Tutakuweka wewe! Ama Mramba arudishwe teh teh! Wewe unafikiri hawa Wananchi wenzetu kama wamekataliwa na serekali yenu wafanyeje. Ukimkataa mtoto akiingia mtaani kumsaka baba yake utamlaumu. Rombo kiloa ya sukari shs 4500/= unategemea nini? Tunashindwa kulinda mipaka yetu tunalinda maslahi ya watu wachache. Kama kwa kuzuia magari yalobeba sukari pale Himo basi tuongeapo sukari ingekuwa inapatikana Moshi nzima na mikoa mingine. Eti sasa imekuwa lazima uende kwa mtendaji ukapate kibali cha sukari. Tanzania hii ya Miaka 50! Kweli tunashindwa kujenga miundo madhubuti ya kutoa huduma kwa wananchi wetu.Aibu sana.
Wa Rombo wapuuzi wakubwa.Wakenya wenyewe wanataka kuwa watanzania kukimbia njaa.Kwani lazima munywe chai,si nyinyi huwa munakunywa uji wa ndizi?.
Yaani kukosa sukari tu munakimbia nchi.si watu wa kuaminika hata kidogo.Ndio nyinyi munaobadili dini na vyama kwa kuhongwa vitu vidogo kama pombe na mitumba.Poleni sana warombo.
Naomba uchunge mdomo wako
Kwa hiyo Wachagga wa Rombo wameamua kuamia Kenya? Vizuri tunaheshimu maamuzi yao
siyo kuheshimu maamuzi yao, inatakiwa ujiulize kwanini wamehamia kenya!
Ingawa siungi mkono kitendo cha kupandisha bendera ya nchi nyingine,lakini serikali ya Tanzania ndiyo imewafanya wananchi wakafikia huko.Sukari imezuiliwa Himo bila kujali kuna Eneo lingine la Tanzania mbele ya Himo linaloitwa Rombo.
Rombo inastahili haki zote kama wananchi wa maeneo mengine.Kwa muda mrefu rombo imekuwa ikikandamizwa na kudharauliwa na watawala wetu,sijui ni kwa nini hasa.
Mkuu wa mkoa ameshindwa kuweka mkakati wa kutosha kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma hii wakati huo huo akidhibiti magendo.Ni kwa nini maeneo mengine yaliyopakana na nchi jirani wameweza kudhibiti hali hii bila kubughudhi wananchi ndani ya territory yake halafu mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ashindwe.Madiwani wa CCM ndiyo wanaoongoza halmashauri hivi kweli wanashindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kuweka ukaguzi katika usambazaji wa sukari kuanzia Himo,Mwika,Mamsera,Mkuu,Mashati,Useri na Tarakea? ni kwanini tusiweke logistics katika level yenye uwajibikaji wa kisiasa kama kata kisha nadharia ya monitoring and evaluation ikatumika?
