Rombo wapandisha bendera ya Kenya?

Rombo wapandisha bendera ya Kenya?



Sasa serikali itende haki,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,madiwani pamoja na Mbunge wa Rombo simamieni maslahi ya wananchi wa Rombo.Serikali iache vitisho,iache kuwatisha wananchi wa Rombo.

Shukrani mkuu kwa kulimulika hili. Nadhani hapa tunayeweza kumuangalia zaidi mbunge kwa kuzingatia kuwa asilimia kubwa ya madiwani ni magamba, na wale wachache wa CDM wanakuwa na influence ndogo kwenye mambo yanayohusu jamii nzima ya Rombo.

Rombo imegubikwa na rushwa ya kutosha, mathalani hakuna OCS aliyewahi kuongoza kituo cha polisi cha Tarakea akakosa kuwa tajiri kwa muda mfupi. Rasilimali nyingi ziko mikononi mwa matajiri wachache ambao wanapigana kufa na kupona kurudisha hilo jimbo CCM. Sio chakula cha msaada tu, hata mashamba ya kulima maeneo yote ya 'Forest' na Rongai, yanagawiwa kisiasa.

Ofisi ya TANESCO wilaya imeghubikwa na utendaji mbovu na rushwa ya ajabu. Leo ukiomba kuunganishiwa umeme Rombo kama wewe sio kigogo basi uandae zaidi ya milioni moja ya hongo ndipo maombi na fedha zako zipokelewe, na zilishapokelewa ujue utahonga sana ndipo uunganishiwe umeme. Sasa hivi pale TANESCO kuna watu wamelipia kuunganishiwa umeme zaidi ya miaka miwili iiyopita lakini wanaendelea kuzungushwa na umeme hawapati.

Mahakama za Rombo zimejaa rushwa za ajabu, yaani ukiwa hata na fomu inayohitaji kuthibitishwa na hakimu, haijaziwi ofisini bali unapelekwa baa unaenda kuacha sio chini ya elfu 20. Kuna tatizo kubwa sana la maji pamoja na ubaguzi wa hali ya juu. Maeneo ya Tarakea maji yanafunguliwa kwenda kwa matajiri tu huku walala hoi wakilipishwa hela za ajabu ajabu bila kupata huduma yeyote.

Nilimtegemea sana mbunge wetu lakini nimeona ni mdhaifu sana na mbaya zaidi ameshatekwa na matajiri wa Rombo. Hayupo karibu na wananchi, hakuna cha maana anachotetea kwenye baraza la madiwani. Kwa kusema cha ukweli pale tumepata hasara...
 
Tatizo siyo Mbunge, tatizo ni JK na serikali yake. wameamua kuwanyanyasa wananchi waliowachagua wabunge wa chadema, na rombo ni mojawapo.
Arusha ni moja ya majimbo yanayonyanyaswa na serikali ya Vasco da Gama

Sawa mkuu lakini wengine japo wananyanyaswa, wanaongea. Umeona akina mnyika ilibidi watishie hadi na nguvu ya umma. Huyu mbunge wetu (Selasini), yuko kimya tu...
 
hivi kuna watu wamefika hapo mbona mbali sana
Si kwamba mbali sana isipokuwa wanatafuta namna ya kupeleka ujumbe kwenye serikali yao ambayo siyo sikivu,na inaonekana wao huduma muhimu wanazipata kutoka Kenya na si TZ kwanini wasipandishe bendera ya Kenya?
 
Asante kaka. Hongera rombo
Ingawa siungi mkono kitendo cha kupandisha bendera ya nchi nyingine,lakini serikali ya Tanzania ndiyo imewafanya wananchi wakafikia huko.Sukari imezuiliwa Himo bila kujali kuna Eneo lingine la Tanzania mbele ya Himo linaloitwa Rombo.

Rombo inastahili haki zote kama wananchi wa maeneo mengine.Kwa muda mrefu rombo imekuwa ikikandamizwa na kudharauliwa na watawala wetu,sijui ni kwa nini hasa.

Mkuu wa mkoa ameshindwa kuweka mkakati wa kutosha kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma hii wakati huo huo akidhibiti magendo.Ni kwa nini maeneo mengine yaliyopakana na nchi jirani wameweza kudhibiti hali hii bila kubughudhi wananchi ndani ya territory yake halafu mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ashindwe.Madiwani wa CCM ndiyo wanaoongoza halmashauri hivi kweli wanashindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kuweka ukaguzi katika usambazaji wa sukari kuanzia Himo,Mwika,Mamsera,Mkuu,Mashati,Useri na Tarakea? ni kwanini tusiweke logistics katika level yenye uwajibikaji wa kisiasa kama kata kisha nadharia ya monitoring and evaluation ikatumika?

