Riwaya ya Kijasusi; Mtoto wa Rais

RIWAYA; MTOTO WA RAIS
IMEANDIKWA NA HALFANI SUDY
WHATSAPP 0652 212391

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

Saa sita hiyo ya usiku, wakati wakina Daniel Mwaseba wakielekea Vikindu, katika nyumba moja iliyopo maeneo ya Magomeni kulikuwa na mvizio. Ilikuwa ni nyumba ya kisasa, ambayo tajiri wake alikuwa Muhindi mmoja, lakini kwasasa ilikuwa inakaliwa na afande Simon baada ya kupangishwa.

Mchana wenye mashaka makubwa ulipita salama kwa Simon. Mchana ambao kwa mara ya kwanza alimsaliti bosi wake, na kufuata maagizo ya Inspekta Adrian.

Simon aliingiza katika tarakilishi yake ile namba ya simu aliyotumiwa na Inspekta Adrian na kuanza kuipekua. Ilikuwa ngumu kidogo kumjua mmiliki wa namba hiyo kwani ilikuwa ina uzio maalum. Ndani ya dakika arobaini na tano wa upekuzi wake, hakuambulia jambo lolote lile. Sio tu hakumjua mmiliki wa namba ile bali pia hakupata taarifa yoyote ile kuihusu. Mwishoni kabisa akiwa amekata tamaa, akapata wazo. Ajaribu kutafuta eneo ambalo simu ile ilipigwa saa chache zilizopita. Lilikuwa ni wazo zuri sana, lakini lilileta matokeo mabaya sana kwake.
Simon kwa muda wa dakika aliganda kuishangaa tarakilishi iliyokuwa mbele yake baada ya majibu kurudi. Alifuta jasho kwa mkono wake wa kushoto huku macho yakiwa yamemtoka pima. Mapigo yake ya moyo yalimsaliti, yalidunda kwa harakaharaka na kwa nguvu kubwa.

"Hii haiwezi kuwa kweli. Simu hii imepigwa kutoka eneo hilihili la kituo kikuu cha Polisi? Nani kapiga simu ya kumtisha Inspekta Adrian aachane na kesi ya uchunguzi juu ya kifo cha Mtoto wa Rais?
Kwa madhumuni gani hasa?"

Simon kila akiwaza na kuwazua, jibu moja tu lilikuja kichwani mwake kuwa Bosco alikuwa anahusika. Kama si yeye basi anamjua mpigaji wa simu ile. Ugunduzi huu ulimuogopesha sana. Alijiona kwa kiasi gani alikuwa anakikimbilia kifo chake mwenyewe.

Wakati Simon akiwa katikati ya mawazo Inspekta Adrian akapiga simu. Laiti angejua kitakachomtokea saa sita usiku, ni bora angemwambia Adrian mashaka yake.

Simu ya Adrian aliipokea, huku akimwahidi kesho yake asubuhi atakuwa na majibu sahihi juu ya namba aliyokuwa anaichunguza.
Kwani kesho asubuhi atafika?

Usiku huu wa saa sita kuna watu watatu walikuwa wanaizunguka nyumba yake. Vijana walikuwa wamevaa mavazi meusi yenye kufanana na giza. Raba nyepesi miguuni mwao zisizoruhusu sauti yoyote kusikika wakanyagapo ardhini. Mgongoni walikuwa na mitungi ambayo ilikuwa na waya mwembamba uliopita katika bega la kulia la kila mmoja hadi katika mkono. Vijana walikuwa wanaongea kwa ishara na kuelewana kwa namna ya pekee sana.

Simon, alikuwa amelala kimwili kitandani akiwa amekumbatiwa na mke wake. Mwili wake ulikuwa pale, lakini mawazo yake yalikuwa maili nyingi sana. Mambo yote yaliyotokea mchana yalijirudia kichwani mwake mithili ya sinema aipendayo. Alidumu katika mawazo hayo kwa takribani dakika kumi na nne, kabla hajahisi harufu isiyoieleweka ikipenya katika tundu mbili za pua yake. Na harufu hiyo ilipita puani kwake kwa sekunde tatu tu.

Wala sijakosea, ni sekunde tatu tu...

Sekunde ya kwanza,

Sekunde ya pili,

Sekunde ya tatu.

Jina la Simon lilibaki katika vitabu vya kumbukumbu katika dunia hii. Na kwa bahati mbaya sana alikuwa ni kati ya watu waliokufa vifo vibaya sana hapa duniani. Ila haikuwa kwake tu. Alikufa pamoja na mke wake kipenzi, Miriam, akiwa amemkumbatia. Alikufa pamoja na majirani zake kadhaa.

Walikufajekufaje?

Saa kumi na mbili kamili asubuhi nchi ya Tanzania ilizizima. Hii ilitokana na habari ya vifo vibaya vilivyowakuta wakazi wa nyumba saba za Magomeni. Ilikuwa ni aina ya vifo ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika historia ya Tanzania. Habari ya ya vifo hivyo ilipaa mithili ya tiara ndefu ya kuchezea watoto wa kihindi, na kufika katika masikio ya watanzania wengi sana. Habari hii iliwaogofya watu isivyo kawaida!

***

Saa kumi na mbili na dakika tisa asubuhi, simu ya mzee mmoja aliyekuwa anakaa mtaa wa Msasani kwa Mwalimu Nyerere iliita. Wakati huo mzee mwenyewe alikuwa katika chumba cha mazoezi, akiviamsha viungo vyake kwa mazoezi mepesi ya asubuhi.
Mkewe, aliyekuwa jikoni akitengeneza chai ya asubuhi, alienda kuichukua simu ya mumewe iliyokuwa ikiita chumbani mwao. Aliangalia jina la mpigaji.
Moyo ulimpasuka!

Kwa haraka aliibeba simu na kukimbilia katika chumba cha mwisho cha nyumba hiyo. Chumba ambacho kilikuwa kimejaa vifaa vingi vya mazoezi, ambamo ndimo alimokuwepo mumewe.

"Mme wangu, simu yako inaita." Mwanamke alisema kwa pupa wakati akisukuma mlango wa kuingia mle ndani.

"Nani anapiga?" Mzee aliuliza huku akiacha kufanya mazoezi.

"Mheshimiwa Rais anapiga." Mke alisema, huku akilitaja jina hilo kwa heshima sana. Hali ya mstuko ilimpata kidogo yule mzee, kusikia kwamba simu ile ilikuwa inatoka kwa Rais Mark. Aliichukua simu kutoka kwa mkewe, akaipokea.

"Habari za asubuhi Mzee Ronald?" Sauti nzito na ya kimamlaka ya Rais Mark ilisikika simuni.

"Nzuri Mheshimiwa Rais.." Mzee Ronald alisita kidogo, kisha akasema "Pole sana kwa kifo cha mtoto wako. Nilikuwa hapo Ikulu leo lakini sikupata nafasi ya kuonana na wewe."

"Ahsante sana mzee Ronald. Leo kulikuwa na shughuli nyingi sana ambazo zilinifanya kushindwa kuungana na waombolezaji. Lakini, mambo yote ya msiba nimeyakaimu kwa mwanangu Moses, nadhani aliyaendesha vizuri." Rais Mark alisema.

"Upo sahihi Mheshimiwa Rais, Moses amejitahidi sana kuweka kila kitu sawa katika shughuli hii. Je kuna tetesi zozote umezipata juu ya waliomuua Aneth kutoka jeshi la Polisi?" Mzee Ronald aliuliza.

"Hiyo ndio sababu ya kukupigia simu hii. Mzee Ronald, kwa sasa nchi imechafuka sana. Kuna matukio mengi ya ajabu yanatokea hapa nchini. Matukio ambayo yananiacha na viulizo vingi sana kichwani mwangu bila ya majibu. Mara kadhaa nimetafuta nafasi ya kukuita Ikulu ili tujadili juu ya matukio hayo lakini nafasi imekuwa finyu sana. Mara kwa mara nimekuwa katika ziara mikoani ili kuhakikisha na huko tunaenda sawa katika kasi ya kupigania maendeleo," Rais akanyamaza kidogo, kuacha maneno yake yamwingie vizuri mzee Ronald kisha akaendelea.

"Kuuwawa kwa mwanangu Aneth ni mfululizo wa matukio hayo ya kutisha, kwanza ilianza kwa ajari ya ajabu ya ndege ya Coastal iliyokuwa inaelekea India. Abiria 356 wasio na hatia walipoteza uhai katika ajari hiyo. Ingawa hadi sasa jeshi letu la Polisi kupitia katika kitengo cha askari wa anga halijapiga hatua yoyote kujua chanzo cha ajari hiyo, lakini mimi ninaamini ajari ile ilikuwa ni ya kupangwa. Na kutoonekana kwa kisanduku cheusi cha ndege ile inazidi kuniongezea mashaka juu ya sababu ya ajari hiyo. Ajari ya ndege ya Coastal ilifuatiwa na kifo cha Makamu wa Rais na walinzi wake wote. Cha kusikitisha hadi leo bado hatujawakamata wauaji. Cha kusikitisha zaidi, hatujaupata hata mwili wake. Yote hayo tisa, kwa kifupi nikwambie tu mzee Ronald hakuna kitu kimewahi kuniumiza hapa duniani kama kifo cha mwanangu. Nilikuwa nampenda sana Aneth kama mwanangu, na pia juu ya maono yake ya mbali na mazuri ambayo yalinisaidia sana katika kuiendesha nchi hii. Kifo chake sio tu kimeondoka na roho ya mwanangu, lakini pia kimeondoka na mshauri wangu mkuu katika mambo mbalimbali. Miongoni mwa sababu zilizonifanya nikupigie simu hii ni juu ya kifo chake. Kifo cha Aneth bado kimebaki kuwa fumbo tata sana, huku jeshi la Polisi wakiwa hawajapiga hatua yoyote ile kulifumbua fumbo hili. Nikiwa bado na majonzi na kifo hiki, nchi yetu inapokea taarifa nyingine mbaya sana. Taarifa ya kifo cha Mpelelezi mahiri hapa nchini, Daniel Mwaseba. Nikwambie mzee Ronald, Daniel amefanya mambo mengi sana ya kukumbukwa hapa nchini. Ni kijana aliyeyatoa maisha yake ili kuhakikisha nchi hii inakuwa salama. Sote tunajua kwamba Tanzania ilikuwa inamuhitaji sana Daniel. Na jukumu letu, lilikuwa ni kuhakikisha wote waliosababisha kifo chake wanakamatwa mara moja. Nilimuagiza hivyo IGP John Zitta, lakini hadi sasa hawajapiga hatua yoyote ile katika uchunguzi wao. Mzee Ronald, Daniel wewe ni kijana wako. Wewe unamjua Daniel kuliko mtu yeyote yule hapa Tanzania. Mmefanya kazi na Daniel kwa zaidi ya miaka kumi, je unaridhika kuona haki ya Daniel inadhulumiwa huku wadhulumaji wakidunda mtaani?"

Mzee Ronald alivuta pumzi kubwa, kisha akaongea "Mheshimiwa Rais, umeongea vitu vikubwa sana, na vimenigusa kwa namna ya pekee sana moyoni mwangu. Pamoja na kunigusa vipo vilivyonishangaza, na vipo vilivyonisikitisha sana. Nikirejea katika swali lako. Kiukweli kama nchi, tutakuwa hatujamtendea haki Daniel tukikaa kimya na kuacha afe kwa mtindo huu. Daniel ni nembo ya nchi hii katika nyanja za ulinzi na usalama. Mara kadhaa Daniel ameiweka rehani roho yake ili kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa salama. Kama nchi, hatupaswi kuacha chanzo cha kifo cha Daniel kikielea hewani namna hii. Namna sahihi ya kumuenzi Daniel ni kuwakamata wote waliohusika na kifo chake."

"Hilo ndio jukumu letu," Rais Mark alidakia "Na kuanzia sasa nalikabidhi jambo hili mikononi mwako Chifu (Kwa mara ya kwanza Rais alimwita mzee Ronald kwa jina hili). Najua una vijana hodari sana pale ofisini kwako. Vijana waliokwiva na ninaamini wataitetea roho ya Daniel kwa nguvu moja kwakuwa ni mwenzio. Pia nakukabidhi suala la uchunguzi wa kifo cha Aneth na Makamu wa Rais Mheshimiwa Jamal. Majukumu hayo nayahamishia katika ofisi yako pia kuhakikisha mnachunguza na kuwakamata wote waliohusika na kusababisha ajari ya ndege ya Coastal. Hatuwezi kuacha roho za watu 356 zikiteketea bure."

"Nashukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuiamini idara yetu. Unaufahamu uimara wa idara hii na ndio maana umetukabidhi sisi tuzifanyie uchunguzi kesi hizo ngumu. Hesabu kesi hizo zimekwisha Mheshimiwa Rais. Tutawasaka wauaji usiku na mchana, tutawasaka popote pale walipo, kuhakikisha tunawatia mbaroni na kuwafikisha katika vyombo vyetu vya sheria. Umetuamini sana, na sisi tuna wajibu wa kufanya jambo hili kwa umahiri mkubwa ili tusikuangushe." Mzee Ronald alisema.

"Umenitia moyo sana Chifu kwa maneno yako. Nilianza kukata tamaa baada ya kutokea kwa matukio haya ya kutisha. Lakini sasa nimezaliwa upya. Na ninaamini nimelitua sehemu sahihi jambo hili. Basi tusiongee sana, nikutakie tu kazi njema. Na pia mkihitaji jambo lolote la kuwasaidia katika uchunguzi wenu usisite kunifahamisha. Mimi nipo hapa kwa ajiri yenu." Rais Mark alisema.

"Sawa Mheshimiwa Rais, nitakujulisha endapo nitahitaji msaada wako. Nakutakia kazi njema." Chifu aliaga.

Na simu ikakatwa.

Mzee Ronald alijifuta jasho lililokuwa linamchuruzika kama maji kwa kutumia taulo lake kubwa jeupe. Taratibu alisogea hadi katika kiti pekee cha plastiki kilichokuwemo pembeni kabisa katika chumba cha mazoezi. Alikaa kwa mtindo wa kujitupa mithili ya furushi.

"Daniel Mwaseba," Alisema kwa sauti ndogo.

Mzee Ronald alikuwa na haki ya kumtaja Daniel Mwaseba, tena sio kwa sauti ndogo kama alivyofanya. Pengine alipaswa hata kupiga kelele wakati akilitaja jina la Daniel Mwaseba. Siku zote ilikuwa Chifu akipewa kazi ngumu kama hizi na mamlaka ya juu, simu ikikatwa tu, mtu pekee anayemjia kichwani mwake ni Daniel Mwaseba. Basi huchukua simu yake na kumpigia, kisha humkabidhi kazi ambapo katu Daniel hajawahi kumuangusha.

Leo hii, Daniel Mwaseba hayupo.

Angekuwa yupo nje ya nchi bila shaka angempigia simu arejee hata kama angekuwa katika mapumziko, na Daniel angetii sekunde hiyohiyo aongeapo na Chifu. Angerudi nyumbani na kuja kufanya kazi kwa moyo wote, huku akitanguliza uzalendo.

Leo hii Daniel Mwaseba amekufa.

Itaendelea...
 
Mkuu hii nchi usiidharau hata kidogo watu wanapoamua kufanya kazi zao bila siasa ndo maana leo hapo umekaa unaenda popote kwa usalama mkubwa ila hujui nyuma ya panzia yanayoendelea..umewahi kujiuliza kwanini wizara ya ulinzi haiko wazi kama zingine?

Nakushauri pia mtafute mwandishi mmoja anaitwa Japhet sud nyang'oro nina vitabu vyake karibia vyote uone balaa la huyo kiumbe ...sijawahi ona nchii hii
Sometimes stori ziwe zina reflect mazingira ya eneo husika. Mfano stori inaongelea Tanzania lkn una kuta mambo ya teknolojia ambayo hata marekani hawajafikia.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom