Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

Jamani nisaidieni... hivi Edger alikufa? kwenye episode ya ngapi?
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 12
Austin alifika ikulu
lakini Dr Fabian
hakuonyesha uchangamfu
kama ambavyo
huchangamka kila
anapokutana na Austin.Sura
yake ilija hasira.Baada ya
Austin kupokelewa Ikulu
waliingia katika chumba cha
mazungumzo ya faragha
kama wafanyavyo kila
Austin afikapo ikulu kwa
mazungumzo.
“Kabla hujanieleza kile
unachotaka kunieleza
naomba nikufahamishe
kwamba nimepokea taarifa
za kifo cha Tamar kwa
masikitiko makubwa na
nimeapa yeyote Yule
aliyehusika katika kifo hicho
nitamsaka hadi apatikane
awe mzima au
amekufa.Hakuna aliyeshiriki
atakayebaki salama !
akasema Dr Fabian kwa
ukali
“Mheshimiwa Rais
usitumie nguvu kubwa sana
kuongelea suala hilo au
kumtafuta muuaji wa Tamar
Axon wakati unaye mbele
yako”
“You?! Akauliza Dr
Fabian
“Yes me and my friends
we killed her”
“Jesus Chris ! akasema
Dr Fabian
“Dr Fabian naomba
kwanza unisikilize kile
ninachotaka kukwambia
halafu mwisho utaamua
kama unataka kunikamata
na kunifungulia mashtaka
au vinginevyo lakini kwanza
nisikilize” akasema
Austin.Dr Fabian hakujibu
chochote aliendelea
kumtazama kwa hasira
“Mheshimiwa Rais
ulitupa kazi mimi na
wenzangu ya kumuua Lucy
Muganza na tukaitekeleza
kazi hiyo vizuri lakini baadae
likaibuka tena suala la balozi
Benjamin nalo ukatukabidhi
sisi tumchunguze kwa bahati
mbaya akafariki wakati
uchunguzi
unaendelea.Mpaka sasa
hatujui nani walimuua balozi
Benjamin na kwa nini”
“Hamjui nani kamuua
balozi Benjamin?Mnadhani
mimi ni mtoto mdogo ambaye
nitashindwa kugundua
mchezo mlioufanya?Wewe na
wenzako mlimuua balozi
Benjamin” akasema Dr
Fabian
“Kwa nini tumuue mtu
ambaye ulitutuma
tumchunguze?akauliza
Austin na Dr Fabian akawa
kimya
“Mheshimiwa Rais
hatukumuua
Benjamin.Kama kuna mtu
amekueleza kwamba sisi
tulimuua
amekudanganya.Sikiliza
namna
ilivyokuwa.Tuligundua
kwamba balozi Benjamin
amealikwa katika hafla ya
uchangishaji fedha za
mabweni ya watoto waishio
kwenye mazingira magumu
na sisi kwa vile tulikwisha
anza kumfuatilia tulikuwepo
ukumbini.Benjamin alitoka
ukumbini akaenda katika
lifti na akiwa ndani ya lifti
mwanamke mmoja
alimuwekea bahasha katika
mfuko wake wa koti na mtu
wangu aliyekuwamo ndani
ya lifti akimfuatilia
Benjamin alikiona kitendo
hicho.Tulimuandama Yule
mwanamke tumjue ni nani
na amempa nini balozi
Benjamin kwa siri namna
ile.Tulifanikiwa kumpata
mwanamke huyo na baada
ya kumuhoji akadai yeye ni
mfanyakazi wa SNSA.Kazi
yake kubwa ni
mdukuaji.Alitueleza kwamba
kwa muda wa wiki kadhaa
amepewa kazi maalum ya
kudukua simu yako na
kuhifadhi mazungumzo yako
yote ya simu,hivyo
mheshimiwa Rais fahami
kila simu unayopiga au
kupigiwa inasikilizwa na
SNSA”
“Simu yangu
unadukuliwa? Dr Fabian
akahamaki
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Simu yako inadukuliwa
na SNSA”
Dr Fabian akasimama na
kushika kiuno.
“Mheshimiwa Rais
mawasiliano yako yote ya
kila siku hurekodiwa na
kisha huwekwa katika faili
maalum”
“SNSA hawawezi
kudukua simu ya Rais !
That’s a big lie ! akafoka Dr
Fabian
“Nisikilize kwanza
mheshimiwa Rais” akasema
Austin
“Mkurugenzi wa SNSA
Tamar Axon ndiye aliyetoa
maelekezo kwamba simu
yako idukuliwe”
“Tamar ! akazidi
kuhamaki Dr Fabian
“Tamar hawezi kabisa
kufanya kitu kama hicho !
akasema Dr Fabian
“Hiki si kitu cha kubuni
mheshimiwa Rais.Ni kweli
jambo hilo linafanyika na
aliyekuwa akifanya ndiye
aliyetueleza
kinachoendelea.Katika
kukusanya rekodi za
mawasiliano yako Agatha
aligundua uliwasiliana na
Rais Patrice Eyenga wa
Congo na mlikuwa
mnazungumzia kuhusu
mauaji ya Lucy
Muganza.Rekodi zako zote
ulizozungumza kuhusu
mauaji ya Lucy Muganza
Agatha alizificha
hakumuonyesha
Tamar.Agatha alipewa diski
mweko na Tamar ampelekee
balozi Benjamin na
alipokuwa njiani
aliichunguza kujua kuna nini
ndani akakuta kuna rekodi
mbili za mazungumzo yako
na Rais Patrice Eyenga
kuhusu mauaji ya Lucy
Muganza”
“Real?!! Akauliza Dr
Fabian Austin akatikisa
kichwa
“Tamar anaweza kweli
akanifanyia mambo kama
hayo? Dr Fabian akabaki
anashangaa
“Ni kweli mheshimiwa
Rais” akasema Austin
“Ni vigumu kuamini”
Austin akatoa diski
mfukoni akaichomeka katika
kompyuta na Rais akaanza
kusikiliza rekodi za
mazungumzo yake ya
simu.Austin akamchezea
rekodi mbili akizungumza na
Patrice Eyenga.
“Mheshimiwa Rais ziko
nyingi hizi ni mbili tu
nimekuchezea” akasema
Austin.
“A..A..AAAA…Austin I
don’t know what to say !
“Don’t say anything Mr
President.Siku ile
tulipokwenda nyumbani kwa
Tamar kufanya uchunguzi
ukatuzuia tulikuwa
tunatafuta faili lenye rekodi
hizi”
“Austin I’m sorry .I didn’t
know anything.Kwa nini
hukunieleza jambo kubwa
kama hili mapema?
“Nilitaka kukueleza
lakini hukunipa nafasi na
badala yake ukatengeneza
mtego ili nikamatwe na
SNSA”
“Austin…”akasema Dr
Fabian na kushindwa
kuendelea.Alikosa neno la
kusema
“Mheshimiwa Rais,Jana
usiku tumevamia nyumbani
kwa Tamar na kufanikiwa
kulipata faili lenye rekodi
zote tumezifuta na zilizobaki
ni hizi hapa” akasema Austin
na kumpatia Dr Fabian ile
diski mweko.Dr Fabian
akashusha pumzi
“Thank you Lord”
akasema na kuichukua ile
diski
“Una hakika hakuna
sehemu nyingine zilipo
rekodi hizi?
“Hakuna mheshimiwa
Rais.Tulipandikiza kirusi
katika mfumo wa kompyuta
wa SNSA na kuharibu kila
kitu rekodi zilikuwa
zimebaki katika kompyuta
ya Tamar”
“Good job
Austin.Ahsanteni sana wewe
na wenzako kwa kazi hii
kubwa mliyoifanya.Naomba
unisamehe sana kwa yale
niliyokufanyia”
“Mheshimiwa
Rais,Tamar alijiua mwenywe
kwa kujipiga
risasi.Tunaamini alikuwa
anashirikiana na balozi
Benjamin lakini mpaka sasa
hatujui nani waliomuua
balozi Benjamin na kwa
nini.Japokuwa wote wawili
wamefariki dunia lakini
hatari bado haijaisha.Kuna
mambo tumeyagundua
kwanza Tamar alikuwa
anapokea fedha kutoka
katika akaunti iliyoko
Ufarnsa ambayo mmiliki
wake amefichwa.Amekuwa
akipokea fedha nyingi
kupitia akaunti
hiyo.Tunatafuta kujua
mmilikiwa hiyo akaunti na
fedha hizo zote zina malengo
gani.Katika akaunti yake
tumekuta ana zaidi ya bilioni
mbili.Tumegundua pia
mawasiliano yake na mtu
anaoitwa Dinosaur.Bado
hatujafahamu mtu huyu
yuko wapi lakini barua pepe
tuliyoikuta katika kompyuta
ya Tamar inasomeka hivi”
akasema Austin na
kumuonyesha Rais barua
pepe waliyoikuta katika
kompyuta ya Tamar.Dr
Fabian akazidi
kuchanganyikiwa
“Ukisoma barua pepe hii
utagundua Tamar na huyo
Dinosaur wana mipango
mikubwa inayokwenda kwa
awamu na tayari awamu
mbili zimekamilika na sasa
wanaingia awamu ya tatu na
njiwa anayetaja hapa si
njiwa mnyama bali ni mtu
anategemewa kuwasili muda
wowote.Bado hatumjui ni
nani na anakuja kufanya
nini”
“Dah ! siamini macho
yangu.Tamar ?!! akasema Dr
Fabian
“Nilimuamini sana
kumbe ni chui.Umesema
anatumiwa fedha kutoka
akaunti iliyoko
Ufaransa,balozi Benjamin
pia anatokea Ufaransa,Lucy
na Laurent Muganza makazi
yao wote ni Ufaransa,Rais
wa umoja wa Ulaya anatokea
Ufaransa na hata ukiangalia
wale waliotuma jumbe katika
kurasa zao zao za twitter
Benjamin na Rais Michael
wote wanatoka Ufaransa.Leo
nimekuwa na malumbano
makubwa na Rais wa
Ufaransa kuhusu kifo cha
Benjamin.Ukiunganisha
haya yote unapata picha
kwamba mchezo huu
tunacheza na
Ufaransa.Ukijiuliza kwa nini
tucheze na Ufaransa?Jibu ni
rahisi jamhuri ya
kidemokrasia ya
Congo.Baada ya kuingia
madarakani Rais Patrice
Eyenga amekata mirija yote
ya mataifa makubwa
kunufaika kwa kuchota
rasilimali za Congo hasa
madini na sasa wanatafuta
namna ya kurudi.Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
inazidi kuimarisha ukuta wa
kuzuia uchotwaji wa
rasilimali zake kwa kujiunga
na jumuiya ya Afrika
mashariki ndiyo maana
mataifa haya ambayo
yanataka kurejea Congo kwa
nguvu wanataka kuanza na
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki halafu
waingie Congo.Kama Tamar
alikuwa na mahusiano na
balozi Benjamin basi ni wazi
anashirikiana pia na umoja
wa Ulaya na ndiye aliyekuwa
akimpatia balozi Benjamin
siri za nchi kwani SNSA ina
siri nyingi za nchi.Ukifuatilia
mtiririko wa mambo ulivyo
toka alipouawa Lucy
Muganza utaona kabisa
kwamba balozi Benjamin na
wenzake walihisi serikali ya
Tanzania inahusika na
mauaji yale hivyo wakawa
wanatafuta
ushahidi.Ninamshukuru
sana huyo ambaye alificha
rekodi za mazungumzo
yangu na Patrice
Eyenga.Alifanya jambo
kubwa na la kishujaa”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais hii ni
vita na ulipaswa kutuamini
vijana wako lakini ulituzuia
hatakuendelea na operesheni
yetu.Licha ya kutuzuia lakini
bado tumeendelea kuweka
hatarini maisha yetu na
kupambana hadi
tukafanikiwa kupata rekodi
hizo.You are safe now Mr
President” akasema Austin
“Austin nimeishiwa
maneno ya kusema.Mimi ni
rais wako lakini ninajiona
mjinga sana kwa mambo
niliyoyafanya.Kwa nini
nilishindwa kukuamini
Austin?Nisamehe sana
kijana wangu najua
nilichokif……….”
“Usijali mheshimiwa
Rais” Austin akamkatisha Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo la mwisho”
“Jambo gani Austin?
“Wakati tunapekua
kompyuta ya Tamar
tumekuta kuna video hizi”
akasema Austin na
kumchezea Dr Fabian video
moja kati ya mbili
walizozikuta katika
kompyuta ya Tamar.
“Stop it ! akafoka Dr
Fabian.Alikuwa anahema
haraka haraka
“Mr President can you
say something about
this?akauliza Austin
Dr Fabian akafikiri kwa
muda halafu akasema
“Kuna mwingine yeyoye
ambaye ameziona video hizi?
“Hapana ni sisi pekee”
akajibu Austin na Dr Fabian
akavuta pumzi ndefu
“Kwa miaka saa
nimekuwa nikiteseka kwa
ajili ya video hizi na nimelipa
gharama kubwa sana mpaka
sasa.Kuna nyakati
nilitamani hata nife
niondokane na adha
nilizokuwa nazipata kutoka
kwa Tamar kwa sababu ya
video hizi” akanyamaza na
kuchukua kitambaa akafuta
jasho usoni akainamisha
kichwa akazama mawazoni
“Mheshimia Rais naomba
unihakikishie je video hizi ni
za kweli na
zimetengenezwa?akauliza
Austin
“Video hizo ni za kweli
kabisa Austin.Unaowaona
ndani ya hiyo video ni mimi
na Tamar.Labda nikupe
picha tu kwamba mimi na
Tamar tulikuwa na
mahusiano ya kimapenzi
lakini yalikuwa ya
siri.Tamar alikuwa ndiye
mwanamke niliyepaswa
kumuoa lakini sikufanya
hivyo kutokana na tabia yake
ya kuwa na wanaume wengi
nikamuoa Millen.Mimi na
Tamar tuna mtoto mmoja wa
kiume anaishi na mama yake
mdogo nchini Hungary,hivyo
Tamar alikuwa sehemu ya
maisha yangu.Nilimjengea
jumba kubwa Afrika kusini
nikampa mahitaji yale yote
aliyohitaji lakini bado Tamar
hakuacha tabia yake ya
kutoka na wanaume wengine
japo kila mwisho wa wiki
nilikuwa nakwenda Afrika
kusini kwa ajili
yake.Niliweka watu wa
kumfuatilia na wakanitumia
picha zake akiwa na
wanaume tofauti ndani ya
nyumba niliyojenga
mimi.Nilikasirishwa na
kitendo hicho ndiyo maana
nikafanya vile
nilivyofanya.Ilikuwa ni
hasira tu” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais mimi
na wenzangu hatuna haja ya
kufahamu chochote wala
kuingilia maisha yako binafsi
lakini kuna kitu tumekiona
katika video hizi.Inaonekana
Tamar alitegemea kitendo
kile kutokea hivyo akatega
kamera mahala ambako
usingeweza kuiona na
akarekodi matukio
yale.Katika video zote mbili
baada ya wewe kuondoka
Tamar anaonekana akiinuka
na kwenda kuzima
kamera”akasema Austin
“Sijawahi kuona kipande
hicho.Mimi alinitumia
kipande kidogo na ndicho
ambacho amekuwa
akikitumia kunitisha
kwamba atakiachia
hadharani watu
wakione.Sikuwa tayari kwa
hilo ndiyo maana
nilimtimizia kila
alichokitaka” akasema Dr
Fabian na Austin
akamuonyesha mwisho wa
video zile Tamar akiinuka na
kwenda kuzima kamera.
“Shetani mkubwa Yule !
akasema kwa hasira
“Mheshimiwa Rais
unaweza kukubaliana nasi
kwamba Tamar alifanya vile
makusudi kabisa kwa
malengo anayoyajua yeye
mwenyewe?akauliza Austin
“Inaweza kuwa kweli
kwani toka alipopata video
hiyo amekuwa akinipa
vitisho vingi na mimi
sikutaka kupoteza heshima
yangu katika jamii ndiyo
maana nikawa tayari
kumtimizia kila
anachokihitaji”
“Uliwahi kumueleza nia
yako ya kuwania urais kabla
ya tukio hili
kutokea?akauliza Austin
“Austin tayari
umekwisha fahamu siri
zangu hivyo siwezi kukificha
kitu.Mimi nilianza
kuandaliwa kuwa Rais
miaka minne kabla ya rais
aliyepita kumaliza muda
wake.Mipango hii ilipoanza
nilimshirikisha pia
Tamar.Kujibu swali lako ni
kweli alifahamu kama
ninaandaliwa kwa nafasi ya
urais.Baada ya mimi kuwa
Rais ndipo alipoanza vituko
vyake kutaka nimtimizie kila
anachokihitaji kwa madai ya
kuachia video ile endapo
nisipomtimizia.Aliyekuwa
mkurugenzi wa SNSA
alifariki dunia nchini Afrika
kusini na Tamar alinitaka
nimteue yeye kuwa
mkurugenzi wa SNSA.Baada
ya kupitia taarifa zake za
kielimu na kuona ana vigezo
nikamteua kuwa mkurugenzi
mkuu wa SNSA” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais
napenda kukutoa hofu
kwamba sasa uko
salama.Kila kitu tunacho
mikononi mwetu na
hakutakuwa tena na kitisho
chochote kwako.Sisi tuko
kwa ajili yako.Tutakulinda
kama tulivyofanya”
“Ahsante sana
Austin.Ninajiona mjinga
sana kwa mambo niliyotaka
kukufanyia kumbe wewe
ndiye mkombozi
wangu.Tamar ndiye
aliyekuwa ananiongoza
kutaka nikupoteze na mimi
kwa ujinga wangu na kwa
kumuogopa nilitekekeleza
kila alichonitaka.Usiku ule
mlipokwenda nyumbani
kwake ni yeye aliyenipigia
simu na kunitaka niwatake
muondoke haraka sana
nyumbani kwake na mimi
nikafanya hivyo japo nilijua
lazima kuna jambo la
muhimu lililowapeleka
pale.Ni yeye aliyetengeneza
ule mtego ili uende pale
Dino’s hotel ukamatwe oh my
God ! akasema Dr Fanian na
kuinama akisikitika
“Mheshimiwa Rais hayo
yote yamebaki historia sasa
tunakwenda kuufungua
ukurasa mpya sisi na wewe”
akasema Austin na
kumtazama Dr Fabian
“Tumefanya kazi kubwa
mheshimiwa Rais
kuhakikisha unakuwa
salama lakini na sisi kuna
kitu tunakihitaji”
“Sema Austin mnahitaji
nini?
“Kwa sasa baada ya
Tamar ambaye ni
mkurugenzi wa SNSA
kufariki idara ile haina
mkurugenzi.Tunataka
umteue mtu kutoka katika
watu wangu kuwa
mkurugenzi wa SNSA”
akasema Austin akimkazia
macho Dr Fabia ambaye
alivuta pumzi ndefu na
ksuema
“Are you blackmailing me
Austin?! Akauliza Dr Fabian
“Hapana mheshimiwa
rais.Bado tuna kazi kubwa
ya kufanya.Bado hatari
haijakwisha.Bado vita
inaendelea .Kuna maswali
mengi ya kuyatafutia
majawabu.Tunahitaji kujua
nani waliomuua balozi
Benjamin?nani anamtumia
fedha Tamar?Dinosar ni
nani?Wana mipango gani
dhidi ya nchi yetu?Mwisho
tunahitaji kujua mtu ambaye
anatarajiwa kuingia nchini
hivi karibuni kutekeleza
awamu ya tatu ya mpango
wa Dinosaur na Tamar ni
nani?Tutaweza kuyapata
majibu hayo kama mmoja wa
watu wangu atakuwa
mkurugenzi wa SNSA.Idara
ile ni nyeti sana na kazi yake
ni kubwa kwa nchi inatakiwa
iongozwe na mtu muadilifu
sana lakini ilikuwa
imeshikwa na madalali wa
mebapari.Tunataka
kuirejesha heshima ya idara
hii” akasema Austin
“Austin sijui niseme nini
kwa hili jambo zito
ulilolizungumza.SNSA ni
idara nyeti kabisa ya
usalama wa nchi lakini
niliiweka mikononi mwa
makuwadi wa
wanyonyaji.Nataka wewe
uwe mkuu wa SNSA kama
itakupendeza” akasema
DrFabian
“Mheshimiwa Rais mimi
ni kiongozi wa kikosi
muhimu kabisa naomba
niendelee kubaki hapohapo
katika nafasi yangu lakini
kuna mtu ninampendekeza
kwako anaitwa Ruby Rafael
Magalla.Huyu ni mtanzania
mwenye uraia wa
Uingereza.Kwa sasa
anafanya kazi katika
mamlaka kuu ya
mawasiliano ya kiintelijensia
Uingereza.Ninamfahamu
Ruby nimewahi kufanya
naye kazi ni mtu mwenye
akili nyingi na ana uwezo
mkubwa sana wa kucheza na
kompyuta.Nina hakika
akiwekwa pale SNSA
atakuwa na msaada mkubwa
sana” akasema Austin
“Austin huna haja ya
kunielezea kwa undani
kuhusu huyo mtu
unayempendekeza.Ninakua
mini.Sina shaka na uzalendo
wako hata kidogo ninaamini
mtu huyo uliyempendekeza
anafaa kabisa.Mimi sina
shida yoyote ya kumteua
kuwa mkurugenzi wa
SNSA.Swali ni je yeye
mwenyewe yuko tayari?
Akauliza Dr Fabian
“Ruby anaipenda sana
Tanzania na si mara moja
amekuwa akija Tanzania
kushiriki katika misheni
mbali mbali toka wakati wa
Rais aliyepita”
“Real?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais”
“Basi vizuri.Nipe
mawasiliano yake
nitazungumza naye mimi
mwenyewe na kumuomba aje
Tanzania.Nitamshawishi
kwa kila namna hadi
akubali” akasema Dr Fabian
“Nakushukuru sana
mheshimiwa Rais”
“Kama kuna kitu kingine
chochote nieleze tafadhali”
“Hakuna mheshimiwa
rais kilichonileta hapa kwako
ni hayo niliyokueleza”
“Austin najua
nimekukosea wewe na
wenzako.Najua haitakuwa
rahisi kuniamini tena lakini
naomba tusameheane kwa
yale yaliyotokea na tufungue
ukurasa mpya.Tuna vita
kubwa inatukabili mbele
yetu nahitaji watu kama
ninyi wazalendo wa kweli
kwa nchoi yenu ambao mko
tayari hata kuyatoa maisha
yenu kwa ajili ya Tanzania.”
“Sisi hatuna tatizo lolote
nawe mheshimiwa Rais
kikubwa tunachokitaka toka
kwako tuamini”
“Siwezi kurudia tena
makosa niliyoyafanya
Austin.Lakini nakuomba
hizo rekodi na hizo video
ziharibuni kabisa”
“Usihofu kuhusu hilo
mheshimiwa Rais.Zote
zitaharibiwa na hakutakuwa
na kitisho kingine chochote
dhidi yako” akasema Austin
na kuzifuta rekodi zile na
video mbele ya Rais
Austin na Dr Fabian
walimaliza mazungumzo yao
na kuagana Austin
akaondoka
RAMALLAH – PALESTINA
Mathew Mulumbi
alifumbua macho baada ya
kusikia sauti za watu
wakikimbia karibu na
dirisha la chumba
alimolala.Alitoka kitandani
akajinyoosha halafu akaenda
kufunua pazia akachungulia
nje.Mara mlago wake
ukagongwa akavaa shati na
kwenda kuufungua
akakutana na Ammar
“Abu Al zalawi” akasema
Ammar
“Ammar”
“Unaendeleaje Abu?
“Ninaendelea vizuri sana
Ammar”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Abu naomba nikutoe
hofu kwa lile tukio la jana
halitajirudia tena.Wewe ni
mtu wetu wa muhimu sana
hivyo unastahili heshima
kubwa.Naomba utambue
kwamba mimi kama kiongozi
wa kikundi hiki ninakuamini
asilimia mia moja hivyo
usiwe na hofu yoyote”
akasema Ammar
“Ahsante sana Ammar
kwa kuniamini” akasema
Mathew
“Abu nimekuja kukuaga
ninatoka kidogo kuna
sehemu ninakwenda
kuangalia kazi za
zinavyokwenda,wewe
utaendelea kupumzika hapa
ukihudumiwa.Unatakiwa
upone kabisa mjeraha yako
yote na utakapokuwa
umepona kabisa tutaanza
kazi” akasema Ammar
“Ahsante sana
Ammar.Ninahudumiwa
vizuri sana hapa.Ninajihisi
nyumbani” akasema Mathew
na Ammar akatabasamu
“Abu sikufanya makosa
kuamua kuungana
nawe.Ninapata picha ya
kundi letu kuwa kubwa na
hatari baada ya kujiunga
kwetu” akasema Ammar
“Usijali Ammar
tutafanya mambo mengi
sana pamoja.Tuzidi kuomba
uzima” akasema Mathew.
“Majeraha yako
yanaendeleaje?akaliza
Ammar.Mathew akavua
shati na Ammar
akamtazama akasikitika
“Watu wale ni wanyama
sana.Atakuja Nawal
kukuganga,ana taaluma ya
uuguzi na amekuwa
akisaidia sana watu wangu
kila pale wanapopatwa na
majeraha” akasema Ammar
na kuondoka
Kupitia dirishani
Mathew aliweza kuona
msafara wa magari
ukiondoka akarejea
kitandani kukaa.
“Natakiwa kuwajulisha
Mossad kwamba tayari
nimekwisha jiunga na
kikundi cha Ammar brigades
lakini sijui namna ya
kuwasiliana nao” akawaza
Mathew na picha ya Peniela
mke wake ikamjia kichwani
“Peniela na wanangu
ndio wanaonipa nguvu ya
kuendelea kuvumilia mateso
hata pale ninapokuwa
nimekata tamaa
kabisa.Nitahakikisha
ninajitahidi kutoka salama
mahala hapa ili nikaungane
nao tena” akawaza Mathew
na kumkumbuka Ruby
“Sipati picha Ruby
atakuwa alilia machozi kiasi
gani alipopata taarifa
kwamba nimefariki
dunia.Yule mrembo
ananipenda kupindukia na
alikuwa tayari kuacha kila
kitu kwa ajili yangu.Alikuwa
tayari hata kuhama London
na kuishi Tanzania kwa ajili
yangu.Sikuwahi kumpa jibu
kama nimekubali ombi lake
la mimi na yeye kuwa
wapenzi nilitaka kumpa jibu
baada ya kurejea kutoka
kuwakomboa Olivia na
Coletha lakini kwa bahati
mbaya sikurejea.Hii itakuwa
ilimuumiza mno.Je tayari
amekwisha pata mwanaume
mwingine kama Peniela?Ni
miaka mitatu tu lakini tayari
Peniela amekwisha pata
mwanaume.Je alikubaliana
na taarifa kwamba
nimefariki dunia?Alikubali
vipi nimekufa bila kuiona
maiti yangu? Alijaribu hata
kidogo kuutafuta ukweli na
kujiridhisha kweli nimekufa?
Akajiuliza Mathew
“Anyway nisimlamu sana
haya yote yaliyotokea ni kwa
sababu yangu.Kama
ningejiweka mbali na hizi
kazi hivi sasa ningekuwa
nafurahi na familia
yangu.Vipi kuhusu
wenzangu akina Gosu
Gosu?Nao pia wamekubali
kweli nimefariki? Gosu Gosu
sikuwa naye usiku ule
hiv……” Mathew akatolewa
mawazoni baada ya mlango
kugongwa.Akaenda
kuufungua akakutana na
Nawal
“Habari za asubuhi Abu
Al zalawi” akasema Nawal
“Habari nzuri
Nawal,karibu” akasema
Mathew na kumkaribisha
Amar ndani.Alikuwa
amebeba sinia lililokuwa na
kifungua kinywa vile vile
alikuwa ni kikapu ambacho
kilikuwa na dawa
“Abu nimeelekezwa nije
kukuganga majeraha yako”
akasema Nawal.Mathew
akavua shati na Nawal
akastuka baada ya kuyaona
majeraha makubwa
mgongoni mwa Mathew
“Pole sana
Abu.Wamekuumiza sana”
akasema Nawal akaanza
kuyasafisha majeraha yale
“Abu kwa nini uko
hapa?akauliza Nawal wakati
akiendelea kumganga
Mathew
“Kwa nini unauliza hivyo
Nawal?
“Hauonekani kama ni
gaidi.Sura na tabia za
magaidi ninazifahamu lakini
wewe si mmoja
wao.Unatafuta nini
hapa?akauliza Nawal
“Nilimuua mkuu wa
Mossad afrika Mashariki na
majasusi wengine
wawili.Niko hapa
kupambana na Israel”
akasema Mathew
“Jina lako halisi ni
nani?akauliza Nawal
“Naitwa Abu Al zalawi”
akasema Mathew
“Jina lako si Abu Al
Zalawi,wala wewe si gaidi”
akasema Nawal
“Amini utakavyo Nawal
lakini mimi jina langu ni
hilo” akasema Mathew
Nawal akaacha kazi
aliyokuwa anaifanya
akaenda kukaa mbele ya
Mathew.Muda wote
walikuwa wakizungumza
kiarabu lakini mara Nawal
akabadili lugha wakaanza
kuzungumza kiingereza
“Your real name is
Mathew Mulumbi and not
Abu Zalawi.You are from
Tanzania and not from
Kenya.You are an agent and
not a terrorist(jina lako ni
Mathew Mulumbi na si Abu
Zalawi.Unatokea Tanzania
na si Kenya.Wewe ni jasusi
na si gaidi)” akasema
Nawal.Mathew alihisi tumbo
linaanza kuunguruma kwa
mstuko alioupata.Akahisi
kijacho kumtoka
GCHQ
LONDON – UINGEREZA
Ruby akiwa katika ofisi
yake akiendelea na
majukumu simu yake
ikaita.Zilikuwa ni namba
ngeni katika simu yake na
simu ile ilitokea Tanzania
“Ni nani huyu?akajiuliza
Ruby akiwa ameishikilia ile
simu akizitazama zile namba
“Anayefahamu namba hii
kutoka Tanzania ni Gosu
Gosu pekee.Kama ni yeye
kwa nini ananipigia muda
huu wakati
nilikwishamuonya asinipigie
wakati niko kazini?akajiuliza
Ruby akionekana
kukasirika.Simu ilikatika
ikaanza kuita tena akaipokea
“Hallow” akasema
“Hallow” ikasema sauti
ambayo Ruby hakuwa
akiifahamu haikuwa sauti ya
Gosu Gosu aliyokuwa
ameitegemea
“Nazungumza na nani?
Akauliza
“Naongea na Ruby Rafael
Magalla?
Ruby akastuka jina lake
lilipotajwa
“Ndiyo unazungumza na
Ruby.Wewe ni nani?Umepata
wapi namba zangu?akauliza
Ruby kwa sauti ya ukali
kidogo
“Naitwa Dr Fabian
Kelelo Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania”
akasema Dr Fabian na Ruby
akabaki
anashangaa.Alistuka sana
“Hallow Ruby”
“Nimestuka kidogo
mheshimiwa Rais”
“Ruby samahani kwa
kukupigia simu hii bila
taarifa lakini nimelazimika
kukupigia kwa ajili ya jambo
moja la muhimu sana”
“Nakusikiliza
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby
“Ruby nimeamua
kukupigia simu mimi
mwenyewe kukujulisha
kwamba nimekuteua uwe
mkuu wa idara ya siri ya
usalama wa ndani wa nchi
SNSA”
“What? Ruby akashangaa
“Ni kweli Ruby
nimekuchagua kuwa
mkurugenzi mkuu wa idara
ya siri ya usalama wa ndani
ya nchi”
Ruby akacheka kidogo na
kusema
“Mheshimiwa Rais sijui
niseme nini lakini nimestuka
sana.Kwanza sifahamu
umenifahamuje hadi
ukaniona ninafaa?Pili mimi
si raia wa Tanzania japo
wazazi wangu ni watanzania
ambao baadae walichukua
uraia wa Uingereza”
“Ruby tafadhali usiseme
hapana.Nimekuteua kwa
kuwa ninaamini unaweza
ukaiongoza idara hii kwa
ufanisi mkubwa.Sikuwa
ninakufahamu lakini
wenzako akina Austin
wamekupendekeza kwangu
kwamba unafaa kwa nafasi
hii”
“Umesema Austin?! Ruby
akashangaa
“Ndiyo.Ninamuamini
sana Austin.Aliponieleza
kuwa unafaa kuongoza idara
hii sikuwa na shaka nawe
hata kidogo.Ruby nchi yetu
kwa sasa iko katika vita
kubwa ya kiuchumi na
tunaitegemea sana idara hii
ambayo nataka
uiongoze.Ruby nafahamu
nimekustukiza jambo kama
hili ila naomba utafakari na
unipe majibu kama utakuwa
tayari”
“Mheshimiwa Rais
nashukuru.Naomba nipe
muda nitafakari halafu
nitakujibu” akasema Ruby
na kuagana na Rais
“Mstuko kama huu
nilioupata leo niliupata siku
ile nilipoambiwa kwamba
Mathew amefariki
dunia.Japo mstuko huu
hawezi kulingana na ule wa
taarifa ya kifo cha Mathew
lakini nimestuka sana.Rais
anataka niwe mkurugenzi
wa SNSA ! Dah hiki si kitu
kidogo.Idara ile ni kubwa
sana na inahitaji mtu
makini.Ni idara ambayo
aliiongoza Devotha ambaye
alitaka kuniua kwa
risasi.Siwezi kusahau
kitendo kile” akawaza
Ruby.Kazi zake zote
zilisimama alishindwa
kuendelea na kazi
“Lazima iko sababu
kubwa hadi Austin
anipendekeze kwa Rais niwe
mkurugenzi wa SNSA.Huu
ni mtihani mkubwa kwangu
kwani hata hapa
wananitegemea sana lakini
asili yangu ni Tanzania.Toka
ndani ya moyo wangu
ninaipenda Tanzania kwani
ndiko atokako Mathew
Mulumbi mwanaume
nimpendaye kuliko wote
ambaye mpaka leo hii bado
siamini kama kweli
amefariki dunia.Nadhani
nafasi hii imekuja kwa
kusudi maalum kwani
nikiwa mkurugenzi wa idara
ile nitafahamu mambo mengi
ya nchi,siri nyingi za nchi
nitazijua na nitapata nafasi
nzuri ya kuupata ukweli
kuhusu Mathew
Mulumbi.Sina haja ya
kukataa nafasi kama hii
wala kujiuliza mara mbili
kama nikubali au nikatae”
akawaza Ruby na kuchukua
simu akapiga namba zile za
Rais
“Ruby” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais sina
sababu ya kutafakari jambo
kama hili wakati nchi
inanihitaji.Japo kwa sasa ni
raia wa nchi nyingine lakini
Tanzania ni nyumbani na
nina mapenzi makubwa na
nchi yangu hivyo nimekubali
uteuzi”
“Ahsante sana
Ruby.Ahsante
sana.Nimefurahi mno.Nchi
inahitaji vijana kama
wewe.Lini utakuja Tanzania?
“Kwanza itanilazimu
kuanza mchakato wa kuacha
kazi hapa ninapofanya kazi”
akasema Ruby na
kunyamaza kidogo
“Mheshimiwa rais
halitakuwa jambo jepesi na
la haraka kuacha kazi hapa
kwani kazi ninayoifanya ni
nyeti sana lakini kwa namna
yoyote ile lazima nihakikishe
nimefanikiwa kuacha kazi
hapa.Ninachokuomba jambo
hili la uteuzi wangu liwe siri
lisitangazwe” akasema Ruby
“jambo hili ni la siri
kubwa na anayefahamu ni
Austin na wenzake na siwezi
kumweleza mtu yeyote.Ruby
nafasi hii hatapewa mtu
mwingine zaidi yako hivyo
basi kamilisha taratibu zako
uje nyumbani tunakusubiri”
akasema Dr Fabian na
kuagana na Ruby
USIKOSE SEHEMU
IJAYO……………..

000000 0
 
Mkuu,Patrick ck. Kwanza nkupongeze sana kwa uandishi mahiri wa riwaya, nmekuwa mfuatiliaji WA riwaya zako kuanzia ile ya penieli mpka hii ya siri..

Kiukwe ww ni miongoni mwa waandishi mahiri kanisa na bora. Ntahakiki baadae katka maudhui ya mwandishi..

Ila ambavyo ni agharabu sanA kukipata kwa waandishi wengi ni uweredi wa mpangilio katika matukio, matumizi ya lugha, mpangilio wa kisimlizi, (ukutumia uwakilishi ktk uhalisia)

Ukwel ni hui mungu amekuba kipaji cha pekee, kunawakati nakusoma nAtamani kakuulza swali hapa uliwaza nn;;,,

Anyway asante. Nkirudi nami ntahakiki kidogo..

B
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 10
Haijulikani ni muda gani
watu walipeana taarifa kwani
kulipopambazuka tu watu
walianza kumiminika katika
ikulu ya Marekani na ilipofika
saa mbili za asubuhi maelfu ya
watu tayari walikwisha
kusanyika nje ya ikulu hiyo na
wengi wakiwa na mabango ya
kulaani kile ambacho nchi yao
imekuwa ikikifanya kupitia
kikundi cha G20.Waliwataka
viongozi wao wakuu
wawajibike
Ndani ya ikulu kulikuwa
na heka heka kubwa.Toka
usiku baada ya video ile ya
Mathew Mulumbi kulikuwa na
vikao mfululizo.
Saa tatu za asubuhi Rais
wa Marekani William
Washington akajitokeza mbele
ya waandishi wa habari
waliokuwa wamekusanyika
katika bustani ya
ikulu.Yalikuwa ni matangazo
ya moja kwa moja kutoka ikulu
na watu wengi walisubiri
kusikia kauli ya Rais kufuatia
kile kilichokuwa kimesemwa
na Mathew Mulumbi.
“Habari za asubuhi ndugu
wamarekani” akaanza hotuba
yake
“Toka usiku wa jana
Marekani haijalala kufuatia
maelezo ya kina aliyoyatoa
Abu Zalawi ambaye tayari
wengi tulikuwa tunamfahamu
kama gaidi aliyelipua ubalozi
wetu nchini Tanzania
Toka alipotoa maelezo
yake,kumekuwa na mjadala
mkubwa sana watu wakijaribu
kuchambua kile kilichoelezwa
na Abu Zalawi na wengine
wakidiriki kutaka kukanusha
au kupindisha ukweli wa kile
alichokisema.Nimesimama
mbele yenu asubuhi hii
kuweka sawa jambo hili” Rais
William akanyamaza kidogo
akawatazama waandishi wa
habari halafu akasema
“Yote aliyoeleza Abu
Zalawi jana ni ukweli
mtupu.Narudia tena kwamba
yote aliyoeleza Abu Zalawi jana
usiku ni kweli hakuna hata
neno moja la uongo
alilolitamka hivyo kusifanyike
juhudi zozote za kutaka
kupindisha ukweli ili
kuwasaidia watu waliohusika
katika uhalifu huu mkubwa.
Ni kweli ndani ya CIA
kumekuwa na kitengo cha siri
chenye jina G20 ambacho kazi
yake kubwa ni kujenga
mashirikiano na makundi
mbalimbali ya kigaidi.Kikundi
hiki kinaendeshwa kwa siri
kubwa na wanaofahamu
uwepo wake ni watu ishirini tu
ndiyo maana wakajiita G20.Hii
imekuwa ni siri kubwa na hata
rais hatakiwi kufahamu uwepo
wa kikundi hiki.
Sina hakika kama marais
wa Marekani waliopita
wanafahamu kitu kama hiki
lakini mimi nilipata bahati hivi
karibuni ya kuwafahamu
uwepo wa kikundi hicho ila
sikuweza kufanya chochote
kwa kuhofia kuuawa.Nilikuwa
mwoga” akanyamaza tena
kidogo
Nilifahamu uwepo wa
kundi hili wakati wakijiandaa
na mpango wa kuchochea
machafuko nchini Tanzania na
katika eneo zima la Afrika
Mashariki.Nilifahamishwa
mpango huo na mimi
nikaushiriki” akanyamaza
akameza mate na kwa mbali
alilengwa na machozi
“Watu wengi wameuawa
Afrika Mashariki hasa nchini
Uganda na Tanzania kufuatia
machafuko ya kidini
yaliyotokea ambayo na mimi
pia nimeyashiriki kwa lengo la
kupata mafuta kutoka nchini
Uganda.Nyote mlishuhudia
damu nyingi iliyomwagika
nchini Tanzania na Uganda
lakini wakati mauaji haya
yakifanyika na damu
ikimwagika sisi tuliendelea
kufurahia neema ya mafuta
.Meli zetu zilikuwa zimepanga
foleni katika bandari ya Tanga
nchini Tanzania zikipakia tani
na tani za mafuta.Huu ni
ukatili mkubwa sana.
Kama haitoshi bado
kulifanyika mpango wa
kwenda kusambaza kirusi
nchini Tanzania na mimi pia
nilishiriki katika mpango huo
lengo kuu likiwa ni kuendelea
kuchota rasilimali mbali mbali
zilizoko nchini humo na hasa
madini.Sitaki kurudia yale
aliyoyasema Abu Zalawi lakini
nataka nifafanue na nyote
msikie kutoka katika kinywa
changu kwamba yote yale yana
ukweli.
Pamoja na hayo yote bado
tulimtuma Abu Zalawi nchini
Iran na katika mpango huo
tukalipua ubalozi wetu jijini
Dar es salaam.Abu Zalawi
hahusiki chochote katika
shambulio lile yeye alitumika
kuingiza gari lenye bomu
katika ubalozi wetu.Gari
lililobeba bomu ni gari la
kwetu na hata bomu lililolipua
ubalozi wetu ni letu hivyo
tumeua watu wetu sisi
wenyewe.
Ndugu zangu wamarekani
kwa hayo niliyoyaeleza na
mengine mengi ambayo
sijayaeleza ninasimama mbele
yenu kukiri kwamba sisi
viongozi wenu
tumewaangusha.Tumetenda
makosa makubwa sana.Jana
usiku nilielekeza G20 wote
wakiongozwa na makamu wa
Rais Mark Piller wakamatwe
na mashitaka dhidi yao yaanze
mara moja kwani ushahidi wa
kutosha wa matendo yao upo.
Pamoja na hatua hiyo ya
kuwakamata viongozi wote wa
G20 lakini zipo pia hatua
nyingine ambazo
nimezichukua katika suala
hili.Kwanza kuna viongozi na
watu kadhaa kutoka Afrika
Mashariki ambao
walishirikiana na G20 katika
kuchochea vurugu ambao
wamekuja kupatiwa hifadhi
nchini Marekani.Mmoja wao
ni aliyewahi kuwa Rais wa
Uganda Jenerali Akiki
Rwamirama aliyepinduliwa na
kukimbilia hapa
Marekani.Huyu amekuwa ni
mmoja wa watu walioasisi kwa
kiasi kikubwa mpango huu wa
kuchochea vurugu na kupata
mafuta.Mbinu zote za
machafuko yale yeye ndiye
aliyebuni.Wapo vile vile
viongozi wengine wa dini na
siasa kutoka nchi za Tanzania
na Uganda walioshiriki katika
machafuko yale kisha
wakakimbilia hapa Marekani
na kupewa hifadhi wao na
familia zao baada ya
machafuko kuwa
makubwa.Hawa wote
watakamatwa na kurejeshwa
makwao kujibu mashitaka
watakayofunguliwa na nchi
zao kwa kushiriki kuchochea
vurugu zile.Ni aibu kwa
viongozi kutoka bara la Afrika
kuwa tayari kuwasaliti watu
wao,kusaliti nchi zao na
kuungana na mataifa
makubwa katika kuchota
rasilimali na wao kufaidika
kidogo.Nakiri kumekuwa na
wizi mkubwa wa rasilimali
mbali mbali katika bara la
Afrika unaofanywa na mataifa
makubwa wakishirikiana na
waafrika wenyewe hasa
viongozi na hivyo kulifanya
bara la Afrika kuendelea kuwa
masikini.Nawasihi waafrika
wawe na uzalendo na
kuzipenda nchi zao na
kuzipigania kama alivyofanya
Abu Zalawi
Jambo la pili,baada ya
kukubali kwamba tumefanya
uhalifu itatulazimu kulipa fidia
kwa nchi zilizoathiriwa.Mafuta
yote tuliyochukua kutoka
Uganda tutayalipa pamoja
tathmini ya fidia
zitakazowasilishwa kwetu
kutoka kwa nchi husika.
Mwisho kabisa kwa kuwa
na mimi ni sehemu ya uhalifu
huu ninapaswa kuwajibika
hivyo ninatangaza kwamba
kuanzia sasa nimejiuzulu
nafasi yangu ya urais ili sheria
iweze kuchukua mkondo
wake.Siwezi kubaki bila
kuwajibika hasa kwa haya
madhambi makubwa ambayo
tumeyafanya.
Mungu ibariki Marekani.
Rais William Washington
akamaliza hotuba yake na
kurejea ndani huku nje ya
ikulu watu wakiendelea
kuongezeka.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Nchini Tanzania bado
gumzo kubwa lilikuwa ni
maelezo ya Mathew Mulumbi
na hotuba aliyoitoa Rais
William Washington
akikubaliana na kile
alichokisema Mathew.Kuanzia
asubuhi ya siku ile kulikuwa na
kamata kamata kubwa.Majina
yote ya watu ambao walishiriki
katika kuchochea vurugu za
kidini zilizopelekea mamia ya
watu kupoteza maisha ambayo
yalitajwa na Assad Ismail
yalikabidhiwa kwa jeshi la
polisi na msako mkubwa
ukafanyika kuwawakamata
wote.
Hotuba ya Rais William
akiwataja baadhi ya watu
kutoka Afrika Mashariki hasa
Jenerali Akiki Rwamirama
aliyewahi kuwa Rais wa
Uganda iliwastua watu wengi
wa Afrika
mashariki.Hawakutegemea
kabisa kama Jenerali Akiki
angeweza kuhusika katika
machafuko yale
Saa mbili za usiku kwa saa
za Afrika Mashariki Rais wa
Tanzania Dr Fabian kelelo
akalihutubia taifa.Katika
hotuba yake akawatangazia
watanzania kwamba hakuna
tena vurugu zitakazotokea
kwani wachochezi wote wa
vurugu zile wamekamatwa na
wengine kuuawa.Aliwasisitiza
watanzania kuendelea kuishi
kwa upendo kama
walivyokuwa wakiishi kabla ya
kuchonganishwa ili
wachukiane.Aliwataka kwa
namna yoyote ile wasikubali
kuchonganishwa tena na mtu
yeyote na kupelekea kupigana
wao kwa wao.Ilikuwa ni
hotuba ndefu iliyobeba mambo
mengi na kubwa likiwa ni
amani upendo na kuvumiliana
hata pale kunapokuwa na
tofauti za kiimani.Mwisho
kabisa aliwaahidi watanzania
kuzilinda rasilimali za nchi
kwa gharama zozote zile na
kuwataka watanzania wote kila
mmoja awe mlinzi wa rasili
mali hizo kwa faida yao na
vizazi vijavyo.Kabla hajamaliza
hotuba yake Dr Fabian
akawamwagia sifa tele Mathew
na wenzake ambao
walipambana usiku na mchana
kuhakikisha kwamba
wanaufahamu ukweli.
Baada ya kumaliza hotuba
yake,simu zikaanza kuingia
mfululizo katika simu ya rais
lakini hakutaka kupokea simu
hata moja kwa wakati ule
lakini alipoiona simu ya Ruby
akaipokea.
“Hallo Ruby” akasema
DrFabian
“Mheshimiwa Rais
nimekupigia kukupongeza kwa
hotuba nzuri uliyoitoa”
akasema Ruby
“Ahante sana
Ruby.Utanisamehe sikuweza
kuwataja kwa majina lakini
nimewashukuru nyote kwa
ujumla wenu kwa kazi kubwa
mliyoifanya”
“Usijali mheshimiwa Rais”
“Vipi kuhusu Mathew
Mulumbi umewasiliana naye?
“Ndiyo nimekuwa
nawasiliana naye mara kwa
mara leo yuko Riyadh Saudi
Arabia.Habiba Jawad
amefariki dunia”
“Habiba amefariki dunia?
“Ndiyo amefarki dunia
amejiua kwa kujipiga risasi”
“Lini atarejea nyumbani?
Akauliza DrFabian
“Bado hajaweka wazi lini
atarejea nyumbani lakini
akiwa tayari atatujulisha”
akajibu Ruby
“Sawa Ruby.Lazima
tumpokee kwa shangwe shujaa
wetu kwani amefanya mambo
makubwa sana” akasema Dr
Fabian na ukimya ukapita
“Ruby kama ukipata nafasi
usiku wa leo tunaweza
kuonana? Akauliza Dr
Fabian.Ruby akafikiri kidogo
na kusema
“Hakuna tatizo nitakuja”
akajibu Ruby ambaye alijawa
na furaha kubwa siku hii
“Kwa sasa baada ya
mambo yote kumalizika ni
wakati wa kumueleza Ruby
ukweli.Ninampenda na
ninataka awe mke wangu.Ana
kila sifa ya kuwa
mke.Yawezekana nikiwa naye
ninaweza kufikiria hata
kuwania kipindi cha pili cha
urais” akawaza Dr Fabian
huku akitabasamu
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa tatu za usiku Mathew
na Nawal waliwasili Riyadh
wakitokea nchini
Marekani.Sayid Omar
alikuwepo uwanjani
kuwapokea ksha wakaelekea
nyumbani.Watu walikuwa
wengi na majonzi yalitawala
.Baada ya Mathew na Nawal
kuwasili nyumbani kwa
Habiba vilio vikaanza
upya.Nawal alilia mno.Mathew
akaenda kuungana na watu
waliokuja kuwafariji na wengi
wakimpongeza kwa kile
alichokifanya.Tayari alikuwa
ni mtu maarufu kufuatia kile
alichokifanya nchini Marekani
ambacho kilitazamwa na
karibu dunia nzima
Ilipofika saa saba za usiku
Mathew akaenda kupumzika
katika nyumba yake kujiandaa
na siku ya kesho ambapo
Habiba angezikwa.
“Imekuwa ni kama filamu
ambayo imefika
mwisho.Nimepitia mengi sana
katika sakata hili toka
lilipoanza.Nafikiri nahitaji
kuyatafakari tena maisha
yangu.Ngoja kwanza tumzike
mama Habiba halafu nitajua
nini kitafuata” akawaza
Mathew na kulala
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliwasili ikulu saa
nne za usiku kama
alivyoombwa na Rais Dr
Fabian ambaye usiku huu
alichangamka sana.
