Nicholas
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 25,260
- 7,195
Wananchi wa Rombo ni watanzania.Huu ubaguzi wa kipuuzi mnaouonyesha hapa unaonyesha ni jinsi gani tuna watu wenye ufinyu wa mawazo
Rombo ni halmashauri inayojiongoza kwa ufanisi.Ni wapenda maendeleo ndiyo maana ni wapenda mabadiliko tofauti na wengine walioko mjini hawajui maana ya mabadiliko ni nini
Mwananchi wa Rombo siku zote yuko proud na anajiskia fahari kufanya kazi kwa bidii
Wanapenda haki zao na hawapendi kunyanyaswa.Ingawa siungi mkono kupandisha bendera lakini ninawapongeza kwa kuwa na msimamo thabiti katika kutetea haki zao na mabadiliko
Mramba alijinasibu amejenga barabara lakini kutokana na dharau zake na kutowathamini walimpiga chini.Ingekua ni majimbo mengine wangeweza kumtangaza mbunge wa kudumu
Rombo hatuna urafiki wa kudumu,tuna maslahi ya kudumu katika maendeleo
Nitoe wito kwa wananchi wote wa Rombo na hasa vijana,tuendelee kupambana na tusapoti maendeleo ya jimbo letu
Naam, warombo hawaogopi kazi halali hata ikiwa ngumu vipi.Ndio maana success kwao ipo tuu hata kama Mrombo husika hajasoma.Belive me katika warombo niliowahi waona wakiwa wafanya kazi wa ndani baada ya miaka 3 ni mamilionea.Siasa za nchi zinawachelewesha sana.Kama unabisha tembe nchi nzima angalia baa na maduka ya warombo zilivyofanikiwa na kuwa ndio tegemeo la sehmu husika.majina yao ya haraka ni shayo, tarakea,rombo shine, massawe na mengine yasiyofanana nao...halafu jaribu ulizia walikujaje mjini....