Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 1
TEHRAN – IRAN
Mlango wa chumba
ulifunguliwa,Mathew Mulumbi
akageuza kichwa taratibu
kutazama mtu aliyeingie mle
chumbani.
“Asalaam alaykum Abu
Zalawi” akasalimu yule jamaa
aliyeingia mle ndani.
“Wa alykum salaam”
akajibu Mathew.Yule jamaa
akamsogelea karibu
“Naitwa Yasser Wajid”
akasema
“Nafurahi kukufahamu
Yasser” akajibu Mathew na
kuinuka kitandani akakaa
“Vipi maendeleo yako?
Akauliza Yasser
“Ninaendelea vizuri japo
nina maumivu mwili mzima”
akajibu Mathew
“Pole Abu Zalawi
umeumizwa sana.Amka
ujiandae nimetaarifiwa
kwamba daktari atafika hapa
muda si mrefu kwa ajili ya
kutazama maendeleo yako”
akasema Yasser
“Ahsante Yasser” akajibu
Mathew na Yasser akaanza
kupiga hatua kutoka
“Yasser samahani”
akasema Mathew na Yasser
akageuka
“Kuna jamaa Yule mfupi
jana alikuwa amevaa suti ya
rangi ya kijivu anaitwa nani?
Akauliza Mathew
“Anaitwa Faqir Jahid”
akajibu Yasser
“Jana nilimuona akitoa
maelekezo kadhaa hapa
ndani.Ana cheo gani? Akauliza
Mathew
“Yule ndiye msimamizi
mkuu wa nyumba hii na
nyumba nyingine zote kama
hizi ambazo ziko chini ya
MOIS”
“MOIS ni nini?akauliza
Mathew
“MOIS ni wizara ya
intelijensia ya Iran” akajibu
Yasser
“Faqir atakuja hapa leo?
Akauliza Mathew
“Ndiyo anakuja na daktari”
akajibu Yasser na kutoka
akamuacha Mathew
akijiandaa.
“Kila ninapovuta pumzi
ninawaza wale jamaa wa
G20.Nilichokiona nyumbani
Tanzania kimenisikitisha
sana.Baba wa taifa letu
alijenga msingi imara kwa
watanzania kutokubaguana
kwa namna yoyote ile kwa
misingi ya dini wala makabila
lakini wamekuja hawa jamaa
na kupandikiza chuki kubwa
za kidini na wakafanikiwa
kuwagombanisha
watanzania.Ni kitu ambacho
kimewashangaza dunia
nzima.Wamesababisha damu
ya watanzania ikamwagika na
wengine kwenda kuishi katika
makambi.Watanzania
hawakuwahi kufikiri kama
siku moja wangeweza kwenda
kuishi katika makambi kama
wakimbizi tena ndani ya ardhi
yao wenyewe.Huu ni ukatili
mkubwa sana” akawaza
Mathew na kuuma meno kwa
hasira alizokuwa nazo
“Nitawalipia
watanzania.Hawa jamaa
hawawezi kumwaga damu
nyingi ya watanzania halafu
wakabaki salama.Lazima
dunia ifahamu nani
aliyepeleka watanzania
kupigana na kuuana wenyewe
kwa wenyewe.Lazima kila kitu
kiwekwe wazi ili dunia
ifahamu ni namna gani haya
mataifa makubwa
yanavyonyanyasa mataifa
madogo.Dunia lazima ifahamu
namna mataifa haya makubwa
yanavyopora rasilimali kutoka
katika mataifa yanayojitahidi
kupiga hatua za maendeleo
hususan mataifa ya bara la
Afrika” akawaza Mathew na
kutoka bafuni akakaa
kitandani
“Natakiwa kuanza kutafuta
namna ya kutoka mahala hapa
na kuanza kuifanya kazi
iliyonileta.Kitu cha kwanza ni
kujenga mtandao hapa Iran na
ili niweze kujenga mtandao
huo lazima nifanye kitu
ambacho kitanifanya
niaminike na hiyo
itanirahisishia kuweza
kukamilisha mipango yangu”
akawaza Mathew na mlango
ukafunguliwa alikuwa ni
Yasser ambaye alimtaka
Mathew akapate kifungua
kinywa.
Wakati Mathew akiendelea
kupata kifungua kinywa,
akaingia Faqir Jahid akiwa
ameongozana na jamaa mmoja
aliyebeba mkoba moja kwa
moja Mathew akahisi Yule
ndiye daktari aliyeambiwa
anakuja kujua maendeleo
yake. Faqir akamsalimu
Mathew halafu
akamtambulisha kwa Yule
daktari.Mathew akaacha
kupata kifungua kinywa
akaongozana na Yule daktari
kwenda katika chumba
akagangwa majeraha yake na
kupewa dawa za kuendelea
kutumia.Baada ya daktari
kumaliza kumganga
Mathew,Faqir akampa taarifa
kwamba amemletea pia
mavazi ya kubadilisha kwani
nguo alizokuwa nazo Mathew
zilikuwa chafu na zilichafuka
kwa damu
“Ahsante sana Faqir”
akasema Mathew
“Umefahamuje jina langu?
Akauliza Faqir na Mathew
akatabasamu kidogo.
“Ninapenda kuwafahamu
watu kwa majina yao ndiyo
maana nikauliza na kufahamu
jina lako” akasema Mathew
“Vipi maendeleo yako kwa
sasa?Faqir akauliza
“Ninaendelea vyema japo
mwili una maumivu bado
kutokana na hivi vidonda
nilivyonavyo”
“Pole sana.Endelea
kupumzika hadi hapo
utakapokuwa umepona
majeraha yako ndipo
maelekezo yatatolewa”
akasema Faqir
“Vipi kuhusu Yasser Wazir
na wenzake wanaendeleaje?
Mathew akauliza
“Wanaendelea
vyema.Wako hospitali
wakitazamwa afya zao ambazo
zimezorota sana” akasema
Faqir na kunyamaza kidogo
kama anafikiria namna ya
kumuuliza kitu Mathew
“Abu Zalawi taarifa ya
awali waliyoitoa akina Yasser
ni kwamba wewe ndiye
uliyewasaidia wakaweza
kurejea tena nyumbani.Ni
kweli? Akauliza Faqir
Mathew akameza mate
halafu akajibu
“Ni kweli
kabisa.Nilipambana
kuhakikisha wanarejea
nyumbani”
“Hongera sana Abu
Zalawi.Wewe ni shujaa”
akasema Faqir na ukimya
mfupi ukapita
“Hapa uko salama na kila
unachohitaji utakipata usiwe
na hofu yoyote.Serikali na raia
wote wa Iran wanakushukuru
sana kwa hili ulilolifanya
kwani tulikwisha amini wale
watu wetu wameuawa”
akasema Faqir na kumueleza
Mathew kwamba yeye
anaondoka kwenda kuendelea
na majukumu yake mengine
“Faqir samahani kuna
jambo ninataka kuzungumza
nawe” akasema Mathew
“Nini unahitaji Abu
Zalawi? Akauliza Faqir
“Jana usiku alikuja hapa
Brigedia Jenerali Ahsan Javad
waziri wa ulinzi wa Iran akiwa
ameambatana na watu
wengine wawili.Kuna Yule
jamaa mnene aliyekuwa
amevaa kanzu nimesahau jina
lake”
“Anaitwa Vahid
Ghorbani.Ni mmoja wa
matajiri wakubwa hapa
Iran.Anamiliki viwanda mbali
mbali na vile vile ana visima
vya mafuta.Ni mmoja wa watu
wanaoheshimika sana”
akasema Faqir
“Ninahitaji kuzungumza
naye.Unaweza kunisaidia
kumfikishia ujumbe kuwa
ninataka kuonana naye?
Akauliza Mathew na Faqir
akatabasamu
“Abu Zalawi kumfikia
Vahid si jambo rahisi kwa mtu
kama mimi.Sina mahusiano
naye yoyote na hata namba
zake za simu sina.Yule ni rafiki
mkubwa wa waziri wa ulinzi”
akasema Faqir
“Ninahitaji sana
kuzungumza naye jambo la
muhimu.Tafadhali nisaidie
kumfikishia ujumbe kuwa
ninamuhitaji kuonana naye
naamini atakuja kuniona.Au
kama ukiweza nipeleke
nyumbani kwake tafadhali
nikaonane naye mimi
mwenyewe” akasema Mathew
“Abu Zalawi wewe
huruhusiwi kutoka ndani ya
nyumba hii kwa sasa.Hayo
ndiyo maelekezo yaliyotolewa
na Sassan”
“Sassan ni nani? Akauliza
Mathew
“Sassan Mahmoud alikuja
jana usiku na waziri wa
ulinzi.Ni waziri wa wizara ya
intelijensia na usalama wa
taifa”
“Kama siruhusiwi kutoka
humu ndani naomba unisaidie
kufikisha ujumbe kwa Vahid
kuwa ninataka kuonana
naye.Ni muhimu sana”
akasema Mathew
“Kwani kuna jambo gani la
muhimu Abu Zalawi hadi
utake kuonana na mtu
mkubwa kama huyu Vahid?
Unaweza ukanieleza tafadhali?
Akauliza Faqir
“Natamani sana
ningekwambia Faqir lakini
siwezi.Nisaidie tafadhali
nionane na Vahid” akasema
Mathew
“Abu Zalawi ninataka sana
kukusaidia lakini uwezo wangu
wa kumfikia Vahid ni
mdogo.Subiri labda akija
Sassan utamuomba anaweza
akakusaidia”
“Atakuja leo huyo Sassan?
Akauliza Mathew
“Sina hakika kama atakuja
leo hii.Sifahamu ratiba zake”
akajibu Faqir
“Faqir sikiliza.Ninahitaji
sana kuonana na Vahid.Kuna
jambo nataka anisaidie na yeye
pekee ndiye anayeweza
kunisaidia.Labda nikugusie
kuwa wale jamaa
niliowakomboa akina Yasser
Wazir wako katika hatari
bado”
“Wako katika hatari?
Akauliza Faqir
“Ndiyo wako katika hatari
kubwa ya kuuawa” akasema
Mathew na kumstua Faqir
“Nani anataka kuwaua?
Akauliza Faqir
“Siwezi nikakueleza kwa
sasa lakini watu wale wako
katika hatari kubwa na bila
kupata msaada wa haraka
wanaweza wakauawa hapa
hapa katika ardhi ya nyumbani
kwao”
“Abu Zalawi umefahamuje
kama kuna watu wanataka
kuwaua? Akauliza Faqir
“Faqir ninachokwambia ni
kitu cha kweli kabisa.Endapo
wakiuawa nitawaeleza
wakubwa zako kwamba
nilikutaarifu juu ya jambo hili
na ukanipuuza” akasema
Mathew
“Kama hicho
unachokizungumza ni kitu cha
kweli basi taarifa hizi
nitazifikisha kwa taasisi husika
ili waongeze ulinzi mahala
walipo wale jamaa” akasema
Faqir
“Hapana hatupaswi
kufanya hivyo.Tafadhali
naomba umtafute Vahid aje
hapa nizungumze naye.Lengo
ni kuwasaidia hawa raia wenu
ambao walikuwa wamepotea
kwa miaka mingi waweze kuwa
salama” akasema Mathew
“Abu Zalawi naomba hiki
unachokisema kiwe ni kitu cha
kweli vinginevyo …..”
“Usihofu
Faqir.Ninachokueleza ni kitu
cha kweli kabisa”
“Sawa ngoja nitafute
namna ya kumpata Vahid na
kumfikishia ujumbe huu na
kama atakubali basi
nitakujulisha” akasema Faqir
na kutoka
“Ninahitaji kuwasiliana na
Habiba na mtu pekee ambaye
ninaweza kutumia simu yake
kuwasiliana naye ni
Vahid.Naamini akipata
ujumbe wangu kwamba
ninamuhitaji lazima atafika
hapa mara moja.Imekuwa
vizuri kwa Habiba
kutengeneza mtandao wake
sehemu mbali mbali” akawaza
Mathew
Faqir baada ya kutoka
chumbani kwa Mathew
akaingia garini na kuondoka.
“Anachokisema Abu
Zalawi ni kitu cha kweli?
Amefahamuje kama kuna
mpango wa kuwaua wale
jamaa waliorejea jana? Hana
simu wala kifaa chochote cha
mawasiliano amepata wapi
taarifa hizi? Akajiuliza Faqir
“Lakini ni vipi kama jambo
hili likawa kweli na watu wetu
wakauawa? Mambo mengine si
ya kupuuza.Ngoja nifikishe
ujumbe kwa Vahid kama Abu
alivyoomba” akawaza Faqir
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 2
Faqir aliwasili katika
makazi ya Vahid
Ghorbani.Bado Vahid
alikuwepo nyumbani
kwake.Faqir akakaribishwa
ndani ambako Vahid alikuwa
katika chumba cha chakula
akipata kifungua kinywa.
“Karibu tupate kifungua
kinywa” akasema Vahid na
Faqir akajumuika
mezani.Baada ya kumaliza
kupata mlo ule wa asubuhi
wakaelekea sebuleni
kuzungumza
“Karibu sana
kijana.Tumewahi kuonana?
Akauliza Vahid
“Hapana mzee naamini
hunifahamu ila mimi
nakufahamu.Naitwa Faqir
Jahid ni mfanyakazi wa MOIS
idara ya nyumba za siri.Jana
usiku ulifika katika mojawapo
ya nyumba za siri za MOIS
ukiwa na waziri wa ulinzi na
waziri wa intellijensia na
usalama wa Taifa” akasema
Faqir na Vahid akastuka
kidogo
“Kuna mtu mmoja anaitwa
Abu Zalawi amenituma kwako
anahitaji kuonana nawe”
akasema Faqir Jahid na Vahid
akavuta pumzi ndefu na
kutazama juu
“Abu Zalawi ! akasema
Vahid kwa sauti ndogo na
kuinamisha kichwa
akionekana kutafakari jambo
“Abu Zalawi anataka kitu
gani? Sitaki ukaribu
naye.Watu wanaweza
wakaanza kuhisi na mimi nina
mashirikiano na magaidi kama
nitaendelea kuonana naye
mara kwa mara.Nitamweleza
Habiba Jawad asinitume tena
kwa Yule jamaa.Sitaki
kuharibu jina na sifa yangu
nzuri kwa watu kunihisi nina
shirikiana na hawa magaidi”
akawaza Vahid
“Mzee Vahid nipeleke jibu
gani kwa Abu Zalawi? Akauliza
Faqir
“Nitakwenda kuonana
naye lakini siwezi kwenda pale
peke yangu lazima niwe na
mwenyeji”
“Usihofu mzee mimi nipo
kama utahitaji kwenda
kuonana naye nitakupeleka”
akasema Faqir
“Nisubiri kidogo” akasema
Vahid na kuelekea chumbani
kwake akachukua simu na
kumpigia Habiba Jawad
“Habari za asubuhi Vahid”
akasema Habiba
“Habiba nimepokea
ujumbe kutoka kwa Abu
Zalawi kwamba anahitaji
kuonana nami asubuhi hii”
akasema Vahid
“Ana tatizo lolote? Habiba
akauliza
“Hajasema chochote kama
ana tatizo ama vipi yeye
ametuma ujumbe nikamuone”
“Vahid naomba ukaonane
naye tafadhali.Nafahamu ni
usumbufu mkubwa unaupata
lakini naomba ukaonane naye
kwani asingeweza kuomba
kuonana nawe kama hana
jambo la muhimu” akasema
Habiba
“Nitakwenda kuonana
naye lakini nitaomba
uzungumze naye na
umwambie mimi ni nani ili
aniheshimu.Mtu mwenye
heshima kubwa kama mimi
sitakiwi kuitwa itwa na
g………..” akasema Vahid na
kusita
“Hutaki kuitwa na
gaidi.Nadhani ndivyo ulitaka
kusema”
“Samahani Habiba kama
nitakukera lakini nilipata
taarifa kuwa Abu Zalawi ni
gaidi na ndiye aliyelipua
ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania.Nilisikitika mno kwa
mtu kama huyu kumuoa
mwanangu
Najma.Ninamsaidia kwa
sababu yako Habiba
vinginevyo nisingethubutu
hata kuzungumza naye.Habiba
wewe mwenyewe unanifahamu
vizuri sipendi sana magaidi na
ndiyo maana hata mimi nawe
tulishindwa kufunga ndoa
baada ya kugundua kwamba
unafadhili makundi ya kigaidi”
akasema Vahid
“Vahid bado hufahamu
chochote kuhusu mimi wala
Abu Zalawi.Naomba
ukamsikilize na kama kuna
tatizo lolote naomba umsaidie”
akasema Habiba akionekana
kutokufurahishwa na maneno
aliyoyasema Vahid
“Sawa Habiba ninakwenda
huko nitakujulisha nini
kimejiri nitakapotoka lakini
naomba hii iwe ni mara ya
mwisho.Sitaki watu waanze
kuhisi kuwa nina mashirikiano
na magaidi” akasema Vahid na
kukata simu
“Habiba ni mwanamke
niliyempenda mno hadi
nikazaa naye mtoto lakini
nilipogundua kuwa ana fadhili
makundi ya kigaidi nikaachana
naye.Nawachukia mno
magaidi lakini ngoja tu niende
nikaonane na Abu Zalawi nijue
ana tatizo gani” akawaza Vahid
na kutoka akaongozana na
Faqir wakaelekea katika
nyumba aliko Mathew.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 3
“Abu Zalawi habari za leo”
akasema Vahid baada ya
kufika mahala aliko Mathew
Mulumbi
“Ahsante kwa kuja Vahid
na samahani sana kwa
usumbufu” akasema Mathew
“Usijali Abu
Zalawi.Niambie kitu gani
umeniitia hapa? Akauliza
Vahid akionekana kuwa na
haraka
“Vahid kubwa ambalo
nimekuitia hapa ninataka
kuzungumza na Habiba
Jawad” akasema Mathew
“Hilo tu? Akauliza Vahid
“Ndiyo Vahid ni muhimu
sana” akasema Mathew na
Vahid akachukua simu
akazitafuta namba za Habiba
Jawad akapiga halafu akampa
Mathew simu ambaye alimtaka
Vahid atoke nje ili aweze
kuzungumza na Habiba
“Hallow Vahid” akasema
Habiba Jawad baada ya
kupokea simu
“Ni mimi Abu Zalawi”
akasema Mathew
“Mathew habari yako”
“Nzuri mama.Vipi wewe
unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri.Kuna
nini Mathew hadi ukataka
kuonana na Vahid?
“Nilihitaji kuzungumza
nawe ndiyo maana
nikamtumia ujumbe Vahid
nionane naye”
akasemaMathew
“Vahid hajafurahishwa na
amekuja kuonana nawe kwa
sababu yangu.Kuna nini
unataka kuniambia?
“Ninakaribia kuianza kazi
niliyotumwa kuja kuifanya
lakini ili niweze kuikamilsha
kazi hiyo napaswa kujenga
kwanza mtandao na ili nipate
mtandao natakiwa kufanya
kitu kitakachowafanya
waniamini”
“Unataka kufanya nini
Mathew? Akauliza Habiba
“Ninataka kuwaanika
majasusi wa Mossad walioko
hapa Iran.Serikali ya Iran
inafahamu kuwa kuna
majasusi wa Israel hapa Iran
lakini haiwafahamu ni akina
nani na wako
wapi.Nitakapowafumbua
macho majasusi hao ni akina
nani na wako wapi nitakuwa
nimewasaidia kitu kikubwa
sana hivyo nahitaji msaada
wako katika hilo.Tafuta namna
unavyoweza kufanya ili
kuipata orodha ya majasusi wa
Israel walioko hapa
Iran.Nikifanikiwa kuipata
orodha hiyo itanisaidia
kunikutanisha na viongozi wa
hapa na hapo ndipo
nitakapoanza kazi yangu”
akasema Mathew
“Mathew hilo ni wazo zuri
sana tatizo ni namna ya
kuweza kuipata orodha hiyo ya
majasusi wa Israel walioko
Iran” akasema Habiba
“Mama Habiba wewe una
mtandao mkubwa hata ndani
ya mashirika haya ya kijasusi
hivyo fanya kila
linalowezekana niweze kuipata
hiyo orodha ya majasusi wa
Mossad ikiwezekana leo hii
hii” akasema Mathew
“Sawa nitajitahidi niweze
kuipata na nitakapofanikiwa
nitakujulisha” akasema
Habiba
“Nashukuru sana
mama.Naomba uliwekee uzito
jambo hilo.Vipi kuhusu wale
jamaa kule Marekani? Kuna
taarifa zozote umezipata
kutoka kwao? Akauliza
Mathew
“Mpaka sasa bado sijapata
taarifa zozote kutoka
kwao.Usijali kila
nitakachokipata
nitakujulisha”akasema Habiba
Jawad na ukimya mdogo
ukapita halafu Habiba
akasema
“Mathew kuna jambo
lingine ninataka
kukufahamisha” akasema
Habiba na kunyamaza kidogo
“Hivi tuzungumzavyo
Nawal yuko angani anarejea
Riyadh akitokea Tanzania”
“Nawal alikwenda
Tanzania? Akauliza Mathew
“Ndiyo Mathew.Nawal
alikwenda Tanzania kutekeleza
misheni muhimu
niliyomtuma.G20 walikuwa na
mpango wa kusambaza kirusi
hatari nchini Tanzania kwa
lengo la kuwawezesha kuwepo
Afrika Mashariki kwa muda
mrefu zaidi ili waendelee na
uporaji wa rasilimali.Baada ya
kuufahamu mpango huo
nikamtuma Nawal kwenda
kuuharibu .Nawal
akishirikiana na Ruby na timu
yake wamefanikiwa kuzima
jaribio hilo la kusambaza
kirusi hatari nchini Tanzania
na nchi iko salama” akasema
Habiba
“Nawal amekutana na
Ruby? Akauliza Mathew
“Ndiyo.Amekutana na
Ruby na wameshirikiana
katika misheni hiyo” akasema
Habiba
“Ahsante sana mama
Habiba kwa msaada huu
mkubwa.Naamini bila wewe
kuwa na taarifa hizo hivi sasa
nchi ya Tanzania ingekwisha
ingia katika janga lingine
kubwa la watu kupoteza
maisha.Mama ninazidi kuwa
na hasira na hawa watu na
ninaapa lazima nihakikishe
ninarudi tena Marekani
kuwamaliza.Hawawezi
kutufanyia mambo mabaya
kama haya na wakabaki
salama” akasema Mathew
akiwa amejaa hasira
“Mathew kuna jambo
lingine nataka
kukufahamisha.Nawal anakuja
Tehran”
“Anakuja huku?! Mathew
akashangaa
“Ndiyo anakuja Tehran
kukusaidia” akajibu Habiba
“Hapana mama.Nawal
hapaswi kabisa kuja huku.Hii
ni misheni ya hatari mno
mama.Nawal hapaswi kabisa
kufika hapa! Akasema Mathew
“Mathew hili si
ombi.Nawal anakuja Tehran
kukusaidia.Mathew misheni
hii ni hatari sana na wewe uko
peke yako.Lazima uwe na mtu
anayeweza kukusaidia.Usihofu
hatavuruga misheni yako bali
anakuja ili kukupa msaada
pale itakapohitajika” akasema
Habiba
“Mama sidhani kama hilo
ni wazo zuri kwa sasa”
akasema Mathew
“Mathew kama
nilivyokwambia kwamba hili si
suala la kujadili.Nimekwisha
fanya maamuzi Nawal anakuja
Tehran.Mathew hii ni misheni
kubwa na lazima utahitaji
msaada” akasema Habiba na
kuagana na Mathew
“Kila uchao hasira dhidi ya
watu hawa wanaojiita G20
zinaongezeka.Ninatafakari
adhabu mbali mbali
wanazostahili watu hawa bado
sijapata jibu lakini kitu
nitakachowafanyia kitabaki
katika historia ya
Marekani.Sikujua kama
walikuwa na mpango
mwingine wa kwenda
kusambaza virusi nchini
Tanzania kwa lengo la
kuendeleza uporaji wa
rasilimali zetu.Kule Tanzania
tunasema za mwizi
arobaini.Hawa jamaa
wamefikisha siku ya 39
arobaini yao iko kwenye
kona.Laiti kama wangefahamu
wangeanza kujiandaa kutoka
sasa kwani tufani
inayowakaribia ni kubwa”
akawaza Mathew
“Naamini Nawal atakuwa
amekiacha kirusi hicho
Tanzania.Ninatamani kirusi
hicho kingerejeshwa Marekani
ili kikawaangamize wao
wenyewe lakini hatupaswi
kufanya hivyo kwani
hatutakuwa na tofauti na
wao.Wamarekani hawafahamu
kile kinachoendelea nchini
mwao na hawana habari kama
kuna kikundi kinajiita G20
ambacho kinafanya mambo ya
kikatili kabisa sehemu mbali
mbali duniani hasa barani
Afrika kwa lengo la kupora
rasilimali kama vile mafuta na
madini.Bara la Afrika
limekuwa likigubikwa na
migogoro ya mara kwa
mara.Mapigano ya wenyewe
kwa wenyewe yanaibuka kila
mara katika nchi za Afrika na
ukiichunguza mingi ya
migogoro hiyo ina mkono
wake kutoka nchi hizi kubwa
ambazo zinafaidika kwa
kuchochea migogoro
hiyo.Wanapata soko la kuuza
silaha,wanapora mali nk.Kwa
bahati mbaya sana kuna
waafrika wenzetu ambao kwa
tamaa za mali wamejikuta
wakishirikiana na mabeberu
hawa katika kuwasaliti wenzao
na hata kuchochea
mifarakano.Natamani
niitangazie dunia hata sasa kile
kinachoendelea lakini ngoja
nivute subira nimalize misheni
yangu hapa Iran ili niweze
kupata kibali cha kuingia tena
Marekani kukimaliza kikundi
cha G20” akawaza Mathew na
kukumbuka kuwa alikuwa na
simu ya Vahid.Akaufungua
mlango na kumfuata Vahid
sebuleni alikokuwa amekaa
akizungumza na Faqir
“Nashukuru sana mzee
kwa msaada huu mkubwa”
akasema Mathew Vahid
akaipokea simu ile na
kusimama akamtaka Mathew
wasogee pembeni wazungumze
“Kijana naamini tayari
umemaliza shida yako”
“Ndiyo mzee.Nilihitaji
sana kuzungumza na Habiba
jambo la muhimu”
“Hii ni mara yangu ya
mwisho kufika hapa.Kama
ukihitaji kuzungumza tena na
Habiba tafuta namna nyingine
ya kuwasiliana naye lakini si
kunitumia ujumbe nyumbani
kwangu.Sina mashirikiano
yoyote na magaidi mimi !
akasema kwa ukali Vahid na
kuanza kuondoka akimuacha
Mathew amesimama
akimtazama.
“Sipaswi
kukasirika.Napaswa
kuvumilia.Ninamshukuru hata
hivyo kwa msaada alionisaidia
kuzungumza na Habiba mara
mbili.Kwa sasa ngoja
niendelee kusubiri majibu
kutoka kwa Habiba” akawaza
Mathew na kurejea chumbani
kwake.
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Imetimu saa nane za
usiku,bado kikao kizito
kiliendelea katika ikulu ya
Marekani kati ya Rais William
Washington na wakuu wa
vyombo vya ulinzi vya
Marekani.Kikao hicho
kilitokana na taarifa ya
kustusha waliyoipata kutoka
Tanzania kwamba kambi
ndogo ya vikosi vya Marekani
vilivyoko nchini Tanzania
ilivamiwa na watu
wasiojulikana ikashambuliwa
na kuteketezwa kabisa huku
wanajeshi wote waliokuwepo
kambini usiku h uo wakiuawa.
Wakati kikao
kikiendelea,walikuwa
wakipokea taarifa mbali mbali
kutoka kwa makamanda
walioko Tanzania vile vile
waliweza kuonyeshwa moja
kwa moja picha za kambi yao
namna ilivyoharibiwa vibaya
sana na wavamizi.Taarifa
nyingine iliyowastua ni
kwamba kuwa nyumba
aliyokuwa akiishi mkuu wa
vikosi vya Marekani vilivyoko
Tanzania Jenerali William
nayo pia ilivamiwa na watu
wasiojulikana,wanajeshi
kadhaa wakauawa na Jenerali
William haikufahamika
mahala alipo.Jumla ya
wanajeshi waliouawa katika
matukio hayo mawili walikuwa
thelathini na moja.
Saa kumi usiku kwa saa za
Marekani ndipo kikoa
kilipomalizika.Baada ya kikao
kumalizika Rais William
hakwenda kulala alikuwa na
kikao kingine muhimu na
makamu wa Rais.Moja kwa
moja wakaenda katika chumba
cha mazungumzo ya
faragha.Bado Mark Piller
alikuwa anazungumza na mtu
simuni.Baada ya muda
akalazimika kumuomba radhi
mtu yule aliyekuwa
akizugumza naye simuni na
kukata simu.
“Mark nimechanganyikiwa
na hiki kilichotokea !
akaanzisha mazungumzo Rais
William Washington
“Mheshimiwa Rais kweli
hili ni jambo la kustusha mno
lakini tunapaswa tuwe
watulivu wakati tunasubiri
kupata taarifa rasmi nini
kimetokea na nani waliofanya
shambulio hilo” akasema Mark
Piller na ukimya ukapita.
“Mark” akaita Rais
William na Mark Piller
akainua kichwa akamtazama
“Tumetazama namna
kambi ilivyoharibiwa vibaya na
wanajeshi wetu walivyouawa
kikatili.Kwa haraka haraka
picha gani inakujia kuhusu
waliofanya tukio lile? Akauliza
Rais William
“Kwa haraka haraka picha
ninayoipata ni kwamba
wavamizi walifanya shambulio
la kustukiza.Inaonekana
wanajeshi wetu hawakuwa
wakifahamu kama
watashambuliwa.Picha
nyingine ninayoipata wavamizi
walikuwa wamejihami kwa
silaha nzito sana na ndiyo
maana wakaweza kuwaua
wanajeshi wetu” akasema
Mark Piller
“Tutajadili kwa kina sana
jambo hili lakini swali ambalo
linatakiwa kutawala vichwa
vyetu muda huu ni nani
waliofanya shambulio lile na
kwa nini?Unadhani ni…ah !
ninazidi kuchanganyikiwa
Mark” akasema Rais William
na kugonga meza kwa hasira
“Halafu mbona hakuna
maiti hata moja ya watu
waliovamia? Je hakuna hata
mmoja aliyeuawa? Akauliza
William
“Mheshimiwa Rais tukio
hili lina utata
mkubwa.Ukizitazama picha za
sehemu ya tukio ninahisi
wanaoweza kufanya shambulio
kama hili ni watu wenye uwezo
mkubwa na mbinu za hali ya
juu za mapigano.Raia wa
kawaida hawana mafunzo ya
hali ya juu namna hii ya
kuweza kusambaratisha kambi
na kuua wanajeshi wetu wote
wenye uwezo mkubwa katika
mapigano”
“Nini unamaanisha Mark?
“Yawezekana ..”Mark
akasita
“Nini Mark? Kama kuna
kitu unakihisi kiweke wazi !
akasema Rais William
“Ninajaribu kujenga picha
mbali mbali kichwani kwangu
lakini ninashindwa
kuziunganisha.Tusubiri tupate
taarifa kutoka kwa wanajeshi
wetu walioko huko Tanzania
ambao wanaendelea na
uchunguzi watatupa picha
nzuri zaidi” akasema Mark
“Mark tuliweke kwanza
pembeni suala hilo nimetaka
tuje hapa tuzungumze
kuhusiana na ule mpango
wenu wa kusambaza kirusi”
akasema Rais William na Mark
akavuta pumzi ndefu
“Mheshimiwa Rais,muda
mwingi wa kikao nilikuwa
nazungumza na simu
nikiwasiliana na wenzagu ili
tufahamu
kinachoendelea.Taarifa si
nzuri hata kidogo” akasema
Mark na sura ya Rais William
ikaonesha mstuko
“Kuna nini kimetokea?
Akauliza
“Kwa taarifa nilizopewa na
wenzangu wanaoendelea
kufuatilia suala hili ni kwamba
mtu tuliyemtuma kwenda
kusambaza kirusi alifika
salama Dar es salaam na
alikabidhiwa kwa Jenerali
William ambaye ndiye
atakayeratibu zoezi zima la
usambazaji akisaidiana na
Assad Ismail kutoka IS.Taarifa
ya kuvamiwa kwa nyumba
anamoishi Jenerali William na
wanajeshi waliokuwa
wakilinda nyumba hiyo
kuuawa na Jenerali William
kutoweka kinaleta wasiwasi
mkubwa sana kuhusu ule
mpango wetu wa kusambaza
kirusi” akasema Mark Piller na
ukimya ukatawala tena
“Huyo mtu wenu wa IS
anapatikana simuni? Akauliza
Rais William
“Hapatikani” akajibu Mark
Piller
“Mark kuna wazo linanijia
japo sijui kama lina msingi
wowote.Hudhani kama watu
wa IS wanaweza kuwa
wamehusika katika shambulio
hili? Akauliza Rais William
“IS? Akauliza Mark Piller
“Ndiyo.Hudhani kama
wanaweza kuwa wamehusika
katika jambo hili?
“IS hawawezi kuhusika
kabisa katika shambulio hili
kwa sababu tunashirikiana nao
na tunawalipa pesa nyingi sana
vile vile tunawawezesha kwa
silaha na mambo mengine
kadhaa” akasema Mark Piller
“Nimejiwa na wazo hilo
kwa sababu yawezekana labda
IS wakawa wanakihitaji hicho
kirusi na wakaamua kufanya
shambulio hilo ili wakichukue
na kukitumia katika mambo
wanayoyajua wenyewe”
akasema Rais William
“Hilo unalosema
mheshimiwa Rais
linawezekana lakini hawa
jamaa tumekuwa
tunashirikiana nao kwa muda
mrefu.Hawawezi kutufanyia
hivi” akasema Mark Piller
“Kama si wao basi nani
aliyefanya shambulio lile?
Akauliza Rais William
“Mheshimiwa Rais kwa
sasa tunahangaika kujua
mahala alipo Jenerali
William.Yeye ndiye
anayefahamu mahala kilipo
kirusi na akipatikana basi
tutafahamu kila kitu” akasema
Mark Piller
“Mark hebu nisaidie
mawazo nini tufanye? Mimi
nimechanganyikiwa hapa”
akasema William
“Rais wa Tanzania
umekwisha zungumza naye?
Akauliza Mark Piller
“Hapana bado
sijazungumza naye”
“Zungumza na Rais wa
Tanzania yawezekana akawa
na taarifa ambazo sisi hatuna
kuhusiana na shambulio
hili.Naamini vyombo vya ulinzi
na usalama vya Tanzania
navyo vinalichunguza jambo
hili na yawezekana tayari
wamepata fununu Fulani
kuhusu nani waliofanya
shambulio hilo” akasema Mark
na simu yake nyingine ambayo
huiweka katika mfuko wa koti
ikaita akaitoa mfukoni
akatazama mpigaji alikuwa ni
Habiba Jawad.Rais William
akamtazama kwa macho ya
udadisi
“Ni Habiba Jawad” Mark
akamwambia Rais kisha
akaipokea ile simu
“Hallow Habiba”
“Mark habari za usiku
huu.Samahani kwa
kukuamsha kama ulikuwa
umelala” akasema Habiba
“Hapana sijalala.Usiku
mzima wa leo umekuwa ni wa
vikao mfululizo.Naamini
umepata taarifa za kile
kilichotokea nchini
Tanzania.Kambi yetu
imeteketezwa na wanajeshi
wengi wameuawa.Ni
shambulio baya kabisa”
akasema Mark Piller
“Tayari nimekwisha zipata
taarifa hizo.Poleni sana kwa
tukio hilo baya.Tayari
mmekwisha fahamu nani
waliofanya shambulio hilo?
Akauliza Habiba
“Mpaka sasa
haijafahamika nani waliofanya
tukio hilo.Habiba tukio hili
limeathiri pia ule mpango
wetu wa kusambaza kirusi”
akasema Mark Piller na
kunyamaza kidogo
“Sattar Sayf Al Din alifika
Tanzania na alipokewa na
mkuu wa vikosi vya Marekani
anaitwa Jenerali William
ambaye ndiye tuliyemkabidhi
jukumu la kumsaidia Sattar
katika mpango wa kusambaza
kirusi hicho.Nyumba anayoishi
Jenerali William nayo pia
imevamiwa na watu
wasiojulikana walinzi wake
wameuawa na yeye mwenyewe
ametoweka hajulikani mahala
alipo.Yeye ndiye mwenye
taarifa zote kuhusiana na
kirusi.Tumekwama na
tunaendelea kusubiri kama
Jenerali William atapatikana
ili tujue kuhusiana na kirusi
kama kiko salama” akasema
Mark Piller
“Vipi kuhusu Assad Ismail
naye pia hapatikani simuni?
Yeye pia alikuwa anategemewa
kumsaidia Sattar katika
usambazaji wa kirusi hicho”
“Assad naye hapatikani
simuni.Hili jambo
linatuchanganya sana Habiba”
“Kama wote hawapatikani
yawezekana wako sehemu
salama wamejificha na
watajitokeza baada ya muda
kupita.Au tayari wako katika
usambazaji wa kirusi” akasema
Habiba
“Hapana Habiba hilo
haliwezekani.Jenerali William
ndiye mkuu wa vikosi vya
Marekani kama angekuwa
amejificha sehemu hadi muda
huu ambao inakaribia saa tano
za asubuhi nchini Tanzania
angekuwa amekwisha jitokeza
lakini hadi sasa hajulikani
alipo.Hii inaongeza wasiwasi
zaidi na kikubwa tunachotaka
kukifahamu ni kama kirusi
kiko salama.Mtu pekee
ambaye anazo taarifa zote za
kuhusiana na kirusi hicho ni
Jenerali William” akasema
Mark Piller
“Mmejiridhisha katika
miili iliyopatikana hakuna
mwili wa Jenerali William au
Sattar au Assad? Akauliza
Habiba
“Hakuna mwili wa Jenerali
William wala hao
wengine.Kukosekana kwa miili
hiyo katika orodha ya
waliouawa inatupa picha
kwamba yawezekana wakawa
hai.Swali ni je wako wapi?
Akauliza Mark Piller
“Kama miili yao
haijapatikana miongoni mwa
wale waliopoteza maisha basi
kuna uwezekano mkubwa
wakawa hai.Ninaamini
watakuwa amejificha sehemu
Fulani na baada ya muda
watajitokeza au yawezekana
tayari usambazaji wa kirusi
umeanza” akasema Habiba
“Tuliweke hilo pembeni
Habiba tunaendelea
kulifuatilia.Nini sababu ya
kunipigia simu? Akauliza Mark
Piller
“Nimekupigia simu
kuhusiana na ile misheni
anayoendelea nayo Abu Zalawi
kule Tehran” akasema Habiba
“Nini kinaendelea huko?
Kuna taarifa yoyote nzuri?
Akauliza Mark
“Nimewasiliana na Abu
Zalawi nikampa taarifa
kuhusiana na ule mpango
wake wa kumuua.Kuna kitu
ameniomba nimsaidie”
“Safi sana Habiba.Ahsante
kwa kumfikishia taarifa hiyo
kwa haraka.Amekuomba
umsaidie nini? Akauliza Mark
Piller
“Abu Zalawi anataka
kuanza kuifanya kazi yake kwa
kujenga mtandao nchini
Iran.Kuna kitu anakihitaji
ambacho kitamsaidia katka
mpango huo” akasema Habiba
“Sema Habiba,Abu Zalawi
anahitaji kitu gani? Akauliza
Mark Piller
“Anahitaji orodha ya
majasusi wa Mossad walioko
nchini Iran” akasema Habiba
“Anahitaji orodha ya
majasusi wa Mossad?! Mark
Piller akashangaa
“Ndiyo Mark.Anaihitaji
orodha hiyo ya majasusi wote
wa Mossad haraka” akasema
Habiba na Mark Piller akavuta
pumzi ndefu
“Hilo ni jambo
lisilowezekana
Habiba.Hatuwezi kuipata
orodha hiyo ya majasusi wa
Mossad.Hata kama tungeweza
kuipata orodha hiyo hatuwezi
kuitoa kwa mtu yeyote kwa
sababu kwa kufanya hivyo
tutakuwa tumehatarisha
usalama wa majasusi hao
kwani watajulikana na
wanaweza kuuawa” akasema
Mark Piller
“Mark kwa namna yoyote
ile lazima orodha hiyo
ipatikane.Abu Zalawi
anaihitaji mno ili kuweza
kujenga mtandao.Hii ni
misheni kubwa na lazima
kufanya kila linalowezekana ili
ifanikiwe.Abu Zalawi anahitaji
kujenga mahusiano na
viongozi wa Iran na orodha
hiyo ndiyo itakayomfanya
aaminiwe na awe na
mahusiano mazuri na
viongozi.Mark ninakuomba
fanya kila uwezalo kuhakikisha
orodha hiyo inapatikana tena
kwa haraka” akasema Habiba
“Habiba narudia tena
kusema kwamba hilo ni jambo
lisilowezekana kabisa.Hakuna
namna ninayoweza kuipata
orodha hiyo ! akasema Mark
Piller
“Mark umewasaliti
wenzako ili misheni ya Abu
Zalawi ikamilike hivyo ni
wajibu wako kuhakikisha
unafanya kila linalowezekana
ili misheni hii
ikamilike.Usiogope kuwaanika
majasusi wa Mossad kwani
kitakachopatikana katika
misheni hii ni kikubwa na kina
umuhimu pia hata kwa Israel
kwani hata wao wamekuwa
wakipokea vitisho vya
mashambulio kutoka kwa
Iran.Mark hii ni nafasi
imepatikana hivyo usiiache
ikapotea bure.Kila
atakachokihitaji Abu Zalawi
anatakiwa akipate ! akasema
Habiba.Mark Piller akafikiri
kidogo na kusema
“Habiba siwezi kukuahidi
chochote kwa sasa.Naomba
unipe muda nilifanyie kazi
jambo hili” akasema Mark
“Mark suala hili ni la leo
hii hii halihitaji kuchukua
muda mrefu”
“Sawa Habiba,nitakupa
majibu baadae kidogo.Naomba
unipe muda nione
ninavyoweza kufanya”
“Sawa Mark
ninakutegemea”
“Habiba tukiliweka hilo
pembeni kuna jambo nataka
tuzungumze na yawezekana
unaweza ukatusaidia kupata
jawabu”
“Nini unahitaji Mark?
“Tumetazama picha za
eneo la tukio limeharibiwa
vibaya mno na waliofanya
shambulio hilo lazima
watakuwa ni watu waliojihami
kwa silaha nzito.Tunahisi
yawezekana kundi la IS
limehusika katika shambulio
hili”
“IS? Habiba akashangaa
“Ndiyo” akajibu Mark
“IS wamekuwa
wakishirikiana nanyi na wao
ndio waliotakiwa kusambaza
kirusi.Iweje wabadilike na
kufanya shambulio?
“Tunahisi labda walikuwa
wanakitaka kirusi” akajibu
Mark Piller
“Hapana Mark.Sina hakika
kama IS wanaweza wakafanya
jambo kama hilo”
“Habiba hatujasema
kwamba IS wamefanya hilo
shambulio ila tunahisi
kwamba yawezekana wakawa
wanahusika.Tunataka
utusaidie kufanya uchuguzi
kujua kama wamehusika na
kama wamehusika kirusi kiko
wapi? Akasema Mark Piller
“Mark nitafanya
uchunguzi huo kujua kama
kweli wamehusika kwa namna
yoyote na shambulio hilo
nikipata chochote
nitakujulisha” akasema
Habiba
“Tunashukuru sana
Habiba.Tunatakiwa kusaidiana
kuhakikisha tunakipata kirusi”
akasema Mark Piller na
kuagana na Habiba Jawad
“Nilikuwa nazungumza na
Habiba Jawad.Nimemuomba
atusaidie kufanya uchunguzi
kufahamu kama IS
wanahusika kwa namna yoyote
na tukio la Dar es salaam”
Mark akamwambia Rais
William
“Amesemaje ulipomtaka
afanye uchunguzi huo?
“Amekubali kufanya
uchunguzi huo na atanijulisha
kile atakachokuwa
amekipata.Hata hivyo
dhumuni kuu la kunipigia ni
kunipa taarifa za maendeleo ya
misheni ya Abu Zalawi”
akasema Mark Piller na rais
William aliyekuwa amegeukia
ukutani akageuka haraka
“Anaendeleaje Abu
Zalawi? Akauliza Rais William
“Abu Zalawi tayari yuko
Tehran na taarifa ya mpango
wa kuuawa imekwisha mfikia”
“Vizuri”akasema William
“Abu Zalawi anajiandaa
kuianza kazi yake lakini kuna
kitu anakihitaji ambacho ni
kigumu kidogo”
“Anataka nini? Akauliza
Rais William
“Anataka apatiwe orodha
ya majasusi wa Mossad
walioko nchini Iran” akasema
Mark
“Anataka orodha hiyo
aifanyie nini? Akauliza Rais
Wiliam
“Anataka awaanike kwa
serikali ya Iran”
“Kwa nini anataka kufanya
hivyo? Hajui kwa kufanya
hivyo majasusi hao watakuwa
katika hatari kubwa ya
kuuawa? Iran na Israel hazina
mahusiano mazuri hivyo
wakiwagundua majasusi wa
Israel walioko nchini Iran
watawaua wote.Hilo ni jambo
la hatari kabisa Mark”
“Ni kweli mheshmiwa
Rais, ni jambo la hatari kubwa
kwa majasusi hao lakini Abu
Zalawi anataka kuitumia
orodha hiyo kwa ajili ya
kutengeneza mtandao.Kwa
kuwapa Iran orodha hiyo ya
majasusi wa Israel anaamini
kwamba watamuamini na
kumuweka karibu zaidi”
akasema Mark Piller
“Bila orodha hiyo ya
majasusi wa Israel hataweza
kuendelea na kazi aliyotumwa?
Akauliza Rais William
“Kwa mujibu wa Habiba
Jawad ni kwamba Abu Zalawi
anadai orodha hiyo ni muhimu
sana aipate tena leo hii hii”
akajibu Mark Piller.Rais
William akatafakari kidogo
halafu akauliza
“Wewe una maoni gani
Mark juu ya suala hilo?
“Tumefanya maamuzi
kwamba Abu Zalawi aendelee
na misheni yake hivyo lazima
tuhakikishe tunamsaidia kwa
kila iwezekanavyo ili aweze
kufanikisha misheni hiyo
muhimu.Hatuna namna
mheshimiwa Rais lazima
tuhakikishe tumeipata orodha
hiyo na kumpatia Abu Zalawi”
akasema Mark Piller
“Lakini Mark kwa kufanya
hivyo tutakuwa tumehalalisha
majasusi wa Israel
wauawe.Iran hawatawaacha
salama”
“Mheshimiwa Rais hapa
tumebanwa katika kona
hatuna namna ya kufanya zaidi
ya kumpatia Abu Zalawi hicho
anachokitaka.Tayari damu
nyingi imekwisha mwagika
hadi hapa tulipofika hivyo
hakuna tatizo kama tukiwatoa
sadaka majasusi hao wachache
wa Mossad ili tuweze
kufanikisha lengo letu.Endapo
misheni hii ikifanikiwa
itakuwa na msaada mkubwa
pia hata kwa Israel yenyewe
ambayo imekuwa ikipokea
vitisho vya kushambuliwa na
Iran” akasema Mark Piller
“Mark hili jambo
linanitatiza sana .Kwanza ni
namna ya kuweza kupata
orodha hiyo na pili hata kama
tukifanikiwa kuipata orodha
hiyo tukampa Abu Zalawi na
majasusi wa Israel wakauawa
ni vipi kama Israel ikigundua
kwamba sisi ndio tuliotoa
orodha hiyo kwa Iran? Hili
jambo linaweza kuleta
mtafaruku mkubwa sana kati
ya nchi zetu” akasema Rais
William
“Mheshimiwa Rais
naomba nikutoe hofu kuhusu
jambo hili.Kwanza kuhusu
kuipata orodha hiyo tunaweza
kuipata.Si jambo gumu sana
kuipata orodha hiyo.Nikiamua
kuipata siwezi
kushindwa.Kuhusu wasiwasi
kwamba Israel wanaweza
wakagundua sisi ndio
tuliowaanika majasusi wao
kwa Iran hilo haliwezi kutokea
kwa sababu Iran hawajui kama
tunashirikiana na Abu Zalawi
na Israel hawatajua chochote
kama sisi ndio tuliowaanika
majasusi wao kupitia kwa Abu
Zalawi.Nakuhakikishia
mheshimiwa Rais kwamba
orodha hiyo itapatikana kwa
namna ambayo Mossad
hawataweza kugundua
chochote”
“Una uhakika Mark?
“Naomba uniamini
mheshimiwa Rais.Jambo hili
litafanywa kitaalamu sana na
halitakuwa na madhara yoyote
kwetu” akasema Mark Piller
“Mark kama una uhakika
jambo hilo linawezekana na
halitakuwa na madhara yoyote
kwetu fanya hivyo
tafadhali.Tunahitaji mno
misheni hii ikamilike na kwa
kuwa tumekwisha kubali
kufanya kila linalowezekana ili
misheni hii ifanikiwe hatuna
namna,hakikisha Abu Zalawi
anapata kila anachokihitaji ili
mradi tuwe na umakini
mkubwa sana ili mambo haya
yasije yakatuletea tena
mgogoro mwingine mkubwa
na washirika wetu kama
Israel” akasema Rais William
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais.Ninakuahidi
hakuna kitakachoharibika.Kila
kitu kitakwenda vizuri”
akasema Mark Piller na
ukimya mfupi ukapita
“Mark kuna jambo lingine
nataka tushauriane.Tayari
imekwisha fahamika kwamba
ndege ile ya Marekani ambayo
ilidhaniwa imeangukia
baharini,imeelekea Iran.Waziri
wa mambo ya nje anajiandaa
kutoa tamko mapema asubuhi
kuitaka Iran irejeshe ndege
yetu pamoja na raia wake wote
waliokuwamo ikiwamo
mtuhumiwa wa ugaidi Abu
Zalawi.Unaonaje mpango huo?
Hautaweza kuvuruga misheni
ya Abu Zalawi? Akauliza Rais
William
“Hapana mheshimiwa
Rais hautaweza kuvuruga
misheni ya Abu Zalawi.Hata
Iran wanajua tumekwisha
fahamu ndege yetu imeelekea
nchini kwao.Tukikaa kimya
watakuwa na wasiwasi kwa
nini tumekuwa kimya?
Muache waziri wetu wa
mambo ya nje atoe tamko lake
hapo asubuhi tena liwe ni
tamko kali kabisa” akasema
Mark Piller
“Hudhani baada ya tamko
hilo,Iran wanaweza
wakamfukuza Abu Zalawi au
wakamtaka aondoke kimya
kimya hivyo misheni yetu
ikashindwa kufanikiwa?
Akauliza Rais William
“Iran hawawezi kwa
namna yoyote ile
wakamfukuza au kumuondoa
Abu Zalawi nchini kwao.Ni
mtu muhimu kwao kwanza
amewakombia watu wao
muhimu ambao naamini
walikwisha wasahau na
kuamini wameuawa,pili
atakuwa na umuhimu mkubwa
zaidi kwao pale atakapo
wakabidhi orodha ya majasusi
wa Israel walioko nchini Iran”
akasema Mark Piller
“Ahsante kwa ushauri huo
Mark lakini lazima
nizungumze na Rais wa
Tanzania nijue wamefikia wapi
katika uchunguzi na vile vile
nataka kufahamu kuhusu
Jenerali William” akasema
Rais William na kuchukua
simu yake yenye namba za
simu za marais wote wa dunia
akazitafuta namba za Rais wa
Tanzania akampigia.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Habari kuu iliyotawala
vinywani mwa watu jijini Dar
es salaam,Tanzania nzima na
dunia kwa ujumla ni
shambulio lililofanywa usiku
na watu wasiojulikana katika
kambi ndogo ya vikosi vya
jeshi la Marekani iliyoko
kandoni mwa bahari jijini Dar
es salaam.Jambo hili lilizusha
hofu kubwa miongoni mwa
wakazi wa jiji la Dar ambalo
kwa siku mbili hakukuwa na
vurugu zozote zilizoripotriwa
na taratibu hali ya maisha
ilianza kurejea na kuwa ya
kawaida.Watu walianza
kuondoka katika makambi
yaliyokuwa yametengwa kwa
ajili ya kuwahifadhi watu
waliokuwa wanakimbia
mapigano na kurejea katika
majumba yao.Baadhi ya
masoko na maduka makubwa
yalianza kufunguliwa japo
yalikuwa chini ya ulinzi mkali.
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Fabian Kelelo akiwa ofisini
kwake alimaliza mazungumzo
na mkuu wa jeshi la polisi
nchini kuhusiana na hali halisi
ya usalama ilivyo katika jiji la
Dar es salaam na katika miji
mingine hasa Tanga.
“Nashukuru sana kwa hali
ya amani kuimarika kwa kiasi
kikubwa.Hii inachangiwa
kwanza na watanzania
kutokuzoea mambo haya ya
mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe na vile vile kitendo
cha SNSA kuwakamata
magaidi waliokuwa
wanachochea vurugu hizi
kimechangia sana kwa vurugu
kukoma.Ruby na wenzake
wamefanya kazi kubwa sana”
Akawaza Dr Fabian ambaye
alitolewa mawazoni baada ya
simu yake kuita.Akaichukua
kutazama mpigaji alikuwa ni
Rais wa Marekani.Dr Fabian
akavuta pumzi ndefu
“Kazi imeanza” akasema
kwa sauti ndogo na kuipokea
simu ile
“Hallo mheshimiwa Rais
William habari za muda huu?
Naamini ni usiku mwingi huko
kwenu”
“Ni kweli mheshimiwa
Rais Dr Fabian,ni usiku
mwingi hapa Marekani lakini
bado tunaendelea na kazi.Vipi
hapo Dar es salaam
mnaendeleaje?
“Sisi tunaendelea vizuri
japo usiku wa kuamkia leo
kumetokea tukio baya ambalo
naamini tayari umekwisha
pata taarifa zake”
“Suala hilo ndilo
limenifanya nikupigie simu Dr
Fabian” akasema William na
kunyamaza kidogo
“Sikuweza kukupigia simu
kwa haraka mara tu baada ya
kupata taarifa za tukio hilo
kwani tumekuwa na mfululizo
wa vikao kujaribu kulitafakari
shambulio hilo na kupata
taarifa kutoka kwa
makamanda wetu walioko
hapo Dar es
salaam.Tumeonyeshwa picha
za tukio tumesikitishwa mno
na jambo hili.Kabla
sijaendelea zaidi naamini
vyombo vyako vya ulinzi na
usalama viliingia kazini
kuanzia muda lilipotokea
shambulio hilo,mmefikia wapi
hadi sasa katika kuwafahamu
waliofanya shambulio hilo?
Akauliza Rais William
“Mheshimiwa Rais kwanza
kabisa ninapenda kutumia
nafasi hii kutoa pole nyingi
sana kwako na kwa wananchi
wa Marekani kwa hiki
kilichotokea na kuwapoteza
wanajeshi wengi.Ni tukio baya
sana na
halivumiliki.Wanajeshi hao
walikuwepo hapa nchini kwa
ajili ya kulinda amani na
hawakustahili haya
yaliyowakuta” akasema Dr
Fabian na kunyamaza kidogo
“Mara tu baada ya kupata
taarifa za shambulio hilo,vikosi
vya jeshi la wananchi wa
Tanzania vilivyokuwa doria
vilifika eneo la tukio kwa
haraka sana lakini tayari
wavamizi hao walikwisha
ondoka.Shughuli za uokozi
kujaribu kutafuta majeruhi
zilianza mara moja lakini
hawakufanikiwa kumpata
yeyote aliye hai.Nilitoa
maelekezo usiku huo huo
kwamba msako uanze haraka
sana kuwatafuta wale
waliofanya shambulio hilo na
mpaka sasa vyombo vyetu vya
uchunguzi vikishirikiana na
wataalamu wa jeshi la
Marekani walioko hapa
wanaendelea na uchunguzi wa
jambo hili na watatupa taarifa
rasmi pale watakapokuwa
wamefanikiwa kugundua
chochote.Ni msiba mkubwa
sana mheshimiwa Rais”
akasema Dr Fabian
“Dr Fabian utanisamehe
kwa hili nitakalolisema lakini
nitalazimika kutuma vyombo
vya uchunguzi kutoka
Marekani kuja kuwatafuta
watu waliofanya shambulio
hilo.Tunahitaji kujua kwa
haraka sana nani
walioshambulia kambi yetu na
kuua wanajeshi wetu” akasema
Rais William
“William hakuna haja ya
kutuma wachunguzi kutoka
Marekani.Tanzania ina
vyombo vya uchunguzi vyenye
ujuzi na weledi mkubwa sana
nina uhakika mkubwa
waliofanya tukio hili
watapatikana hata kama
haitakuwa mapema kama
unavyotaka lakini lazima
watapatikana” akasema Dr
Fabian
“Dr Fabian Marekani tuna
vyombo vyenye uwezo
mkubwa sana na nina imani
ndani ya muda mfupi
watakuwa wamegundua nani
waliofanya tukio hi…..”
“Mheshimiwa Rais
William nina imani na vyombo
vyangu vya ndani hivyo
uchunguzi wa suala hili
utafanywa na vyombo vya
uchunguzi vya Tanzania na
sintaruhusu wachunguzi
wowote wa kutoka nje”
akasema Dr Fabian
“Dr Fabian una historia ya
kutoruhusu wachunguzi
kutoka nje ya nchi yako pale
kunapotokea shambulio baya
katika nchi yako likilenga mali
au watu wa kutoka mataifa ya
kigeni hata kama vyombo vya
uchunguzi vya nchi yako
havina uwezo wa kutosha
kulifanyia uchunguzi jambo
hilo.Tulioshambuliwa ni sisi
na tunataka kushirkiana na
vyombo vyenu katika
kuwatafuta waliotufanyia
hivi.Ugumu uko wapi?
Akauliza Rais William
“Rais William kwanza
nakuomba ufute kauli yako ya
kwamba vyombo vya Tanzania
havina uwezo wa kutosha !
akasema kwa ukali Dr Fabian
“Huo ni ukweli Dr Fabian
kama kweli vyombo vyako
vingekuwa na uwezo mkubwa
mpaka hivi sasa tayari
mngekwisha fahamu nani
walioshambulia kambi yetu !
mkuu wa vikosi vya Marekani
hapo Tanzania Jenerali
William nyumba yake pia
imevamiwa, wanajeshi
waliokuwa wanamlinda
wameuawa na hadi sasa
Jenerali William hajulikani
alipo na vyombo vyako
vimekuwa vikichunguza toka
usiku hadi muda huu na bado
hamna hata fununu za nani
wameshambulia na kuua watu
wetu.Huu ni udhaifu mkubwa
wa vyombo vyako Dr Fabian..”
akasema Rais William
“Rais William sintavumilia
dharau hizo dhidi ya vyombo
vyangu vya uchunguzi.Narudia
tena kukuhakikishia kwamba
tukio hilo limetokea katika
ardhi ya Tanzania na
litachunguzwa na vyombo vya
Tanzania.Hakuna chombo
chochote cha uchunguzi
kutoka nje kitakachoruhusiwa
kuingilia uchunguzi
unaofanywa na vyombo vya
Tanzania ! akasema kwa ukali
Dr Fabian
“Dr Fabian sielewi kwa
nini unapata kigugumizi katika
jambo hili.Au kuna kitu hutaki
kijulikane? Akauliza Rais
William
“Vyovyote utakavyofikiria
William lakini narudia tena
kauli yangu kwamba
uchunguzi wa shambulio
katika kambi ya wanajeshi wa
Marekani utafanywa na
vyombo vya uchunguzi vya
Tanzania pekee.Pale
uchunguzi utakapokuwa
umekamilika basi tutawapeni
taarifa nani waliohusika katika
shambulio hilo.Mheshimiwa
Rais kama hauna jambo
lingine la kuzungumza zaidi ya
hili ninaomba nikuache nina
kikao muhimu kinanisubiri”
akasema DrFabian
“Ni hilo tu kwa sasa Dr
Fabian nitawasiliana nawe
tena baadae saa kumi na mbili
kwa saa za Afrika mashariki
nifahamu kama mmekwisha
wafahamu waliofanya
shambulio hilo na kama
Jenerali William amepatikana
! akasema Rais William na
kukata simu
“Mataifa haya makubwa
yana dharau sana mataifa
kama yetu kwamba hatuwezi
chochote katika masuala ya
ulinzi na usalama.Ninaamini
muda si mrefu sana
tutawaumbua na hawataamini
macho yao ! akawaza Dr
Fabian na kuchukua simu
akampigia Ruby
“Ruby uko wapi?
Niliwataka mje hapa ikulu
baada ya kutoka uwanja wa
ndege” akasema DrFabian
“Tumekaribia mheshimiwa
Rais ndani ya dakika chache
tutakuwa hapo” akajibu Ruby
“Fanyeni haraka nina
vikao vingi siku ya leo.Kuna
masuala ya msingi nataka
kuzungumza nanyi” akasema
Dr Fabian
“SNSA walifanya kazi
nzuri sana kwani mpaka sasa
hakuna hata fununu za nani
waliofanya shambulio lile kwa
mujibu wa mkuu wa jeshi la
polisi.Kinachofuata ni
kuviondoa vikosi vya Marekani
hapa nchini bila wao kujua
kama tayari tumefahamu
kinachoendelea nyuma ya
pazia.Ninajilaumu sana kwa
kukubali haraka haraka
msaada wao lakini sikujua
kama walikuwa na ajenda yao
iliyojificha” akaendelea
kuwaza
Ruby na Gosu Gosu
waliwasili ikulu kuonana na
Rais.Siku zote Dr Fabian
azungumzapo na akina Ruby
hupenda kutumia chumba cha
mazungumzo ya faragha ili
kuzuia mtu mwingine asiweze
kusikia mazungumzo yao.
“Poleni sana naamini
hamjapata muda wa
kupumzika kutokana na kazi
kubwa mliyokuwa
nayo.Msichoke vijana wangu
hadi pale tutakapohakikisha
tumewaondoa mabeberu hawa
nchini kwetu na Afrika
Mashariki kwa ujumla”
akasema Dr Fabian
“Hatujachoka mheshimiwa
Rais na hatuwezi kuchoka hadi
pale tutakapohakikisha beberu
wa mwisho ameondoka katika
nchi yetu hivyo tutaendelea
kukesha macho kupigania nchi
yetu” akajibu Ruby
“Mungu anaipenda sana
nchi yetu na ndiyo maana
ameweza kuwaumbua wabaya
wetu na tumeweza kuifahamu
mipango yao miovu dhidi
yetu.Muda mfupi uliopita
nimezungumza na Rais wa
Marekani .Alitaka kufahamu
kama tayari tumekwisha
wapata waliofanya shambulio
lile nikamjibu vyombo vya
uchunguzi viko kazini
vinaendelea kuwatafuta akadai
atatuma timu ya wachunguzi
kutoka Marekani kuja nchini
kuchunguza tukio hilo lakini
nilimkatalia nikamwambia
kwamba tukio hili
litachunguzwa na vyombo vya
ndani hakuna mtu kutoka nje
ya Tanzania atakayeruhusiwa
kuja kuchunguza kitu chochote
hapa nchini.Mazungumzo yetu
hayakuisha vizuri kwani alitoa
dharau kwa vyombo vyetu
kwamba havina ujuzi mkubwa
lakini pamoja na dharau hizo
nimesimamia msimamo
wangu kwamba hakuna
mchunguzi kutoka nje ya nchi
ataingia hapa nchini”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais kwa
maamuzi hayo” akasema Ruby
“Nilitamani nimweleze
ukweli kwamba tumekwisha
fahamu kile wanachotufanyia
lakini nikajizuia kutomweleza
chochote kwa sasa hadi pale
mambo yote yatakapokuwa
yamekamilika.Nawapongeza
mlifanya kazi nzuri kwani hadi
sasa hakuna hata dalili za
kuwafahamu nani waliofanya
shambulio katika kambi
yao.Baada ya tukio la jana
nataka kufahamu nini
kinafuata? Akauliza Dr Fabian
“Tunao watu muhimu
tunawashikilia ambao
tutaendelea kuwahoji ili
kuupata mtandao mzima
uliohusika kuchochea vurugu
za kidini zilizopelekea vifo vya
watu wengi hapa
nchini.Tunaye Jenerali
William na vile vile tunaye
Assad Ismail.Kupitia kwao
tutawafahamu watu wote
waliokuwa wanashirikiana
nao”akajibu Ruby
“Nataka kufahamu hatima
ya huyu Jenerali William
kwani tayari amekwisha
julikana ametoweka na
wanamtafuta.Mnadhani
kuendelea kumshikilia
hakutakuwa na madhara
yoyote kwetu?
“Huyu jamaa tutaendelea
kumshikilia na atatusaidia
kutoa ushahidi wa kile
ambacho alitumwa kuja
kukifanya hapa Tanzania na
Afrika Mashariki.Ni mtu
muhimu sana ambaye
hatuwezi kumuachia kwa
sasa.Huyu ni mmoja wa watu
waliochangia katika
machafuko yaliyotokea hapa
nchini.Atakiri kila kitu”
akasema Ruby
“Huyu ni mwanajeshi mna
uhakika anaweza akakubali
kufunguka na kutoa siri za
nchi yake? Akauliza Dr Fabian
“Usihofu mheshimiwa
Rais atafunguka na kueleza
kila kitu.Tutatumia kila mbinu
kuhakikisha anafunguka”
akajibu Gosu Gosu
“Vizuri sana.Hili jambo
linatakiwa lifanyike haraka ili
tuwafahamu watu ambao
wamekuwa wakishirikiana nao
hapa nchini,tuwakamatwe
haraka kabla hawajatoroshwa
ili kuharibu ushahidi” akasema
Dr Fabian
“Tutafanya hivyo
mheshimiwa rais” akasema
Ruby
“Jambo lingine.Jana
tulizungumza kuhusu namna
ya kuviondoa vikosi vya
Marekani hapa nchini na
tulikubaliana kwamba
tuwaondoe kimya kimya kwa
kukata kile ambacho
wamekifuata yaani
mafuta.Damu yote hii
iliyomwagika ya waganda na
watanzania ni kwa sababu ya
mafuta hivyo pale
watakapoyakosa hawatakuwa
na sababu ya kuendelea
kuviweka vkosi vyao hapa
Tanzania na Uganda
wataviondoa mara
moja.Tulikubaliana kulipua
sehemu ya bomba la mafuta”
akasema Dr Fabian na
kufungua droo ya kabati
akatoa karatasi kubwa
akaiweka mezani.Ilikuwa ni
ramani ya bomba la mafuta
kutoka nchini Uganda hadi
Tanga Tanzania.
“Hii ndiyo ramani ya
bomba la mafuta kutokea
Uganda hadi
Tanga.Ninawakabidhi ninyi
jukumu hili.Mtaipitia ramani
hii na kuchagua sehemu
ambapo mtalipua sehemu ya
bomba.Kazi hiyo nataka
ifanyike usiku wa leo.Sitaki
hadi asubuhi ya kesho
Marekani waendelee kuchota
mafuta kwani baada ya kulipua
kipande hicho mafuta
yatafungwa na wamarekani
hawatapata kitu tena hivyo
hawatakuwa na sababu ya
kuendelea kuwepo hapa
nchini.Nadhani mmenielewa
vijana wangu”
“Tumekuelewa
mheshimiwa Rais na
tunakuahidi kazi nzuri”
akasema Ruby
“Nawashukuru sana.Muda
wowote mtakapohitaji msaada
wa aina yoyote nijulisheni
haraka sana” akasema Dr
Fabian kisha wakaagana Ruby
na Gosu Gosu wakaondoka.
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Saa mbili za asubuhi kwa
saa za Marekani John Pasero
anayefanya kazi CIA aliwasili
katika makazi ya makamu wa
Rais Mark Piller.Alishuka
garini na kuelekea ndani
ambako makamu wa Rais
alikuwa anajiandaa kuelekea
ofisini kwake.Wakasalimiana
halafu John akatoa bahasha na
kumpatia makamu wa Rais
“Ile kazi yote uliyonituma
iko humu” akasema John
“Ahsante sana
John.Umekwisha ipitia na
kuthibitiosha kwamba ni
halisi?
“Ndiyo nimeipitia na
kujiridhisha ni halisi”akasema
John
“Sitaki kujua namna
ulivyoweza kuipata orodha hii
lakini naamini imechukuliwa
kitaalamu sana kiasi kwamba
haitakuwa na matatizo upande
wetu” akasema Mark Piller
“Usihofu
mheshimiwa,jambo hili
limefanywa kwa umakini
mkubwa sana na hakuwezi
kukawa na tatizo lolote
kwetu.Tunao mawakala wetu
ndani ya Mossad ambao
ameweza kufanikisha orodha
hii ikapatikana” akasema John
“Safi sana John” akasema
Mark Piller na kuelekea ndani
akatoka na bahasha iliyokuwa
na fedha akamkabidhi John
wakaagana akaondoka
zake.Mark Piller akaenda
katika ofisi yake ndogo
akaifungua ile bahasha
aliyopewa na John ndani yake
kulikuwa na diski mweko
akaishika mkononi akaitazama
“Tunafanya kitu cha hatari
sana hiki.Hawa majasusi
wakijulikana watakuwa katika
hatari kubwa ya kuuawa lakini
lazima tufanye hivi kwa
maslahi ya nchi yetu” akawaza
Mark Piller na kuirejesha ile
diski mweko katika bahasha
akaiweka katika mfuko wa
ndani wa koti halafu
akajiandaa kuelekea ofisini.
Mark Piller alipowasili
ofisini kwake, kitu cha kwanza
alichokifanya ni kwenda
kuonana na rais William
Washington
“Mark kuna maendeleo
yoyote toka tulipoachana?
Akauliza Rais William
“Maendeleo ni makubwa
mheshimiwa
Rais.Nimefanikiwa kuipata ile
orodha tuliyoihitaji” akasema
Mark na Rais William
akashusha pumzi
“Safi sana.Lakini imekuwa
mapema sana”
“Nimemtumia mmoja wa
vijana wangu ndani ya CIA
kuipata orodha hiyo.CIA tunao
mawakala wetu ndani ya
Mossad hivyo haikuwa kazi
ngumu kuweza kuipata orodha
hiyo” akasema Mark Piller na
kuitoa ile bahasha
akamuonesha Rais William
“Kila kitu kiko humu”
akasema Mark
“Mark hili ni jambo gumu
sana lakini lazima tulifanye.Ila
bado ninatoa angalizo kwamba
kila juhudi lazima ifanyike ili
kuhakikisha Israel
hawafahamu kama sisi ndio
tuliowaanika majasusi wao”
akasema Rais William
“Narudia tena
kukuhakikishia mheshimiwa
Rais kwamba kila kitu
kimeandaliwa vizuri na
hakutakuwa na tatizo lolote
kwa upande wetu”
“Sawa Mark.Tulipoachana
nilizungumza na Rais wa
Tanzania lakini mazungumzo
yetu hayakwenda
vizuri.Amekataa timu ya
wachunguzi wetu kwenda
kuchuguza shambulio lile
akadai watalichunguza wao
nikajikuta nikipandwa na
hasira na hatukupata muafaka
wowote lakini hadi muda ule
hawakuwa wamepata taarifa
zozote za nani wameshambulia
kambi yetu” akasema Rais
William
“Mheshimiwa
Rais,hukupaswa kutumia
hasira na wala Rais wa
Tanzania hapaswi kuona kama
vile tunalazimisha watu wetu
waende kufanya
uchunguzi.Utakapozungumza
naye wakati mwingine itabidi
ujishushe kidogo umuombe
msamaha kama kuna maneno
ulimtamkia ambayo si mazuri”
“Hapana Mark siwezi katu
kujishusha kwa mtu mweusi !
akasema Rais William kwa
sauti ya ukali
“Mheshimiwa Rais sisi
ndio tunaotafuta kitu,hivyo
lazima tutumie kila aina ya
mbinu.Tumfanye Rais wa
Tanzania awe rafiki yetu na
tujizuie kutumia kauli za
kumshinikiza afanye vile
tunavyotaka sisi.Twende naye
taratibu” akasema Mark Piller
na Rais William hakujibu kitu
na mara ujumbe ukaingia
katika simu ya Mark
akaufungua akausoma
“Mheshimiwa Rais
nitakujulisha baadae kile
kinachoendelea.Kuna mtu
ananisubiri ofisini” akasema
Mark Piller na kutoka
akaelekea ofisini kwake
“David Walker” akasema
Mark Piller baada ya kuingia
ofisini kwake na kumkuta
David Walker akimsubiri.
“Karibu sana David”
akasema Mark Piller
“Ahsante sana Mark”
akajibu David na Mark
akafunga mlango ili aweze
kuzungumza na David
“Mark nimepita hapa mara
moja kukupa mrejesho wa kile
kinachoendelea hadi muda
huu” akasema David na
kunyamaza kidogo
“Mpaka sasa bado hatuna
taarifa zozote za kuhusiana na
kirusi kilipo.Nimekuwa na
mawasiliano ya karibu na
mkuu wa majeshi na bado
taarifa ya mwisho ni ile ile
kwamba mwenye taarifa zote
za kuhusiana na kirusi ni
Jenerali William.Yeye ndiye
aliyekabidhiwa kirusi hicho
baada ya Sattar kuwasili Dar es
salaam.Tumekwamia hapo
kwani watu wetu wote
hawajulikani
walipo.Tumejaribu
kuwasiliana na viongozi wa IS
nao pia hawajui watu wao
akina Assad Ismail wako
wapi.Wote wametoweka.Mark
tunahitaji sana kujua mahala
walipo hawa watu.Tunahitaji
kujua kama ni miongoni mwa
watu waliofariki au
vipi.Nimepita hapa kwako
nikiamini labda ninaweza
kupata taarifa ya tofauti na ile
ya mkuu wa majeshi” akasema
David Walker macho yake
yakiwa mekundu na hii ni
kutokana na kutokulala
usiku.Mark Piller akavuta
pumzi ndefu na kusema
“Ni kweli usiku mzima
nilikuwa na rais na viongozi
wengine wa vyombo vya ulinzi
na usalama tukipokea taarifa
mbali mbali kutoka
Tanzania.Tayari miili yote ya
wanajeshi imekwisha
tambuliwa lakini hakuna mwili
wa Jenerali William,Sattar
wala Assad Ismail” akasema
Mark Piller
“Mungu wangu ! Nini hiki
kimetokea? akasema David
Walker na kukuna kidevu.
“Rais amezungumza na
Rais wa Tanzania kwa simu
akamuuliza kuhusiana na
uchunguzi wa jambo hili lakini
mpaka sasa hakuna taarifa
yoyote waliyoipata ya nani
walioshambulia kambi yetu”
akasema Mark Piller
“Mark hili suala linaumiza
mno vichwa vyetu na hasa
suala la kupotea kwa Jenerali
William na akina Sattar.Sisi
hatutakiwi kupoteza muda
kufuatilia nani kashambulia
kambi au nani kaua sisi
tunachohitaji ni kujua kirusi
kiko wapi? Je kiko
salama?Mtu pekee wa kutupa
majibu ya maswali hayo ni
Jenerali William ambaye
hajulikani alipo hadi hivi
sasa.Nguvu kubwa tuielekeze
hapo kujua mahala alipo
Jenerali William” akasema
David Walker na ukimya
mfupi ukapita
“Mark itumie nafasi yako
kama makamu wa rais
kuhakikisha tunafahamu
mahala alipo Jenerali
William.Bila kumpata huyu
mtu misheni yetu itakuwa
imeharibika.Kama kuna
ulazima wa kutuma hata kikosi
maalum kwenda kumsaka
shughulikia hilo! Mshinikize
Rais aongeze mbinyo kwa
serikali ya Tanzania hata kama
ikibidi kutumianguvu basi
itumike ili kumpata Jenerali
William ! Kama tuliweza
kumpata na kumuua Osama
Bin Laden hatuwezi
kushindwa kumpata mtu wetu
katika nchi kama Tanzania !
akasema David Walker
“David kuna kitu
ninakihisi.Ni vipi kama
Jenerali William amekwenda
na akina Sattar kuanza kazi ya
usambazaji wa kirusi?
Nimekuwa na hisia hizo
kwamba yawezekana hakutaka
kupoteza muda akaamua
kukisambaza kirusi hicho
mara moja kwani ukiangalia
wote wametoweka tena kwa
wakati mmoja” akasema
Mark.David akafikiri kidogo na
kusema
“Hilo linawezekana lakini
nyumba aliyokuwa anaishi
tumeambiwa nayo imevamiwa
na watu wote kuuawa.Je
aliondoka kabla wavamizi
hawajafika? Halafu taarifa
inasema kwamba
anayekosekana si Jenerali
William peke yake bali pia
kuna wafanyakazi wengine
wawili waliokuwa
wakihudumu katika nyumba
hiyo aliyokuwa akiishi nao pia
hawajulikani walipo.Kama
amekwenda kusambaza kirusi
je amekwenda nao? Kama
amekwenda nao ni kwa
madhumuni gani? Walikuwa
na umuhimu wowote? Halafu
jukumu la kusambaza kirusi
halikuwa la Jenerali
William.Yeye jukumu lake
lilikuwa ni kumpokea Sattar na
kumkabidhi kwa Assad na
kuwasaidia waweze
kufanikisha usambazaji.Mark
mpaka hapo bado unaamini
Jenerali William amekwenda
kusambaza kirusi?Akauliza
David Walker na Mark Piller
akazama mawazoni kwa muda
halafu akasema
“Sina hakika David”
akajibu Mark Piller
“Mark kazi kubwa
tuliyonayo ni kuhakikisha
tunajua mahala alipo Jenerali
William.kama nilivyokwambia
kwamba unapaswa kuitumia
vyema nafasi yako kuhakikisha
tunalifahamu hili” akasema
David
“Nitajitahidi.Vipi kuhusu
mpango wa kumteka Habiba
Jawad unaendeleaje? Akauliza
Mark
“Tayari kuna timu
imetumwa Riyadh na…” David
akatazama saa yake ya
mkononi
“Naamini hadi muda huu
watakuwa tayari wamekwisha
fika”
“Vizuri sana.Mpango wa
kumteka umekaaje? Lazima
uwe ni mpango ulioandaliwa
kipekee kabisa ili isijulikane
kama sisi ndio tuliomteka
Habiba.Nilitoa angalizo awali
kwamba Habiba ana
mahusiano ya karibu na
mfalme wa Saudi Arabia
ambaye ni mshirika mkubwa
wa Marekani”
“Tumeuandaa mpango
vizuri Mark usihofu.Habiba
hafahamu chochote hivi
sasa.Nitampigia simu na
kumtaka aende sehemu Fulani
akakutane na mtu mwenye
ujumbe muhimu na akienda
huko atatekwa na kupelekwa
katika ubalozi wetu jijini
Jerusalem.Baada ya
kumpeleka Jerusalem
tutawaita Mossad na
watathibtisha kwamba tunaye
Habiba ili waweze kuharakisha
zoezi la kumuua Abu Zalawi”
“Sawa David.Utanijulisha
kile kitakachokuwa
kinaendelea katika mipango
yote.Mimi nitashughulikia
suala la Jenerali
William.Halafu kuna suala
lingine ambalo nimekuwa
nikilifikiria.Je IS hawawezi
kuwa wanahusika na
shambulio hili? Akauliza Mark
Piller
“Kwa nini umehisi hivyo
Mark? David naye akauliza
“Kwa namna shambulio
lilivyotokea inaonesha wazi
kwamba limefanywa na watu
waliokuwa wamejiandaa
vilivyo tena kwa silaha
nzito.Sina hakika lakini
ninahisi yawezekana IS
wamehusika katika
shambulkio hili na ndiyo
maana Assad na watu wake
wote wametoweka na hatujui
mahala walipo” akasema Mark
Piller.David Walker akafikiri
kwa muda na kusema
“IS wana sababu yoyote ya
kufanya hivyo? Wamekuwa ni
washirika wetu wa muda
mrefu.Tumewawezesha kwa
silaha na tunawapa fedha
nyingi kupitia Habiba Jawad”
akasema David walker
“Ni vipi kama nao
wanakihitaji kirusi kwa ajili ya
mipango yao ya kigaidi au hata
kukiuza kwa mataifa
mahasimu zetu ? Akauliza
Mark Piller na ukimya mfupi
ukapita
“Hilo ni wazo la msingi
Mark.Tusilidharau tulifanyie
uchunguzi kwa sababu haiingii
akilini watu wote hawa
wakatoweka kwa wakati
mmoja na hawajulikani
walipo.Yawezekana IS
wametugeuka wakamteka
Jenerali William wakaua
wanajeshi wetu,wakavamia pia
kambi wakaondoka na kirusi”
“Niachie mimi suala hili
nitalifanyia kazi.Hadi jioni ya
leo tutakuwa na majibu ya
kutosha kuhusu suala hili”
akasema Mark Piller na
kuagana na David Walker .
Baada ya David
kuondoka,Mark akachukua
simu anayoitumia kuwasiliana
na Habiba akampigia
“Hallo Mark Piller”
akasema Habiba
“Habiba habari ya muda
huu”
“Nzuri Mark.Habari za
huko kwenu?
“Huku bado mambo si
mazuri.Mpaka sasa hakuna
taarifa yoyote kuhusiana na
tukio la Tanzania.Kibaya zaidi
hakuna taarifa zozote za
kumuhusu Jenerali William au
akina Sattar” akasema Mark
“Mark tuvute subira
tutafahamu walipo.Kama
hawapo katika orodha ya watu
waliouawa basi wapo sehemu
Fulani.Mimi pia ninaendelea
na ule uchunguzi kama IS
wanahusika katika shambulio
hilo nikipata chochote
nitakujulisha” akasema
Habiba
“Jitahidi Habiba ili
tulifahamu jambo hili kwani
kadiri muda unavyozidi
kwenda ndivyo suala hili
linavyozidi kuwa
gumu.Tuachane na hilo
nimekupigia kwa ajili ya
mambo mawili.Kwanza ni
kukupa taarifa kwamba ile
orodha nimeipata”
“Umeipata? Habiba
akauliza
“Ndiyo
nimeipata.Nitakutumia muda
si mrefu.Jambo la pili ni
kuhusiana na ule mpango wa
kukuteka” akasema Markna
kumuelezea Habiba mpango
wote ulivyoandaliwa
“Mark nakushukuru sana
kwa taarifa hizo.Kuhusu
usalama wangu usiwe na hofu
nimekwisha jiandaa vya
kutosha.Kitu cha msingi
nitumie hiyo orodha nianze
kuifanyia kazi” akasema
Habiba
“Nitakutumia muda si
mrefu Habiba” akasema Mark
Piller na kuagana na Habiba
kwa miadi ya kuwasiliana tena
baadae kupeana taarifa za kile
kinachoendelea.
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa kumi na mbili za jioni
ndege ya Rais wa Tanzania
iliyombeba Nawal iliwasili
jijini Riyadh katika uwanja wa
ndege ambao hutumiwa na
Habiba na familia yake.Nawal
aliwashukuru marubani wa
ndege ile kwa kumfikisha
salama Riyadh na kuwatakia
safari njema ya kurejea
Tanzania.Uwanjani pale
alipokewa na wasaidizi wa
Habiba akaondoa kuelekea
katika makazi ya Habiba
Jawad.
“Karibu tena
Nawal.Nimefurahi mno kuiona
tena sura yako.Wewe na
Mathew ni watoto pekee nilio
baki nao hivyo kukuona tena
ni faraja kubwa mno kwangu”
akasema Habiba Jawad
akimkaribisha Nawal katika
makazi yake baada ya kuwasili
akitokea Tanzania
“Hata mimi nimefurahi
sana kuonana nawe tena
mama Habiba” akasema
Nawal.
“Nawal najua umechoka
na safari ndefu lakini pamoja
na uchovu wa safari nataka
ukajiandae kuna kazi ya
kufanya usiku huu” akasema
Habiba
“Usijali mama mimi nipo
tayari kwa kazi muda
wowote.Niambie ni kazi gani
natakiwa kuifanya” akasema
Nawal
“Nilikueleza kuhusu
mpango wa G20 wa kutaka
kumua Mathew
Mulumbi.Mpango wenyewe
tayari umeanza.Ili Israel itume
majasusi wake wamuue
Mathew wanataka CIA
iwathibitishie kwamba niko
katika mikono yao na baada ya
kumuua Mathew
nitakabidhiwa kwao.Tayari
majasusi wamekwisha tumwa
kuja kuniteka na kunipeleka
Israel katika ubalozi wa
Marekani ambako nitakaa
hapo kabla ya kukabidhiwa
kwa Israel lakini CIA mpango
wao ni kuniua kabla ya
kunikabidhi kwa Mossad”
akasema Habiba
“Nimepigiwa simu na
David Walker jioni hii
amenipa maelekezo ya kwenda
kukutana na hao majasusi wa
CIA waliotumwa kuja
kuniteka.Hawafahamu kama
tayari ninafahamu mipango
yao.Kazi uliyonayo ni
kuhakikisha unawamaliza
majasusi hao wa CIA” akasema
Habiba na kumuelezea Nawal
namna mpango utakavyokuwa
“Usijali mama utakuwa
salama.Hesabu jambo hilo
limekwisha malizika” akasema
Nawal
“Ahsante Nawal.Jambo
lingine ni kwamba Mathew
alihitaji orodha ya majasusi wa
Mossad walioko Iran na tayari
nimeipata orodha hiyo
nitamtumia ili iweze
kumsaidia” akasema Habiba
“Anaendeleaje Mathew?
Nawal akauliza
“Mathew anaendelea
vizuri na baada ya kuipata
orodha hiyo ndipo
atakapoanza rasmi kazi
yake.Mambo mengi
utayafahamu utakapokutana
naye” akasema Habiba na
Nawal akaenda
kujiandaa.Habiba akaelekea
ofisini kwake na kumpigia
simu Vahid Ghorbani.
“Habari yako Vahid”
akasema Habiba baada ya
Vahid kupokea simu
“Habiba naomba nikuweke
wazi mapema kabisa kwamba
kama unahitaji msaada
kuhusu Abu Zalawi utafute
mtu mwingine wa kukusaidia
lakini mimi sitaki tena kuwa
na ukaribu na Yule gaidi”
akasema Vahid
“Vahid ninahitaji msaada
wako na yawezekana hii ikawa
ni mara ya mwisho lakini ni
muhimu mno”
“Unahitaji nini Habiba?
Akauliza Vahid
“Kuna kitu nahitaji
umfikishie Abu Zalawi”
“Habiba utanisamehe
sitaki tena kwenda kule.Sitaki
kuonekana mara kwa mara
ninazungumza na Yule mtu
kwani hata mimi ninaweza
kuanza kuhisiwa vibaya”
“Nalifahamu hilo Vahid
lakini naomba
unisaidie.Nakuhakikishia
kwamba hii itakuwa ni mara
ya mwisho na hutanisikia
nikikuomba tena msaada.Ni
jambo la muhimu mno”
akasema Habiba.Vahid
akafikiri kidogo halafu
akauliza
“Nini unataka nimpelekee
Abu Zalawi?
“Kuna faili nitakutumia
nataka uliweke katika diski
mweko na umfikishie Abu
Zalawi leo hii hii” akasema
Habiba
“Linahusu nini hilo faili?
Akauliza Vahid
“Vahid utanisaidia au vipi?
Akauliza Habiba
“Tuma hilo faili
nitalifikisha kwa Abu Zalawi
ila nakuomba Habiba hii iwe
ni mara ya mwisho kunituma
kwa Abu Zalawi.Mimi ni mtu
mwenye heshima zangu na
sitaki kuanza kuhisiwa vibaya
kuwa ninashirikiana na
magaidi”
“Nakuahidi hii itakuwa
mara ya mwisho” akajibu
Habiba
“Sawa tuma hilo faili”
akasema Vahid na Habiba
akamtumia faili lenye orodha
ya majasusi wote wa Mossad
walioko nchini Iran.
Vahid hakutaka
kusumbuka kulifungua faili lile
akaliweka katika diski mweko
na kumpigia simu Faqir
akamueleza kwamba anahitaji
kuonana na Abu Zalawi.Fakiri
akamuahidi kumfuata pale
nyumbani kwake ili aweze
kuongozana naye kuelekea
katika nyumba aliko Mathew.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 4
“Faqir ahsante sana kwa
msaada huu mkubwa”
akasema Vahid akiwa garini na
Faqir aliyemfuata nyumbani
kwake kama alivyomuahidi
“Usijali mzee” akasema
Faqir aliyekuwa katika
usukani.Vahid akatoa bahasha
katika mfuko wa koti na
kumpatia Faqir
“Hii ni ahsante yangu kwa
msaada wako” akasema Vahid
“Mzee hakuna haja.Huu ni
wajibu wangu kukusaidia”
akasema Faqir
“Faqir naomba uchukue
ahsante hii” akasisitiza Vahid
na Faqir akachukua bahasha
ile iliyokuwa na fedha.
Walifika katika nyumba
alimo Mathew Mulumbi Faqir
akaelekeza kamera zote
kuzimwa kisha akamuongoza
Vahid hadi katika chumba cha
Mathew aliyekuwa amejilaza
kitandani.Faqir akatoka mle
ndani na kuwaacha Vahid na
Abu Zalawi.
“Abu Zalawi habari yako”
“Nzuri mzee Vahid karibu
tena”
“Ahsante.Nimekuja tena
kukuona na hii itakuwa ni
mara ya mwisho kuniona
hapa” akasema Vahid na kutoa
ile diski mweko akamkabidhi
Mathew
“Habiba Jawad
amenituma nikuletee mzigo
huu” akasema Vahid.Mathew
akaitazama ile diski mweko
halafu akasema
“Nashukuru sana mzee
kwa kunifikishia mzigo huu
muhimu.Kama hutojali
ninaweza kuzungumza na
Habiba Jawad? Akauliza
Mathew.Vahid akatoa simu na
kumpigia Habiba halafu
akampa Mathew ile simu
“Hallo Vahid” akasema
Habiba
“Mama Habiba unaongea
na Abu Zalawi” akasema
Mathew
“Mathew unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri
mama.Wananitunza vizuri
ninapata kila ninachohitaji”
“Vizuri sana.Naamini
Vahid amekufikishia mzigo”
“Nimeupata mama
nashukuru sana”
“Sawa Mathew nakutakia
kila la heri na pale
utakapohitaji chochote usisite
kunijulisha nitakusaidia kadiri
niwezavyo”
“Nashukuru sana.Baada ya
kuipata orodha hii sasa
ninaanza rasmi kazi yangu”
“Sawa Mathew.Nawal
tayari amekwisha fika hapa
akitokea Tanzania na kesho
atakuja Tehran.Utaonana naye
hiyo kesho” akasema Habiba
na kuagana na Mathew
ambaye alimrejeshea Vahid
simu yake
“Nashukuru sana mzee”
akasema Mathew na Vahid
hakutaka maongezi zaidi
akamuaga Mathew na
kuondoka.
“Habiba amefanya jambo
la maana sana kunipatia
orodha hii” akawaza Mathew
baada ya Vahid kuondoka.
************
Saa mbili kasoro dakika
kumi na saba,gari dogo
liliwasili katika geti la nyumba
alimo Mathew
Mulumbi.Kutoka katika lile
gari akashuka mtu mmoja
aliyevalia nadhifu sare za
uhudumu wa hoteli akaenda
kugonga geti la nyumba ile na
mmoja wa walinzi akafungua
mlango mdogo akatoka
wakasalimiana na muhudumu
Yule wa kike mwenye
tabasamu la kuvutia
“Nimeagizwa kuleta
chakula hapa” akasema Yule
muhudumu aliyejitambulisha
kwa jina la Munira.
“Chakula? Akauliza Yule
mlinzi
“Ndiyo” akajibu Munira
“Nani amekutuma ulete
chakula hapa? Akauliza Yule
mlinzi
“Yametolewa maelekezo
na kiongozi mmoja wa serikali
katika hoteli yetu kuwa
chakula kiletwe hapa” akasema
Munira
“Kiko wapi hicho chakula?
Akauliza Yule mlinzi na
Munira akaenda katika gari
akafungua mlango na maboksi
ya chakula yakaonekana.
“Subiri kidogo” akasema
Yule mlinzi na kurejea ndani
akawafuata wenzake
waliokuwa sebuleni wakicheza
karata akawaeleza kuhusu
chakula kile kilicholetwa.Wote
wakabaki wanashangaa na
kujiuliza nani ametuma
chakula kile.Baada ya
kujadiliana kwa muda
wakakubaliana wachukue
chakula kile wakiamini labda
kimetumwa na mmoja wa
wakubwa zao.Mchezo wa
Karata ukaishia pale wakatoka
kwenda kuchukua chakula kile
kilicholetwa.Munira
hakuruhusiwa kuingia ndani
akaagana nao na
kuondoka.Maboksi yale ya
chakula yakapelekwa sebuleni
na kufunguliwa.Wote
wakapatwa na mshangao
mkubwa kwa vyakula
walivyovikuta ndani ya makosi
yale.Kulikuwa na chakula ghali
sana kinachoitwa Saffron na
kingine ni Cavier.Walibaki
wanashangaa kiongozi gani
aliyeweza kuwanunulia
chakula ghali namna ile.
“Hakuna haja ya
kushangaa ndugu zangu.Hii ni
neema imetuangukia hivyo
tukae mezani tuendelee
kula.Sijawahi kuonja hiki
chakula Saffron katika maisha
yangu leo itakuwa mara ya
kwanza” akasema mmoja wa
walinzi aliyefahamika kama
Mehdi.
Maandalizi yakafanyika na
wote wakakaa mezani
wakaanza kupata chakula
huku geti likiwa
limefungwa.Hawakuacha hata
mlinzi mmojan je.Hakuna
aliyekuwa na wasi wowote na
usalama wao.Sebuleni
kulitawala vicheko vya furaha
wote wakikifurahia chakula
kile ghali sana
“Jamani mbona tunakula
peke yetu na kumsahau Abu
Zalawi? Akauliza Najib
ambaye huusika na mfumo wa
kamera wa nyumba ile
“Najib anasema kweli.Abu
Zalawi ni mtu muhimu
sana.Anatakiwa aje kujumuika
nasi hapa katika chakula hiki
kitamu” akasema Shams
aliyekuwa kiongozi wa walinzi
usiku ule.Najib akainuka
kwenda kumuita Mathew.
“Abu Zalawi tunaomba
uungane nasi katika chakula”
akasema Najib na Mathew
ambaye alihisi njaa akainuka
wakaelekea sebuleni.Mara tu
walipotembea hatua tatu
baada ya kutoka chumbani
ikasikika sauti ya muanguko
wa viti na sahani.Mathew
akasimama na kumtaka Najib
kusimama.
“Subiri kidogo ! akasema
Mathew na kutega sikio
kusikiliza
“Hakuna kitu Abu Zal….”
“Shhhh !! akasema
Mathew na kumfanyia ishara
anyamaze kimya kisha
akamtaka amfuate wakaanza
kutembea kwa kunyata
kuelekea sebuleni .Nyumba ile
ilikuwa kubwa na yenye
vyumba vingi.
Mara tu walipokaribia
kufika sebuleni wakasikia sauti
kali ikiuliza
“Yuko wapi Abu Zalawi ?!
“Yuko chumbani kwake !
akajibu mmoja wa wale
walinzi.Mwili wa Mathew
ukasisimka.
“Jina lako nani? Akauliza
Mathew
“Naitwa Najib”
“Sikiliza Najib
tumevamiwa.Hawa
waliovamia hapa wananitafuta
mimi.Una bastola? Au kuna
chumba cha silaha humu
ndani?
“Ninayo bastola lakini iko
ofisini kwangu” akajibu Najib
“Naihitaji hiyo bastola ili
niweze kupambana na hawa
jamaa” akasema Mathew kisha
kwa kunyata wakarudi nyuma
na kuelekea katika ofisi ya
Najib
“Kuna kamera ngapi za
ulinzi katika nyumba hii?
Akauliza Mathew akiyaelekeza
macho yake katika runinga
iliyokuwa inaonesha picha
mbali mbali kutoka katika
kamera zinazoizunguka ile
nyumba.
“Kuna kamera kumi na
sita” akajibu Najib
“Nataka kamera ya
sebuleni nijue wavamizi wako
wangapi” akasema Mathew na
Najib akabofya kamera ya
sebuleni na kile kilichokuwa
kinaendelea sebuleni
kikaonekana.Walinzi wawili
walikuwa wamelala chini
wakivunja damu ni wazi
walikuwa
wameuawa.Wavamizi
hawakuweza kuonekana sura
zao walikuwa wamezifunika
kwa kofia maalum za kuziba
uso na kuacha macho pekee.
Jumla yao walikuwa saba mle
ndani.Nje walionekana wawili
wakiwa katika kibaraza
wakiwa na bunduki
Najib alifungua droo ya
meza yake ambamo kulikuwa
na bastola mbili akampatia
Mathew moja naye akabakiwa
na moja.Mathew akaihakikisha
ina risasi za kutosha kisha
wakatoka ndani ya kile
chumba Najib akaanza
kumuelekeza Mathew njia ya
kuelekea sebuleni kwani
nyumba ile ilikuwa na zaidi ya
korido moja.Mara wakasikia
hatua za watu wakielekea
upande ule waliopo
wakajibanza pembeni ya
kabati tupu.Baada ya muda
mfupi wakapita wavamizi
wawili wakiwa
wamemtanguliza mbele
mmoja wa walinzi.
“Hawa jamaa lazima
wanaelekea katika chumba
changu” akasema Mathew na
kutoka mahala walipokuwa
wamejibanza akaanza kunyata
kuwafuata wale jamaa ambao
kama alivyokuwa amehisi
kweli walikwenda hadi katika
chumba cha Mathew.Mlinzi
akakinyonga kitasa na
kuufungua mlango.Mmoja wa
wale jamaa akamrukia mlinzi
teke zito akaangukia ndani ya
kile chumba kisha kwa kasi ya
upepo jamaa wale wakajitoma
ndani.Chumba kilikuwa
kitupu.Mathew hakuwemo.
“Abu Zalawi hayupo katika
hiki chumba.Narudia
tumemkosa Abu Zalawi”
akasema mmoja wa wale
wavamizi aliyekuwa ameweka
sikioni kifaa cha kumuwezesha
kuwasiliana na wenzake.
“Tuonyeshe haraka wapi
alipo Abu Zalawi? Akauliza
mmoja wa wavamizi wale huku
akimuelekezea Yule mlinzi
bastola kichwani akitishia
kumuua
“Chumba chake ni
hiki.Alikuwemo humu ndani
na sijui amekwenda wapi!
Akajibu Yule mlinzi huku
akitetemeka kwa woga.
“Kwa mara ya mwisho
nakuuliza kiko wapi chumba
cha Abu Z…………..”
Hakumaliza sentensi yake
kwani mlango ulipigwa teke
zito ukafunguka na mtu
mmoja akajiviringisha hewani
na kutua mle
chumbani.Wakati akitua
aliwaona wale jamaa namna
walivyokuwa wamesimama na
wakati wakijiuliza nini
kimetokea Mathew
akazunguka mateke mawili
mfululizo na wale jamaa
wawili wote wakajikuta
chini.Mmoja wa wale majasusi
akainuka haraka lakini macho
ya Mathew yalikuwa makali
kama macho ya tai yalikwisha
muona Yule jamaa.Kwa kasi ya
ajabu akaruka juu na kwa
kutumia mguu wake wa kulia
akamtandika Yule jamaa teke
kali katika mkono wake
uliokuwa umeshika
bastola,akiwa bado hewani
mguu wake wa kushoto ambao
huutumia mara chache katika
mapigano kutokana na
umuhimu wake ukatua katika
shingo ya Yule jamaa ambaye
alijibamiza ukutani kwa
kishindo na kuanguka
chini.Mathew akatua chini na
kugeuka haraka sana
akamuona Yule jamaa
mwingine akiwa ameizinga
bastola akimuelekezea lakini
ukasikika mlio wa risasi na
Yule jamaa akaanguka
chini.Mlangoni alikuwa
amesimama Najib akiwa na
bastola.Ndiye aliyempiga risasi
yule jamaa.
“Ahsante Najib” akasema
Mathew na kuiokota bastola ya
yule jamaa aliyempiga
teke,akamfuata akamtazama
alikuwa anatokwa na damu
mdomoni.Hakuwa na dalili za
uhai.Mlinzi Yule aliyekuwa
chini hakuamini kile
kilichokuwa kimetokea mle
ndani.Aliona kama filamu.
“Bastola za hawa jamaa
zote zimefungwa kiwambo cha
kuzuia sauti hivyo basi mlio wa
risasi uliosikika lazima
utawapa mashaka wenzao na
wanaweza wakafika hapa
kujua kile
kinachoendelea.Tunatakiwa
kwenda kuwakomboa wenzetu
walioshikiliwa kule
sebuleni.Kuna mlango
mwingine wa kutokea nje?
Mathew akauliza
“Ndiyo upo mlango wa
nyuma” akajibu Najib kisha
wakatoka ndani ya kile
chumba kila mmoja akiwa na
bastola wakatembea kwa
tahadhari kuelekea katika
mlango wa kutokea upande wa
nyuma wa ile nyumba.Mathew
akawataka Najib na Yule
mlinzi mwingine wajifiche
sehemu na wamuache yeye
akapambane na wale wavamizi
kwani alikwisha tambua uwezo
wao katika mapambano ni
mdogo kuliko wa wale
wavamizi.Mkononi alikuwa na
bastola moja ya wale jamaa
waliowaua ndani ya kile
chumba.
Mbele ya kibaraza
kulikuwa na watu wawili
wakiwa na bunduki
ndogo.Mathew aliyekuwa
amejificha sehemu yenye kiza
akazidungua taa mbili kubwa
zilizokuwa zinamulika sehemu
ya mbele ya ile nyumba.Eneo
la mbele likawa na mwanga
hafifu kutoka katika taa ya
barazani.Wale jamaa wawili
wakastuka sana kwa kile
kilichotokea.Kabla
hawajatafakari nini cha
kufanya Mathew akaizinga
tena bastola na kuachia risasi
mbili akiwalenga wale jamaa
vichwani.Walipoanguka chini
Mathew akatoka mbio
kuelekea katika kibaraza na
kabla hajakifikia mlango
ukafunguliwa wakatoka jamaa
wawili.Mathew hakuwakawiza
akajitokeza na kuachia risasi
zilizompata jamaa mmoja na
mwingine akaurukia mlango ili
kurejea ndani lakini Mathew
alikuwa mwepesi zaidi yake
akamuwahi kwa risasi na
jamaa akaanguka ndani kwa
kishindo kama jiwe huku
akivuja damu.
Kitendo cha mwenzao
kuanguka mle ndani akiwa
anavuja damu kiliwastua
wavamizi watatu waliokuwa
sebuleni wakiwashikilia
mateka walinzi wa ile
nyumba.Kabla hawajafanya
chochote kufumba na
kufumbua Mathew Mulumbi
akiwa na bastola mkononi
akaviringika akitokea nje na
kuingia mle sebuleni huku
macho yake yakizunguka kama
kinyonga na kuwatazama
namna wale wavamizi
walivyokaa mle sebuleni.Kabla
hajatua chini tayari mmoja wa
wale wavamizi alikuwa chini
akivuja damu baada ya
kuchakazwa kwa risasi.Mmoja
wa walinzi baada ya kuwaona
wale wavamizi wote
wameyaelekeza macho yao
kwa Mathew akachomoa kisu
taratibu na kumrukia mmoja
wao akamchoma kisu cha
mgongo akachomoa na
kumchoma tena halafu
akamtandika teke akaanguka
chini.Walinzi wote
wakasimama na kunyakua
silaha zao.Alibakia mvamizi
mmoja akaielekeza bastola
kichwani na kujipiga risasi
akaanguka chini.Mathew
akiwa ameongozana na walinzi
wale wakatoka nje ya ile
nyumba na kuanza kuikagua
kama kuna mtu mwingine
aliyebakia lakini hakukuwa na
mtu yeyote.
“Hawa jamaa walikuja bila
gari? Akauliza mmoja wa
walinzi
“Hawakuwa peke
yao.Lazima walikuwa na
wenzao ambao baada ya
kugundua wenzao waliokuwa
ndani wamezidiwa nguvu na
kuuawa wakakimbia” akasema
Mathew
Walirejea ndani na
kuwatazama wale walinzi
wawili waliokuwa wamelala
chini wamepigwa risasi,tayari
awlikuwa wamekufa.Simanzi
kubwa ikatanda.Wakati
wakihuzunika Mathew
akaanza kuwapekua wale
wavamizi kuona kama
angepata kitu chochote kutoka
kwao lakini hawakuwa na kitu
zaidi ya kuvaa vifaa vya
mawasiliano.
“Hawa ni wale majasusi
wa Mossad waliotumwa kuja
kuniua.Kazi imeanza” akawaza
Mathew na kumuelekeza
Shams kutoa taarifa kwa Faqir
kumjulisha kile kilichotokea.
RIYADH – SAUDI ARABIA
Gari la kifahari la
Mercedece Benz likiendeshwa
na Habiba Jawad liliwasili
katika hoteli ambako
alielekezwa na David Walker
kwenda kukutana na mtu
aliyepewa ujumbe muhimu
ampelekee.Usiku huu Habiba
alikuwa peke yake garini kwani
David alimtaka asiongozane na
walinzi wake au mtu yeyote
anapokwenda kuonana na
huyo mtu kwani ni mtu
ambaye hataki kuonekana na
watu.Habiba hakuwa na wasi
wasi hata kidogo,akashuka
garini na kuelekea katika
sehemu ya chakula
akasalimiana na watu kadhaa
waliokuwa wanamfahamu
aliowakuta pale hotelini halafu
akatoka na kuelekea katika
lifti.Lengo la Habiba kupita
sehemu ya chakula ni kumpa
ishara Nawal aliyekuwa katika
mojawapo ya meza akipata
kinywaji taratibu .Nawal alikaa
sehemu ambayo angeweza
kumuona kila aingiaye na
alimuona Habiba Jawad mara
tu alipoingia
Habiba Jawad akaelekea
katika lifti akapanda na
kuelekea ghorofa ya kumi na
sita ambako ndiko alielekezwa
kukutana na mtu huyo
mwenye ujumbe
maalum.Alishuka katika lifti
na kuelekea katika chumba
alichoelekezwa.Wakati akipiga
hatua kuelekea katika chumba
hicho Nawal alikuwa nyuma
yake kwa mbali kidogo
akimfuata taratibu.Usiku huu
Nawl alivaa mavazi ambayo
haingekuwa rahisi
kumtambua.
Habiba alibonyeza kengele
ya mlango wa chumba
alichoelekezwa na mlango
ukafunguliwa.Wakati mlango
ukifunguliwa Nawal alikuwa
anapita na kuchungulia ndani
akamuona mtu mmoja
aliyekuwa amevaa suti ya
bluu.Habiba akakaribishwa
ndani.
“Habiba Jawad karibu”
akasema Yule jamaa
aliyekuwamo mle chumbani.
“Habari yako” akasema
Habiba
“Nzuri Habiba.Karibu
uketi”
“Sina muda mrefu
hapa.Nimefuata ujumbe
wangu” akasema Habiba
“Sawa karibu uketi”
akasema Yule jamaa.Habiba
alikuwa amevaa kifaa cha
kunasa mawasiliano ambacho
kilimuwezesha Nawal
kufuatilia mazungumzo yake
na Yule jamaa
Habiba akaketi sofani na
Yule jamaa akaenda katika
meza akafungua sanduku dogo
akaanza kutoa makaratasi na
kuyaweka pembeni kana
kwamba kuna karatasi
anazitafuta.Wakati akipekua
mle sandukuni akapeleka
mkono na kubonyeza kifaa
Fulani kidogo halafu
akalifunga sanduku na
kuchukua makaratasi Fulani
akayaweka katika meza ndogo.
“Kuna ujumbe nimetumwa
nikufikishie.Ni ujumbe
muhimu mno na wa siri kubwa
ndiyo maana ulipewa
maelekezo uje peke yako bila
walinzi kwani sitaki kujulikana
kama nimeonana nawe”
akasema Yule jamaa ambaye
hakuwa amejitambulisha jina
lake.
Wakati akiyapanga yale
makaratasi mara mlango
ukafunguliwa wakaingia watu
wanne na bila kuongea
chochote Habiba akakamatwa
na kuwekewa kitambaa cheupe
puani baada ya muda
akapoteza fahamu.
Nawal aliyekuwa
amejibanza katika kona
akiyaelekeza macho kule
katika chumba alimoingia
Habiba,aliuona mlango wa
chumba kinachotazamana na
kile alimoingia Habiba
ukifunguliwa wakatoka watu
wanne na kuingia katka
chumba alimo Habiba.
“Kazi imeanza” akawaza
halafu akatoka pale mahala
alipokuwa akaanza kuelekea
katika chumba walimoingia
wale jamaa ambamo ndimo
alimo Habiba Jawad.Gauni
refu alilokuwa amelivaa
akalifungia kiuononi halafu
akachomoa bastola yake
iliyofungwa kiwambo cha
kuzuia sauti akausogelea
mlango
Mle ndani ya chumba wale
jamaa wakajiandaa kumbeba
Habiba ili kumtoa ndani ya
kile chumba.Jamaa mmoja
akaufungua mlango kwa lengo
la kuchungulia nje kama kuna
mtu katika korido.Mara tu
alipofungua mlango na kutoa
kichwa alikutana na teke zito
toka kwa Nawal lililomrejesha
ndani akaangukia meza ya
kioo ikavunjika.Kwa kasi ya
kimbunga Nawal akajitoma
ndani.Kilikuwa ni kitu cha
ghafla sana ambacho wale
jamaa hawakuwa
wamekitarajia hivyo Nawal
hakupoteza muda akaanza
kugawa dozi ya risasi kutoka
katika bastola yake.Hakuna
aliyekuwa amejiandaa kwa
shambulio hivyo Nawal
alimiliki mchezo na hakuna
aliyepata nafasi ya kuchomoa
bastola yake.Ndani ya sekunde
chache chumba kilikuwa
kimya.Wale jamaa wote
walikuwa chini wakivuja
damu.Wote walikuwa na
matundu ya risasi katika
mapaji yao ya uso.Baada ya
kumaliza mchezo ule Nawal
akachukua chupa Fulani
ndogo kutoka mfukoni
akaifungua na kumuwekea
Habiba puani baada ya muda
Habiba akaanza kupiga chafya
mfululizo na kuzinduka.
“Pole sana
mama.Unajisikiaje? akauliza
Nawal.Habiba akazungusha
macho mle chumbani
akawaona wale jamaa waliolala
chini wakivuja damu
“Ahsante Nawal” akasema
Habiba.
“Mama tunatakiwa
kuondoka mahala hapa haraka
sana kwani tayari mauaji
yamekwisha fanyika humu”
akasema Nawal na kumsaidia
Habiba kunyanyuka
“Una hakika hakuna
aliyesalia? Akauliza Habiba
“Nmewamaliza wote
hakuna aliyebaki” akajibu
Nawal kisha wakatoka ndani
ya kile chumba mlimojaa
harufu ya damu wakaenda
kupanda lifti wakashuka
chini.Nawal akaushika usukani
wakaondoka mahala pale
kurejea nyumbani.
Mara tu baada ya kufika
nyumbani Habiba akampigia
simu Mark Piller akamjulisha
kwamba lile zoezi la kumuua
limeshindwa kufanikiwa.
“Nafurahi kusikia uko
salama Habiba.Hata hivyo huu
ni mwanzo wa mapambano
mapya.G20 wataendelea
kukusaka hadi wahakikishe
wamekupata ili Mossad
waweze kuendelea na mpango
wa kumuua Abu
Zalawi.Ninashauri uondoke
Riyadh kwa muda ukajifiche
sehemu Fulani hadi pale
mambo yatakapotulia.Niko
tayari kukusaidia kwa hilo
Habiba.Ninasema hivyo kwa
sababu bado tunakuhitaji
sana.Wewe ndiye kiungo
muhimu kati yetu na Abu
Zalawi.Sitaki jambo lolote
likupate Habiba ndiyo maana
nikaamua kukupa siri zote za
mipango ya G20 juu yako”
akasema Mark Piller
“Mark ninakushukuru
sana kwa yote lakini suala la
kuondoka na kwenda kujificha
halimo kichwani
mwangu.Ningeweza kufanya
hivyo lakini siwezi
kukimbia.Nitaendelea kuwepo
hapa hapa Riyadh na mipango
yote itakwenda kama
kawaida.Usiwe na wasiwasi
wowote kuhusu Abu Zalawi
atamaliza misheni yake salama
hata kama sintakuwepo”
akasema Habiba
“Habiba bado ushauri
wangu unabaki ule ule
kwamba uondoke hapo Riyadh
uende mahala
ukajifiche.Narudia tena
ninaweza kukusaidia kwa
hilo”akasema Mark Piller
“Huna haja yakunisaidia
Mark kama ninataka kukimbia
na kwenda kujificha ninaweza
kufanya hivyo muda wowote
bila msaada wako lakini kwa
sasa siwezi kukimbia.Mark
naomba tujielekeze zaidi
katika misheni ya Abu Zalawi
tuachane na hili suala la
kutoroka.Endelea kufutailia
mipango yote ya G20 na
unijulishe” akasema Habiba na
kuagana na Mark Piller
“Siwezi kukimbia na
kwenda kujificha kwani kifo
tayari
kinaniandama.Ninamuona
ziraili nyuma yangu hivyo hata
nijifiche katika mwamba gani
lazima nitakufa tu.Kitu
kikubwa ambacho ninajivunia
hata kama nikifa leo ni
kwamba tayari nimetengeneza
bomu litakalokwenda
kuwalipua G20 ambalo ni
Mathew Mulumbi.Huyu nina
uhakika mkubwa sana hata
kama nisipokuwepo kwa hatua
aliyofikia atakwenda
kukisambaratisha kabisa
kikundi cha G20 na dunia
nzima itafahamu udhalimu
unaofanywa na watu hawa”
akawaza Habiba Jawad na
kumfuata Nawal
“Nawal kesho asubuhi
utapanda ndege kuelekea
Tehran tayari kabisa kwa
kumsaidia Mathew Mulumbi”
akasema Habiba
“Mama nina wasi wasi
sana na usalama wako.Hawa
jamaa hawataacha
kukuandama.Kama utaona
inafaa naomba niwepo hapa
kwa siku kadhaa kwa ajili ya
kuhakikisha unakuwa salama”
akasema Nawal
“Nawal usihofu kuhusu
mimi.Kwa sasa tunapaswa
kuelekeza nguvu kubwa
kumsaidia Mathew
Mulumbi.Misheni yake ni
kubwa na yenye manufaa
makubwa hivyo kila aina ya
msaada tuielekeze
kwake.Kesho utakwenda
Tehran mimi nitakuwa
salama” akasema Habiba
TEHRAN – IRAN
Faqir Jahid msimamizi
mkuu wa nyumba zote za siri
zilizo chini ya MOIS alifika
kwa haraka sana baada ya
kupata taarifa kwamba
nyumba ya akina Mathew
imevamiwa na watu
wasiojulikana.
“Poleni sana” Faqir
akawapa pole walinzi
aliowakuta nje
wakilinda.Aliposhuka garini
akakimbilia ndani.Kitu cha
kwanza alichotaka kufahamu
ni kama Abu Zalawi ni mzima
“Abu Zalawi ni mzima
kabisa tumempeleka kwenye
chumba cha mapumziko”
akasema Shams na kuanza
kumuelezea Faqir namna tukio
lile lilivyotokea.Baada ya
kupokea maelezo Faqir
akaelekea katika chumba
alimo Mathew
“Pole sana Abu Zalawi kwa
hiki kilichotokea.Ahsante pia
kwa kuwaokoa walinzi wangu
kwani maelezo niliyoyapata
kutoka kwao kama si wewe
wote wangeuawa” akasema
Faqir
“Faqir nilikueleza asubuhi
kuhusiana na jambo hili
nadhani sasa umeniamini”
akasema Mathew
“Utanisamehe sana Abu
Zalawi ni kweli sikuyaamini
maneno yako uliponiambia
kwamba kuna hatari lakini
sasa nimekuamini.Hata hivyo
bado najiuliza maswali watu
hawa ni akina nani?
Wamefahamuje kama uko
hapa? Akauliza Faqir
“Faqir nina ombi moja
kwako na ninataka unisaidie”
“Sema Abu nini unahitaji?
Akauliza Faqir
“Nataka kuzungumza na
waziri wa intelijensia wa Iran”
“Sassan Mahmoud?
Akauliza Faqir
“Sifahamu anaitwa nani
lakini ninahitaji kuzungumza
naye”
“Abu Zalawi zipo taratibu
za kufuata ka………” akasema
Faqir lakini Mathew
akamkatisha.
“Faqir huu si muda wa
kufuata taratibu.Naomba
tafadhali unisaidie niweze
kuzungumza naye.Kuna
mambo ya muhimu sana
nataka kumueleza kuhusiana
na hiki kilichotokea leo
hapa.Bado hatari
haijakwisha.Naomba
uniunganishe naye nionane
naye ana kwa ana usiku huu
huu” akasema Mathew na
Faqir akaonekana kusita
“Faqir ninaomba
uniamini.Mimi si mtu mbaya
na nina malengo mazuri kwa
nchi yenu ndiyo maana
niliweza kuweka maisha yangu
katika hatari nikawakomboa
wale mateka sita
nikawarejesha nyumbani.Bado
kuna mambo mazito ambayo
nataka kuyafikisha kwa waziri
muhusika.Nisaidie kwa hilo
tafadhali” akasema Mathew na
Faqir akaonekana
kumuelewa.Akachukua simu
na kumpigia waziri Sassan
Mahmoud akamfahamisha
kuhusiana na tukio lile la
uvamizi katika ile nyumba na
namna Mathew alivyoendesha
mapambano hadi akafanikiwa
kuwaokoa wale walinzi na
kuwaua wavamizi wote.Ilikuwa
ni taarifa iliyomstua sana
waziri Sassan
“Watu hao ni akina nani
na wamefahamuje kama Abu
Zalawi amepelekwa katika
nyumba hiyo? Akauliza Sassan
“Mheshimiwa waziri kuna
mtu mmoja tu ambaye
anaweza akajibu swali hilo”
akasema Faqir
“Ni nani huyo mtu?
Akauliza Sassan
“Abu Zalawi”
“Abu Zalawi?! Waziri
Sassan akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
waziri.Anahitaji kuzungumza
nawe usiku huu kuna masuala
muhimu anadai anataka
akueleze”akasema Faqir
“Anataka kunieleza kitu
gani?
“Sifahamu mheshimiwa
waziri hajanieleza lakini
inaonekana ana jambo la
muhimu sana la kukueleza”
akasema Faqir
“Unamuamini? Akauliza
Sassan baada ya kutafakari
kwa muda
“Mheshimiwa waziri
ninadhani ungeonana naye
ingekuwa vizuri zaidi.Huyu
jamaa anaonekana anafahamu
mambo mengi” akasema Faqir
“Sawa Faqir fanya
utaratibu umlete hapa
nyumbani kwangu usiku huu
na vile vile maiti zote
zipelekwe hospitali hadi pale
uchunguzi wa suala hili
utakapokamilika” akaelekeza
waziri Sassan
“Waziri amekubali
ukaonane naye usiku
huu.Nitakupeleka nyumbani
kwake” akasema Faqir na
kutoka akaenda kutoa
maelekezo halafu akamchukua
Mathew wakaondoa kuelekea
nyumbani kwa waziri Sassan
Mahmoud.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Helkopta ya SNSA ambayo
hutumiwa na makomando wa
idara hiyo katika operesheni
mbali mbali za usiku ilirejea
katika ofisi kuu za SNSA ikatua
na makomando
wakashuka.Walikuwa
wametoka kutekeleza misheni
ya kulipua sehemu ya bomba
la mafuta ili kuzuia mafuta
kwenda bandari ya tanga
ambako meli za mafuta za
Marekani zilikuwa zinapakia
na kuyapeleka Marekani
Mkuu wa timu ile ya
makomando akamfahamisha
Ruby namna kazi ilivyofanyika
“Ahsanteni sana kwa kazi
hii muhimu” akasema Ruby na
kuwataka makomando wale
wakapumzike akampigia simu
Rais Dr Fabian Kelelo
“Mheshimiwa Rais
nimekupigia simu kukujulisha
zoezi limekamilika na
makomando wamerejea
salama” akasema Ruby
“Kazi nzuri sana
Ruby.Tayari taarifa
zimekwisha fika kwa mamlaka
husika na wanalishughulikia
suala hilo kuhakikisha
kwamba hakuna madhara
makubwa yanayotokea.Tayari
mafuta yamekwisha fungwa
hivyo hakuna mafuta
yanayokwenda
Tanga.Nimezungumza na Rais
wa Uganda na kumtaka
ahakikishe uchimbaji wa
mafuta unasimamishwa mara
moja.Ruby ninao uhakika
mkubwa kwamba mpango huu
utakuwa na matokeo mazuri
na vikosi vya Marekani
vitaondolewa hapa nchini
haraka kwani havitakuwa na
sababu ya kuendelea kuwepo
hapa wakati mipango yao yote
imeshindwa kufanikiwa.Kirusi
hakijasambazwa na sasa
mafuta yamekatwa.Mmepata
taarifa zozote kutoka kwa
Mathew Mulumbi kuhusiana
na misheni yake? Akauliza Dr
Fabian
“Tumewasiliana na Nawal
tayari amefika Ruyadh na
kesho ndipo ataanza safari ya
kuelekea Tehran kuonana na
Mathew.Akifika huko
atatujuza kile kinachoendelea”
akasema Ruby
“Vizuri sana.Naamini kila
kitu kitakwenda vizuri.Ruby
hakikisheni mnafanya kila
linalowezekana kupata taarifa
muhimu kutoka kwa hao
jamaa mnaowashikilia
mkianza na huyo Jenerali
William na wale wengine
magaidi.Kuna mambo mengi
sana tunahitaji kuyajua na
kubwa zaidi ni watu
wanaoshirikiana nao hapa
nchini.Tunatakiwa kufanya
usafi mkubwa sana kusafisha
hawa wote na asibaki hata
mmoja wao.Kitendo cha
kushirikiana na hawa
mabeberu kuvuruga
amani,kuchochea watanzania
wauane wenyewe kwa
wenyewe ni kitendo kibaya
sana na wanastahili adhabu
kali ili liwe fundisho kwa
wengine ! akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais kazi
hiyo tunaianza usiku wa leo
kwani kutwa nzima tulikuwa
tunashughulikia mpango wa
kulipua bomba la mafuta.Kwa
kuwa tayari tumeukamilisha
sasa tunahamia katika
kuwahoji hawa jamaa na
ninakuahidi lazima watasema
kila kitu”
“Sawa Ruby .Kama kuna
msaada wowote mtauhitaji
msisite kunieleza nami
nitawasaidia” akasema Rais Dr
Fabian na kuagana na Ruby
“Rais anatoa pongezi
nyingi kwa mafanikio
makubwa na ameelekeza kwa
namna yoyote ile lazima
tuhakikishe tunapata taarifa
muhimu kutoka kwa hawa
jamaa.Gosu Gosu uwanja huu
ni wako.Sintakuingilia tena
naomba utumie kila mbinu
kuhakikisha hawa jamaa
wanafunguka.Tutaanza na
Jenerali William halafu
tutaendelea na wengine akina
Assad” akasema Ruby
“Ahsante
Ruby.Nakuhakikishia hawa
jamaa watafunguka na
watasema kila kitu.Jenerali
William alituita sisi ni watu
wenye akili finyu hivyo basi
nitamuonesha watu wenye
akili finyu ni watu wa namna
gani” akasema Gosu Gosu na
kwenda kufanya maandalizi
kwa ajili ya kuanza kumuhoji
Jenerali William
TEHRAN – IRAN
Faqir aliwasili katika
makazi ya Sassan Mahmoud
waziri wa intelijensia na
usalama wa taifa wa
Iran.Japokuwa Faqir ni mmoja
wa wafanyakazi wa MOIS
lakini gari lake lilikaguliwa na
bastola yake ikachukuliwa na
walinzi kisha wakaruhusiwa
kuingia ndani kuonana na
waziri Sassan.
“Karibuni sana na poleni
kwa yote yaliyotokea” akasema
Waziri Sassan baada ya
kuwakaribisha akina Mathew
sebuleni kwake
“Tunashukuru
mheshimiwa waziri”
“Nataka kujua nini hasa
kimetokea? Akauliza Sassan
“Abu Zalawi wewe
ulikuwepo eneo la tukio
unaweza ukaelezea vizuri zaidi
nini hasa kilitokea” akasema
Faqir
“Nikiwa chumbani kwangu
nimejipumzisha,lilifika gari
likiwa na chakula na
muhudumu akawaambia
walinzi waliokuwepo kwamba
chakula kile kimetumwa na
mmoja wa viongozi.Walinzi
walikipokea chakula kile na
kukusanyika mezani wakaanza
kula.Wakati wakila
wakakumbuka kwamba
nimeshaulika wakamtuma
Najib kuja chumbani kwangu
kuniita.Ni wakati huo ndipo
wavamizi walipovamia.Kile
chakula ulikuwa ni mtego
wao,walikitanguliza ili waweze
kupata nafasi ya kuingia ndani
kirahisi.Baada ya kugundua
kwamba tumevamiwa ndipo
tulipoanza kuchukua hatua
kupambana nao hadi
tulipofanikisha kuwamaliza
kabisa” akasema Mathew
“Hongera sana Abu Zalawi
na ahsante kwa kuwaokoa
watu wetu ambao walinasa
katika mtego kwa tamaa ya
chakula.Lakini najiuliza watu
hawa ni akina nani?
Wamefahamuje kama wewe
uko pale? Nini dhumuni la
kukutafuta? Akauliza Sassan
“Mheshimiwa waziri
ningeomba tuzungumze
faragha kama hutajali”
akasema Mathew na Sassan
akamuomba radhi Faqir na
kumtaka Mathew amfuate
wakaenda katika chumba
kidogo kilichokuwa na sofa
mbili.
“Karibu Abu Zalawi.Nini
unataka kunieleza?
Aliponipigia simu Faqir
alisema unataka kuonana nami
kuna jambo muhimu unataka
kuniambia.Nieleze tafadhali”
akasema Sassan
“Mheshimiwa waziri ni
kweli kuna jambo muhimu
sana nataka kukufahamisha.Ni
kuhusiana na hiki kilichotokea
leo” akasema Mathew na
Sassan akawa kimya
akisikiliza.
“Naamini tayari
unafahamu mimi ni nani”
akasema Mathew
“Ndiyo Abu.Tayari tunazo
taarifa zako kwamba
unahusika katika kulipua
ubalozi wa Marekani jijini Dar
es salaam”
“Ni kweli.Nililipua ubalozi
wa Marekani na kukamatwa
jijini Nairobi wakati nikitafuta
usafiri wa kuelekea Mogadishu
Somalia.Baada ya kukamatwa
nilipelekwa Victoria nchini
Sheli Sheli ambako nilipatiwa
mateso makali sana halafu
nikaunganishwa na akina
Yasser Wazir.Baadae nikaja
kufahamiana nao wakanieleza
kwamba walitekwa na
kupelekwa mahala pale.Baada
ya siku kadhaa za kuwepo pale
Victoria tukapandishwa ndege
kuelekea Marekani hapo ndipo
nilipoamua kujitoa mhanga
kuiteka ndege ile na kuielekeza
Iran” akasema Mathew na
kumuelezea Sassan namna
walivyofanikiwa kuiteka ile
ndege
“Dah !Abu Zalawi wewe ni
shujaa mkubwa.Unastahili
pongezi” akasema Sassan
“Ahsante sana” akasema
Mathew na ukimya mfupi
ukapita
“Marekani wanafahamu
niko hapa Iran na
wananitafuta kwa udi na
uvumba” akasema Mathew
“Hilo ni kweli.Leo hii
waziri wa mambo ya nje wa
Marekani ametoa maneno
makali sana akiipa Iran saa
sabini na mbili tuwe
tumekusalimisha wewe
pamoja na raia wa Marekani
waliokuwamo ndani ya ndege
hiyo pamoja na kuiachia ndege
ya Marekani.Amedai kwamba
Marekani itachukua hatua kali
sana dhidi ya Iran endapo
tutashindwa kumkabidhi kwao
mtuhumiwa wa ugaidi
aliyelipua ubalozi wao”
akasema Sassan na kutoa
kicheko
“Hayo ni mambo ya
kawaida tumeyazoea.Utoaji wa
matamko na vitisho haujaanza
leo.Tuendelee” akasema
Sassan
“Marekani wananisaka
wanikamate na watatumia kila
mbinu ili kufanikisha mpango
huo.Hawana majasusi wao
hapa Iran hivyo basi
wanashirikia na na Mossad
ambao wana majasusi wao
ndani ya Iran.Wale waliovamia
leo katika nyumba ninakoishi
ni majasusi wa Mossad ambao
wametumwa na Marekani”
akasema Mathew
“Wamefahamuje kama uko
katika nyumba ile?
Ninashangaa kwa kuwa
mahala ulipo palifanywa siri
kubwa”akauliza Sassan
“Mossad tayari wana
mtandao wao mkubwa hapa
nchini na wamejipenyeza
katika sehemu mbali mbali
muhimu na wakati mwingine
wanashirikiana na
wafanyakazi katika idara za
serikali” akasema Mathew
“Tumejitahidi sana
kudhibiti majasusi hasa wa
Mossad na CIA kujipenyeza
hapa nchini na kuzifanyia
ujasusi nchi zao.Tumekuwa
tukiwapa adhabu ya kifo kila
pale tunapowabaini majasusi
hao” akasema Sassan
“Mheshimiwa waziri kuna
jambo muhimu nataka
tuzungumze mimi na
wewe.Kuna kitu nitakupatia
lakini na mimi kuna kitu
nitakihitaji” akasema Mathew
na Sassan akacheka kidogo
“Nini unakihitaji Abu
Zalawi? Akauliza Sassan
“Mheshimiwa waziri kama
ulivyoshuhudia mwenyewe
siko salama.Marekani
wananiwinda waniue kwa
gharama zozote.Ninaomba
hifadhi hapa Iran ambako kwa
kiasi Fulani ninajiona niko
salama” akasema Mathew na
sura ya Sassan ikaonesha
mabadiliko kidogo.
“Nafahamu mheshimiwa
waziri kwamba jambo hilo
litakuwa ni kama kuongeza
mafuta kwenye
moto,litachochea zaidi
mgogoro uliopo baina ya Iran
na Marekani.Hata hivyo kuna
kitu muhimu sana nitakupatia
kama gharama za kupewa
hifadhi hapa Iran” akasema
Mathew
“Abu Zalawi imekuwa
vyema umefahamu kwamba
uwepo wako hapa tayari
umekwisha ongeza
mzozo.Kama nilivyokueleza
awali kwamba tumepewa
muda tukusalimishe kwa
Marekani ama sivyo
tutakiona.Hivyo ni vitisho vya
kawaida hatuviogopi.Hata
hivyo hatuwezi kukusalimisha
kwao kwani wewe ni mtu wetu
wa muhimu sana.Umefanya
kitu cha kishujaa mno kwa
kuwarudisha nyumbani watu
wetu muhimu ambao tayari
tulikwisha amini
wameuawa.Hata kama
usingeomba hifadhi sisi tayari
tumekwisha kupa hifadhi na
hatuwezi kukukabidhi kwao
labda wakuue kama
walivyojaribu leo.Utaishi hapa
kwa amani hata kama
ukipenda kwa maisha yako
yote yaliyobakia japokuwa ni
kwa sharti moja kwamba
uachane na mambo ya ugaidi
na ujifunze kuwa raia mwema”
akasema Sassan
“Nashukuru sana
mheshimiwa waziri.Ni jambo
kubwa
mmenifanyia.Nakuahidi
mheshimiwa waziri kwamba
nitaachana na masuala haya ya
ugaidi na kuwa raia mwema”
“Kama utakuwa tayari kwa
hilo basi karibu Iran Abu
Zalawi”akasema Sassan na
kumpa mkono Mathew
“Ahsante mheshimiwa
waziri” akasema Mathew
“Ulisema kuna kitu
muhimu unataka kunipatia.Ni
kitu gani hicho? Akauliza
Sassan.Mathew akaingiza
mkono mfukoni akatoa diski
mweko(flash disc) na
kumpatia Sassan
“Nini hiki? Akauliza
Sassan
“Mheshimiwa waziri ndani
ya hiyo diski mweko kuna
orodha ya majasusi wote wa
Mossad walioko hapa Iran”
akasema Mathew na sura ya
Sassan ikaonesha mshangao
mkubwa.
“Unasema? akauliza
Sassan
“Hiyo ni orodha ya
majasusi wote wa Mossad
walioko hapa Iran” akasema
Mathew na Sassan akaitazama
ile diski kama vile haamini kile
alichoelezwa.
“Abu Zalawi hicho
unachokisema ni kitu kikubwa
sana na
kisichowezekana.Kupata
orodha ya majasusi wa Mossad
si kitu rahisi” akasema Sassan
“Nafahamu si kitu rahisi
lakini nakuhakikishia kwamba
hiyo ni orodha ya majasusi
wote wa Mossad walioko hapa
Iran” akasema Mathew.Sassan
akamtaka Mathew watoke mle
katika kile chumba wakaelekea
katika ofisi yake.Alibonyeza
namba kadhaa katika kifaa
kilichokuwa pembeni ya
mlango ukafunguka wakaingia
ofisini.Akachukua kompyuta
ndogo akaiwasha na
kuchomeka ile diski halafu
akalipakua faili lililokuwemo
ndani yake akalifungua na
kuanza kulipitia.Mwili
ulimsisimka.Akageuka na
kumtazama Mathew
“Umetoa wapi hiki kitu?
Akauliza
“Ninao watu wangu ndani
ya Mossad ambao
wamenisaidia nikaweza
kuipata hiyo orodha” akajibu
Mathew
“Nini hasa sababu ya
kuitaka orodha hii? Akauliza
Sassan
“Kama nilivyoikueleza
kwamba Marekani
wanawatumia majasusi wa
Mossad katika mpango wa
kuniua ndiyo maana nikataka
nipate orodha ya majasusi
wote wa Mossad na mahala
walipo kwa ajili ya
kujihakikishia usalama wangu
nikiwa hapa Iran lakini
nimeona halitakuwa jambo
jema kukaa na orodha hii
nikaamua nije nikukabidhi ili
muifanyie kazi na kuwaondoa
majasusi wote wa Mossad”
akajibu Mathew.
Sassan akaipitia tena
orodha ile akakuna kichwa
“Abu Zalawi siwezi
kukuficha mwili wangu
umenisisimka.Tunafahamu
kuna majasusi wa Israel hapa
Iran lakini kuwabaini imekuwa
vigumu sana.Sikujua kama
wako wengi kiasi hiki.Majasusi
zaidi ya thelathini.Nimestuka
zaidi kwani wengine
ninawafahamu ni wafanyakazi
wa idara za usalama hapa Iran
na wengine ni marafiki zangu
sikujua kama wanaifanyia
ujasusi Israel.Majasusi hawa ni
wengi na hatua za haraka sana
zinapaswa kuchukuliwa.Rais
anapaswa kulifahamu jambo
hili.Kwa usiku wa leo
utapumzika hapa.Nina
vyumba vya wageni hivyo
karibu jisikie nyumbani”
akasema Sassan wakatoka mle
ndani na kurejea
sebuleni.Sassan
akamfahamisha Faqir kwamba
Abu Zalawi atalala pale
nyumbani kwake kwa usiku
ule.Akamuita mtumishi wa
ndani na kumuelekeza
amuandalie Abu chumba cha
wageni kisha yeye na Faqir
wakaondoka.Dakika chache
baadae mfanyakazi Yule wa
ndani akamfuata Mathew na
kumjulisha kwamba chumba
tayari kimeandaliwa na
Mathew akainuka akaenda
kupumzika.
“Nimeanza vizuri.Jamaa
wamenikubali.Mungu
anisaidie niweze kukamilisha
misheni yangu salama”
akawaza Mathew na kujilaza
kitandani
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Saa kumi za alasiri jijini
Washington DC,David Walker
aliwasili katika ofisi ya
makamu wa Rais Mark Piller
ambaye bado alikuwa ofisini.
“Mark umenistua kwa wito
wako wa haraka.Kuna taarifa
yoyote umeipata? Akauliza
David Walker
“Kuna taarifa imefika
kutoka Tanzania”akasema
Mark Piller
“Jenerali William
amepatikana? Akauliza David
“Hapana bado hakuna
taarifa zozote za kupatikana
kwa Jenerali William.Kuna
taarifa nyingine kuhusiana na
mafuta”
“Kuna tatizo lolote?
Akauliza David
“Hivi sasa ni saa sita
inaelekea saa saba za usiku
nchini Tanzania.Tumepokea
taarifa kwamba bomba la
mafuta limelipuliwa usiku
huu”
“Bomba la mafuta
limelipuliwa? Akauliza
David.Taarifa ile ilionekana
kumstua sana
“Ndiyo.Bomba
limelipuliwa”
“Mungu wangu ! akasema
David na kuegemea kiti
akashusha pumzi na ukimya
wa muda ukapita
“Kuna taarifa zozote za
kuhusiana na watu waliofanya
kitendo hicho? Akauliza David
“Hakuna taarifa zozote
kutoka serikali ya
Tanzania.Taarifa hizi
tumezipata kutoka kwa
makamanda wetu walioko
jijini Tanga Tanzania”
“Hii taarifa ni ya kustusha
na inazidi kuongeza
mkanganyiko katika kile
kinachoendelea kutokea
Tanzania.Nani waliofanya kitu
cha kijinga kama hiki?
Akauliza David
“David ni kweli hili jambo
linastusha na nimekuita hapa
ili tuweze kujadiliana
kuhusiana na jambo hili.Ni
wazi kwa hiki kilichotokea
hakuna mafuta yatakayokuwa
yanakwenda jijini Tanga hivyo
uchukuaji wa mafuta
unasimama.Nini
kinachoendelea Tanzania?
Akauliza Mark
“Mark swali hilo ni zuri
kwa kuanzia kujiuliza kuhusu
kile kinachoendelea
Tanzania.Inaonekana mipango
yetu imeanza kufeli.Nini
kimetokea? Wapi tumekosea?
Mbona tulijipanga vizuri sana
na mambo yakaenda vizuri
nini kimetokea hadi mambo
yakaanza kwenda mrama
ghafla tu? Akauliza Mark Piller
“Matatizo yameanza baada
ya kutuma kirusi.Kirusi
kilipofika Tanzania ndipo
wanajeshi wetu
wakashambuliwa na kuuawa
huku wale wahusika wakuu
waliokuwa na kirusi wakipotea
na hawajulikani walipo.Kama
haitoshi bomba la mafuta nalo
limelipuliwa.Ukiunganisha
matukio haya yote yaliyotokea
mfululizo unaona kabisa
kwamba kuna kitu kinaendelea
hapa” akasema David Walker
“Unadhani nini
kinachoendelea David?
“Mark ni wazi matukio
haya yote yanayoendelea
kutokea nchini Tanzania yana
lengo la kukwamisha mipango
yetu isifanikiwe.Tazama tukio
la kushambuliwa kwa kambi ya
wanajeshi wetu limekwenda
sambamba na kupotea kwa
Jenerali William na wale watu
wa IS ambao tumekuwa
tunashirikiana nao.Kama hiyo
haitoshi tukio la kulipuliwa
bomba la mafuta linaashiria
kwamba upo mpango
unaoendelea wa kuhujumu
mipango yetu nchini
Tanzania.Kulipua bomba la
mafuta hakujafanywa
makusudi.Ni mpango wa
kuhakikisha kwamba
hatuendelei kuchukua mafuta”
akasema David.Mark Piller
akazama katika tafakari halafu
akasema
“Kwa mtazamo David
unadhani tayari mipango yetu
imekwisha fahamika? Akauliza
Mark
“Hilo liko wazi
Mark.Matukio haya mfululizo
hayajatokea kwa bahati
mbaya.Tazama matukio yote
yamelenga Marekani.Hili la
kulipuliwa bomba la mafuta
ndilo linaashiria kabisa
kwamba kuna kitu hakiko
sawa” akasema David Walker
“Unahisi serikali ya
Tanzania inahusika katika
matukio haya? Mark akauliza
“Sina hakika kama serikali
ya Tanzania inahusika katika
matukio haya.Tunahitaji
kufanya uchunguzi kulibaini
hilo” akasema David
“Kama si serikali ya
Tanzania nani ambaye
anafanya mtukio haya ya
kutuhujumu? Akauliza Mark
Piller
“Nina mashaka si serikali
ya Tanzania inayohusika na
matukio haya kwani kama
ingekwisha gundua kuhusu
mipango yetu isingeweza
kukaa kimya hadi sasa hivi
isitoe tamko lolote.Tayari
vikosi vya Marekani
vingekwisha timuliwa nchini
Tanzania na hata mahusiano
ya Tanzania na Marekani
naamini yangekuwa katika hali
mbaya sana” akasema David
Walker
“Nakubaliana nawe
David.Jambo tulilolifanya
nchini Tanzania ni
kubwa.Damu nyingi
imemwagika na serikali ya
Tanzania isingeweza kukaa
kimya hadi sasa bila kusema
chochote kama kweli
wangekuwa wamegundua sisi
tunahusika na kile kilichotokea
Tanzania.Swali tunalopaswa
tulitafutie majibu kama si
serikali ya Tanzania nani
anahusika na matukio haya
yanayoendelea nchini
Tanzania ambayo ni wazi
yanalenga kuvuruga mipango
yetu? Akauliza Mark Piller
“Abu Zalawi ! akasema
David kwa sauti ndogo
“Unasema nini David?
“Abu Zalawi ndiye
anayefahamu mipango yetu na
yeye anatokea Tanzania.Nahisi
atakuwa anahusika na haya
matukio.Lakini…..” David
akanyamaza kuna kitu
alikumbuka.
“Lakini kuna kitu
nimekikumbuka.Abu Zalawi
alipokwenda Tanzania alikuwa
katika udhibiti
mkali.Hakuruhusiwa kuonana
au kuwasiliana na mtu yeyote
na hata alipokabidhiwa kwa
Assad alikuwa chini ya ulinzi
na walihakikisha hatoki katika
mazingira yao hadi
alipokwenda kutekeleza kazi
aliyotumwa.Hakuweza
kuonana wala kuwasiliana na
mtu yeyote Tanzania” akasema
David na ukimya ukapita
halafu akasema
“Lakini haya yote
yameanza kutokea wakati Abu
Zalawi akiwa nchini
Iran.Yawezekana baada ya
kufika huko amewasiliana
watu wake au serikali yake na
wakatekeleza mipango hii.Kwa
namna yoyote ile lazima
anahusika”
“Kwani mpango wa
kumuua umefikia wapi?Vipi
kuhusu Habiba Jawad tayari
amekwisha patikana? Akauliza
Mark Piller kana kwamba
hajui chochote kinachoendelea
na David akaonekana kusita
kidogo
“Kuna nini David? Abu
amekwisha uawa?
“Nilipokea taarifa kutoka
kwa mkurugenzi wetu Jason
kwamba…..” akasema David na
kusita
“Mbona unasita
David.Kuna nini? Akauliza
Mark Piller.David akakuna
kichwa na kusema
“Majasusi wa Mossad
waliotumwa kumuua Abu
Zalawi wote wameuawa”
“Wameuawa? Akauliza
Mark kwa mshangao
“Ndiyo wameuawa
wote.Mossad wanaendelea na
uchunguzi kujua
kilichotokea.Baada ya kupokea
taarifa hivyo tumewatafuta
wale watu wetu tuliowatuma
kwenda kumteka Habiba ii
wasitishe mpango huo lakini
mawasiliano yao yamepotea na
hawapatikani
tena.Tunaendelea kuwatafuta
lakini ukimya wao hauleti
picha nzuri” akasema David
Walker
“David hao majasusi wa
Mossad waliouawa hawawezi
kugundulika kama ni watu wa
Mossad? Nauliza hivyo kwa
sababu wakigundulika kama ni
watu wa Mossad huu utakuwa
ni mgogoro mpya kati ya Iran
na Israel”Akasema Mark Piller
“Kwa mujibu wa Jason ni
kwamba haitakuwa rahisi
kugundulika kwa kuwa watu
wote hao ni raia wa Iran hivyo
hakuna anayejua kama
wanafanya kazi na Mossad”
akasema David
“Lakini imetokeaje
majasusi hao wakauawa?
Akauliza Mark
“Hakuna anayejua Mark
lakini taarifa rasmi ni kwamba
Abu Zalawi bado mzima na
mipango ya kumteka Habiba
Jawad itasitishwa kwa muda
hadi pale tutakapowasiliana
tena na Mossad kujua kama
wana mpango mwingine
mbadala wa kumuua Abu
Zalawi” akasema David
“David mambo yanazidi
kutuendea kombo.Kila
tunalolifanya linakuwa na
mkwamo ndani yake.Hebu
nipe ushauri tufanye nini?
Akasema Mark
“Kwanza ni kuhusu suala
la Tanzania. Hatupaswi
kuingilia au kusema chochote
kuhusiana na hiki kitendo cha
kulipua bomba la mafuta
ambacho tunajua wazi
kimefanywa kwa lengo la
kutukosesha mafuta.Kuna
jambo moja tu ambalo
tunaweza kulifanya katika
mkanganyiko huu nalo ni
kuwarejesha nyumbani
wanajeshi wetu.Tutumie
kigezo cha kuvamiwa kwa
kambi na wanajeshi wetu
kuuawa kuwarejesha wengine
wote waliobaki.Rais anatakiwa
kutoa tamko kali kwamba
tunawaondoa wanajeshi wetu
waliokuwa wanasaidia kulinda
amani nchini Tanzania baada
ya kushambuliwa na
kuuawa.Dunia nzima itajua
kwamba sababu kuu ya
kuondoka Tanzania ni kuuawa
kwa wanajeshi wetu.Kwa sasa
ni usiku nchini Tanzania hivyo
basi hadi kufika kesho asubuhi
meli zetu zote zilizokuwa
zinasubiri kupakia mafuta
katika bandari ya Tanga ziwe
zimeondoka zibaki zile za
kijeshi zikipakia vifaa vya
jeshi.Hiyo ni hatua ya kwanza
tunayotakiwa kuichukua na
baada ya hapo tutaingia katika
uchunguzi kujua nini hasa
kimetokea.Nani
waliotushambulia? Je serikali
ya Tanzania inafahamu
kuhusu mipango yetu au haijui
chochote? Mwisho kabisa
tunatakiwa kujua wapi aliko
Jenerali William pamoja na
akina Assad” akasema David
“Ushauri wako ni mzuri
David.Nadhani kuna haja ya
kurudi nyuma kwanza na
kujipanga tena vizuri baada ya
kujua nini kimetokea.Lazima
tujue tumekosea wapi.Hata
hi….” Akanyamaza Mark baada
ya simu ya David Walker
kuita.Akaipokea akazungumza
kwa muda halafu akamtazama
Mark Piller kwa macho ya
wasiwasi
“Kuna nini David?
“Nimezungumza na
mkurugenzi Jason.Anasema
kwamba amepokea taarifa
muda mfupi uliopita kutoka
Riyadh kwamba wale watu
wetu tuliowatuma kwenda
kumteka Habiba Jawad wote
wamekutwa wameuawa katika
hoteli”
“Mungu wangu ! Mark
Piller akashangaa.
“Mark mambo yanazidi
kuwa magumu kwa upande
wetu.Kwa nini kila
tunachokifanya kinashindwa
kufanikiwa? Haijawahi
kutokea tukashindwa vibaya
namna hii” akasema David
“David kama watu wetu
wameuawa ni wazi kwamba
tayari Habiba amekwisha
fahamu kilichokuwa
kinakwenda kutokea kwamba
ulikuwa ni mpango wa
kumteka .Kwani mpango huu
mliuandaa vipi? Akauliza Mark
na David akamueleza namna
walivyokuwa wameuandaa
mpango ule wa kumteka
Habiba Jawad
“David haya mambo si
madogo.Tunapaswa
kuchunguza kwa makini nini
kimetokea.Mimi nitamshauri
Rais afanye kama ulivyoshauri
lakini nataka kujua kuhusu
Abu Zalawi?
“Abu Zalawi kwa namna
yoyote ile lazima auawe.Ngoja
tuwasikilize Mossad
wanasemaje kwani
tunawategemea wao katika
jambo hili lakini Habiba
Jawad..….” Akasema David na
kunyamza kidogo
“Kitendo cha watu wetu
kuuawa kinaonyesha wazi
kwamba Habiba Jawad
amekwisha fahamu kuhusu
mpango wetu wa kutaka
kumteka na kumuua.Huyu
amegeuka kuwa mtu hatari
zaidi kuliko hata Abu Zalawi
kwani anafahamu mambo yetu
mengi.Lazima mpango wa
kumuua uanze haraka
sana.Kwa kutumia njia yoyote
ile lazima tumuue Habiba
Jawad ! Nikitoka hapa
ninakwenda kukutana na
wenzangu tujadiliane kuhusu
mpango mpya wa kumuua
Habiba Jawad” akasema David
Walker.
“Sawa David.Tusipoteze
muda nenda kakutane na G20
mimi ninakwenda kuzungmza
na Rais sasa hivi ili nimpe
ushauri huu angali mapema
asije akafanya maamuzi
mengine yanayoweza kutuletea
matatizo” akasema Mark Piller
“Angalizo Mark.Kumbuka
kwamba Rais hapaswi
kufahamu chochote kuhusu
mambo haya hivyo
unapozungumza naye
hakikisha unakuwa makini
asigundue kama kuna kitu
kilikuwa kinaendelea kule
Tanzania” akasema David
Walker
“Nalifahamu hilo David
usihofu” akasema Mark na
kuagana na David akaondoka.
“Nakubaliana na David
kwamba matukio haya
yanalenga kuvuruga mipango
yetu kule Tanzania.Lakini nani
anayefanya haya? Je ni serikali
ya Tanzania? Lakini bado
nakubaliana na David kwamba
kama serikali ya Tanzania
ingeyafahamu haya
isingeweza kukaa kimya lazima
hivi sasa dunia nzima
ingefahamu.Lazima kuna
kikundi cha watu kinafanya
haya mambo ili
tushindwe.Hata hivyo kiasi cha
mafuta tulichokichukua bado
ni kikubwa na kama mipango
yetu isingevurugika hivi sasa
tungekuwa tunajiandaa
kuingia katika madini ambako
nako tungekusanya kiasi
kikubwa sana cha
madini.Ushauri wa David ni
mzuri ngoja kwanza turejeshe
wanajeshi wetu halafu
tujitafakari upya nini
kimetokea? Lingine kubwa
ambalo bado tunapaswa
kulitafutia majibu ni mahala
alipo Jenerali William na akina
Sattar” akaendelea kuwaza
Mark Piller halafu akatoka
kwenda kuonana na Rais
William
“Mark karibu” akasema
Rais William baada ya
kumaliza kuzungumza na simu
“Ahsante mheshimiwa
Rais”
“Mark naamini
kilichokuleta hapa ni taarifa ya
kilichotokea Tanzania”
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ni kuhusiana na
kulipuliwa kwa bomba la
mafuta”
“Nimezipokea taarifa hizo
tayari kutoka kwa waziri wa
ulinzi.Nimestuka kidogo kwa
jambo hili kutokea hasa kwa
wakati huu” akasema Rais
William
“Muda mfupi uliopita
nilikuwa na David Walker
tukilijadili jambo hili na
tulijiuliza swali hilo hilo kwa
nini iwe sasa? Akasema Mark
“Nini maoni yako Mark
juu ya jambo hili? Akauliza
Rais William
“Mheshimiwa Rais
ukiyatazama matukio haya
yaliyotokea kwa ujumla wake
utagundua kuna kitu
kinaendelea chini kwa chini
ambacho mpango wake ni
kuvuruga mipango yetu
isiendelee.Matukio haya
yalianza pale kirusi kilipofika
nchini Tanzania ambapo
kambi yetu ikavamiwa na
wanajeshi kuuawa.Ambacho
kinatufanya tuhisi huu ni
mpango wa kuvuruga mipango
yetu ni kupotea kwa Jenerali
William na akina Satter ambao
walifahamu kuhusu mpango
ule wa kusambaza kirusi
nchini Tanzania.Kabla hilo
hilo halijapoa bomba la mafuta
limelipuliwa na hatuwezi tena
kupata mafuta.Mheshimiwa
Rais huoni kama huo ni
mpango wa kuvuruga mipango
yetu? Aliyelipua bomba la
mafuta ni wazi alifahamu kile
kilichokuwa kinaendelea kule
Tanga na lengo lake ni
kutuzuia tusiendelee kuchukua
mafuta” akasema Mark Piller
na Rais William akavuruga
nywele zake kwa hasira
“Mark unataka kuniambia
kwamba tayari mipango yenu
yote imekwisha fahamika?
Akauliza Rais William
“Mheshimiwa Rais
kutokana na namna matukio
yalivyotokea mfululizo ni wazi
mipango yetu imekwisha
fahamika” akasema Mark
Piller
“Unahisi ni serikali ya
Tanzania? Akauliza William
“Hapana mheshimiwa
Rais kama serikali ya Tanzania
ingefahamu mipango hii
isingeweza kukaa kimya.Tayari
mambo yangekwisha wekwa
hadharani lakini mpaka sasa
wako kimya na hii inaashiria
kwamba hawafahamu
chochote.Bado ninaendelea
kuhisi kwamba kuna
uwezekano mkubwa mambo
haya yanafanywa na kundi la
IS” akasema Mark Piller
“Lakini IS mmekuwa
mkishirikiana nao kwa muda
mrefu katika mipango
mbalimbali”
“Ndiyo mheshimiwa
tumekuwa tukishirikiana nao
kwa muda mrefu lakini
wanaweza wakatugeuka na
kuvuruga mipango yetu.Ndiyo
maana nilimuomba Habiba
Jawad atusaidie kuchunguza”
akasema Mark Piller
“Umemtaja Habiba
nimekumbuka kuhusu
mipango iliyokuwa inafanywa
na kundi lako
kumteka.Wamefikia wapi?
“Mambo yamekwenda
vizuri mheshimiwa Rais.Wale
jamaa wote waliotumwa
kwenda kumteka wameuawa”
“Vizuri sana.Vipi kuhusu
Abu Zalawi? Akauliza William
“Taarifa niliyoipata ni
kwamba majasusi wote wa
Mossad waliotumwa kumuua
Abu Zalawi wameuawa.Jambo
hili limewastusha sana
Mossad.Hata hivyo bado G20
wanaendelea na mipango ya
kumuua Habiba Jawad kwani
tayari amekwishafahamu kuwa
anatakiwa kuuawa”akasema
Mark
“Mark kuna jambo
ninalifikiria ila sijui kama lina
msingi wowote.Hudhani kama
Habiba Jawad yuko nyuma ya
matukio haya yanayotokea hivi
sasa? Akauliza Rais William
“Habiba Jawad tumekuwa
naye kwa muda mrefu na
tumempa utajiri mkubwa na
yeye ametusadia katika
mipango mingi.Sina hakika
kama anaweza akahusika na
mambo haya.Kwa nini umehisi
Habiba anaweza
kuhusika?akauliza Mark Piller
“Kinachonifanya nihisi
Habiba akahusika na matukio
haya yaliyotokea ni kitendo
chake cha kumleta Abu Zalawi
akidai ni gaidi wakati si
kweli.Huoni kuna kitu hakiko
sawa hapa? Japokuwa
anatusaidia sana lakini kuna
wakati ninapoteza imani na
huyu mama.Anaweza kuwa ni
muhusika mkuu katika haya
yanayoendelea.Yawezekana
yeye mwenyewe ameshirikiana
na IS na wakafanya hujuma hii
kubwa.Pamoja na kushirikiana
naye hebu tumchunguze kwa
makini huyu Habiba Jawad
kuna mambo naamini
tunaweza kuyafahamu kutoka
kwake” akasema Rais William
“Mheshimiwa Rais
mawazo yako ni mazuri lakini
bado moyo wangu unakataa
kabisa kama Habiba anaweza
akatuzunguka kiasi kikubwa
namna hii.Tumeshirikiana
naye kwa muda mrefu na
hakujawahi kutokea matatizo
yoyote hata mara moja.Habiba
hana sababu zozote za kufanya
mambo kama haya” akasema
Mark Piller
“Mark usimuamini
mwanadamu kiasi
hicho.Kumbuka hata Kristo
alisalitiwa na mmoja wa
wafuasi wake hivyo si ajabu
kwa Habiba kuwazunguka hata
kama mmekuwa naye kwa
muda mrefu na mmempa
utajiri mkubwa.Usiyapuuze
mawazo yangu jaribu kufanya
uchunguzi wako kimya kimya”
akasema Rais William
“Sawa mheshimiwa rais
nitafanya hivyo.Tukiliweka
pembeni hilo nataka
tujielekeze zaidi katika hili la
Tanzania.Nini mawazo yako
mheshimiwa Rais? Akauliza
Mark
“Mpaka sasa sijafanya
maamuzi yoyote Mark” akajibu
William
“Mheshimiwa rais
nimekuja na wazo nini cha
kufanya”
“Karibu”
“Kama nilivyokueleza
awali kwamba mipango yetu
inahujumiwa isifanikiwe hivyo
basi tunatakiwakuwaondoa
wanajeshi wetu Afrika
mashariki haraka
sana.Hakuna sababu ya
wanajeshi wetu kuendelea
kuwepo nchini Tanzania au
Uganda wakati kitu kikubwa
tulichokifuata kule ambacho ni
mafuta hakipo tena.Itachukua
muda mrefu kufanya
marekebisho katika bomba
hilo na hadi wakati huo tayari
eneo lote la Afrika mashariki
litakuwa shwari na wanajeshi
wetu hawatahitajika tena”
akasema Mark Piller
“Mark ule mpango wa
kirusi umeishia wapi? Kama
kirusi kile kingefanikiwa
kusambazwa wanajeshi wetu
wangeendelea kuwepo
Tanzania tena tungeongeza
vikosi na badala ya mafuta
tungeanza kusomba madini”
akasema Rais William
“Mheshimiwa Rais mpaka
sasa hakuna kinachojulikana
kuhusiana na mahala kirusi
kilipo kwani wale wahusika
wakuu wote wamepotea na
hawajapatikana bado.Baada ya
kuwarejesha wanajeshi wetu
nyumbani tutaanza kufuatilia
taratibu kujua mahala waliko
Jenerali William na akina
Sattar lakini kwa sasa ushauri
wetu ni kwamba wanajeshi
warudi nyumbani.Kigezo
kikuu cha kuwarejesha
nyumbani wanajeshi wetu
ambacho kila mtu anaweza
akakielewa ni kutokana na
shambulio lililofanywa na
wanajeshi wetu kuuawa.Katika
maelezo yako utakayoyatoa
onyesha kwamba wanajeshi
wetu wamekufa kishujaa
kwani walikuwa katika
kutimiza wajibu wao wa
kulinda amani lakini watu
wasio na huruma wakawaua
hivyo basi hakuna sababu ya
kuwaweka wanajeshi mahala
ambako hawatakiwi” akasema
Mark Piller
“Sawa Mark nitafanya
hivyo lakini bado kutakuwa na
maswali mengi kuhusiana na
Jenerali William.Lazima
wamarekani watataka
kufahamu tumechukua hatua
gani kumtafuta? Kibaya zaidi
Rais wa Tanzania hataki
tutume wachunguzi wetu
kwenda kumtafuta”
“Nilikueleza mheshimiwa
Rais kwamba jishushe kwa
Rais wa Tanzania.Watu weusi
wanapenda kuonekana wako
juu.Rais kama wewe
ukijishusha kwake atajiona wa
thamani kubwa na atafanya
kila utakachomuelekeza”
akasema Mark
“Mark hilo ni suala gumu
sana.Kujishusha kwa mtu
mweusi?!
“Usihofu mheshimiwa
Rais.Hiyo nayo ni mbinu
wakati wa mapambano”
“Nitaangalia nini cha
kufanya lakini kitu kikubwa
kwa sasa ni kuhakikisha
wanajeshi wetu wanarejea
kwanza nyumbani.Lakini
tumefanikiwa kupata mafuta
ya kutosha?
“Tumepata mnafuta mengi
mheshimiwa Rais.Mengi sana”
“Sawa Mark
nitalishughulikia hilo ili pale
miili ya wanajeshi wetu
waliouawa inaporejea
nyumbani basi iambatane na
wanajeshi wengine wote”
akasema Rais William
TEHRAN – IRAN
“Sassan kuna jambo gani
la muhimu usiku huu ambalo
haliwezi kusubiri hadi kesho?
Akauliza Rais Armen Hijazi wa
Iran baada ya Sassan
Mahmoud kuwasili katika
makazi yake.
“Mheshimiwa Rais
samahani sana kwa usumbufu
usiku huu lakini kuna jambo
muhimu sana ambalo
ninadhani haliwezi kusubiri
hadi kesho” akasema Sassan
“Haya karibu” akasema
Rais Armen
Sassan akakohoa kidogo
halafu akasema
“Mheshimiwa Rais kama
unavyofahamu kuwa wale
ndugu zetu sita waliokuwa
wamepotea wamerejea
nyumbani na kwa mujibu wa
maelezo yao mtu
aliyefanikisha kurejea kwao ni
Abu Zalawi ambaye
tumekwisha fahamu kuwa ni
Gaidi na amehusika katika
kulipua ubalozi wa Marekani
nchini Tanzania.Kwa ruhusa
yako ulikubali tumpokee na
tumpe hifadhi hapa
nchini.Tulifuata maelekezo
yako na kumpatia
hifadhi.Tulimuweka katika
mojawapo ya nyumba zetu za
siri.Usiku wa leo nimepigiwa
simu na mkuu wa kitengo
kinachosimamia nyumba zetu
za siri anaitwa
Faqir,akanijulisha kwamba
kuna jambo limetokea,watu
wamevamia nyumba alimo
Abu Zalawi na kutaka
kumuua.Aliniambia kwamba
Abu Zalawi anataka kuniona
na nikamuelekeza amlete
nyumbani kwangu.Baada ya
kufika kwangu walinipa
maelezo ya namna tukio lile
lilivyotokea” akasema Sassan
na kumsimulia Rais Armen
namna tukio lile lilivyotokea.
“Ni akina nani hao watu na
walifahamuje kama Abu
Zalawi yuko katika nyumba
hiyo? Akauliza Rais Armen
“Hilo ni swali ambalo sote
tulijiuliza lakini Abu Zalawi
akaniomba tuzungumze
faragha na ndipo aliponipa siri
ya tukio lile.Wale watu
waliotaka kumuua ni majasusi
wa Mossad”
“Mossad?
“Ndiyo ni majasusi wa
Mossad.Marekani tayari
wanafahamu kuwa Abu Zalawi
yuko hapa Iran na waziri wao
wa mambo ya nje tayari
ametoa tamko la kututaka
tumsalimishe kwao.Wanajua
kwamba hatuwezi kufanya
hivyo ndipo wakaja na mpango
wa kumuua kwa kuwatumia
majasusi wa Mossad ambao
wamejitahidi kutafuta hadi
wakafahamu mahala alipo na
kwa bahati nzuri mpango wao
umeshindwa kufanikiwa”
akasema Sassan
“Abu Zalawi amefahamuje
kama wale watu waliokwenda
kutaka kumuua ni majasusi wa
Mossad? Akauliza Rais Armen
“Abu Zalawi ana watu
wake ndani ya Mossad ambao
wamekuwa wakimpa taarifa
mbali mbali za mpango ya
Mossad.Kikubwa zaidi
amenipatia hii” akasema
Sassan na kumuonyesha Rais
Armen diski mweko(flash disc)
“Hiki nini? Akauliza Rais
Armen
“Hiki ni kitu ambacho
tumekuwa tunakitafuta kwa
muda mrefu sana bila
mafanikio.Ni orodha ya
majasusi wote wa Israel
walioko hapa nchini kwetu”
akasema Sassan na Rais
Armen akashusha pumzi
“Sassan una uhakika hicho
alichokupatia ni kitu cha
kweli? Akauliza Rais Armen
“Nimeipitia orodha hii ni
ya kweli.Haina mashaka hata
kidogo” akasema Sassan na
kuichomeka ile diski mweko
katika kompyuta yake
aliyekwenda nayo na kuanza
kumuonyesha Rais Armen kile
kilichokuwa ndani ya ile diski
mweko.
“Hiki ni kitu muhimu sana
kwetu.Nilifahamu kuna
majasusi wa Israel hapa Iran
lakini sikujua kama wako
wengi kiasi hiki.Abu Zalawi
ameipataje orodha hii?
Akauliza Rais Armen
“Kama nilivyokwambia
mheshimiwa Rais kwamba
Abu ana watu wake ndani ya
Mossad ambao wamekuwa
wakimpa taarifa muhimu
kwani Abu anasakwa pia na
Israel.Amewahi kutoroka
gerezani nchini Israel na vile
vile amehusika katika
shambulio la bomu jijini
Jerusalem.Abu amekuwa
akishirikiana na mojawapo ya
kundi la wanamgambo wa
kipalestina katika kuendesha
mashambulio dhidi ya Israel
hivyo kuna watu ndani ya
Mossad ambao wanawasaidia
kwa kuwapa taarifa muhimu”
akasema Sassan
“Sassan nataka ukae na
wataalamu wako kesho
muipitie orodha hiyo kama ni
ya kweli.Mkijiridhisha kuwa ni
ya kweli basi hili litakuwa ni
jambo kubwa sana kwetu”
akasema Rais Armen
“Ndiyo maana nikaona
nije nikuone usiku huu huu
kuhusu jambo hili”
“Ni jambo kubwa sana hili
Sassan kama orodha hiyo
itakuwa ya kweli”
“Sina mashaka nayo lakini
nitafanya kama
ulivyoelekeza.Nitakaa na
wataalamu wangu na kuipitia
kujiridhisha kama ni ya
kweli.Hata hivyo mheshimiwa
Rais Abu Zalawi ana maombi
yake”
“Anataka nini? Akauliza
Rais Armen
“Anaomba apewe hifadhi
hapa Iran kwani hana sehemu
nyingine ya kwenda kwa sasa
na kwa namna anavyofuatiliwa
akitoka nje ya hapa atauawa
haraka sana” akasema Sassan
“Kuhusu hifadhi hilo
halina tatizo.Ataishi hapa
kwani anaonekan anaweza
akawa na msaada
kwetu.Sassan namuhitaji Abu
Zalawi kesho jioni hapa
kwangu.Nitakuwa na
mazungumzo naye” akasema
Rais Armen
“Sawa mheshimiwa Rais
nitalifanikisha hilo” akasema
Sassan wakaendelea na
mazungumzo na walipomaliza
Sassan akaondoka kurejea
nyumbani kwake.Kitu cha
kwanza alichokifanya alipofika
nyumbani kwake ni kugonga
mlango wa chumba cha wageni
alimolala Mathew akaamka
“Abu Zalawi samahani kwa
kukuamsha.Nimekuja kukupa
taarifa kwamba
nimezungumza na Rais.Kubwa
lilikuwa ni hii orodha
uliyonipatia.Rais amelipokea
ombi lako la kupewa hifadhi
hapa Iran na ameelekeza
tukutafutie makazi maalum na
vibali vya ukaazi lakini wakati
mchakato huo ukifanyika
utaendelea kuishi hapa
nyumbani kwangu kwa ajili ya
usalama wako” akasema
Sassan
“Nashukuru sana Sassan
kwa jambo hili
kubwa.Nifikishie pia salamu
zangu kwa mheshimiwa Rais”
akasema Mathew
“Nitafikisha shukrani hizo”
akasema Sassan na
kumtazama Mathew
“Abu Zalawi” akaita
“Naam” akaitika Mathew
“Jambo hili tayari limefika
ngazi za juu,nataka
unihakikishie kwa mara
nyingine tena kwamba orodha
hii ni ya kweli” akasema
Sassan
“Nakuhakikishia kwamba
hii ni orodha ya kweli kabisa
Sassan.Siwezi kuja na kitu
kikubwa kama hiki halafu
kikawa si cha kweli.Ifanyieni
uchunguzi ili mjiridhishe kama
ni ya kweli au si kweli.Kama
mkigundua si ya kweli niko
tayari kupata adhabu yoyote
hata kufukuzwa nchini”
akasema Mathew kwa
kujiamini
“Unajiamini sana Abu
Zalawi.Ahsante kwa uhakika
huo” akasema Sassan na
ukimya mdogo ukapita
“Sassan kuna jambo
nataka kukuomba unisaidie”
“Jambo gani Abu Zalawi?
“Nataka kuonana na
Yasser Wazir hapo kesho kama
itawezekana” akasema Mathew
“Hilo halitakuwa jambo
rahisi.Yasser na wenzake
wamehifadhiwa sehemu
maalum kwa sasa wakipatiwa
matibabu katika mojawapo ya
hospitali za jeshi.Bado
hajaruhusiwa mtu yeyote
kuonana nao.Vuta subira pale
watakapokuwa wametoka
hospitali utaonana nao”
akasema Sassan na kumuaga
Mathew
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Simu ya Dr Fabian Kelelo
Rais wa Tanzania iliita.Ni saa
kumi na moja kasoro dakika
kumi na nane lakini Dr Fabian
alikuwa macho hakuwa na
usingizi hata
chembe.Akanyoosha mkono na
kuichukua ile simu akatazama
mpigaji na kuinuka halafu
akashusha pumzi.Alikuwa ni
William Washington Rais wa
Marekani.
“Hallow Rais William”
akasema Dr Fabian baada ya
kupokea simu
“Habari za asubuhi
mheshimiwa Rais Dr
Fabian.Naamini ni alfajiri kwa
saa za huko kwenu”akasema
Rais William
“Ndiyo mheshimiwa Rais
ni alfajiri.Habari za huko
kwenu?
“Huku bado ni majonzi
kufuatia vifo vya wanajeshi
wetu.Hata hivyo tuliweke hilo
pembeni kwani tayari
tumekwisha
lizungumza.Kikubwa
nilichokupigia simu ni
kukujulisha kwamba kufuatia
tukio lile la kushambuliwa na
kuuawa kwa wanajeshi wetu
tumefikia maamuzi ya
kuwaondoa wanajeshi wetu
wote waliobaki.Mheshimiwa
Rais nia yetu ilikuwa nzuri
sana kusaidia ndugu zetu na
marafiki zetu wa muda mrefu
kurejesha amani kufuatia
machafuko yaliyotokea nchini
kwako na wanajeshi wetu
wamefanya kazi nzuri sana na
tungependa waendelee
kuwepo nchini kwako lakini
dosari imetokea pale
walipovamiwa
wakashambuliwa na
kuuawa.Jambo hili
limewachukiza mno
wamarekani na wanataka
wanajeshi wao waliobaki
warejee nyumbani mara moja
hivyo nimeona nikujulishe
angali bado mapema kwamba
kuanzia leo wanajeshi wetu
wataanza kuondoka kurejea
nyumbani.Kama ulivyotuahidi
kwamba mnafanya uchunguzi
wa shambulio lile naomba
mtakapokuwa mmekamilisha
uchunguzi wenu mtujulishe
mara moja tufahamu nani
walioshambulia na kuua
wanajeshi wetu.Vile vile bado
kuna mwanajeshi wetu mmoja
aliyekuwa mkuu wa vikosi
vyetu hapo Tanzania Jenerali
William mpaka sasa hajulikani
alipo.Ningeomba mtusaidie
kumtafuta huyo mtu wetu na
kama ikiwezekana tunaweza
kutuma watu wetu
wakashirikiana na idara zenu
katika kumtafuta” akasema
Rais William
“Mheshimiwa Rais kwanza
kabisa niendelee kutoa pole
nyingi sana kwa vifo vya
wanajeshi wenu na
ninakuahidi kwamba idara
zetu za uchunguzi zinafanya
kila lililo ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha waliofanya mauaji
yale wanapatikana na
kufikishwa mbele ya
sheria.Kuhusu Jenerali
William tutaendelea kumtafuta
hadi tuhakikishe
anapatikana.Kama
nilivyokwambia awali kwamba
hatuhitaji msaada kutoka nje
idara zetu zina uwezo mkubwa
wa kufanya uchunguzi na
ninakuhakikishia kwamba
tutawapata waliofanya
shamulio lile.Kuhusu
kuwaondoa wanajeshi wa
Marekani walioko hapa nchini
sina kipingamizi katika hilo na
ninawashukuru sana kwa kazi
kubwa waliyoifanya ya
kusaidia kurejesha amani na
hadi sasa hivi hali inarejea kwa
kasi kuwa ya kawaida.Watu
wameanza kuendelea na
maisha yao ya kila siku”
“Ahsante Dr Fabian.Ni
hilo tu nililotaka kukujulisha
alfajiri ya leo.Natumai
tutaendelea kuwasiliana zaidi”
akasema Rais William
wakaagana na kukata simu
“Mshenzi mkubwa huyu !
akasema Dr Fabian na kuitupa
simu pembeni
“Mpango wetu
umefanikiwa.Walichokuwa
wanakihitaji ni mafuta tu na
baada ya kuyakosa wameamua
kuondoa wanajeshi
wao.Namuombea Mathew
Mulumbi huko aliko amalize
misheni yake haraka ili tuweze
kuwaeleza dunia nini
kimefanywa na Marekani”
akawaza Dr Fabian na
kuchukua simu akampigia
Ruby
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby
“Ruby samahani kwa
kukuamsha”
“Hapana sijalala
mheshimiwa rais sisi bado
tunaendelea na
kazi.Tulikuahidi kwamba
hatutalala hadi tuhakikishe
tumemaliza zoezi”
“Poleni na ahsanteni sana
kwa kazi hiyo kubwa
mnayoifanya.Kuna lolote
mmelipata mpaka hivi sasa
kutoka kwa wale jamaa
mnaowahoji?
“Watu wale ni wagumu
sana kufunguka hasa huyu
jenerali William.Lakini Gosu
Gosu anaendelea na zoezi la
kuwafungua na nina uhakika
watafunguka na kueleza kila
kitu” akasema Ruby
“Sawa Ruby.Nimekupigia
kukujulisha kwamba nimetoka
kuzungumza na Rais wa
Marekani muda mfupi
uliopita.Alinipigia kunijulisha
kwamba wameamua
kuwaondoa wanajeshi wao
kufuatia shambulio katika
kambi yao lililopelekea
wanajeshi kuuawa.Mpango
wetu umekwenda vizuri kama
tulivyokuwa tunataka na baada
ya kukosa mafuta wenyewe
wameamua kuondoka”
akasema Dr Fabian na Ruby
akacheka kidogo
“Wameona hakuna tena
sababu ya kuendelea kutumia
gharama kuhudumia
wanajeshi wao hapa wakati
hakuna manufaa yoyote
wanayoyapata.Hii inaonyesha
kuwa hupeleka wanajeshi wao
mahala ambako kuna maslahi
kwao.Unapoona mahala kuna
wanajeshi wao ujue lazima
kwa namna moja au nyingine
kuna kitu wanafaidika nacho
kwa wanajeshi wao kuwapo
mahala hapo lakini sehemu
ambazo hakuna faida katu
hawatumi wanajeshi ndiyo
maana wameamua kuondoka
baada ya mafuta
kukatika.Wasidhani kwamba
mambo yameishia hapa bado
hayajakwisha.Yawezekana
wanadhani hatujui chochote
kuhusiana na mipango yao
miovu juu yetu” akasema Ruby
“Kuna taarifa zozote
kutoka kwa Mathew Mulumbi?
“Nimezungumza na Nawal
leo saa tisa akaniambia
kwamba ataanza safari ya
kuelekea Tehran leo saa mbili
za asubuhi.Ni safari ya saa
tano hadi sita hivi na
tunategemea kuanzia saa saba
atakuwa amefika Tehran na
ndiye atakayetupa taarifa zote
za kuhusiana na Mathew
Mulumbi” akasema Ruby
“Sawa Ruby.Naomba
mjitahidi sana kuwabana hao
jamaa hadi wafunguke kila
kitu”
“Tunajitahidi mheshimiwa
Rais” akasema Ruby na
kuagana na Rais.
Ruby akitoka ofisini kwake
na kuelekea katika upande wa
afya ambako Jenerali William
alipelekwa baada ya kupoteza
fahamu akamkuta Gosu Gosu
akisubiri ili akaendelee
kumuhoji
“Vipi maendeleo yake?
Ruby akauliza
“Tayari amezinduka ila
madaktari wameshauri
tumpumzishe kidogo kama saa
moja ndipo zoezi likaendelee”
akasema Gosu Gosu.Jenerali
William alikuwa amelala
kitandani na mikono
imefungwa pingu.Uso wake
haukuwa ukitazamika.
“Nimezungumza na Rais
muda si mrefu” akasema Ruby
na kumueleza Gosu Gosu kila
kitu alichoelezwa na Rais
“Hatimaye wameondoka
hawa ambao naweza kuwaita
majambazi wa rasilimali
zetu.Imetumika akili kubwa
kuwaondoa vinginevyo
wangeendelea kuchukua
mafuta hadi yakauke”akasema
Gosu Gosu
“Tunaendelea kuishinda
hii vita japo bado mapambano
yanaendelea lakini hakuna
kukata tamaa tutapambana
hadi mwisho wake” akasema
Ruby
“Huyu mwanajeshi wao
alituita sisi watu wenye akili
finyu na hivi sasa
ninamuonyesha watu wenye
akili finyu ni watu wa namna
gani.Analia kama mtoto
mdogo na kuomba msamaha
hatarudia tena kutamka
maneno yale.Kiburi
kimemuisha” akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu unadhani
anaweza akafunguka hivi
karibuni?
“Itachukua muda.Huyu ni
mwanajeshi mkomavu na kwa
mwanajeshi wa aina yake si
jambo jepesi kutoa siri lakini
tutatumia kila njia hadi
tuhakikishe anafunguka na
kusema ukweli” akasema Gosu
Gosu
“Ninataka kumuhoji tena
kabla ya kumpumzisha kisha
nimuanze Yule gaid Assad”
“Sawa Gosu Gosu.Kabla
hujaendelea kwa nini
usichukue mapumziko mafupi
halafu uendelee baadae?
“Hakuna muda wa
kupumzika Ruby.Hawa jamaa
hawakupumzika kuchukua
mafuta na mipango yao
inafanyika usiku kucha.Hapa
ni kazi tu.Wewe nenda
kapumzike Ruby mimi hapa
umenifikisha
nyumbani.Nilipokuwa msituni
hatukuwa na muda wa kulala
hivyo hadi hawa jamaa
watakapofunguka ndipo
nitakwenda kupumzika”
akasema Gosu Gosu
“Sawa Gosu Gosu mimi
ngoja nikapumzike kidogo
umekuwa ni usiku mrefu sana
lakini wenye mafanikio”
akasema Ruby na kutoka
akaenda kupumzika.
TEHRAN – IRAN
Nawal aliwasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Imam Khomein jijini
Tehran.Baada ya kukamilisha
taratibu zote na kuruhusiwa
kuingia nchini Iran, Nawal
alipokelewa na mtu
aliyekuwapo pale uwanjani
akimsubiri akampeleka katika
hoteli alikoandaliwa kisha
akapelekwa nyumbani kwa
Vahid Ghorbani
“Nawal karibu sana
Tehran” akasema Vahid baada
ya Nawal kuwasili katika
makazi yake
“Ahsante sana” akajibu
Nawal
“Mara ya kwanza Tahran?
Akauliza Vahid
“Ndiyo hii ni mara yangu
ya kwanza ninafika hapa
Tehran”
“Karibu sana
Tehran.Jisikie nyumbani”
akasema Vahid kisha
wakaungana wote katika
chumba cha chakula kupata
chakula cha mchana baada ya
hapo Vahid na Nawal wakawa
na mazungumzo
“Nawal naamini Habiba
amekwisha kueleza mengi
kuhusu mimi” akasema Vahid
“Mama Habiba alinipa
maelezo mafupi tu kwamba
nitapokelewa uwanja wa ndege
lakini hakuniambia nani
atanipokea hivyo sifahamu
chochote kuhusu wewe”
akajibu Nawal
“Naitwa Vahid
Ghorbani.Mimi na Habiba
tuliwahi kuwa katika
mahusiano na mimi ndiye
baba mzazi wa Najma”
akasema Vahid na Nawal
akaonyesha mshangao
“Wewe ndiye baba mzazi
wa Najma?
“Ndiyo.Mimi ni baba yake
mzazi”
“Hata hivyo mmefanana
sana.Pole mzee kwa
kuondokewa na mwanao”
akasema Nawal
“Ahsante nashukuru”
akajibu Vahid na ukimya
mfupi ukapita
“Umemuita Habiba
mama.Wewe pia ni mwanae?
Akauliza Vahid
“Mimi nilikuwa mke wa
mwanae Abu Dahir”
“Ouh kumbe wewe ndiye
uliyekuwa mke wa Abu
Dahir.Pole sana pia kwa kifo
cha mumeo.Habiba amepata
pigo kubwa kwa kupoteza
watoto wawili ndani ya kipindi
kifupi” akasema Vahid
“Ni kweli inaumiza mno
kupoteza mtu unayempenda”
akasema Nawal
“Nini hasa dhumuni la
kuja Tehran Nawal? Uko hapa
kwa mapumziko? Habiba
aliniambia nikupokee lakini
hakunieleza nini unakuja
kufanya hapa Tehran”Akauliza
Vahid
“Hapana mzee siko hapa
kwa ajili ya mapumziko.Niko
hapa kuonana na Abu Zalawi”
“Abu Zalawi?! Vahid
akashangaa
“Ndiyo.Habiba aliniambia
wewe ndiye utakayenisaidia
niweze kuonana naye”
akasema Nawal.Vahid akavuta
pumzi ndefu
“Nilikwisha mueleza
Habiba kwamba sitaki
kujihusisha tena na suala
lolote linalohusiana na Abu
Zalawi.Sitaki kuwa na ukaribu
wowote na magaidi ! akasema
Vahid kwa sauti kali kidogo
“Mzee Vahid ninaomba
unisaidie niweze kuonana na
Abu Zalawi ni muhimu sana”
“Wewe naye unahusika na
mambo hayo? Akauliza Vahid
“Mambo gani mzee?
Akauliza Nawal
“Ugaidi.Nawe pia
unajishughulisha na mambo
hayo?
“Hapana mzee mimi
sijihusishi na hayo mambo ila
nina ujumbe muhimu sana
kwa Abu Zalawi kutoka kwa
Habiba.Nisaidie nionane naye
tafadhali.Sina mtu mwingine
hapa Iran anayeweza
kunisaidia zaidi yako” akasema
Nawal na Vahid akakunja sura
“Nilimwambia Habiba na
ninarudia kukwambia nawe
pia kwamba hii itakuwa ni
mara ya mwisho mnanihusisha
na Abu Zalawi.Nitakusaidia
kwa sababu umesafiri umbali
mrefu lakini ni marufuku
kunihusisha na Abu
Zalawi.Sitaki kulisikia tena
jina Abu Zalawi katika masikio
yangu.Umenielewa Nawal?
Akauliza Vahid
“Nimekuelewa mzee”
akasema Nawal.
“Vizuri” akasema Vahid na
kuchukua simu yake na
kumpigia waziri wa ulinzi wa
Iran Brigedia Jenerali Ahsan
Javad ambaye ni rafiki yake
mkubwa
“Vahid habari yako”
akasema Brigedia Jenerali
Ahsan Javad
“Nzuri sana mheshimiwa
waziri.Nimekupigia ninahitaji
msaada wako tena”
“Nini unahitaji Vahid?
Akauliza waziri wa ulinzi.
“Ninahitaji kuonana tena
na Abu Zalawi” akasema Vahid
na Brigedia Jenerali Ahsan
Javad akasita
“Mheshimiwa waziri”
akaita Vahid
“Vahid kuna jambo
limetokea jana usiku na sina
hakika kama umepata taarifa”
“Jambo gani mheshimiwa
waziri?
“Nyumba aliyokuwa
anakaa Abu Zalawi ilivamiwa
na watu jana usiku wakitaka
kumuua”
“Abu Zalawi ni mzima?
Akauliza Vahid kwa wasi wasi
“Usihofu,Abu Zalawi ni
mzima.Waliweza kupambana
na wavamizi hao na
wakawashinda.Kwa sasa Abu
Zalawi amehamishwa kutoka
katika yale makazi na
kupelekwa sehemu
nyingine.Nitawasiliana na
waziri wa intelijensia
mheshimiwa
Sassan.Nitawasiliana na
Sassan kufahamu mahala alipo
kisha nitakufuata hapo kwako”
akasema Brigedia Jenerali
Ahsan Javad
“Ahsante sana waziri”
akasema Vahid na kukata simu
“Abu Zalawi alivamiwa
jana usiku na watu
wasiojulikana” Vahid
akamwambia Nawal
“Abu ni mzima? Akauliza
Nawal kwa wasi wasi
“Ndiyo ni mzima.Hana
tatizo lolote.Wavamizi zote
waliuawa.Hata hivyo
amehamishwa makazi na
kupelekwa katika makazi
mengine” akasema Vahid
wakaendelea na mazungumzo
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 5
Toka asubuhi Mathew
alikuwa amepumzika katika
jumba kubwa la Sassan.Ulinzi
ulikuwa mkali kuzunguka
jumba hili la waziri wa
intelijensia na usalama wa
taifa wa Iran.Akiwa
amepumzika pembeni ya
bwawa la kuogelea baada ya
chakula cha mchana Mathew
akafuatwa na mlinzi na
kujulishwa kwamba
anahitajika ndani.Mathew
akanyanyuka na kuelekea
ndani akidhani labda Sassan
amerejea.Mara tu alipoingia
ndani akapatwa na mstuko
baada ya kukutana na watu
ambao hakuwatarajia.Waziri
wa ulinzi wa Iran Brigedia
Jenerali Ahsan Javad alikuwa
ameongozana na Vahid
pamoja na Nawal
“Karibuni” akasema
Mathew.Nawal akainuka na
kwenda kumkumbatia
“Abu Zalawi nimefurahi
kukuona tena” akasema Nawal
“Mimi pia Nawal
nimefurahi,sikutegemea
kukuona hapa” akasema
Mathew
“Abu Zalawi pole sana kwa
tukio la jana usiku” akasema
Brigedia Jenerali Ahsan Javad
“Ahsante sana
mheshimiwa waziri” akasema
Mathew
“Hawakufanikiwa
kukuumiza wale wavamizi?
Akauliza Vahid
“Hawakufanikiwa.Tuliwaw
ahi kabla hawajafanikiwa
lengo lao” akasema Mathew
“Abu Zalawi tunashukuru
kwa kuwa uko mzima na
unaendelea
vizuri.Kilichotuleta hapa
mchana huu ni huyu mgeni
wako ambaye amekuja
kuonana nawe.Tutamuacha
hapa mtazungumza kisha
baadae atakuja kuchukuliwa
kurejeshwa hotelini
kwake”akasema Vahid
Brigedia Jenerali Ahsan
Javad na Vahid waliondoka na
kumuacha Nawal ambaye
aliongozana na Mathew
kwenda katika bwawa la
kuogelea.
“Nawal karibu sana
Iran.Niliambiwa na Habiba
kwamba unakuja Tehran
nikadhani ni
utani.Nilipokuona nimestuka
sana sikutegemea” akasema
Mathew
“Mathew mimi nawe
tumekwisha kuwa kama
mapacha.Ulipo nami
nipo.Mahala pekee ambako
siwezi kukufuata ni mbinguni
ambako kila mmoja ataenda
kwa wakati wake lakini kwa
hapa duniani siwezi kukuacha
ukawa sehemu ya hatari
lazima niwepo karibu yako ”
“Ahsante sana
Nawal.Karibu tena kwa mara
nyingine” akasema Mathew na
muhudumu akafika
akawaletea vinywaji
“Mahala pazuri sana hapa
na unapata huduma nzuri”
akasema Nawal
“Hapa ni nyumbani kwa
waziri wa Intelijensia na
usalama wa taifa anaitwa
Sassan” akasema Mathew
“Inapendeza kama tayari
umekwisha tengeneza
mtandao” akasema Nawal
“Ili kufanikisha misheni
yangu lazima nitengeneze
mtandao kwanza na
ninashukuru Mungu kwamba
mipango yangu yote
inakwenda vizuri kabisa.Kabla
hatujaendelea mbele nataka
unipe habari za Tanzania.Ruby
na Gosu Gosu wazima?
Akauliza Mathew na Nawal
akaanza kumsimulia kila
kilichotokea nchini
Tanzania.Ilikuwa ni simulizi
iliyomsisimua sana Mathew
“Nawal nimekosa neno la
kukushukuru kwa haya
uliyoyafanya kwa kushirikiana
na akina Ruby.Bila ninyi hivi
sasa Tanzania ingekwisha
tumbukia katika janga lingine
kubwa sana na maelfu ya watu
wangepoteza uhai.Ahsante
sana Nawal” akasema Mathew
“Mathew anayepaswa
kushukuriwa katika hili ni
Mungu pekee ambaye
ametuwezesha sisi kuhakikisha
mipango ile miovu haifanikiwi
na vile vile tumshukuru pia
mama Habiba
Jawad.Amewasaliti wenzake ili
Tanzania iwe salama” akasema
Nawal
“Kila ninapomtafakari
Habiba ninashindwa
nimuweke katika kundi
gani.Siamini kama mtu yule
ambaye nilikula kiapo cha
kumuua amegeuka na kuwa
mmoja kati ya watu muhimu
mno” akasema Mathew
“Sote hatukuwa
tukimfahamu vyema Habiba
Jawad hapo kabla” akasema
Nawal
“Vipi maendeleo yake?
Akauliza Mathew na Nawal
akamueleza kila kitu
kuhusiana na kile kilichotokea
Riyadh.Mathew aliyekuwa
ameinamisha kichwa
akitafakari akainua kichwa na
kusema
“Nawal umefanya kosa
kuja Tehran.Unapaswa kurejea
Riyadh.Mama Habiba hapaswi
kabisa kuwa peke
yake.Hapaswi kuwa katika
hatari yoyote kwa sasa kwani
bado tunamuhitaji mno.Yeye
ndiye daraja kati yetu na G20
na mipango yote ya G2o yeye
ndiye anayetupatia hivyo
hapaswi kwa namna yoyote ile
kuwa katika hatari” akasema
Mathew
“Mathew mama Habiba
analifahamu hilo lakini yeye
mwenyewe ameweka
kipaumbele kikubwa kwako na
ndiyo maana akanituma nije
hapa kukusaidia na
kuhakikisha unakuwa salama”
akasema Nawal
“Hapana Nawal lazima
urejee Riyadh.Hatuwezi
kumuacha Habiba peke
yake.Yuko katika hatari
kubwa” akasema Mathew
“Mathew misheni
unayoifanya ni kubwa sana na
ndiyo maana Habiba ameona
maisha yake hayana thamani
kama hiki unachokifanya huku
na akanitaka nije kukusaidia”
“Nalifahamu hilo Nawal
lakini lazima tumlinde Habiba
na tuhakikishe anakuwa
salama.Usihofu kuhusu mimi
nitakuwa salama na
nitaifanikisha misheni yangu
bila matatizo” akasema
Mathew
“Mathew ! akasema Nawal
“Nawal naomba
tusiendelee kujadili hilo.Sote
tunafahamu umuhimu wa
Habiba hivyo lazima tuendelee
kumlinda.Habiba akiuawa
kuna mengi tutayakosa hivyo
basi naomba urudi Riyadh
kuhakikisha Habiba anakuwa
salama.Endapo nitahitaji
msaada sintasita kukuomba
uje unisaidie” akasema
Mathew wakaendelea na
maongezi mengine.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 6
Saa moja za jioni Sassan
Mahmoud akiwa na Mathew
waliwasili ikulu kama
alivyokuwa ameelekeza Rais
Armen Hijazi ambaye alitaka
kuonana na
Mathew.Walipokewa na
wafanyakazi wachangamfu
sana na kukaribishwa katika
makazi ya Rais wa Iran.Baada
ya muda Rais Armen Hijazi
akajitokeza na
kuwakaribisha.Armen Hijazi
alikuwa ni mcheshi tofauti na
anavyoonekana katika hotuba
zake mbali mbali
“Abu Zalawi nimefurahi
kukutana nawe.Karibu sana
Iran” akasema Rais Armen
halafu akamuomba radhi
Mathew kuwa ana
mazungumzo muhimu na
waziri Sassan.Mathew akabaki
peke yake pale sebuleni Rais
Armen na Sassan wakaenda
katika chumba kingine kwa
ajili ya mazungumzo.
“Sassan nataka kupata
mrejesho kuhusu ile
orodha.Tayari mmeipitia na
kujiridhisha kama ni ya kweli?
Akauliza Rais Armen
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Tumeipitia ile orodha na
tumejiridhisha ni ya kweli”
akajibu Sassan
“Vizuri sana.Sasa baada ya
kujiridhisha kwamba ni ya
kweli nataka hatua za haraka
sana zianze kuchukuliwa kwa
wale wote walioorodheshwa
katika ile orodha.Nataka kazi
hiyo ianze usiku huu.Nataka
hadi kufika kesho asubuhi
majasusi wote wa Israel wawe
wametiwa nguvuni na jambo
hili lifanyike kimya kimya bila
kutumia nguvu
yoyote.Wakisha kamatwa
wapelekwe mahala wakahojiwe
tujue kile ambacho wamekuwa
wakikichunguza hapa Iran”
akasema Rais Armen halafu
wakatoka ndani ya kile
chumba wakarejea sebuleni na
Sassan hakukaa akamuaga
Mathew kwamba anakwenda
katika majukumu mengine.
“Abu Zalawi ,mheshimiwa
Sassan anaondoka kidogo
anakwenda kuendelea na
majukumu mengine.Kazi yake
ilikuwa kukuleta tu
hapa.Naomba Kama hutajali
tutoke nje kidogo.Mimi
hupenda kufanya
mazungumzo na wageni
wangu nikiwa bustanini”
akasema Rais Armen wakatoka
mle ndani wakatembea
kuelekea katika bustani nzuri
ambako kulikuwa na sehemu
nzuri kwa ajili ya kupumzika
na maongezi.
“Abu Zalawi napenda
kwanza kuchukua nafasi hii
kukukaribisha sana Iran”
akaanzisha maongezi Rais
Armen
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais”
“Pili napenda nikupe
shukran nyingi sana kwa
kitendo cha kishujaa
ulichokifanya cha kuwarejesha
nyumbani watu wetu ambao
tulikwisha hisi wameuawa
.Kila mtu hapa Iran anafurahi
sana kwa kitu
ulichokifanya.Hongera sana”
akasema Rais Armen na
Mathew akatabasamu
“Kabla sijaenda mbali
zaidi nataka nikupe pole sana
kwa kile kilichotokea jana
usiku.Alinifuata waziri Sassan
na kunieleza kilichokuwa
kimetokea pale mahala
ulipokuwa
ukiishi.Nikushukuru tena kwa
kuongoza mapambano na
kuwashinda wale
wavamizi.Bila wewe watu wetu
wote wangeuawa.Ahsante sana
Abu Zalawi” akasema Rais
Armen na Mathew akatingisha
kichwa kupokea shukran zile
“Bado nitaendelea
kukushukuru kwa kutupatia
orodha ya majasusi wa Israel
walioko hapa nchini.Kwa
muda mrefu mahusiano yetu
na Israel yamekuwa si mazuri
.Israel wanatutuhumu kwa
kufadhili makundi ya
wanamgambo wa
Hezbollah,Islamic Jihad na
Hamas ambao wamekuwa
wakipambana na serikali ya
Israel kwa muda
mrefu.Tunafahamu kuwa
Israel wana majasusi wao hapa
Iran lakini ilikuwa ni kazi
ngumu kwetu kuwabaini ni
akina nani na wako wapi hivyo
basi kwa orodha ile
uliyotupatia itatusaidia mno
katika kuwabaini majasusi
hawa na kuchukua hatua kali
dhidi ya😵rodha hii hata
majasusi wetu wameshindwa
kuipata hivyo narudia tena
kukupa pongezi nyingi kwa
jambo hili kubwa” akasema
Rais Armen na kunyamaza
kidogo
“Waziri Sassan alinieleza
kwamba unaomba kupatiwa
hifadhi hapa Iran.Usihofu
kuhusu hilo kwani tayari
nimekwisha toa maelekezo
kwamba upatiwe hifadhi hapa
Iran na mchakato huo
umekwisha anza.Ninaamini
hapa utakuwa salama”
akasema Rais Armen
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais kwa
kukubali kunipatia
hifadhi.Hapa naamini
nitakuwa salama zaidi”
akasema Mathew na
wahudumu wakafika
wakawaandalia kahawa.Rais
Armen hupenda sana kunywa
kahawa nyakati za jioni
“Abu Zalawi” akasema
Rais Armen baada ya
wahudumu kuondoka
“Ujio wako hapa Iran
umekuwa ni kama vile
kuongeza mafuta kwenye
moto.Umezidi kuchochea
msuguano wetu na Marekani
kwani tayari wanafahamu uko
hapa na tayari wamekwisha
toa tamko kupitia kwa waziri
wao wa mambo ya nje kwamba
tukusalimishe wewe na wale
mateka wengine lakini
ninakuhakikishia kwamba
hatuwezi kufanya kitu kama
hicho.Ninafahamu kitendo
ulichowafanyia cha kulipua
ubalozi wao nchini Tanzania
kitawafanya wakusake usiku
na mchana hadi pale
watakapohakikisha
wamekupata lakini narudia
tena kukuhakikishia Abu
Zalawi kwamba hatutaweza
kamwe kukukabidhi kwa
wamarekani.Utaishi hapa
ikiwezekana kwa maisha yako
yote yaliyobaki kama utapenda
na tutakulinda” akasema Rais
Armen
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mathew
“Mzozo wetu na Marekani
unazidi kukua siku hadi
siku.Kama unavyofahamu
kuwa tumewekewa vikwazo
vingi vya kiuchumi kwa lengo
la kuporomosha uchumi wetu
lakini vikwazo hivyo
vinawaumiza raia wa Iran
ndiyo maana kwao mtu
anayefanya jambo baya kwa
wamarekani anaonekana
shujaa.Raia wamejenga chuki
kubwa sana dhidi ya Marekani
kutokana na ukandamizaji
inaoufanya kwa taifa letu
ndiyo maana hawatatuelewa
endapo tutakukabidhi kwa
Marekani.Abu Zalawi naomba
kama hutajali unieleze historia
yako ili nikufahamu vyema
kwani tayari nimeelezwa
mambo kadhaa na wasaidizi
wangu lakini nitafurahi zaidi
kama nikisikia kutoka kwako
wewe mwenyewe” akasema
Rais Armen na Mathew
akamuelezea historia yake ile
ya kutengeneza kama Abu
Zalawi
“Historia yako inasisimua
sana japo ndani yake ina
mambo ya kigaidi lakini kwa
ukandamizaji unaofanywa na
nchi za Marekani na Israel
ninathubutu kusema kwamba
wanastahili
kushambuliwa.Siku za
karibuni mzozo wetu umekuwa
mkubwa zaidi na tumefikia
hadi hatua ya kutishiana
kushambuliana.Marekani
wamekuwa wakifanya mazoezi
ya kijeshi na washirika wao
ambao ni nchi jirani zetu na
sisi tumetoa onyo kwamba
wakithubutu kurusha hata
risasi moja katika ardhi ya Iran
basi tutaiharibu
Marekani.Tutaichakaza vibaya
mno kipigo ambacho
hawataamini” akasema Rais
Armen
“Hapa sasa amenifikisha
ninapopahitaji” akawaza
Mathew
“Marekani” akasema
Mathew
“Imejiona ni mtawala wa
ulimwengu huu na kwamba
wanaweza kufanya chochote
katika taifa lolote lile
wakiamini wao ndio wenye
uwezo mkubwa kijeshi kuliko
mataifa mengine duniani”
akasema Mathew na Rais
Armen akacheka kidogo
“Wanajidanganya.Nchi
nyingi kwa sasa zinapanua
teknolojia yao ya silaha hivyo
basi wakijidanganya kwamba
wao ndio wenye uwezo
mkubwa kijeshi watajikuta
wakipigwa kipigo kikali sana
siku moja” akasema Rais
Armen
“Mheshimiwa Rais
Marekani wamekuwa
wanatishia kuishambulia Iran
vitisho vilivyoanza muda
mrefu.Unadhani kwa nini
mpaka leo hii hawajaweza
kufanya hivyo? Ni kwa sababu
ya vitisho mnavyowapa?
“Si
vitisho.Tunachokiongea sisi si
vitisho ni vitu vya
kweli.Nikisema tutaichakaza
Marekani ni kitu cha kweli
kwani uwezo huo tunao”
“Kwa sasa Iran inao uwezo
wa kurusha kombola
linaloweza kufika Marekani?
Akauliza Mathew
“Bajeti yetu ya ulinzi
haiwezi kulingana na ile ya
Marekani lakini uwezo wetu
wa kivita umeimarika mno hivi
sasa.Tumesomesha watu wetu
wengi na sasa wanatusaidia
katika kupanua teknolojia yetu
ya silaha na kwa taarifa yako
hata wale raia wetu
uliowakomboa na kuwarejesha
nyumbani ni wanasayansi
walioko jeshini na walikwenda
Urusi kujifunza teknolojia
mbali mbali za utengenezajiw
a silaha.Tunazo silaha kali
sana hivi sasa na tunao uwezo
wa kuishambulia
Marekani.Tumekuwa
tunasaidiana na washirika
wetu wa karibu katika
kupanua teknolijia yetu ya
silaha na hili ndilo
limeiogopesha Marekani
kutaka kuingia katika vita na
sisi na yamebaki maneno tu
kwamba watatushambulia”
akasema Rais Armen
“Mheshimiwa Rais
kumekuwa na tuhuma kutoka
kwa Marekani kwamba Iran
inazo au inakusudia
kutengeneza silaha za nyuklia
kuna ukweli gani juu ya jambo
hili? Akauliza Mathew
“Abu Zalawi ungefaa sana
kuwa mwandishi wa habari
kwa maswali unayouliza lakini
kujibu swali lako hizo ni
propaganda tu za Marekani na
washirika wake hazina
ukweli.Bado hatujafikia hatua
ya kutengeneza bomu la
nyuklia japo tukiamua
hatuwezi kushindwa.Abu
Zalawi suala hili la sisi na
Marekani ni suala pana sana
na lenye mambo mengi hivyo
hatuwezi kulimaliza kwa usiku
huu.Hayo tuliyoyazungumza
hayakuwa msingi wa kile
nilichokuitia hapa.Kubwa hasa
ukiacha shukrani kwako ni
kutaka kufahamu namna
ulivyoweza kupata orodha ile
ya majasusi wa Mossad
walioko hapa Iran” akasema
Rais Armen
“Mheshimiwa rais ninao
watu wangu ndani ya Mossad
ambao wameniwezesha
kuipata orodha ile”
“Abu Zalawi kama
umeweza kupata orodha kama
hii basi unaweza ukafanya
mambo mengine makubwa
zaidi kwetu.Ninakuona ni mtu
mwenye faida kubwa kwetu na
kwa kuwa utaishi hapa Iran
ninataka kukupatia kazi”
akasema Rais Armen
“Nipo tayari mheshimiwa
Rais kwa kazi yoyote
utakayonipatia”
“Ninataka utoke kuwa
gaidi na kuwa
jasusi.Nitakupeleka mafunzoni
utafundishwa masuala ya
ujasusi na utakapomaliza
utafanya kazi katika wizara
yetu ya ujasusi ukijielekeza
zaidi Israel ambako tayari una
watu wako ndani ya
Mossad.Utaachana na mambo
ya kuua watu kwa ugaidi na
badala yake utafanya kazi
kubwa zaidi ya kuwalinda watu
wa Iran” akasema Rais Armen
na ukimya ukatanda
“Picha imegeuka
tena.Nikikubali kwamba
nikafundishwe ujasusi ni
mafunzo ya muda mrefu na
mimi sina muda wa kuendelea
kupoteza hapa Iran.Nikisema
hapana wataanza kuwa na
mashaka nami.Hapa
nimewekwa mtegoni na
endapo nikikosea kidogo tu
misheni nzima itaharibika”
akawaza Mathew
“Abu Zalawi usihofu
utakuwa salama.Maisha yako
yatakuwa mazuri na
utayafurahia.Nimefanya
maamuzi haya baada ya kuona
uwezo mkubwa ulio nao hivyo
nimeona unafaa zaidi kuwa
jasusi kuliko kuwa gaidi.Hata
hivyo sikulazimishi unipe jibu
leo.Nakupa muda ukafikirie
hadi kesho uwe tayari
umefanya maamuzi ili
maandalizi yaanze mara moja”
akasema Rais Armen.Mathew
akazama mawazoni kwa muda
halafu akasema
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo nataka nikueleze lakini
ninakuomba kile
nitakachokueleza kibaki baina
yetu.Nataka nikueleze ukweli”
“Usihofu Abu Zalawi
niambie chochote nitakitunza”
akasema Rais Armen
“Mheshimiwa Rais kama
nilivyokwambia kwamba
nataka nikueleze ukweli…”
akasema Mathew na kusita
kidogo
“Endelea Abu Zalawi”
“Mheshimiwa Rais mimi si
gaidi,mimi ni jasusi” akasema
Mathew na nusura kikombe
cha kahawa alichokishika Rais
Armen kimponyoke na
kuanguka
“Unasema? Akauliza Rais
Armen
“Mimi si gaidi kama
ninavyojulikana sasa bali mimi
ni jasusi”
“Jasusi ? Mbona sikuelewi
Abu Zalawi?
“Jina langu ni Mathew
Mulumbi na si Abu
Zalawi.Mimi mtanzania”
akasema Mathew na kuzidi
kumchanganya Rais Armen
“Bado sikuelewi Abu
Zalawi.Hebu jaribu kutafuta
namna ya kunifanya nikuelewe
hicho unachoniambia”
akasema Rais Armen
“Nafahamu mheshimiwa
Rais haitakuwa rahisi
kunielewa lakini nataka
nirudie tena kukuhakikishia
kwamba mimi ni jasusi na si
gaidi kama ninavyojulikana
hivi sasa.Jina langu ni Mathew
Mulumbi mzaliwa wa Tanzania
na nimefanya kazi katika
shirika la ujasusi Tanzania kwa
muda mrefu hadi nilipoamua
kuachana na shirika hilo na
kuanza kufanya shughuli
zangu binafsi” akasema
Mathew na kunyamaza kidogo
huku sura ya Rais Armen
ikiendelea kuonyesha
mshangao mkubwa.
“Pamoja na kuacha kazi
katika shirika la ujasusi la
Tanzania niliendelea bado
kushirikishwa katika misheni
mbali mbali za kijasusi na hadi
misheni ya mwisho ambayo
ndiyo imenipelekea mimi
kufika hapa nilipofika leo na
kufahamika kama Abu Zalawi”
Mathew akamsimulia Rais
Armen mkasa mzima wa
kutekwa kwa Olivia namna
alivyoweza kupambana na
magaidi wa IS hadi alipotekwa
na majasusi wa Mossad na
kupelekwa Israel.
“Haya mbona maajabu”
akawaza Rais Armen
akimtazama Mathew kwa jicho
la mshangao.Mathew
hakumjali akaendelea
“Nilifungwa katika gereza
nchini Israel kwa miaka mitatu
nikipatiwa mateso makali
lakini sikuwahi kufumbua
mdomo wangu kutamka
chochote hadi pale
walipoamua kuigusa familia
yangu ndipo tulipoingia
makubaliano na Mossad ya
kumsaka Habiba Jawad
ambaye alikuwa mfadhili
mkuu wa makundi ya kigaidi
ya IS na mengine ya
wanamgambo wa kipalestina
wanaopigana na serikali ya
Israel” akasema Mathew na
kumuelezea Rais Armen
makubaliano aliyoyafanya na
Mossad na namna alivyoweza
kujenga urafiki na Ammar
Nazari.
“Hapo ndipo jina la Abu
Zalawi lilipoanza.Taarifa zote
za kuhusiana nami kama Abu
Zalawi si za kweli bali
zimetengenezwa na Mossad
kunifanya nikubalike na
Ammar Nazari” akasema
Mathew na kuendelea
kumsimulia namna alivyoweza
kutoroka gerezani na Ammar
Nazari na kujiunga katika
kundi lake la Ammar Nazari
brigades.Mathew alimueleza
Rais Armen kila kitu
alichokifanya akiwa na kundi
la Ammar Nazari brigades hadi
pale Israel walipoweza
kugundua maficho ya Ammar
na kumshambulia wakamuua
huku yeye na Nawal
wakinusurika baada ya
kutaarifiwa kuhusu shambulio
hilo
“Baada ya kunusurika
katika shambulio hilo
niliendelea na safari ya
kumsaka Habiba Jawad”
akasema Mathew na kueleza
mambo waliyoyaptia hadi
walipofanikiwa kukutana na
Habiba Jawad.
“Baada ya kuonana na
Habiba Jawad ile mipango
yangu yote niliyokuwa nayo ya
kutaka kumuua ikayeyuka”
akasema Mathew na
kumtazama Rais Armen
ambaye bado alikuwa
anamtazama kwa macho
yaliyojaa mshangao
“Najua utaniuliza nini
sababu ya kubadili mpango
wangu wa kumuua Habiba
ambaye alifadhili kundi la
kigaidi la IS lililofanya
matukio mabaya nchini
Tanzania.Jibu ni kwamba
nilimuoa mtoto wa Habiba
anaitwa Najma.Kumuoa mtoto
wa Habiba peke haikuwa
sababu ya kunifanya nibadili
mtazamo wangu bali kulikuwa
na sababu nyingine
kubwa.Niligundua kwamba
Habiba Jawad ambaye
nilikuwa namfikiria kabla ya
kukutana naye ni tofauti na
Habiba Yule ambaye
nilimfahamu baada ya
kuonana naye.Alinisaidia
nikafahamu mambo mengi”
akasema Mathew na
kumweleza Rais Armen
kuhusiana na namna Habiba
alivyomsaidia katika misheni
ile ya kupambana na Melanie
Chuma.
“Baada ya kufanikisha
misheni hiyo na Tanzania
ikawa salama nilirejea Riyadh
na hapo ndipo nilipogundua
jambo kubwa na la siri ambalo
wengi hawalifahamu” akasema
Mathew na kumuelezea Rais
Armen kuhusiana na kikundi
cha G20.
“Abu Zalawi unazidi
kunichanganya .Hebu nieleze
taratibu nikuelewe.Hicho
unachonieleza ni kitu kigeni
kabisa kwangu” akasema
Armen na Mathew akaanza
kumueleza tena kuhusiana na
kikundi cha G20.
“Kwa hiyo Habiba Jawad
alikuwa anafadhili makundi ya
kgaidi kwa niaba ya G20”
akasema Mathew
“Abu haya unayonieleza ni
mambo ya kweli au ni hadithi
umetunga? Akauliza Rais
Armen
“Haya yote ninayokueleza
ni ya kweli mheshimiwa Rais”
akasema Mathew na
kumueleza Rais Armen kile
kilichotokea nchini Tanzania
na namna Marekani
walivyofanikiwa
kuwachonganisha watanzania
kwa kutumia dini na kupelekea
mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe kuibuka huku wao
wakichukua mafuta.
“Wote tulistushwa na
mapigano yale yaliyotokea
Tanzania.Tunaifahamu
Tanzania ni nchi iliyojaa
amani na watu wake wanaishi
kwa upendo mkubwa licha ya
tofauti zao za dini na rangi
lakini kitendo cha kuanza
kushambuliana wao kwa wao
kiliishangaza dunia.Kumbe
hizi zote ni fitina za Marekani
kwa ajili ya kuchota mafuta !
akasema Rais Armen kwa
hasira
“Mambo haya
yanaendeshwa kwa siri kubwa
hata Rais wa Marekani
hatakiwi kufahamu chochote
kuhusu uwepo wa G20”
akasema Mathew na
kunyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Habiba alinipeleka
Marekani nikakutana na
kikundi hiki cha watu hatari
kabisa duniani” akasema
Mathew na kuelezea yale
aliyopitia kabla ya kukutana
nao
“Waliporidhika na uwezo
wangu ndipo nikakutana nao
kwa ajili ya kunikabidhi kazi
waliyotaka nikaifanye”
akasema Mathew na
kumuelezea Rais Armen kazi
ambayo alitumwa
kuifanya.Sura ya Rais Armen
libadilika na kujikunja
zaidi.Alipandwa na hasira
“Hivyo basi nililipua
ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania kama nilivyokuwa
nimeelekezwa”
“Kumbe kulipua ubalozi
ulikuwa ni mpango wao
wenyewe?
“Ndiyo ulikuwa ni mpango
wao ili nionekane gaidi na
nianze kutafutwa” Mathew
akamueleza mpango mzima
namna ulivyoandaliwa.
“Na wewe kwa nini
ulikubali kuingia katika kazi
yao na kuchafua jina lako?
Tazama sasa dunia nzima
wanafahamu wewe ni gaidi. !
akaendelea kusema kwa ukali
Armen
“Nilikubali kwa kuwa
nilikuwa na mpango mahususi
na Habiba Jawad” akasema
Mathew na kuendelea kueleza
namna alivyokamatwa jijini
Nairobi hadi alivyopelekwa
jijini Victoria nchini Sheli Sheli
ambako alikutanishwa na wale
raia sita wa Iran waliokuwa
wametekwa na kufichwa
hapo.Akaeleza namna mpango
ulivyoandaliwa wa
kuwawezesha kuiteka ndege
hadi walivyoingia nchini
Iran.Rais Armen alibaki
mdomo wazi
“Baada ya kufika hapa
ndipo wakagundua kwamba
mimi ni jasusi na si gaidi kama
walivyoelezwa na Habiba na
mpango wa kuniua ukaanza
wakiwatumia majasusi wa
Mossad”
“Wewe ulifahamu vipi
kuhusu mpango huo wa
kukuua?
“Ni kupitia Habiba
Jawad”akasema Mathew na
kumueleza namna Habiba
anavyowasiliana na makamu
wa Rais Mark Piller na hadi
walivyoweza kuipata ile
orodha ya majasusi wa Israel
“Mheshimiwa Rais
utanisamehe kwa maelezo
yangu marefu lakini
nimelazimika kutumia
maelezo hayo marefu ili uweze
kunielewa.Kwa hiyo
mheshimiwa Rais hapa nilipo
nipo katika misheni.Nimevaa
joho la ugaidi lakini mimi si
gaidi ni jasusi” akasema
Mathew.Zilipita dakika tano za
ukimya halafu Rais Armen
akasema
“Abu Zalawi usinione niko
kimya namna hii ni kwa
sababu nimekosa maneno ya
kuongea.Haya uliyonieleza
yamenipa baridi ya ghafla na
sijui niseme nini.Ni mambo
mazito ambayo sikuwa
nimetarajia kuyasikia.Lakini
kwa nini umeamua kunieleza
ukweli? Kwa nini
usingeendelea na misheni yako
kimya kimya?
“Nimeamua kukueleza
ukweli kwa sababu ninahitaji
msaada wako ili niweze
kurejea tena Marekani na
kukimaliza kikundi hiki cha
G20 ambacho kimesababisha
damu nyingi imwagike sehemu
mbali mbali duniani na hasa
nchini kwangu Tanzania”
“Marekani na dunia nzima
wanafahamu wewe ni gaidi na
unatafutwa kwa kulipua
ubalozi wao nchini
Tanzania.Huoni kwamba
unataka kujiweka katika hatari
kubwa sana endapo utataka
kurejea Marekani?
“Wamarekani
hawaufahamu ukweli.Hawajui
nini kinachoendelea nchini
mwao.Ninataka kwenda
kuwaeleza ukweli.Ninataka
kuwafumbua macho
wafahamu udhalimu
unaofanywa na watu wao
wenyewe.Hawana habari kama
kuna kirusi kilitakiwa
kusambazwa nchini Tanzania
ambacho kingeweza kusambaa
dunia nzima.Nataka
nikayaweke haya yote wazi
wayafahamu” akasema
Mathew
“Abu Zalawi hiki
unachotaka kukifanya ni kitu
cha hatari kubwa.Hawa jamaa
hawataweza kukuacha hai”
“Nalifahamu hilo
mheshimiwa Rais lakini
niliweka ahadi lazima
nikimalize kikundi hiki
ambacho kimetesa watu wengi
sana duniani hadi sasa.Lazima
nihakikishe nimekiondoa na
kuwalipia kisasi watu wote
ambao damu zao
zimemwagika kwa sababu ya
kundi hili hivyo siogopi
kufa.Nimepitia magumu
mengi hadi kufika hapa na
siwezi kuishia njiani lazima
nihakikishe nimeimaliza
misheni hii.Damu za watu
zimemwagika katika misheni
hii,maisha ya watu muhimu
kama Habiba Jawad yako
hatarini kwa sababu ya
misheni hii hivyo kwa namna
yoyote ile lazima nihakikishe
ninaimaliza” akasema Mathew
“Abu Zalawi
nimekuelewa.Ninaiona ndani
mwako dhamira ya dhati ya
kukimaliza kikundi hiki hatari
na mimi siwezi kukuzuia hasa
kwa kuzingatia kwamba
umepitia mchakato mgumu
sana hadi kufika hapa
ulipofika na umekuwa mkweli
kwangu.Nini unataka
nikusaidie ili uweze
kufanikisha misheni yako kwa
sabau hata mimi ninatamani
sana kikundi hicho kiondoke
naamini kimekuwa
kinachochea zaidi mgogoro
kati yetu na Marekani”
“Ninataka kupata picha
halisi ya kile kinachoendelea
katika vinu vyenu vya nyuklia
ili nipate kitu cha
kunikutanisha tena na Mark
Piller makamu wa rais wa
Marekani.Walitaka nilipue
kinu hicho lakini siwezi
kufanya hivyo wakati tuhuma
kwamba kuna utengenezaji wa
silaha za nyuklia si za kweli
hivyo nitahitaji nipate picha
kwa ajili ya kwenda
kuwathibitishia
kilekinachoendelea katika kinu
hicho.Jambo la pili nataka
itengenezwe taarifa bandia
kuhusu mfumo wa silaha wa
Iran ambayo ndani yake
kutakuwa na silaha kali
ambazo zina uwezo wa
kushambulia nchi zote jirani
na Iran,makombora ya masafa
marafu ambayo yanaweza
kuzishambulia manowari za
adui hata zikiwa umbali mrefu
na katika taarifa hiyo ionekane
kuna kazi inaendelea ya
kutengeneza kombora ambalo
litakuwa na uwezo wa kubeba
kichwa cha nyuklia na kufika
hadi katika jiji la Los
angeles.Wamarekani
wanaogopa kushambuliwa
nyumbani hivyo baada ya
kuiona taarifa hiyo wataogopa
na kusitisha mpango wa
kuishambulia Iran
kijeshi.Mpango huo ukifutika
dirisha la mazungumzo
litafunguliwa ili kutafuta
amani na hapo ndipo Iran
itasimama kidete kutaka
vikwazo vyote vya kiuchumi
viondolewe.Mwisho kabisa
nitaomba wale mateka wa
marekani waachiwe pamoja na
ile ndege ili kuondoa
msuguano unaoweza
kujitokeza.Huo ndio msaada
ninaoutaka mheshimiwa Rais”
akasema Mathew na zaidi ya
dakika tano za ukimya zikapita
“Abu Zalawi nimejaribu
kuyatafakari maombi yako
yana msingi.Wewe ni mtu
mwenye akili nyingi
sana.Ulipaswa kuzaliwa Iran
wewe” akasema Rais Armen na
wote wakacheka kidogo
“Kwa ujumla ni mpango
mzuri hata mimi
ninakubaliana nao.Kesho
nitatoa maelekezo na
utapelekwa katika kinu
kikubwa kabisa cha nyuklia
ambacho Marekani na
washirika wake wamekuwa
wakipiga kelele kwamba
tunakitumia katika
kutengeneza silaha za
nyuklia.Utapiga picha
uthibitishe kwamba madai yao
si ya kweli na wakati huo huo
taarifa hiyo ya silaha
unayoihitaji itakuwa
inaandaliwa” akasema Rais
Armen
Mazungumzo ya Mathew
na Rais Armen yaliendelea
hadi ilipofika saa sita za usiku
ndipo Mathew aliporejeshwa
katika makazi ya waziri
Sassan.Mara tu alipofika
alichukua simu ya nyumbani
kwa Sassan na kupiga hotelini
alikofikia Nawal akaomba
kuunganishwa na chumba
chake
“Hallow” ikasema sauti ya
Nawal akionekana kutoka
katika usingizi
“Nawal ni mimi
Mathew.Samahani kwa
kukuamsha”
“Usijali”
“Nawali nimekupigia
kukujulisha kwamba nimetoka
ikulu ya Iran sasa hivi
kuzungumza na Rais Armen
Hijazi”akasema Mathew na
Nawal akastuka
“Umetoka ikulu?
“Ndiyo nimetoka
ikulu.Nimezungumza kwa
kirefu sana na Rais Armen na
taarifa nzuri ni kwamba
misheni yetu inakaribia kufika
ukingoni” akasema Mathew na
kumueleza Nawal kila kitu
walichokizungumza na Rais
Armen Hijazi.
“Mathew umenitoa
machozi.Sikutegemea kama
mambo yangekwenda namna
hii” akasema Nawal
“Hata mimi sikuwa
nimetegemea jambo kama
hili.Nilipata akili hii hapo hapo
wakati ninazungumza na Rais
na ninashukuru kwamba
ameyakubali mawazo yangu”
“Mungu ashukuriwe
sana.Mathew mimi kesho
ninakwenda Riyadh kama
tulivyokuwa
tumekubaliana.Nitaondoka
saa mbili za asubuhi nadhani
hatutapata nafasi ya kuonana”
akasema Nawal
“Nawal tunakaribia kufika
mwisho wa misheni yetu hivyo
kuna mambo
yatabadilika.Kwanza
nitakuhitaji Marekani.Ili
kuimaliza misheni hii nahitaji
msaada wako kule.Pili
ulinieleza kwamba kuna Yule
mkuu wa vikosi vya Marekani
vilivyoko Tanzania
anashikiliwa na SNSA .Nataka
kuipata rekodi yake akikiri
kushiriki katika mipango ya
G20.Vile vile wale magaidi nao
pia lazima wakiri kuhusika
katika mipango ya G20 ya
kuchochea vurugu.Vile vile
nakihitaji kirusi ambacho
kilitakiwa kusambazwa
Tanzania” akasema Mathew
“Mathew kwa mpango
huo,itanilazimu nirejee tena
Tanzania ili nikakamilishe
hayo mambo.Nimewasiliana
na Ruby nilipofika hapa
hotelini akaniambia kwamba
Jenerali William amekubali
kueleza kila kitu.Amepewa
mateso makali na Gosu Gosu”
akasema Nawal na Mathew
akatabasamu
“Kama alikuwa anahojiwa
na Gosu Gosu lazima
afunguke.Basi anatakiwa
arekodiwe akikiri kuhusika
katika mipango yote ya G20 na
vile vile wale magaidi nao
wanatakiwa wakiri kuhusika
katika mipango ile
iliyosababisha machafuko
makubwa nchini
Tanzania.Unadhani ukifika
Riyadh unaweza ukapata
ndege ya kuelekea Afrika
mashariki hiyo kesho?
Akauliza Mathew
“Mathew nimepata
wazo.Kwa kuwa Rais wa
Tanzania yuko upande wetu na
yuko tayari kutusaidia kila
aina ya msaada kwa nini
nisizungumze na Ruby
nimuombe azungumze naye ili
atoe ndege yake ianze safari
kesho alfajiri na mapema
kuelekea Riyadh?Ni mwendo
wa takribani saa tisa kutoka
Dar es salaam hadi Riyadh na
mimi nikiondoka hapa Iran
saa mbili asubuhi nitafika
Riyadh saa saba za mchana
hivyo nitazungumza kidogo na
Habiba kisha nitaondoka
kuelekea Tanzania na kurudi
na ndege hiyo hiyo” akasema
Nawal
“Huo ni mpango mzuri
sana Nawal.Fanya hivyo”
akasema Mathew na kumpa
Nawal maelekezo
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Bado taarifa kuu
iliyotawala vyombo vya habari
asubuhi hii nchini Tanzania ni
kuondoka kwa wanajeshi wa
Marekani kufuatia shambulio
lililofanywa na watu
wasiojulikana na kuua
wanajeshi zaidi ya
thelathini.Habari nyingine
ilikuwa ni kulipuliwa kwa
sehemu ya bomba la mafuta
litokalo nchini Uganda.
Maisha katika jiji la Dar es
salaam kwa kiasi kikubwa
yalirejea kuwa ya kawaida japo
doria za magari na miguu za
askari na wanajeshi bado
ziliendelea.Maduka ,masoko
na biashara nyingine
zilifunguliwa lakini bado
wanafunzi hawakuruhusiwa
kwenda mashuleni hadi hapo
serikali itakapojiridhisha
kwamba hakuna kitisho
chochote cha kuibuka tena kwa
vurugu.
Katika ofisi kuu za SNSA
kazi ziliendelea kama
kawaida.Chini ya ardhi
kulikokuwa na vyumba
maalum kwa ajili ya mahojiano
na watuhumiwa,mkurugenzi
msaidizi wa SNSA Papi Gosu
Gosu akiwa kifua wazi alikuwa
amesimama pembeni
akimsubiri mtu aliyekuwa
anafunga kamera amalize ili
shughuli nyingine
ziendelee.Baada ya kumaliza
kufunga kamera taa
zikawashwa na majaribio
yakafanyika halafu Gosu Gosu
akaagiza aletwe katika chumba
kile Jenerali William.
Baada ya dakika chache
mlango ukafunguliwa
akaingizwwa Jenerali William
ambaye hakuweza kutembea
alikuwa anavutwa na watu
wawili.Mikononi alikuwa
amefungwa pingu na uso wake
ulikuwa umevimba.Jicho lake
moja halikuwa likiona
kutokana na kuvimba.Alikuwa
kifua wazi na mwili wake wote
ulijaa vidonda.Jenerali
William alitia huruma sana
kumtazama.
Aliketishwa kitini hakuwa
na nguvu kichwa
kikainama.Gosu Gosu
akamshika nywele na kukiinua
kichwa.
“Kama tulivyokubaliana
sasa unakwenda kukiri mbele
ya kamera yale mambo yote
uliyokiri kule ndani ili tuweke
kumbu kumbu.Tafadhali
angalia kamera na endapo
ukijaribu kuleta upuuzi
wowote nitakurejesha kule
ndani na safari hii
nitakuondoa uume
wako.Umenisikia?! akauliza
Gosu Gosu kwa ukali
“Nimekusikia ! akasema
Jenerali William kwa sauti
dhaifu.Gosu Gosu akaelekeza
anyweshwe maji halafu zoezi
likaanza mara moja.Jenerali
William akaeleza kila kitu
alichokifanya na maelekezo
yote aliyokuwa anapewa na
mwisho akakiri kupokea
maelekezo ya kusambaza
kirusi nchini Tanzania.Baada
ya zoezi kukamilika Gosu Gosu
akaelekeza Jenerali William
apelekwe akapumzishwe
kitengo cha afya akaelekeza
aletwe Assad Ismail.
Assad akaletwa naye kama
ilivyokuwa kwa Jenerali
William hakuwa na nguvu za
kutembea.Alichafuka damu
kana kwamba alikuwa
anaogelea katika dimbwi la
damu.Hakuwa na sikio la
upande wa kushoto na mkono
wake wa kulia haukuwa na
kidole hata kimoja alikuwa
amefungwa bandeji.Mkono wa
kushoto aliwekewa kifaa
maalum kwani ulikuwa
umevunjika.Mdomo ulikuwa
umemvimba na kinywani
hakuwa na meno
kadhaa.Assad hakuwa
akitazamika
“Nataka dunia ione
kwamba Tanzania hatuna
mchezo na magaidi au wale
wote wanaochezea amani yetu”
akawaza Gosu Gosu
akimtazama Assad.
“Assad umeletwa hapa
kwa ajili ya kukiri mbele ya
kamera yale yote
uliyoyafanya.Ongea kila kitu
kama ulivyokiri tukiwa kule
ndani” akasema Gosu Gosu na
kisha kwa taabu Assad akaanza
kueleza kila kitu namna
alivyoshiriki katika kuandaa
machafuko ya kidini
yaliyotokea nchini Tanzania na
kupelekea mamia ya watu
kufariki dunia.
Baada ya kumaliza Assad
naye akapelekwa katika
sehemu ya afya kwa ajili ya
kupatiwa matibabu
“Ruby nimemaliza kazi”
akasema Gosu Gosu
“Ahsante sana Gosu Gosu
kwa kazi kubwa
uliyoifanya.Watu hawa ni
wagumu na kama isingekuwa
wewe sijui kama wangeweza
kufunguka”
“Tujipongeze sote kwa kazi
kubwa na nzuri tuliyoifanya”
“Gosu Gosu sasa ni wakati
wako wa kwenda kupumzika
mimi ninakwenda kuonana na
Rais nimkabidhi majina ya
watu wote hapa nchini ambao
wametajwa na Assad kwamba
walikuwa wanashirikiana nao
katika kuratibu na kuchochea
vurugu ili ayakabidhi kwa
vyombo husika viyafanyie
kazi” akasema Ruby na Gosu
Gosu akaondoka kurejea
nyumbani kwake kupumzika.
TEHRAN - BAADA YA SIKU 2
Saa mbili za usiku jijini
Tehran,magari matatu
yaliwasili katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Imam
Khomein.Gari zile zilipita
katika geti wanako ingilia
viongozi wakuu wa kitaifa na
kuelekea karibu na ndege
moja.Milango ya gari la mbele
ikafunguliwa na watu wanne
wakashuka na kutoka katika
gari la nyuma watu watatu
wakashuka halafu mmoja wao
akafungua mlango wa gari la
kati kati akashuka Mathew
Mulumbi akiwa amevalia
nadhifu.Akaagana na wale
jamaa kisha akaanza kupiga
hatua kuelekea ndegeni mara
akasimamishwa na mmoja wa
wale jamaa aliyemkimbilia na
kumpa simu
“Rais anataka kuzungumza
nawe” akasema Yule jamaa na
Mathew akaichukua ile simu
“Mheshimiwa Rais”
akasema
“Abu Zalawi kabla
hujaondoka ninapenda
nikutakie kila la heri katika
misheni yako.Ninategemea
kila kitu kitakwenda
vizuri.Kuhusu wale mateka na
ndege yao wataondoka kesho”
“Nashukuru mheshimiwa
Rais”
“Mimi ndiye ninapaswa
kukushukuru wewe Abu zalawi
kwa kitendo chako cha
kuamua kuwa muwazi
kwangu.Hakikisha kwa namna
yoyote unafanikisha misheni
hiyo ambayo ina umuhimu pia
kwa Iran na endapo
utafanikisha misheni yako
salama unakaribishwa tena
Iran muda wowote”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mathew
“Kila la heri” akasema Rais
Armen na kukata simu
Mathew akairejesha simu
kisha akaelekea ndegeni na
kuondoka kuelekea Riyadh
Saudi Arabia.
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa saba za usiku Mathew
aliwasili jijini Riyadh.Nawal
alikuwepo uwanjani kumpokea
kisha wakaelekea moja kwa
moja nyumbani.Habiba Jawad
alikumbatiana kwa furaha na
Mathew huku machozi
yalimdondoka
“Mathew sikutegemea
kama ningeweza kukuona tena
mapema namna
hii.Nilitegemea misheni
ingechukua muda mrefu na
pengine tusingeweza kuonana
tena.Karibu nyumbani
Mathew” akasema Habiba
Baada ya mapokezi yale
hakukuwa na muda wa
kupumzika usiku ule ule
kukawa na kikao muhimu cha
kupanga kuhusiana na kile
wanachokwenda kukifanya
nchini Marekani.Waliweka
mikakatio mizito namna
misheni ile itakavyokwenda
kumalizika nchini
Marekani.Nawal akamkabidhi
Mathew rekodi za Jenerali
William na Sattar wakikiri
kuhusika katika kuratibu na
kuchochea vurugu nchini
Tanzania kwa maelekezo ya
G20.
“Mama Habiba sijui
nikushukuruje kwa mafanikio
haya makubwa tuliyoyapata”
akasema Mathew
“Tunayepaswa
kumshukuru ni Mungu wa
mbinguni kwa kutusimamia na
kutuongoza hadi hapa
tulipofika.Yote haya
yanafanikiwa kwa maongozi
yake.Mathew hakuna kupoteza
muda bado unayo safari
ndefu.Bado unazo saa kumi na
tatu kusafiri angani kwenda
kumaliza misheni yako.Tayari
nimekwisha mjulisha Mark
PIller kwamba misheni yako
Iran imekamilika na
anakusubiri kwa hamu
kubwa.Mathew hakikisha
hakuna anayebaki hai.Watu
wengi wamepoteza maisha
kwa sababu ya kikundi hiki
hivyo nao lazima waonje ladha
ya kifo ! akasema Habiba
“Mama Habiba kwa sasa
wakati tunaelekea mwisho wa
misheni yetu ni wakati wa
wewe kuondoka kwenda
mahala kuweka makazi.Rais
Armen Hijazi yuko tayari
kukupokea na ukaishi kule
kwa amani” akasema Mathew
“Mathew usihofu kuhusu
mimi nitakuwa salama.Nenda
kakamilishe misheni yako”
akasema Habiba halafu
akampatia Diski mweko
akamtaka aihifadhi inaweza
ikamsaida
“Humo ndani nimeweka
ushahidi wote wa kuhusiana
na mashirikiano yangu na
G20.Kuna video mbali mbali
ambazo nimekuwa
nikiwasiliana nao,kuna kila
kitu humo.Nina imani inaweza
kuwa na msaada mkubwa
kwako” akasema Habiba
Mathew akaagana na
Habiba akapanda gari
kuelekea uwanja wa ndege wa
bilionea Habiba Jawad
ambako ndege maalum ilikuwa
inamsubiri tayari kwa safari ya
kuelekea Marekani
“Safari njema
Mathew.Mimi pia niko nyuma
yako kwa saa moja.Tutakutana
Washington DC” akasema
Nawal wakaagana Mathew
akaingia ndegeni na kuondoka.
Baada ya kuhakikisha
Mathew ameondoka,Nawal
akarejea katika makazi ya
Habiba ambako alistushwa na
kukuta magari ya polisi
yakiwasha vimuli muli na vilio
vilisikika.Nawal akalazimika
kushuka garini akakimbia
kuelekea ndani kujua nini
kimetokea.Mapigo ya moyo
yalimuenda mbio.Katika
mlango wa kuingilia ndani ya
nyumba ya Habiba kulikuwa
na askari na hakuruhusiwa
mtu yeyote kuingia
ndani.Nawal akajitambulisha
kwamba yeye ni mmoja wa
wanafamilia lakini
hakuruhusiwa kuingia
ndani.Mara akamuona mmoja
wa wafanyakazi wa Habiba
aliyekuwa amekaa chini akilia
akamfuata
“Nasra nini kimetokea
hapa? Akauliza
“Mama Habiba amejiua
kwa kujipiga risasi” akasema
Nasra.Nawal akahisi nguvu
zinamuisha akaanguka
chini.Haraka haraka
akachukuliwa na kukimbizwa
katika gari la wagonjwa
lililokuwepo pale ndani kwa
ajili ya kupatiwa huduma
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 7
Nawal alirejewa na
fahamu na kuanza kuangua
kilio baada ya kusikia vilio vya
akina mama wengine
nje.Akiwa mle ndani akaingia
mtumishi wa muda mrefu wa
Habiba
“Nawal pole sana”
“Kwa nini mama Habiba
amefanya hivi? Akauliza Nawal
huku akilia.
“Nimeachana naye usiku
huu nikamsindikiza Abu
Zalawi uwanja wa ndege
kumbe tulikuwa tunaagana!
Akasema Nawal akiendelea
kumwaga machozi
“Inauma sana
Nawal.Muda mfupi kabla
hajajiua alikuja kunigongea
mlango wa chumbani kwangu
akanipa bahasha akaniambia
nikupatie ukirudi akaenda
chumbani kwake na mara
tukasikia mlio wa
risasi.Walinzi wakakimbilia
ndani na kuvunja mlango
wakakuta tayari
amekufa.Bahasha aliyonipa
nikupatie ni hii hapa” akasema
Yule mama na kumpatia
Nawal ile bahasha akaifungua
na kukutana na kipande cha
karatasi akakikunjua
akakisoma huku machozi
yakimdondoka
“Nawal najua
nimewaumiza sana lakini
nawaomba msiumie
wanangu.Haya ni maamuzi
magumu nimeyafanya
ambayo yataumiza wengi
lakini imenilazimu kufanya
hivi.Nimekuandikia namba za
kufungulia kasiki chumbani
kwangu utakuta
nimewaandalia nyaraka za
umiliki wa mali zangu zote
wewe na Mathew kwani ndio
wanangu pekee
waliobaki.Ninawapenda sana
mbaki salama”
Ndiyo ulivyosomeka ule
ujumbe wa Habiba. Nawal
alilia machozi mengi sana.
“Kwa nini mama Habiba
hakusubiri hadi misheni
ikamilike ndipo ajiue?Mbona
ameniweka katika wakati
mgumu sana? Natakiwa
kwenda Marekani kuungana
na Mathew je niondoke na
kuacha msiba? Akajiuliza
Nawal
“Kwa namna yoyote ile
lazima misheni ikamilike hivyo
nitakwenda Marekani.Habiba
atazikwa pale misheni yetu
itakapokuwa
imekamilika.Ametuchagua
mimi na Mathew kuwa warithi
wake hivyo basi tunao uwezo
wa kuzuia mazishi yasifanyike
hadi hapo
tutakaporejea.Natakiwa
kuanza kulishughulikia hili
mapema” akawaza Nawal na
kuinuka akawasiliana na Sayid
Omar mmoja wa watu wa
karibu sana na Habiba
akamtaka wakutane
wazungumze kuhusiana na
suala lile.Haikuwa vigumu kwa
Sayid Omar kukubaliana na
Nawal kwani alifahamu namna
Habiba alivyowapenda Nawal
na Mathew.Baada ya
makubaliano yale Nawal
akaondoka kuelekea uwanja
wa ndege akitumia ndege
binafsi ya Habiba akaondoka
kuelekea Marekani kuungana
na Mathew
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Saa tano kasoro kwa saa za
Marekani ,ndege aliyopanda
Mathew Mulumbi ilitua katika
uwanja wa ndege wa kampuni
moja kubwa ya kutengeneza
madawa ya mifugo kama
malekezo yalivyotolewa na
Mark Piler.Tayari walikwisha
andaliwa watu wa kumpokea
pale uwanjani haraka haraka
akaingizwa katika helkopta na
kuondoka.Alikuwa amevaa
kofia kubwa ya mzunguko na
kuyaficha macho yake kwa
miwani myeusi.Kidevuni
aliweka ndevu bandia hivyo
haikuwa rahisi kumtambua
kwa haraka.
“Naomba Mungu
kusitokee tatizo lolote
nikajulikana kabla ya kuonana
na Mark Piller” akawaza
Mathew
Helkopta ile ilikwenda
kutua katika jumba moja
kubwa Mathew akashushwa na
kuingizwa ndani.Kulikuwa na
walinzi wachache wakiwa
wamevalia suti zao nadhifu
pamoja na vifaa vya
mawasiliano masikioni
mwao.Moja kwa moja Mathew
akapelekwa katika chumba
kimoja kikubwa
“Utakaa humu hadi hapo
baadae yatakapotolewa
maelekezo mengine.Hakuna
kutoka ndani ya chumba hiki
na kama kuna kitu chochote
unakihitaji basi utabonyeza
hapa kisha atakukuja mtu
kukusikiliza” akasema Yule
mlinzi na kumuelekeza
Mathew sehemu ya kubonyeza
kama akihitaji kitu
chochote.Ndani ya chumba
kile kuliwekwa kila
kitu.Kulikuwa na friji kubwa
lililosheheni vinywaji na
vyakula vya kila aina,kulikuwa
na sehemu ya jiko dogo kama
angependa kupika,kwa ujumla
kila kitu muhimu
kilichohitajika
kilikuwemo.Mathew akaenda
katika friji akalifungua na
kuchukua kinywaji baridi
akanywa kisha akaenda
kujilaza kitandani.
“Naamini macho ya dunia
yataelekezwa Marekani siku ya
leo kwa kile kinachokwenda
kutokea.Naomba Mungu
anisaidie” akawaza Mathew
Kama walivyokuwa
wamepanga,saa mbili baada ya
Mathew kuwasili,ndege ya
Habiba Jawad iliyombeba
Nawal ilitua katika uwanja
mdogo wa ndege ulio pembeni
ya makazi ya bilionea mmoja
anayeishi nje kidogo ya jiji la
Washington DC.
Derrick Jones mmoja wa
marafiki wa karibu sana wa
Nawal aliyewahi kufanya naye
kazi katika shirika la ujasusi la
Marekani CIA alikuwepo
katika uwanja huo kumpokea
Nawal.Wakakumbatiana kwa
furaha kubwa
“Chloe ! akasema Derrick
wakiwa wamekumbatiana kwa
nguvu.Derrick alilifahamu jina
la Chloe.Hakulifahamu jina la
Nawal
“Derrick ! akasema Nawal
“Huu ni kama
muujiza.Sikujua kama
nitakuona tena.Karibu tena
nyumbani Chloe” akasema
Derrick
“Ahsante Derrick”
akasema Nawal kisha
wakaingia katika gari na
kuondoka
“Uliponiambia kwamba
unakuja sikuamini.Nilidhani
labda ni mtu anaigiza sauti
yako” akasema Derrick wakiwa
garini
“Ni mimi Derrick.Mambo
yanakwenda je hapa?
“Kila kitu kinakwenda
vizuri.Maisha yanakwenda
vizuri .Nini kilikutokea Chloe?
Sote tuliamini tayari
umekwisha poteza maisha
katika misheni uliyotumwa
mashariki ya kati” akasema
Derrick
“Derrick tuna mengi ya
kuzungumza lakini kuna
jambo la muhimu lililonileta
na ninahitaji sana msaada
wako”
“Jambo gani Chloe?
Akauliza Derrick
“Tutazungumza tukifika
nyumbani” akasema Nawal na
safari ikaendelea kimya kimya
“Chloe ungependa kwanza
kupita nyumbani kwako?
Akauliza
“Hapana.Nataka twende
nyumbani kwako.Kuna tatizo
lolote?
“Hakuna tatizo.Mimi bado
niko peke yangu.Sijapata bado
mwanamke ambaye ninaweza
kumpenda kama wewe Nawal”
akasema Derrick
“Acha mambo hayo
Derrick yamekwisha pita muda
mrefu sana” akasema Nawal
“Huwezi amini Chloe
kwamba pamoja na kwamba
umepita muda mrefu lakini
bado wewe ndiye mwanamke
wa pekee ambaye ninataka
kuwa naye katika maisha
yangu.Najua kwa wakati ule
ilikuwa vigumu……………..”
akasema Derrick Nawal
akamkatisha
“Derrick sitaki
tuzungumzie masuala
hayo.Nimekuja kwako
ninahitaji msaada unisaidie
hivyo sitaki hadithi zozote za
mapenzi” akasema Nawal
“Nimekuelewa
Chloe.Samahani” akasema
Derrick na safari ikaendelea
kimya kimya hadi walipofika
katika makazi ya Derrick
“Nyumba hii ni yako?
Akauliza Nawal
“Ndiyo ni nyumba yangu”
“Hongera.Maisha yako
yamebadilika sana siku hizi”
“Samahani sikuwa
nimekueleza kwamba
nimekwisha acha kazi CIA kwa
sasa ni mlinzi binafsi wa
bilionea ambaye ndege
iliyokuleta imetua katika
uwanja wake.Ninalipwa
mshahara mzuri na maisha
yanakwenda vizuri.Karibu
ndani Chloe” akasema Derrick
kisha wakaingia ndani.
“Jisikie nyumbani.Hapa ni
nyumbani kwako pia” akasema
Derrick
“Ahsante Derrick”
akasema Nawal na kwenda
katika friji akajihudumia
kinywaji.Derrick haraka
haraka akaenda jikoni kufanya
maandalizi ya chakula.Nawal
akiwa sofani alikuwa
anatazama kifaa mithili ya
simu ambacho kilikuwa na
ramani na sehemu katika hiyo
ramani ikiwaka taa ya kijani
hapo ndipo alipo Mathew
Mulumbi ambaye alikuwa
amevaa saa maalum
iliyounganishwa na kifaa kile
na kumuwezesha Nawal kujua
mahala alipo.
Derrick akaweka mezani
chakula wakala na baada ya
kula wakaenda sebuleni
“Chloe ni muda sasa wa
kunieleza kitu ulichokuja
kukifanya hapa DC” akasema
Derrick
“Derrick sote tumefanya
kazi CIA lakini kuna mambo
hatukuyafahamu.Kuna siri
kubwa ambayo ni watu
wachache tu wanaifahamu
hata rais wa nchi haijui”
“Kuna nini Chloe?
Akauliza Derrick kwa wasi
wasi kidogo
“Kuna idara ndogo ndani
ya CIA ambayo ni ya siri
kubwa inaitwa G20’
“G20?
“Ndiyo inaitwa hivyo kwa
kuwa ina watu ishirini ndani
yake na ndiyo maana
wakaamua kujiita G20.Idara
hii kazi yake kubwa ni
kushirikiana na makundi ya
kigaidi katika kufanikisha
mipango yenye maslahi ya
Marekani sehemu mbali mbali
duniani” akasema Nawal na
kumuelezea kwa kina Derrick
kile kinachofanywa na G20.
“Haya ni maajabu
Chloe.Ndani ya CIA kuna kitu
kama hicho? Akauliza Derrick
“Ndiyo maana
nikakwambia hiki ni kitu cha
siri sana na wamarekani
hawajui chochote
kinachoendelea”
“Dah ! akasema Derrick na
kutingisha kichwa kwa
masikitiko
Nawal akaendelea
kumueleza kuhusu kile
kilichofanywa nchini Tanzania
na G20 na Derrick akaonekana
kupandwa na hasira
“Kile tulichokishuhudia
kinatokea Tanzania ni
mipango ya nchi yetu?
Akauliza Derrick
“Ni mipango ya hiki
kikundi kidogo.Wamarekani
hawajui chochote” akasema
Nawal
“Hii haikubaliki hata
kidogo.Yaani kusababisha
machafuko na damu
kumwagika kwa sababu ya
kupata mafuta? Huu ni wizi na
hakuna mmarekani
atakayekubali kitu kama hiki”
Nawal akaendelea
kumueleza Derrick kuhusiana
na ule mpango wa kusambaza
kirusi nchini Tanzania mpango
ambao umeshindwa
kufanikiwa.Akayafungua
masanduku mawili yaliyokuwa
na kirusi ndani yake
akamuonyesha Derrick
akatetemeka.
“Endapo kirusi hiki
kingeweza kusambazwa nchini
Tanzania kuna uwezekano
mkubwa kingesambaa dunia
nzima kwani hakina kinga na
kingeweza kufika hata
Marekani na kutuangamiza sisi
wenyewe.Derrick nadhani
umeuona unyama unaofanywa
na hiki kikundi kidogo
kinachodai kinafanya haya
yote kwa maslahi ya Marekani”
akasema Nawal.Bado Derrick
alikuwa anatetemeka kwa
woga
“Derrick nimekuja
kukimaliza kikundi hiki”
akasema Nawal
“Chloe ni namna gani
utaweza kupambana na watu
hawa ambao wanaonekana
wana nguvu kubwa ya kufanya
chochote ndani na nje ya nchi?
Akauliza Derrick
Nawal akamueleza Derrick
namna mpango
ulivyoandaliwa.
“Nataka kujua Derrick
kama uko nami katika jambo
hili.Nahitaji sana msaada
wako” akasema Nawal
Bila kupepesa macho
Derrick akasema
“Nawal jibu
unalifahamu.Siwezi kukuacha
peke yako katika jambo kubwa
kama hili.Tutakuwa pamoja”
akasema Derrick kisha
wakaanza maandalizi
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 8
Saa mbili za usiku,Mathew
akachukuliwa na gari maalum
na kupelekwa katika nyumba
Fulani ambako alikaribishwa
sebuleni.Baada ya nusu saa
Mathew wakachukuliwa na
kupelekwa katika chumba
kimoja kilichokuwa na meza
na viti viwili.Kilionekana ni
maalum kwa ajili ya
mazungumzo.Zilipita tena
dakika tano mlango
ukafunguliwa na walinzi
wakaingia halafu akafuata
makamu wa Rais Mark Piller
ambaye aliwataka walinzi wake
wawape nafasi ya
kuzungumza.Baada ya walinzi
kutoka,Mathew na Mark
wakatazama kwa muda halafu
Mark akasema
“Abu Zalawi karibu tena
Marekani.Nimefurahi kukuona
tena ukiwa mzima”akasma
Mark Piller
“Ahsante”akajibu Mathew
“Pole pia kwa yote
uliyokumbana nayo hadi
kufika Iran.Najua ni mambo
mengi tuyaweke pembeni na
tujielekeze katika kile kitu cha
msingi ambacho ni misheni
yako nchini Iran” akasema
Mark Piller na Mathew
akavuta pumzi ndefu
“Nilielezwa kila kitu na
Habiba kuhusiana na mipango
ya kuniua.Nakushukuru kwa
kumjulisha Habiba mipango
ya G20 na kuokoa maisha
yangu.Kama si wewe
ningekwisha uawa kwani wale
jamaa walikuwa wamejipanga
vyema”akasema Mathew na
Mark akatabasamu
“Ni kweli Abu kulikuwa na
mipango ya kukuua baada ya
kugundua kwamba wewe si
gaidi bali ni jasusi.Sikutaka
uuawe wakati umekwisha fika
nusu ya misheni yako hivyo
nikawasaliti wenzangu ili
wewe uwe hai na umalizie
misheni yako” akasema Mark
Piller
“Nashukuru sana”
akasema Mathew
“Abu Zalawi kitu
nilichokifanya ni kitu kibaya
sana na endapo nikijulikana
nitauawa hivyo basi mara tu
utakaponikabidhi taarifa ya
kile ulichokipata nchini Iran
utaondoka kimya kimya hapa
Marekani na kwenda sehemu
yoyote unakotaka ukaanze
maisha mapya.Nitakupatia
kiasi kikubwa cha fedha kwa
ajili ya kukuwezesha kuishi
maisha mapya sehemu ya
mbali kabisa” akasema Mark
Piller.Mathew akafungua
mkoba wake akatoa diski
mweko akampatia Mark
ambaye aliinuka akafungua
mlango na kumtaka mmoja wa
walinzi wake akamletee
kompyuta yake
garini.Kompyuta ilipoletwa
akaweka ile diski akakuta kuna
picha na video mbali mbali
“Hiki nini? akauliza
“Hicho ni kinu cha nyuklia
ambacho nilipewa maelekezo
ya kukilipua lakini sikuona
sababu ya kukilipua.Video hizo
ni kile ambacho kinaendelea
ndani ya kinu hicho unaweza
kushuhudia wewe mwenyewe”
akasema Mathew
“Video hizi umezitoa wapi?
“Nimezichukua mimi
mwenyewe.Nimeingia katika
kinu hicho na kupita kila
sehemu nikachukua hizo video
ili kuwathibitishia kwamba
madai ya Iran kutengeneza
silaha za nyuklia katika kinu
hicho si ya kweli” akasema
Mathew na Mark Piller
akabadili sura.
Mathew hakumjali akatoa
diski mweko nyingine
akampatia Mark Piller
“Utapitia taratibu na kwa
nafasi video hizo.Naomba
uitazame na hii pia” akasema
Mathew na Mark akaichomeka
ile diski nyingine
“Hiyo ina taarifa zote za
kuhusiana na silaha za Iran”
akasema Mathew na Mark
akapitia haraka haraka.
“Umewezaje kuzipata hizi
taarifa? Akauliza Mark huku
sauti yake ikionekana kuwa na
kitetemeshi
“Mlinituma kazi na
nimeifanya kazi mliyonituma
kama mnavyotaka” akasema
Mathew halafu akatoa diski
nyingine na kuinuka akaenda
katika kompyuta ya makamu
wa Rais akaichomoa ile diski
na kuiweka nyingine na mara
akaonekana mtu mmoja
aliyevimba uso wake
“Naitwa Jenerali William
kutoka jeshi la Marekani
ambaye ni mkuu wa vikosi vya
Marekani vilivyoko nchini
Tanzania”
Mark Piller akatetemeka
na kugeuka akamtazama
Mathew
“Kitu gani hiki? Akauliza
Mark
“Endelea kutazama”
akasema Mathew na Mark
akaendelea kuitazama ile video
ambayo Jenerali William
alieleza kila kitu
alichoelekezwa kukifanya
kuanzia kuratibu na kuchochea
vurugu hadi mpango wa
kusambaza kirusi.Mark Piller
midomo ilimtetemeka alitaka
kusema kitu akashindwa
Mathew akatoa diski ile na
kuweka nyingine ambayo
ilimuonyesha Assad Ismail
akikiri kuhusika katika
kuchochea vurugu nchini
Tanzania kwa maelekezo ya
G20.Alieleza kila kitu
“Mark Pil…..” akasema
Mathew lakini kwa haraka
Mark akaunyoosha mkono
wake akataka kubonyeza kitufe
kidogo kilichokuwa chini ya
meza ambacho kingewapa
ishara walinzi wake ili waingie
mle ndani mara moja lakini
Mathew alikwisha kiona
kitendo hicho akamtandika
ngumi nzito Mark akaanguka
chini pamoja na kiti
alichokuwa amekalia.
“Hakuna chochote
unachoweza kukifanya kwa
sasa Mark Piller.Uongozi
ninao mimi na utafuata kile
nitakachokueleza.Nyanyuka!
akasema Mathew na Mark
Piller akanyanyuka akatoa
kitambaa na kujifuta damu
zilizotoka mdomoni
“Abu Zalawi
unajidanganya
kjana,hautaweza kutoka
salama ndani ya nyumba
hii.Huu ni mwisho wako !
akasema Mark kwa hasira
“Sikiliza Mark Piller.Wewe
ni makamu wa Rais wa
Marekani na una uwezo wa
kutoa maelekezo nikauawa
lakini kabla hujafanya hivyo
naomba unisikilize” akasema
Mathew na kutazamana na
Mark aliyefura kwa hasira
“Siko peke yangu
ninayeifahamu siri hii.Nina
wenzangu wako hapa
Marekani ambao kama
hawatapata taarifa zozote
kutoka kwangu kwa muda
tuliopanga watajua nimeuawa
hivyo wataanika mambo yote
mnayoyafanya wewe na
wenzako kwa wamarekani na
dunia nzima ili wafahamu
uovu wenu mashetani
wakubwa nyie.Kama hiyo
haitoshi kirusi ambacho
mlitaka kukisambaza nchini
Tanzania tayari kiko hapa
Marekani na ikitokea
nimeuawa basi kitasambazwa
hapa Marekani” akasema
Mathew.Mark Piller aliyekuwa
anahema haraka haraka
akasema
“Nini unakitaka Abu
Zalawi?
“Nataka umpigie simu
David Walker awakusanye
G20 wote mkutane mahala
ambako huwa mnakutana kila
siku !
“Hilo haliwezekani.Mimi
ni makamu wa Rais wa
Marekani na siwezi usiku huu
kwenda sehemu kama hizo
hatarishi !
“Kama umeweza kufika
hapa basi unaweza kwenda
sehemu yoyote muda wowote”
akasema Mathew
“Abu Zalawi hapa ni
nyumbani kwangu .Nini
unakitaka? Tafadhali Abu
Zalawi usilifanye jabo hili liwe
gumu kwa upande
wako.Achana na hiyo mipango
yako,mimi ninakupa fursa ya
kuyaanza maisha mapya
sehemu yoyote duniani na
tutakuwezesha kwa kila
kitu.Tafadhali sana” akasema
Mark Piller
“Mark chukua simu mpigie
David Walker haraka sana
nataka G20 wote wakusanyike
ndani ya dakika ishirini kutoka
sasa”
“Abu Zalawi unajiweka
katika matatizo makubwa
sana.Naomba kubali fursa
niliyokupa uondoke usiku huu
na ukayaanze maisha
yako.Nimekuandalia
masanduku sita yaliyojaa
fedha ili ukayaanze maisha
mapya.Nakuomba kijana
usiiache fursa hii ikakupita”
akasema Mark Piller
“Mark unapiga simu
hupigi? Akauliza Mathew
“Utanifanya nini nikisema
hapana?Utaniua? akauliza
Mark
“Nina saa hii mkononi na
endapo nikibonyeza kitufe hiki
hapa nitawapa ishara
wenzangu ambao watatekeleza
yale niliyokwambia
tutayafanya.Huu si utani
MarkPller.Una sekunde tano
za kufanya maamuzi” akasema
Mathew akiwa ameishika saa
yake akahesabu sekunde tano.
“Subiri! Akasema Mark
Piller
“Nini unataka kukifanya
Abu Zalawi? Akauliza Mark
Piller
“Fanya kile
nilichokuelekeza Mark!
Akafoka Mathew na Mark
Piller akapiga simu kwa David
Walker akamtaka awakusanye
watu wote wa G20 katika ofisi
yao ya siri.
“Wakati tukiwasubiri
wenzako wakusanyike endelea
kutazama video hii” akasema
Mathew na kumuwekea Mark
Piller video ya Habiba Jawad
akijieleza na kuzungumzia
mambo mbali mbali ambayo
amekuwa akiyafanya kwa
kushirikiana na G20.Ilikuwa ni
video ndefu na kabla
hajaimaliza kuitazama
akapigiwa simu na David
Walker ambaye alimjulisha
kwamba tayari wamekwisha
kusanyika wanamsubiri.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 9
Mathew akiwa na makamu
wa Rais Mark Piller waliwasili
katika nyumba ambayo G20
huitumia kama ofisi yao na
mara nyingi hukutana
hapo.Ndani ya nyumba hiyo
kulikuwa na ukumbi mzuri wa
mikutano ambao huutumia
kwa vikao vyao.
Baada ya kushuka garini
Mark akapokewa na David
Walker ambaye hakuweza
kumtambua Mathew kwa
namna alivyokuwa
amejibadilisha.Mark
alionekana kuwa na haraka
sana wakaongozana kuelekea
ndani na David akamzuia
Mathew kuingia ndani ya ule
ukumbi akidhani ni mmoja
kati ya walinzi wa makamu wa
Rais lakini Mark Piller
akamtaka amruhusu aingie
ndani
“Hapana Mar…………”
kabla David hajamaliza
sentensi yake akajikuta
amepigwa teke akaangukia
ndani.Walinzi wa makamu wa
Rais wakataka kumdhibiti
Mathew lakini Mark Piller
akawataka wasifanye hivyo na
Mathew akaingia ndani ya ule
ukumbi na kufunga
mlango.Bado David Walker
alikuwa amelala
chini.Wenzake wakamuinua na
kumkalisha kitini huku
akigugumia kwa maumivu
makali ya mbavu.Mathew
akabonyeza moja ya kitufe
katika simu yake ambacho
kiliwapa ishara akina Nawal
kwamba pale alipo ndipo
mahala ambapo kila kitu
kitafanyika.Nawal na Derrick
wakiwa na kundi la watu
ishirini waliowakodisha kwa
ajili ya kazi ile hawakuwa
mbali kwani walikuwa
wanamfuatilia Mathew kupitia
kile kifaa alichokuwa nacho
Nawal.
“Tusikilizane
tafadhali.Nataka kila mmoja
achukue nafasi yake ! akasema
Mathew na sauti ile ikawastua
wale watu mle ndani hasa
David Walker ambaye licha ya
maumivu makali lakini
akainua kichwa kumtazama
mtu Yule.Mathew akavua kofia
na miwani halafu akavua zile
ndevu bandia na taharuki
iliyotokea ndani ya ukumbi ule
haielezeki.
“Ni mimi Abu Zalawi
naomba msistuke ! akasema
Mathew.Bado watu
hawakuamini kama
walichokuwa wanakiona mbele
yao ni kitu cha kweli.
“Nafahamu
hamkutegemea kuniona tena
hapa lakini atakayeweza
kuiondoa roho yangu katika hii
dunia ni Mungu pekee”
akasema Mathew
“Tayari mmekwisha
nifahamu lakini rasmi
nitajitambulisha kwenu kuwa
jina langu halisi ni Mathew
Mulumbi na si Abu Zalawi na
kikubwa zaidi ni kwamba mimi
si gaidi bali ni
jasusi.Mlinituma nchini Iran
lakini nikiwa kule mlituma
watu kuniua na mpango huo
haukufanikiwa.Mnajua kwa
nini? Ni kwa sababu
mwenzenu Mark Piller
aliwasaliti !
“Abu Zalawi ! akasema
Mark kwa ukali
“Tulia Mark Piller !
akasema Mathew
“Mathew na Rais walitaka
misheni iendelee na
wakanisaidia hadi nilipomaliza
misheni yangu na leo niko
hapa mbele yenu kuhitimisha
uovu wenu.Kulipa damu ya
watanzania na wale wa sehemu
nyingine duniani ambao
wamepoteza maisha yao kwa
sababu ya mipango yenu kwa
kushirkiana na makundi ya
kigaidi.Leo ni mwisho wenu”
akasema Mathew akainuka
Donald Cooper na
kumnyooshea Mathew bastola
“Kama ulishindwa kuuawa
nchini Iran kwa sababu ya
usaliti wa huyu shetani Mark
basi umejileta wewe
mwenyewe katika mdomo wa
kifo ! akasema Donald na
Mathew akacheka kidogo
“Weka silaha yako chini
Donald.Najua ninyi nyote mna
bastola na mnaweza kuniua
lakini hebu nipeni dakika kumi
tu nizungumze nanyi” akasema
Mathew
“Donald kaa chini
tafadhali ! akasema Mark
Piller
“Mark ni wewe
uliyesababisha haya yote.Kwa
nini ukatusaliti wenzako ?
Akauliza kwa hasira Donald
Mark akawa kimya.Mathew
akachukua diski mweko na
kuichomeka katika kompyuta
iliyounganishwa na projekta
na katika runinga kubwa mtu
mmoja akaonekana .Baada ya
mtu yule kujitambulisha kuwa
ni jenerali William wote
wakabaki midomo
wazi.Waliitazama video ile
hadi ilipomalizika kisha
akawawekea video ya Assad
Ismail na wakati wakiendelea
kuitazama saa yake ikatoa mlio
mnara tatu akaitazama
“Mmefanya mambo mengi
maovu sehemu mbali mbali
duniani.Mmemwaga damu
nyingi…..” akanyamza Mathew
baada ya milio ya risasi
kusikika nje ya mlango wa kile
chumba kisha mlango
ukapigwa teke ukafunguka
akaingia Nawal akiwa na
bunduki inayofuka moshi.
“Mathew tumalize mambo
haraka haraka imesikika
milioya risasi kutoka kwa
walinzi wa makamu wa Rais
hivyo askari wanaweza
wakafika hapa muda wowote !
Nawal akamwambia
Mathew.Mara Mathew na
Nawal wakarukiwa na Derrick
akawaangusha chini na
ukasikika mlio wa risasi
kutoka katika bastora ya
Donald akitaka kumuua
Mathew.Derrick akageuka
haraka na kummiminia risasi
Donald akaanguka na kufariki
pale pale.
“Ahsante Derrick”
akasema Nawal
Haraka haraka wakaingia
vijana wawili wakiwa na
kamera wakaiungansha na
kompyuta halafu wakawapa
ishara akina Mathew kwamba
kila kitu kiko tayari.Mathew
akajitokeza mbele ya Kamera
na matangazo ya moja kwa
moja yakaanza
“Habari zenu
Marekani.Sura hii si ngeni
kwenu.Ninatafutwa kwa
tuhuma za kulipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam
Tanzania.Mnanifahamu kwa
jina la Abu Zalawi lakini hilo si
jina langu halisi.JIna langu
halisi ni Mathew Mulumbi na
ninatokea Tanzania.
Ndugu wamarekani
ninazungumza nanyi nikiwa
hapa Washington DC
Marekani na lengo la kuja
mbele yenu usiku huu ni
kuwaeleza ukweli ambao
hamuufahamu” akasema
Mathew na kugeuka.
“Ndani ya chumba hiki
kuna watu wapatao ishirini
wakiongozwa na makamu wa
rais wa Marekani Mark
Piller.Hawa wote ni
wafanyakazi wa shirika la
ujasusi la Marekani.Ndani ya
CIA kuna idara ndogo ya siri
yenye watu ishirini
inayojulikana kama G20
ambayo majukumu yake ni
kushirikiana na magaidi katika
kufanikisha mipango mbali
mbali yenye maslahi kwa
Marekani” akasema Mathew
Taarifa za kuwepo kwa
video ile ya moja kwa moja ya
gaidi Abu Zalawi akizungumza
ilisambaa kwa haraka sana na
watu wengi wakasimamisha
shughuli zao kuitazama.Vituo
mbali vya runinga na redio
vilikatisha matangazo yao na
kuanza kurusha video
ile.Runinga kubwa zilizokuwa
katika majengo makubwa zote
ziliunganishwa na matangazo
yale na watu waliokuwa
mabararani wakafuatilia kile
kilichokuwa kinaendelea.
Rais William Washington
akiwa amepumzika katika
makazi yake ikulu alitaarifiwa
kuhusu uwepo wa video ile
akataka kuitazama lakini
tayari sehemu kubwa
imekwisha mpita
“Tukio la kulipuliwa kwa
ubalozi wa Marekani ni tukio
la kupangwa na wamarekani
wenyewe kupitia watu hawa
waliomo humu ndani ukiwa ni
mpango wa kuniwezesha
kuingia nchini Iran” akasema
Mathew na kueleza kila kitu
kuhusiana na mipango ile ya
kumpeleka Iran.
Rais Wiliam akampigia
simu mkuu wa FBI na
kumuuliza kuhusu hatua
walizozichukua kufuatia
matangazo yale ya moja kwa
moja ya gaidi Abu Zalawi
“Tayari tumekwisha
fahamu mahala matangazo
hayo yanakotokea na hivi sasa
vikosi vinaelekea huko.Tayari
helkopta zimekwisha izingira
nyumba hiyo na kuzuia jaribio
lolote la magaidi hao
kutoroka.Vikosi vitakapowasili
vitafanya kila linalowezekana
kuweza kumuokoa makamu
wa rais na watu wengine
walioshikiliwa mateka na huyu
gaidi Abu Zalawi ! akasema
mkuu wa FBI
“Izingireni nyumba hiyo
lakini kusifanyike jaribio lolote
la kutaka kuivamia nyumba
hiyo hadi pale Abu Zalawi
atakapomaliza kutoa maelezo
yake ! Jambo lingine kwa
namna yoyote ile Abu Zalawi
hapaswi kuuawa.Tumieni
mbinu za kumpata akiwa
mzima”akaelekeza Rais
William
“Wamarekani wana haki
ya kuufahamu ukweli wa kile
kinachoendelea katika nchi
yao.Imekuwa vyema
amejitokea huyu Abu Zalawi
na kuweka wazi kila kitu.Ni
uovu mkubwa umefanyika
kupitia kundi hili” akawaza
Rais William Washington
Video ile ya Mathew
haikusambaa tu Marekani bali
pia vituo vingine vikubwa vya
habari navyo vilirusha video
hiyo na sehemu mbali mbali
duniani wakafuatilia
mubashara kile kilichokuwa
kinaendelea kule Marekani
Taarifa za kuwepo kwa
video hiyo zilimfikia Rais wa
Tanzania ambaye kwa haraka
akatafuta chaneli iliyokuwa
inarusha video ile halafu
akampigia Ruby na kumtaka
aitafute chaneli ile
aitazame.Taarifa zilisambaa
kwa haraka .
Wakati kijua kikichomoza
nchini Tanzania watu walikuta
matngazo yale yakiendelea na
kwa kuwa taarifa zilisambaa
kwa kasi kubwa watu wengi
waliweza kuifuatilia japo
walikuwa wamepitwa na
mambo mengi aliyoyazugumza
Mathew.
Mathew aliendelea kutoa
maelezo yake akaletewa
sanduku moja lenye kirusi
akalifungua na kutoa chupa
nyembamba yenye urefu
mithili ya bomba la sindano
“Humu ndani kuna kirusi
ambacho kilitakiwa
kikasambazwe nchini
Tanzania.Kirusi hiki
kimetengenezwa hapa
Marekani kwa lengo la kwenda
kuwaangamiza watanzania ili
watakapoanza kuumwa na
kufa kama ndege wamarekani
watume watu wao kwa lengo la
kwenda kutoa msaada lakini
nyuma ya pazia ajenda yao
kubwa ni kuchota madini ya
Tanzania” akaendelea kueleza
Mathew hadi alipomaliza
maelezo yake
“Baada ya maelezo yangu
marefu nataka mpate
ushuhuda mwingine wa maovu
ya watu hawa” akasema
Mathew na kuweka diski
mweko katika kompyuta na
kupitia projekta watu
wakaanza kumshuhudia
Jenerali William akikiri kila
kitu alichokifanya nchini
Tanzania.Baada ya maelezo ya
Jenerali William Mathew
akaweka tena video ya Assad
Ismail akikiri kuhusika katika
kuchochea vurugu na mauaji
nchini Tanzania.
“Ndugu wamarekani
naamini kwa maelezo haya
marefu tayari mmefahamu kile
kinachoendelea katika nchi
yenu.Hii ni siri kubwa ambayo
msingeweza kuifahamu na leo
nimeamua kuweka wazi kila
kitu.Kwa mambo
waliyoyafanya hawa jamaa
walistahili kumalizwa hapa
hapa lakini mimi na wenzangu
wote si makatili kama wao
hivyo nitaviachia vyombo
husika vitafanya kazi
yake.Lengo langu lilikuwa ni
kuwaeleza ukweli.Sasa
ninajisalimisha kwa vyombo
vya dola.Ahsanteni na usiku
mwema” akasema Mathew na
kamera ikazimwa
Kwa takribani saa
tatu,Marekani ilisimama
kufuatia Mathew kuviteka
vyombo vyote vya habari kwa
video yake ile ya moja kwa
moja.
“Mathew unataka kufanya
nini? Mbona mipango yetu
haikuwa kuwaacha hai hawa
watu? Tulipanga tuwamalize
kwani wamekwisha fanya uovu
mkubwa.Adhabu yao ni
kuuawa ! akasema Nawal kwa
ukali
“Hapana Nawal.Tukiwaua
hawa tutakuwa sawa na
wao.Sisi si wauaji Nawal.Kitu
kikubwa ni kwamba
wamarekani wameufahamu
ukweli”
“Mathew ! akasema Nawal
“Nawal tumemaliza kazi
tujisalimishe kwa vyombo vya
dola” akasema Mathew
“Mathew tumezungukwa
na vyombo vya dola.Hatuwezi
kutoka humu ndani
salama.Tunajulikana kuwa
tumemteka makamu wa Rais !
akasema Nawal
“Nawal narudia tena kazi
imekwisha ! akasema Mathew
kwa ukali
Nawal akampa maelekezo
Derrick ya kuwataka watu
wake wote waweke silaha chini
na wasalimu amri.
Wakati Mathew akijianda
kujisalimisha,Rais William
akampigia simu mkuu wa FBI
akamueleza kwamba anahitaji
kuonana na Mathew Mulumbi
usiku ule.Vile vile akaelekeza
watu wote wa G20 wakamatwe
usiku ule ule akiwamo
makamu wa Rais Mark Piller.
Mathew akafungua geti na
kutoka nje akanyoosha mikono
juu akasalimu amri na
wenzake pia wakafanya hivyo
wakafungwa pingu na
kuingizwa katika
magari.Mathew akachukuliwa
katika gari maalum na
kupelekwa ikulu kama rais
Wiliam alivyoelekeza
“Abu Zalawi karibu sana
ikulu.Nimelazimika kutoa
maelekezo uletwe hapa baada
ya kufuatilia maelezo yako
uliyoyatoa usiku huu” akasema
Rais William baada ya Mathew
kufika ikulu
“Kwanza nakupongeza
kwa ujasiri wako na
kupambana hadi hapa
ulipofka.Hili si jambo jepesi
najua umepitia mengi
magumu”
“Ndiyo mheshimiwa Rais
haikuwa rahisi” akasema
Mathew ukapita ukimya halafu
Rais akasema
“Sikuwa nikifahamu
kuhusu hiki kikundi cha G20
hadi hivi karibuni ambapo
Mark Piller aliamua kunieleza
kuhusu uwepo wake.Ah ! …”
akasema Rais William kwa
masikitiko.
“Mathew sijui hata
ninataka kusema nini lakini
kuna jambo moja tu ambalo
nataka ulifahamu ni kwamba
yote uliyoeleza ni ya kweli
kabisa.Ni mambo mengi
maovu yamefanywa na kikundi
hiki na tayari nimeelekeza
wote wakamatwe.Usiku huu
wa leo ndio mwisho wa hiki
kitu kinachoitwa G20.Ahsante
sana Abu Zalawi kwa kuuanika
ukweli huu kwa wamarekani ili
hatua stahiki zichukuliwe kwa
wahusika.Abu Zalawi
nimeishiwa maneno ya
kusema lakini kuna mambo
mawili ya muhimu” akasema
Rais William na kuvuta pumzi
ndefu
“Kwanza ninataka
kukuhakikishia kwamba
hautafunguliwa shtaka lolote
hapa Marekani kwani
haujahusika katika jambo
lolote.Kila kitu kimefanywa na
wamarekani wenyewe na hata
bomu lile lililolipua ubalozi
wetu limetoka
Marekani.Tumelipua ubalozi
wetu sisi wenywe.Hii ni aibu
kubwa.Abu Zalawi uwe na
kosa au huna kosa mimi
ninakuachia uende
zako.Nitatoa ndege ya
kukupelekea sehemu yoyote
unayotaka kwenda”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais lakini
huwezi ukaniachia mimi peke
yangu.Kuna wengine
niliokuwa nao ambao
wanashikiliwa hivi sasa”
“Usijali wote wataachiwa
huru” akasema Rais William
“Jambo la pili ambalo
wewe ni mtu wa kwanza
kukwambia ni kwamba kesho
nitalihutubia taifa na
nitatangaza kuachia
ngazi.Nitajiuzulu nafasi yangu
kwani na mimi nimeshiriki
katika uovu huu mkubwa
uliofanyika.Kila mtu anastahili
adhabu kwa nafasi yake.Mara
tu baada ya kujiuzulu nafasi
yangu nitajikabidhi kwa
vyombo vya husika kwa ajili ya
hatua stahiki kuanza
kuchukuliwa.Ninaomba
uondoke Marekani wakati
bado nikiwa rais kwani baada
ya mimi kuondoka na kuja
utawala mpya unaweza
ukapata ugumu wa kuondoka
hapa kwani umegusa maslahi
ya watu wengi.Suala hili
litabeba watu wengi sana”
akasema Rais William
“Mwisho kabisa
ninakushauri endelea na moyo
huo huo wa kizalendo kwa
nchi yako.Umeonyesha mfano
kwa vijana wa nchi za kiafrika
kwa kupigania nchi
yako.Mungu akipenda
yawezekana siku moja
tukaonana tena” akasema Rais
Wiliam.
Mathew alilengwa na
machozi ya furaha kwa
maneno yale ya Rais William
akamshukuru na kumpatia zile
rekodi zote alizokuwa nazo
halafu Rais akapiga simu
akaelekeza wale watu
waliokamatwa pamoja na
Mathew waachiwe
huru.Mathew akapewa gari
maalum na walinzi akaenda
kukutana na akina Nawal
wakakumbatiana kwa furaha
kubwa wakapongezana.
“Nawal hatuna muda
mrefu wa kuwepo
hapa.Tumekwisha imaliza kazi
yetu na Rais ametoa muda wa
sisi kuondoka haraka
iwezekanavyo.Ametoa ndege
kwa ajili ya kutusafirisha
kwenda sehemu yoyote
tuitakayo” akasema Mathew
“Mathew hatuhitaji ndege
kwani ndege niliyokuja nayo
bado iko hapa hapa Marekani
tutaitumia hiyo kuondoka
nayo” akasema Nawal
wakaingia katika magari na
kuelekea katika uwanja wa
ndege ilikokuwa ndege ya
Habiba.Waliagana na Derrick
wakamshukuru kwa msaada
wake mkubwa halafu
wakaingia ndegeni na baada ya
muda ndege ikapaa.
Baada ya ndege kukaa
sawa,Mathew na Nawal
wakapongezana
“Mathew tumefanya jambo
kubwa tunastahili furaha
lakini kuna jambo lilitokea
ambalo ni la huzuni kubwa”
“Jambo gani?
“Mama Habiba amefariki
dunia” akasema
Nawal.Ilimchukua Mathew
zaidi ya dakika tano kutamka
neno
“Nawal tafadhali naomba
unieleze ukweli”
“Si utani Mathew.Mama
Habiba amefariki dunia”
akasema Nawal na kumueleza
Mathew kila kitu
kilichotokea.Mathew
akadondosha machozi
“Mama Habiba alistahili
kushuhudia namna
tulivyolimaliza kundi la
G20.Naamini aliogopa fedheha
baada ya ukweli kujulikana
ndiyo maana alirekodi maelezo
yale mapema akijua ana
mpango wa kujiua” akasema
Mathew
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 6 : EPISODE 10
Haijulikani ni muda gani
watu walipeana taarifa kwani
kulipopambazuka tu watu
walianza kumiminika katika
ikulu ya Marekani na ilipofika
saa mbili za asubuhi maelfu ya
watu tayari walikwisha
kusanyika nje ya ikulu hiyo na
wengi wakiwa na mabango ya
kulaani kile ambacho nchi yao
imekuwa ikikifanya kupitia
kikundi cha G20.Waliwataka
viongozi wao wakuu
wawajibike
Ndani ya ikulu kulikuwa
na heka heka kubwa.Toka
usiku baada ya video ile ya
Mathew Mulumbi kulikuwa na
vikao mfululizo.
Saa tatu za asubuhi Rais
wa Marekani William
Washington akajitokeza mbele
ya waandishi wa habari
waliokuwa wamekusanyika
katika bustani ya
ikulu.Yalikuwa ni matangazo
ya moja kwa moja kutoka ikulu
na watu wengi walisubiri
kusikia kauli ya Rais kufuatia
kile kilichokuwa kimesemwa
na Mathew Mulumbi.
“Habari za asubuhi ndugu
wamarekani” akaanza hotuba
yake
“Toka usiku wa jana
Marekani haijalala kufuatia
maelezo ya kina aliyoyatoa
Abu Zalawi ambaye tayari
wengi tulikuwa tunamfahamu
kama gaidi aliyelipua ubalozi
wetu nchini Tanzania
Toka alipotoa maelezo
yake,kumekuwa na mjadala
mkubwa sana watu wakijaribu
kuchambua kile kilichoelezwa
na Abu Zalawi na wengine
wakidiriki kutaka kukanusha
au kupindisha ukweli wa kile
alichokisema.Nimesimama
mbele yenu asubuhi hii
kuweka sawa jambo hili” Rais
William akanyamaza kidogo
akawatazama waandishi wa
habari halafu akasema
“Yote aliyoeleza Abu
Zalawi jana ni ukweli
mtupu.Narudia tena kwamba
yote aliyoeleza Abu Zalawi jana
usiku ni kweli hakuna hata
neno moja la uongo
alilolitamka hivyo kusifanyike
juhudi zozote za kutaka
kupindisha ukweli ili
kuwasaidia watu waliohusika
katika uhalifu huu mkubwa.
Ni kweli ndani ya CIA
kumekuwa na kitengo cha siri
chenye jina G20 ambacho kazi
yake kubwa ni kujenga
mashirikiano na makundi
mbalimbali ya kigaidi.Kikundi
hiki kinaendeshwa kwa siri
kubwa na wanaofahamu
uwepo wake ni watu ishirini tu
ndiyo maana wakajiita G20.Hii
imekuwa ni siri kubwa na hata
rais hatakiwi kufahamu uwepo
wa kikundi hiki.
Sina hakika kama marais
wa Marekani waliopita
wanafahamu kitu kama hiki
lakini mimi nilipata bahati hivi
karibuni ya kuwafahamu
uwepo wa kikundi hicho ila
sikuweza kufanya chochote
kwa kuhofia kuuawa.Nilikuwa
mwoga” akanyamaza tena
kidogo
Nilifahamu uwepo wa
kundi hili wakati wakijiandaa
na mpango wa kuchochea
machafuko nchini Tanzania na
katika eneo zima la Afrika
Mashariki.Nilifahamishwa
mpango huo na mimi
nikaushiriki” akanyamaza
akameza mate na kwa mbali
alilengwa na machozi
“Watu wengi wameuawa
Afrika Mashariki hasa nchini
Uganda na Tanzania kufuatia
machafuko ya kidini
yaliyotokea ambayo na mimi
pia nimeyashiriki kwa lengo la
kupata mafuta kutoka nchini
Uganda.Nyote mlishuhudia
damu nyingi iliyomwagika
nchini Tanzania na Uganda
lakini wakati mauaji haya
yakifanyika na damu
ikimwagika sisi tuliendelea
kufurahia neema ya mafuta
.Meli zetu zilikuwa zimepanga
foleni katika bandari ya Tanga
nchini Tanzania zikipakia tani
na tani za mafuta.Huu ni
ukatili mkubwa sana.
Kama haitoshi bado
kulifanyika mpango wa
kwenda kusambaza kirusi
nchini Tanzania na mimi pia
nilishiriki katika mpango huo
lengo kuu likiwa ni kuendelea
kuchota rasilimali mbali mbali
zilizoko nchini humo na hasa
madini.Sitaki kurudia yale
aliyoyasema Abu Zalawi lakini
nataka nifafanue na nyote
msikie kutoka katika kinywa
changu kwamba yote yale yana
ukweli.
Pamoja na hayo yote bado
tulimtuma Abu Zalawi nchini
Iran na katika mpango huo
tukalipua ubalozi wetu jijini
Dar es salaam.Abu Zalawi
hahusiki chochote katika
shambulio lile yeye alitumika
kuingiza gari lenye bomu
katika ubalozi wetu.Gari
lililobeba bomu ni gari la
kwetu na hata bomu lililolipua
ubalozi wetu ni letu hivyo
tumeua watu wetu sisi
wenyewe.
Ndugu zangu wamarekani
kwa hayo niliyoyaeleza na
mengine mengi ambayo
sijayaeleza ninasimama mbele
yenu kukiri kwamba sisi
viongozi wenu
tumewaangusha.Tumetenda
makosa makubwa sana.Jana
usiku nilielekeza G20 wote
wakiongozwa na makamu wa
Rais Mark Piller wakamatwe
na mashitaka dhidi yao yaanze
mara moja kwani ushahidi wa
kutosha wa matendo yao upo.
Pamoja na hatua hiyo ya
kuwakamata viongozi wote wa
G20 lakini zipo pia hatua
nyingine ambazo
nimezichukua katika suala
hili.Kwanza kuna viongozi na
watu kadhaa kutoka Afrika
Mashariki ambao
walishirikiana na G20 katika
kuchochea vurugu ambao
wamekuja kupatiwa hifadhi
nchini Marekani.Mmoja wao
ni aliyewahi kuwa Rais wa
Uganda Jenerali Akiki
Rwamirama aliyepinduliwa na
kukimbilia hapa
Marekani.Huyu amekuwa ni
mmoja wa watu walioasisi kwa
kiasi kikubwa mpango huu wa
kuchochea vurugu na kupata
mafuta.Mbinu zote za
machafuko yale yeye ndiye
aliyebuni.Wapo vile vile
viongozi wengine wa dini na
siasa kutoka nchi za Tanzania
na Uganda walioshiriki katika
machafuko yale kisha
wakakimbilia hapa Marekani
na kupewa hifadhi wao na
familia zao baada ya
machafuko kuwa
makubwa.Hawa wote
watakamatwa na kurejeshwa
makwao kujibu mashitaka
watakayofunguliwa na nchi
zao kwa kushiriki kuchochea
vurugu zile.Ni aibu kwa
viongozi kutoka bara la Afrika
kuwa tayari kuwasaliti watu
wao,kusaliti nchi zao na
kuungana na mataifa
makubwa katika kuchota
rasilimali na wao kufaidika
kidogo.Nakiri kumekuwa na
wizi mkubwa wa rasilimali
mbali mbali katika bara la
Afrika unaofanywa na mataifa
makubwa wakishirikiana na
waafrika wenyewe hasa
viongozi na hivyo kulifanya
bara la Afrika kuendelea kuwa
masikini.Nawasihi waafrika
wawe na uzalendo na
kuzipenda nchi zao na
kuzipigania kama alivyofanya
Abu Zalawi
Jambo la pili,baada ya
kukubali kwamba tumefanya
uhalifu itatulazimu kulipa fidia
kwa nchi zilizoathiriwa.Mafuta
yote tuliyochukua kutoka
Uganda tutayalipa pamoja
tathmini ya fidia
zitakazowasilishwa kwetu
kutoka kwa nchi husika.
Mwisho kabisa kwa kuwa
na mimi ni sehemu ya uhalifu
huu ninapaswa kuwajibika
hivyo ninatangaza kwamba
kuanzia sasa nimejiuzulu
nafasi yangu ya urais ili sheria
iweze kuchukua mkondo
wake.Siwezi kubaki bila
kuwajibika hasa kwa haya
madhambi makubwa ambayo
tumeyafanya.
Mungu ibariki Marekani.
Rais William Washington
akamaliza hotuba yake na
kurejea ndani huku nje ya
ikulu watu wakiendelea
kuongezeka.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Nchini Tanzania bado
gumzo kubwa lilikuwa ni
maelezo ya Mathew Mulumbi
na hotuba aliyoitoa Rais
William Washington
akikubaliana na kile
alichokisema Mathew.Kuanzia
asubuhi ya siku ile kulikuwa na
kamata kamata kubwa.Majina
yote ya watu ambao walishiriki
katika kuchochea vurugu za
kidini zilizopelekea mamia ya
watu kupoteza maisha ambayo
yalitajwa na Assad Ismail
yalikabidhiwa kwa jeshi la
polisi na msako mkubwa
ukafanyika kuwawakamata
wote.
Hotuba ya Rais William
akiwataja baadhi ya watu
kutoka Afrika Mashariki hasa
Jenerali Akiki Rwamirama
aliyewahi kuwa Rais wa
Uganda iliwastua watu wengi
wa Afrika
mashariki.Hawakutegemea
kabisa kama Jenerali Akiki
angeweza kuhusika katika
machafuko yale
Saa mbili za usiku kwa saa
za Afrika Mashariki Rais wa
Tanzania Dr Fabian kelelo
akalihutubia taifa.Katika
hotuba yake akawatangazia
watanzania kwamba hakuna
tena vurugu zitakazotokea
kwani wachochezi wote wa
vurugu zile wamekamatwa na
wengine kuuawa.Aliwasisitiza
watanzania kuendelea kuishi
kwa upendo kama
walivyokuwa wakiishi kabla ya
kuchonganishwa ili
wachukiane.Aliwataka kwa
namna yoyote ile wasikubali
kuchonganishwa tena na mtu
yeyote na kupelekea kupigana
wao kwa wao.Ilikuwa ni
hotuba ndefu iliyobeba mambo
mengi na kubwa likiwa ni
amani upendo na kuvumiliana
hata pale kunapokuwa na
tofauti za kiimani.Mwisho
kabisa aliwaahidi watanzania
kuzilinda rasilimali za nchi
kwa gharama zozote zile na
kuwataka watanzania wote kila
mmoja awe mlinzi wa rasili
mali hizo kwa faida yao na
vizazi vijavyo.Kabla hajamaliza
hotuba yake Dr Fabian
akawamwagia sifa tele Mathew
na wenzake ambao
walipambana usiku na mchana
kuhakikisha kwamba
wanaufahamu ukweli.
Baada ya kumaliza hotuba
yake,simu zikaanza kuingia
mfululizo katika simu ya rais
lakini hakutaka kupokea simu
hata moja kwa wakati ule
lakini alipoiona simu ya Ruby
akaipokea.
“Hallo Ruby” akasema
DrFabian
“Mheshimiwa Rais
nimekupigia kukupongeza kwa
hotuba nzuri uliyoitoa”
akasema Ruby
“Ahante sana
Ruby.Utanisamehe sikuweza
kuwataja kwa majina lakini
nimewashukuru nyote kwa
ujumla wenu kwa kazi kubwa
mliyoifanya”
“Usijali mheshimiwa Rais”
“Vipi kuhusu Mathew
Mulumbi umewasiliana naye?
“Ndiyo nimekuwa
nawasiliana naye mara kwa
mara leo yuko Riyadh Saudi
Arabia.Habiba Jawad
amefariki dunia”
“Habiba amefariki dunia?
“Ndiyo amefarki dunia
amejiua kwa kujipiga risasi”
“Lini atarejea nyumbani?
Akauliza DrFabian
“Bado hajaweka wazi lini
atarejea nyumbani lakini
akiwa tayari atatujulisha”
akajibu Ruby
“Sawa Ruby.Lazima
tumpokee kwa shangwe shujaa
wetu kwani amefanya mambo
makubwa sana” akasema Dr
Fabian na ukimya ukapita
“Ruby kama ukipata nafasi
usiku wa leo tunaweza
kuonana? Akauliza Dr
Fabian.Ruby akafikiri kidogo
na kusema
“Hakuna tatizo nitakuja”
akajibu Ruby ambaye alijawa
na furaha kubwa siku hii
“Kwa sasa baada ya
mambo yote kumalizika ni
wakati wa kumueleza Ruby
ukweli.Ninampenda na
ninataka awe mke wangu.Ana
kila sifa ya kuwa
mke.Yawezekana nikiwa naye
ninaweza kufikiria hata
kuwania kipindi cha pili cha
urais” akawaza Dr Fabian
huku akitabasamu
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa tatu za usiku Mathew
na Nawal waliwasili Riyadh
wakitokea nchini
Marekani.Sayid Omar
alikuwepo uwanjani
kuwapokea ksha wakaelekea
nyumbani.Watu walikuwa
wengi na majonzi yalitawala
.Baada ya Mathew na Nawal
kuwasili nyumbani kwa
Habiba vilio vikaanza
upya.Nawal alilia mno.Mathew
akaenda kuungana na watu
waliokuja kuwafariji na wengi
wakimpongeza kwa kile
alichokifanya.Tayari alikuwa
ni mtu maarufu kufuatia kile
alichokifanya nchini Marekani
ambacho kilitazamwa na
karibu dunia nzima
Ilipofika saa saba za usiku
Mathew akaenda kupumzika
katika nyumba yake kujiandaa
na siku ya kesho ambapo
Habiba angezikwa.
“Imekuwa ni kama filamu
ambayo imefika
mwisho.Nimepitia mengi sana
katika sakata hili toka
lilipoanza.Nafikiri nahitaji
kuyatafakari tena maisha
yangu.Ngoja kwanza tumzike
mama Habiba halafu nitajua
nini kitafuata” akawaza
Mathew na kulala
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliwasili ikulu saa
nne za usiku kama
alivyoombwa na Rais Dr
Fabian ambaye usiku huu
alichangamka sana.
“Ruby karibu” akasema Dr
Fabian na kumkaribisha katika
sebule yake
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu
Ruby huku akitabasamu
“Ruby kabla ya yote nataka
kwanza tufungue shampeni
kusherehekea ushindi mkubwa
tulioupata” akasema Dr Fabian
na kufungua shampeni
wakagonganisha glasi
Baada ya maongezi kidogo
Dr Fabian akasema
“Ruby hii imekuwa ni vita
ngumu lakini tumeipigana
tumeimaliza ahsante kwako na
wenzako.Kwa sasa baada ya
vita hii kumalizika maisha
lazima yaendelee.Nimekuita
hapa usiku huu sitaki
tuzungumze kuhusu kazi
kwani kila tunapokutana
imekuwa ni mazungumzo ya
kazi.Nataka usiku huu
tuzungumze kuhusu
maisha.Tusizame katika kazi
na kusahau kwamba kuna
muda na sisi tunahitaji kuwa
na maisha ya kawaida kama
wengine” akasema Dr Fabian
“Ni kweli mheshimiwa
Rais” akajibu Ruby
“Nini mipango yako hasa
baada ya jambo hili kubwa
kumalizika?
“Mheshimiwa Rais hiki
kilichotokea kimenifundisha
mambo mengi .Nimeingia
katika kazi hii ya kuongoza
idara nyeti kama SNSA bila
kuwa na ujuzi mkubwa wa
masuala ya ujasusi.Mimi ni
mtaalamu wa kompyuta na
kinachonisaidia ni uzoefu
mdogo nilionao baada ya kuwa
karibu na Mathew Mulumbi na
nikashiriki naye katika
misheni mbali mbali.Kwa hiyo
mheshimiwa Rais nimeamua
kwenda kusomea masuala ya
ujasusi ili niive kabisa”
akasema Ruby
“Ruby una uhakika
unataka kwenda kusomea
masuala ya ujasusi?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ninataka kusomea
ujasusi” akajibu Ruby
“Ruby naomba niwe
muwazi kwako.Binafsi sitaki
uendelee na kazi hii ya
ujasusi.Nimeshuhudia ni kazi
iliyojaa hatari sana na kwa
mtoto mzuri kama wewe
haikufai.Ninataka kukutafutia
nafasi nzuri zaidi kuliko hiyo”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais ulinitoa
Uingereza nije niifanye kazi hii
hivyo nataka nikasome ili
niifanye kwa ufanisi”
“Hapana Ruby sitaki
uende ukasomee masuala
haya” akasema Dr Fabian
“Kwa nini mheshimiwa
rais”
“Ruby sisi ni watu wazima
hivyo sitaki kuzunguka
zunguka kama wafanyavyo
vijana.Naomba niwe mkweli
kwako.Ninakupenda sana
Ruby na lengo langu ni mimi
nawe tuwe na mahusiano na
ikiwezekana tuishi pamoja”
akasema Dr Fabian na Ruby
hakustuka akatabasamu
“Mheshimiwa Rais
ninashukuru kwa kunieleza
ukweli.Hili ni jambo ambalo
siwezi kulitolea majibu ya
haraka.Naomba unipe muda
mheshimiwa Rais nitafakari
halafu nitakujibu” akasema
Ruby
“Ruby naomba ujipe muda
kisha utanijibu na
nitakubaliana na jibu lolote
utakalonipatia lakini narudia
tena Ruby kwamba
ninakupenda na ninakuhitaji
mno katika maisha
yangu.Baada ya kumpoteza
Millen ni wewe ambaye Mungu
amekuleta karibu yangu”
akasema Dr Fabian
“Nimekwisha kuelewa
mheshimiwa Rais usihofu”
akasema Ruby
Walizungumza mambo
mengi kuhusiana na maisha
yao kisha wakaagana Ruby
akaondoka
RIYADH – SAUDI ARABIA
Mazishi ya Habiba Jawad
yalilifanya jiji la Riyadh
lizizime.Umati mkubwa mno
ulijitokeza kumsindikiza
Habiba Jawad katika safari
yake ya mwisho.
Saa nne za usiku baada ya
watu kuondoka Mathew na
Nawal waliingia ndani ya
chumba cha Habiba
Jawad,Nawal akafungua kasiki
la Habiba ambako walikuta
nyaraka ambazo Habiba
aliziandaa zinazoonyesha
kwamba utajiri wake wote
amewaachia Mathew na
Nawal.
“Mathew tumeachiwa
utajiri mkubwa sana na
Habiba.Nini mawazo yako?
Akauliza Nawal
“Nawal kitu kimoja tu
ninachoweza kusema ni
kwamba utajiri huu wote
ninaukabidhi kwako”
“Hapana Mathew.Mama
Habiba ametukabidhi sote
utajiri huu wote”
“Nakubali lakini na mimi
ninakukabidhi wewe utajiri
huu”
“Kwa nini Mathew?
“Ninahitaji
kupotea.Nahitaji kwenda
mahala mbali kabisa ambako
nitapata muda wa kutafakari
kuhusu maisha yangu na
kusahau yale yote
niliyoyapitia.Nimepitia
mambo mengi sana Nawal”
“Vipi kuhusu Ruby?
“Ninampenda Ruby lakini
sina hakika kama mimi ni
mwanaume sahihi
kwake.Maisha yangu
yamekuwa namna hii na siwezi
kumpatia furaha ya maisha
anayoihitaji.Yawezekana haya
ndiyo maisha niliyopangiwa na
Mungu.Utazungumza naye na
kumwambia kwamba
ninampenda lakini aendelee
na maisha yake na asinisubiri”
akasema Mathew wakaendelea
na mazungumzo yao.
BAADA YA MWAKA MMOJA
Watuhumiwa wote wa
vurugu zilizopelekea
umwagikaji mkubwa wa damu
Afrika Mashariki walikwisha
hukumiwa kuanzia miaka
thelathini hadi kifungo cha
maisha gerezani.Amani
ilitamalaki tena watu
wakiendelea kuishi kama
ndugu.
Baada ya kujiuzulu Rais
William Washington,Marekani
ilipata Rais mpya ambaye
alifanya mazungumzo na Rais
wa Iran na baada ya muda
mrefu muafaka kati ya mataifa
haya mawili ukapatikana na
nchi ya Iran ikaondolewa
vikwazo vya kiuchumi
ilivyowekewa.
Baada ya kukosa ufadhili
wa fedha,makundi mbali mbali
ya kigaidi yalidhoofika na
mengine kufa kabisa.
Idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi SNSA ilipata
mkurugenzi mpya baada ya
Ruby na Gosu Gosu kuacha
kazi.Gosu Gosu aliendelea
kusimamia biashara za
Mathew
Tukio kubwa kabisa
lililotokea baada ya mwaka
mmoja ni ndoa ya Dr Fabian
Kelelo na Ruby.Ilikuwa ni
sherehe kubwa iliyolitikisa jiji
la Dar es salaam.Ruby aliamua
kufunga ndoa na Dr Fabian
baada ya kuhakikishiwa na
Nawal kwamba Mathew
amempa ruhusu ya kuendelea
na maisha yake.
Watu wengi walijiuliza
mahala alipo shujaa Mathew
Mulumbi na wengi wakijiuliza
kwa nini hakurejea nyumbani
ili wampongeze baada ya
jambo kubwa alilolifanya miezi
kumi na mbili
iliyopita.Mathew alifanya siri
kubwa mahali alipo.Hakutaka
kujulikana alikwenda wapi
kwani alihitaji mapumziko
marefu na kujitafakari kuhusu
maisha yake.
TAMATI

NDUGU
MSOMAJI,AHSANTE
KWA KUIFUATILIA
SIMULIZI HII NDEFU YA
SIRI.TUNA UHAKIKA
UTAENDELEA
KUTUUNGA MKONO
KWA KUFUATILIA
SIMULIZI ZETU
NYINGINE
ZITAKAZOFUATA
BAADA YA KUMSOMA
MATHEW MULUMBI
KATIKA SIMULIZI
KADHAA JE
UMEMFAHAMU VIZURI
MATHEW NI MTU WA
NAMNA GANI?
KUMFAHAMU VYEMA
MATHEW NI MTU WA
NAMNA GANI USIKOSE
SIMULIZI INAYOFUATA
YA
SCANDAL(KASHFA)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom