Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Ukijibu swali hili nitakubaliana na wewe kuwa Dr Slaa hakupaswa kwenda Ikulu 2010.
Je, bosi wako mkulu analiyeko magogoni ana watoto wangapi na kwa wanawake wangapi?
Hakuna mtu atakayekusumbua hata kama una watoto mia saba lakini unawatunza na mama zao mnaheshimiana. Ila ukishaanza kupelekwa mahakamani, inaonyesha kuna issues fulani zinakutatiza (responsibility?).
 
Katika hati ya mashtaka aliyo nayo Rose analalamikia kutelekezwa yeye na watoto wake wawili baada ya Josephine kuingilia ndoa yao

​Please naomba kujua ukweli huu indeep
 
imekaa vizuri hii...............maana kwenye kampeni walipanda kwenye jukwaa moja leo imekuwaje?
 
Jibu hoja

Hoja ipi unayotaka nikujibu acha kwanza jmjadili mzinifu na kahaba asiye na aibu amefanya mambo mengi machafu.
1. Kamkimbia mke
2. Kachukua mke wa mtu
3. Katekeleza watoto
4.Kuwadanganya watanzania eti ana mke kumbe ni kimada
Tujadili hayo hapo juu hiyo ndiyo hoja ya msingi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Aweda.
Kila siku nasema huyu mzinifu Dr. Slaa hana credibility uzinifu uweke kando basi hata hili kulea watoto wako mwenyewe? Kama ni US huyu alikuwa keshalazimishwa zamani ajiuzulu, ndani ya CCM hakuna mke aliyepeleka kesi mahakamani kuweka pingamizi la mume wake asioe kimada kama yupo tuwekee hadharani tumseme, katika mambo ya familia hatutaki mchezo, kama alijuwa hawezi kulea kwa nini asivae mpira? Watu kama Dr. Slaa ndio wanaompka kazi ya ziada mh. Raisi imebidi aende kwenye mkutano wa mpango. Kama huwezi kulea usizae!

Chama
Gongo la mboto DSM

Mosi, jibu swali langu, Bosi wako aliyeenda Majuu kupigania Family planning ili kumsaidia Slaa ana watoto wangapi na kwa wake wangapi?
Sheria gani inamtaka slaa kulea watu wazima wa zaidi ya miaka 25 na zaidi? Hivi unajua kuwa hao watoto wa Slaa sasa nao wanapaswa kuwa na familia yao?
Tatu, Hoja ni kwamba Dr Slaa ameshatakiwa au hoja ni kwamba amekosea? Kama ni kushtakiwa hata mimi naweza kufungua kesi ili nijue kodi yangu inalipa wake na watoto wangapi wa Rais wetu. Ni haki yangu kujua matumizi ya kodi yangu. Kama hoja ni kosa, nitafutie mtakatifu moja aliyeko ccm. Kama wameshindwa kujizuia kufisadi fedha zetu, wamewezaje kutozini?
 
Wananchi wakimtaka Dr. Slaa, hakika watampata kama rais wao; Mengine ni maigizo tu, Yupo mandela, clinton, zuma na wengine wengi tu.
 
Katika hati hiyo ya madai, mbunge huyo anadai kuwa ndoa inayotarajiwa kufungwa kati ya Dk Slaa na Mushumbusi ni batili kwa sababu kuna ndoa nyingine halali na inayoendelea kuishi kati ya Slaa na Kamili iliyofungwa mwaka 1985.
Kamili pia amewasilisha hati hiyo ya mashtaka kwa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akimweleza Askofu Mkuu huyo wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam kuwa moja ya Parokia za Dar es Salaam zina taarifa ya ndoa hiyo.
Nakala ya madai hayo pia imewasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Msajili wa Ndoa na kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbulu.

REJEA: Mwananchi ya leo(12/07/2012)


Naomba nirudie tena kwamba Slaa hakuwahi asilani kufunga ndoa na Rose ila wamezaa watoto 2.Hivi mkuu unadhani Slaa ni mjinga kiasi hicho? Ndio maana ujue tayari Siasa imeingia.
 
Katika kile kinachoonekana kupunguza kasi ya CDM na kiongozi wake machachari Dr Wilbroad Slaa Mbunge wa viti Maalum wa chama hicho Rose Kamili amekwenda mahakamani kumshtaki Katibu mkuu wake Dr Wilbroad Slaa kwa kile anachopinga uhusiano wa Dr Slaa na mke wake mtarajiwa Josephine Mushumbusi.

Katika hati ya mashtaka aliyo nayo Rose analalamikia kutelekezwa yeye na watoto wake wawili baada ya Josephine kuingilia ndoa yao.Anaiomba mahakama itamke uhusiano wa Dr Slaa na Josephine ni batili.

