Riwaya: Mahojiano na Rais

Riwaya: Mahojiano na Rais

Ashes

New Member
Joined
May 26, 2024
Posts
3
Reaction score
0
Nilishawahi kumuuliza mama swali, asubuhi moja kupindi bado mdogo, alikuwa anakanda unga wa ngano kwa ajili ya biashara yake ya chapati, muda mfupi kabla sijaenda shule.

Swali lilikuwa kuhusu "vyanzo"

“Ni suala pana, Helena,” alisema huku akiniangalia kwa macho ya kunipima, “Unataka kujua vyanzo vya nini hasa?”

Nilisita.
Nilikuwa na miaka kumi na tatu tu, lakini nilijua namna mama angeichukulia hamasa yangu.

Alitamani nije kuwa daktari. Ndoto zangu… hazikuwa huko. Sikuwahi kuwa shabiki wa sare.

“Simulizi,” nilisema, nikifungua daftari langu kana kwamba ni kazi ya shule.

“Ili simulizi iwe nzuri na ya kuvutia… inapaswa kuanzia wapi?”

Mama alitabasamu. Akachukua muda kidogo kufikiria, “Kwa mtazamo wangu? Kokote.”

“Kokote?” nikauliza.

Aliitikia, akisema, “Niambie, Helena… mimi ni nani?”

“Mama?” nilijibu, bila uhakika kama hilo ndilo jibu alilotaka.

Alitabasamu zaidi, “Ukielezea kuhusu mimi, utaanzia wapi?”

“Ningesema wewe ni mama yangu… mrembo, unayenipenda kuliko chochote, unauza chapati stendi kuu ya mabasi Mbezi… unapenda nikifaulu kwa sababu unapenda kununua chipsi mayai tukisherehekea…”

Nilinyamaza. Nilikuwa nimeishiwa sifa.

Mama wala hakukasirika. Alitabasamu tu.

“Lakini mimi ni zaidi ya mama, Helena. Na wewe ni zaidi ya mwanangu.”

Akaacha kukanda, akanigeukia. “Kabla sijawa mama, nilijua tayari nitakuwa mama. Nilihisi hivyo nikiwa shuleni, nyumbani, hata ndotoni. Ndiyo maana sikujilaumu nilipohadaika nikiwa binti. Sikulaumu baba yako alipoikataa mimba… kwa sababu kwangu, haukuwa bahati mbaya wala mgeni wa ghafla.”

Alinitazama.

“Unasemaje hapo, kwa mwanzo wa simulizi ya maisha yetu?”

“Wow, mama… unajua sana!” nilisema nikicheka, nikipiga makofi madogo.

Lakini moyoni nilijirudia jambo moja, tena na tena: Nataka kuteka fikra kama yeye.

“Acha sasa,” alicheka, akiendelea kukanda unga. “Umeelewa nini hapo, Helena?”

"Simulizi huanza popote" Nilijibu na mama alinisifu.

Kusema kweli… sikuwa nimeelewa chochote kipindi kile zaidi ya kupendezwa na simulizi ya mama.

Lakini Leo?

Leo nimeelewa kwa nini mama hakuanzia pale nilipotungwa mimba, wala nilipozaliwa, wala hata nilipokua.

Alianzia kwenye nia yake ya kuwa mama, kwa sababu, kwake? Ndiyo ulikua msingi wa maisha yetu.

Kwa upande wangu, kwa miaka saba sasa, nimekuwa na nia moja: kuijenga jamii yangu kupitia uandishi wa habari.

Nimeona mengi mpaka sasa. Hakuna kilichobaki kigeni tangu nitimize miaka kumi na sita.

Kesi za ubakaji, mauaji, utekaji, athari za umasikini, mimba za utotoni, madawa ya kulevya, mmomonyoko wa maadili, dhuluma, unyanyasaji... Ni baadhi tu ya mambo ya kila siku katika jamii yangu.

Kila ninapopita, naona hofu na chuki zikijaa kwenye nyuso za watu.

Kila mtu ana wa kwake wa kumlaumu.
Nafsi.
Wazazi.
Serikali.
Marafiki.
Mitandao.

Labda ni kweli, huu utofauti wa kipato ni muhimu katika chachu ya kuleta maendeleo nchini.

Lakini mbona sio kipato tu, tunachotofautiana? Kwa nini wengine wale mpaka watupe mabaki, wakati kuna watu wanakufa njaa?

Jua moja. Anga moja. Nchi moja. Lakini hali za wananchi ni tofauti daima.

Nilipata kibali cha kuchapisha makala yangu, yakiangazia maisha halisi ya asilimia themanini na mbili ya wananchi mwenzangu.

Watu waliyapenda makala yangu kiasi cha kupata nafasi ya makala zangu katika gazeti la kila siku.

Haikuchukua muda, nikaanza kupokea shuhuda, tuhuma na hata maoni kutoka kwa wananchi juu ya makala zangu.

Wengine walifika mpaka ofisini kwangu kwa ajili ya mahojiano na mimi. Haikuwa nzuri kwa kuwa wengi walikuwa wanataka misaada.

Na wala havikuwa vitu vikubwa: mitaji, haki, kusikika...

Hatimaye, nikasukumwa na sauti zao, nikaandika barua ya kuomba mahojiano na Rais wa nchi.

Sikuandika barua moja.

Wala mbili.

Kwenda kwa mtu mwenye ratiba isiyo na pumzi.

Lakini mimi nilikuwa na kitu kimoja: kung’ang’ania.

Mpaka nilipopata majibu.
Nilikaa ofisini mpaka saa kumi na moja na nusu jioni, nikiitazama ile email kutoka Ikulu.

“Mungu wangu…” nilijikuta nikisema, bila hata kujua nifanye nini. “…Naenda Ikulu.”

Nilijaribu kujisemea kwa sauti, labda nitaamini.

Lakini bado ilikuwa kama ndoto.

Ghafla, mlango wa ofisi ukagongwa na mtu akichungulia ndani.

“Hey, girlfriend! What's for dinner?”

Alikuwa Paulina.

Rafiki yangu wa chuo. Mtu ambaye haogopi kitu chochote.
Alikuja karibu, akinitazama kwa wasiwasi.
“Mama kazidiwa?”
“Mungu aepushe mbali,” nilisema, nikivua miwani. “Ni kazi tu.”

Hakuniamini.

Nikageuza laptop, nikamuonyesha.

“So… that’s happening,” alisema baada ya kusoma.

“Umeandaa maswali ya mahojiano?”

Nikacheka.

“Paulina… sijaandaa chochote.”

Aliniangalia kama nimepoteza akili.

“Helena, usiniambie umehangaika mwezi mzima kupata interview na Rais… halafu huna maswali?”

Sikujibu.

Alielewa.

“So we only have today,” alisema, akikaa vizuri. “Swali la kwanza, unataka kujua nini?”

"Lazima leo?" Niliuliza kwa kuwa nilikua nimechoka mpaka akili.

"Hey" Aliniita kwa huzuni, "What's wrong? Did the boss-man humiliated you again?"

Nilitikisa kichwa kwa kukataa. "I'm used to that..."

Nilivuta pumzi.
“Honestly? Sijui kama nataka kukutana na Rais"

Hakuongea kitu kwa muda. Akiniangalia tu.

"Why did you write those letters, Helena?"

"Kwa sababu!" Nilisema na nisijue cha kuendelea.

"Kwa nini?" Akauliza tena.

"Watu wanaumia, Paulina!" Nilianza kwa hasira, "Na hakuna anayejua kuhusu yeye, zaidi ya mikopo na kuanzisha tume ambazo hazina msingi!"

Paulina wala hakutetereka, aliniuliza tena. "Tunaanza na swali gani?"

"Nataka kujua kama anajihisi yupo salama.”
Paulina alinyamaza kwa sekunde kadhaa.

“You have sixty million people behind you… and that’s your first question?”

Nilikumbuka maneno ya mkuu wangu wa kitengo: Mimi si mwandishi wa habari kwa kuwa nachagua upande.

“You know that’s controversial, right?” Paulina alisema tena.

“Andika,” nilimwambia. “Najua ninachofanya.”

Alinitazama kwa makini.

“I hope so… kwa ajili yako.”

Akaanza kuandika.

Na huo ndo ulikuwa mwanzo wa simulizi yangu.

To Be Continued…
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom