Riwaya: Siri

Nimefika! It is better to be late, than never!
JamiiForums-600547178.jpg
 
SIRI
Episode 29

Mtunzi.Patrick CK

“Ngoja nikamuulize mama
yake yawezekana amewahi
kumueleza chochote kuhusiana
na tatizo lake” akasema Agrey
“Hakuna sababu ya
kumsumbua mama.Naamini
hajamweleza kwani kama
angekuwa anafahamu chochote
angekwisha kwambia” akasema
Mathewna ukimya mfupi
ukapita halafu Mathewakasema
“Mzee ninaomba nikueleze
jambo kubwa ambalo limenileta
hapa lakini naomba jambo hilo
libaki kati yetu”
“Nakusikia Mathew” “Mimi nimewahi kufanya
kazi katika idara ya ujasusi
lakini kwa sasa nimeachana na
shughuli hizo na ninaendelea na
biashara zangu lakini kuna
nyakati hulazimika kurejea tena
katika kazi yangu hiyo ya
zamani pale linapotokea jambo
ambalo linanilazimu niwepo
kulishughulikia.Mara nyingi
nimekuwa nikiombwa na
serikali kushughulikia masuala
Fulani pale penye ulazima na
siwezi kukataa kwani nina
mapenzi makubwa na nchi
yangu” akasema Mathew.Agrey Themba akamuangalia kwa
macho yaliyojaa mshangao
mkubwa
“Wewe ni
mpelelezi?akauliza Agrey
“Ndiyo.Nimewahi kuifanya
kazi hiyo lakini kwa sasa
ninafanya shughuli zangu
binafsi”akasema
MathewMulumbi
“Nimeshangaa sana
Mathewsikutegemea kabisa
bilionea kama wewe unaweza
kuwa mpelelezi” akasema Agrey
“Niliwahi kufanya kazi hiyo
zamani lakini kwa sasa nimekwisha achana nao
ninajishughulisha na biashara
zangu kama nilivyokueleza
awali.Mzee Themba,Olivia ni
rafiki yangu mkubwa na kwa
sababu yake nimeamua
kutumia ujuzi wangu nilio nao
katika masuala haya ya
uchunguzi kumtafuta na
kuhakikisha ninampata”
akasema Mathew
“Mathewahsante sana kwa
kujitolea kutumia ujuzi wako
kumtafuta mwanangu lakini
suala hili tayari liko katika
mikono ya jeshi la polisi na wanatumia kila nguvu
waliyonayo kuhakikisha
wanampata Olivia.Ninashauri
kama unalo jambo lolote
linaloweza kusaidia kupatikana
kwa Olivia liwasilishe kwa jeshi
la polisi walifanyie kazi kwani
wao wana nguvu kubwa na
mtandao mrefu.Hata hivyo
nakushukuru sana Mathewkwa
moyo wako wa kujitolea kwa
ajili ya Olivia”akasema Agrey
Themba
“Mzee,kwa uzoefu wangu
nimegundua watekaji hawa ni
watu waliojiandaa na hawajakurupuka.Wanafahamu
Olivia ni mwanao,wanafahamu
ukaribu wako na rais na
wanajua kabisa kwamba
kutokana na ukaribu huo nguvu
itakayotumika kumtafuta Olivia
ni kubwa hivyo wamejiandaa
vyema kukabiliana na nguvu
yoyote
itakayotumika.Ukifuatilia
namna walivyomchukua Olivia
ndipo utagundua kwamba watu
hawa si watu wa kufanyia
mzaha na operesheni hii
hawakukurupuka wamejipanga
vyema.Operesheni kama hizi hufanywa na watu wenye
utaalamu mkubwa hasa
majasusi pale wanapomuhitaji
mtu Fulani muhimu.Nimefanya
kazi katika idara ya ujasusi
nikiwa tegemeo hivyo mambo
kama haya ninayafahamu
vyema na ndiyo maana
nimejitolea kumtafuta Olivia
kwani nina uhakika mkubwa wa
kumpata kwa kuwa
ninazifahamu mbinu zote za
kijasusi”akasema Mathew.Agrey
akafikiri kwa muda na kusema
“Mathewmaneno yako
yanazidi kunipa woga kuhusu mwanangu kama huko aliko
atakuwa salama ninatamani
sana kukupa jukumu hili la
kumtafuta mwanangu lakini
tayari polisi wanaendelea na
uchunguzi na hatuwezi kuwa na
timu mbili za uchunguzi kwa
wakati mmoja.Polisi wana
mtandao mkubwa sana na
wanaweza wakampata Olivia
kwa haraka zaidi kuliko ukiwa
peke yako.Ushauri wangu
Mathewnitakuunganisha na
mkuu wa jeshi la polisi
uzungumze naye na kama kuna
kitu chochote ambacho unadhani kinaweza kusaidia
katika uchunguzi utawaeleza na
wao watakifanyia kazi.Kwa sasa
jeshi la polisi wanatafuta sana
taarifa zozote ambazo zinaweza
kusaidia kumpata Olivia wewe
unaweza kuwa mtu muhimu
sana kwao” akasema Agrey
“Mzee suala hili la la Olivia
ni pan asana na ninakuomba
usilichukulie krahisi.Hatuwezi
kuwaachia jeshi la polisi peke
yao na ndiyo maana nimeamua
kusaidia uchunguzi kwa
kutumia uzoefu nilio nao lakini kwa mbinu zangu ninazozijua”
akasema Mathew
“Mathewnimekuelewa sana
kijana wangu lakini hofu yangu
ni kwamba nikikuruhusu
ufanye uchunguzi wako peke
yako unaweza ukaingiliana na
jeshi la polisi na kumuweka
Olivia katika hatari zaidi ndiyo
maana nikashauri kwamba
uungane na jeshi la polisi au
kama una taarifa zenye msaada
basi wape polisi.Binafsi bado
nina imani kubwa na jeshi la
polisi kwamba watampata
Olivia ndani ya muda mfupi kwani nguvu waliyoanza nayo
ni kubwa” akasema
Agrey.Mathewakamtazama
Agrey na kusema
“Olivia ametekwa saa tano
asubuhi,tayari giza limeingia na
hakuna taarifa yoyote yenye
kutia matumaini kuhusu mahala
aliko Olivia.Mzee nafahamu