Wananchi wa Rombo hata katika ugawaji wa Mahindi ya misaada madiwani wa CCM na wenyeviti wa vitongoji walitaka watu waonyeshe vitambulisho kwanza yaani kadi za CCM ndiyo wagawiwe.Nina ushahidi wa majina ya watu wasiojiweza kabisa hawakupewa mahindi,na pia hujuma iliyotumika kudhulumu watu waliostahili kupewa mahindi hawakupewa.Nimeorodhesha malalamiko na ushahidi wote ukajadiliwe kwenye vikao vya baraza la madiwani walifanyie kazi watoe ripoti kwa wananchi wa Rombo
Wananchi wa rombo wanatia huruma kwa jinsi wanavyobambikiwa kesi na watendaji wa serikali,ni ukandamizaji uliopitiliza.Kulikuwa hakuna vituo vya polisi na hata vilivyopatikana vinatumika kama tools za kutisha raia na kujipatia hela.Mojawapo ni kesi iliyomuhusu mwananchi mmoja anaitwa Aristariki Kimaryo aliyewekwa mahabusu na mtoto wake pamoja na mkwe wake kituo cha polisi Mashati kisa hawajatoa hongo ya kumnusuru mtoto wake,hivyo polisi wakaamua kuwasweka mahabusu.Tulipowahoji polisi sababu ni nini wakaishia kutoa vitisho hadi tulipotishia kutumia nguvu ndipo walipowaachia
Tembo wanaotoka nchi jirani wamekuwa wakivamia mashamba ya wananchi,wakiharibu na hata kuuwa watu lakini hakuna fidia ya maana iliyofanyika.Wanachi wa Rombo sasa inabidi kwa ruthless,wanyama wanaoingia kwenye mashamba inabidi wauwa na hakuna kutoa taarifa kwa idara ya maliasili,wauawe na pembe ziuzwe hela iingizwe kwenye akaunti maalumu ya kufidia walioathiriwa na wanyama hao
Leo hii watu wanawalaumu watu wa Rombo kwa kujiskia sehemu ya kenya bila kufikiria saikolojia iliyowaathiri ya muda mrefu.Huduma za kijamii na kiuchumi zimekuwa attached na wakenya.Hata Radio ya Taifa TBC haifiki kule badala yake KBC ndiyo inasikika sijui kama watu walioko Tunduma,Songea na kigoma wanasikiliza redio za Zambia,malawi,msumbiji au DRC kuliko TBC au ni Rombo peke yake?
Sasa serikali itende haki,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,madiwani pamoja na Mbunge wa Rombo simamieni maslahi ya wananchi wa Rombo.Serikali iache vitisho,iache kuwatisha wananchi wa Rombo.
Kwa hiyo Wachagga wa Rombo wameamua kuamia Kenya? Vizuri tunaheshimu maamuzi yao
Usiwe unaaandika kwa kukurupuka wewe Kibaraka wa CCM!! Unajua taabu ya sukari kule Rombo wewe.
Unajua kilo moja ya sukari sasa hivi kule Ni shilingi Ngapi. Jaribu kufuatilia mambo ndio uandike *****.
Yaani wewe kwasababu ni mwana CCM hutaki kusikia mwananchi akilalamika Matatizo yake.
Jaribu Kutumia Kichwa angalau.
Kwa kupandisha hiyo Bendera serikali yenu sasa itatambua the seriousness of the situation.
Sishabikii kupandishwa Bendera ya Kenya. Ila nafurahia kuwa Hii serikali ya CCM itaona kule kule kuna tatizo.
Tafuta Sehemu nyingine ya kuwatetea magamba. lakini sio katika matatizo yetu.
sawa wewe unayejiita Mzee asiye na hekima?
Unaweza kuonyesha nilikounga mkono?mzeee unaunga mkono warombo kupandisha bendera ya kenya?nassari naye alidai jamhuri ya kaskazini
Siamini kama kuna Mtanzania Mzalendo anaweza Kufanya ujinga Kama Huu.
Kama ni kweli, basi Hao ni wahaini....serikali ipeleke JWTZ wazunguke na magari yao mitaani
Baada ya kunyanyaswa na vizuizi vya polisi vilivyomo mji mdogo wa Himo, viliosababsha upungufu mkubwa wa sukari na bidhaa nyingine za chakula, kiasa cha Rombo jimbo linaloongozwa na CDM, na linalopakana na nchi ya Kenya, kujisiakia wageni nchini mwao Tanzania, wamechukizwa na kitendo cha serikali yao ya Tanzania kuwanyanyapaa na wameamua kupandisha bendera ya Kenya! Source ITV
Tusitafute njia za mkato.Mbona ilikua rahisi kushulikia madai ya wananchi wa Rombo kuliko kutumia nguvu zote hizo?
Wananchi wa Rombo hawatishwi tena na matumizi ya ngivu kama serikali ilivyokua ikifanya kuwatisha watu kwa kuwapiga na kuwapeleka vijana kwa nguvu maituni kuzima moto katika mlima kilimanjaro
Badala ya serikali kuelimisha wananchi kutunza mazingira na kuwapa wananchi wake haki ili kujenga uzalendo mioyoni mwake wanaona ni afadhali watumie nguvu