Rombo wapandisha bendera ya Kenya?

Rombo wapandisha bendera ya Kenya?

Ujumbe umefika,wasipo soma nyakati tutapandisha ya AL SHABAB
 
Ukisikia wananchi wamechoshwa na serikali yao na ikafikia wakaamini serikali ya nchi nyingine hadi kufikia kupandisha bendera yake ujue viongozi wa serikali wasipobadilika basi nchi inaingia ktk mgogoro na raia wake. Yani wananchi wamepoteza kabisa uzalendo wao na kuichukia nchi yao kwa sababu ya dhuluma, hujuma, ukosefu wa huduma muhimu za kijamii, unyanyasaji, tuhuma za ufisadi na maovu mengine kabao kwa raia wasiokuwa an hatia kutoka kwa wakubwa wa nchi.

Mungu atuepushe na balaa lolote.
 
Hivi sasa ile nchi (TZ) ya asali na maziwa iko wapi?
 
Baada ya kunyanyaswa na vizuizi vya polisi vilivyomo mji mdogo wa Himo, viliosababsha upungufu mkubwa wa sukari na bidhaa nyingine za chakula, kiasa cha Rombo jimbo linaloongozwa na CDM, na linalopakana na nchi ya Kenya, kujisiakia wageni nchini mwao Tanzania, wamechukizwa na kitendo cha serikali yao ya Tanzania kuwanyanyapaa na wameamua kupandisha bendera ya Kenya! Source ITV

Huku ni kutokujua mzizi wa tatizo ili kupata suluhisho sahihi. Wameingia chaka mbaya sana na wanaoneka ni watu wakukimbia matatizo na wala si kukabiliana nayo.
 
nawaamini sana kina baba, kaka, mama, na dada zangu pia wadogo wangu mlio nyumbani rombo chochote mnachokifanya mna sapoti yetu tulio mbali kidogo hata huku tunafanya harakati za kupambana na huyu mfalme juha
 
Duh watanzania wanajivunia kuwa wakenya,truly kenyans all the time! Siamini ,hatari,ccm imefanya makubwa lakini hili la kuwanyanganya watanzania uzalendo wao hili kwa kweli ndio funga kazi.
 
Kutaka kujiunga na Kenya kwa matatizo ya sukari ni u-ignorance usio na kipimo. Kenya kuna njaa usawa huu, kwa aliyeenda Kenya hivi karibuni anajua hilo.

Na Rombo sasa ni jimbo la upinzani, ina maana hali ilikuwa bora wakati wa Mramba wa CCM? Mbunge wa CHADEMA afanye kazi, sio kupandisha bendera ya Kenya. Nimesikia watu wanataka kujitoa kwenye nchi na kujitangazia uhuru, sijasikia watu wanataka kujiunga na nchi nyingine, tena nchi yenyewe Kenya.

CHADEMA ianze kuwekeza kwenye elimu ya makada wa chama.
 
nakuunga mkono ben mm wakati ningali mdogo nlidhani MTUKUFU RAIS DANIEL ARAP MOI ndio rais wangu kwani sikujua kama kuna RTD AU MWINYI.kila kitu kuanzia vyakula nguo nk tulitoa kenya,hata sukari na bia za kenya. ITV ndio walau kwa sasa wameweka mnara wao kama 4 years ago.HAKUNA CHA TBC WALA NN. KBC TV HATA KAMA UNA ANTENA YA CHADEMA inashika bila chenga,na radio kibao za FM zote kenya. MM NADHANI ROMBO NI SEHEMU YA KENYA KWANI WAO WANATUTHAMINI ZAIDI KULIKO SERIKALI YETU YA MKWARE. elimu vijana wanavuka boda, biashara wanafanya bila hata pasport hata mashamba twalima kule. ntajivunia nn kuitwa mtanzania wkt serikali imetutenga kisa jimbo pinzani??? WAMETUWEKEA LAMI LKN WAKATUTENGA. ole wao magamba. soon tutaungana na arusha,mwanza na mbeya mikoa mingine itafuatia ndio kiama kwa magamba.



Tembo wanaotoka nchi jirani wamekuwa wakivamia mashamba ya wananchi,wakiharibu na hata kuuwa watu lakini hakuna fidia ya maana iliyofanyika.Wanachi wa Rombo sasa inabidi kwa ruthless,wanyama wanaoingia kwenye mashamba inabidi wauwa na hakuna kutoa taarifa kwa idara ya maliasili,wauawe na pembe ziuzwe hela iingizwe kwenye akaunti maalumu ya kufidia walioathiriwa na wanyama hao

Leo hii watu wanawalaumu watu wa Rombo kwa kujiskia sehemu ya kenya bila kufikiria saikolojia iliyowaathiri ya muda mrefu.Huduma za kijamii na kiuchumi zimekuwa attached na wakenya.Hata Radio ya Taifa TBC haifiki kule badala yake KBC ndiyo inasikika sijui kama watu walioko Tunduma,Songea na kigoma wanasikiliza redio za Zambia,malawi,msumbiji au DRC kuliko TBC au ni Rombo peke yake?

Sasa serikali itende haki,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,madiwani pamoja na Mbunge wa Rombo simamieni maslahi ya wananchi wa Rombo.Serikali iache vitisho,iache kuwatisha wananchi wa Rombo.
aku
 
Wa Rombo wapuuzi wakubwa.Wakenya wenyewe wanataka kuwa watanzania kukimbia njaa.Kwani lazima munywe chai,si nyinyi huwa munakunywa uji wa ndizi?.
Yaani kukosa sukari tu munakimbia nchi.si watu wa kuaminika hata kidogo.Ndio nyinyi munaobadili dini na vyama kwa kuhongwa vitu vidogo kama pombe na mitumba.Poleni sana warombo.
 
Binafsi simfagilii kabisa mbunge wangu huyu. nadhani 2015 CDM tutafute mtu mwingine...

Tutakuweka wewe! Ama Mramba arudishwe teh teh! Wewe unafikiri hawa Wananchi wenzetu kama wamekataliwa na serekali yenu wafanyeje. Ukimkataa mtoto akiingia mtaani kumsaka baba yake utamlaumu. Rombo kiloa ya sukari shs 4500/= unategemea nini? Tunashindwa kulinda mipaka yetu tunalinda maslahi ya watu wachache. Kama kwa kuzuia magari yalobeba sukari pale Himo basi tuongeapo sukari ingekuwa inapatikana Moshi nzima na mikoa mingine. Eti sasa imekuwa lazima uende kwa mtendaji ukapate kibali cha sukari. Tanzania hii ya Miaka 50! Kweli tunashindwa kujenga miundo madhubuti ya kutoa huduma kwa wananchi wetu.Aibu sana.
 
Hatuna rais bali yupo mfano wa rais

Unanikumbusha ile ya mjerumani, mchina na mtanzania!
Ujerumani mtoto alizaliwa hana mikono madaktari wakamfanyia upasuaji akawekewa mikono na akawa bondia maarufu.
China alizaliwa mtoto hana miguu wakamwekea miguu ya bandia akabata medali ya dhahabu ya marathon
Tanzania sasa akazaliwa mtoto ................... malizia bana
 
serikali ya ccm isipokuwa makini nchi inawashinda-
mara mbeya,mara rombo,mara arusha,huku zanzibar wanataka kujitenga,bakiibuka mikoa mingine michache tu,basi tutakuwa tunasema byebye kwa ccm na system yake nzima
 
Unamaanisha Kyela au Tunduma wapandishe bendera za nchi wanazopakana nazo maana nao wanatumia vitu vya nchi jirani hasa sukari na radio ni mwendo wa kichewa!
Serikali ina haja ya kutake special measures uko Rhombo
 
Back
Top Bottom