juhudi kubwa zinafanyika
kumtafuta Olivia lakini bado
haitoshi.Nguvu zaidi inahitajika
na ninaomba ridhaa yenu ili na
mimi nitoe msaada wangu”
akasema Mathew “Mathewbado imani yangu
ni kubwa kwa jeshi la polisi
kwamba watampata
Olivia.Wamekwisha jipanga
vyema kabisa na kwa mipango
yao namna walivyonieleza
wanakwenda vizuri.Kupitia
tukio hili la Olivia jeshi la polisi
wanataka kuchimba hadi mzizi
wa mtandao huu wa watekaji
hapa nchini na kuusafisha
kabisa.Mathewnadhani hatuna
cha kuzungumza zaidi nina
wageni wananisubiri
ndani.Kama utakuwa tayari
kushirikiana na jeshi la polisi basi utanijulisha ili
nikuunganishe na viongozi wa
polisi” akasema Agrey Themba
na kumpa mkono
Mathewakimuaga
“Mzee ni vipi nikikueleza
kwamba tayari ninafahamu
mahala alipo Olivia? akauliza
Mathew
“What?!! Agrey akapatwa
na mstuko mkubwa.
“Mzee nisikilize vizuri”
akasema Mathewhuku Agrey
akimtazama kwa macho yenye
woga “Baada ya Olivia
kunidokeza kwamba ana
matatizo na watu fulani
niliingiwa hofu kuhusu maisha
yake na nilichokifanya nilimpa
namba Fulani nikamtaka
azipige namba hizo pindi
anapokuwa katika
matatizo.Namba hizo ni za
program maalum ambayo
ninaitumia kwa ajili ya usalama
wa familia yangu.Nikiwa
mkutanoni Arusha nilipata
ujumbe ukinijulisha kuwa
namba ile imepigwa nikatazama
ni nani amepiga nikagundua ni Olivia.Programu ikanionyesha
hadi mahala ambapo namba
hiyo ilipigwa na ninaamini
ndipo alipo Olivia”akasema
Mathew
“Jesus Christ !! akasema
Agrey.Mathewakamtaka
waelekee katika gari lake
akachukua kompyuta na
kumuonyesha Agrey
“Namba zile nilizompa
Olivia zilipigwa hapa kwenye
huu mduara mwekundu
ambako ramani hii
inatuonyesha kwamba ni
sehemu fulani Kigamboni”akasema
Mathew.Agrey akaitazama
ramani ile kwa makini huku
midomo ikimtetemeka
“Ma.mma…Mathewunachok
isema ni cha kweli?akauliza
“Ndiyo mzee ni kitu cha
kweli kabisa.Nimerejea kutoka
Arusha kwa sababu nina
uhakika wa kumpata
Olivia.Ninayo sehemu ya
kuanzia kumtafuta Olivia.Kabla
sijaenda mahala hapo niliona ni
vyema nikafika kwanza hapa
kuzungumza nanyi na
kuwaeleza mipango yangu kuhusiana na kumpata
Olivia.Mzee ninaomba
mniruhusu nikamtafute
Olivia.Ninawaahidi ninao uwezo
mkubwa wa kumpata kwa
haraka” akasema Mathew
“Nadhani mama yake naye
anatakiwa kulifahamu suala
hili” akasema Agrey na
kumpigia simu mke wake
akamtaka awafuate pale
bustanini ambaye alifika mara
moja.
“Lucy utatusamehe tulitoka
nje kuna suala nyeti sana
tulikuwa tunazungumza.Mathewameniel
eza jambo zito sana” akasema
Agrey
“Ni jambo gani?akauliza
Lucy
“Mathewhebu mueleze mke
wangu naye asikie”akasema
Agrey,Mathewakamueleza kila
kitu alichomueleza Agrey,Lucy
akaanza kumwaga machozi
“Lucy usilie
tafadhali.Nimekuita hapa ili
tushirikiane katika kutoa
maamuzi nini
kifanyike.Mathewamenieleza
historia yake amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na
ameomba atusaidie katika
kumtafuta Olivia.Nilisita
kumruhusu afanye hivyo kwa
kuwa tayari jeshi la polisi
wanalishughulia hili suala hivyo
nikaogopa kusitokee mgongano
katika uchunguzi” akasema
Agrey
“Agrey are you out of your
mind? Mtoto wetu ametekwa na
watu wasiojulikana na hatujui
mpaka sasa hivi yuko
wapi.Amekuja mtu mwenye
taarifa nyeti kama hii ambayo
inaweza ikasaidia kumpata mwanetu halafu hutaki kumpa
ushirikiano!! Akafoka Lucy
“Lucy si kwamba sitaki
kumpa ushirikiano ninaogopa
kuleta mgongano kwani tayari
jeshi la polisi wanalishughulikia
suala hili.Nimekuita hapa ili
tujadiliane tuone nini cha
kufanya” akasema Agrey
“Agrey hupaswi kuweka
mjadala katika suala hili.Kwa
hapa tulipofika tunahitaji
msaada wa kila aina kumpata
Olivia.Hata kama jeshi la polisi
wanaendelea na uchunguzi
bado haizuii na sisi kuendelea na jitihada nyingine za
kumtafuta Olivia.Hatuwezi
kukaa na kulitegemea jeshi la
polisi peke yake.We need to do
something! Mungu amemleta
huyu kijana ambaye ameacha
shughuli zake zote na kuamua
kutusaidia kumtafuta
Olivia,lazima tumpe ushirikiano
mkubwa” akasema Lucy
“Mathewtunakusikiliza
wewe una ushauri
gani?akauliza Agrey
“Kilichonileta hapa
kuzungumza nanyi ni kuomba
mnipe ruhusa ya kumtafuta Olivia.Nina uhakika mkubwa
nitampata.Ninao uzoefu
mkubwa sana katika masuala
haya ndiyo maana nina uhakika
wa kumpata Olivia na tayari
ninayosehemu ya
kuanzia.Naombeni wazee
wangu mnikubalie niweze
kumtafuta Olivia.Ninakuondoa
hofu mzee wangu kwamba
uchunguzi wangu hautaweza
kuleta mgongano wowote au
kuingilia uchunguzi wa jeshi la
polisi.Ningeweza kufanya
uchunguzi huu kimya kimya
bila kumtaarifu mtu yeyote lakini nimeona haitakuwa
vyema kufanya hivyo bila
kupata Baraka zenu.Nafahamu
si jambo jepesi,ni jambo la
hatari sana lakini niko tayari
kulifanya na nitahakikisha
Olivia anapatikana” akasema
Mathew
“Mathewninatamani sana
kusema nenda kamtafute Olivia
lakini ninasita kukutuma uende
huko peke yako
Mathew.Nashauri taarifa hii
tuwape jeshi la polisi
wakaifanyie kazi,wao wana nguvu kubwa kuliko ukiwa
peke yako”akasema Agrey
“Mzee laiti ungenifahamu
hata kidogo usingekuwa na
hofu nami.Ninapoamua kuingia
katika kazi hizi siogopi
kitu.Hata hao waliomteka Olivia
kama wananifahamu na
wakasikia kwamba
MathewMulumbi anajiandaa
kumsaka Olivia mioyo yao
itabadili mapigo wataingiwa na
hofu kubwa kwa sababu
wanajua ziraili ameanza kazi
yake.Siogopi chochote mzee
wangu kwa ajili ya Olivia.Ninaomba mnipe ruhusa
niende nikaanze kazi usiku huu”
akasema Mathew
“Mathewhakuna mjadala
katika suala hili.Tunahitaji sana
msaada wako kumtafuta
Olivia.Ninakupa Baraka zote
kijana wangu nenda kamtafute
Olivia.Tumia kila aina ya uwezo
ulio nao kuhakikisha unasaidia
kumpata mwanangu” akasema
Lucy Themba mama yake
Olivia.Agrey Themba alitaka
kusema kitu mke wake
akamzuia “Agrey nimekwisha toa
Baraka zangu Mathewakasaidie
kumtafuta Olivia sitaki maelezo
zaidi.Mathewunaweza kwenda
baba kama kuna tatizo lolote
utalipata chukua namba yangu
hii ya simu utawasiliana
nami.Mimi ndiye nina uchungu
mkubwa kwa mwanangu
kupotea hivyo siwezi kukataa
msaada wako Mathew”
akasema Lucy Themba na
kumpatia Mathewnamba zake
za simu
“Mzee ninaondoka
tutaendelea kuwasiliana.Kila nitakachokipata nitawasiliana
nanyi” akasema Mathewna
kupiga hatua ndefu hadi katika
gari lake akaondoka
“Lucy sijafurahishywa na
hiki ulichokifanya” akasema
Agrey baada ya
Mathewkuondoka
“Sihitaji mjadala wowote
katika suala hili Agrey na kama
umechukia mimi sijali kwani
ninachohitaji ni mwanangu
apatikane.Kijana amekuja na
anazo taarifa zinazoweza
kusaidia kupatikana kwa Olivia
kwa nini tusimpe nafasi ya kusaidia na isitoshe ni
mpelelezi anazo mbinu nyingi
za kuweza kusaidia kumpata
Olivia.Kwa nini unakuwa na
wasi wasi katika suala
hili?Nashindwa kukuelewa
Agrey” akasema Lucy
“Lucy wote tuna uchungu
mkubwa kwa tukio la leo lakini
tunapaswa tuwe makini sana
katika hatua tunazozichukua
kwani nyingine zinaweza
kusababisha madhara badala ya
kuwa msaada kwetu.Jeshi la
polisi hivi sasa wako kazini
wakimtafuta Olivia.Wanakwamba lazima mwanao
atapatikana.Msihi pia Lucy
asiwe na wasi wasi,jeshi la
polisi wako kazini na
wanaendelea kufanya kila
waliwezalo kuhakikisha
kwamba wanampata
Olivia.Mimi bado siamini kama
jeshi la polisi wanaweza
wakashindwa kumpata
Olivia.Mtandao wao ni mkubwa
sana na nguvu kubwa kwa sasa
wameielekeza katika suala hili
hivyo ninawatoa wasiwasi
kwamba Olivia lazima
atapatikana.Tuendelee kushikamana.Kama mtapata
taarifa zozote zinazoweza
kusaidia katika uchunguzi huu
tuzifikishe haraka kwa jeshi la
polisi ili zifanyiwe
kazi”akasema Dr Evans
“Nimekuelewa Evans na
ninakushukuru sana kwa
kuweka uzito mkubwa katika
suala hili.Nina imani kubwa na
jeshi la polisi chini ya
maelekezo yako kwamba Olivia
atapatikana” akasema Agrey
“Agrey nitaendelea
kuwasiliana nawe na
kukujulisha kila nitakachokuwa ninakipata kutoka kwa jeshi la
polisi” akasema Dr Evans
wakaagana
“Agrey amenistua sana.Hili
suala la Olivia litanipasua moyo
wangu” akawaza Dr Evans na
kuweka mkono kifuani mahala
unakokaa moyo.Mapigo ya
moyo wake yalibadilika na
kwenda kwa kasi kubwa.
“Siri imegundulika”
akawaza
“Yote ambayo huyo
Mathewamemueleza Agrey ni
ya kweli kabisa.Ni kweli Olivia
yuko kitalu 7 Kigamboni.Maelezo
niliyoyapata kutoka kwa
Devotha ni kwamba walimtaka
Olivia awape namba za Sayid
Omar ambaye amekuwa
akiwasiliana naye mara kwa
mara na akawapa namba zile
ambazo walipozipiga mfumo
wote ukajifunga.Kompyuta zote
zikazima na hakuna
kilichoendelea hadi sasa.Kumbe
namba zile Olivia alipewa na
Mathew.Who is this
MathewMulumbi?akajiuliza Dr
Evans “Kwa kuwa tayari
amekwisha fahamu mahala
alipo Olivia hatua za haraka
sana zinatakiwa kuchukuliwa
ama sivyo mpango wetu
utaharibika.Kwanza kabisa
Olivia anatakiwa aondolewe
haraka sana mahala pale na
jambo la pili ni kuhakikisha
kwamba huyo
Mathewanapatikana kwa
sababu tayari ni mtu hatari
kwetu.Hiki ni kirusi hatari
ambacho kinatakiwa
kudhibitiwa haraka mno”
akawaza Dr Evans na kuzitafuta namba za simu za Devotha
Adolph akampigia
“Mr president” akasema
Devotha
“Devotha uko wapi?
“Niko hapa kitalu 7
mheshimiwa rais”
“Devotha we have a big
problem”akasema DrEvans
“Tatizo gani mheshimiwa
rais?
“Nitakueleza lakini kwa
sasa kuna mambo nataka
ufanye kwa haraka.Kwanza
kabisa nataka Twiga atolewe
kitalu 7 na apelekwe kitalu 2 ambako ni salama
zaidi”akasema Dr Evans
“Kuna tatizo gani
mheshimiwa rais?Kwa nini
tumuhamishe?akauliza Devotha
“Nisikilize Devotha na
utekeleze kile
ninachokuagiza.Hakikisha sasa
hivi Twiga anaondolewa hapo
kitalu 7 na kupelekwa kitalu
2.Peleka timu P3 unit hapo
kitalu 7 wakalinde na
wahakikishe kwamba hakuna
mtu yeyote anayeingia mle
ndani.Yeyote atakayekaribia
eneo hilo akamatwe haraka sana.Nataka kila kitu
kiondolewe hapo kitalu 7 na
nyumba ibaki tupu.Tekeleza
hayo yote haraka
sana.Nitaonana nawe usiku huu
kukueleza kuna nini
kinaendelea”akasema Dr Evans
na kukata simu
“Natakiwa kuonana na
daktari wangu naona
mabadiliko makubwa ya
kiafya.Hili suala la Olivia
limeniletea matatizo makubwa”
akawaza Dr Evans na jina la
Mathewlikamjia kichwani
“Who is this guy !! Is he real
or a ghost? Huyu amekuja
kuharibu kila kitu na anatakiwa
adhibitiwe haraka sana kabla
hajaharibu kila kitu.Kwa
maelezo aliyonipa Agrey
inaonekana Mathewanafahamu
alipo Olivia lakini hajui
anashikiliwa na akina nani
ndiyo maana anataka
kuchunguza.Naomba iwe hivyo
asifahamu chochote” akawaza
Dr Evans na kuchukua simu
akazitafuta namba za
mkurugenzi wa idara ya ujasusi
akampigia “Mheshimiwa rais”akasema
mkurugenzi wa idara ya ujasusi
baada ya kupokea simu ya rais
“Jacob habari za usiku huu”
“Nzuri kabisa mheshimiwa
rais”
“Jacob nahitaji
msaada.Nataka upitie katika
kumbu kumbu za watu
waliowahi kufanya kazi katika
idara yako na angalia kama
kuna mtu anaitwa
MathewMulumbi” akasema Dr
Evans “Sawa mheshimiwa
rais.Unahitaji jibu kwa usiku
huu?
“Now ! akasema Dr Evans
kwa saui ya juu
“I need the answer now!!
Akasisitiza
“Naomba dakika chache
mheshimiwa rais” akasema
Jacob silele mkurugenzi wa
idara ya ujasusi
Baada ya dakika tatu Jacob
akapiga simu
“Niambie Jacob”
“Mheshimiwa rais
nimezipata taarifa hizo.Ni kweli kuna mtu aliwahi kufanya kazi
katika idara yetu ya ujasusi
anaitwa MathewMulumbi”
akasema Jacob.Dr Evans
akashusha pumzi akatafakari
kwa sekunde chache na kusema
“Nataka unitumie faili lenye
taarifa zake sasa hivi katika
barua pepe yangu sasa hivi”
akasema Dr Evans
“Sawa mheshimiwa
rais”akasema Jacob
“Damn ! akasema Dr Evans
kwa hasira.Tayari walikwisha
ingia ikulu gari likasimama
akashuka haraka haraka na kuelekea ndani moja kwa moja
katika ofisi yake ndogo
akawasha kompyuta yake na
kuanza kulipitia faili
alilotumiwa lenye taarifa za
MathewMulumbi.Kadiri
alivyoendelea kusoma taarifa za
MathewMulumbi ndivyo
alivyoendelea kuhisi
baridi.Alimaliza kulipitia faili
lile akajiegemeza kitini.Kichwa
kilibeba mzigo wa mawazo.
“MathewMulumbi !!
akasema
“Taarifa zake zinatisha.Ni
mmoja kati ya majasusi mahiri kabisa kuwahi kutokea nchini
mwetu.Nimepitia misheni zote
alizozifanya na zote
amezikamilisha vyema kwa
umahiri mkubwa sana.Mambo
yaliyomo katika faili hili ni
mazito kabisa” akawaza Dr
Evans
“Imeibuka vita mpya.Huyu
mtu aliyejitokeza naweza
kusema ni jeshi la mtu mmoja
kutokana na uwezo wake
mkubwa.Tunatakiwa
kupambana naye kwa umakini
mkubwa sana kwani huyu
jamaa amekusudia kumtafuta Olivia na anaweza akampata
kutokana na uwezo mkubwa
alio nao” akawaza Dr Evans na
kumpigia simu Devotha
“Devotha zoezi
linakwendaje?akauliza
“Kwa sasa tunamuondoa
Twiga hapa kitalu 7 kuelekea
kitalu 2 na tayari timu P3 Unit
wako njiani wanakuja hapa
kuimarisha ulinzi kama
ulivyoelekeza” akasema
Devotha
“Good.Naomba baada ya
kutoka kitalu 2 njoo hapa ikulu
moja kwa moja kuna masuala muhimu sana ya kuzungumza”
akasema Dr Evans na kukata
simu
“Hili suala la Olivia linazidi
kuwa kubwa.Kabla hatujapata
majibu kutoka kwa Olivia
kuhusiana na ukaribu wake na
kikundi cha IS ambao ameibuka
MathewMulumbi ambaye ni
tatizo kubwa
pia.Mathewamedhamiria
kumkomboa Olivia kutoka
katika mikono ya watekaji na
tayari anafahamu mahala
alipo.Je anafahamu kama ni
serikali ndio tunaomshikilia Olivia?Anafahamu kama Olivia
ana ukaribu na watu wa IS?
Naye pia ni mmoja wao? Dr
Evans akajiuliza maswali
“Nashukuru kwa Agrey
kunipa taarifa mapema
kuhusiana na Mathewna baada
ya kufahamu uwepo wake
kinachofuata sasa ni
kupambana naye.Hatampata
Olivia tena kwani mahala
alikopelekwa si rahisi
kupafikia.Wakati tukiendelea na
suala la Olivia tutaendelea pia
kushughulika naye.Tutaelekeza
nguvu kubwa kumsaka na kuhakikisha
anapatikana.Hawezi kunishinda
mtu mmoja” akawaza Dr Evans.
 
Mtunzi.Patrick CK

Season 1.SIRI

Simu.0764294499

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Ndege ilisimama mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kushuka.

Mtu mmoja ambaye mavazi yake yalionyesha ni mfanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni alikuwa amejibanza mahala Fulani akiwa ameyaelekeza macho yake katika ndege ile akatoa simu na kupiga “Mlango umefunguliwa na abiria wameanza kushuka Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ndege ilisimama mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kushuka. Mtu mmoja ambaye mavazi yake yalionyesha ni mfanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni alikuwa amejibanza mahala Fulani akiwa ameyaelekeza macho yake katika ndege ile akatoa simu na kupiga “Mlango umefunguliwa na abiria wameanza kushuka”

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Ndege ilisimama mlango ukafunguliwa naabiria wakaanza kushuka.

.Mtu mmoja ambaye mavazi yake yalionyesha ni mfanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni alikuwa amejibanza mahala Fulani akiwa ameyaelekeza macho yake katika ndege ile akatoa simu na kupiga “Mlango umefunguliwa na abiria wameanza kushuka” “Sijakosea ni mwenyewe” akawaza na kupiga simu “Ameshuka ndegeni.

Amevaa suruali ya jeans ya bluu, fulana nyeupe,miwani myeusi ya jua” akasema yule jamaa “Una hakika ni yeye?akauliza jamaa wa upande wa pili wa simu “Ninamuona kwa mbali lakini nina uhakika ni yeye” “C’mon Denis.Get closer to her and confirm it’s her !!

Akasema kwa ukali jamaa aliyekuwa anazungumza na Denis simuni.Haraka haraka Denis akaanza kusogea kuwafuata abiria waliokuwa wanashuka lengo likiwa ni kumkaribia mrembo yule.

Hakuna aliyemtilia shaka kwani alikuwa ni mfanyakazi wa mle uwanjani.Alijitahidi sana na kumsogelea mrembo yule ambayealikuwa amevaa spika za masikioni na hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote. “Confirmed.Ni yeye” Denisakatoa taarifa

“Good job Denis.Malipo yako yatakuja baadae” akasema yule jamaa upande wa pili wa simu na kukata simu. Msichana yule mrembo aliingia ndani ya jengo la uwanja na kukamilisha taratibu zote halafu akatoka akiwa na mkoba mweupe na sanduku dogo la chuma alilokuwa analikokota.Katika sehemu ya kusubiria wageni watu watatu walikuwa
wanamsubiri.

Wote walikuwa wamevaa suti nzuri zilizowapendeza,wakasalimiana kisha mmoja wao akalibeba sanduku la yule mrembo wakaelekea garini. “Anaelekea garini,yuko na walinzi wake” jamaa mmoja aliyekuwa katika sehemu ya kupokelea wageni akawasiliana na wenzake

“Wako walinzi wangapi?akaulizwa “Ana walinzi watatu”akajibu "Good.Kila kitu kiende kama kilivyopangwa” akasema jamaa aliyeonekana ndiye mkubwa wa wale jamaa waliokuwa wakimfuatilia yule mrembo Msichana yule mrembo akaelekea katika gari moja zuri jeusi aina ya Landcruiser V8 akafunguliwa mlango akaingia pamoja na mlinzi mmoja.

Wengine wawili wakaingia katika gari la nyuma yake kisha wakaondoka pale uwanjani. “She’s on move” Jamaa
mwingine aliyekuwa katika gari lililokuwa pale uwanjani akatoa taarifa kisha akawasha gari wakaondoka wakaanza kulifu lile gari alilopanda yule msichana.Jamaa walikuwa wamejipnga kwa kuweka watu katika barabara kadhaa kwa ajili ya kumfuatilia yule msichana lengo kwa kupokezana ili asiweze kugundua kama anafuatiliwa.

Walitumia magari tofauti tofauti ili wasigundulike Gari la yule msichana liliingia barabara ya Msanda ambayo inaelekea pembezoni mwa jiji “Ameingia barabara ya Msanda nadhani anaelekea nyumbani kwake” akasema jamaa aliyekuwa katika gari lililoshika zamu ya kumfuatilia.Wale jamaa walikuwa sahihi kwani msichana yule alikuwa anaeleka nyumbani kwake katika makazi mapya ya Urangi.

Ni eneo tulivu nje kidogo ya jiji ambalo limejengwa majumba ya kifahari sana. Barabara ilikuwa na magari
machache hivyo mwendo wa gari ulikuwa mkali.Gari zile mbili za yule msichana ziliacha barabara kuu na kufuata barabara ya changarawe lakini iliyojengwa vizuri sana, gari zile ambazo zilikuwa zinamfuatilia hazikumfuata tena bali zikaegesha pembeni ya barabara kusubiri maelekezo Mita kama mia tano kabla ya kulifikia jumba lake ikatokea helkopta yenye rangi nyeupe ambayo ilikuwa inapita chini sana.

Helkopta ile ilipofika usawa wa nyumba ya yule mrembo ikageukia barabarani ambako magari mawili ambalo moja wapo amepanda yule msichana yalikuwa yamepunguza mwendo kwani yalikaribia kufika katika jumba kubwa la yule msichana.Kitendo cha helkopta ile kupita chini sana na vile vile kusimama katika jumba lile kiliwashangaza walinzi wa yule mrembo.

“Something is not right.Olivia get down!! Akasema mlinzi aliyekuwa garini na yule msichana kisha akatoa bastora yake.Mlango wa helkopta ukafunguliwa na jamaa mmoja aliyekuwa na bunduki kubwa akajitokeza na kwa kasi ya aina yake akaanza kumimina risasi kuelekea katika yale magari ambayo yalibakiza mita chache sana kufika nyumbani na tayari geti lilikwisha funguliwa.

Dereva wa gari la mbele alilopanda yule msichana mrembo akapigwa risasi ya kichwa na gari lile likapoteza uelekeo na kwenda kugonga ukuta.Mvua ya risasi ikaendelea kunyeshea gari lililokuwa nyuma ambalo lilikwenda kuligonga kwa nyuma gari la mbele alimokuwa amepanda yule msichana mrembo aliyekuwa amelala chini ya kiti.Watu wote waliokuwa katika gari lile la nyuma walikuwa wameuawa na ile mvua ya risasi toka kwa mtu aliyekuwa katika mlango wa helkopta.

Mlinzi mmoja tu aliyebaki alifungua mlango na kutaka kutoka nje ili kukabiliana na watu wale katika helkopta lakini hakufanya chochote kwani alijikuta akichakazwa kwa risasi akaanguka na kufa pale pale. Kwa kasi kubwa zikafika gari mbili ,wakashuka watu sita,waliokuwa na silaha wakiwa wamefunika nyuso zao na kujihami kwa fulana za kujikinga kwa risasi.

Haraka haraka wakaenda katika gari na kumtoa msichana yule mrembo wakamuingiza katika gari lao,likachukuliwa pia sanduku lake pamoja na mkoba mdogo aliokuwa nao kisha magari yale mawili yakaondoka kwa kasi kubwa.Helkopta nayo ambayo bado ilikuwa pale juu ikapaa na kutoweka.

“We have giraffe..I repeat we have giraffe” jamaa mmoja aliyekuwa katika gari moja kati ya zile mbili akawajulisha wenzake “Good job.Kila kitu kiende kama kilivyopangwa” akatoa maelekezo“Sawa mkuu”akajibu yule jamaa. Gari zile zilikwenda kwa mwendo wa kasi na baada ya kufika katika mzunguko wa picha ya kiboko,zikaachana kila moja ikafuata njia yake.

Moja ikafuata barabara ya umoja wa Afrika na nyingine ikafuata barabara ya Kannani.Gari zote mbili zilikuwa na namba zinazofanana ili kuwachanganya wale watakaozifuatilia.Gari ile iliyopita barabara ya Kannani ndiyo ambayo msichana yule mrembo alikuwemo,ilielekea moja kwa moja hadi katika nyuma moja maeneo ya vigenge likafunguliwa geti likaingia ndani.

Haraka haraka msichana yule akashushwa garini akafungwa mikono na miguu akaingizwa katika buti ya gari lingine aina ya mercedece benzi na gari lile likatoka bila kupoteza muda.Lile gari lingine lililokuwa limembeba mwanzo likafunguliwa namba zile za bandia na kufungwa namba zake halisi kisha nalo likatoka.

Gari lile aina ya Mercedece Benz lililokuwa na watu watatu ndani yake,lilikwenda hadi katika jumba moja kubwa likafunguliwa geti na kuingia ndani hadi gereji.Wale jamaa wakashuka garini,buti likafunguliwa yule msichana mrembo akashushwa akaingizwa ndani ya lile jumba akapelekwa katika chumba kimoja akawekwa kitandani.Bado mikono na miguu ilikuwa imefungwa pia usoni alikuwa amefungwa kitambaa hakuweza kuona chochote na mdomoni aliwekewa kitu cha kumzuia kupiga kelele.

Mlango ukafungwa wale jamaa wakatoka. Dakika chache baadae gari mbili zikawasili na kutoka katika gari la nyuma akashuka jamaa mmoja mnene. “Mr Kaiza kazi imemalizika na Dr Olivia yuko ndani tayari”akasema mmoja wa wale jamaa waliofanikisha kumteka Olivia “Kazi nzuri sana Godson” akasema Kaiza

“Huu hapa mkoba wake ndani yake kuna mkufu,simu na vifaa vidogo vidogo” akasema Godson na kumkabidhi Kaiza vile vifaa
******************

Taarifa za tukio la kutekwa kwa Dr Olivia Themba mtoto wa bilionea Agrey Themba zilianza kusambaa kwa kasiya upepo kwani ni mtu ambaye anafahamika sana.Kwanza ni kutokana na shughuli anayoifanya ya udaktari na utafiti wa magonjwa mbali mbali na vile vile kuwa mtoto wa bilionea Agrey Themba. Dr Olivia Themba ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto watano wa mabilionea Agrey na Lucy Themba.

Baada ya kuhitimu masomo yake ya udaktari alirejea nchini na kufanya kazi katika hospotali kuu ya magonjwa ya moyo kabla ya kuanzisha kituo chake cha utafiti wa magonjwa mbalimbali ya binadamu na wanyama.Kupitia kituo hicho kikubwa cha utafiti katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wamefanikiwa kupata tiba ya magonjwa mbali mbali ya wanadamu na wanyama waliyoyafanyia utafiti.

Ni kituo ambacho kimekuwa na mafanikio makubwa na hata seriali wamekuwa wakikitegemea sana
kituo hiki katika tafiti mbali mbali za magonjwa ya binadamu na wanyama. Agrey Themba alipokea taarifa za kutekwa mwanae OIivia akiwa katika kikao muhimu cha kibiashara ikamlazimu kutoka kikaoni haraka sana na kumtaka dereva amuwahishe nyumbani kwa mwanae kujua kilichotokea na kuthibitisha kama taarifa zile ni za kweli.

“Ee Mungu kama kweli mwanangu ametekwa nyara,mlinde dhidi ya mikono ya watu hao waovu ambao hatujui wana lengo gani naye” Agrey akaomba akiwa garini.Alikuwa na wasi wasi mwingi “Nani hawa ambao wamethubutu kumteka mwanangu?Wanataka nini?

Akajiuliza Agrey aliyeonekana kuchanganyikiwa huku simu zake zikiendelea kuita mfululizo lakini alihisi mikono mizito hata kupokea simu “Ninawaza sana lakini mpaka sasa bado sijapata jibu nini hasa ambacho hawa jamaa wanakitaka hadi wamteke mwanangu.Je wamemteka ili wadai malipo ya fedha? Mbona hawajapiga simu kudai chochote mpaka
sasa? Akaendelea kujiuliza Agrey.

Simu aliyoamua kuipokea ni simu ya mke wake Lucy Themba ambaye alitaka kujua kama taarifa zile ni za kweli.Agrey alimueleza kuwa yuko njiani akielekea eneo la tukio kuthibitisha kama ni kweli mwanae ametekwa nyara.Mke wake naye alipanda gari haraka haraka akaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mwanae.

Agrey alifika nyumbani kwa Olivia na kitu cha kwanza kilichomthibitishia kwamba taarifa zile ni za kweli ni uwepo wa magari ya polisi pamoja na askari polisi kadhaa wenye silaha wakilinda eneo lile.Eneo lote la nyumba ya Dr Olivia lilizungushiwa utepe wa njano kulifunga eneo lile na kuzuia watu wasiingie wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wao.

Agrey alishuka garini akapokewa na kamanda wa polisi wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na kikosi cha askari waliofika haraka sana eneo la tukio baada tu ya kupewa taarifa za tukio lile.Kamanda Sospeter Mwarabu akamjulisha Agrey kwamba taarifa zile za kutekwa kwa mwanae ni za kweli,akampeleka kumuonyesha gari alimokuwa amepanda Dr Olivia.Miili ya walinzi wa Olivia ilitolewa na kupelekwa hospitali kuhifadhiwa.

Askari polisi walikuwa wamezagaa kila kona ya nyumba ile wengine walikuwa ndani ya nyumba wengine shambani wote wakichunguza tukio lile.Agrey alichanganyikiwa baada ya kuona namna damu ilivyotapakaa ndani ya magari. “Kamanda Mwarabu una uhakika mwanangu ni mzima?akauliza Agrey kwa wasi wasi “Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa mlinzi wa getini ambaye wakati tukio linatokea alikuwa amejificha mwanao alichukuliwa ndani ya gari akiwa mzima na kuingizwa katika gari la watekaji.

Inaonekana hao jamaa lengo lao lilikuwa ni kumpata Olivia ndiyo maana wakawaua walinzi wake wote lakini yeye hawakumgusa.Ni watu wataalamu sana na mpango huu waliupanga kimakini mno” akasema kamanda wa polisi aliyekuwepo eneo la tukio. “My God please help my daughter !! akasema Agrey huku macho yake yakilengwa na machozi.Muda huo huo Lucy Themba mama yake Olivia naye aliwasili eneo la tukio na kushuka garini haraka haraka huku akifuta machozi akamfuata mumewe.

“Agrey tell me it’s not true! Akasema Lucy “Calm down my love.Tum…..” Kabla Agrey hajamaliza mke wake akaangua kilio kikubwa. “Lucy nyamaza kulia.We have to be strong for our daughter” akasema Agrey na kumnyamazisha mke wake. “Agrey please find my daughter!! Fanya kila uwezalo na hakikisha unampata Olivia.Nitakufa kama Olivia hatapatikana!! Akalia Lucy

“Lucy usihofu.Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba Olivia anapatikana.Polisi wanafanya kila wanaloweza kuhakikisha Olivia anapatikana haraka sana”akasema Agrey “Hao watekaji kama wanataka pesa wapatie kiasi chochote cha pesa wakitakacho ili mradi mwanangu awe salama” akasema Lucy kwa sauti ya chini “Ninaamini hao watekaji shida yao ni pesa hivyo lazima watapiga simu na kudai kiasi kikubwa cha fedha ili waweze kumuachia Olivcia.

Ninakuahidi Lucy kama wakipiga simu na kudai pesa nitawapa kiasi chochote wakitakacho ili wamuache huru binti yetu” akasema Agrey na kamanda wa polisi akawasogelea na kumpa pole Lucy “Kamanda kuna chochote mmekipata hadi sasa kinachoweza kupelekea kuwafahamu hao watekaji ni akina nani?akauliza Agrey

“Mpaka sasa bado ila tunaendelea na uchunguzi na kila pale tutakapopata chochote tutakuwa tunawajulisha.Kwa sasa ninawahitaji tuzungumze kidogo” akasema kamanda Mwarabu wakaelekea ndani sebuleni. “Bwana na bi Themba napenda kuwajulisha kwamba jeshi la polisi tulipokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Dr Olivia aliyetujulishja kuhusu tukio lililotokea na tukafika hapa ndani ya muda mfupi sana lakini tayari watekaji walikwisha mchukua Dr Olivia na kutoweka.

Tumeambiwa kwamba watekaji walikuwa na helkopta na mtu aliyekuwa na bunduki ambaye alikuwa anarusha risasi kutokea ndani ya helkopta na baadae yakatokea magari mawili na watu wakashuka wakiwa na silaha na kumchukua Dr Olivia.Tayari tunawashikilia watumishi wote wa ndani pamoja na mlinzi aliyekuwepo getini kwa mahojiano,tunafuatilia vile vile picha za kamera za ulinzi kwani jumba hili la Dr OIivia kuna kamera nne.

Ninawahakikishia kwamba tunafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba mwanenu anapatikana haraka tena akiwa hai. Ninachoomba ni ushirikiano wenu mkubwa.Bado hatujui lengo la watekaji hawa ni nini, lakini kuna mambo mengi yanayoweza kupelekea wakamteka Dr Olivia.

Yawezekana watekaji wanahitaji fedha,yawezekana ikawa ni visasi,na yawezekana ikawa hata ni wivu wa kimapenzi. Sababu ziko nyingi na tunajaribu kuangalia sababu inayoweza kupelekea Dr Olivia akatekwa.Katika hili tunahitaji sana msaada wenu.Ninyi ni wazazi wake na mwanenu mnamfahamu vyema, nataka kufahamu kutoka kwenu kuhusu maisha yake kwa ujumla”akasema Kamanda Mwarabu Agrey akavuta pumzi ndefu na kusema

“Olivia ni mtu anayependa kuishi maisha ya kawaida sana.Hata baada ya kumaliza masomo yake ya udaktari na kuanza kazi bado tulikuwa tukiishi naye nyumbani kwetu.Ni binti wa pekee kwetu na hatukuwa tayari kumuacha akaishi peke yake lakini alituomba kwamba tayari amekwisha kuwa mtu mzima na anahitaji kuanza maisha yake mwenyewe ndipo tulipomruhusu akaja kuishi hapa katika nyumba hii.

Olivia ni mpole na sina hakika kama ana maadui wowote.Aliamua kusomea udaktari ili awasaidie watu kwani ni kitu alichokipenda toka akiwa mtoto mdogo.Amekuwa anaifanya kazi yake ya udaktari kwa moyo na upendo mkubwa ndiyo maana akawa ni mmoja wa madaktari maarufu hapa nchini”akasema Agrey “Mara ya mwisho kuwasiliana naye ilikuwa lini?akauliza kamanda “Leo asubuhi.Alitupigia simu akiwa Cogo DRC alikoenda kwa shughuli zake za udaktari na akatujulisha kwamba anarejea nchini leo mchana” akajibu Agrey “Dr Olivia yuko kwenye mahusiano? Mnamfahamu mpenzi wake?

“Mpaka sasa Olivia bado hajamuweka wazi mpenzi wake.Kila ninapomuuliza kuhusu suala la mahusiano jibu lake ni kwamba ataweka wazi mambo yote muda ukifika.Amejikita zaidi katika kazi zake ndiyo maana hajaweka wazi mpenzi wake hadi sasa”akajibu Agrey “Bwana na Bi Themba, kama hawa jamaa lengo lao la kumteka Dr Olivia ni kujipatia fedha tuna hakika watawasiliana nanyi na kudai fedha.Kama wakiwapigia simu tafadhali tuwasiliane haraka sana.

Najua wakipiga simu watawatisha msitoe taarifa kwa polisi ama watamuua mtoto wenu lakini nawaomba msiogope,wasilianeni haraka sana na jeshi la polisi na tutafanya kila juhudi za kumkomboa Olivia na kudhibiti matukio kama haya yasiendelee hapa nchini.Endapo pia mtapata taarifa zozote zinazoweza kusaidia kuwafahamu watekaji hawa msisite kutujulisha haraka sana” akasema kamanda wa polisi “Afande tutatoa ushirikiano mkubwa sana kila pale tutakapopata chochote kile kuhusiana na kutekwa kwa binti yetu.

Nakuomba vilevile muwe mnatujulisha kila hatua mnayopiga katika uchunguzi huu” akasema Agrey Themba na kamanda wa polisi akatoka kwenda kuendelea na uchunguzi wao.Agrey akamshika mkono mke wake wakatoka mle ndani hadi katika gari lake wakaondoka eneo la tukio.Bado Lucy alikuwa anaendelea kulia.

KItendo cha binti yake kutekwa nyara kilimuumiza mno.Wakiwa garini Agrey alikuwa na kazi ya kupokea simu zilizokuwa zinaingia mfululizo kutoka kwa watu mbali mbali wakiwapa pole kufuatia kitendo kile cha kutekwa binti yao Dr Olivia.Simu ya Agrey ambayo huitumia kuwasiliana na watu wake wa muhimu ikaita, alikuwa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Evans mwaluba.

Agrey akamuonyesha mke wake “Rais anapiga” akasema Agrey na kupokea ile simu “Dr Evans” akasema Agrey “Agrey nimepata taarifa za tukio la kutekwa Dr Olivia nimestuka sana” akasema Dr Evans Agrey akavuta pumzi ndefu na kusema “Mheshimiwa rais ni kweli tukio hili limetokea na Olivia ametekwa.Lucy na mimi tumetoka eneo la tukio sasa hivi na hali tuliyoikuta pale ni ya kutisha.Walinzi wote wa Olivia wameuawa na yeye kutekwa nyara.

Hatujui ni nani waliomteka nyara na kwa kusudi lipi” akasema Agrey “Poleni sana Agrey.Hizi ni taarifa za kustusha mno.Matokeo kama haya ya utekaji ni mageni sana hapa nchini kwetu.Hatukuzoea mambo ya namna hii”akasema rais “Mheshimiwa rais naomba tafadhali utusaidie binti yetu apatikane na watekaji hawa wajulikane.Kama familia tumeumizwa mno na kitendo hiki” akasema Agrey

“Agrey mimi kama mtu wa karibu na familia yako nimeumizwa pia na jambo hili na ninakuahidi kwamba kwa namna yoyote ile lazima Olivia apatikane akiwa mzima wa afya. Nitatumia kila nguvu niliyonayo kuhakikisha Olivia anapatikana.Tayari nimekwisha toa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini kwamba wahakikishe hadi kufika jioni ya leo Olivia awe amepatikana.Nimeelekeza nguvu kubwa iwekwe katika kuwasaka watekaji ambao tunaamini bado wako hapa hapa Dar es salaam.

Tayari njia zote za kuingia na kutoka Dar es salaam zimefungwa na msako mkali umekwisha anza.Nimeelekeza ikiwezekana ufanyike msako wa nyumba kwa nyumba hadi Olivia apatikane.Ninawatoa hofu Agrey na familia yako kwamba kama serikali tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba Dr Olivia anapatikana.Hatuwezi kuwapa nafasi watekaji hawa ya kufanya kila watakacho katika nchi yetu hii iliyotamalaki amani” akasema Dr Evans naye akionekana kuumizwa sana na tukio lile

“Mheshimiwa rais ninakushukuru sana kwa maneno hayo ambayo yametupa faraja kubwa sana na matumaini ya kumpata mwanetu akiwa salama.Kwa niaba ya familia yangu ninasema ahsante sana” akasema Agrey “Nimeagiza kupewa ripoti kila baada ya saa moja kuhusiana na mwenendo mzima wa kuwasaka hao watekaji na kila nitakapokuwa ninapata taarifa nitakuwa ninawajulisha” akasema rais na kuagana na Agrey.

“Mheshimiwa rais naye ameguswa sana na ameahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha Olivia anapatikana.Amekwisha toa maelekezo kwa jeshi la polisi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha Olivia anapatikana” Agrey akamwambia mke wake wakiwa garini wakirejea nyumbani kwao Mara tu rais alipomaliza kuzungumza na Agrey
Themba, akazitafuta namba za Devotha Adolph mkurugenzi wa idara maalum ya siri ya usalama wa ndani wa nchi akapiga na simu ikapokelewa.

“Devotha what’s the situation? akauliza Dr Evans “Kila kitu tayari mheshimiwa rais.We have Olivia in our custody”akajibu Devotha “Good.Hakikisha kila kitu kinakwenda vyema.Sitaki tatizo lolote litokee.Hakikisheni mnatumia kila aina ya mbinu kupata taarifa kutoka kwake.Taarifa alizonazo ni muhimu sana kwetu” “Sawa mheshimiwa rais,tayari tumejipanga vyema kwa ajili ya kuhakikisha anatupa taarifa zote” akasema Devotha

SIKU NNE ZILIZOPITA

Saa kumi na mbili za jioni gari moja jeusi liliwasili katika makazi ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jijini Dar es...
Kazi kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom