Waandaaji wa sherehe kubwa ya Wakunyumba Traditional Party, MS Production chini ya mkurugenzi Lucy Francis Komba, wamesema bado wanahitaji wadhamini kutoka pande zote za nchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Lucy Komba amesema kuwa, baadhi ya makampuni yamejitokeza kudhamini hafla hiyo lakini bado wadhamini zaidi wanakaribishwa.
"Ee, katika kipindi hiki cha kuelekea hafla yetu ya Wakunyumba Traditional itakayofanyika Agosti 14 pale Makumbusho ya Taifa, bado tunahitaji wadhamini zaidi.
"Hatuwezi kusema wadhamini wametosha kwa sababu bado kuna mambo mengi ya kufanywa na wadhamini. Kwa hiyo tunakaribisha makampuni ya umma, makampuni binafsi, taasisi na hata watu binafsi kujitokeza kutuunga mkono," alisema Lucy Komba.
Lucy aliongeza kuwa, kuna madaraja matano ya udhamini ambapo kila mdhamini anaweza kujichagulia daraja analotaka.
Aliyataja madaraja hayo kuwa ni; Platinum Sponsor, Gold Sponsor, Silver Sponsor, Bronze Sponsor na Community Supporter.
Alisema madaraja yote hayo yana viwango tofauti vya udhamini huku Platinum ikiwa na kiwango cha kwanza na Community ikiwa na kiwango cha mwisho.
Amesema kwa mdhamini aliye tayari anaweza kuwasiliana waandaaji kwa kupitia namba ya simu ya mkononi; 0753 121 955.
Sherehe ya Wakunyumba Traditional Party imeandaliwa na Mwendo wa Saa Production na Ngoni By DNA chini ya Mkurugenzi Lucy Francis Komba ambaye pia ni staa wa Bongo Muvi.
Kwa mujibu wake Lucy, hafla hiyo ni endelevu kwani itakuwa ikifanyika kila mwaka katika maeneo yatakayotajwa na waandaaji katika mwaka husika.