Wananchi wa Rombo hata katika ugawaji wa Mahindi ya misaada madiwani wa CCM na wenyeviti wa vitongoji walitaka watu waonyeshe vitambulisho kwanza yaani kadi za CCM ndiyo wagawiwe.Nina ushahidi wa majina ya watu wasiojiweza kabisa hawakupewa mahindi,na pia hujuma iliyotumika kudhulumu watu waliostahili kupewa mahindi hawakupewa.Nimeorodhesha malalamiko na ushahidi wote ukajadiliwe kwenye vikao vya baraza la madiwani walifanyie kazi watoe ripoti kwa wananchi wa Rombo

Wananchi wa rombo wanatia huruma kwa jinsi wanavyobambikiwa kesi na watendaji wa serikali,ni ukandamizaji uliopitiliza.Kulikuwa hakuna vituo vya polisi na hata vilivyopatikana vinatumika kama tools za kutisha raia na kujipatia hela.Mojawapo ni kesi iliyomuhusu mwananchi mmoja anaitwa Aristariki Kimaryo aliyewekwa mahabusu na mtoto wake pamoja na mkwe wake kituo cha polisi Mashati kisa hawajatoa hongo ya kumnusuru mtoto wake,hivyo polisi wakaamua kuwasweka mahabusu.Tulipowahoji polisi sababu ni nini wakaishia kutoa vitisho hadi tulipotishia kutumia nguvu ndipo walipowaachia

Tembo wanaotoka nchi jirani wamekuwa wakivamia mashamba ya wananchi,wakiharibu na hata kuuwa watu lakini hakuna fidia ya maana iliyofanyika.Wanachi wa Rombo sasa inabidi kwa ruthless,wanyama wanaoingia kwenye mashamba inabidi wauwa na hakuna kutoa taarifa kwa idara ya maliasili,wauawe na pembe ziuzwe hela iingizwe kwenye akaunti maalumu ya kufidia walioathiriwa na wanyama hao

Leo hii watu wanawalaumu watu wa Rombo kwa kujiskia sehemu ya kenya bila kufikiria saikolojia iliyowaathiri ya muda mrefu.Huduma za kijamii na kiuchumi zimekuwa attached na wakenya.Hata Radio ya Taifa TBC haifiki kule badala yake KBC ndiyo inasikika sijui kama watu walioko Tunduma,Songea na kigoma wanasikiliza redio za Zambia,malawi,msumbiji au DRC kuliko TBC au ni Rombo peke yake?

Sasa serikali itende haki,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,madiwani pamoja na Mbunge wa Rombo simamieni maslahi ya wananchi wa Rombo.Serikali iache vitisho,iache kuwatisha wananchi wa Rombo.

 
Mtakavoenda Hija krismas mtawapelekea sukari wajameni. Wanajua msimu wa kwenda umefika.
 
Isijepelekea mambo kuzaliwa kwa Southern Sudan!
 
Rombo wapandisha bendera ya Kenya?
Baada ya kunyanyaswa na vizuizi vya polisi vilivyomo mji mdogo wa Himo, viliosababsha upungufu mkubwa wa sukari na bidhaa nyingine za chakula, kiasa cha Rombo jimbo linaloongozwa na CDM, na linalopakana na nchi ya Kenya, kujisiakia wageni nchini mwao Tanzania, wamechukizwa na kitendo cha serikali yao ya Tanzania kuwanyanyapaa na wameamua kupandisha bendera ya Kenya! Source ITV
HTML:

waende Kenya na kuipandisha bendera ya enya huko. Watuachie Tanzania yetu.​
 
hivi kuna watu wamefika hapo mbona mbali sana

Mkuu ni mbali ila serikali yenyewe ndo imeamua kututenga kwa kuweka vizuizi himo umbali wa wastani wa 60km kufika mpaka wa kenya kupitia rombo ni wazi kabisa serikali haiitambui rombo, ni muda mrefu tangia waanze kuzuia mahindi na sukari kuvuka kwenda rombo wakidai inaelekea kenya na wakikamata gari lenye sukari au maindi likiwa rombo wanadai wamelikata likiwa kenya hali hii imesababisha mahindi na sukar kuzidi kupanda
 
Itasaidia kuwakumbusha mpaka haupo himo kwahiyo wawatume polis wao mipakani sio kucreate mipaka ambayo hatuitambui
 
Kodi yako wanaichukua halafu huduma muhimu hupati je kuna haja gani yakuwang'ang'ania utaifa? Na bado lazima hii itajitokeza sehemu nyingi za nchi hii kabla ya anguko la ccm
 
Nionavyo mimi hawa ndugu zetu wamejidharirisha sana, wanapopandisha bendela y Kenya, kwani Kenya wamewaambia kuwa wanawahitaji?
Kama wanakatiwa huduma muhimu kwa kadiri ya ilivyoripotiwa hili si zuri na serikali inastahili lawama.
Ila kwa response waliyofanya ni Afadhali wangetangaza kukubali 'kutengwa' na hivyo kujipandishia bendela yao wenyewe lakini si ya Kenya, walichoonyesha ni woga,uchonganishi na mengine ya aina hiyo.
 
Mimi mwenyewe cjamfurahia kwa hili kwani kashindwa kulitetea jimbo lake na wiki mbili zilizopita alikuwa na mikutano na wananchi wake na hatua yoyote aliyochukua baada ya mikutano hiyo. Pia wakati wa kampeni alituhadaa kutupatia namba yake ya simu ili kukiwa na tatizo tujulishe ila bado msaada hatujauona chakumwambia ni kwamba "Ndugu THELASINI angalia tusije tukakuchoka mapema kama tulivyoichoka serikali ya magamba na mramba wao"
 
Nionavyo mimi hawa ndugu zetu wamejidharirisha sana, wanapopandisha bendela y Kenya, kwani Kenya wamewaambia kuwa wanawahitaji?
Kama wanakatiwa huduma muhimu kwa kadiri ya ilivyoripotiwa hili si zuri na serikali inastahili lawama.
Ila kwa response waliyofanya ni Afadhali wangetangaza kukubali 'kutengwa' na hivyo kujipandishia bendela yao wenyewe lakini si ya Kenya, walichoonyesha ni woga,uchonganishi na mengine ya aina hiyo.
We wachaa weee usiombe baba Kenya wanalilia lile jimbo/wilaya ile vibaya muno! ikumbukwe 3/4 ya mlima Kilimanjaro upo Rombo angalia ramani! Kwa hiyo ni strategic kwa Jamhuri ya Kenya! Na ikumbukwe ule uwanja wa Ndege wa Kimataifa unaojengwa utakuwa Taveta/Holili border piga mahesabu kwa nini wasiujenge border ya upande wa Same au Hai au Namanga? Maana ile dhana ya Kilimanjaro is in Kenya itatimia!
 
Mkuu umesahau hii ruhswa ya polisi kwa kipindi hiki cha mahindi yaliyokuwa yanatoka kiteto kwenda kenya kabla ya kuzuia himo. Nikwamba polis walikuwa wakisimama barabarani kuzuia magari ya mahindi nakuchukua rushwa kutokana na walivyokuwa wanasema madereva wa malori ni kwamba mpaka kuingia kenya ni lazima uwe na wastani wa laki saba na ishirini elfu (720,000)
Himo unaacha laki
Mkuu unaacha laki
Mashati elfu Thelathini (polis wa mashati walikuwa wanasimama sehem moja inajulikana kama TAUS or Latemba road)
Useri mitaa ya mlembea unaacha elfu thelathini (na hawa ni polis wa tarakea wanakuja kusimamia hapo, na pindi ukipita mashati kiujanja bila kulipa ukikutana na hawa wa useri wanakuambia mashati hujatoa tuachie)
Tarakea unaacha laki

Hizo ni baadhi ya sehemu nilizo weza kupata taarifa zao.

Polis wengi waliokuja rombo kipindi cha miaka 2 iliyopita wamepata kununua magari yakutembelea ikiwemo Noa ambazo zinafanya safari toka Moshi to Tarakea. namalizia kwakusema Rombo ndo ilikolala rushwa Tanzania hii haki haipatikani kwa walala hoi
 
Naunga hoja mkono! Acha wapandishe tena ingewezekana na wafanye mchakato ya kwmb huduma zote ya kuanzia za afya wapate huko.

Siku nyingi sana walianza kuitambua Kenya kama taifa lao kwa hata baadhi ya kodi wanalipia huko, mfano Usajili wa vyombo vya moto kama Pikipiki.
 
mie mke wangu nimemnumnulia khanga zenye maandishi " nchi yangu kenya naipenda sana"
 
Back
Top Bottom