Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 254
- 892
Matairi meusi ya ndege ya shirika la ndege la kimataifa la Kenya (Kenya airways) yaligusa taratibu katika ardhi ya uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es salaam. Abiria wengi walianza kushuka katika ndege hiyo kwa kutumia ngazi ndefu nyeupe iliyotokea baada ya ndege hiyo kutua. Baada ya abiria wote kushuka ndani ya ndege na kumaliza taratibu zote za uwanja wa ndege, walianza kutoka nje ya uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.
Katika eneo la kupokea wageni kulikuwa na umati mkubwa sana wa madereva teksi na watu mbalimbali waliokuwa wakisubiri wageni wao. Wengi wao walikuwa na vibao vyenye majina ya ndugu zao walivyovinyoosha juu. Miongoni mwa washika vibao hao alikuwemo Joyce.
Joyce alikuwa amevaa suti nyeusi ya kike iliyombana vyema hasa katika maeneo ya mapaja, huku kwa chini akiwa amevaa viatu virefu vya rangi nyeusi pia. Mkono wake wa kulia alishika kibao kidogo chenye maandishi meusi alichokinyoosha juu, kilikuwa kimeandikwa maneno sita...
'Karibu sana Tanzania Bwana Alexander Helb'.
Macho ya Joyce yalikuwa hayatulii sehemu moja. Mara kwa mara yalikuwa katika ziara isiyo rasmi ya kuangalia huku na kule, yakimtafuta huyo mgeni wake. Kama ungelikuwa umekaa pembeni na kumtazama kwa 'makini' Joyce, kitu ambacho ungegundua kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa amejawa na wasiwasi na uwoga.
Kwa mbali, mita kama ishirini hivi mbele yake alimwona kijana mmoja wa kizungu. Kijana alikuwa amevaa fulana ya rangi nyeupe ambayo kwa mbele ilikuwa na picha ya mbwa mdogo mweusi, huku chini akiwa amevaa suruali nyeusi ya kitambaa na raba nyeupe zenye mchoro wa mbwa mdogo mweusi pia. Mgongoni kwake alikuwa amebeba begi kubwa kiasi lenye rangi nyeusi lenye mchoro wa nyota tatu nyeupe.
Kwa tahadhari kubwa, Joyce alimsogelea yule mzungu.
"Ni mwenyewe niliyemuona kwenye picha.." Joyce alijisemea kimoyomoyo huku akimsogelea kwa tahadhari kubwa.
"Karibu sana Tanzania, Mr Alexander Helb" Joyce alisema kwa Kingereza huku akimpa mkono yule mzungu.
"Ahsante sana binti" Alexander alijibu huku akimpa naye mkono wake.
"Kumbe unajua kiswahili?' Joyce aliuliza kwa mshangao.
"Nafahamu lugha kumi na tatu za mataifa mbalimbali hapa duniani, kiswahili ikiwa ni lugha mojawapo" Alexander alijibu kwa kiswahili safi.
"Safi sana, ni fahari sana kwetu kuona lugha yetu imefika mbali kiasi hicho, mimi ninaitwa Joyce , nimetumwa na Mzee nije kukupokea" Joyce alisema huku akitabasamu.
"Ahsante sana Joyce. Mimi ninaitwa Thamani." . Alexander alisema huku akisugua pua mara tatu kwa mkono wake wa kushoto. Hapo ndipo Joyce alipoamini kwamba huyu ndiye aliyepaswa kumpokea.
Huyu ndiye Alexander Helb...
Joyce na Alexander waliongozana hadi katika gari la Joyce alililokuwa amelipaki pembezoni mwa uwanja wa ndege.
Wakaingia.
Joyce akiwa kaingilia upande wa kulia, wakati Alexander aliingilia upande wa kushoto. Joyce alishika usukani kwa mkono wa kushoto na kutia gari moto kwa mkono wake wa kulia, wakaanza kutoka taratibu katika eneo la uwanja wa ndege.
"Karibu sana kazini.." Joyce alimwambia Alexander.
Alexander alimwangalia tu, akatabasamu.
"Ni yeye" Joyce alisema kwa sauti ndogo.
***
Mita kama mia mbili, kutoka katika gari waliloingia wakina Joyce, kulikuwa na gari nyingine ndogo nyeusi ikiwatazama. Ndani ya gari hiyo kulikuwemo na watu wawili.
Upande wa kulia wa gari hiyo alikuwemo kijana mmoja mtanashati. Kiumri alikuwa na miaka ishirini na tisa. Pamoja na kuwa alikuwa amekalia anayeitwa Daniel Mwaseba. Daniel alikuwa ni mpelelezi katika idara ya usalama wa Taifa. Pembeni yake, alikuwemo Martin Hisia. Martin alikuwa ni mpelelezi wa kujitegemea.
"Hatimaye hisia za Hannan zimekuwa kweli. Alexander Helb ameingia Tanzania akitokea nchini Kenya. Nampongeza sana Hannan. Alifanya jambo la maana sana kudukua simu ya balozi Rwekaza. Hatimaye sasa tunaenda kugundua mpango wa watu hawa..." Daniel alisema huku akiliangalia gari walilopanda wakina Joyce likiondoka.
"Upo sahihi Daniel, Hannan amefanya jambo kubwa sana kwa nchi yake. Alexander Helb, mgeni akiyemuongelea balozi Rwekaza sasa yupo mbele yetu. Sasa, lazima tuhakikishe tunamtia mikononi mwetu kabla hajafika katika milki yao!" Martin alisema.
"Alexander inaonesha ni mtu hatari sana, ndio maana wametumia gharama kubwa sana kumtoa nchi za mbali ili aje kuwasaidia katika mpango wao, yatupasa tuwe makini sana ili kumnasa" Martin alisema tena.
"Jinsi ya kumpata hakuna tatizo. Ni uharaka wetu tu, nimekata breki waya wa breki wa gari yao, sio muda tutaishuhudia ajali ambayo itatupa urahisi kumnasa Alexander Helb" Daniel alisema kwa uhakika.
"Daniel!! Umeifanya saa ngapi hiyo kazi ya kwenda kukata breki? Tumekuja wote hapa, tumekaa wote hapa na hujatoka ndani ya gari hata dakika moja?" Martin aliuliza kwa mshangao.
"Kazi hizi hufanywa kwa ushirikiano Martin, nina vijana wangu hapa uwanja wa ndege ambao ninawatumia katika mambo kama haya mara kadhaa. Kuna kijana wangu mmoja nimemtumia meseji na ameitekeleza hiyo kazi kikamilifu. Kazi hii..." Daniel hakumalizia alichotaka kusema, mbele yao waliishuhudia ajari mbaya sana ya gari. Gari aliyopanda Alexander na yule mwanamke ilikuwa nyang'anyang'a!!!
"Twende fasta tukamchukue kabla watu hawajajaa na kupata nafasi ya kutafakari.." Daniel alisema.
Mkukumkuku walitoka kwenye gari yao na kuelekea kule ilikotokea ajari. Kwa haraka walimbeba yule mzungu aliyekuwa hajitambui na kumkimbiza katika gari yao, wakawasha na kutimka zao. Kilikuwa ni kitendo cha muda mfupi sana ambacho hakikuwapa watu nafasi ya kutafakari..
"Safi sana, tumempata kirahisi sana huyu mtu, sasa ataenda kufunguka kila kitu anachokijua" Martin alisema kwa furaha.
"Ni kweli, ingawa haitakuwa kazi rahisi kumfungua. Bila shaka ni jasusi huyu, na majasusi wote wapo tayari wafe kuliko kuzianika siri zao" Daniel alisema.
"Mbele ya Daniel Mwaseba, atasema tu!" Martin alisema kwa kujiamini.
***
Taarifa ya ajari ya gari iliyotokea katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere ilivuma mithili ya upepo wa kusi. Vyombo vya habari vikisindikizwa na mitandao ya kijamii iliipeperusha habari hiyo kila kona ya nchi. Kutoka Kipawa ulipo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, taarifa za ajari zikafika hadi Sinza, nyumbani kwa balozi Rwekaza.
"Haiwezekani! Haiwezekani! Joyce na Alex wapate ajari? Hiyo haiwezi kuwa ajari ya kawaida! Kwanini iwe leo?" Balozi Rwekaza alisema peke yake huku akizunguka kitanda chake. Moja ilikuwa haikai, mbili ilikuwa haikai.
Akiwa katikati ya mzunguko wa kitanda, simu yake ya mkononi ilipata uhai.
"Haloo balozi Rwekaza"
"Haloo mheshimiwa Donald Tengo"
"Balozi Rwekaza umesikia kwamba gari yetu imepata ajari uwanja wa ndege?"
"Ndio nimesikia. Ni kwa bahati mbaya sana gari ya watu wetu muhimu sana ndio iliyopata ajari, hapa nipo katika harakati za kuelekea eneo la ajari"
"Sawa Balozi Rwekaza, fanya hivyo haraka sana, Joyce na Alexander ni watu muhimu sana katika mpango wetu. Wakipotea tutakuwa tumerudi nyuma kwa hatua nyingi sana" Donald alisisitiza.
"Naelewa Donald. Na ninakuahidi kila kitu kitakuwa sawa" Balozi Rwekaza alisema.
Baada ya kukata simu ya Donald Tengo, balozi Rwekaza alitoka nje na kuingia katika gari yake.
"Tunaelekea uwanja wa ndege" Alimwambia dereva wake aliyekuwa amekaa kitini.
Gari yake ilivyotoka, gari nyingine ilifata nyuma, ilikuwa ni gari ya walinzi wake.
Saa moja na nusu baadae walifika uwanja wa ndege. Hali ilikuwa shwari na harakati zilikuwa zinaendelea kama kawaida. Ilikuwa ni kama hapajatokea ajari mbaya saa moja na nusu iliyopita.
Balozi Rwekaza alishuka garini, huku walinzi wake wanne wakiwa nyuma yake, wakifuata hatua zake. Alielekea katika duka moja ambalo lilikuwa linauza vinyago na maua ambalo lilikuwa jirani tu na mahali ilipotokea ajari.
"Habari yako kaka?" Mzee Rwekaza alisalimu.
"Mzuri mzee, shikamoo. Karibu sana dukani kwetu"
"Ahsante sana kijana. Samahani naomba nikuulize vitu, nimetanguliza samahani kwakuwa vipo nje ya biashara"
"Haina shida mzee"
Mzee Rwekaza alimwangalia yule kijana muuza duka kisha akasema.
"Ulikuwepo hapa asubuhi wakati ajari ya gari lililogongwa na gari la majitaka ikitokea?"
"Ndio, nilikuwa hapa wakati ajari ile inatokea"
"Kama hutojari kijana, naomba uniambie nini kilitokea?"
"....ile gari nahisi ilikatika breki! Nililiona likiserereka kwa kasi na kwenda kujibamiza vibaya katika gari la majitaka lililokuwa linatokea katika vyoo vya uwanja wa ndege"
"Halafu?"
"Watu walianza kujaa na baadae gari ya wagonjwa ikaja na kuondoka na majeruhi"
"Unahisi wamepelekwa hospitali gani majeruhi?"
"Mimi sifahamu kwakweli"
"Hukuona jambo lengine lolote la ajabu?"
Muuza duka alifikiria kidogo. Hofu ilionesha katika sura yake. Balozi Rwekaza alitoa pochi yake, akatoa shilingi laki mbili. Akampa huku akimuuliza.
" Uliona tukio gani la ajabu"
"Nilionaaa....."
"Jambo gani hilo uliloliona?" Balozi Rwekaza aliuliza akiwa na wahka mkubwa.
"Kuna tukio la kushangaza kidogo lilitokea baada ya ajari kutokea. Kwa wakati ule nililichukulia ni tukio la kawaida tu, nikihisi labda ni wasamaria wema, lakini baadae nilijiuliza mwenyewe, kwanini wamchukue majeruhi mmoja tu na mwengine wamuache?" Muuza duka alisema huku akimwangalia balozi Rwekaza aliyekuwa katika hamu kubwa ya kusikia...
"Sijakuelewa kijana.."
"Ni hivi, kwenye gari kulikuwa na watu wawili, lakini mmoja alichukuliwa na vijana wawili kabla gari ya wagonjwa haijafika"
"Unasema?"
"Baada tu ya kutokea ile ajari kuna watu wawili walikimbilia, wakavunja kioo cha mbele na kukimbia na majeruhi mmoja. Kilikuwa ni kitendo kilichofanyika kwa haraka sana, ni watu wachache sana waliokishuhudia"
"Ooh Mungu wangu!, Itakuwa wameondoka na Alexander Helb!! Ni watu gani hao? Walifahamu vipi ujio wa Alexander?" Balozi Rwekaza alijiuliza mwenyewe, lakini hakukuwa na wa kumjibu.
Kijana muuza duka alibaki akimshangaa.
Je Alexander Helb ni nani? Wakina Daniel watapata kitu gani kutoka kwa Alexander Helb? Je wakina Donald Tengo wana mpango gani?
Hii ni sehemu ya kwanza ya mtoto wa rais..
Tuwe wote katika sehemu ijayo...