Kuna tetesi zimezagaa Rose Kamili amenunuliwa ili kuvuruga mijakati ya CDM kuiandama serikali ya CCM

Source:Tanzania Daima

Updates from Mwananchi...Majibu ya Dr Slaa
Dk Slaa: Nimeyazoea
Alipotakiwa kuzungumzia kesi hiyo nje ya Mahakama, Dk Slaa alisema: “Hayo mambo nimeyazoea na kimsingi hayanipi shida yoyote.”
Alipoulizwa endapo anajipanga vipi kulipa fidia hiyo alijibu: “Kesi ni kesi hivyo siyo kila kinachoombwa kwenye kesi lazima kilipwe.”
Hata hivyo, Dk Slaa alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kuwa liko kwa mawakili wake lakini akasema amebaini kuwa hizo ni hila na michezo michafu ya kisiasa.
“Kwanza siyo pingamizi moja tu, kuna pingamizi mbili mahakamani lakini kwa ufupi ifahamike kuwa hizo ni hila.”
Anunuliwe na Nani mtu anadai haki yake na wanae mbona mnapenda kupindisha kila kitu!Akitokea mume wa Mshumbuzi kudai ametumwa akitokea mke wa Dr Slaa kudai haki zake ametumwa.Dr anaelewa fika alitakiwa kumalizana na Mkewe hasa ukizingatia sheria ya ndoa ya Kikatoliki.
 
Hakuna mtu atakayekusumbua hata kama una watoto mia saba lakini unawatunza na mama zao mnaheshimiana. Ila ukishaanza kupelekwa mahakamani, inaonyesha kuna issues fulani zinakutatiza (responsibility?).

Jibu hoja,
JK ana watoto wangapi kwa wanawake wangapi? Anawatunza kwa kodi yangu lazima pia nijue kiasi cha fedha inayotumika. Sawa!
 
Jibu hoja,
JK ana watoto wangapi kwa wanawake wangapi? Anawatunza kwa kodi yangu lazima pia nijue kiasi cha fedha inayotumika. Sawa!
Anawatunza kwa kodi yako? Kwani yeye halipi kodi? Hafanyi kazi halali inayompatia mshahara?
Let's say an watoto mia na wanawake mia, whats your point?
 
Kwa hili, Dr Slaa kajichafua mwenyewe. Yupo mzee wangu mmoja alipata kuniambia usipokuwa mpenda MALI utapenda wanawake/wanaume. Haya mawili hayakwepeki. Na baadhi yetu tunapenda vyote viwili. Dr Slaa anamfahamu vizuri Rose Kamili. Kwa nini leo wamefikishana hapa ni jambo la kushangaza kidogo. Alidhani kwa kumleta CHADEMA na kumpa UBUNGE vingemtosha kweli? Rose Kamili hawezi kutosheka bila kumpata Dr Slaa mwenyewe.
 
Ukijibu swali hili nitakubaliana na wewe kuwa Dr Slaa hakupaswa kwenda Ikulu 2010.
Je, bosi wako mkulu analiyeko magogoni ana watoto wangapi na kwa wanawake wangapi?
Aweda
Mh. Raisi Kikwete ni muislamu dini inamruhusu kuoa mke zaidi mmoja, dini zetu hazijatupangia idadi ya watoto tunachopaswa ni kulea malaika wa mwenyezi Mungu; sasa kama mh. Raisi ana mke zaidi ya mmoja hajafanya kosa la kikatiba wala la kidini, kama ana watoto 50 pia hajafanya kosa la kidini wala la kikatiba, mh. Raisi analea familia yake wala hajamkimbia mama Salma kwenda kuishi na kimada, je kuna yeyete ambaye amekwenda mahakamani kudai mh. Raisi katekeleza familia yake?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Naomba nirudie tena kwamba Slaa hakuwahi asilani kufunga ndoa na Rose ila wamezaa watoto 2.Hivi mkuu unadhani Slaa ni mjinga kiasi hicho? Ndio maana ujue tayari Siasa imeingia.

Nashukuru kwa kunihakikishia hilo mkuu wangu maana nilikuwa disturbed sana ukizingatia kuwa namuamini sana na pia ni mtu makini anayefuata sheria na taratibu !!!
 
Watu kama hawa wanakwamisha na kuchelewesha ukombozi !
Ashindwe na alegee.lol
Mnamlaumu huyu mama badala ya kumlaumu Dr!Dr aliendaje kutangaza ndoa nyingine wakati sheria za kanisa katoliki zinasema wazi kwamba ndoa ni ya mke mmoja na hamtengani mpaka kifo!
 
Jamani em tuache itikadi za kisiasa pembeni kama mtu anashindwa kutatua mgogoro binafsi wa kifamilia kama baba, atawezaje kuja kuliongoza Taifa lenye migogoro lukuki kama Rais kutoka kila kona ya mipaka ya Tanzania.

Pia turudi nyuma kidogo huyu mzee inasemekana alikua Padri, mbona matendo yake hayaendani na maisha ya upadri alioisha kwa miaka mingi nyuma.

Hata kama aliacha kazi hiyo ya Mungu hatukutegemea kabisa kuwa na matendo machafu ya namna hii.

Mkuu swali dogo,
Kwani Slaa anashindwaje wakati mkulu aliyeko magogoni ameweza na mmeshindwa kunitajia idadi ya watoto wake na wake zake?
Hivi unajua kuwa Rais wa pili kwa heshima USA, Abraham Lincolin alikuwa na matatizo ya ndoa na hayakumzuia yeye kuwa Rais Bora? Wengi hamjui kuwa mke wa sasa wa mandela si wa pili, bali ni watatu. Je, heshima yake imeshuka?
Hoja ya Upadre inabidi uanzishe uzi mwingine maana ni mjadala mwingine pana.

 
Mkuu swali dogo,
Kwani Slaa anashindwaje wakati mkulu aliyeko magogoni ameweza na mmeshindwa kunitajia idadi ya watoto wake na wake zake?
Hivi unajua kuwa Rais wa pili kwa heshima USA, Abraham Lincolin alikuwa na matatizo ya ndoa na hayakumzuia yeye kuwa Rais Bora? Wengi hamjui kuwa mke wa sasa wa mandela si wa pili, bali ni watatu. Je, heshima yake imeshuka?
Hoja ya Upadre inabidi uanzishe uzi mwingine maana ni mjadala mwingine pana.


Ahaaaaaaaaaaaaaaa nilishakuambia acha kumfananisha kituko Dr. Slaa na viongozi mahiri hapa kinachojadiliwa si matatizo ya ndoa ni UZINIFU kumkimbia mke, kuvunja ndoa ya watu na kutekeleza watoto mbona unataka kubadilisha mada.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mbona naona huyu aliyetuma hii thread kama haeleweki vile slaa hatak kugombea ila kwa kubalika sana ni lazima agombee!
 
Wananchi wakimtaka Dr. Slaa, hakika watampata kama rais wao; Mengine ni maigizo tu, Yupo mandela, clinton, zuma na wengine wengi tu.

Kabla hajafika kwa watu kuna factor ya party nomination, ndiyo anaweza kuwa anapambana nayo.
 
Wewe unasema kama tunataka mtu thabiti wa kutusimamia kwenye issues zetu nyingi ikiwemo madini. Sasa bro! Ikiwa huyu mtu ameshindwa hata kuisimamia nafsi, heshima, dini yake na dhamira yake kwa:-

1) Kushindwa kufuata maadili ya u-padre mpaka akafukuzwa

2) Kuamua kukaa na Kimada (bi Josephine) bila kujali nafasi yake kama kiongozi mwandamizi wa chama ''makini''

3) Kutelekeza familia yake. Hivi kama watoto wake binafsi amewafanyia hii kitu, je atamkumbuka Mahimbo kule Kijijini kwetu!

Kikwebo.

Walau wewe umekuja kwenye hoja ingawa bado unadeal na personalities lakini nitakujibu.....Kwanza hujajibu hoja yangu kuwa hawa "watakatifu" ambao wako CCm na ambao wana "maadili" na "wanaheshimu ndoa zao" mbona wanazidi kutuingiza kaburini??...Mbona nchi nyingine zinaendelea wakati marais wake ni wazinifu?? je tunamchagua kiongozi wa kidini au kiongozi wa nchi??

Kwenye RED si kweli na Dr Slaa hajawahi kufukuzwa upadre bali aliacha kwa hiari yake....kama una ushahidi wa hili weka hapa vinginevyo usipende kubeba majungu ambayo hayana ukweli wowote...

Kwenye Blue ni bora anayekaa na kimada (kama kweli uko sahihi) kuliko uchafu uinaofanywa na hawa watakatifu wa CCM ...sijui kama mmehskwenda kusuluhisha ndoa aliyovunja Nchemba igunga anyway.... kuna mmoja pia kauliza kuwa baba Mwanaasha ana watotot wangapi kwa kina mama wangapi? tukiingia huko nina uhakika wengine tutakula ban soon kwakuwa tutaanika uozo wa kutisha hapa....

Kwenye Green subiri mahakama itatoa majibu ya hilo kama kweli wametelekezwa na ni kwa misingi ipi wametelekezwa..



 
Back
Top Bottom