Balozi Simbachawene: Watanzania mnaokuja Kenya hakikisheni mmepima Corona ndani ya saa 72 na mna vyeti

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,776
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr. John Simbachawene amewataka Watanzania wanaosafiri kwenda nchini humo kuhakikisha wanafuata masharti ya nchi hiyo kwa wageni.

Masharti hayo ni pamoja na kupima Corona katika muda usiozidi saa 72 na kuwa na vyeti vya uthibitisho.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Tanzania tunajitia hamnazo. Halafu wakaweka picha ya mkuu. Ha ha haaa. Wakenya raha sana
 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr John Simbachawene amewataka Watanzania wanaosafiri kwenda nchini humo kuhakikisha wanafuata masharti ya nchi hiyo kwa wageni.

Masharti hayo ni pamoja na kupima Corona katika muda usiozidi saa 72 na kuwa na vyeti vya uthibitisho.

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Viongozi wa CCM wanadanganya wananchi kuwa hamna korona ila changamoto za upumuaji.
Watanzania wengi waendao ughaibuni hurudishwa kwa kukutwa na korona
 
Sasa tutapima kwa vipimo gani wakati tuliambiwa kuwa vipimo vyetu vinapima damu ya mbuzi na mapapai? Pia tumeambiwa wazungu wanatuletea corona kwa kupitia bidhaa zao wakati huo sisi hatuna uwezo wa kutengeneza vipimo
 
Balozi anajaribu kuwashauri viongozi wa Tanzania nao kufanya hivyohivyo.

Sijui kuna kigugumizi gani kuwadai watu wapime kwanza kutoka huko wanakotoka? Mtu hawezi kuahirisha safari yake kisa tu kaambiwa aje na cheti
 
Sasa tutapima kwa vipimo gni wakati tuliambiwa kuwa vipimo vyetu vinapima damu ya mbuzi na mapapai? Pia tumeambiwa wazungu wanatuletea corona kwa kupitia bidhaa zao wakati huo sisi hatuna uwezo wa kutengeneza vipimo
Acha kukariri bwashee!
 
Dah huyu balozi hovyo kweli, jana nilimsikia Itv kwenye taharifa ya habari nikacheka sana, eti Tanzania inafuata masharti yote ya WHO kuhusu Corona nikajua anadanganya sasa nikajiuliza anamdanganya nani nikakosa jibu.

Kwanza kupima hatupimi, atutoi takwimu za wagonjwa wapya, vifo na waliopona atuna social distance nk sasa yeye bwana balozi anazungumzia vigezo gani tunavyo vifuata?,kwa kweli hii hawamu sifa moja ya kuwa Kiongozi ni kuwa hamnazo.
 
Back
Top Bottom