa mbili?na kama waliachana kwa nini Slaa asingezingatia taratibu za kisheria kuachana ikiwa ni pamoja na kugawana mali? Mwanamke anayeishi nae sasa hivi iliwahi kusemwa ni mke wa mtu na kesi ikafunguliwa mahakamani je hukumu imetolewa? kama bado inakuwaje slaa anataka kufunga ndoa na Josephine wakati kuna kesi inayohusu uhusiano wao??Namwamini na namheshimu sana Dr.Slaa kama mtu makini na anayefanya mambo kwa makini sana na kufuata sheria je ukweli kuhusu hili upoje?? Amenukuliwa na ,MWANANCHI akisema kuwa hizi ni siasa je ni siasa kivipi? hebu wana JF mwenye ukweli au ufafanuzi kuhusu hayo niliyo jaribu kuyachanganua auweke hapa ili niwe comfortable!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ritz,
Upo hapo ! hivi kweli tumeishiwa na viongozi? Mtu mzinifu mkubwa hana hata maadili maisha katelekeza mpaka watoto wake mwenyewe, ndiye Dr. Slaa huyu huyu ambaye baadhi ya mapimbi wanadai ni mtu makini? Huku akipanda kwenye majukwaa anajinadi ni mtu safi kweli wanafiki wana mji wao na mji wao ni Chadema

Chama
Gongo la mboto DSM


Hatuchagui Askofu Mkuu wa Tanzania au Shehe Mkuu...tungeangalia hayo.....Tunapaswa kuchagua mtu atakayetutoa hapa tulipo na kutupeleka sehemu nyingine ....atakayetutoa kwenye mikataba ya kipuuzi, atakayesimamia vyema rasilimali nyingi za taifa hili...swala la kuwa na mke, kutokuwa naye is immaterial.....Malawi maskini wenzetu lakini tuliowazidi kwa utajiri wana mwanamke asiye na mume...ni mtalaka..... kwa mikakati aliyo nayo huyu mama wataanza kutupumulia sasa hivi...south Africa wanaongozwa na mzinzi aliyekubuhu.....wanapeta...Hata kenya Kibasi ana Lusi na wengineo....wanasonga mbele....Hawa "watakatifu" wetu wa tanzania wenye first lady mmoja wametupeleka wapi??
 
Siasa bwana! Amekataa kuonana nao, sasa naona wanatumia kila njia wamfanyie interview!

Ndoa hailazimishwi!
Chakujiuliza huyo rose ana ng'ang'a nia nini?
Watoto hawafikishi miaka miaka 18? Kama wanazidi miaka hiyo sidhani kama bado wanahitaji matunzo!
 
Huyu rose kamili na Dr. Slaa anatudhalilisha WAKRISTO. Na mapadri wetu na Muadharm PP wamekaa kimya kama vile UKRISTO NDIVYO unavyofundisha.

Kama utaratibu ndio huu wa Dr. Slaa, basi WAKRISTO HATUMTUMIKII MUNGU WA KWELI BALI SHETANI.
 
Molemo;
Na wale wenzako mlikokuwa mkisimama kidete kumtetea Dr. Slaa hivi nyuso zenu mtaziweka wapi? Ikiwa ameshindwa hata kutunza watoto wake ataweza kulitunza taifa? Yaani watu wa umri wake hivi sasa wanaishi kwa bonus umri umeshapita badala ya kuwa mcha mungu yeye anaendekeza mambo yasiyo na msingi. Jamani upadri ulimshinda basi hata kutunza viumbe wa Mungu kweli ni haki? Kumwachia mama wa watu akihangaika kutunza watoto peke yake huku yeye akivunja amri ya Mungu na mwanamke wake mwengine kweli hii ni sahihi wanachadema?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hiyo labda ni Bongo, lakini kwa nchi za wenzetu, the minute mmeanza kutumia address moja au mki-file kodi pamoja, majirani, ndugu, jamaa na marafiki hawahusiki tena. Sheria inafuata mkondo wake.
Si dhani kama ni hivyo hasa maana hiyo dhana ya ndoa naamini sehemu nyingi duaniani ni dhana inayokanushika (rebuttable presumption).

Maana pamoja na hilo la muda, na umma unaozunguka pia kuna masharti mengine ambayo ni muhimu sana pia - kama wahusika kuwa katika umri unaokubalika kisheria wakati wanaanza kukaa pamoja, mwanamke asiwe na ndoa nyingine inayoendelea (kwa nchi ambazo polyandry haikubaliki kama Tanzania), mwanaume asiwe na ndoa ya kikristo inayoendelea au asiwe na ndoa nne za kiislamu zinazoendelea, wawili hao wawe na uwezo wa kuwa mume na mke (mf: wasiwe ndugu wa karibu - dada na kaka, baba na mtoto, babu na mjukuu nk).
 
Sina uhakika sana na maisha ya ndoa ya Rose na Slaa yalivokuwa ila kama kweli walifunga ndoa kanisa katoliki inakuwaje Slaa anataka kufunga ndoa nyingine huku akielewa wazi kanisa katoliki haliruhusu ndoa mbili?na kama waliachana kwa nini Slaa asingezingatia taratibu za kisheria kuachana ikiwa ni pamoja na kugawana mali? Mwanamke anayeishi nae sasa hivi iliwahi kusemwa ni mke wa mtu na kesi ikafunguliwa mahakamani je hukumu imetolewa? kama bado inakuwaje slaa anataka kufunga ndoa na Josephine wakati kuna kesi inayohusu uhusiano wao??Namwamini na namheshimu sana Dr.Slaa kama mtu makini na anayefanya mambo kwa makini sana na kufuata sheria je ukweli kuhusu hili upoje?? Amenukuliwa na ,MWANANCHI akisema kuwa hizi ni siasa je ni siasa kivipi? hebu wana JF mwenye ukweli au ufafanuzi kuhusu hayo niliyo jaribu kuyachanganua auweke hapa ili niwe comfortable!!

Hajawahi kufunga ndoa na Rose ila walizaa watoto.
 
Hii kali mbunge na mshahara wake na posho zote analalamika kutelekezwa?

Je alikuwa wapi toka slaa alipotangaza uchumba na josefine 2010?

Viongozi wa chadema akina mdee, komu kamati kuu wako wapi kumwita mama huyu kupata sluu nje ya mahakama?

Ila kikubwa wananchi wanajua na hili litamuongezea umaarufu slaa.
 
Mkuu Chama,

Hivi tukiweka kigezo cha uzinzi kwenye katiba mpya kuwa ye yote ambaye aliwahi kutembea na mwanamke nje ya ndoa yake hapaswi kugombea urais. Je, ndani ya ccm wewe unampendekeza nani atatimiza kigezo hicho?
 
Siku si nyingi ukweli utaujuwa na utajutia posti yako hii.
Dr hakumuoa huyo Kamili, na wanao wajuwa wametanabaisha kuwa hawakuwahi hata kukaa pamoja.
Sasa hii ndoa mnayoilazimisha hapa ni ipi?

Duuh! Yaani Dr na Padre Mstaafu alikuwa ana hit and run for that long since 1987. Duu huyu kiboko!
 
Dr.Slaa kwenye maisha ya ndoa ni kama anagiza, haiwezekani umwache mke bila utaratibu maalumu,hapohapo unaenda kuishi na mke wa mtu ambae kisheria hawajaachana rasmi na bwaanake...tunajua haya ni maisha binafsi ya Dr. Lakini tunaoathirika na vituko vyake ni sisi tuliojenga imani naye.!!
 
Katika kile kinachoonekana kupunguza kasi ya CDM na kiongozi wake machachari Dr Wilbroad Slaa Mbunge wa viti Maalum wa chama hicho Rose Kamili amekwenda mahakamani kumshtaki Katibu mkuu wake Dr Wilbroad Slaa kwa kile anachopinga uhusiano wa Dr Slaa na mke wake mtarajiwa Josephine Mushumbusi.

Katika hati ya mashtaka aliyo nayo Rose analalamikia kutelekezwa yeye na watoto wake wawili baada ya Josephine kuingilia ndoa yao.Anaiomba mahakama itamke uhusiano wa Dr Slaa na Josephine ni batili.

Dr Slaa ameachana lini na Bi Rose?
Waliachana kwa sababu ya Bi Josephine au kulikuwa na sababu nyingine?
Dr Slaa ameacha kugharamia matunzo ya watoto wake kuanzia lini?

Najiuliza maswali haya huku nikitazama "timing" ya mashitaka ya Bi Rose nasikia harufu ya siasa zetu zile zilee....

Ghafla nimemkumbuka Bi Angelina yule mzazi mwenza wa Mheshimiwa Agustine Lyatonga Mrema na drama alizozimwaga hadharani wakati ule.....
 
Back
Top Bottom