Mkuu mimi nakubaliana na wewe....Kwanza tukubaliane kwamba Kama kweli hili tukio limefanyika basi ni Uhaini...
Pili Kuna njia nyingi amabazo ni halali kikatiba amabazo Mtanzania anaweza kuzipitia kufikisha Malalamiko(Maoni).....
Anaweza Kuandamana...anaweza Kufungua Kesi....na mengineyo.....
Lakini Huwezi kufikisha ujumbe kwa Kupandisha bendera ya nchi JIRANI....Huku ni kujidharau na kudharau Wa-Tanzania wengine ....
Nimewahi kuishi na Wakenya ...Ki ukweli Wakenya wana dharau ya Hali ya juu kwa wa-Tanzania,Lakini walikuwa wanakoma Na mimi....
Wa-Tanzania ambao Hawapati huduma za kijamii ni wengi sana.....Kila pande za nchi hii kuna watu wanataabika kuhusu Hospitali,Wajawazito wanakufa Barabarani ,watu hawapati maji ya kunywa ...watu hawana hela ya kununua dawa...shule hakuna...chakula cha Tabu.....
Je hawa wote wapandishe Bendera za Kenya ?
Mimi nimesikia Kuwa Huko kilimanjaro(Rombo) Kuna Maendeleo Kuliko Sehemu nyingi za Tanzania....
Je Wana-Rombo wana Haki zaidi ya Kupandisha Bendera ya Kenya Kuliko Wa-Tanzania wengine ?
Mimi Naunga Mkono harakati zote za Kujiletea Maendeleo...Lakini Siungi Mkono kupandisha Bendera ya nchi Nyengine
Especially Kenya ... angalu wangepandisha ya Rwanda ningeweza Kuvumilia..lakini Kenya...Hapana..Hapana