“Ruby karibu” akasema Dr
Fabian na kumkaribisha katika
sebule yake
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu
Ruby huku akitabasamu
“Ruby kabla ya yote nataka
kwanza tufungue shampeni
kusherehekea ushindi mkubwa
tulioupata” akasema Dr Fabian
na kufungua shampeni
wakagonganisha glasi
Baada ya maongezi kidogo
Dr Fabian akasema
“Ruby hii imekuwa ni vita
ngumu lakini tumeipigana
tumeimaliza ahsante kwako na
wenzako.Kwa sasa baada ya
vita hii kumalizika maisha
lazima yaendelee.Nimekuita
hapa usiku huu sitaki
tuzungumze kuhusu kazi
kwani kila tunapokutana
imekuwa ni mazungumzo ya
kazi.Nataka usiku huu
tuzungumze kuhusu
maisha.Tusizame katika kazi
na kusahau kwamba kuna
muda na sisi tunahitaji kuwa
na maisha ya kawaida kama
wengine” akasema Dr Fabian
“Ni kweli mheshimiwa
Rais” akajibu Ruby
“Nini mipango yako hasa
baada ya jambo hili kubwa
kumalizika?
“Mheshimiwa Rais hiki
kilichotokea kimenifundisha
mambo mengi .Nimeingia
katika kazi hii ya kuongoza
idara nyeti kama SNSA bila
kuwa na ujuzi mkubwa wa
masuala ya ujasusi.Mimi ni
mtaalamu wa kompyuta na
kinachonisaidia ni uzoefu
mdogo nilionao baada ya kuwa
karibu na Mathew Mulumbi na
nikashiriki naye katika
misheni mbali mbali.Kwa hiyo
mheshimiwa Rais nimeamua
kwenda kusomea masuala ya
ujasusi ili niive kabisa”
akasema Ruby
“Ruby una uhakika
unataka kwenda kusomea
masuala ya ujasusi?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ninataka kusomea
ujasusi” akajibu Ruby
“Ruby naomba niwe
muwazi kwako.Binafsi sitaki
uendelee na kazi hii ya
ujasusi.Nimeshuhudia ni kazi
iliyojaa hatari sana na kwa
mtoto mzuri kama wewe
haikufai.Ninataka kukutafutia
nafasi nzuri zaidi kuliko hiyo”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais ulinitoa
Uingereza nije niifanye kazi hii
hivyo nataka nikasome ili
niifanye kwa ufanisi”
“Hapana Ruby sitaki
uende ukasomee masuala
haya” akasema Dr Fabian
“Kwa nini mheshimiwa
rais”
“Ruby sisi ni watu wazima
hivyo sitaki kuzunguka
zunguka kama wafanyavyo
vijana.Naomba niwe mkweli
kwako.Ninakupenda sana
Ruby na lengo langu ni mimi
nawe tuwe na mahusiano na
ikiwezekana tuishi pamoja”
akasema Dr Fabian na Ruby
hakustuka akatabasamu
“Mheshimiwa Rais
ninashukuru kwa kunieleza
ukweli.Hili ni jambo ambalo
siwezi kulitolea majibu ya
haraka.Naomba unipe muda
mheshimiwa Rais nitafakari
halafu nitakujibu” akasema
Ruby
“Ruby naomba ujipe muda
kisha utanijibu na
nitakubaliana na jibu lolote
utakalonipatia lakini narudia
tena Ruby kwamba
ninakupenda na ninakuhitaji
mno katika maisha
yangu.Baada ya kumpoteza
Millen ni wewe ambaye Mungu
amekuleta karibu yangu”
akasema Dr Fabian
“Nimekwisha kuelewa
mheshimiwa Rais usihofu”
akasema Ruby
Walizungumza mambo
mengi kuhusiana na maisha
yao kisha wakaagana Ruby
akaondoka
RIYADH – SAUDI ARABIA
Mazishi ya Habiba Jawad
yalilifanya jiji la Riyadh
lizizime.Umati mkubwa mno
ulijitokeza kumsindikiza
Habiba Jawad katika safari
yake ya mwisho.
Saa nne za usiku baada ya
watu kuondoka Mathew na
Nawal waliingia ndani ya
chumba cha Habiba
Jawad,Nawal akafungua kasiki
la Habiba ambako walikuta
nyaraka ambazo Habiba
aliziandaa zinazoonyesha
kwamba utajiri wake wote
amewaachia Mathew na
Nawal.
“Mathew tumeachiwa
utajiri mkubwa sana na
Habiba.Nini mawazo yako?
Akauliza Nawal
“Nawal kitu kimoja tu
ninachoweza kusema ni
kwamba utajiri huu wote
ninaukabidhi kwako”
“Hapana Mathew.Mama
Habiba ametukabidhi sote
utajiri huu wote”
“Nakubali lakini na mimi
ninakukabidhi wewe utajiri
huu”
“Kwa nini Mathew?
“Ninahitaji
kupotea.Nahitaji kwenda
mahala mbali kabisa ambako
nitapata muda wa kutafakari
kuhusu maisha yangu na
kusahau yale yote
niliyoyapitia.Nimepitia
mambo mengi sana Nawal”
“Vipi kuhusu Ruby?
“Ninampenda Ruby lakini
sina hakika kama mimi ni
mwanaume sahihi
kwake.Maisha yangu
yamekuwa namna hii na siwezi
kumpatia furaha ya maisha
anayoihitaji.Yawezekana haya
ndiyo maisha niliyopangiwa na
Mungu.Utazungumza naye na
kumwambia kwamba
ninampenda lakini aendelee
na maisha yake na asinisubiri”
akasema Mathew wakaendelea
na mazungumzo yao.
BAADA YA MWAKA MMOJA
Watuhumiwa wote wa
vurugu zilizopelekea
umwagikaji mkubwa wa damu
Afrika Mashariki walikwisha
hukumiwa kuanzia miaka
thelathini hadi kifungo cha
maisha gerezani.Amani
ilitamalaki tena watu
wakiendelea kuishi kama
ndugu.
Baada ya kujiuzulu Rais
William Washington,Marekani
ilipata Rais mpya ambaye
alifanya mazungumzo na Rais
wa Iran na baada ya muda
mrefu muafaka kati ya mataifa
haya mawili ukapatikana na
nchi ya Iran ikaondolewa
vikwazo vya kiuchumi
ilivyowekewa.
Baada ya kukosa ufadhili
wa fedha,makundi mbali mbali
ya kigaidi yalidhoofika na
mengine kufa kabisa.
Idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi SNSA ilipata
mkurugenzi mpya baada ya
Ruby na Gosu Gosu kuacha
kazi.Gosu Gosu aliendelea
kusimamia biashara za
Mathew
Tukio kubwa kabisa
lililotokea baada ya mwaka
mmoja ni ndoa ya Dr Fabian
Kelelo na Ruby.Ilikuwa ni
sherehe kubwa iliyolitikisa jiji
la Dar es salaam.Ruby aliamua
kufunga ndoa na Dr Fabian
baada ya kuhakikishiwa na
Nawal kwamba Mathew
amempa ruhusu ya kuendelea
na maisha yake.
Watu wengi walijiuliza
mahala alipo shujaa Mathew
Mulumbi na wengi wakijiuliza
kwa nini hakurejea nyumbani
ili wampongeze baada ya
jambo kubwa alilolifanya miezi
kumi na mbili
iliyopita.Mathew alifanya siri
kubwa mahali alipo.Hakutaka
kujulikana alikwenda wapi
kwani alihitaji mapumziko
marefu na kujitafakari kuhusu
maisha yake.
TAMATI

NDUGU
MSOMAJI,AHSANTE
KWA KUIFUATILIA
SIMULIZI HII NDEFU YA
SIRI.TUNA UHAKIKA
UTAENDELEA
KUTUUNGA MKONO
KWA KUFUATILIA
SIMULIZI ZETU
NYINGINE
ZITAKAZOFUATA
BAADA YA KUMSOMA
MATHEW MULUMBI
KATIKA SIMULIZI
KADHAA JE
UMEMFAHAMU VIZURI
MATHEW NI MTU WA
NAMNA GANI?
KUMFAHAMU VYEMA
MATHEW NI MTU WA
NAMNA GANI USIKOSE
SIMULIZI INAYOFUATA
YA
SCANDAL(KASHFA)
Ahsante mkuu
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 10
Haijulikani ni muda gani
watu walipeana taarifa kwani
kulipopambazuka tu watu
walianza kumiminika katika
ikulu ya Marekani na ilipofika
saa mbili za asubuhi maelfu ya
watu tayari walikwisha
kusanyika nje ya ikulu hiyo na
wengi wakiwa na mabango ya
kulaani kile ambacho nchi yao
imekuwa ikikifanya kupitia
kikundi cha G20.Waliwataka
viongozi wao wakuu
wawajibike
Ndani ya ikulu kulikuwa
na heka heka kubwa.Toka
usiku baada ya video ile ya
Mathew Mulumbi kulikuwa na
vikao mfululizo.
Saa tatu za asubuhi Rais
wa Marekani William
Washington akajitokeza mbele
ya waandishi wa habari
waliokuwa wamekusanyika
katika bustani ya
ikulu.Yalikuwa ni matangazo
ya moja kwa moja kutoka ikulu
na watu wengi walisubiri
kusikia kauli ya Rais kufuatia
kile kilichokuwa kimesemwa
na Mathew Mulumbi.
“Habari za asubuhi ndugu
wamarekani” akaanza hotuba
yake
“Toka usiku wa jana
Marekani haijalala kufuatia
maelezo ya kina aliyoyatoa
Abu Zalawi ambaye tayari
wengi tulikuwa tunamfahamu
kama gaidi aliyelipua ubalozi
wetu nchini Tanzania
Toka alipotoa maelezo
yake,kumekuwa na mjadala
mkubwa sana watu wakijaribu
kuchambua kile kilichoelezwa
na Abu Zalawi na wengine
wakidiriki kutaka kukanusha
au kupindisha ukweli wa kile
alichokisema.Nimesimama
mbele yenu asubuhi hii
kuweka sawa jambo hili” Rais
William akanyamaza kidogo
akawatazama waandishi wa
habari halafu akasema
“Yote aliyoeleza Abu
Zalawi jana ni ukweli
mtupu.Narudia tena kwamba
yote aliyoeleza Abu Zalawi jana
usiku ni kweli hakuna hata
neno moja la uongo
alilolitamka hivyo kusifanyike
juhudi zozote za kutaka
kupindisha ukweli ili
kuwasaidia watu waliohusika
katika uhalifu huu mkubwa.
Ni kweli ndani ya CIA
kumekuwa na kitengo cha siri
chenye jina G20 ambacho kazi
yake kubwa ni kujenga
mashirikiano na makundi
mbalimbali ya kigaidi.Kikundi
hiki kinaendeshwa kwa siri
kubwa na wanaofahamu
uwepo wake ni watu ishirini tu
ndiyo maana wakajiita G20.Hii
imekuwa ni siri kubwa na hata
rais hatakiwi kufahamu uwepo
wa kikundi hiki.
Sina hakika kama marais
wa Marekani waliopita
wanafahamu kitu kama hiki
lakini mimi nilipata bahati hivi
karibuni ya kuwafahamu
uwepo wa kikundi hicho ila
sikuweza kufanya chochote
kwa kuhofia kuuawa.Nilikuwa
mwoga” akanyamaza tena
kidogo
Nilifahamu uwepo wa
kundi hili wakati wakijiandaa
na mpango wa kuchochea
machafuko nchini Tanzania na
katika eneo zima la Afrika
Mashariki.Nilifahamishwa
mpango huo na mimi
nikaushiriki” akanyamaza
akameza mate na kwa mbali
alilengwa na machozi
“Watu wengi wameuawa
Afrika Mashariki hasa nchini
Uganda na Tanzania kufuatia
machafuko ya kidini
yaliyotokea ambayo na mimi
pia nimeyashiriki kwa lengo la
kupata mafuta kutoka nchini
Uganda.Nyote mlishuhudia
damu nyingi iliyomwagika
nchini Tanzania na Uganda
lakini wakati mauaji haya
yakifanyika na damu
ikimwagika sisi tuliendelea
kufurahia neema ya mafuta
.Meli zetu zilikuwa zimepanga
foleni katika bandari ya Tanga
nchini Tanzania zikipakia tani
na tani za mafuta.Huu ni
ukatili mkubwa sana.
Kama haitoshi bado
kulifanyika mpango wa
kwenda kusambaza kirusi
nchini Tanzania na mimi pia
nilishiriki katika mpango huo
lengo kuu likiwa ni kuendelea
kuchota rasilimali mbali mbali
zilizoko nchini humo na hasa
madini.Sitaki kurudia yale
aliyoyasema Abu Zalawi lakini
nataka nifafanue na nyote
msikie kutoka katika kinywa
changu kwamba yote yale yana
ukweli.
Pamoja na hayo yote bado
tulimtuma Abu Zalawi nchini
Iran na katika mpango huo
tukalipua ubalozi wetu jijini
Dar es salaam.Abu Zalawi
hahusiki chochote katika
shambulio lile yeye alitumika
kuingiza gari lenye bomu
katika ubalozi wetu.Gari
lililobeba bomu ni gari la
kwetu na hata bomu lililolipua
ubalozi wetu ni letu hivyo
tumeua watu wetu sisi
wenyewe.
Ndugu zangu wamarekani
kwa hayo niliyoyaeleza na
mengine mengi ambayo
sijayaeleza ninasimama mbele
yenu kukiri kwamba sisi
viongozi wenu
tumewaangusha.Tumetenda
makosa makubwa sana.Jana
usiku nilielekeza G20 wote
wakiongozwa na makamu wa
Rais Mark Piller wakamatwe
na mashitaka dhidi yao yaanze
mara moja kwani ushahidi wa
kutosha wa matendo yao upo.
Pamoja na hatua hiyo ya
kuwakamata viongozi wote wa
G20 lakini zipo pia hatua
nyingine ambazo
nimezichukua katika suala
hili.Kwanza kuna viongozi na
watu kadhaa kutoka Afrika
Mashariki ambao
walishirikiana na G20 katika
kuchochea vurugu ambao
wamekuja kupatiwa hifadhi
nchini Marekani.Mmoja wao
ni aliyewahi kuwa Rais wa
Uganda Jenerali Akiki
Rwamirama aliyepinduliwa na
kukimbilia hapa
Marekani.Huyu amekuwa ni
mmoja wa watu walioasisi kwa
kiasi kikubwa mpango huu wa
kuchochea vurugu na kupata
mafuta.Mbinu zote za
machafuko yale yeye ndiye
aliyebuni.Wapo vile vile
viongozi wengine wa dini na
siasa kutoka nchi za Tanzania
na Uganda walioshiriki katika
machafuko yale kisha
wakakimbilia hapa Marekani
na kupewa hifadhi wao na
familia zao baada ya
machafuko kuwa
makubwa.Hawa wote
watakamatwa na kurejeshwa
makwao kujibu mashitaka
watakayofunguliwa na nchi
zao kwa kushiriki kuchochea
vurugu zile.Ni aibu kwa
viongozi kutoka bara la Afrika
kuwa tayari kuwasaliti watu
wao,kusaliti nchi zao na
kuungana na mataifa
makubwa katika kuchota
rasilimali na wao kufaidika
kidogo.Nakiri kumekuwa na
wizi mkubwa wa rasilimali
mbali mbali katika bara la
Afrika unaofanywa na mataifa
makubwa wakishirikiana na
waafrika wenyewe hasa
viongozi na hivyo kulifanya
bara la Afrika kuendelea kuwa
masikini.Nawasihi waafrika
wawe na uzalendo na
kuzipenda nchi zao na
kuzipigania kama alivyofanya
Abu Zalawi
Jambo la pili,baada ya
kukubali kwamba tumefanya
uhalifu itatulazimu kulipa fidia
kwa nchi zilizoathiriwa.Mafuta
yote tuliyochukua kutoka
Uganda tutayalipa pamoja
tathmini ya fidia
zitakazowasilishwa kwetu
kutoka kwa nchi husika.
Mwisho kabisa kwa kuwa
na mimi ni sehemu ya uhalifu
huu ninapaswa kuwajibika
hivyo ninatangaza kwamba
kuanzia sasa nimejiuzulu
nafasi yangu ya urais ili sheria
iweze kuchukua mkondo
wake.Siwezi kubaki bila
kuwajibika hasa kwa haya
madhambi makubwa ambayo
tumeyafanya.
Mungu ibariki Marekani.
Rais William Washington
akamaliza hotuba yake na
kurejea ndani huku nje ya
ikulu watu wakiendelea
kuongezeka.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Nchini Tanzania bado
gumzo kubwa lilikuwa ni
maelezo ya Mathew Mulumbi
na hotuba aliyoitoa Rais
William Washington
akikubaliana na kile
alichokisema Mathew.Kuanzia
asubuhi ya siku ile kulikuwa na
kamata kamata kubwa.Majina
yote ya watu ambao walishiriki
katika kuchochea vurugu za
kidini zilizopelekea mamia ya
watu kupoteza maisha ambayo
yalitajwa na Assad Ismail
yalikabidhiwa kwa jeshi la
polisi na msako mkubwa
ukafanyika kuwawakamata
wote.
Hotuba ya Rais William
akiwataja baadhi ya watu
kutoka Afrika Mashariki hasa
Jenerali Akiki Rwamirama
aliyewahi kuwa Rais wa
Uganda iliwastua watu wengi
wa Afrika
mashariki.Hawakutegemea
kabisa kama Jenerali Akiki
angeweza kuhusika katika
machafuko yale
Saa mbili za usiku kwa saa
za Afrika Mashariki Rais wa
Tanzania Dr Fabian kelelo
akalihutubia taifa.Katika
hotuba yake akawatangazia
watanzania kwamba hakuna
tena vurugu zitakazotokea
kwani wachochezi wote wa
vurugu zile wamekamatwa na
wengine kuuawa.Aliwasisitiza
watanzania kuendelea kuishi
kwa upendo kama
walivyokuwa wakiishi kabla ya
kuchonganishwa ili
wachukiane.Aliwataka kwa
namna yoyote ile wasikubali
kuchonganishwa tena na mtu
yeyote na kupelekea kupigana
wao kwa wao.Ilikuwa ni
hotuba ndefu iliyobeba mambo
mengi na kubwa likiwa ni
amani upendo na kuvumiliana
hata pale kunapokuwa na
tofauti za kiimani.Mwisho
kabisa aliwaahidi watanzania
kuzilinda rasilimali za nchi
kwa gharama zozote zile na
kuwataka watanzania wote kila
mmoja awe mlinzi wa rasili
mali hizo kwa faida yao na
vizazi vijavyo.Kabla hajamaliza
hotuba yake Dr Fabian
akawamwagia sifa tele Mathew
na wenzake ambao
walipambana usiku na mchana
kuhakikisha kwamba
wanaufahamu ukweli.
Baada ya kumaliza hotuba
yake,simu zikaanza kuingia
mfululizo katika simu ya rais
lakini hakutaka kupokea simu
hata moja kwa wakati ule
lakini alipoiona simu ya Ruby
akaipokea.
“Hallo Ruby” akasema
DrFabian
“Mheshimiwa Rais
nimekupigia kukupongeza kwa
hotuba nzuri uliyoitoa”
akasema Ruby
“Ahante sana
Ruby.Utanisamehe sikuweza
kuwataja kwa majina lakini
nimewashukuru nyote kwa
ujumla wenu kwa kazi kubwa
mliyoifanya”
“Usijali mheshimiwa Rais”
“Vipi kuhusu Mathew
Mulumbi umewasiliana naye?
“Ndiyo nimekuwa
nawasiliana naye mara kwa
mara leo yuko Riyadh Saudi
Arabia.Habiba Jawad
amefariki dunia”
“Habiba amefariki dunia?
“Ndiyo amefarki dunia
amejiua kwa kujipiga risasi”
“Lini atarejea nyumbani?
Akauliza DrFabian
“Bado hajaweka wazi lini
atarejea nyumbani lakini
akiwa tayari atatujulisha”
akajibu Ruby
“Sawa Ruby.Lazima
tumpokee kwa shangwe shujaa
wetu kwani amefanya mambo
makubwa sana” akasema Dr
Fabian na ukimya ukapita
“Ruby kama ukipata nafasi
usiku wa leo tunaweza
kuonana? Akauliza Dr
Fabian.Ruby akafikiri kidogo
na kusema
“Hakuna tatizo nitakuja”
akajibu Ruby ambaye alijawa
na furaha kubwa siku hii
“Kwa sasa baada ya
mambo yote kumalizika ni
wakati wa kumueleza Ruby
ukweli.Ninampenda na
ninataka awe mke wangu.Ana
kila sifa ya kuwa
mke.Yawezekana nikiwa naye
ninaweza kufikiria hata
kuwania kipindi cha pili cha
urais” akawaza Dr Fabian
huku akitabasamu
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa tatu za usiku Mathew
na Nawal waliwasili Riyadh
wakitokea nchini
Marekani.Sayid Omar
alikuwepo uwanjani
kuwapokea ksha wakaelekea
nyumbani.Watu walikuwa
wengi na majonzi yalitawala
.Baada ya Mathew na Nawal
kuwasili nyumbani kwa
Habiba vilio vikaanza
upya.Nawal alilia mno.Mathew
akaenda kuungana na watu
waliokuja kuwafariji na wengi
wakimpongeza kwa kile
alichokifanya.Tayari alikuwa
ni mtu maarufu kufuatia kile
alichokifanya nchini Marekani
ambacho kilitazamwa na
karibu dunia nzima
Ilipofika saa saba za usiku
Mathew akaenda kupumzika
katika nyumba yake kujiandaa
na siku ya kesho ambapo
Habiba angezikwa.
“Imekuwa ni kama filamu
ambayo imefika
mwisho.Nimepitia mengi sana
katika sakata hili toka
lilipoanza.Nafikiri nahitaji
kuyatafakari tena maisha
yangu.Ngoja kwanza tumzike
mama Habiba halafu nitajua
nini kitafuata” akawaza
Mathew na kulala
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliwasili ikulu saa
nne za usiku kama
alivyoombwa na Rais Dr
Fabian ambaye usiku huu
alichangamka sana.
“Ruby karibu” akasema Dr
Fabian na kumkaribisha katika
sebule yake
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu
Ruby huku akitabasamu
“Ruby kabla ya yote nataka
kwanza tufungue shampeni
kusherehekea ushindi mkubwa
tulioupata” akasema Dr Fabian
na kufungua shampeni
wakagonganisha glasi
Baada ya maongezi kidogo
Dr Fabian akasema
“Ruby hii imekuwa ni vita
ngumu lakini tumeipigana
tumeimaliza ahsante kwako na
wenzako.Kwa sasa baada ya
vita hii kumalizika maisha
lazima yaendelee.Nimekuita
hapa usiku huu sitaki
tuzungumze kuhusu kazi
kwani kila tunapokutana
imekuwa ni mazungumzo ya
kazi.Nataka usiku huu
tuzungumze kuhusu
maisha.Tusizame katika kazi
na kusahau kwamba kuna
muda na sisi tunahitaji kuwa
na maisha ya kawaida kama
wengine” akasema Dr Fabian
“Ni kweli mheshimiwa
Rais” akajibu Ruby
“Nini mipango yako hasa
baada ya jambo hili kubwa
kumalizika?
“Mheshimiwa Rais hiki
kilichotokea kimenifundisha
mambo mengi .Nimeingia
katika kazi hii ya kuongoza
idara nyeti kama SNSA bila
kuwa na ujuzi mkubwa wa
masuala ya ujasusi.Mimi ni
mtaalamu wa kompyuta na
kinachonisaidia ni uzoefu
mdogo nilionao baada ya kuwa
karibu na Mathew Mulumbi na
nikashiriki naye katika
misheni mbali mbali.Kwa hiyo
mheshimiwa Rais nimeamua
kwenda kusomea masuala ya
ujasusi ili niive kabisa”
akasema Ruby
“Ruby una uhakika
unataka kwenda kusomea
masuala ya ujasusi?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ninataka kusomea
ujasusi” akajibu Ruby
“Ruby naomba niwe
muwazi kwako.Binafsi sitaki
uendelee na kazi hii ya
ujasusi.Nimeshuhudia ni kazi
iliyojaa hatari sana na kwa
mtoto mzuri kama wewe
haikufai.Ninataka kukutafutia
nafasi nzuri zaidi kuliko hiyo”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais ulinitoa
Uingereza nije niifanye kazi hii
hivyo nataka nikasome ili
niifanye kwa ufanisi”
“Hapana Ruby sitaki
uende ukasomee masuala
haya” akasema Dr Fabian
“Kwa nini mheshimiwa
rais”
“Ruby sisi ni watu wazima
hivyo sitaki kuzunguka
zunguka kama wafanyavyo
vijana.Naomba niwe mkweli
kwako.Ninakupenda sana
Ruby na lengo langu ni mimi
nawe tuwe na mahusiano na
ikiwezekana tuishi pamoja”
akasema Dr Fabian na Ruby
hakustuka akatabasamu
“Mheshimiwa Rais
ninashukuru kwa kunieleza
ukweli.Hili ni jambo ambalo
siwezi kulitolea majibu ya
haraka.Naomba unipe muda
mheshimiwa Rais nitafakari
halafu nitakujibu” akasema
Ruby
“Ruby naomba ujipe muda
kisha utanijibu na
nitakubaliana na jibu lolote
utakalonipatia lakini narudia
tena Ruby kwamba
ninakupenda na ninakuhitaji
mno katika maisha
yangu.Baada ya kumpoteza
Millen ni wewe ambaye Mungu
amekuleta karibu yangu”
akasema Dr Fabian
“Nimekwisha kuelewa
mheshimiwa Rais usihofu”
akasema Ruby
Walizungumza mambo
mengi kuhusiana na maisha
yao kisha wakaagana Ruby
akaondoka
RIYADH – SAUDI ARABIA
Mazishi ya Habiba Jawad
yalilifanya jiji la Riyadh
lizizime.Umati mkubwa mno
ulijitokeza kumsindikiza
Habiba Jawad katika safari
yake ya mwisho.
Saa nne za usiku baada ya
watu kuondoka Mathew na
Nawal waliingia ndani ya
chumba cha Habiba
Jawad,Nawal akafungua kasiki
la Habiba ambako walikuta
nyaraka ambazo Habiba
aliziandaa zinazoonyesha
kwamba utajiri wake wote
amewaachia Mathew na
Nawal.
“Mathew tumeachiwa
utajiri mkubwa sana na
Habiba.Nini mawazo yako?
Akauliza Nawal
“Nawal kitu kimoja tu
ninachoweza kusema ni
kwamba utajiri huu wote
ninaukabidhi kwako”
“Hapana Mathew.Mama
Habiba ametukabidhi sote
utajiri huu wote”
“Nakubali lakini na mimi
ninakukabidhi wewe utajiri
huu”
“Kwa nini Mathew?
“Ninahitaji
kupotea.Nahitaji kwenda
mahala mbali kabisa ambako
nitapata muda wa kutafakari
kuhusu maisha yangu na
kusahau yale yote
niliyoyapitia.Nimepitia
mambo mengi sana Nawal”
“Vipi kuhusu Ruby?
“Ninampenda Ruby lakini
sina hakika kama mimi ni
mwanaume sahihi
kwake.Maisha yangu
yamekuwa namna hii na siwezi
kumpatia furaha ya maisha
anayoihitaji.Yawezekana haya
ndiyo maisha niliyopangiwa na
Mungu.Utazungumza naye na
kumwambia kwamba
ninampenda lakini aendelee
na maisha yake na asinisubiri”
akasema Mathew wakaendelea
na mazungumzo yao.
BAADA YA MWAKA MMOJA
Watuhumiwa wote wa
vurugu zilizopelekea
umwagikaji mkubwa wa damu
Afrika Mashariki walikwisha
hukumiwa kuanzia miaka
thelathini hadi kifungo cha
maisha gerezani.Amani
ilitamalaki tena watu
wakiendelea kuishi kama
ndugu.
Baada ya kujiuzulu Rais
William Washington,Marekani
ilipata Rais mpya ambaye
alifanya mazungumzo na Rais
wa Iran na baada ya muda
mrefu muafaka kati ya mataifa
haya mawili ukapatikana na
nchi ya Iran ikaondolewa
vikwazo vya kiuchumi
ilivyowekewa.
Baada ya kukosa ufadhili
wa fedha,makundi mbali mbali
ya kigaidi yalidhoofika na
mengine kufa kabisa.
Idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi SNSA ilipata
mkurugenzi mpya baada ya
Ruby na Gosu Gosu kuacha
kazi.Gosu Gosu aliendelea
kusimamia biashara za
Mathew
Tukio kubwa kabisa
lililotokea baada ya mwaka
mmoja ni ndoa ya Dr Fabian
Kelelo na Ruby.Ilikuwa ni
sherehe kubwa iliyolitikisa jiji
la Dar es salaam.Ruby aliamua
kufunga ndoa na Dr Fabian
baada ya kuhakikishiwa na
Nawal kwamba Mathew
amempa ruhusu ya kuendelea
na maisha yake.
Watu wengi walijiuliza
mahala alipo shujaa Mathew
Mulumbi na wengi wakijiuliza
kwa nini hakurejea nyumbani
ili wampongeze baada ya
jambo kubwa alilolifanya miezi
kumi na mbili
iliyopita.Mathew alifanya siri
kubwa mahali alipo.Hakutaka
kujulikana alikwenda wapi
kwani alihitaji mapumziko
marefu na kujitafakari kuhusu
maisha yake.
TAMATI

NDUGU
MSOMAJI,AHSANTE
KWA KUIFUATILIA
SIMULIZI HII NDEFU YA
SIRI.TUNA UHAKIKA
UTAENDELEA
KUTUUNGA MKONO
KWA KUFUATILIA
SIMULIZI ZETU
NYINGINE
ZITAKAZOFUATA
BAADA YA KUMSOMA
MATHEW MULUMBI
KATIKA SIMULIZI
KADHAA JE
UMEMFAHAMU VIZURI
MATHEW NI MTU WA
NAMNA GANI?
KUMFAHAMU VYEMA
MATHEW NI MTU WA
NAMNA GANI USIKOSE
SIMULIZI INAYOFUATA
YA
SCANDAL(KASHFA)

Safi sana... Story nzuri sana...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom