Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 13
Helkopta ya SNSA ilitua
katika sehemu yake ikitokea
katika operesheni maalum ya
makomando waliovamia
nyumba ya magaidi wa
IS.Mlango wa helkopta
ukafunguliwa akashuka
komando mmoja kisha
akamshusha Marwan
Hossam.Gosu Gosu akasogea
na kumchukua Marwan
akaelekea ndani na helkopta
ile ikaondoka kwenda
kuwachukua watu
wengine.Gosu Gosu
akamchukua Marwan na
kumpeleka katika chumba
maalum cha mahojiano
kilichopo mita kadhaa chini ya
jengo lile akamfungia katika
chumba chenye baridi kali
kisha akamfuata Ruby
aliyekuwa katika ofisi yake
“Ruby tayari tumempata
Marwan hakuna haja ya
kuendelea kusubiri .Tukaanze
kumuhoji mara moja ili
ikiwezekana usiku huu huu
tumpate pia Assad kwani hana
taarifa kama wenzake
wamevamiwa.Tukichelewa
hadi kesho atagundua
kilichotokea na atajificha
itakuwa kazi ngumu kwetu
kumpata” akasema Gosu Gosu
kisha Ruby akaelekeza
Marwan atolewe katika
chumba kile cha baridi
apelekwe katika chumba cha
mahojiano halafu wakashuka
chini
“Nina muda mrefu
sijawahoji watu kama
hawa,ana bahati mbaya sna
Marwan ameingia katika anga
zangu.Leo atanena lugha zote
anazozifahamu” akawaza Gosu
Gosu wakiwa ndani ya lifti
wakishuka chini.
MPENZI MSOMAJI
MATHEW AMELIPUA
UBALOZI WA MAREKANI
NCHINI TANZANIA IKIWA
NI MWANZO WA MISHENI
NZITO YA KUELEKEA
IRAN,JE MISHENI YAKE
ITAFANIKIWA?
GOSU GOSU NA RUBY
WAMEANZA KUUSAKA
MTANDAO WA CHANZO
CHA VURUGU TANZANIA JE
WATAFANIKIWA
KUWAPATA WOTE
WANAOHUSIKA?
NAWAL ATAFANIKIWA
MISHENI YAKE YA KUZUIA
KIRUSI KISISAMBAE
TANZANIA?
USIKOSE SEHEMU IJAYO..
Sawa.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 1
“Gosu Gosu na Ruby
waliingia katika chumba
maalum cha mahojiano
ambacho ndani yake kulikuwa
na meza mbili,viti vitano na
baadhi ya vifaa vingine vya
kuwezesha mahojiano
kufanyika.Baada ya dakika
chache mlango ukafunguliwa
Marwan akaingizwa ndani ya
kile chumba.Aliwekwa katika
kiti na kufungwa
pingu.Alikuwa anatetemeka
mwili kwani alitolewa katika
chumba chenye baridi
kali.Gosu Gosu akamtazama
kwa hasira
“Relax.Take a deep breath
! akasema Gosu Gosu lakini
Marwan alimtazama Gosu
Gosu kwa jicho la chuki.
“Hata ukinitazama kwa
hasira tutaelewana tu !
akasema Gosu Gosu
“Jina lako nani?akauliza
Gosu Gosu.Marwan
akamtazama na huku
akitetemeka akasema
“la ‘astatie al’iijabat lak
alkalaba ! akajibu Marwan kwa
lugha ya kiarabu akimaanisha
kwamba hawezi kuwajibu
mbwa.Ruby na Gosu Gosu
wakatazamana
“Ninapokuuiza swali
nataka ujibu aidha kwa
Kiswahili au kiingereza
.Umenisikia? ! akauliza Gosu
Gosu huku akimtazama
Marwan kwa macho yake
makali yaliyoonyesha ukatili
mkubwa
“Nataka utuambie jina
lako nani? Akauliza tena Gosu
Gosu
“turid miny ‘an ajyb?
Aismaahu li ‘an ‘atahadath
‘iilaa sahib alkilab ty ! akasema
Marwan akimaanisha
“Mnataka niwajibu?Nataka
nizungumze na mwenye mbwa
!
Gosu Gosu akageuka na
kumtazama Ruby
“Ruby huyu jamaa
anaonekana ana kiburi sana
nami ninawapenda watu
wenye viburi kama
huyu.Naomba dakika tatu
nimuonyeshe hapa yuko
sehemu gani” akasema Gosu
Gosu
“Go ahead ! akasema Ruby
na Gosu Gosu akainuka
akaenda katika kabati
akalifungua na kuchukua kopo
dogo la gesi akaliwasha na
kumsogelea Marwan.
“madha tuhawil ‘an tfel?
Akauliza Marwan akimaanisha
“Nini unataka kukifanya?
“Sifahamu lugha hiyo
unayoizungumza lakini
tutaelewana tu.Muda si mrefu
tutazungumza lugha moja !
akasema Gosu Gosu na
kumtandika Marwan kofi zito
lililomfanya aweweseke .Kabla
hajakaa sawa akakigandamiza
kichwa chake juu ya meza
halafu akaanza kulichoma
sikio la Marwan
“Aaaagghhh !! Marwan
akapiga ukelele mkubwa .
“Gosu Gosu stop !
akasema Ruby na Gosu Gosu
akazima ile gesi.Kwa hasira
Marwan akagongesha paji lake
la uso katika ile meza na damu
ikaanza kumtoka sehemu ya
juu ya jicho iliyokuwa
imechanika.Gosu Gosu
akamnasa kofi halafu
akamuinua kichwa
“Nataka uzungumze aidha
Kiswahili au kiingereza.Ukileta
kiburi nitakukata masikio
yako.Umenisikia? akauliza
Gosu Gosu halafu
akamsindikiza na kofi zito
“Hawa si watu wa kucheka
nao Ruby.Ni watu makatili
sana wasio na ubinadamu hata
kidogo hivyo ukitaka kupata
taarifa kutoka kwao nawe
lazima ujitoe ubinadamu uwe
kama wao” Gosu Gosu
akamwambia Ruby
Marwan bado aliendelea
kugugumia kwa maumivu yale
makali ya kuchomwa sikio la
upande wa kulia.
“Tunaanza upya.Nataka
utuambie jina lako
nani?akauliza Gosu
Gosu.Marwan hakujibu kitu
aliendelea kutoa mguno wa
maumivu
“Nakuuliza kwa mara
nyingine jina lako
nani?akauliza Gosu Gosu
akiwa amekasirika.Marwan
hakujibu kitu.Kwa hasira Gosu
Gosu akasimama na kuwasha
lile kopo la gesi.
“Mimi sipendi kuchezewa
na watu kama ninyi ! akasema
na kuanza kumuendea
Marwan
“Hapana ! Hapana !
Usinichome t….” akasema
Marwan na Gosu Gosu
akasimama
“Kumbe unafahamu
Kiswahili ng’ombe wewe !
akasema Gosu Gosu na
kumtandika Marwan kofi
halafu akarejea kukaa
“Naomba unitazame
machoni” akasema Gosu Gosu
lakini Marwan alikuwa
ameinamisha kichwa.Gosu
Gosu akaipiga meza kwa
nguvu
“Inua kichwa nitazame
usoni ! akasema kwa ukali na
Marwan akamtazama
“Mimi ni mkatili sana na
ukinifanyia mchezo
nitakufanyia ukatili ambao
hujawahi kuushuhudia katika
maisha yako.Nataka unieleze
ukweli wa kila nitakacho
kuuliza.Umenielewa? akauliza
Gosu Gosu na Marwan
akaitika kwa kutikisa kichwa
“Nataka utufahamishe jina
lako tafadhali ! akasema Gosu
Gosu
“Marwan” akajibu
“Marwani nani?akauliza
Gosu Gosu
“Marwan Hossam !
“Marwan wewe ni
mtanzania?
“Hapana ninatokea
Mombasa Kenya” akajibu
“Hapa Tanzania umekuja
kufanya nini?akauliza Gosu
Gosu,Marwan akabaki kimya
“Nakuuliza hapa Tanzania
umekuja kufanya nini?
Ukimya wa Marwan
ukazidi kumchafua Gosu
Gosu.Akainuka na kwenda
kufungua kabati la vifaa
akachukua nyundo akarejea
mezani akamnasa kofi Marwan
halafu kwa nguvu akaweka
kiganja cha mkono juu ya
meza akainua nyundo na
kuishusha katika vidole
Marwan akapiga ukelele kwa
maumivu makali aliyoyapata.
“Nimekwambia sitaki
mchezo.Jibu kwa ufasaha kila
ninachokuuliza ! akasema
Gosu Gosu huku Marwan
akirusha rusha kiganja cha
mkono kwa maumivu
“Mhh ! Kwa pigo hili la
Gosu Gosu vidole vya huyu
jamaa viko salama kweli? Ruby
akajiuliza
“Nini umekuja kukifanya
hapa Tanzania? Akauliza Gosu
Gosu
“Nilikuja kuwatembelea
ndugu zangu machafuko
yalipotokea nikajikuta
nimekwama hapa hapa”
akasema Marwan
“Mahala tulipoachukua
wewe na wenzako kuna
nyumba moja na majengo
mawili yenye muundo wa
bohari.Mnajishughulisha na
nini mahala pale? Akauliza
Gosu Gosu
“Hakuna kitu
tunachokifanya zaidi ya
makazi” akajibu Marwan
“Mko wangapi jumla
yenu?akauliza Gosu Gosu
“Juma tuko….” Marwan
akasita
“Nataka ujibu ama sivyo
nitaendelea kukuharibu
kiungo kimoja kimoja !
akasema Gosu Gosu
“Tuko kumi na sita jumla
yetu”
“Una uhakika
kinachofanyika pale ni makazi
na hakuna kitu kingine?
Akauliza Gosu Gosu
“Tuko wengi ndiyo maana
wengine wanaishi katika zile
nyumba mbili za kuhifadhi
mizigo” akasema Marwan
Gosu Gosu akafunua faili
lililokuwa mezani akachukua
picha moja na kuiweka mbele
ya Marwan
“Unamfahamu huyu mtu
pichani? akauliza Gous Gosu
Marwan akaitazama ile
picha na kusema
“Hapana simfahamu”
“Una uhakika humfahamu
huyu mtu?akauliza Gosu Gosu
“Ndiyo simfahamu”
akasema Marwan
Gosu Gosu akachukua tena
picha ya Mathew
akamuonyesha
“Huyu naye unamfahamu
?akauliza Gosu Gosu.Marwan
akaitazama ile picha ya
Mathew na kusema
“Hapana simfahamu huyu
mtu”
“Una uhakika hujawahi
kumuona huyu mtu? Akauliza
Gosu Gosu
“Sijawahi kumuona huyu
mtu na simfahamu” akajibu
Marwan.Gosu Gosu
akaendelea kumtazama kwa
hasira
“Marwan nakuuliza kwa
mara nyingine tena hawa watu
niliokuonyesha picha zao
unawafahamu? Akauliza Gosu
Gosu
“Siwafahamu” akajibu
Marwan.
“Mara ya
mwisho.Unawafahamu hawa
watu?
‘Hapana siwafahamu”
akajibu Marwan.
“Ruby huyu mtu ana
kiburi.Nataka nimpeleke
chumba cha pili.Hatuwezi
kuendelea kumbembeleza
wakati anafahamu kila kitu”
akasema
Gosu Gosu
“Endelea Gosu Gosu.Fanya
kila kinachowezekana hadi
afunguke ! akasema Ruby.
Gosu Gosu akamfungua
Marwan pingu alizokuwa
amefungwa akamkunja suruali
na kumtoa ndani ya kile
chumba akampeleka katika
chumba kingine maarufu kama
chumba cha pili akaufungua
mlango na kumuingiza
Marwan.Hiki kilikuwa ni
chumba cha kutesea.Ndani ya
chumba hiki kulikuwa na meza
kadhaa na mitambo mbali
mbali maalum kwa ajili ya
kutesea.Kwa nguvu Gosu Gosu
akamuinua Marwan na
kumrushia juu ya meza halafu
akamfunga mikono na miguu
kwa mikanda maalum
iliyokuwa pembeni ya meza
ile.Ruby alikuwa pembeni
kimya akishuhudia kile
alichokuwa anakifanya Gosu
Gosu
“Marwan
nilikutahadharisha awali
kwamba mimi ni mtu mbaya
sana hasa ninapokutana na
watu wenye viburi na wakaidi
kama wewe.Nimekuonyesha
picha mbili nikakuuliza kama
unawafahamu watu wale
pichani ukakana
kuwafahamu.Umeniudhi sana”
akasema Gosu Gosu na
kulichukua lile faili lenye picha
kutoka kwa Ruby,akaichuka
picha ya Mathew akamuoyesha
Marwan
“Huyu anaitwa Abu Zalawi
ametokea Saudi Arabia.Nataka
uniambie amekuja kufanya
nini hapa Tanzania? Kwa nini
akafikia mahala mnapoishi?
Akauliza Gosu Gosu
` “Simfahamu na hajawahi
kuishi pale tunapoishi”
“Marwan nitakuharibu
naomba unieleze ukweli.Abu
Zalawi amekuja kufanya nini
hapa Tanzania?
“Simfahamu huyu mtu na
sijawahi kumuona” akasema
Marwa.Mara simu ya Ruby
ikaita akatazama mpigaji na
kumtaka Gosu Gosu
aendelee,yeye akatoka nje ya
kile chumba kwa ajili ya
kuipokea ile simu
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby
“Ruby ninakuhitaji hapa
ikulu haraka sana.Unaweza
kuja mara moja?
“Mheshimiwa Rais usiku
huu tuko katika operesheni
muhimu sana hivyo sintaweza
kufika ila nitajitahidi kesho
nifike”
“Kuna nini kinaendelea
hapo SNSA?akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo tunalifuatilia na
tutakapokuwa tayari
nitakueleza”
“C’mon Ruby I need to
know now ! Sina muda wa
kusubiri.Niambie tafadhali
nini kinachoendelea?
“Mheshimiwa Rais
ninaomba unipe muda kidogo
niweze kulishughulikia suala
hili na nitakapokuja kwako
niwe na taarifa zenye uhakika
mkubwa.Naomba nisikupe
taarifa nusu nusu” akasema
Ruby
“Sawa Ruby nataka mpaka
kesho jioni uwe na kitu cha
kunieleza.Umenielewa?”
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais”
“Umekwishapata taarifa
kwamba ubalozi wa Marekani
hapa Tanzania umelipuliwa?
“Ubalozi wa Marekani
umelipuliwa?! Ruby
akashangaa
“Ndiyo.Tukio hilo
limetokea usiku huu” akasema
Dr Fabian na Ruby akabaki
kimya
“Ruby ! akaita Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
nimestushwa sana na taarifa
hizi. Kuna taarifa zozote
zinazoonyesha nani
wanahusika katika shambulio
hilo? Ruby akauliza
“Bado hakuna taarifa
yoyote iliyotolewa hadi sasa
kwani juhudi za uokozi
zinaendelea.Tukio hili linazidi
kufanya hali ya amani kuwa
tete.Ninaziona kila dalili za
vurugu kuhama kutoka katika
machafuko ya kidini na
kuhamia katika ugaidi.Hiki
kilichotokea usiku huu katika
ubal;ozi wa Marekani naamini
ni tukio la kigaidi na
halihusiani na vurugu za kidini
zilizotokea ila uchunguzi
unaendelea na
watakapokamilisha
watatujulisha” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais kuna
kila dalili kwamba magaidi
wameanza kujipenyeza na
kutumia hali hii inayoendelea
hapa nchini kwa sasa kufanya
mambo yao ya kigaidi kama
tukio hilo la kulipua ubalozi wa
Marekani.Mimi na idara yangu
bado tunaendelea kutafura
mzizi wa vurugu
zilizotokea.Napenda nikupe
uhakika mheshimiwa Rais
kwamba tunaelekea pazuri na
nitakapokuja kukuona kesho
nitakuwa na taarifa kutosha
kuhusu mahala tulipofikia hadi
sasa kujua chanzo cha vurugu”
akasema Ruby
“Nimekuelewa
Ruby.Naomba muendelee na
uchunguzi wenu ii tulifahamu
kwa undani zaidi suala hili”
akasema Dr Fabian
“Tutafanya hivyo
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby na kukata simu
“Duh ! nani kalipua
ubalozi wa Marekani?
Akajiuliza Ruby
“Tutajua hapo baadae kwa
sasa ngoja tuendelee na zoezi
letu la kuwahoji hawa
magaidi” akawaza Ruby na
kupiga hatua kurejea katika
chumba ambacho alimuacha
Marwan akiendelea kuhojiwa
na Gosu Gosu.Mlinzi
akamfungulia mlango akaingia
ndani.Alipatwa na mstuko
mkubwa kwa kile
alichokishuhudia mle
ndani.Sakafu ilitapakaa
damu.Marwan Hossam
hakuwa akitazamika.Uso wake
wote ulikuwa umechafuka
damu.Alikuwa anakoroma
sauti yake haikuweza kutoka
tena kwa maumvu
aliyoyapata.Mezani kulikuwa
na sikio limekatwa huku Gosu
Gosu akiwa na kisu kikali
akijiandaa kukata sikio lingine
“Gosu Gosu ! akasema
Ruby
“What have you done?!
Akauliza Ruby na
kumnyang’anya Gosu Gosu
kile kisu.
“Ruby hawa si watu wa
kuonea huruma.Hawa magaidi
ni wanyama kabisa na wagumu
mno kufunguka ! akasema
Gosu Gosu aliyekuwa
amechafuka damu
“Gosu Gosu
hapana.Hatupaswi kufanya
hivi.Watu hawa wanazo taarifa
muhimu sana na tunatakiwa
kuwahoji na kuhakikisha
wanafunguka na kutueleza kile
wanachokifahamu.Tazama
ulivyomfanya huyu jamaa.Hiki
unachotaka kukifanya si
utesaji bali ni uuaji.Amepoteza
damu nyingi sana huyu jamaa
na anaweza akapoteza maisha
na huyu ndiye
tunayemtegemea aweze
kutupa taarifa za mahala alipo
Assad ! akasema Ruby
akionekana kutokufurahia kile
alichokifanya Gosu
Gosu.Haraka haraka akapiga
simu kitengo cha afya wakafika
haraka na kumchukua Marwan
wakamkimbiza katika zahanati
yao kwa matibabu
“Gosu Gosu umekosea
sana ! Huyu jamaa ni mtu
muhimu ambaye
tunamtegemea atuelekeze
mahala alipo Assad.Kwa hiki
ulichokifanya itatuchukua
muda kufahamu mahala alipo
Assad ! akasema Ruby
“Ruby watu hawa ni
wakatili,hawaogopi kufa na
ndiyo maana wanaweza
kubeba mabomu na
kujilipua.Hawa si watu wa
kuwahoji huku
ukiwachekea.Unapowahoji
watu kama hawa inakulazimu
kujitoa ubinadamu na kuwa
mkatili kama wao ! akasema
Gosu Gosu halafu wakatazama
kwa sekunde kadhaa
“Ruby nakushauri usiwepo
katika chumba hiki wakati
ninawahoji hawa jamaa kwani
mimi siogopi kumchomoa mtu
moyo wake na kuuweka
mezani nikaukata kata kwa
kisu.Lazima tutumie nguvu
vinginevyo hatutapata taarifa
zozote kutoka kwa hawa
jamaa” akasema Gosu Gosu
huku akinawa mikono kisha
wakatoka ndani ya kile
chumba.
“Rais alinipigia
simu.Amenipa taarifa kwamba
ubalozi wa Marekani
umelipuliwa usiku huu”
akasema Ruby
“Ubalozi wa Marekani
umelipuliwa?
“Ndiyo” akajibu Ruby
“Hawa lazima ni magaidi
wa IS.Hawa jamaa
tunaowashikilia lazima
wanafahamu jambo hili.Ruby
tuendelee kuwahoji mmoja
mmoja nina uhakika atatokea
mmoja ambaye atasema kila
kitu” akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu unanipa
mashaka sana kwa namna
unavyomuhoji
Marwan.Kitendo
ulichomfanyia
sijakipenda.Najua una hasira
na magaidi lakini tunatakiwa
kufuata kanuni zetu namna ya
kuhoji watu tunaowashikilia
na kanuni zetu hazielekezi
matumizi ya nguvu kupita
kiasi wakati wa kuwahoji
watuhumiwa” akasema Ruby
“Ruby please don’t be so
soft on them ! Hakuna
kuwac………..”
“I’m not soft ! akasema
Ruby kwa sauti kali
“Gosu Gosu tafadhali
niahidi kile ulichokifanya kwa
Marwan hakitajirudia tena
kama unataka nikuruhusu
endelee kuwahoji hawa jamaa”
akasema Ruby
“Ruby siwezi
kukudanganya kwamba
nitawahoji hawa jamaa kwa
lugha laini.Mimi siwezi.Kama
huridhiki kwa namna
nilivyomuhoji Marwan
ninakuruhusu utafute mtu
mwingine” akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu please !
akasema Ruby
“Ruby naomba niwe
mkweli kwako,siwezi kuwahoji
hawa jamaa kwa kutumia njia
nyepesi kwani ni sawa na
kuwatekenya wauaji wakubwa
hawa ! Lazima nitumie nguvu !
Kama hutaridhika na aina
yangu ya kuwahoji hawa
magaidi tafuta mtu mwingine
wa kuendelea kuwahoji hawa
jamaa ! akasema GosuGosu na
milango ya lifti
ikafunguka.Walipotoka tu
katika lifti simu ya Ruby ikaita
alikuwa ni katibu wake
muhtasi ambaye alimjulisha
kwamba wanamuhitaji haraka
katika chumba cha
operesheni.Ruby na Gosu
Gosu wakaelekea haraka huko.
“Kuna nini?akauliza Ruby
baada ya kuingia ndani ya
chumba kile na kuwakuta
viongozi wa idara mbali mbali
ndani ya SNSA wakitazama
video katika runinga
“Kuna video imetumwa
mtandaoni muda si mrefu”
akasema Latifah na kubonyeza
kitanza mbali video ile ikaanza
upya.Mtu mmoja akaonekana
akiwa amejifunga kitambaa
kichwani akiwa nyuma ya
kitambaa cheusi chenye
maandishi ya kiarabu ambayo
ni bendera ya kundi la IS.Mtu
Yule alijitambulisha kwa jina
la Abd Al ziz Atwah mmoja
kati ya viongozi wa IS na
katika maelezo yake alidai
kwamba IS ndio wnaohusika
katika kulipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam
usiku ule.Wakati akina Ruby
wakiendelea kuitazama video
ile akaingia mkuu wa kikosi
cha makomando
“Mkurugenzi
tumeikamilisha kazi
uliyotutuma.Kwa ujumla
haikuwa kazi ngumu na
hatukupata upinzani wowote
kwani wale jamaa hawakuwa
wametegemea kama
wangevamiwa.Tumeua walinzi
wanne waliokuwa nje
wakilinda eneo lao na
tumewachukua watu wengine
kumi na mbili wakiwa hai
akiwemo na
Marwan.Tumepekua nyumba
yao tumekuta silaha nyingi na
baada ya kuzichunguza
tumegundua ni silaha
zinazotumiwa na jeshi la
Marekani.Vile vile katika moja
ya nyumba zao tulikuta
masalia ya baadhi ya vifaa vya
kutengenezea bomu na
tunaamini bomu hilo tayari
limekwisha tengenezwa na
yawezekana limekwenda
kutumiwa sehemu Fulani”
akasema mkuu Yule wa
makomando wa SNSA
“Ahsanteni sana kwa kazi
nzuri.Tunaendelea kuwahoji
hawa watu mliowakuta mle
ndani ili tufahamu mambo
mengi wanayoyafanya.Usiku
huu kumefanyika shambulio la
bomu katika ubalozi wa
Marekani na video Ambayo
tunaitazama hivi sasa ni ya
kiongozi mmoja wa IS ambaye
amekiri kwamba wao ndio
wanaohusika katika kulipua
ubalozi ule wa Marekani hivyo
tunataka kuwahoji hawa jamaa
na kujiridhisha je bomu hilo
ambalo limetumika kulipua
ubalozi wa Marekani ni wao
wamelitengeneza? Vile vile
tunatakiwa tufanye uchunguzi
kuhusiana na silaha ambazo
unadai ni za jeshi la Marekani
tujue wamezipataje?
Tunaendelea na zoezi hilo na
ninaamini tutapata taarifa
tunazozihitaji” akasema Ruby
na kutoa maelekezo kadhaa
halafu yeye na Gosu Gosu
wakaenda ofisini kwake
“Gosu Gosu sina hakika
kama nawe unafikiri
ninavyofikiria mimi” akasema
Ruby
“Nini unakifikiria Ruby?
“Mathew alituambia
kwamba amekuja nchini kwa
misheni maalum na
akatuambia kwamba tusivamie
nyumba ile aliyokuwa akiishi
na magaidi hadi baadae usiku
wa leo.Unahisi nini
alikimaanisha kwa hiyo kauli
yake? Hudhani
alichokimaanisha kina
mahusiano na hiki
kilichotokea yaani kulipuliwa
kwa ubalozi wa Marekani?
akauliza Ruby
“Ruby uko sahihi.Hata
mimi nimejaribu kuunganisha
picha na picha kubwa
ninayoipata ni kwamba kuna
uwezekano mkubwa Mathew
akawa anahusika katika tukio
hili la kulipua ubalozi wa
Marekani.Nadhani ndiyo
maana alikataa tusivamie ile
nyumba jana usiku kwani
alijua tukivamia kila kitu
kuhusu mipango yao
kitaharibika” akasema Gosu
Gosu
“Ooh Mathew ! Kwa nini
lakini amefika hapa
alipofika?Kwa nini
akashirikiana na
magaidi?akasema Ruby kwa
masikitiko
“Ruby kumbuka
alichokisema Mathew kwamba
tusistuke kwa kile
tutakachokisikia kwani yuko
katika misheni maalum”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu utanisamehe
kwa hili nitakalolisema lakini
naona kama taratibu ninaanza
kutokumwamini
Mathew.Amekuwa mtu wa
tofauti na Mathew yule
ninayemfahamu mimi”
akasema Ruby
“Ruby sikiliza.Mathew kwa
vyovyote itakavyokuwa
anahitaji sana msaada wetu na
ndiyo maana akatuandaa kwa
sababu alijua tutakapofahamu
kuhusu kinachoendelea
tutavunjika moyo sana.Mimi
bado nina imani kubwa
naye.Hata pale dunia nzima
itakapogeuka na kumuona
Mathew ni mtu asiyefaa mimi
bado nitaendelea kusimama
naye na nitaendelea
kumuamini.Nakushauri nawe
pia usikate tamaa kuhusu
Mathew.Bila yeye
tusingefanikiwa kuwapata hata
hawa akina Marwan” akasema
Gosu Gosu na Ruby akafikiri
kidogo kisha akasema
“Nadhani tukaendelee
kuwahoji wengine lakini safari
hii nitapeleka mtu mwingine
wa kuhoji.Gosu Gosu wewe
una hasira sana na sitaki
kilichotokea kwa Marwan
kitokee kwa watu wengine
kwani tutashindwa kupata
taarifa muhimu tunazozihitaji
sana.Utanisamehe kwa hilo
Papii” akasema Ruby
“Fine” akasema Gosu Gosu
kisha Ruy akampigia simu
jamaa mwingine anaitwa Chris
akamtaka afike ofisini kwake
akampa maelekezo ya taarifa
wanazozihitaji kutoka kwa
wale magaidi waliokamatwa
kisha wote wakaelekea chini
mahala kulikokuwa na chumba
cha mahojiano na Chris
akaanza kuwahoji wale
magaidi
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Rais William Washington
wa Marekani alijitokeza mbele
ya waandishi wa habari
waliofika katika viwanja vya
ikulu ya Marekani.
“Habari za mchana ndugu
waandishi wa habari.Kama
nyote mlivyosikia saa chache
zilizopita ubalozi wetu jijini
Dar es salaam Tanzania
umeshambuliwa kwa bomu na
kuharibiwa vibaya.Watu wengi
waliokuwepo katika ubalozi
huo wakiwemo wamarekani na
raia wa mataifa mengine
ambao walikuwa wanapatiwa
hifadhi ubalozini hapo
kufuatia vurugu za kidini
zinazoendelea nchini Tanzania
wanahofiwa kupoteza maisha.
Kundi la kigaidi la IS tayari
limekiri kuhusika na
shambulio hilo
“Ndugu waandishi wa
habari,kupitia kwenu nataka
nitoe pole kwa wamarekani
walipoteza wapendwa wao
katika shambulio hilo lakini
nataka niwaahidi kwamba
hatutakaa
kimya.Tumechokozwa na
tutajibu vikali.Tutawasaka
magaidi wa IS kokote waliko
duniani na kuhakikisha
tunalifutilia mbali kundi hili
hatari kwa sasa
ulimwenguni.Hizi ni salamu
ninatuma kwa IS na makundi
mengine ya kigaidi duniani
kwamba siku zao
zinahesabika.Hawana sehemu
ya kukimbilia kujificha kwani
hakuna jiwe litasalia juu ya
jiwe hadi tutakapoakikisha
gaidi wa mwisho
amepatikana.Nawaomba
wamarekani waendelee na
shughuli zao za kila siku bila
hofu yoyote.Ahsanteni sana”
Rais William akamaliza
hotuba yake fupi na hakukuwa
na maswali akarejea ndani na
moja kwa moja akaelekea
ofisini kwake.Kabla hajafanya
chochote akampigia simu Rais
wa Tanzania Dr Fabian Kelelo
“Mheshimiwa Rais habari
yako” akasema Rais Willaim
baada ya Dr Fabian kupokea
simu
“Habari si nzuri
mheshimiwa Rais.Nadhani
umekwisha pata taarifa za
magaidi kushambulia ubalozi
wa Marekani hapa Dar es
salaam”
“Tayari nimepata taarifa
hizo.Poleni sana kwa hiki
kilichotokea”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais”
“Dr Fabian nimekupigia
kukujulisha kwamba
nimezipokea kwa mstuko
taarifa za shambulio la bomu
katika ubalozi wetu na
ninaahidi kwamba tutawasaka
magaidi hao kokote waliko na
kuwapata wote.Hatutalala hadi
pale gaidi wa mwisho
atakapopatikana.Kwa ajili hiyo
basi nitatuma vikosi zaidi vya
wanajeshi nchini Tanzania
kuwasaka magaidi
hawa.Naamini hakutakuwa na
tatizo katika suala hilo
mheshimiwa Rais” akasema
Rais William
“Hakuna tatizo
mheshimiwa Rais.Vikosi hivyo
vitakavyokuja vitashirikiana na
vikosi vyetu katika
kuhakikisha tunawasaka na
kuwatia nguvuni magaidi
wote” akasema Dr Fabian
Mazungumzo kati ya Dr
Fabian na William Washington
yaliendelea na zaidi sana
yalilenga katika mashirikiano
ya kijeshi kuwasaka magaidi
waliolipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam
na kutuliza vurugu zilizokuwa
zinaendelea.
Wakati Rais William
Washington akizungumza na
Rais wa Tanzania Dr,makamu
wake Mark Piller alitembelewa
na David Walker mkuu wa
idara ile ndogo ndani ya CIA
inayojishughulisha na
mahusiano na makundi ya
kigaidi.
“Karibu sana David”
akasema Mark
“Ahsante sana
Mark”akajibu David ambaye
kiumri ni mkubwa kuliko Mark
Piller
“Hongera sana
David.Nimepata taarifa za
kilichotokea Dar es salaam
nimefurahi sana.Mipango yetu
inakwenda vizuri kama
tunavyotaka” akasema Mark
Piller
“Pongezi kwetu sote Mark
kwa maendeleo haya
mazuri.Hivi sasa dunia nzima
inafahamu kuwa ni IS
walioshambulia ubalozi wetu
jijini Dar es salaam.Tumeanza
vyema na nina uhakika
mkubwa kwamba safari hii
tutapenya hadi zile sehemu za
siri za Iran kwani mpango huu
wa kumtumia Abu Zalawi ni
mpango mkubwa sana”
akasema David
“Ni kweli David mpango
huu nina uhakika mkubwa
utafanikiwa kwani Yule jamaa
ni mmoja wa magadi ambaye
ameonyesha uwezo mkubwa
sana tofauti na magaidi
tunaowafahamu ambao
wanachojua ni kulipua
mabomu na kuua watu”
“Tukiachana na hilo kuna
jambo ambalo limenileta
hapa.Ni kuhusiana na ule
mpango wetu wa kusambaza
kirusi nchini Tanzania”
akasema David
“Kuna nini katika mpango
huo?
“Tayari mtu wa kupeleka
kirusi hicho Tanzania
amepatikana na tayari
amekwisha wasili hapa
Marekani”
“Safi sana” akasema Mark
“Hata hivyo kuna tatizo
limejitokeza”
“Tatizo gani?
“Nilikuwa na mazungumzo
na wanasayansi wetu
wanaotutengenezea hicho
kirusi.Maendeleo ni
mazuri.Tulipowataka
watutengenezee kirusi maalum
cha maangamizi tayari
walikuwa na aina ya kirusi
kilicho na sifa ka kile
tunachokihitaji kinaitwa
March26.Kirusi hicho
kinasambaa kwa njia ya hewa
na kinapoingia mwilini mwa
binadamu humchukua saa
ishirini na nne kuanza kupata
dalili za mwanzo ambazo ni
homa na mafua makali sana na
baada ya muda mgonjwa
huanza kukohoa na kutokwa
na damu puani.Mgonjwa
hufariki ndani ya saa 48 toka
apate dalili za mwanzo za
maambukizi ya virusi hivyo
hatari” akasema David
“Hicho ndicho hasa kirusi
tunachokihitaji sisi” akasema
Mark Piller
“Ni kweli ni kirusi
ambacho tunakihitaji mno
lakini kuna tatizo ambalo
limemjitokeza”
“Nini kimejitokeza David?
Akauliza Mark Piller
“Wanasayansi wale bado
hawajafanikiwa kupata kinga
ya kirusi hicho” akasema
David
“Hawajapata kinga?
Akauliza Mark Piller
“Ndiyo bado hawajapata
kinga zoezi ambalo
wanaendelea nalo hivi
sasa.Hilondilo tatizo lililopo
Mark” akasema David
Walker.Mark Piller
akajiegemeza kitini na kuvuta
pumzi ndefu.
“Kweli hili ni
tatizo.Tunahitaji kirusi
ambacho tayari kina kinga
yake ili tuweze kuwakinga
watu wetu.Tunao wanajeshi
wetu kule Afrika mashariki na
vile vile lazima tujihadhari
endapo kirusi hicho kitavuka
mipaka ya Tanzania na
kusambaa hadi Marekani”
akasema Mark Piller na
kuzama mawazoni halafu
akauliza
“Wanasayansi hao
wamesema itawachukua muda
gani kuweza kupata kinga
hiyo?akauliza Mark
“Hawana uhakika
itachukua muda
gani.Yawezekana ikawa ni
wiki,miezi au hata mwaka
lakini ni zoezi wanaloendelea
nalo usiku na mchana”
akasema David Walker
“Pamoja na jitihada hizo
wanazoendelea nazo lakini
tunahitaji kirusi chenye
kinga.Hatutaki kuweka
hatarini maisha ya watu wetu
huko Afrika mashariki”
akasema Mark Piller na
ukimya ukapita
“Mark kuna jambo ambalo
wanasayansi wamelishauri”
“Wameshauri kitu gani?
Akauliza Mark Piller
“Walichonieleza ni
kwamba kuandaa kirusi
kingine cha aina tunayoihitaji
itachukua muda mrefu na sisi
hatuna muda mrefu wa
kusubiri.Mpango wetu
unahitaji kirusi kwa haraka
zaidi na kirusi ambacho
wanasayansi wetu wanacho ni
hicho ambacho bado hakina
kinga yake”
“Nini unataka kukisema
David?akaliza Mark Piller
“Ninataka kushauri
kwamba tukitumie kirusi
hicho..”
“Hapana David ! akasema
Mark
“Hatuwezi kwa namna
yoyote ile kutumia kirusi
hicho” akasema Mark
“Nisikilize Mark” akasema
David
“Wanasayansi hao
wameshauri kwamba
tunaweza kukitumia kirusi
hicho na kikasambazwa nchini
Tanzania labla hata kinga yake
haijapatikana.Kuna namna
ambayo wanajeshi na raia
wengine wanaweza
wakakingwa kwa vifaa
maalum” akasema David
“Ni vipi kama kirusi hicho
kitavuka mipaka ya Tanzania
na kusambaa katika nchi
nyingine za jirani,baadae
Afrika nzima na kisha dunia
nzima?Wasiwasi wangu ni pale
ambapo kirusi kitasambaa
wakati kinga yake bado
haijapatikana”
“Uwezekano wa virusi
hivyo kufika Marekani ni
mdogo sana kwani kutafanyika
udhibiti mkubwa.Angalia kuna
virusi vya ugonjwa wa Ebola
ambao ni mbaya sana lakini
havijafika bado Marekani nina
uhakika mkubwa kwamba hata
kama tukipeleka kirusi hicho
Afrika hakitaweza kufika
Marekani”
“Nakubali inaweza
kuchukua muda mrefu kwa
kirusi hicho kufika Marekani
lakini ukumbuke tuna
wanajeshi wetu kule Tanzania
ambao kuna uwezekano
mkubwa sana wakaweza
kupata maambukizi ya virusi
hivi na ndiyo maana nilitaka
tuwakinge kwanza watu wetu
ndipo kirusi hicho kisambazwe
lakini tukisambaza kirusi bila
kuwakinga tutakuwa
tumewazika watu wetu
wenyewe.Kama watu wetu
wataathirika basi kuna
uwezekano mkubwa dhumuni
la operesheni hii likashindwa
kufanikiwa kwani tunataka
kuendelea kuchota madini na
mafuta”
“Usiwe na hofu
Mark.Watu wetu kule
Tanzania watapewa suti
maalum za kuvaa kujikinga na
maambukizi hayo na
wataendelea na shughuli zao
kama kawaida” akasema David
“Pamoja na vifaa hivyo
David lakini tunawaweka watu
wetu katika hatari kubwa ya
kupata maambukizi ! akasema
Mark Piller
“Mark hii ni kama vita
tunapigania uchumi wa nchi
yetu hivyo basi kama
wakitokea wanajeshi wetu
kadhaa wakapoteza maisha
nchini Tanzania,watakuwa ni
mashujaa waliokufa
wakilipigania taifa
lao.Hatuwezi kuogopa
kupoteza watu kumi au ishirini
kwa maslahi mapana ya nchi
yetu.Lazima tufanye maamuzi
magumu sana ya kusambaza
kirusi hivyo hivyo hata kama
hakina kinga ila tuchukue
tahadhari za kuwasaidia watu
wetu kule wasipate
maambukizi na wakati huo
huo wanasayansi wetu
watakuwa wanaendelea
kutafuta kinga dhidi ya kirusi
hicho.Kwa kuwa wanajeshi na
watu wetu wanarejea
nyumbani kila mara tutatenga
sehemu maalum kwa ajili yao
ambako watakaa kwa muda
kabla hawajakutana na watu
wengine watachunguzwa kama
wameambukizwa virusi hivyo
na kama wakithibitika hawana
maambukizi basi
wataruhusiwa kwenda
kuonana na familia zao lakini
naamini ndani ya kipindi
kifupi wanasayansi wetu
watafanikiwa kupata kinga
dhidi ya kirusi hicho” akasema
David Walker
“David umenipa wakati
mgumu sana wa kufanya
maamuzi kuhusu hili jambo
ambalo linaweza kuwa hatari
sana kwa mustakabali wa
dunia” akasema Mark
“Mark usiwe na
hofu.Kirusi hiki hakitaweza
kufika Marekani kwani
udhibiti wa virusi kusambaa
utakuwa mkubwa.Jambo
lingine la faida kwetu ni
kwamba pale wanasayansi
wetu watakapofanikiwa
kuipata kinga hiyo itatuingizia
mabilioni ya dola kama nchi
kwani dunia nzima watanunua
kinga hiyo kwa hofu ya kile
watakachokuwa wamekiona
kimetokea
Tanzania.Nakushauri Mark
tufanye maamuzi haya
magumu ya kusambaza kirusi
hicho Tanzania ili mipango
yetu iendelee.Hili ni dirisha
ambalo hatupaswi kuliacha
likafungwa” akasema David na
Mark akakuna kichwa
“Taarifa kutoka Tanzania
si nzuri.Tulitegemea baada ya
mauaji ya kiongozi mkuu wa
waislamu Tanzania zingeibuka
vurugu kubwa lakini imekuwa
tofauti.Hakuna vurugu na
viongozi wa dini na serikali
wanajitahidi sana kuzuia
vurugu hizo zisiendelee.Kuna
kila dalili amani inaanza
kurejea Tanzania na kwa sasa
wanajitahidi kutafuta chanzo
cha vurugu zilizopelekea
kushambuliana wao kwa wao
na wakigundua kwamba
wamefarakanishwa basi
mipango yetu yote itakuwa
imekwama kwani watajiunga
tena na kuwa wamoja na
ikifikia hatua hiyo hakuna
kitakachoweza
kuwafarakanisha.Hii ni nafasi
ambayo lazima tuitumie
kikamilifu.Wakati wakijaribu
kutafuta amani tukasambaze
kirusi .Tutaanza kusambaza
sehemu zile ambazo
tumezilenga.Kwenye
machimbo ya madini kama
Tanzanite,dhahabu
nk.Ugonjwa ukianza kusambaa
sehemu hizo tutapeleka watu
wetu kwa lengo la kutoa
msaada na hiyo ndiyo fursa
yetu ya kuchukua madini kiasi
chochote tukitakacho na
wakati huohuo mafuta
yataendelea kumiminika
katika hifadhi yetu” akasema
David Piller
“David ninakuelewa sana
lakini kuna sauti ninaisikia
ndani mwangu inanionya
tusifanye hicho
unachonishauri
tukifanye”akasema Mark Piller
“Mark sauti hiyo ni
uoga.Usiiruhusu ikatawala
ndani mwako.Huu ni wakati
wa kuzikataa sauti zote
unazozisikia na kujielekeza
katika suala moja tu la faida
zitakazopatikana kwa nchi yetu
pale tutakaposambaza kirusi
hiki” akasema David Walker
na Mark akanyamaza
akitafakari
“Mark ninasubiri jibu lako
ili maandalizi
yaendelee.Wengine wote
wamekubali ni wewe pekee
tunayekusubiri” akasema
David
“David siwezi kusema
hapana kama ninyi nyote
mmelikubali jambo
hili.Mipango iendelee lakini
lazima wanasayansi hao
wapewe muda maalum wa
kuhakikisha wamepata kinga
ya kirusi hicho vinginevyo
tutakuwa tumeiweka dunia
katika hatari kubwa.Vile vie
watu wetu kule Tanzania
lazima tuwakinge” akasema
Mark Piler
“Hayo yote yatatekelezwa
Mark.Nakuhakikishia
maamuzi haya tuliyoyafanya ni
sahihi na yana maslahi
makubwa sana kwa nchi yetu”
akasema David Walker na
kuagana na makamu wa Rais
akaondoka
“Siamini kama hiki
tunachokwenda kukifanya ni
kitu sahihi.Kusambaza kirusi
bila kinga yake ni hatari
sana.Ni vipi kama kirusi hicho
kitasambaa sehemu mbali
mbali duniani na kusababisha
maangamizi makubwa? Ni vipi
kama kitasambaa na kufika
Marekani? Ilipaswa tuwakinge
kwanza watu wetu kabla ya
kukisambaza kirusi hicho”
akawaza Mark
“Lakini kwa upande wa pili
wazo la David ni
zuri.Tunahitaji kusambaza
kirusi haraka ili mipango yetu
iendelee japo tulipaswa kuwa
na kinga kwanza ndipo
tusambaze kirusi .Mimi peke
yangu siwezi kuwa na nguvu ya
kuzuia maamuzi ya wenzangu”
Mark Piller alijawa na mawazo
mengi sana baada ya David
kuondoka
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Hadi kunapambazuka ni
matukio machache tu ya
vurugu yalikuwa yameripotiwa
jijini Dar es salaam.Asubuhi
hii jiji la Dar lilionekana kuwa
shwari licha ya hofu kubwa
kuendelea kutanda kufuatia
kulipuliwa kwa ubalozi wa
Marekani usiku wa kuamkia
siku hii.Tukio hilo ndilo
lililotawala vyombo vyote vya
habari asubuhi.Maduka
machache yalifunguliwa katika
baadhi ya mitaa ili watu
waweze kujipatia mahitaji
muhimu na ulinzi
uliimarishwa sana katika
mitaa mingi magari ya doria
yaliendelea kuzunguka
kuhakikisha hali inaendelea
kuwa shwari.
Katika ofisi za SNSA kazi
kubwa iliyofanyika usiku
kucha ilikuwa ni kuwahoji
magaidi waliokamatwa ili
kufahamu mahala alipo Assad
Ismal.Hadi jua lilipoanza
kuchomoza hakuna gaidi hata
mmoja miongoni mwa wale
magaidi wote waliokamatwa
aliyekubali kusema mahala
alipo Assad.
“Ruby tumekesha usiku
mzima tukiwahoji hawa jamaa
lakini hakuna
walichokisema.Nilikutahadhar
isha mapema kwamba hawa
watu ni wagumu mno
kufunguka na wako tayari hata
kufa kuliko kutoa siri.Kwa
namna walivyokuwa
wanahojiwa ni kama walikuwa
wanapapaswa tu ndiyo maana
wameendelewa kuwa na
kiburi.Ruby niruhusu niwahoji
hawa watu.Nakuhakikishia
lazima mmoja wao
atafunguka” akasema Gosu
Gosu wakiwa ofisini kwa Ruby
“Gosu Gosu
hapana.Ulichokifanya jana
kwa Marwan
hakikunifurahisha.Japo kuwa
ni watu makatili lakini lazima
tuwe na
ubinadamu,tusiwatendee
ukatili kama ule uliomfanyia
Marwan.Kama nisingeingia
mle ndani ulikuwa tayari
kuendelea kukata viungo vyake
halafu nini
kingefuata?Marwan
angepoteza maisha na
tungekosa kila
kitu.Utanisamehe GosuGosu
lakini sintakuruhusu uwatese
hawa jamaa kwani una hasira
za karibu sana na huogopi
kuua” akasema Ruby
“Ruby hawa jamaa hawana
ubinadamu hata kidogo na
hawastahili huruma.Tazama
walichokifanya katika nchi
yetu.Ni hawa ambao
wametumiwa kuchochea
vurugu na watanzania
wakaanza kushambuliana na
kuuana.Hawa wamechangia
kwa kiasi kikubwa kuifikisha
nchi yetu hapa ilipofik…...”
“Gosu Gosu nimekwisha
sema hautawahoji hawa jamaa
and that’s final ! akasema
Ruby akionekana
kuchoka.Gosu Gosu
akamtazama halafu akatikisa
kichwa
“Nakuhakikishia Ruby
kwamba kwa staili hii
hatutaweza kupata kitu
chochote kutoka kwa hawa
jamaa.Umesahau namna
Mathew anavyowahoji watu
wa namna hii? Akauliza Gosu
Gosu
“Mathew hayuko hapa na
hatuwezi kuiga ufanyaji kazi
wake.Watu hawa tutakwenda
nao taratibu na nina uhakika
mkubwa lazima
watafunguka.Zipo njia nyingi
tu za kuwafungua watu wa
namna hii lakini si kwa
kuwakata viungo vyao kama
ulivyofanya jana.Jiandae
unakwenda Kilimanjaro
kumpokea Nawal”
“Mimi? Nakumbuka
ulisema wewe ndiye
utakayekwenda huko”
“Nimebadili mipango
utakwenda wewe badala yangu
na mimi nitabaki hapa
kuhakikisha mambo
yanakwenda vizuri” akasema
Ruby na kutazamana na Gosu
Gosu
“Ruby kwa nini niko hapa?
Kwa nini uliniomba niwe
msaidizi wako?Ulinileta hapa
niwe mlinzi wako au
tusaidiane katika kazi?
Akauliza Gosu Gosu
“Gosu Gosu najua hili
halijakupendeza lakini
naomba uvumilie.Naamini
hadi jioni ya leo tutakuwa
tumepata kitu Fulani kutoka
kwa hawa jamaa” akasema
Ruby
“Kama isingekuwa ni
Mathew ameniomba niendelee
kuwepo hapa nihakikishe
unakuwa salama ningeondoka
hapa dakika hii hii ! akawaza
Gosu Gosu.Ruby akataka
kusema kitu lakini simu yake
ikaita
“Rais anapiga” akasema
Ruby na kuipokea ile simu
“Mheshimiwa Rais
shikamoo” akasema Ruby
“Ruby uko wapi? Akauliza
Dr Fabian
“Niko ofisini mheshimiwa
Rais”
“Tazama runinga sasa hivi
halafu tutazungumza”
akasema Dr Fabian na haraka
haraka Ruby akawasha
runinga na kukuta kuna habari
mpasuko iliyokuwa
inaendelea.Katika habari ile
kulikuwa na picha ya Mathew
Mulumbi na maandishi
yaliyopita chini yaliandikwa
Gaidi aliyelipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam
akamatwa Nairobi Kenya.Ruby
alihisi nguvu zinamuisha
akataka kuanguka Gosu Gosu
akawahi kumdaka
akamketisha kitini.
“Ruby relax ! Take a deep
breath ! akasema Gosu Gosu
na Ruby akavuta pumzi ndefu
mara tatu.
“Gosu Gosu
nimechoka.Najuta kwa nini
nilikuja Tanzania ! Najuta kwa
nini nilimfahamu Mathew
Mulumbi ! akasema Ruby
“Shhhhh ! akasema
GosuGosu
“Gosu Gosu nitakwenda
wapi mimi? Mathew ndiye
mwanaume ninayempenda
kuliko wote duniani kwa nini
akafanya hivi?
“Usiseme chochote na
wala usijilaumu Ruby.Mathew
alikwisha tuandaa kwa jambo
hili”
“Mwongo mkubwa Yule !
akasema kwa ukali Ruby huku
akilia.
“Ruby usiseme hivyo
tafadhali.Mathew si
mwongo.Alijua tutastuka sana
na kuumia ndiyo maana akaja
kwetu kutuandaa na
alitusisitiza kwamba tusistuke
tutakaposikia kitu kibaya
kuhusu yeye.Kile alichokuwa
anakisema ni hiki” akasema
Gosu Gosu
“Gosu Gosu ni misheni
gani hii aliyonayo Mathew
hadi akaamua kujiingiza katika
ugaidi? Mathew ni jasusi na ..”
akasema Ruby na simu yake
ikaita alikuwa ni Dr Fabian
Kelelo Rais wa Tanzania.Ruby
akafuta machozi na kuipokea
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby
“Ruby tafadhali niambie
nini kinaendelea?
“Mheshimiwa Rais hata
mimi sielewi chochote.Wote
hapa tumebaki midomo wazi
hatuamini hiki tunachokiona”
“Mathew Mulumbi !
akasema Dr Fabian naye akiwa
haamini
“Toka mwanzo sikuwahi
kumkubali Yule jamaa.Kumbe
nilikuwa sahihi kabisa
kutokumwamini na hiki
alichokifanya naamini wote
walionipibnga watakubaliana
nami kwamba nilikuwa sahihi
kutomkubali
Mathew.Inaniuma kwa sababu
tulimuacha akazifahamu
baadho ya siri zetu za nchi mtu
ambaye ni gaidi ! Imeniumiza
sana Ruby “ akasema Dr
Fabian kwa masikitiko
“Mheshimiwa Rais sijui
niseme nini lakini hata mimi
binafsi bado
siamini.Ninamfahamu
Mathew
Mulumbi,nimeshirikiana naye
katika misheni kadhaa lakini
hata siku moja sikuwahi kuota
kama angeweza kubadilika na
kuingia katika
ugaidi.Nimepatwa na mstuko
mkubwa sana mheshimiwa
Rais” akasema Ruby
“Ruby,wewe na Gosu Gosu
ni watu wake wa karibu
sana.Je mlifahamu uwepo
wake hapa nchini? Akauiliza
Dr Fabian
“Hapana mheshimia
Rais.Hatukujua kuhusu uwepo
wake hapa nchini na wala
hatukuhisi kama anaweza
akahusika na shambulio lile
hadi baada ya taarifa ya
kukamatwa kwake
kutangazwa” akajibu Ruby
“Dah ! ninazidi
kuchanganyikiwa kwa mambo
haya yanayoendelea hapa
nchini kwetu.Naomba
tafadhali leo jioni tukutane
tujadiliane na unipe taarifa za
mahala mlikofikia katika
uchunguzi wenu” akasema Dr
Fabian
“Nitakuja mheshimiwa
Rais” akasema Ruby na Dr
Fabian akakata simu
“Gosu Gosu
nimechanganyikiwa sijui
nianzie wapi,sijui nifanye nini”
akasema Ruby
“Ruby naomba unisikilize”
akasema Gosu Gosu na Ruby
akainua kichwa akamtazama
“Mathew alijua haya yote
yatatokea na alijua kwamba
dunia nzima itamgeuka lakini
akatutaka sisi wawili tusimame
naye.Tutafanya kosa kubwa
sana kama na sisi tutashindwa
kumuamini Mathew.Binafsi
naamini yuko katika misheni
kubwa kama alivyosema yeye
mwenyewe.Hata siku moja
Mathew hawezi kuwa
gaidi.Lazima ameingia katika
mitandao hiyo ya kigaidi kwa
lengo maalum.Mtu yeyote
anayemfahamau vyema
Mathew Mulumbi hataamini
akisikia eti amekuwa
gaidi.Hebu jiulize kwa nini
akajenga mahusiano na
Habiba Jawad ambaye
anajulikana kwa kufadhili
ugaidi duniani? Hapa lazima
kuna kitu hatukifahamu.Tuwe
na subira na tutafahamu
mambo mengi lakini kubwa
tumuamini” akasema Gosu
Gosu na Ruby akavuta pumzi
ndefu
“Ruby mambo ndiyo
kwanza yameanza.Mathew
alitufumbua kwamba hiki
kinachoendelea hapa nchini
kina pande mbili ndani na nje
ya nchi na akaweka wazi
kwamba yeye
atawashughulikia wale watu
wa nje na sisi akatutaka
tuwashughulikie wale watu wa
ndani. Mathew ameanza
sehemu yake na sisi
tunatakiwa kuendelea na
sehemu yetu”akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu sitaki
nikudanganye lakini hili
alilolifanya Mathew limevuka
mpaka.Mathew si mwenzetu
tena na hapaswi kuaminiwa
kwa lolote.He’s a liar and a
traitor ! akasema Ruby
“Is that what you think?
Akauliza Gosu Gosu
“Gosu Gosu jiandae
unaelekea Kilimanjaro
kumpokea Nawal.Leave me
alone for now ! akasema Ruby
na Gosu Gosu akatoka
“Kwa nini Mathew
ameamua kubadilika namna
hii? Ni mtu ambaye
amekwisha fanya mambo
makubwa kabisa hapa nchini
lakini leo hii ameamua
kujiunga na magaidi.Natamani
hata nigeuke upepo nipotee
kabisa nisionekane ! akawaza
Ruby
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 2
Helkopta ya jeshi la
Marekani iliyombeba Mathew
Mulumbi ikitokea jijini
Nairobi,ilitua katika kambi ya
jeshi la wanamaji wa Marekani
iliyoko Mombasa
Kenya.Mathew alishushwa
katika helkopta akiwa
amefunikwa mfuko kichwani
na mikono yake ikiwa
imefungwa pingu.Akiwa
ameongozana na makachero
wa shirika la ujasusi la
Marekani waliomkamata
wakati akijaribu kutafuta
usafiri wa kumpeleka
Mogadishu Somalia,aliingizwa
katika boti maalum na safari
ya kilometa 1750 kueleka jiji la
Victoria nchini Seychelles
ikaanza.Ndani ya boti ile
kulikuwa na watu wapatao
sita.
“Mambo
yameanza.Naamini mpaka
sasa tayari taarifa zimekwisha
sambaa duniani kwamba
nimekamatwa kwa kulipua
ubalozi wa Marekani jijini Dar
es salaam.Nilifanya vizuri
kuwapa tahadhari mapema
akina Gosu Gosu wasistuke
watakapopata taarifa hizi
kwani ni moja ya misheni
zangu.Naamini watayazingatia
yale niliyowaelekeza” akawaza
Mathew huku boti ile yenye
mwendokasi wa kilometa 250
kwa saa ikichana mawimbi
kwa kasi kubwa.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 3
Ndege ya shiria la ndege la
Ethiopia ikitokea Riyadh Saudi
Arabia kupitia Adis Ababa
ilitua katika uwanja wa ndege
wa Kilimanjaro.Tayari
ilikwisha timu sa kumi na
moja na nusu za jioni.Gosu
Gosu akiwa na watu wawili wa
SNSA kanda ya Kaskazini
tayari walikwisha wasili
uwanjani kwa ajili ya
kumpokea Nawal.Gosu Gosu
ambaye alikuwa amevaa suti
nyeusi siku hii aliitoa mfukoni
picha ya Nawal akaitazama na
kuirudisha mfukoni.
“ Anaonekana mrembo
sana huyu mwanamke japo
anajihusisha na ugaidi”
akawaza Gosu Gosu huku
akitabasamu
“Sitakiwi kwa namna
yoyote ile kuruhusu akili yangu
ikavutiwa na wanawake hasa
hawa warembo.Nimekwisha
umwa na nyoka na sasa kila
nikiguswa na juani
ninastuka.Nilichungulia kaburi
kwa kujiingiza katika
mahusiano na Melanie na toka
wakati ule nimewaogopa sana
wanawake ! akawaza Gosu
Gosu wakiwa katika sehemu ya
kusubiria abiria wanaowasili.
Abiria walishuka na
kuelekea katika jengo la kisasa
la kupokelea abiria kwa ajili ya
kukamilisha taratibu mbali
mbali na walihudumiwa
haraka haraka na kuanza
kuelekea sehemu ya kutokea
abiria wanaowasili. Macho ya
Gosu Gosu yaliyoangaza kama
tai yalimuona Yule waliyekuwa
wanamsubiri ambaye ni
Nawal.Alikuwa amevaa suruali
ya jeans ya bluu na nywele
zake ndefu nyeusi alizibana
kwa nyuma huku macho yake
akiyafunika kwa miwani
myeusi.Ili kujiridhisha Gosu
Gosu akaingiza mkono katika
mfuko wa koti na kutoa picha
akaitazama
“That’s her” akawaza Gosu
Gosu kisha akaanza
kumsogelea.
“Nawal ! akaita baada ya
kukaribia.Nawal akageuka na
kumtazama Gosu Gosu
ambaye alimpa ishara ya
kichwa na Nawal akaielewa
akamfuata wakasalimiana
“Karibu sana
Tanzania.Naitwa Papi Gosu
Gosu.Nimetumw ana Ruby
kukupokea” akasema Gosu
Gosu
“Jna lako gumu sana.Gasu
Gasu !
“Gosu Gosu” Gosu Gosu
akamsahihisha
“Usijali utazoea tu”
akasema Gosu Gosu na
kumsaidia Nawal kukokota
mabegi yake hadi kwenye gari
kisha wakaondoka pale
uwanjani
“Tunaelekea wapi?
Akauliza Nawal
“Tunaelekea Arusha”
akasema Gosu Gosu
“Ruby yuko wapi?akauliza
Nawal
“Ruby yuko Dar es salaam
na amenituma mimi nije
kukupokea badala yake”
akajibu Gosu Gosu na Nawal
akayaelekeza macho yake nje
“Dah ! mtoto huyu si
mchezo.Amependelewa uzuri
lakini kasoro yake ni hiyo moja
tu mama yake ni mfadhili wa
magaidi naamini hata huyu
kilichomleta huku Tanzania ni
kuhusiana na mambo hayo ya
kigaidi” akawaza Gosu Gosu
akimtazama Nawal kwa kuibia.
“Mara ya kwanza kufika
Tanzania?akauliza Gosu Gosu
“Ndiyo.Ni mara ya kwanza
ninafika Tanzania lakini mara
ya pili ninafika bara la Afrika”
“Ouh kumbe umekwisha
tembelea bara la Afrika”
“Ndiyo nilikwenda kwenye
matembezi nchini Misri”
“Karibu sana Tanzania”
“Ahsante nashukuru”
akasema Nawal
“Nimeshangaa kidogo hali
ninayoishuhudia huku ni
tofauti na ile tunayoiona katika
vyombo vya habari vya
nje.Tunashuhudia vurugu
kubwa sana maiti za watu
zimezagaa
barabarani,majumba
yanachomwa nk” akasema
Nawal
“Siku zote vyombo vya
habari vya nje vina lengo moja
tu la kupotosha taswira halisi
ya bara la Afrika na
yanapotokea machafuko kama
haya yaliyotokea nchini mwetu
basi huripoti tofauti na hali
halisi ilivyo kwa malengo yao
wanayoyajua lakini sikatai
vurugu zipo ila kwa hapa
Tanzania kuna baadhi ya
mikoa ambayo vurugu hizo
zilikuwa kubwa sana kama vile
mikoa ya Dar es salaam na
Tanga.Mikoa mingine kama
huku Kaskazini na kwingineko
vurugu zilitokea kidogo lakini
vyombo vya ulinzi vikawahi
kudhibiti na hali imeendelea
kuwa shwari.Mikoa ambayo
mpaka sasa naweza kusema
hali si shwari ni Dar es salaam
na Tanga kidogo na mkoa wa
Pwani.Miji hiyo miwili naweza
kusema ilikuwa imesimama
kutokana na machafuko
makubwa yaliyotokea.Kwa
sasa kidogo hali imeanza
kutulia japo bado yapo
makundi ya watu wenye silaha
ambao wanazunguka mitaani
kuendeleza vurugu lakini kwa
kiasi kikubwa hali ya sasa si
kama vile ilivyokuwa
mwanzo.Wakati naondoka Dar
es salaam leo asubuhi
nilishuhudia baadhi ya
maduka yamefunguliwa na
watu kujipatia mahitaji na
nimepata taarifa kuna masoko
mawili matatu yalifunguliwa
leo japo bado watu wana hofu
kubwa kuonekana katika
mikusanyiko ya watu.Kwa
ujumla naweza kusema hali
imeanza kutulia.Watanzania si
watu wa kupenda vurugu na
ndiyo maana vurugu hizi
zitamalizika muda si mrefu
sana na maisha kurejea
kawaida” akasema Gosu Gosu
“Poleni sana.Ni mara ya
kwanza Tanzania inakumbwa
na machafuko makubwa kiasi
hiki” akasema Naal
“Ni kweli watanzania
wamezoea amani na siku zote
tumekuwa tukiishi kama
ndugu kila mtu anajiuliza nini
hasa kimetokea hadi
tukajikuta hapa tulipofika
kuanza kushambuliana na
kuuana sisi kwa sisi kwa
sababu ya dini?
“Serikali yenu inasema
nini kuhusu jambo hili?
Waasisi wa vurugu hizi tayari
wamekamatwa?
“Kwa sasa serikali bado
inaendelea na jitihada za
kutuliza vurugu,kudhibiti
makundi ya watu wenye silaha
ambao wamekuwa
wakiendesha mashambulio
mbali mbali na hata kuua
viongozi wa dini kwa mfano ni
juzi tu wamemuua Mufti wa
Tanzania.Jana usiku ubalozi
wa Marekani umelipuliwa na
kundi la kigaidi la IS.Matukio
kama haya yanazidi kuleta
hofu lakini serikali inaendelea
kujitahidi kudhibiti matukio
kama haya yasiendelee
kutokea.Baada ya kurejesha
hali kuwa ya amani ndipo
wataanza kulifanyia uchunguzi
jambo hili kulifahamu
kiundani na kuwabaini watu
waliosabaisha tukafika hapa”
akasema Gosu Gosu na ukimya
ukatawala garini
“Nimetaja kundi la IS
amenyamaza kimya.Huyu
lazima ni mmoja wao na
lazima atakuwa amekuja kwa
mipango ya kundi
hilo.Imekuwa bahati mbaya
kwake ameangukia katika
mikono yangu na lazima
atasema kila kilichomleta hapa
Tanzania. Mama yake ni gaidi
lazima huyu naye ni gaidi !
akawaza Gosu Gosu huku
akiendelea kumtazama Nawal
kwa jicho la wizi.
“Hata hivyo ni mrembo na
anaonekana kujiamini sana”
akawaza Gosu Gosu.
Nawal hakuonekana kuwa
na wasi wasi wowote
aliyaelekeza macho yake nje na
mara kadha alikuwa
anatabasamu
“Mbona unatabasamu
Nawal? Akauliza Gosu Gosu ”
“Ninatabasamu kwa uzuri
wa mkoa huu.Ukijani kila
sehemu,mito mingi
inabubujisha maji,majengo
mazuri kila mahali
nimeupenda sana mkoa huu”
akasema Nawal
“Bado haujashuhudia
uzuri wake.Ukiacha haya
unayoyaona njiani lakini kuna
mbuga za wanyama katika
mkoa huu kama vile
Manyara,Arusha na Tarangire
vile vile kuna bonde la
Ngorongoro,kuna mlima Meru
na mambo mengine mengi ya
kuvutia” akasema Gosu Gosu
“Unaonekana ni mkoa
uliobarikiwa kuwa na vivutio
vingi.Nitakapomaliza shughuli
yangu iliyonileta hapa
Tanzania nitakuja kutembelea
Arusha kuona vivutio hivyo
ulivyonitajia” akasema Nawal
“Una siku ngapi za kukaa
hapa Tanzania?akauliza Gosu
Gosu
“Hapa nina siku tisini”
“Ouh ni muda mrefu sana
huo.Kama ni mpenzi wa
kwenda katika vivutio vya
kitalii basi utatembelea vivtio
vyote vilivyopo hapa nchini
kwetu”
“Unaweza ukanitajia
tafadhali vivutio vingine
vilivyopo hapa Tanzania?
Akauliza Nawal
“Hapa ndipo mtu mzima
unaweza
kuumbuka.Watanzania tuna
vivutio vingi katika nchi yetu
lakini hatuvijui.Kwa bahati
nzuri nilipokuwa naumwa
nilikuwa natazama ile chaneli
ya utalii ya taifa na
nikabahatika kuvifahamu
baadhi ya vivutio vya
utalii.Ngoja nimshushie huyu
gaidi wana pesa za kuharibu
hawa” akawaza Gosu Gosu
“Ukicha vivutio
nilivyokueleza
vinavyopatikana hapa
Arusha,vivutio vingine ni
mlima Kilimanjaro,mbuga za
Serengeti,Mikumi,Ruaha,Buri
gi n.k” akanyamaza kidogo
akikumbuka
“Vile vile kuna
Saadan,Gombe,Mahare, na
vivutio vingine vingi” akasema
Gosu Gosu
“Nashukuru kwa ufafanuzi
huo.Muda ukiruhusu
nitatembelea vivutio hivyo
vyote bila kuacha hata kimoja”
“Karibu sana” akasema
Gosu Gosu na tayari
walikwisha ingia katika jiji la
Arusha ambako maisha
yaliendelea kama kawaida na
hakukuwa na dalili zozote za
vurugu ila ulinzi ulikuwa
mkali sana.
“Hili ndilo jiji la Arusha”
akasema Gosu Gosu lakini
Nawal hakumjibu kitu
aliyaelekeza macho yake nje.
Walikwenda hadi katika
ofisi za SNSA zilizoko eneo la
Njiro.Gosu Gosu akaagana na
wafanyakazi wa SNSA walioko
Arusha kisha akamuongoza
Nawal wakaelekea katika
helkopta tayari kwa safari ya
kuelekea Dar es salaam
“Tunaelekea Dar es
salaam” Gosu Gosu
akamwambia Nawal
Baada ya dakika chache
helkopta ikapaa na kuondoka
Arusha
“Ni gharama kiasi gani
imetumika kukodisha helkopta
hii?Nataka nijue
nizirejeshe,sitaki kuwaingiza
gharama” akasema Nawal
“Usijali Nawal” akasema
Gosu Gosu.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 4
Inakaribia saa mbili za
usiku helkopta ya idara ya
SNSA ilipotua katika ofisi kuu
za SNSA Dar es salaam.
“Tumefika Dar es salaam
karibu sana” Gosu Gosu
akamwambia Nawal baada ya
helkopta kutua
“Hapa ni wapi?akauliza
Nawal akionekana kuwa na
wasi wasi baada ya kuwaona
watu kadhaa wakiwa na
bunduki wakizunguka kulinda
jengo lile.Gosu Gosu
hakumjibu kitu akampigia
simu Ruby akamjulisha
kwamba tayari wamekwisha
rejea,Ruby akatoka haraka
akawafuata.
“Hallo Nawal karibu sana
Tanzania.Naitwa Ruby”
akasema Ruby
“Nimefurahi kuonana
nawe Ruby” akajibu Nawal
wakapeana mikono kisha Ruby
akamuomba Gosu Gosu
waongee pembeni
“Tuna kikao na Rais usiku
huu hivyo huyu Nawal
tutamuacha hapa akilindwa ili
tukazungumze kwanza na
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby
“Hapana Ruby.Huyu mtu
ametoka kwa mfadhili wa
magaidi duniani.Ni mtu hatari
huyu kumuacha peke
yake.Kitendo cha kumpokea
mtu kama huyu ni cha hatari
sana kwetu hivyo nashauri
wewe nenda ikulu kazungumze
na Rais mimi nitampeleka
Nawal nyumbani
kwangu.Nitamchunga hadi
pale utakapomaliza kikao na
Rais halafu utanikuta
nyumbani ninakusubiri.”
akasema Gosu Gosu
“Umemueleza chochote
kuhusu sisi na shughuli zetu?
Ruby akauliza
“Hapana sijamueleza
chochote ingawa amekwisha
anza kuwa na wasi wasi baada
ya kuona watu wenye silaha
wakizunguka zunguka humu
ndani”
“Sawa Gosu
Gosu.Hakikisha
unamchunga.Nitakapomaliza
kikao na Rais nitakuja
nyumbani kwako” akasema
Ruby
“Kuna chochote
mmekipata kutoka kwa wale
magaidi?akauliza Gosu Gosu
“Hapana hatujapata kitu
chochote mpaka
sasa.Wameendelea kuwa
wagumu kufungunguka lakini
naamini watafunguka tu”
akasema Ruby.Gosu Gosu
akataka kusema kitu lakini
Ruby akamuwahi
“Not now Gosu
Gosu.Tutazungumza baadae”
akasema Ruby kisha
akamfuata Nawal
“Nawal karibu sana Dar es
salaam,karibu sana Tanzania”
“Ahsante Ruby”
“Gosu Gosu atakupeleka
mahala ukapumzike mimi
nitakuja kukuona baadae
kidogo” akasema Ruby na
kuagana na Nawal.Mabegi ya
Nawal yakapakiwa katika gari
la Gosu Gosu ambalo
lilitanguliwa na gari la walinzi
wa SNSA wakaondoka
kuelekea nyumbani kwa Gosu
Gosu.
“Ruby anafanya kazi
gani?Pale tulipomkuta ni
wapi?akauliza Nawal
“Ruby ni mfanya biashara
na mimi ni mfanyakazi
wake.Pale alipo ni moja ya
ofisi zake” akadanganya Gosu
Gosu
“Nimeona watu wana
silaha kali za kivita wakilinda
eneo lile” akasema Nawal
“Kuna watu wamepewa
hifadhi pale kufuatia vurugu
hivyo wanalindwa na vikosi
vya ulinzi ndiyo maana
umeona kuna watu wana
silaha.Wale walio katika gari la
mbele yetu ni askari
wanatusindikiza kuhakikisha
tunafika salama nyumbani”
akaendelea kudanganya Gosu
Gosu na Nawal akawa kimya
Jiji la Dar es salaam usiku
huu lilikuwa kimya.Karibu
maeneo yote waliyopita akina
Gosu Gosu yalikuwa tulivu
hakukuwa na vurugu kama zile
zilizokuwepo siku kadhaa
nyuma.Walifika nyumbani kwa
Gosu Gosu ambako tayari
walinzi wake walikwisha pewa
taarifa na Lucy aliyepigiwa
simu na Gosu Gosu
akimtaarifu kwamba
anakwenda na mgeni.Gosu
Gosu akaagana na wale walinzi
waliowasindikiza kisha
wakaingia ndani.Kulikuwa giza
Gosu Gosu akaelekeza jenereta
liwashwe mara moja
“Nawal karibu sana.Hapa
ni katika makazi yangu na
katika muda wote ambao
utakuwa hapa Tanzania utaishi
hapa” akasema Gosu Gosu
“Ruby anaishi wapi?
Nawal akauliza
“Anaishi mbali na
hapa.Atakuja baadae baada ya
kumaliza kazi zake.Kwa sasa
nenda kaoge kisha upate
chakula na umsubiri Ruby”
akasema Gosu Gosu na
kumpeleka Nawal katika
chumba cha wageni.
“Ruby tayari tumefika
salama” Gosu Gosu
akamjulisha Ruby
“Sawa Gosu Gosu endelea
kumchunga.Ninakaribia kufika
Ikulu.Kama nilivyokwambia
nikitoka huku nitakuja.Kuna
chochote amekuuliza?akauliza
Ruby
“Aliuliza unafanya kazi
gani na pale ulikuwa wapi
nikamwambia wewe ni mfanya
biashara na pale ulikuwa
katika ofisi yako” akasema
Gosu Gosu na kumweleza
Ruby kila kitu
walichozungumza na Nawal
Nawal alikikagua kile
chumba alichopewa ili
kujiridhisha usalama wake
halafu akaufunga mlango na
funguo akazima taa akatoa
kifaa fulani kidogo akakiwasha
kwa lengo la kuangalia kama
kuna kamera au kifaa
chochote cha siri kimetegwa
ndani ya kile chumba lakini
hakubaini kamera au kifaa
chochote.Akawasha taa na
kuingia bafuni kuoga.
“Nimefurahi kufika
Tanzania nchi anakotoka
Mathew Mulumbi.Nimependa
zaidi Arusha kuna hali ya hewa
safi sana na hata madhari yake
ni ya kuvutia
mno.Ningetamani kama
ningeweza kuonana na
Mathew Mulumbi.Nitamuuliza
Ruby kama anaweza
akafahamu mahala alipo
Mathew ili nionane naye
nimfahamishe kile nilichokuja
kukifanya hapa
Tanzania.Lazima nihakikishe
kwa namna yoyote ile mpango
wa kusambaza kirusi hapa
Tanzania haufanikiwi.Mathew
ni mtu wangu wa karibu sana
na lazima nimsaidie kuiweka
nchi yake salama” akawaza
Nawal akiendelea kuoga
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 5
“Ruby karibu sana”
akasema Dr Fabian baada ya
Ruby kuwasili ikulu
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu
Ruby
“Gosu Gosu yuko wapi?
“Gosu Gosu nimempangia
kazi nyingine ndiyo maana
nimekuja peke yangu”
“Watu wako wote pale
SNSA wako salama? Akauliza
Dr Fabian
“Tunashukuru wote wako
salama kabisa”
“Nafurahi kusikia hivyo”
akasema Dr Fabian na ukimya
mfupi ukapita
“Nilitaka tukutane ili
unipe ripoti ya kile ambacho
mmekuwa mnaendelea
kukichunguza ndani ya SNSA
lakini kabla ya yote nataka
kufahamu kuhusu Mathew
Mulumbi.Huyu ni mtu wako
wa karibu.Je ulifahamu
kuhusu uwepo wake hapa
Tanzania? Nilikuuliza swali
hili asubuhi kwenye simu
lakini nataka kukuuliza ana
kwa ana”akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo ambalo sikutaka
kulizungumza simuni lakini
kwa kuwa tumeonana ana kwa
ana nitakueleza ila nitaomba
libaki kwako na asifahamu
mtu mwingine yeyote”
“Nieleze tafadhali”
akasema Dr Fabian
akionekana kuwa na shauku ya
kutakakufahamu jambo hilo
“Ni kweli Mathew
Mulumbi alikuwepo hapa
nchini” akasema Ruby na
ukimya ukapita
“Ni kweli alikuwepo hapa
nchini ndiyo maana akalipua
ubalozi wa Marekani lakini je
wewe ulifahamu kama yuko
hapa nchini? Hilo ndilo swali
langu” akasema Dr Fabian
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Alinitafuta na tukaonana”
akajibu Ruby na Rais
akamkazia macho
“Kuna chochote
alikwambia kuhusiana na hiki
alichokifanya?
“Hapana mheshimiwa
Rais hakunieleza kuhusiana na
hiki alichokifanya.Hata mimi
nilistuka sana baada ya kusikia
kwamba ndiye aliyelipua
ubalozi wa Marekani hapa Dar
es salaam”
“Nimesikitishwa sana
Ruby kwa hiki alichokifanya
Mathew.Nimejiuliza maswali
mengi kwa nini aamue
kujiunga na kundi la
kigaidi?Hata hivyo sishangai
sana kwani toka nilipopata
taarifa zake na hata
nilipoonana naye ana kwa ana
sikuwahi kumuamini.Kibaya
zaidi amebadili hadi jina
anaitwa sijui jina gani lile”
“Abu Zalawi” akasema
Ruby
“Ndiyo.Anajiita hivyo.Nani
amemroga Yule jamaa hadi
akafanya maamuzi haya
mabaya ya kujiunga na IS?
Akauliza Dr Fabian
“Tena imekuwa vyema
amebadili jina na uraia wake
na hajulikani kama ni raia wa
Tanzania kwani angetutia aibu
kubwa endapo angejulikana ni
raia wa
Tanzania.Nimemchukia sana
Yule jamaa na ninaomba
afungwe hata maisha huko
gerezani au auawe kabisa !
akasema kwa ukali Dr Fabian
na Ruby akaonekana
kuchukizwa na kauli ile ya Dr
Fabian
“Samahani Ruby hili suala
la Mathew limenikasirisha
sana hadi nikasahau kama
tuna mazungumzo
muhimu.Ulisema kuna jambo
la muhimu unataka kunieleza”
“Ndiyo mheshimiwa Rais
lakini linahusiana na huyo
Mathew”
“Jambo gani hilo?
“Alipofika hapa nchini
alinitafuta na lengo kubwa la
kunitafuta kwake ni kunipa
taarifa muhimu” akasema
Ruby na kumtazama Rais
aliyekuwa akimsikiliza huku
sura yake ameikunja kwa
hasira
“Mathew alinipa taarifa za
watu waliomuua mufti wa
Tanzania na akanielekeza
mahala wanakoishi”
“Aliwafahamu watu
waliomuua mufti wa Tanzania!
DR Fabian akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa Rais
anawajua na alinielekeza
mahala wanakoishi”
“Ulimuamini hicho
alichokwambia? Akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninamuamini na tuliifanyia
kazi taarifa yake”
“Ruby usiniambie baada
ya haya yote aliyoyafanya bado
unamuamini Yule jamaa !
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais.Ni
kweli Mathew anashirikiana na
kundi la kigaidi la IS na katika
mazungumzo yetu alikiri hilo
lakini aliniambia ana sababu
maalum ya kushirikiana na
kundi hilo la IS.”
“And you believe
him?akauliza Dr Fabian kwa
ukali
“Yes I do Mr President !
akajibu Ruby kwa sauti ya juu
kidogo
“Ruby siamini kama haya
maneno yanatoka katika
kinywa chako.Unawezaje
kumuamini Yule jamaa wakati
ni gaidi?Zaidi ya watu sabini
wameuawa na idadi inaweza
kuongezeka.Unawezaje
kumuamini huyu muuaji
mkubwa? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninamfahamu Mathew
Mulumbi na nimelazimika
kuamini kile
alichoniambia.Alinipa taarifa
muhimu kwamba IS wako
hapa nchini na ndiyo
wanaendesha mashambulio
mbali mbali ya kuua viongozi
wa dini na kuchochea
vurugu.Alituelekeza mahala
wanakoishi magaidi hao na
tukafanya operesheni ya
kuvamia makazi yao kwa
kuwatumia makomando
tukafanikiwa
kuwakamata.Katika upekuzi
wa makazi yao tuligundua vitu
kadhaa ikiwemo mabaki ya
vifaa vya kutengenezea
bomu.Tunahisi yawezekana
bomu lililotumika kulipua
ubalozi wa Marekani
lilitengenezwa hapo” akasema
Rub na kumtazama Dr Fabian
halafu akaendelea
“Tuliwakamata watu wote
waliokutwa hapo na
tunaendelea kuwahoji.Kuna
mtu ambaye Mathew
alituelekeza tumtafute anaitwa
Assad Ismail ambaye ni
kiongozi wao.Tukimpata huyo
tutafahamu mengi kuhusiana
na hizi vurugu
zinazoendelea.Mheshimiwa
Rais hiki kinachoendelea hivi
sasa kina sababu zake na
ningeomba utupe muda zaidi
wa kuendelea kulichunguza
jambo hili nina uhakika siku si
nyingi tukafanikiwa kujua kiini
cha hizi vurugu.Kama
tukifanikiwa kumpata huyo
Assad Ismal tutamuhoji kujua
nani aliyemtuma afanye
mauaji ya viongozi wa dini na
kuchochea vurugu ?
Mheshimiwa Rais tunaelekea
kuzuri katika uchunguzi wetu”
akasema Ruby
“Ruby umeniweka njia
panda sijui nishike
lipi.Nashangaa kwa Mathew
ambaye amejiunga na magaidi
kuwapa taarifa ambazo
zitawaweka wenzake katika
hatari.Hili haliingii akilini hata
kidogo.Iweje awauze wenzake?
Akauliza Dr Fabian
“Ni kwa sababu Mathew si
gaidi” akajibu Ruby
“Huo ni iongo Ruby.Kama
asingekuwa gaidi asingefanya
shambulio lile baya na kuua
watu.Hakuna sababu yoyote ya
kumtetea mtu huyu ni gaidi na
muuaji!! Akasea Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais, ni
kweli Mathew anashirikiana na
magaidi lakini ni kwa sababu
ya misheni maalum ya siri”
“Alikueleza ni operesheni
ipi hiyo ya siri? Dr Fabian
akauliza
“Hakunieleza lakini …”
“Hakuna lakini
Ruby.Kama hakukueleza basi
ni mwongo.Mathew Mulumbi
amekuwa mnyama na ………”
“Mheshimiwa Rais
nakubali umuite Mathew
majina yote mabaya kwa hili
alilolifanya lakini ningeomba
unisikilize mimi ambaye
ninamfahamu Mathew vizuri
kuliko wewe ! akasema Ruby
kwa sauti ya juu kidogo halafu
wakatazama kwa muda Ruby
akaendelea
“Ninamuamini Mathew na
ninaamini hiki alichokifanya ni
kwa sababu maalum.Hata siku
moja Mathew hawezi
akashirikiana na magaidi
kama hana sababu ya kufanya
hivyo.Tukiweka pembeni
hilo,ni yeye ambaye ametupa
mwanga kuhusiana na hiki
kinachoendelea hapa
nchini.Tulikuwa tumekwama
hatujui tuanzie wapi lakini ni
yeye ambaye ametusaidia na
sasa ninaweza kusema tuna
sehemu ya kuanzia kufahamu
chanzo cha vurugu zilizotokea
hapa nchini” akasema Ruby.Dr
Fabian akamtazama kwa muda
na kusema
“He lied to you ! akasema
Dr Fabian kwa ukali
“Amekudanganya nawe
ukakubali.Anacheza na akili
zenu Yule jamaa na hakuna
chochote cha maana.Kama
kweli watu hao aliowaelekeza
ni magaidi kuna chochote
mmekwisha kipata hadi sasa
kutoka kwao?
“Bado tunaendelea
kuwahoji mheshimiwa Rais
lakini taarifa aliyotupa
Mathew ni ya kweli kabisa na
haina mashaka hata
kidogo.Mheshimiwa Rais
nakuomba uweke akiba ya
maneno kwa sasa kwani
baadae jambo hili
litakapokuwa limefika mwisho
usijilaumu kwa maneno
yako”akasema Ruby
“Usinifundishe nini cha
kuzungumza Ruby.Ni aibu
sana kwa mtu mkubwa kama
wewe kuchezewa akili yako na
mtu kama huyu asiye na hata
chembe ya utu !
“Mheshimiwa Rais
naomba uniamini na uamini
kazi inayofanywa na idara
yangu.Nakuhakikishia
tutaupata mzizi wa hizi
vurugu.Tayari tumekwishapata
mwanga” akasema Ruby na Dr
Fabian akacheka kidogo
“Mwanga ulioonyeshwa na
gaidi? Katu hiyo si taarifa ya
kuamini na sina hakika kama
kweli hao mliowakamata ni
magaidi” akasema DrFabian
“Mheshimiwa Rais
uliniamini na kunipa idara ya
SNSA niiongoze.Sintaweza
kufanya kazi yangu kikamilifu
kama
hautaniamini.Mheshimiwa
Rais kama hauna tena imani
nami kwamba kwa
kushirikiana na wenzangu
tunaweza kulishughulikia
suala hili la vurugu zilizotokea,
naomba uteue mtu mwingine
ambaye unadhani anaweza
akaongoza vyema idara ya
SNSA kama unavyotaka.Mimi
niko tayarikuacha kazi muda
huu huu ! akasema Ruby
akionekana kukasirika
“Ruby huu si wakati wa
kufikiria mambo kama
hayo.Taifa liko kwenye wakati
mgumu mno.Sitaki kusikia
tena ukizungumza au hata
kufikiria kitu kama hicho cha
kuacha kazi.Ninakuamini
ndiyo maana nilikutoa
Uingereza nikakuleta hapa
kufanya kazi hii”
“Kama ni hivyo
mheshimiwa Rais naomba
utuamini mimi na
wenzangu.Nakuhakikishia
mheshimiwa Rais si muda
mrefu kutoka sasa kuna
mambo mengi yatajulikana
kuhusiana na hiki
kinachoendelea.Naomba
uniamini na utupe nafasi”
akasema Ruby na baadaya
muda Dr Fabian akauliza
“Ukiacha hao jamaa
mliowakamata mkidai ni
magaidi kuna mpango gani
mwingine mnao wa
kutuwezesha kufahamu chanzo
cha hizi vurugu?Wale watu
mnaowatafuta mnaohisi wana
mahusiano na hizi vurugu
mmefikia wapi kujua mahala
walipo? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
mpango tunaoendelea nao ni
kuwahoji wale magaidi
tuliowakamata ili tupate
taarifa za mahala alipo Assad
Ismail ambaye anaweza
akatupa maelezo ya kutosha
kuhusiana na hizi vurugu
kwani ni wao wanaoendesha
mauaji ya viongozi wa dini”
“Mathew Mulumbi again”
akasema Dr Fabian kwa sauti
ndogo
“Ruby nenda kaendelee na
mipango yenu
sintawaingilia.Kama kuna
chochote mtakipata ambacho
unadhani ninapaswa
kukifahamu utanijulisha”
akasema Dr Fabian
“Nashukuru mheshimiwa
Rais nitafanya hivyo” akajibu
Ruby huku akinyanyuka
akaagana na Rais akaondoka
“Sina imani tena na
SNSA.Hakuna chochote
tunachoweza kukipata kutoka
kwao kama tayari
wanaongozwa na akili ya
Mathew Mulumbi.Ningeweza
kumtoa Ruby na kumuweka
mtu mwingine lakini nilimtoa
Uingereza aje aongoze idara
hii na amepitia mambo mengi
mazito hadi kufika hapa ngoja
nimpe muda nione muelekeo
wake.Ameniudhi mno leo kwa
namna alivyomtetea Mathew
Mulumbi eti kitendo
alichokifaya cha kulipua
ubalozi wa Marekani ni moja
ya operesheni zake.Stupid !
akawaza Dr Fabian akiwa na
hasira
VICTORIA – SEYCHELLES
Boti aliyopanda Mathew
Mulumbi iliwasili katika pwani
ya jiji la Victoria nchini Sheli
Sheli.Bado Mathew alikuwa
amevishwa mfuko kichwani
hivyo hakufahamu walikuwa
wapi.Alishushwa kutoka katika
ile boti na kuingizwa garini
milango ikafungwa magari
yakaondoka.Baada ya mwendo
wa takribani dakika ishirini
gari alilopanda Mathew
likapunguza mwendo halafu
likasimama.Milango
ikafunguliwa akashushwa
ndani ya gari akaingizwa
katika nyumba,akahisi kama
vile wanashuka ngazi kuelekea
chini.Akasikia mlango
ukifunguliwa akaingizwa ndani
ya chumba halafu mlango
ukafungwa na watu wote
wakatoka kukawa
kimya.Chumba kilikuwa na
giza nene.
Zilipita dakika kama kumi
hivi mlango ukafunguliwa
tena,taa ikawashwa halafu
Mathew akavuliwa ule mfuko
kichwani.Mtu mmoja
akamsogelea Mathew
akachuchumaa na kumfungua
pingu za miguu na mikono
akamtaka Mathew amfuate
wakaingia katika chumba
kimoja ambamo waliwakuta
watu wanne wakipata chakula.
“Karibu Abu Zalawi”
akasema Yule jamaa
aliyekwenda kumfungua na
Mathew akaketi kitini na
kujumuika na wale jamaa
katika chakula,alihisi njaa
kali.Hakuwa ameweka
chochote tumboni toka
asubuhi.Walikula kimya kimya
bila mazungumzo na baada ya
kumaliza kula mazungumzo
yakaanza
“Abu Zalawi pole sana kwa
safari ndefu”
“Ahsante nashukuru”
akajibu Mathew
“Naitwa Jeffrey,wenzangu
ni Richard,William,Brian,na
Christopher” akasema Jefrey
akiwatambulisha wenzake kwa
Mathew
“Tumepewa maelekezo
maalum na viongozi wetu ya
kuhakikisha misheni yako
inakamilika lakini hapo hapo
jambo hili lisionekane kama ni
tukio la kutengenezwa ndiyo
maana utaona ilitumika nguvu
kidogo wakati wa kukukamata
ili tukio lionekane ni halisi”
akasema Jeffrey na kunyamaza
kidogo
“Muda mfupi ujao
tutakufanyia mahojiano
ambayo yatafuatiliwa moja
kwa moja na makao yetu
makuu Langley.Baada ya
mahojiano hayo tutakupeleka
katika chumba cha mateso ili
kukutesa ufunguke na hapo
utatusamehe kwani tutatumia
nguvu ili ionekane ni jambo la
kweli.Tutafanya namna ili
upoteze fahamu halafu
tutakupeleka katika chumba
walimo wale wanasayansi wa
Iran na utaanza kujenga
ukaribu nao” akasema Jeffrey
na kumuelekeza Mathew
namna mahojiano yao
yatakavyokuwa maswali
atakayoulizwa na majibu
anayotakiwa kuyatoa.Baada ya
mazungumzo yale Mathew
Mulumbi akarejeshwa katika
kile chumba na kufungwa
pingu akavishwa mfuko
kichwani.
Zilipita dakika kadhaa taa
yeye mwanga mkali ikawaka
mle ndani halafu mlango
ukafunguliwa wakaingia watu
wanne mle ndani.Mathew
akainuliwa na kutolewa
akapelekwa katika chumba
kingine akafungwa mikono
katika pingu za mezani halafu
ikawashwa taa yenye
mwangaza mkali na ule mfuko
aliofunikwa kichwani
ukatolewa.Ndani ya chumba
kulikuwa na watu wapatao
nane wakiwamo wale ambao
alikula nao chakula muda
mfupi uliopita.Kulikuwa pia na
kamera imeelekezwa upande
wake.Mbele yake alikaa Jeffrey
akivuta sigara.
“Unafahamu hapa uko
wapi?akauliza Jeffrey
“Nitafahamu vipi wakati
mmenifunika na mfuko
kichwani muda wote? akajibu
Mathew
“Usijali uatafahamu
tu.Hapa ni moja ya sehemu
wanakoletwa watu kama wewe
kwa ajili ya kufanyiwa
mahojiano.Naomba nikuweke
wazi kwamba hapa ni mahala
panapoogopwa mno na mtu
yeyote aliyewahi kupita
mahala hapa ukimwambia
kwamba unataka kumrejesha
hapa ataongea kila lugha
anayoifahamu ili asiweze
kuletwa hapa.Taarifa nyingine
ya mahala hapa ni kwamba
wote waliowahi kuletwa hapa
wote walifunguka na kutoa
ushirikiano.Nikupe mifano ya
watu waliowahi kupita
hapa.Hasan Izz Al
Din,Abdelkarim Hussein Al
Nasser,Jaber Elbaneh,Ali Saed
Bin Ali El Hoorie, na wengine
wengi.Hawa wote ni magaidi
wakubwa na walihusika katika
matukio mbali mbali ya kigaidi
na kuua wamarekani.Wote
walipofika hapa walifunguka
na kutaja mtandao wao
wote.Wapo vile vile ambao
walifikishwa hapa na
hawakutoka hai na wapo
ambao kwa miaka mingi
wameendelea kushikiliwa
sehemu hii kwa kushindwa
kutoa ushirikiano.Hakuna
yeyote kati ya watu wako
anayeweza kukusaidia ukiwa
hapa hivyo ni jukumu lako
kujisaidia wewe mwenyewe”
akasema Jeffrey na kuwasha
sigara nyingine.
“Anza kwa kututajia jina
lako na umetokea wapi”
akasema Jeffrey.Mathew
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Naitwa Abu Zalawi,raia
wa Saudi Arabia” akasema
Mathew na kunyamaza
akawatazama wale watu mle
ndani
“Abu Zalawi unafahamu ni
kwa nini uko hapa? Akauliza
Jeffrey lakini kabla Mathew
hajajibu akaingia mtu
mwingine akamnong’oneza
Jeffrey kitu sikioni
“Jibu Abu Zalawi
unafahamu kwa nini uko
hapa?Jeffrey akauliza
“Nimelipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam”
akajibu Mathew
“Abu Zalawi nataka
utufahamishe umewahi
kushiriki katika matukio
mangapi ya kigaidi kabla ya
hili la Dar es salaam? Akauliza
Jeffrey
“Mengi” akajibu Mathew
“Unaweza kuyataja?Jeffrey
akauliza
“Nilimuua mkuu wa
Mossad Afrika
Mashariki,nimeshirikiana na
kundi la wanamgambo la
Ammar Nazar Brigades
kufanya mashambulio kadhaa
ndani ya Israel” akajibu
Mathew bila woga
“Sababu gani ilikupelekea
ukalipua ubalozi wetu Dar es
salaam? Akauliza Jeffrey.Sura
ya Mathew ikabadilika na
akaonyesha hasira
“Ni kwa sababu ya
dhuluma na ukandamizaji
kunakofanywa na Marekani
kwa nchi za kiislamu.Marekani
ina chuki dhidi ya uislamu na
ndiyo maana kila uchao
imekuwa ikizikandamiza nchi
za kiislamu na
waislamu.Mfano ni nchi ya
Iran imekuwa inawekewa
vikwazo chungu nzima na
Marekani na kama haitoshi
bado wana mpango wa
kuishambulia kijeshi.Hiki
nilichokifanya ni kuionya
Marekani kwamba waislamu
tutasimama imara kutetea dini
yetu dhidi ya ukandamizwaji
wowote ule ! Hiki kilichotokea
Tanzania kitaendelea sehemu
nyingine mbali mbali duniani
hadi pale nchi yenu
itakapoacha unyanyasaji kwa
waislamu na nchi zao !
akasema Mathew kwa
ukali.Huku akitabasamu
Jeffrey akasema
“Abu Zalawi umejinadi
kwamba ulichokifanya ni kwa
ajili ya kupigania haki za
wasilamu wanaonyanyaswa na
Marekani lakini Marekani
hainyanyasi waislamu na
jambo lingine ni kwamba
Uislamu hauamini katika
ugaidi.Katika shambulio lile
umeua pia waislamu.Hivyo
ndivyo kitabu kitukufu
kinaelekeza kuua watu wasio
na hatia yoyote hata waislamu
wenzako? Akauliza Jeffrey
“Vyovyote mjuavyo ninyi
lakini fahamuni mapambano
haya yataendelea sehemu
mbali mbali duniani ! akasema
Mathew
“Abu Zalawi shambulio lile
ulilolifanya limeua watu zaidi
ya sabini na miongoni mwao ni
wanawake na watoto wapo
waislamu wenzako pia
waliokuwa wamepewa hifadhi
katika ubalozi wetu wakiamini
ni sehemu salama na hii
inaonyesha wazi kwamba
hatuchukii uislamu na
waislam.Damu ya watu hao
wote inakulilia wewe.Wengi
wa watu uliowaua ni waafrika
wenzako na huwezi kujua
yeawezekana katika
mkusanyiko ule wapo pia
ndugu zako.Nafsi yako
haikusuti kwa hiki
ulichokifanya? Akauliza
Jeffrey na Mathew
akawakumbuka wale watoto
aliowakuta ndani ya gari
lililobebab bomu
“Masikini wale watoto
bado wadogo sana sijui kama
walisalimika” akawaza
“Abu Zalawi ukimya huo
unaonyesha wazi kwamba hata
wewe nafsi yako inakusuta kwa
hiki ulichokifanya.Hata
nikiitazama sura yako
haionyeshi ukatili na hii
inanipa picha kwamba
umefanya kitendo hiki bila
ridhaa yako.Nataka utuambie
nani waliokutuma ukafanye
shambulio lile?Nani viongozi
wako? Abu Zalawi tunataka
kuzuia mashambulio ya kigaidi
yasiendelee kutokea na kuua
watu wasio na hatia na wewe
nayo nafasi kubwa kabisa ya
kusaidia hilo
liwezekane.Tuambie nani
waliokutuma ukafanye
shambulio lile? Akauliza
Jeffrey.Mathew akawatazama
kisha akasema
“Tayari nimetimiza kazi
yangu niliyotakiwa kuifanya
hapa duniani hivyo sioni
sababu ya kuendelea kupoteza
muda wenu kunihoji kutafuta
taarifa ambazo hamtaweza
kuzipata. Nipelekeni huko
mnakowapeleka mashujaa
kama mimi mkanitese
mtakavyo na hata ikiwezakana
nichomeni sindano ya sumu
nife kabisa siogopi chochote na
niko tayari kufa hata sasa
kwani naamini kwa
nilichokifanya ninangojewa
kwa hamu peponi ! akasema
Mathew.Jeffrey akamtazama
na kusema
“Abu Zalawi katika
matamshi yako uliitaja nchi ya
Iran kwamba inaonewa na
Marekani.Kuna nchi nyingi za
kiislamu kwa nini ukachagua
kuitaja Iran? Kwa nini isiwe
Iraq,Syria au nchi yoyote
nyingine?akauliza Jeffrey
“Iran ni mfano wa nchi
inayochukiwa na
kukandamizwa na Marekani
lakini zipo nyingi” akajibu
Mathew
“Ulitumwa na serikali ya
Iran kufanya shambulio lile?
akauliza Jeffrey
“Mnapoteza muda wenu
bure hapa na kunichelewesha
kuiona pepo.Niueni haraka
kwani hamtaweza kupata kitu
chochote kutoka kwangu”
akasema Mathew
“Nilikuelekeza hapo awali
kwamba ukiingia mahala hapa
utake usitake lazima
utafunguka lakini wewe naona
bado hujapafahamu vizuri
mahala hapa.Nitakuchukua na
kukutembeza mahala hapa
upafahamu vizuri halafu
tutakuja tena kuzungumza
baadae” akasema Jeffrey na
kuelekeza Mathew afunguliwa
pingu
“Twende tukatembee rafiki
yangu.Usiwe na hofu” akasema
Jeffery kisha akatoka mle
ndani akiwa na Mathew
Walitembea katika
vyumba kadhaa vya jumba lile
huku Jeffrey akimpa Mathew
maelezo na mara wakaingia
katika chumba kimoja
kikubwa chenye vifaa kama
chumba cha mazoezi.
“Abu Zalawi hapa
tutafanya mazoezi kidogo
lakini hautafanya na mimi”
akasema Jeffrey na kugonga
ukuta mlango miwili
ikafunguka wakatokea watu
sita.Ilikuwa ni mijitu ya
miraba minne na yenye sura za
kuogofya
“Hawa ndio utakaofanya
nao mazoezi” akasema Jeffrey
na kuwageukia wale jamaa
“Nimewaleteeni mgeni
anahitaji mazoezi kidogo ili
achangamke” akasema Jeffrey
na kumsukuma Mathew
akaangukia katika mikono ya
mmoja wa wale jamaa
akamdaka na kumuinua juu
juu kisha akamrusha kwa
mwenzake akamdaka na
kumtandika ngumi nzito
ambayo ilimfanya Mathew
aone nyota akapepesuka na
kupigwa teke akajikuta katika
mikono ya mwingine ambaye
alimtandika ngumi akanguka
chini.Akainuliwa na mwingine
akamtandika ngumi Mathew
akaenda chini.Alikuwa
anapigwa kwa zamu.Ndani ya
muda mfupi hakuwa
akitazamaika.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliwasili nyumbani
kwa Gosu Gosu akitokea ikulu
alikokuwa na mazungumzo na
Rais.Alipokewa na Gosu Gosu
wakaelekea katika chumba cha
mapumziko
“Mgeni yuko wapi?
Akauliza Ruby
“Yuko chumbani kwake
anapumzika”
“Umezungumza naye
chochote?
“Hapana Ruby
sijazungumza naye
chochote.Uliniambia
nisimuulize chochote hadi
utakapofika wewe mwenyewe”
akasema Gosu Gosu
“Good.Umekuwa naye
toka Arusha unaweza
ukamuelezeaje? Akauliza Ruby
“Hatukuwa na
mazungumzo mengi lakini kwa
haraka haraka anaonekana ni
mjanja na mwenye kuchukua
tahadhari na vile vile hapendi
kuchunguzwa .Nadhani
utakapozungumza naye
tutafahamu mambo mengi
kuhusu yeye.Vipi uko utokako?
“Huko mambo
hayakwenda vizuri na
Rais.Mazungumzo
yalitawaliwa na mtu mmoja tu
Mathew Mulumbi.Rais
alikuwa mbogo akitoa
matamshi makali kumuhusu
Mathew.Nilijaribu kumdokeza
Rais kwa kifupi kuhusu kile
tunachoendelea nacho hivi
sasa ndani ya SNSA
nikamdokeza kwamba
mafanikio haya yote hadi
tukafanikiwa kuwafahamu na
kuwapata magaidi
wanaoendesha matukio ya
mauaji hapa nchini ni kwa
sababu ya Mathew Mulumbi
lakini hatukuelewana pale
nilipomwambia kwamba
Mathew yuko katika misheni
maalum na kile alichokifanya
ni mojawapo ya misheni
hiyo.Kwa ujumla maongezi
yetu hayakwenda vizuri
kufuatia suala hili la
Mathew.Rais ametoa maneno
mengi ya dharau kwetu ilifika
wakati nilitaka kuachana na
kazi hii” akasema Ruby
“Usijali Ruby.Haya yote
Mathew aliyafahamu ndiyo
maana akatutahadharisha
mapema.Sisi tunaoelewa
kinachoendelea tuendelee
kusimama naye.Tuendelee
kupambana kuhakikisha nchi
inakuwa shwari na
tunawafahamu wale wote
waliochochea vurugu hizi”
akasema Gosu Gosu
“Twende tuka zungumze
na Nawal” akasema Ruby na
Gosu Gosu akamuongoza
wakaenda katika chumba
alimo Nawal akagonga na
Nawal akafungua mlango
akawakaribisha ndani.Nawal
alimtazama Ruby kwa jicho
ambalo Ruby alilielewa.Nawal
alikuwa anamtaka Gosu Gosu
atoke mle ndani.
“Usihofu Nawal tunaweza
kuendelea Gosu Gosu
akiwepo” akaema Ruby
“Karibu Tanzania.Pole kwa
safari “
“Ahsante.Poleni na nyie
kwa yanayoendelea hapa
Tanzania”
“Tunashukuru Mungu
mpaka sasa tu wazima”
akasema Ruby na ukimya
mfupi ukapita kisha akasema
“Nawal nadhani ni wakati
sasa wa kuzungumza
kuhusiana na kile kilichokuleta
hapa Tanzania.Mama yako
Habiba Jawad aliponipigia
simu aliniomba nikusaidie
kufika Dar es salaam na vile
vile katika kile kilichokuleta
hapa Tanzania.Tayari
nimekusaidia umeweza kufika
salama Dar es salaam na sasa
ninataka kufahamu kuhusu
kile ambacho umekuja
kukifanya hapa Tanzania”
akasema Ruby
“Kwanza kabisa
nawashukuruni sana Ruby na
Gasu Gasu”
“Gosu Gosu” akasema
Ruby na kumrekebisha Nawal
“Jina gumu linanisumbua
kutamka hata hivyo
ninawashukuruni sana kwa
kuniwezesha kufika salama
Dar es salaam.Kama
ningekuwa mwenyewe
ingeniwia ugumu kuingia Dar
es salaam haraka na kwa
urahisi namna hii.Ahsanteni
na ningeomba nipewe
gharama zilizotumika
kunifuata kule Arusha ili
nizirejeshe” akasema Nawal
“Usijali Nawal.Wewe ni
mgeni wetu hivyo lazima
tuhakikishe tunakuhudumia
kwa kila kitu kama mama yako
alivyompokea na kumtunza
Mathew Mulumbi” akasema
Ruby
“Anaendeleaje Mathew
Mulumbi?akauliza Nawal
“Mathew hatujui kwa sasa
anaendeleaje.Kwani si mko
wote Saudi Arabia? Ruby
akauliza
“Mathew yuko hapa
Tanzania.Hamjaonana bado?
Akauliza Nawal .Ruby na Gosu
Gosu wakatazamana
“Ina maana hajui Mathew
alichokuja kukifanya hapa
Tanzania? Gosu Gosu na nawal
wakaongea kwa Kiswahili na
Nawal hakuelewa chochote
kwani hakuifahamu lugha ya
Kiswahili.
“Twende naye taratibu
tutafahamu kila kitu” akajibu
Ruby
“Ndugu zangu kitu
kikubwa cha kwanza ambacho
nataka mnisaidie ni kuonana
na Mathew Mulumbi.Tafadhali
sana nisaidieni kwa hilo”
akasema Nawal
“Nawal utatusamehe
kwani kwa sasa hatufahamu
mahala aliko Mathew
Mulumbi” akasema Nawal
“Mathew yuko hapa Dar es
salaam.Hamjaonana
naye?Mnafahamu makazi yake
yalipo? Akauliza Nawal
“Nawal tafadhali usitake
kutuchanganya akili zetu.Ina
maana huna taarifa za
alichokifanya Mathew?
Akauliza Gosu Gosu huku
akimtazama Nawal kwa macho
makali
“Gosu Gosu.! Taratibu”
akasema Ruby
“Ruby ni kweli ninahitaji
mno kuonana na Mathew
Mulumbi kabla ya mambo
yote.Kama bado hamjaonana
naye Mathew yuko hapa
Tanzania.Nipelekeni katika
makazi yake yawezekana
akawa huko” akasema Nawal
“Nawal hapa tulipo ndipo
makazi ya Mathew Mulumbi
ila anayeishi hapa kwa sasa ni
Gosu Gosu na sisi tote hapa ni
kama nyumbani kwetu kwani
Mathew ni mtu wetu wa
karibu sana”akasema Ruby
“Ina maana Mathew
hajawasiliana nanyi alipokuja
hapaTanzania? Akauliza
Nawal
“Hapana hajawasiliana
nasi na hatukujua kama
Mathew yuko hapa Dar es
salaam”
“Mathew aliiandika namba
yako katika kitabu chake cha
kumbu kumbu na kwa kuwa ni
namba yako pekee
iliyoandikwa humo tuliamini
wewe ni mtu wake wa muhimu
sana ndiyo maana tutakutafuta
tukijua kwamba unaweza
ukanielekeza mahala alipo
Mathew” akasemaNawal
“Nilipigiwa simu na mtu
aliyejitambulisha anaitwa
Najma ambaye ni mke wa Abu
Zalawi ambaye baadae
niligundua ndiye Mathew
Mulumbi akaniambia kwamba
Mathew alikuwa ananitafuta
simuni.Nimeshangaa
unaponiambia kwamba
Mathew alikuwepo hapa
Tanzania”
“Ni kweli Ruby.Mathew
Mulumbi amekuja Tanzania”
“Amekuja kufanya
nini?Kwa nini amekuja kwa
siri?Hapa ni nyumbani kwake
kwa nini hajakanyaga kama
amefika Tanzania? Ruby
akauliza
“Sifahamu amekuja
kufanya nini lakini najua
amekuja Tanzania”
“Kwa nini unasisitiza sana
kutaka kuonana na Mathew
Mulumbi? Akauliza Gosu Gosu
“Kuna taarifa muhimu
nataka kumpatia”
“Taarifa ipi?
“Ni kuhusu mke wake
Najma.Alijiua kwa kujipiga
risasi baada ya Mathew
kuondoka na hafahamu
chochote juu ya jambo hilo”
“Nini kilisababisha Najma
akajiua?Ruby akauliza
“Inadaiwa ni wivu.Alihisi
labda Mathew ana mwanamke
mwingine na ndiyo maana
Mathew alipoondoka tu Najma
akabaki akajiua” akasema
Nawal
“Anafahamika kama Abu
Zalawi.Wewe umefahamuje
anaitwa Mathew Mulumbi?
akauliza Gosu Gosu
“Niliambiwa hivyo na
mama kwamba jina halisi la
Abu Zalawi ni Mathew
Mulumbi na anatokea
Tanzania ambako
hawalifahamu jina la Abu
Zalawi”akajibu Nawal
“Hapa naona tunacheza
mchezo wa kitoto.Tunapoteza
muda bila sababu ya msingi”
akasema Gosu Gosu kwa
hasira na kuinuka
“Gosu Gosu nini unataka
kukifanya?akauliza Ruby
“Ruby hatuwezi kuendelea
na mchezo huu wa
kipuuzi.Huyu mwanamke
asitufanye sisi wajinga”
akasema Gosu Gosu
“Sikiliza Nawal Mathew
Mulumbi amelipua ubalozi wa
Marekani hapa Dar es salaam
usiku wa kuamkia leo na
asubuhi ya leo amekamatwa
jijini Nairobi na makachero wa
CIA akitafua usafiri wa kumtoa
nchini Kenya ili akimbilie
Somalia na mpaka sasa hatujui
mahala alipo.Nataka utuambie
ukweli hukufahamu alichokuja
kukifanya Mathew huku
Tanzania?akauliza Gosu Gosu
“Naomba mniamini ndugu
zangu sifahamu chochote
kuhusu jambo hilo.Ni Mathew
kweli aliyefanya hicho kitu au
ni mtu aliyefanana naye?
Mathew katu hawezi kufanya
kitu kama hicho” akasema
Nawal na Gosu Gosu
akamtazama kwa hasira halafu
akasema
“Nawal nitazame vizuri”
akasema Gosu Gosu na Nawal
akamtazama bila hofu.
“Gosu Gosu anataka
kufanya nini?akawaza Ruby
“Nimeishi msituni katika
mapigano makali toka nikiwa
na umri chini ya miaka
kumi.Kabla sijawa na maisha
haya unionayo sasa
nilichokuwa nakifahamu ni
bunduki ,risasi na kuua
tu.Muziki wangu ni milio ya
risasi na mabomu.Kwangu
mimi kutoa roho ya mtu ni
kama kunywa maji.Usinione
hivi mimi ni mkatili mno na
usijaribu kuingia katika anga
zangu utajuta na kumlaumu
mama yako kwa nini alikuleta
duniani” akasema Gosu Gosu
na kunyamaza kidogo
“Nimeanza na utangulizi
huo ili ufahamu umekutana na
watu wa namna gani.Mimi na
mwenzangu Ruby tunafahamu
kila kitu kuhusu ninyi.Mama
yako Habiba Jawad ni mfadhili
mkubwa wa ugaidi
duniani.Ndiye anayekifadhili
kikundi cha IS na makundi
mengine
mbalimbali.Tulifahamu hiki
alichokuja kukifanya Mathew
hapa Tanzania.Tulionana naye
akatueleza alichokuja
kukifanya.Tunataka kufahamu
wewe nini kimekuleta hapa
Tanzania?Kuna shambulio
lingine la kigaidi mnapanga
kulifanya Tanzania?Tueleze
tafadhali muda wa michezo
umeisha ! akasema Gosu
Gosu.Nawal akavuta pumzi
ndefu
“Sikiliza Nawal” akasema
Ruby
“Kwanza kuna kitu
ambacho wewe na hata mama
yako Habiba Jawad
yawezekana hamkifahamu
kuhusu Mathew.Amejiunga
nanyi na anafanya mambo ya
kigaidi lakini Mathew si gaidi
ni jasusi.Pili ni kuhusu
sisi.Mimi na huyu mwenzangu
Gosu Gosu ni wakurugenzi wa
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi ijulikanyo kama
SNSA.Jukumu letu ni
kuhakikisha nchi inakuwa
salama.Tunafahamu wewe
umetoka katika familia ya
kigaidi na umekuja hapa
Tanzania kwa malengo hayo ya
kufanya ugaidi.Nawal kwa
ufupi tu nataka ufahamu
kwamba umeingia katika
mkono wa serikali na
tutakuchukua kwa ajili ya
mahojiano hivyo nakushauri
tueleze kile kilichokuleta hapa
Tanzania.Huna sababu ya
kutuficha kitu kwani
tunafahamu kila kitu kuhusu
Habiba Jawad.Tuanzie hapo
Nawal nini umekuja kukifanya
hapa Tanzania? Akauliza
Ruby.Nawal
akatabasamu.Gosu Gosu
akaonekana kukasirishwa na
kitendo kile cha Nawal
kutabasamu alipoulizwa
swali,akasimama
“Tunachokifanya hapa ni
mzaha?akauliza Gosu Gosu
Ruby akawahi kumshika
mikono kwani tayari mkono
wa kulia ulianza kuinuka
“Jizuie GosuGosu !
akasema Ruby
‘Msinielewe vibaya ndugu
zangu.Nimetabasamu baada ya
kugundua kwamba nimefika
mahala nilipopahitaji mno”
akasema Nawal.Ruby na Gosu
Gosu wakatazamana
“Hatujakuelewa Nawal
unamaanisha nini unaposema
umefika mahala ulipopahitaji?
Akauliza Ruby
“Chloe Bennet.Ndilo jina
langu halisi” akasema Nawal
na kuwasimulia akina Ruby
historia yake hadi alivyofikia
kuolewa na Ammar Nazar.
“Oh my God ! Ama kweli
dunia hii imejaa siri.Kumbe
huyu mwanamke naye ni
jasusi dah ! Gosu Gosu
akashangaa
“Nikiwa kwa Ammar
Nazari ndipo nilipokutana na
Mathew ambaye kwa wakati
huo alikuwa anatumiwa na
Mossad kwa lengo la kumsaka
Habiba Jawad akifahamika
kama Abu Zalawi.Nilijenga
naye mazoea na baada ya
kufahamiana vizuri
nikamfahamisha kuwa mimi
pia ni jasusi na nilikuwa pale
katika misheni maalum”
akasema Nawal na
kuwasimulia akina Ruby
kuhusiana na safari ya Mathew
hadi alipofika pale kwa Ammar
Nazari na kujiunga na kikundi
kile cha wanamgambo.Ruby
alilengwa na machozi baada ya
kuelezwa mambo aliyoyapitia
Mathew
“Sikujua kama Mathew
ameteseka namna hii” akawaza
Ruby
“Israel walifahamu
maficho ya Ammar
wakayashambulia lakini kwa
bahati nzuri mimi na Mathew
tulifanikiwa kutoroka na hapo
ndipo tulipoanza kumsaka
Habiba Jawad.Haikuwa kazi
rahisi kumfikia Habiba”
akasema Nawal na
kuwasimulia akina Ruby safari
ngumu waliyopitia hadi
kumfikia Habiba Jawad.
“Baada ya kufika kwa
Habiba misheni ya kumuua
ikabadilika na tukajikuta
tukiungana naye.Mimi
niliolewa na mwanae anaitwa
Abu Dahir na Mathew
akamuoa mtoto mwingine wa
Habiba anaitwa Najma
ambaye ndiye alikupigia simu
kukuuliza kama unamfahamu
Abu Zalawi” akasema Nawal
“Kitu gani kiliwapelekea
mkabadili misheni mliyokuwa
nayo ya kumuua Habiba
wakati mkifahamu fika ni
mfadhili mkuu wa ugaidi?
Akauliza Gosu Gosu
“Tulipofika kwa Habiba
kwanza tayari alikuwa
anatufahamu sisi ni akina
nani.Kupitia vyanzo vyake
aliweza kufahamu sisi ni
majasusi na lengo letu lilikuwa
ni kumuua.Alitueleza bila
kutuficha kwamba tulikuwa
pale kwa ajili ya kumuua na
akatutaka tusiendelee na
mipango yetu kwani ana
malengo mazuri na sisi na
ndipo misheni ilipobadilika
tukajikuta tukiingia katika
familia yake.Kwa ufupi tu
Habiba Jawad ni tofauti na
watu wanavyomfikiria.Baada
ya kuwa naye karibu tumepata
bahati ya kumfahamu vizuri na
yawezekana msinielewe lakini
ni mtu wa tofauti na wengi
wamjuavyo” akasema Nawal
na sura ya Gosu Gosu
ikaonekana kubadilika
“Mtu wa
tofauti?Anafadhili makundi ya
kigaidi na kuua watu halafu
unatuambia ni mtu wa tofauti?
Habiba ni muuaji mkubwa
kwani bila yeye makundi haya
ya kigaidi yasingeendelea
kuwepo na kustawi ! akasema
Gosu Gosu
“Usemayo ni kweli Gosu
Gosu lakini nina sababu ya
kusema kwamba Habiba ni
mtu wa tofauti na wengi
mnavyomdhania.Niwape
mfano mdogo.Miezi kadhaa
iliyopita mtu mmoja
aliyefahamika kama James
Kasai akishirikiana na kundi la
IS walifanya mauaji makubwa
hapa Tanzania ambapo wake
kadhaa za marais waliuawa.Ni
Habiba Jawad aliyemuwezesha
Mathew kumpata na kumuua
James Kasai.Mnalifahamu
hilo? Akauliza Nawal.Gosu
Gosu na Ruby wakatazamana.
“Naamini hamkuwa
mkilifahamu hilo.Huo ni
mfano mdogo tu kuhusu
Habiba Jawad.Bila yeye
Mathew asingeweza
kufanikisha kumpata James
Kasai” akasema Nawal
“Sasa nimepata picha
kamili.Wakati wa operesheni
ile ya kumsaka James
Kasai,Mathew alikuwa
anazungumza na mtu simuni
kila usiku na kila walipomaliza
mazungumzo yao alikuwa
anakuja na taarifa
mpya.Kumbe alikuwa
anazungumza na Habiba
Jawad.Nadhani ndiyo maana
alinikataza nisimfuatilie ili
nsigundue kama alikuwa na
mashirikiano na Habiba
Jawad” akawaza Ruby
“Habiba Jawad” Nawal
akaendelea
“Anatumika tu kufadhili
makundi ya kigaidi lakini wapo
wahusika wakuu wa ufadhili
huo nyuma yake” akasema
Nawal na kuwapa maelezo
marefu akina Ruby kuhusiana
na idara ile ndogo ndani ya
CIA ambayo ni maalum kwa
mashirikiano na makundi ya
kigaidi lakini akina Ruby
hawakuonekana kushangaa
sana
“Usiku wa kuamkia jana
tulionana na Mathew na
akatueleza kuhusiana na hiyo
idara na mahusiano yake na
hiki kinachoendelea hapa
nchini kwa sasa na akatusaidia
pia kutuelekeza mahala walipo
magaidi wa IS ambao
wanatumiwa kuchochea
vurugu ambao tumewakamata
tunaendelea kuwahoji.Katika
mazungumzo yetu alikwepa
sana kutueleza kuhusiana na
kile alichokuja kukifanya hapa
Tanzania ambacho ni kulipua
ubalozi wa Marekani hadi leo
asubuhi ilipotangazwa
kwamba amekamatwa jijini
Nairobi akituhumiwa kuwa
ndiye aliyelipua ubalozi ule.
Nataka kufahamu ni misheni
gani aliyonayo Mathew hadi
akalipua ubalozi ule wa
Marekani? Akauliza Ruby
Nawal akawaeleza kwa
kina kuhusiana na misheni
ambayo Mathew anaendelea
nayo iliyompelekea alipue
ubalozi wa Marekani.Gosu
Gosu na Ruby wakabaki
vinywa wazi.
“Oh Mungu wangu ! Kwa
nini Habiba akamuhusisha
Mathew katika jambo hili? Hii
ni misheni ya hatari sana na
lengo lake ni ili Mathew auawe
kwani uwezekano wa kumaliza
salama misheni hii ni mdogo”
akasema Ruby
“Nakubaliana nawe Ruby
kwamba misheni hii ni ngumu
na ya hatari kubwa sana
yawezekana ni misheni ngumu
kuliko zote alizowahi kupitia
Mathew na Habiba
analifahamu hilo lakini ilikuwa
lazima Mathew aifanye”
akasema Nawal na kuwaeleza
akina Ruby umuhimu wa
misheni ile anayokwenda
kuifanya Mathew.
“Naamini mmeona
umuhimu wa Mathew
kushiriki katika misheni hii”
akasema Nawal na Ruby
akatikisa kichwa
“Japo ni misheni ya
muhimu sana hasa kwa nchi
yetu na dunia kwa ujumla
lakini ni misheni ya kifo”
akasema Ruby
“Jukumu letu ni
kumuombea ili aweze
kumaliza misheni hiyo akiwa
salama kabisa” akasema Nawal
“Nawal umesema wewe ni
jasusi wa CIA.Unaweza
kuwasiliana na wenzako na
kufahamu mahala alipo
Mathew hivi sasa? Nataka
kujua kama bado yuko Nairobi
ili tufanye mipango ya
kumuokoa kwani misheni hii
ni mbaya mno na tunaweza
kumpoteza” akasema Gosu
Gosu
“Nikurekebishe Gosu Gosu
kwa sasa siko tena
CIA.Nilipoamua kuolewa na
Abu Dahir ulikuwa ni mwisho
wangu na CIA na mpaka sasa
hawajui niko wapi hivyo sina
mawasiliano na watu wa
CIA.Jambo lingine hata kama
ningekuwa bado CIA
nisingeweza kufahamu mahala
alipo Mathew kwa kuwa ni
misheni ya siri kubwa.Tatu
hata kama tungefahamu
mahala alipo hatuwezi kwenda
kumuokoa Mathew kwani yeye
mwenyewe ametaka kuifanya
misheni hii kwa kuelewa
umuhimu wake.Nawashauri
ndugu zangu kitu kikubwa kwa
sasa ni kuendelea kumuombea
tu Mathew ili akamilishe
misheni hii akiwa
salama.Binafsi nina uhakika
kwamba atamaliza na atakuwa
salama.Nawaomba na ninyi
muwe na uhakika huo.Msiwe
wepesi kuamini kwamba
Mathew ni gaidi.Ameingizwa
katika ugaidi kwa malengo
maalum lakini ukweli utabaki
pale pale kwamba Mathew ni
jasusi na hata siku moja
hawezi kuwa
gaidi.Tumeelewana katika
hilo?akauliza Nawal
“Hata yeye mwenyewe
alitueleza hivyo kwamba
tusiamini kile tutakachokisikia
juu yake.Tunamfahamu
Mathew,tumekuwa naye muda
mrefu na
tunamuamini”akasema Ruby
“Vizuri.Huo ni upande
mmoja wa Mathew Mulumbi
ambaye anaendelea na
misheni yake” akasema Nawal
na kunyamaza kidogo
“Watu hawa ambao
wanaichezea dunia watakavyo
bado wana uchu na rasilimali
za Afrika.Ndugu zangu mimi ni
mmarekani lakini nina damu
ya Afrika.Baba yangu asili yake
ni Libya hivyo japokuwa
nimechanganya damu lakini
mimi bado ni mwenzenu mimi
ni mtoto wa Afrika na
dhumuni la kuja hapa ni
kuwasaidia ndugu zangu”
akasema Nawal.Ruby na Gosu
Gosu wakatazamana
wakatabasamu
“Karibu Afrika Ruby bara
lililojaa utajiri lakini likiongoza
kwa umasikini mkubwa kwa
sababu ya kunyonywa na hayo
mataifa makubwa.Madini
yanasombwa tunabaki na
mashimo makubwa,rasilimali
za misitu zinavunwa na utajiri
mwingine mwingi
unachukukuliwa na sisi
tunachoambulia ni misaada
kidogo,mikopo yenye masharti
magumu na silaha ambazo
tunazimia kuuana wenyewe
kwa wenyewe.Libya nchi
alikotoka baba yako amani
imetoweka.Kumekuwa na
mapigano kila
uchwao.Kinachoendelea Libya
kiko sehemu nyingi ya
Afrika.Mapigano ya wenyewe
kwa wenyewe na mingi ya
migogoro hiyo inasababishwa
na wanasiasa wanaogombea
madaraka.Viongozi hawataki
kung’oka madarakani na
mambo mengine mengi.Hiyo
ndiyo Afrika.Lakini mengi ya
haya niliyokueleza
ukichunguza chanzo chake ni
mataifa makubwa” akasema
Gosu Gosu
“Uko sahihi Gosu Gosu.
Mataifa makubwa yamekuwa
ni chanzo cha migogoro mingi
inayoendelea barani
Afrika.Nchi za kiafrika
hazikupaswa kuwa na
umasikini mkubwa kama
uliopo sasa” akasema Nawal
na Gosu Gosu akaingilia kati
“Tazama nchi kama
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo ni nchi yenye utajiri
mkubwa wa madini na
rasilimali nyingine lakini
imekuwa ni nchi masikini
kutokana na migogoro
isiyokwisha.Kila uchao
makundi ya waasi
yanaibuka.Ukijiuliza
yanatokea wapi? Wanatoa
wapi silaha ? Utapata jibu
kwamba kuna nguvu kubwa
kutoka nje ya Afrika” akasema
Gosu Gosu
“Mfano mwingine ni haya
machafuko yaliyotokea hapa
Tanzania na
Uganda.Yametengenezwa kwa
kusudi maalum.Wakati ninyi
mkigombana wao wanapata
nafasi ya kujipenyeza na
kuchukua kile wanachokihitaji
na sasa wanayabeba mafuta ya
Uganda mapipa kwa mapipa
bila kujali damu ya watu
inayoendelea kumwagika.Huu
ni ukatili mkubwa na aibu kwa
nchi kubwa kama Marekani na
ndiyo maana niko hapa”
akasema Nawal na kunyamaza
kidogo
“Baada ya mpango wao wa
kupata mafuta kufanikiwa sasa
wamenogewa na wanataka
kwenda mbali zaidi ya
mafuta.Wanataka kuingia
katika rasilimali nyingine
kama vile madini na mazao ya
misitu.Ili kulifanikisha hilo
lazima vikosi vya Marekani
vilivyopo hapa Tanzania
viendelee kuwepo kwa muda
mrefu na ikiwezekana
viongezwe zaidi hivyo basi
wameamua kuja na mpango
mwingine na safari hii
wanataka kuja kusambaza
kirusi hatari kitakacholeta
maangamizi makubwa”
akasema Nawal
“Kirusi?! Akauliza Ruby
kwa mshangao
“Ndiyo wanataka
kusambaza kirusi hatari
ambacho kiko kwenye
maandalizi hivi sasa”Nawal
akawaeleza kwa kina
kuhusiana na mkakati ule wa
kusambaza kirusi nchini
Tanzania halafu akainuka
akaenda katika sanduku lake
akalifungua na kutoa faili dogo
akatoa picha akampatia Ruby
“Anaitwa Sattar Sayf Al
Din” Akasema Nawal.Ruby
akazitazama picha zile halafu
akampa Gosu Gosu naye
akazitazama
“Ni nani huyu
mtu?akauliza Gosu Gosu
“Huyu anatokea kundi la
IS na ndiye anayekuja
kusambaza kirusi hicho hapa
Tanzania.Hivi sasa tayari yuko
Marekani akiandaliwa kwa
kazi hiyo” akasema Nawal.
“Hiyo ndiyo misheni
iliyonileta hapa
Tanzania.Nimekuja
kuhakikisha kwamba mpango
huo haufanikiwi na Tanzani
ainaendelea kuwa sehemu
salama.Kwa mara nyingine
tena ni Habiba Jawad ambaye
amenituma nije kutekeleza
mpango huu kwa siri.Nadhani
sasa mtaweza kuona ni kwa
nini hata Mathew aliamua
kushirikiana na huyu
mama.Hayakuwa maamuzi
rahisi kuamua kushirikiana
mtu ambaye kwa muda mrefu
tumekuwa tukiamini ni
mfadhili mkuu wa ugaidi
duniani”`
“Kwa nini Habiba anauma
na kupuliza? Akauliza Gosu
Gosu
“Nimekwisha waambia
sababu ya Habiba kufanya hivi
anavyofanya ni kwamba
anataka kukimaliza kikundi
kile kidogo ndani ya CIA
ambao wanasababisha haya
yote kutokea.Watu hao wasio
na huruma hata chembe ndio
ambao Mathew Mulmbi
amechagua kupita njia ngumu
yenye mateso makali ili
kuwafikia na kuwamaliza.Kwa
hili nathubutu kumuita Habiba
Jawad ni shujaa kwani
angeweza kuacha wakaendelea
na mipango yao na watu wengi
wakapoteza maisha lakini
amekataa kuendelea kuwa
mtumwa wa hawa watu,hataki
tena kuendelea kufadhili
mauaji ya watu wasio na hatia
na ndiyo maana anatutumia
mimi na Mathew
Mulumbi.Ndugu zangu
ninataka tushirikiane katika
hili.Peke yangu sintaweza”
akasema Nawal.Ruby
akamgeukia Gosu Gosu
“Gosu Gosu
unasemaje?Unamuamini huyu
mtu? akauliza Ruby kwa
Kiswahili
“Ruby nadhani
tungejadiliana kwanza
pembeni kabla ya kumpa jibu”
akasema Gosu Gosu
wakamtaka radhi Nawal
wakatoka mle ndani wakaenda
kusimama katika varanda.
“Umemsikiliza vyema
maelezo
yake.Umemuamini?akauliza
Ruby
“Kwa maelezo aliyoyatoa
kuna kitu kinaniambia
nimuamini japo lazima tuwe
na tahadhari sana
tunaposhirikiana na watu
kama hawa ambao wametoka
katika mzizi wa ugaidi”
akasema GosuGosu
“Nini ushauri
wako?Tushirikiane naye
au?akauliza
Ruby.Walijadiliana kwa muda
wa dakika kama tano hivi
kisha wakakubaliana
kushirikiana na Nawal halafu
wakarejea ndani
“Nawal tumekubaliana
kushirikiana nawe.Kama
nilivyokueleza awali kwamba
sisi ni viongozi wa idara
inayoshughulika kwa siri na
usalama wa ndani wa
nchi.Tunazo rasilimali za
kutosha kutuwezesha
kutekeleza hicho ulichokuja
kukifanya.Tunataka kujua je
huyu mtu anayeleta kirusi
anakuja lini?Anafikia wapi?
Tukifahamu hayo itakuwa
rahisi kwetu kufanya
maandalizi” akasema Ruby
“Kwa sasa bado sina
taarifa zozote lakini nategemea
kupata taarifa kutoka kwa
Habiba Jawad.Yeye anafuatilia
kila kinachoendelea kuhusiana
na mpango huo wa
kukisambaza kirusi.Kitu cha
kanza ninachohitaji ni kupata
mawasiliano ili niwasiliane na
Habiba Jawad” akasema
Nawal
“Mawasiliano
utapata.Lakini tungetaka
kufahamu kuhusu huyo mtu
anayekuja kusambaza kirusi
anakuja kwa kutumia njia
gani?Atakuja lini? Akauliza
Ruby
“Kama nilivyosema
kwamba ninategemea kupata
taarifa zote kutoka kwa Habiba
Jawad.Hatua ya kwanza
ilikuwa ni mimi kufika Dar es
salaam halafu nitawasiliana
naye na atanipa
maelekezo.Nisaidieni niweze
kuwasiliana naye na kama
tayari anazo taarifa
atanijulisha” akasema
Nawal.Ruby akampa Nawal
simu yake ili awasiliane na
Habiba Jawad.Nawal
akafungua sanduku lake
akatoa kijitabu kidogo
akaandika namba za Habiba
katika simu akapiga simu
ikaanza kuita baada ya muda
ikapokelewa
“Hallo”akasema Habiba
“Mama Habiba ni mimi
Nawal”
“Ouh Nawal.Nimefurahi
kusikia sauti yako.Tayari
umefika Tanzania? Akauliza
Habiba
“Ndiyo mama.Tayari
nimekwisha fika Tanzania na
tayari nimefika Dar es salaam
na tayari nimeonana na
Ruby”akasema Nawal
“Nafurahi kusikia hivyo
Nawal.Hautaweza kuonana na
Mathew kwani tayari
amekwisha anza misheni
yake.Jana usiku alilipua
ubalozi wa Marekani na leo
amekamatwa jijini Nairobi
hivyo kwa sasa mpango ule wa
kumpeleka Iran
unaendelea”akasema Habiba
“Tayari nimekwisha zipata
taarifa hizo mama.Imekuwa
bahati nzuri kwangu kwani
Ruby ni mkurugenzi wa SNSA
idara ya usalama wa ndani ya
nchi hivyo tutasaidiana katika
hilo zoezi”
“Ouh kweli ! Habiba
akashanga
“Ndiyo mama”
“Vizuri sana .Basi
saidianeni kuhakikisha
kwamba mnaokoa raia wa
Tanzania na dunia kwa ujumla
kwani kirusi hicho endapo
kikisambazwa basi kinaweza
kuvuka mipaka ya Tanzania na
kusambaa hadi sehemu
nyingine za dunia”
“Sisi hapa tuko
tayari.Kuna taarifa zozote
umezipata tayari kuhusiana na
Sattar Sayf Al Din?akauliza
Nawal
“Taarifa nilizo zipata ni
kuwa kirusi kinachotarajiwa
kuja kusambazwa Tanzania
kiko tayari lakini tatizo lililopo
ni kwamba wanasayansi bado
hawaja pata kinga
yake.Mpango ulikuwa kabla ya
kusambaza kirusi hicho lazima
iwe imepatikana kinga yake ili
kuwakinga wanajeshi wa
Marekani walioko Tanzania na
vile vile kuwakinga
wamarekani endapo kirusi
hicho kitavuka mipaka ya
Tanzania”
“Kwa hiyo
wameahirisha?akauliza Nawal
“Hapana
hawajaahirisha.Mpango uko
pale pale.Kwa mujibu wa
taarifa nilizozipata ni kwamba
kwa sasa vurugu zinaonekana
kupungua na hii imewapa hofu
hivyo wameamua kukisambaza
kirusi hicho hivyo hivyo bila
kinga yake kuwa tayari”
akasema Habiba
“Dah ! akasema Nawal
“Nawal kwa namna yoyote
ile hakikisha kirusi hiki
hakisambai Tanzania au katika
ardhi ya Afrika.Watu wengi
watakufa kwani hakina kinga
bado”
“Nakuhakikishia mama
kwamba kirusi hicho
hakitasambazwa hapa
Tanzania.Mipango yao ikoje?
Sattar Sayf Al Din anakuja lini
Tanzania? Akauliza Nawal
“Bado sijajua anakuja lini
lakini kwa taarifa nilizozipata
ni kwamba atakapofika
Tanzania Sattar atapokelewa
na mtu anaitwa Assad
Ismail.Huyu anaishi Mombasa
Kenya lakini nimetaarifiwa
kwamba kwa sasa yuko hapo
Tanzania na ndiye
atakayemsaidia Sattar katika
zoezi hilo la kusambaza hicho
kirusi.Ili kuweza kumpata
Sattar lazima umpate kwanza
Assad”akasema Habiba
“Umesema anaitwa Assad
Ismail?akauliza Nawal
“Ndiyo Assad Ismail”
akajibu Habiba na Nawal
akamgeukia Ruby
“Andika katika karatasi
Assad Ismail” akasema Nawal
“Huyu Assad nitampata
vipi hapa Dar es
salaam?Anaishi wapi?akauliza
Nawal
“Bado sijapata taarifa
kamili za mahala alipo lakini
hadi kufikia kesho mchana
nitakuwa nimejua wapi
unaweza ukampata”
“Mama ahsante kwa
taarifa hizi nitazifanyia kazi
kwa kushirikiana na wenzangu
niliowakuta hapa” akasema
Nawal
“Sawa Nawal.Naomba uwe
makini sana unapolishghulikia
jambo hili kwani ni mpango
wa siri wa taifa kubwa hivyo
lazima watakuwa wamechukua
kila aina ya tahadhari
kuhakikisha mpango wao huo
haukutani na vikwazo vya aina
yoyote.Nawal katika misheni
hii hakuna kitu kushindwa
umenielewa? Akasema Habiba
“Nimekuelewa mama”
akasema Nawal na kuagana na
Habiba.Nawal akawaeleza kile
alichoelezwa na Habiba
“Huyu Assad Ismail
Mathew alikwisha tupa taarifa
zake na tayari tumeanza
kumsaka.Huyu ndiye ambaye
amekuwa mchochezi mkuu wa
vurugu zinazoendelea.Kwa
kushirikiana na wenzake
wamekuwa wakiendesha
mauaji ya viongozi wa dini kwa
lengo la kuwafarakanisha
waumini wa dini
kushambuliana.Tayari tunao
watu wanaoshirikiana na
Assad unaendelewa
kuwahoji”akasema Ruby
“Mmekwisha pata taarifa
zozote za mahala alipo
Assad?akauliza Nawal
“Hapana.Tumewahoji
watu wale na mpaka sasa bado
hatujapata
chochote.Wamekuwa wagumu
sana kusema chochote.Kuna
mtu anaitwa Marwan ambaye
Mathew alituelekeza kwamba
ndiye anafahamu mahala alipo
Assad.Tayari
tumempata.Tumemfanyia
mahojiano lakini bado
hajafunguka” akasema Ruby
nawal akashusha pumzi na
kusema
“Nimeishi na magaidi kwa
miaka kadhaa ninawafahamu
vyema.Naweza kusema
kwamba tayari wameharibiwa
akili zao na wako tayari kufa
muda wowote.Kupata taarifa
kwa hawa watu si jambo la
mchezo inahitaji kutumika
nguvu kubwa.Kuwahoji
magaidi si sawa na kuwahoji
wahalifu wengine wa
kawaida.Magaidi ni watu
wanyama sana na
unapowahoji unapaswa nawe
uwe kama wao nadhani
mmenielewa ndugu zangu ”
akasema Nawal na Gosu Gosu
akamtazama Ruby
“Ruby nafahamu mimi si
mtanzania na wala si mtu wa
idara yenu lakini ni
mwenzenu.Nina ombi moja
kwako”akasema Nawal
“Omba Nawal”
“Ninataka kumuhoji huyo
Marwan ambaye Mathew
alielekeza kwamba ndiye
anayefahamu mahala alipo
Assad” akasema Nawal sura ya
Ruby ikaonyesha
kutokukubaliana na wazo la
Nawal
“Nawal yuko
sawa.Nilikwambia jambo hili
toka awali Ruby.Watu hawa
wanapaswa kuhojiwa tofauti
na watu wengine.Tupe nafasi
mimi na Nawal tuwahoji tena
wale jamaa.Nina uhakika kuna
kitu tutakipata kutoka kwao”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu sipendi
namna ulivyomfanyia
Marwan.Si…..”
“Ruby hii ni vita.Kila
mbinu lazima itumike kupata
taarifa.Tafadhali kwa mara ya
kwanza Ruby fumba macho
kuwa na moyo wa jiwe.Ruhusu
nguvu itumike kuwahoji hawa
magaidi ili tuweze kumpata
Assad ambaye lazima tumpate
kwa gharama yoyote” akasema
Gosu Gosu.
“Gosu Gosu kanuni za
idara haziruhusu matumizi ya
nguvu katika kuwahoji
watu.Ulichokifanya ni
kinyume na kanuni
zetu.Lazima tufuate maelekezo
yaliyotolewa katika kufanya
mahojiano na kupata taarifa
kutoka kwa watu tunaowahoji”
“C’mon Ruby.Huu si
wakati wa kufuata hizo kanuni
ambazo hazitoi
matokeo.Tazama kwa kufuata
kanuni hizo hizo mpaka leo hii
hakuna tulichokipata kutoka
kwa wale magaidi ! akasema
Gosu Gosu kwa sauti ya juu
kidogo
“Gosu Gosu mimi ndiye
kiongozi wa idara na ndiye
mwenye maamzi ya mwisho
hivyo siwezi kuruhusu
matumizi ya nguvu kubwa
kama ulivyofanya kwa
Marwan.Sikufurahi hata
kidogo kwa kile ulichokifanya !
Ruby naye akajibu kwa sauti
ya juu
“Kuna nini ndugu
zangu?akauliza Nawal baada
ya kuona Gosu Gosu na Ruby
wakibishana kwa kutumia
kiswahili
“Hakuna tatizo” akajibu
Gosu Gosu
“Kama hakuna tatizo
nadhani mmenielewa ombi
langu la kutaka niwahoji hawa
jamaa mliowakamata kwa
maelekezo ya Mathew.Si kazi
nyepesi kupata taarifa kutoka
kwa magaidi kama
nilivyowaeleza na wakati
mwingine inalazimu kutumia
nguvu kubwa”akasema Nawal
“Hapo ndipo kuna tatizo
Nawal.Idara yangu hairuhusu
matumizi makubwa ya nguvu
katika kuwahoji watu
tunaowashikilia”akasema
Ruby na Nawal akamtazama
kwa macho ya mshangao
“Ruby ni kweli hapo kuna
tatizo.Tazama” akasema Nawal
“Mimi si mtanzania lakini
nimekuja hapa kuwasaidia
watanzania na janga kubwa
linalowakabili.Katika
kulitimiza jukumu langu hilo
sintahitaji vikwazo vya aina
yoyote ile.Kirusi hicho
kikisambaa hapa Tanzania
halitakuwa janga la kwenu
pekee bali la kidunia hivyo
nalazimika kutumia kila njia
kuhakikisha kwamba mpango
huo wa kusambaza kirusi
haufanikiwi.Naomba
tushirikiane Ruby.Nafahamu
kila idara ina kanuni zake
lakini huu si wakati wa kufuata
hizo kanuni.Haya ni
mapambano ya kufa na
kupona.Lazima tuwe na
kanuni zetu wenyewe aidha
gaidi atoe siri au afe ! akasema
Nawal na kwa mbali Gosu
Gosu akatabasamu
“Nimempenda
Nawal.Huyu ndiye anayenifaa
kufanya naye kazi ! akawaza
Gosu Gosu
“Ruby kuna tatizo lolote
katika suala hilo? Akauliza
Nawal
“Hakuna tatizo lakini
itabidi tutafute sehemu
nyingine kwa ajili ya
kuwafanyia mahojiano hao
jamaa.Hatuwezi kutumia ofisi
za SNSA kwa jambo hilo”
“Hakuna tatizo.Tunazo
nyumba tatu kwa ajili ya kazi
hiyo hapa Dar es salaam
tutatumia moja wapo”
akasema Gosu Gosu
Kwa shingo upande Ruby
akiongozana na Nawal na Gosu
Gosu wakaondoka kuelekea
ofisi kuu ya SNSA
VICTORIA – SHELI SHELI
Mathew alianguka chini na
kupoteza fahamu kufuatia
kipigo kikali
alichopewa.Hakuwa
anatazamika usoni, alikuwa
amechafuka damu.Yote haya
yaliyokuwa yanaendelea
yalikuwa yakifuatiliwa na
viongozi wa CIA nchini
Marekani.Baada ya kupoteza
fahamu maelekezo yakatolewa
kwamba wampumzishe hadi
baadae.Mathew akaburuzwa
na kutolewa ndani ya kile
chumba akashushwa chini
zaidi na lango la chumba
kimoja likafunguliwa na
Mathew akarushiwa ndani ya
kile chumba akiwa bado
hajitambui kisha lango
likafungwa.Ndani ya kile
chumba kulikuwa na watu
sita.Watu wale walionekana
wachovu na waliokata
tamaa.Walikuwa na ndevu
nyingi na nguo chafu.Watu
wale sita kila mmoja alikuwa
amelala juu ya godoro dogo na
chumba kilikuwa na
mwangaza hafifu.Pembeni ya
kile chumba kulikuwa na
mlango wa choo na
bafu.Kulikuwa na meza ya
chakula iliyokuwa na viti
sita.Pembeni ya chumba
kulikuwa na meza ya kusomea
yenye viti viwili na juu yake
kulikuwa na vitabu vitatu vya
quran.
Baada ya Mathew kutupwa
mle ndani wote waliinuka
kutoka katika magodoro yao
wakamkazia
macho.Hawakumfahamu ni
nani.Mmoja wa wale jamaa
akainuka na kwenda
kumgeuza akamtazama na
kutikisa kichwa wa masikitiko
kutokana na hali aliyokuwa
nayo.Uso wake ulikuwa
umevimba na kuchafuka damu
“Hawa watu ni wanyama
sana” akasema huku akimvua
Mathew shati alilokuwa
amevaa wale wengine nao
wakainuka wakamfuata
“Ni mzima? Akauliza
mwingine
“Hana fahamu amepigwa
mno”
“Ni nani huyu
mtu?Amefanya nini? Kwa nini
aje aunganishwe nasi?
Mwingine akauliza
“Tumsaidie aweze
kuzinduka halafu atatueleza”
Haraka haraka wakaanza
jitihada za kumsaidia Mathew
aweze kurejewa na fahamu.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby akiwa na Gosu Gosu
na Nawal waliwasili katika
makao makuu ya SNSA
wakashuka garini na kuelekea
ofisini kwa Ruby ambaye
aliwataka Gosu Gosu na Nawal
wabaki mle ofisini yeye
akaelekea katika idara ya afya
kutazama maendeleo ya
Marwan.
“Idara kubwa sana hii na
nyeti kwa nchi.Haipaswi kuwa
na kiongozi mwoga
anayeogopa kufanya maamuzi
magumu” akasema Nawal
baada ya Ruby kutoka mle
ofisini
“Usijali Nawal.Tutapata tu
kile tunachokitafuta” akajibu
Gosu Gosu
“Sifahamu lugha yenu
mnayozungumza lakini wakati
mkizungumza niliona kama
vile Ruby anaonyesha wasi
wasi” akasema Nawal
“Ruby anajaribu
kuzingatia kanuni lakini kwa
hatua hii tuliyofika kanuni
hazina nafasi.Nakubaliana na
ushauri wako kwamba tuwe na
kanuni zetu wenyewe gaidi
aidha aseme ukweli au ateseke
hadi kufa” akasema Gosu Gosu
“Uliniambia kwamba
ulikuwa mwanajeshi? Akauliza
Nawal
“Ndiyo.Nilikuwa
mwanajeshi wa kikundi kimoja
cha waasi waliokuwa
wakipigana vita na serikali ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Nimekaa msituni toka
nikiwa mdogo kabisa
nikipigana vita”
“Ouh kumbe asili yako ni
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo?
“Ndiyo.Lakini kwa sasa ni
raia wa Tanzania” akajibu
Gosu Gosu na mlango
ukafunguliwa akaingia Ruby
“Marwan anaendelea
vizuri.Nimekwisha elekeza
apakiwe katika gari maalum
yeye na wenzake wawili kisha
tutawapeleka katika moja ya
nyumba zetu kwa ajili ya
mahojiano” akasema Ruby
“Ahsante sana Ruby kwa
kukubali kufanya maamuzi
haya magumu” akasema
Nawal.Gosu Gosu akatoka mle
ofisini na kwenda kukusanya
vifaa kwa ajili ya kuwasaidia
katika mahojiano yao na
kuvipakia garini.Marwan na
wengine wawili wakaingizwa
katika gari kisha wakaondoka .
“Gosu Gosu anafurahi kwa
kumpata mwenzake ambaye
anaonekana anapenda
matumizi ya nguvu katika
kutafuta taarifa.Sifurahi hiki
wanachokwenda kukifanya
kwani ni kinyume na kanuni
zetu na hata haki za
binadamu.Si kila wakati njia
ya mateso inakuwa na
manufaa.Watu kama hawa
kuna njia za kuwahoji kwani
tayari wamekwisha haribiwa
kisaikolojia hivyo inabidi
kuanza kwanza kuwarejesha
katika maisha ya kawaida
ndipo hapo unaweza ukapata
kile unachokihitaji kutoka
kwao.Sina hakika kama nguvu
itafanikisa kupata chochote”
akawaza Ruby wakiwa garini.
Iliwachukua dakika
hamsini na mbili kuwasili
katika nyumba ambayo
wangeitumia kuwahoji wale
magaidi.Nyumba ilikuwa giza
na walinzi walikuwa
wamejificha kwa ndani.Ruby
akawapigia simu akawajulisha
kuwa tayari wamefika na geti
likafunguliwa.Marwan na wale
magaidi wenzake wakaingiza
katika chumba wakiwa
wamefungwa vitambaa usoni
na mikono yao ikiwa
imefungwa pingu.Ruby
akaelekeza jenereta liwashwe
na maandalizi yakaanza.Nawal
na Gosu Gosu wakafanya
maandalizi ndani ya chumba
watakachokitumia kuwahoji
wale magaidi na walipokuwa
tayari magaidi wote watatu
wakaletwa ndani ya kile
chumba wakafunguliwa
vitambaa walivyokuwa
wamefungwa usoni .
“Hello Marwan ! akasema
Gosu Gosu baada ya
kukutanisha macho na
Marwan ambaye alionyesha
hofu kubwa
“Tumekutana tena siku ya
leo.Tutaendelea pale
tulipoishia siku ile” akasema
Gosu Gosu na kumuinua
Marwan akampeleka katika
kiti.Ruby hakuwemo ndani ya
kile chumba alikuwa
anafuatilia kinachoendelea
akiwa katika chumba kingine
“Huyu ndiye Marwan”
Gosu Gosu akamwambia
Nawal
“Asalaam alaikum
Marwan” Nawal akamsalimu
Marwan ambaye sura yake
ilionyesha hasira kubwa baada
ya kusalimiwa na Nawal
“Hata kama usipojibu
lakini tutaelewana tu” akasema
Nawal kwa lugha ya
kiarabu.Marwan kwa dharau
kubwa akamtemea mate.Gosu
Gosu aliyekuwa karibu
akainua mkono wake na
kumnasa Marwan kofi zito
“Taratibu Gosu Gosu.Hizi
dharau ni za muda tu
zitakwisha” akasema
Nawal,Gosu Gosu akamuinua
Marwan akamketisha kitini
“Marwan,naomba nianze
kwa kujitambulisha
kwako.Naitwa
Nawal.Nimekuwa katika kundi
la Ammar Nazari brigades
kama mke wa Ammar Nazari
naamini umewahi
kumsikia.Leo hii niko hapa
Tanzania kuzungumza
nawe.Kuna kitu kimoja tu
ambacho nakitaka kutoka
kwako.Wapi alipo Assad
Ismail? Akauliza Nawal kwa
lugha ya kiarabu.Marwan
akamtazama kwa hasira na
kusema
“Shetani wa kike
wewe.Kwa nini umetusaliti
kiasi hicho na kuungana na
hawa viroboto wasio na
thamani yoyote?
Nakuhakikishia utajutia hiki
ulichokifanya ! akasema
Marwan kwa hasira naye
akitumia lugha ya kiarabu
“Marwan ninarudia
tena,ninataka kufahamu
mahala alipo Assad
Ismail”akasema Nawal
“Fanya chochote
ukitakacho lakini siwezi
kukueleza chochote msaliti
mkubwa wewe ! akafoka
Marwan
“Gosu Gosu tuanze kazi
hadi atakapokuwa tayari
kusema ! akasema Nawal.Gosu
Gosu akamuinua Marwan
kutoka kwenye kiti
akampandisha katika kitanda
akamfunga vizuri kwa
mikanda mikononi na miguuni
“Hakuna mateso yoyote
mtakayonitesa
yatakayonipelekea nikafungua
mdomo wangu na kuwapa kile
mkitakacho ! akasema Marwan
“Usimjali Gosu Gosu
atasema tu ! akasema Nawal
kisha Gosu Gosu kwa nguvu
akaupanua mdomo wa
Marwan na Nawal akaingiza
mpira halafu akafungulia maji
na tumbo la Marwan likaanza
kujaa maji.Baada ya muda
akafunga maji na kuuchomoa
ule mpira.Marwan alikuwa
anaweweseka
“Wapi alipo
Assad?akauliza Nawal lakini
Marwan hakujibu.Nawal
akampa ishara Gosu Gosu
ambaye aliuinua mguu wake
wa kulia akaushusha katika
tumbo la Marwan ambaye
aliyatapika yale maji
yaliyokuwa tumboni.
“Tunaanza upya hadi
utakaposema mahala alipo
Assad ! akasema Nawal na
zoezi lile likaendelea
Mara nne tumbo la
Marwan lilijazwa maji na
kutapishwa lakini hakusema
chochote.
“Sijawahi ona mijitu
migumu kama hii ! akasema
Gosu Gosu
“Usichoke Gosu Gosu
atasema tu” akasema Nawal
kisha akaelekeza Marwan
atolewe pale kitandani
wakamfunga katika chuma
maalum kilichotengenezwa
mfano wa goli la mpira wa
miguu.Marwan alining’inizwa
akiwa mtupu .Alikuwa
amechoka mwili wake
haukuwa na nguvu
“Marwan kabla
hatujaendelea na zoezi la pili
nataka utueleze mahala alipo
Assad ! akasema Nawal lakini
Marwan hakufumbua mdomo
wake kusema chochote.Gosu
Gosu akapanga vipande vya
mbao chini ya miguu ya
Marwan akamwagia mafuta
“Mara ya mwisho
Marwan.Wapi alipo
Assad?akauliza Nawal lakini
Marwan aliendelea kutoa
matamshi kwa lugha ya
kiarabu.Nawal akampa ishara
Gosu Gosu akawasha kiberiti
na kutupia katika zile mbao
moto ukalipuka na kufikia
miguu ya Marwan ambaye
alishindwa kuvumilia akaanza
kupiga kelele kubwa kwa
maumivu makali aliyoyapata
baada ya moto kuanza
kuunguza miguu yake.
“Assad yuko wapi?akauliza
Nawal lakini Marwan hakujibu
aliendelea kulia
“Gosu Gosu akalegeza
mnyororo na Marwan
akashuka chini akiukaribia
zaidi moto ambao uliendelea
kuwa mkali.Kilio kikazidi
“Nitasema alipo Assad !
Mmoja wa wale magaidi
waliokuwamo ndani ya kile
chumba akasema baada ya
kuona mateso yale makali
aliyopewa Marwan.Gosu Gosu
akageuka na kumtazama kwa
hasira
“Tafadhali msiendelee
kumtesa Marwan nitawaeleza
kila kitu kuhusiana na mahala
alipo Assad ! akasema Yule
jamaa na Gosu Gosu
akapunguza ule moto.Bado
Marwan aliendelea kupiga
kelele za maumivu na sauti
ilielekea kumkauka
“Haya tueleze haraka alipo
Assad ama nitakupandisha
wewe kukuchoma na moto ule
! akafoka Gosu Gosu
“Nitawaeleza jamani
naomba msiendelee kumtesa
Marwan namna hii ! akasema
Yule jamaa ambaye alionekana
kuwa na umri mdogo tofauti
na wenzake
“Unaitwa nani? Gosu Gosu
akamuuliza
“Naitwa Jabir Hafidh”
akasema Yule jamaa
“Jabir una miaka
mingapi?akauliza GosuGosu
“Nina miaka ishirini na
mbili”
“Ana miaka ishirini na
mbili” GosuGosu akamwambia
Nawal kwani hakuelewa lugha
ya Kiswahili
“Kijana mdogo sana kwa
nini akaingia katika makundi
haya ya kigaidi” akasema
Nawal
“Jabir tueleze alipo Assad
na ninakuonya kama
ukitudanganya basi mateso
utakayoyapata ni makubwa
kuliko haya ya Marwan !
akasema Gosu Gosu
“Nitawaeleza ukweli”
akasema Jabir
“Mimi si mwenyeji wa Dar
es salaam lakini kuna sehemu
inaitwa Sarara.Pale kuna hoteli
moja ambayo bado
haijafunguliwa hapo ndipo
anapoishi Assad”
“Umewahi kufika mahala
hapo?akauliza GosuGosu
“Ndiyo nimewahi kufika
hapo nikiwa na Marwan kuna
vitu tulikwenda kuchukua kwa
Assad” akajibu Jabir.Gosu
Gosu akamweleza Nawal kile
alichoambiwa na Jabir
“Unamuamini?akauliza
Nawal
“Anaonekana anasema
ukweli” akajibu Gosu Gosu
“Sawa mshushe huyo
gaidi” akasema Nawal.Gosu
Gosu akazima ule moto halafu
akamshusha Marwan.Mlango
ukafunguliwa akaingia Ruby
moja kwa moja akaenda
kumtazama Marwan
“Ameungua vibaya mno
miguu yake” akasema Ruby
huku Marwan akiendelea
kugugumia kwa maumivu
makali
“Hakuna dawa yoyote ya
kumpunguzia huyu mtu
maumivu makali?akauliza
Nawal
“Hatuna dawa yoyote kwa
hapa hadi makao makuu ndiko
kuna kitengo cha tiba”
akasema Ruby
“Kwa hapa
tumemaliza.Tayari tumepata
kile tulichokuwa
tunakihitaji.Turejee makao
makuu tumuwahishe huyu
jamaa akapate matibabu”
akasema Gosu Gosu.Ruby
akawaita walinzi wa nyumba
ile wakambeba Marwan na
kumuingiza garini
wakaondoka kurejea makao
makuu.Safari ilikuwa ya kimya
kimya
“Japo tumefahamu alipo
Assad lakini hiki kilichofanyika
ni ukatili mkubwa
sana.Sijawahi kushuhudia
mateso ya namna hii yaani
mtu anachomwa taratibu
anaungua kama nyama.Dah !
akawaza Ruby
“Hawa jamaa wamekutana
wote wakatili.Gosu Gosu
namfahamu ni mkatili sana
lakini sikutegemea na huyu
mwanamke naye awe na
ukatili kama wa Gosu
Gosu.Nadhani ndiyo maana
yeye na Mathew walielewana
sana kwani hata Mathew naye
aina yake ya kufanya kazi ni
hivi hivi kutumia mateso
makali.Yawezekana labda
mambo haya ninayaona
mageni kwangu kwa sababu
mimi si jasusi lakini kwa hawa
waliosomea kazi hii kwao
wanayaona ni mambo ya
kawaida sana.Naanza kufikiria
labda na mimi yanipasa
kusomea mambo haya kwani
nimeingia kuongoza idara hii
nikiwa sina ujuzi mkubwa wa
mambo haya ya kijasusi.Baada
ya suala hili la vurugu
kumalizika nitaangalia kama
nitaweza kwenda kusomea
masuala haya ya ujasusi na
kuwa mjuzi kama huyu Nawal”
akawaza Ruby
Walifika katika ofisi zao na
kwa haraka Marwan
akashushwa akakimbizwa
upande wa afya ili kuanza
kupatiwa matibabu kwani hali
yake ilikuwa mbaya.Hakuweza
kuongea zaidi ya
kukoroma.Wale magaidi
wengine wakaenda kufungiwa
katika vyumba maalum vya
kuhifadhia
watuhumiwa.Ruby,Gosu Gosu
na Nawal wakaelekea katika
ofisi ya Ruby ambaye alikaa
katika kiti chake akainamisha
kichwa
“Ruby samahani kwa kile
ulichokishuhudia mle ndani
lakini ilibidi kutumia njia ile ya
mateso ili kuwafungua hawa
jamaa.Mambo kama yale ni ya
kawaida sana katika shughuli
hizi.Wakai mwingine inabidi
kujitoa ubinadamu ili kupata
taarofa za
muhimu.Utatusamehe kama
tuliku…...”
“Hakuna tatizo.Kitu
kikubwa ni kuwa tumepata
taarifa za muhimu
tulizozihitaji sana.Nini
kinafuata baada ya kupata
taarifa hizi?Tunavamia hoteli
hiyo alipo Assad?akauliza
Ruby
“Hapana.Hatuwezi
kuvamia hoteli hiyo hadi pale
tutakapojiridhisha ni kweli
Assad anaishi hapo.Hawa watu
si wa kuwaamini asilimia mia
moja” akasema Nawal
“Sawa.Kwa sasa ni usiku
hivyo zoezi la kufuatilia
nyumba ile kujua kama Assad
yuko mle ndani litaanza
asubuhi.Tunazo drone kubwa
ambazo huzitumia kufuatilia
mambo mbali mbali hapa Dar
es salaam tutaelekeza moja
katika nyuma ile na
kuchunguza kila
kinachoendelea lakini ushauri
wangu kama huyo jamaa
anayekuja kusambaza kirusi
anamtegemea Assad
kumsaidia kusambaza kirusi
hicho basi hatuna sababu ya
kumkamata Assad.Tuendelee
kumfuatilia Assad kimya
kimya na pale tukihakikisha
tayari amekwisha onana na
Sattar basi utakuwa ni wakati
wetu wa kuwatia nguvuni wote
wawili na kuchukua kirusi
hicho” akasema
“Hilo ni wazo zuri sana
Ruby.Tutafanya hivyo lakini
nina ushauri.Hili suala la
virusi liwe ni siri yetu sisi watu
watatu.Wasifahamu watu
wengine ili kuzuia kutokea
taharuki” akasema Nawal
“Ushauri mzuri.Gosu Gosu
mpeleke Nawal nyumbani
akapumzike.Amesafiri
kilometa nyingi na anahitaji
kupumzika.Kesho asubuhi
tunakutana hapa kuendelea na
kazi” akasema Ruby
“Vipi kuhusu wewe?
Akauliza Gosu Gosu
“Usihofu kuhusu mimi
.Nikimaliza kazi zangu
nitakwenda kupumzika pia”
akasema Ruby akaagana na
Nawal ambaye aliondoka na
Gosu Gosu
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 6
“Ruby anaishi wapi?Nawal
akauliza baada ya kufika katika
makazi ya Gosu Gosu
“Kwa sasa wote tumepiga
kambi pale ofisi kuu za SNSA
ka sababu ya usalam wetu”
akasema Gosu Gosu
“Nahisi njaa kuna
chochote cha kula
humu?akauliza Nawal.Gosu
Gosu akaenda jikoni
akaangalia katika friji akakuta
kuna kuku wawili
akamuamsha Lucy awaandalie
chakula
“Hapana mwambie Lucy
akapumzike nitaandaa mimi”
akasema Nawal na Lucy
akaenda kulala Nawal akaingia
jikoni akaanza kuandaa
chakula akisaidiana na Gosu
Gosu
“Mke wako yuko
wapi?akauliza Nawal
“Bado sijaoa”
“Unasubiri nini Gosu
Gosu? Akauliza Nawal
“Ni kutokana na aina ya
maisha niliyoishi.Naweza
kusema kwamba nimekulia
msituni katikati ya mapigano
makali.Nimelelewa na kundi la
waasi na kufundishwa
ukatili.Baadae niliondoka
msituni na kuja Tanzania
kutafuta maisha na ndipo
nilipofanikiwa kukutana na
Mathew Mulumbi ambaye
aliyabadili maisha yangu na
kuwa hivi nilivyo.Lakini
pamoja na maisha yangu
kubadilika na kuwa mazuri
hivi sasa lakini bado najiona
kama siwezi tena kuishi
maisha yale ya kawaida kama
wenzangu.Bado nahisi kuwa
na furaha kufanya kazi kama
hizi za kupigana ,kutumia
silaha na kutesa watu”
akasema Gosu Gosu
“Kwa upande Fulani
naweza kukubalioana nawe
Gosu Gosu kwani ukiwa katika
kazi hizi ni mara chache sana
utakuwa na furaha endapo
utakuwa na familia.Kwanza
familia yako watakukosa sana
muda mwingi utakuwa
kazini,pili ni hatari.Familia
yako inaweza kulengwa na
watu wabaya kwa hiyo nadhani
ni vyema ukaishi mwenyewe
kuliko kuwa na familia.Tazama
maisha ya Mathew Mulumbi
yalivyo kwa sasa” akasema
Nawal
“Vipi kuhusu wewe
hufikirii kuolewa tena? Gosu
Gosu akauliza
“Unataka kunioa?akauliza
Nawal na wote wakacheka
“Nani anaweza kukataa
kumuoa mtoto mzuri kama
wewe? Akasema Gosu Gosu
wakaangua tena kicheko
“Sina mpango wa kuolewa
tena.Nimekwisha olewa mara
mbili na watu ambao
sikuwatarajia kabisa,Ammar
Nazari na Abu Dahir.Labda
atokee mtu ambaye ataufanya
moyo wangu usimame na hata
akitokea mwanaume huyo sina
sifa za kuwa mke” akasema
Nawal
“Mungu ameumba
wanawake ili waolewe na
wanaume hivyo kila binadamu
mwanamke tayari ana sifa ya
kuwa mke” akasema Gosu
Gosu
“Mwanamke anaolewa ili
azae watoto na kuijaza dunia
ndiyo sifa kuu ya mke lakini
mimi sina uwezo wa kuzaa
mtoto hivyo tayari nimepoteza
sifa ya kuwa mke.Ni nani
anaweza akakubali kuoa
mwanamke ambaye
hatamzalia watoto? Kwa dunia
ya sasa inahitaji mwanaume
mwenye moyo wa malaika
ndiyo maana sihitaji kuolewa
tena” akasema Nawal
“Una uhakika kwamba
huna uwezo wa kuzaa?akauliza
Gosu Gosu na Nawal
akamsimulia kisa chote
kilichosababisha apoteze
uwezo wake wa kupata
ujauzito.
“Pole sana Nawal.Ulifanya
haya yote kwa ajili ya nchi
yako uipendayo lakini kwa
bahati mbaya watu hawajui ni
madhira gani wanayokutana
nayo watu walioyatoa maisha
yao kuhakikisha wanakuwa
salama.Ni kama anayopitia
Mathew Mulumbi kwa sasa”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu tuachane na
hayo mambo kwa sasa chakula
tayari twende tukale tujiandae
kwa ajili ya siku ya kesho.”
akasema Nawal wakaelekea
mezani.Gosu Gosu akamvutia
kiti Nawal akaketi na
kumshukuru
“Mimi ni mmoja wao
mwenye roho ya
kimalaika”akasema Gosu Gosu
na wote wakacheka
“Gosu Gosu huwezi kuwa
na sifa hiyo.Macho yako
yanaonyesha una kiu ya damu
! akasema Nawal na kuangua
kicheko kikubwa
“Niwapo kazini ni kweli
ninakuwa mkatili sana lakini
katika maisha ya kawaida
mimi ni mtu mpole sana”
akasema Gosu Gosu huku
wakiendelea kula
“Nawal mimi nawe tuna
vitu vingi tunafanana.Sisi ni
kama ndege wa rangi
moja.Tunaweza kuruka
pamoja” akasema Gosu Gosu
“Una maanisha nini Gosu
Gosu?
“Nina maanisha kama
tukiamua kuwa pamoja
tunaweza kuwa na maisha
mazuri kwa kuwa tunaendana
sana” akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu bado
hunifahamu vyema mimi ni
mtu wa namna gani”
“Sitakiwi kufahamu kila
kitu lakini kwa haya machache
niliyoyafahamu naamini
kabisa kwamba mimi nawe
tunaweza kuwa na furaha sana
endapo tutaamua kuwa
pamoja” akasema GosuGosu
“Umeniona leo tu na
unataka tuwe na mahusiano !
akasema Nawal huku akicheka
“Kwani inahitaji muda
gani mtu kujiridhisha kuwa
Fulani anakufaa? Akauliza
Gosu Gosu
“Gosu Gosu hicho
unachohisi unacho kuhusu
mimi ni tamaa tu za mwili na
si kitu kingine.Ungeniambia
kwamba umenitamani
ningekuelewa” akasema Nawal
huku akicheka
“Kuna kitu nakihisi ndani
mwangu toka nilipokuona sasa
sijui ni tamaa kama
unavyosema au ni hisia za
kweli juu yako” akasema
GosuGosu
“Hizo ni tamaa tu Gosu
Gosu na hiyo huwatokea
wanaume wengi hasa
wanapokutana na wanawake
wenye maumbo mazuri kama
mimi.Kwa bahati nzuri
ninajifahamu ni mzuri na
ninatamanisha” akasema
Nawal huku akicheka
“Hata hivyo kuna ubaya
wowote kutamani?akauliza
Gosu Gosu
“Si vibaya kutamani lakini
inaumiza pale ambapo waweza
kutamani kitu halafu
usikipate” akasema Nawal
“Sababu zipi zinaweza
kupeleka nisipate kile
nikitamanicho?
“Gosu Gosu tuko
kazini.Mambo hayo yana
wakati wake.Tumalize kwanza
kuondoa hii hatari inayoikabili
dunia kwa sasa halafu
tunaweza kuzungumza”
akasema Nawal wakaendelea
kupata chakula
“Baada ya kuchungulia
kaburi kwa sababu ya Melanie
naona kama vile ninaanza
kuvutwa na sumaku ya uzuri
wa huyu Nawal.Lakini huyu ni
tofauti sana na Melanie.Huyu
nina uhakika kabisa tunaweza
kuendana.Ngoja niende naye
taratibu.Sitakiwi kuwa na
papara nitaharibu mambo”
akawaza Gosu Gosu
VICTORIA – SHELI SHELI
Mathew alirejewa na
fahamu akajaribu kufumbua
macho lakini jicho moja
halikuweza kufunguka lilikuwa
limevimba kufuatia kipigo
kikali alichopewa.Alisikia watu
wakizungumza lugha ya
kiarabu akakohoa kidogo ili
kuwapa ishara watu wale
kwamba tayari amekwisha
zinduka.Haraka haraka
akasaidiwa kunyanyuka
akakalishwa katika gorodo
akapewa maji ya kunywa.
“Ahsante” akasema
Mathew kwa taabu akitumia
kiingereza.Mdomo wa chini
ulikuwa umevimba vibaya
“Wale jamaa walitaka
kuniua nini manake
wamenipiga kupitiliza”
akawaza Mathew
“Pole sana” akasema
mmoja wa wale jamaa kwa
lugha ya kiarabu
“Unaweza kuzungumza
kiarabu?akauliza Yule jamaa
na Mathew akatikisa kichwa
kukubali wale jamaa
wakatazamana halafu
wakatabasamu
“Tuambie wewe ni nani
umetokea wapi na kwa nini
hawa jamaa wamekutesa
namna hii? Akauliza Yule
jamaa
“Naitwa Abu
Zalawi.Ninatokea kundi la
wanamgambo la Ammar
Nazari Brigades lililokuwa
likiongozwa na Ammar Nazar
ambaye aliuawa na vikosi vya
Israel.Usiku wa kuamkia leo
nimelipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam
Tanzania na asubuhi ya leo
nilikamatwa jijini Nairobi
wakati nikitafuta usafiri wa
kuelekea Mogadishu.Ninyi ni
akina nani na kwa nini mko
hapa?akauliza Mathew
“Umelipua ubalozi wa
Marekani?akauliza Yule jamaa
“Ndiyo.Nimelipua ubalozi
wa Marekani” akajibu Mathew
“Hongera sana.Wewe ni
shujaa ! wakasema wale jamaa
huku kila mmoja akiinuka na
kumpa mkono wa pongezi
“Ninyi ni akina nani?
Mathew akauliza
“Mimi naitwa Yasser
Wazir” akasema Yule jamaa
aliyeonekana mkubwa kuliko
wote
“Wenzangu ni Abdul
Razzaq Zafar,Tayeb
Burhan,Shams Fayez,Sajid
Hassim na wa mwisho Yule
pale ni Muharrem Idris.Sisi
wote tunatokea Iran”
“Mnatokea Iran? Mathew
akauliza
“Ndiyo” akajibu Tayeb
“Mmefanya nini kwa
Marekani hadi mkaletwa
hapa? Akauliza Mathew
“Hatujafanya chochote
kwa Marekani .Sisi ni
wanasayansi tulitekwa
tukitokea nchini Urusi na
tumekuja kutupwa hapa
tukisubiri siku yetu ya
kufa.Toka tumeletwa hapa
hatujawahi kuona mwangaza
wa jua na wala hatujui kitu
gani kinaendelea huko
duniani.Hatujui huu ni mwaka
gani hatujui kama ni usiku au
ni mchana.Tunapewa mlo
mmoja kwa siku na hatujui ni
mlo wa asubuhi au wa
mchana.Ni mateso makubwa
tunayapata”
“Poleni sana.Huu ni ukatili
mkubwa uliovuka
mipaka.Kwani hapa ni wapi?
Mathew akauliza
“Hakuna ajuaye hapa tuko
wapi.Mateso haya makubwa
yote tumemuachia Mungu
ndiye atakayetulipia.Wewe
Abu Zalawi kwa nini umelipua
ubalozi huo wa Marekani?
Akauliza Abdul Razzaq
“Ni kwa sababu ya
dhuluma zinazofanywa na taifa
hilo hasa kwa nchi za
kiislamu.Ndugu zangu,jamaa
zangu wameuawa na majeshi
ya Marekani hivyo nina hasira
nao sana ndiyo maana
nililipua ubalozi wao na kama
wasingenikamata basi
ningeendelea kulipua balozi
nyingine za Marekani katika
nchi mbali mbali”
“Abu Zalawi wewe ni
shujaa kwa hiki
ulichokifanya.Marekani
imekuwa ikizikandamiza mno
nchi za kiarabu na hasa
Iran.Hatujui hali ikoje kwa
sasa lakini hadi tulipokamatwa
Iran ilikuwa imewekewa
vikwazo vingi vya kiuchumi
huku ikizuiwa kuuza mafuta
yake kwa lengo la kuizorotesha
kiuchumi.Pamoja na vikwazo
hivyo vya kiuchumi bado
Marekani na washirika wake
walikuwa wana mipango ya
kuishambulia kijeshi.Ni nchi
ya Urusi ambayo ilikuwa
mshirika wa Iran na ambayo
iliisaidia Iran kujenga vinu vya
nyuklia kwa ajili ya kuzalisha
nishati na hata sisi tulitekwa
tulipotoka nchini Urusi katika
mafunzo ya namna ya
kuendesha vinu hivyo vya
nyuklia kuzalisha nishati ya
umeme” akasema Yasser.
“Karibu ndugu yetu Abu
Zalawi katika maisha haya
tukisubiri siku ya kuchukuliwa
na Mungu wetu.Kitu
tunachowashukuru
wametupatia Quran
tukufu,tunasoma na
kumtafakari Mungu
tukimuomba atupokee pale
tutakapoaga dunia”akasema
Shams Fayez
“ Abu Zalawi nadhani
utumie muda huu
kupumzika.Tutakuwa na muda
mwingi wa mazungumzo
kwani tumetupwa katika hili
shimo na hatujui kama iko
siku tutatoka salama
humu.Pumzika” akasema
Yasser na kumtaka Mathew
alale katika kitanda chake.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Mshale wa saa ulionyesha
saa kumi na mbili za
asubuhi,Gosu Gosu na Nawal
tayari walikwisha fika makao
makuu ya SNSA.Moja kwa
moja wakaelekea katika ofisi
ya Ruby na kumkuta akiwa
amekiegemeza kichwa katika
kiti amesinzia.Taratibu Gosu
Gosu akamuamsha
“Ouh tayari mmefika”
akasema Ruby huku akifikicha
macho
“Ruby hupaswi kuendelea
namna hii.Unapaswa
kupumzika”
“Usijali Gosu Gosu I’m
fine” akasema Ruby na
kusalimiana na Nawal kisha
akaomba wamsubiri akaoge
Ilimchukua dakika kumi
na tano Ruby kurejea
“Sasa tunaweza
kuendelea” akasema Ruby na
kuwataka wafanyakazi ambao
tayari walikuwa kazini zamu ya
usiku na wale walioingia
asubuhi wakusanyike sehemu
ya kupeana taarifa muhimu za
kazi.Kama ulivyo utaratibu
aliouanzisha kabla ya kuanza
kwa kikao cha asubuhi
hutanguliwa na maombi
ambayo yalifanywa kwa dini ya
kikristu na kiislamu halafu
kikao kikaendelea
“Habari za asubuhi ndugu
zangu.Tunamshukuru Mungu
kwa kutukutanisha tena siku
hii ya leo.Kama mtakumbuka
juzi tuliendesha zoezi la
kuwakamata magaidi ambao
tunaamini ndio waliohusika na
mauaji ya viongozi kadhaa wa
dini na kuchochea vurugu za
kidini hapa
nchini.Tumewafanyia
mahojiano na tumefanikiwa
kupata mahala anapoishi
Assad Ismail ambaye ndiye
kiongozi wa magaidi
hao.Tumeambiwa ni eneo la
Sarara katika hoteli moja
ambayo bado
haijafunguliwa.Hatuwezi
kuvamia hoteli hiyo hadi
kwanza tujiridhishe kama
kweli Assad yuko hapo hivyo
basi leo tutafanya zoezi la
kuchunguza hoteli
hiyo.Asubuhi hii timu ya watu
wachache watamchukua gaidi
mmoja ambaye atakwenda
kuwaonyesha ilipo hiyo
hoteli.Wakati wakielekea huko
sisi tutaendelea kuwafuatilia
kwa kutumia drone yetu hadi
watakapofika hapo katika
hoteli.Baada ya kuipata hiyo
hoteli litaendelea zoezi la
kuchunguza kila anayeingia na
kutoka humo ndani ya hoteli
kwa lengo la kumpata Assad
Ismail.Hiyo ndiyo kazi ya
kipaumbele kwa siku ya
leo”akasema Ruby na
kuwataka wafanyakazi
wakaendelee na kazi yeye na
Gosu Gosu wakaondoka
kurejea ofisini .
“Gosu Gosu utaongoza
timu itakayompeleka Jabir
kutuonyesha hoteli aliko
Assad” akasema Ruby
Ndani ya muda mfupi timu
ya makomando wanne ilikuwa
tayari wakaongozana na Gosu
Gosu na Nawal bila kumsahau
Jabir ambaye ndiye aliyekuwa
anapafahamu mahala hapo
wakaondoka huku SNSA
wakiwafuatilia kwa kutumia
drone
Jabir aliwaongoza akina
Gosu Gosu hadi katika hoteli
ambako anaishi Assad.
“SNSA jengo lililo mbele
yetu ndilo hotel anakoishi
Assad” akasema Gosu Gosu
wakiwa wamesimamisha gari
mita kadhaa kutoka mahala
lilipo jengo lile refu lililopata
ghorofa nane.
“Tumekupata Gosu Gosu
sasa mrudi huku
ofisini.Tunaendelea kufuatilia
kwa kutumia drone” akasema
Ruby na Gosu Gosu akatoa
maelekezo kwa dereva wa lile
gari kugeuza na safari ya
kurejea SNSA ikaanza.
VICTORIA – SHELI SHELI
Mlango wa chumba
walimokuwamo akina Mathew
ukafunguliwa wakaingia watu
sita wanne wakiwa na
silaha.Walimchukua Mathew
wakamfunga pingu na
kumvisha mfuko kichwani
wakaondoka naye.Bado jicho
lake moja lilikuwa limevimba
na halifunguki
vizuri.Akaingizwa katika
chumba cha mahojiano
akaketishwa kitini na mikono
yake ikafungwa katika pingu za
mezani kisha akatolewa ule
mfuko kichwani akajikuta
akitazama uso kwa uso na
Jeffrey na wenzake
Richard,William,Brian a
Christopher.
“Karibu tena Abu
Zalawi.Naamini baada ya
kupata makaribisho siku ya
jana leo utakuwa tayari
kuzungumza nasi” akasema
Jeffrey.Mathew hakujibu kitu.
“Abu Zalawi unaendelea
pale tulipoishia jana.Tunataka
kufahamu watu unaoshirikiana
nao ambao walikutuma
ukalipue ubalozi wetu jijini
Dar es salaam” akasema
Jeffrey na kushika karatasi ili
aweze kuandika majina
“Abu tunataka majina ya
watu unaoshirikiana nao”
akasema tena Jeffrey
“Mnajisumbua bure.Siwezi
kuwaeleza chochote.Niuen
tafadhali niko tayari” akasema
Mathew
“Abu Zalawi hatuko hapa
kufanya mzaha tafadhali !
akasema Jeffrey
“Hata mimi sifanyi
mzaha.Nataka mniue kwa nini
mnanichelewesha?akauliza
Mathew
“Abu Zalawi unaonekana
bado hujapafahamu vizuri
mahala hapa” akasema Jeffrey
na kubonyeza kitufe pembeni
ya meza yake na baada ya
sekunde kadhaa mlango wa
kile chumba ukafunguliwa
wakaingia jamaa wanne
miongoni mwa wale
waliomtesa jana Jeffrey
akawataka waondoke na
Mathew wakaendelee kumtesa
Mathew akaingizwa tena
katika chumba cha mateso
akavuliwa nguo na kubakiwa
na nguo ya ndani akafungwa
katika mti halafu akaanza
kuchapwa kwa kutumia fimbo
ambazo zilimsababisha atokwe
na damu
nyingi.Yakachukuliwa maji
Fulani katika kopo dogo
akamwagiwa mwilini na kutoa
ukelele mkubwa kwa maumivu
makali.Alihisi kama mwili
wake unawaka moto baada ya
kumwagiwa maji yale.
“Nataka majina ! akasema
Jeffrey
“Niueni wapuuzi ninyi !
akasema Mathew akaendelea
kuteswa hadi alipopoteza
fahamu akachukuliwa na
kurejeshwa tena katika kile
chumba walimo wale mateka
wa Iran.Yasser Wazir na
wenzake wakaanza tena zoezi
la kumsaidia Mathew
kuzinduka.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Katika makao makuu ya
SNSA kilichokuwa kinaendelea
ni kufuatilia hoteli anamoishi
Assad.Hadi ilipotimu saa tisa
za alasiri bado hakukuwa na
mtu yeyote aliyeonekana
kuingia au kutoka ndani ya
jengo lile
“Ninaanza kupatwa na
wasi wasi kama kweli jengo hili
ndimo anamoishi Assad”
akasema Ruby
“Usikate tamaa
Ruby.Tuendelee kusubiri hadi
jioni kama hakuna chochote
tutakachokuwa tumekipata
basi tutatuma timu kwenda
kuingia ndani ya ile nyumba”
akasema Gosu Gosu
“Imani imeanza kunitoka
kama kweli Assad anaishi
ndani ya jengo hili.Naanza
kuhisi Jabir amecheza na akili
zetu” akasema Ruby
“Nilimtazama Jabir
machoni.Aliogopa kupewa
mateso aliyoona akipewa
Marwan ndiyo maana
akaamua kusema
ukweli.Naamini kabisa ndani
ya jengo hili ndimo anamoishi
Assad”akasema Gosu Gosu
“Tuendelee kuvuta subira
na ikifika saa kumi na mbili
jioni hakuna mtu aliyeingia au
kutoka basi tutatuma kikosi
usiku wa leo kwenda
kuchunguzandani ya jengo lile
kujua nini kinachoendelea na
kama Assad anaishi pale”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu anza kuandaa
timu ya makomando kwa ajili
ya kuvamia hii nyumba na
kujiridhisha kama kweli Assad
anaishi hapa.Nina mashaka
kama tumepewa taarifa ya
kweli.Kama kweli Assad
angekuwa anaishi humu ndani
ungekwisha muona kwani
tumeanza kufuatilia hii
nyumba kuanzia asubuhi na
hatujaona mtu yeyote akiingia
au kutoka ! akasema Ruby
akionekana kukata tamaa ya
kuendelea kufuatilia ile hoteli
VICTORIA – SHELI SHELI
Chumba cha akina
Mathew kilifunguliwa na
Mathew akachukuliwa.Hali ya
Mathew haikuwa nzuri.Kila
sehemu ya mwili wake ilikuwa
imevimba.
Tayari kiza kilikwisha
ingia Mathew akaingiza katika
chumba kimoja kilichokuwa na
vifaa kadhaa vya matibabu
haraka haraka akapokewa na
watu watatu waliokuwa
wamevaa makoti meupe
akalazwa kitandani akaanza
kuhudumiwa.Aliongezewa
damu na kupewa dawa za
kumsaidia kutuliza maumivu
aliyokuwa anayapata kutokana
na mateso aliyoteswa
Baada ya saa mbili hali ya
Mathew ilibadilika na mara
akaingia Jeffrey.
“Habari yako Abu
Zalawi.Unajisikiaje?
“Mwili umechoka hauna
nguvu! Akasema Mathew kwa
sauti dhaifu
“Pole sana” akasema
Jeffrey na kuwataka wale
mdaktari watoke nje kwa
muda akavuta kiti akaketi
karibu na Mathew
“Abu kama nilivyokueleza
awali kwamba mateso haya
yote unayoyapitia ni ili
kuonyesha
uhalisia.Tunafuatiliwa na
viongozi wetu kila
tunachokifanya hapa hivyo
tunapaswa kuwaonyesha kitu
halisi.Umeanza vizuri
ninaomba endelea
kuvumilia.Safari ya
kuwahamisha wewe na wale
wanasayansi wa Iran
inaandaliwa na itakapokuwa
tayari utajulishwa namna
utakavyofanya kuwatorosha ili
uweze kuingia Iran” akasema
Jeffrey
Mathew aligangwa
majeraha yake halafu akapewa
chakula kisha akarudishwa
katika chumba chao
“Pole sana Abu Zalawi”
Mathew akapewa pole
“Ahsanteni sana”
“Hata sisi walitutesa hivi
hivi wanavyokutesa wewe
wakitaka tuwaeleze tulitoka
Urusi kufanya nini lakini
tulikuwa na msimamo mmoja
na hatukuwahi kuwaeleza kitu
chochote.Walipochoka
kututesa wakaamua kuja
kututupa humu na
hwasumbuki na sisi
tena.Nadhani wanatutesa
kisaikolojia .Ninachokuomba
Abu Zalawi vumilia mateso
yote na usiwaeleze chochote”
akasema Yasser
“Kikubwa wanachokitaka
kutoka kwangu ni kupata
majina ya watu
ninaoshirikiana nao.Mimi
nimekwisha kula kiapo cha
kutokutoa siri hivyo niko
tayari kufa kuliko kuwaeleza
chochote kuhusiana na
mtandao wangu” akasema
Mathew
“Safi sana Abu
Zalawi.Wewe ni shujaa wa
kweli.Usifumbue mdomo wako
kuwaeleza chochote watu hawa
waonevu wakubwa ! akasema
Sajid Hassim
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Tayari imetimu saa moja
za jioni lakini bado
hakuonekana mtu yeyote
akiingia au kutoka ndani ya ile
nyumba ambayo SNSA
walielezwa kwamba ndimo
anamoishi Assad Ismail.Kikosi
cha makomando kilikuwa
tayari kimejiandaa wakisubiri
kupewa ruhusa ya kuondoka
kwenda kuingia ndani ya
nyumba ile.
“Kutwa nzima ya leo
tumeshinda humu ofisini
tukifuatilia nyumba hii lakini
hakuna chochote
tulichokipata.Nina wasiwasi na
taarifa tuliyopewa” akasema
Ruby wakiwa ofisini kwake
pamoja na Gosu Gosu na
Nawal wakijadiliana
kuhusiana na operesheni ile
“Ruby umekuwa na
wasiwasi tangu mchana lakini
nimekuhakikishia kwamba
alichokisema Jabir ni kitu cha
kweli”akasema Gosu Gosu
“Nenda kamchukue Jabir
mlete tena hapa atuhakikishie
kama kweli Assad anaishi
katika nyumba hii ! akasema
Ruby na Gosu Gosu akatoka
haraka akaenda kumchukua
Jabir akamleta katika ofisi ya
Ruby akaketishwa kitini
“Jabir ulitueleza kwamba
Assad anaishi katika nyumba
hii lakini tumefuatilia kuanzia
asubuhi mpaka giza limeingia
hakuna mtu yeyote aliyeingia
wala kutoka ndani ya hii
nyumba.Nikisema
ulitudanganya nitakosea?
Akauliza Ruby
“Sijawadanganya.Hapo
ndipo anapoishi Assad na
nilikwenda nikiwa na Marwan”
akajibu Jabir
“Jabir nitaaamuru
urejeshwe tena katika mateso
yale makali kama
uliyomshuhudia Marwan
akiteswa.Nataka unieleze
ukweli”
“Tafadhali naomba
msinipeleke kule kwenye
mateso.Nilichowaeleza ni kitu
cha kweli kabisa siwezi
kuwadanganya” akasema Jabir
“Ruby huyu jamaa
anasema kweli ! akasema
Nawal.Ruby akamuelekeza
Gosu Gosu kumrejesha Jabir
“Roho yangu inasita sana
kutuma kikosi kuvamia
nyumba hii” akasema Ruby
“Ruby nafahamu wasiwasi
wako kwamba yawezekana
Assad haishi katika hii nyumba
lakini nakutoa wasiwasi
kwamba Assad anaishi
hapa.Yule kijana
hajatudanganya” akasema
Nawal kisha wakatoka
wakaenda kuzungumza na
makomando walio tayari
kwenda katika nyumba
ile.Kikosi cha ardhini kikiwa
na makomando nane
kikatangulia na gari huku
kikosi cha helkopta kikisubiri
kikosi cha ardhini wafike.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 7
Makomando waliokuwa na
gari walikaribia kufika katika
jengo wanalokwenda
kulivamia na kuwajulisha
SNSA kisha kikosi cha
helkopta kikitumia helkopta
maalum inayotumika katika
operesheni za usiku ambayo
imetengenezwa kwa teknolojia
ya kutokutoa sauti,kiliondoka
kuelekea eneo la tukio.
Sehemu kubwa ya jiji la
Dar es salaam bado iliendelea
kuwa gizani.Kwa siku ya pili
jiji liliendelea kuwa
tulivu.Hakukuwa na zile
vurugu zilizokuwepo siku
kadhaa zilizopita.Taratibu
maisha yalianza kurejea katika
baadhi ya sehemu na biashara
ndogo ndogo zikifunguliwa
huku amri ya kutotembea
hovyo kuanzia saa moja za
jioni ikiendelea.Magari ya
doria ya vikosi vya jeshi na
polisi yaliendelea kuzunguka
katika mitaa mbali mbali ya jiji
la Dar es salaam kuimarisha
ulinzi.
Helkopta ya makomando
wa SNSA ilikaribia kufika
katika jengo lile na
wakawajulisha wale waliokuwa
katika gari ambao walianza
kusogea karibu zaidi na jengo
lile.Helkopta ilifika juu ya
jengo lile na makomando sita
wakashuka kwa kutumia
kamba na helkopta
ikaondoka.Wakiwa wamevaa
miwani maalum ya
kuwawezesha kuona katika
giza makomando wale
waliokuwa katika gari
wakashuka na kuelekea katika
geti ambalo lilikuwa limefugwa
kwa kutumia mnyororo na
kufuli kwa nje.Toka mchana
tayari walikwisha chunguza
kila kitu na kujiandaa.Mkasi
mkubwa ukaletwa kufuli
likakatwa wakaingia
ndani.Wale wengine waliopitia
juu nao wakavunja mlango wa
pande wa juu na kuingia
ndani.
Mlango mkubwa wa
kuingilia ndani ulikuwa
umefungwa.Haraka haraka
wakabandika utepe Fulani
katika mlango uliounganishwa
kwa waya na kifaa fuani
ambacho kiliwashwa na baada
ya muda mlango ule
ukalipuliwa .Kiongozi wa
kikosi kile cha chini akatoa
maelekezo na kisha wakaanza
kukagua sehemu ya chini.Mara
ghafla mmoja wa wale
makomando akasimama na
kuwataka wenzake wasimame.
“Kuna nini?akauliza
kiongozi wao na wote wakawa
kimya wakasikia sauti ya kitu
kama saa kutoka karibu na
pale walipokuwa wamesimama
.Wakaanza kufuatilia sauti ile
hadi katika jokofu
wakalifungua na ndani yake
wakakuta bomu likiwa na kifaa
mfano wa saa kikihesabu.
Kiongozi wa makomando
wale akawataka watu wake
wasogee mbali kidogo.
“SNSA kuna tatizo
limejitokeza”kiongozi wa
kikosi kile akatoa taarifa kwa
SNSA
“Tatizo gani
limetokea?akauliza Ruby
“Tumegundua uwepo wa
bomu katika jokofu ambalo
tayari limekwisha anza
kuhesabu.Nadhani bomu hili
lilikuwa limeunganishwa na
mlango mkubwa ili
ukifunguliwa tu basi bomu
linaanza kuhesabu kabla ya
kuipuka.Tuna dakika kumi na
tatu tu kabla ya bomu
kulipuka” akasema Yule mkuu
wa kikosi cha makomando
“Eneo hilo tayari ni
hatarishi ondokeni hapo
haraka sana” akasema Ruby
“Hapana mkuu hatuwezi
kuondoka kabla
hatujaikamilisha kazi
tuliyokuja kuifanya.Tunazo
dakika za kutosha tunaweza
kulitegua hili bomu na
tukaendelea na uchunguzi
wetu”akasema Yule kiongozi
wa makomando na kutaka
aitwe mtaalamu wa mabomu
ambaye alibaki pale makao
makuu anaitwa Cyril.
Haraka haraka Cyril
aliyekuwa katika kambi yao nje
ya ofisi za SNSA akaitwa na
kiongozi Yule wa makomando
akatuma picha za bomu lile
Cyril akalitazama na kusema
“Hili ni bomu la
kutengenezwa
kienyeji.Mabomu ya namna hii
ni magumu sana kuyategua
ukikosea kidogo unaua watu
wote”akasema Cyril
“Unaweza kulitegua au
huwezi?Kama huwezi kuwa
muwazi niwaondoe watu
wangu haraka sana mahala
walipo ! akasema Ruby
“Ninaweza”
“Dakika nane zimebaki !
akasema Ruby
“Naomba dakika mbili”
akasema Cyril na kuitazama
picha ile ya bomu halafu
akaanza kuwasiliana na Yule
kiongozi wa makomando
akimpa maelekezo.
“Cyril imebaki dakika moja
! akasema Ruby
“Sekunde hamsini na tatu !
akasema Ruby kwani
maelekezo yote aliyoyatoa
Cyril hayakuzaa matunda
Cyril akamuelekeza
Godwin kiongozi wa
makomando kukata waya
Fulani na kama bomu
litaendelea kuhesabu basi
hakutakuwa na namna
nyingine zaidi ya kukimbia
.Kila mtu aliweka mikono
kichwani kusikiliza kile
kitakachotokea
“SNSA bomu
limezima.Narudia tena bomu
limezima.Ahsante SNSA.Sasa
tunaendelea na upekuzi”
akasema Godwin .Watu wa
SNSA wakashangilia kwa
furaha.
Upekuzi ulifanyika kwa
saa mbili lakini hawakuweza
kupata mtu au kitu chochote
ndani ya nyumba ile cha
kumuhusu Assad.
“Tayari alifahamu wenzake
wametekwa na alijua lazima
watateswa ili waeleze mahala
alipo ndiyo maana akaondoka
na kutega bomu mahala pale
akijua lazima watakwenda pale
kumtafuta” akasema Nawal
wakiwa katika ofisi ya Ruby
baada ya kupokea taarifa ya
makomando kumkosa Assad
“Nawal yuko sahihi.”
akasema Gosu Gosu
“Tumekwama
tena.Tusaidiane mawazo
namna tunavyoweza kumpata
Assad ! akasema Ruby
“Nahitaji kuzungumza na
Habiba Jawad nimuulize kama
kuna taarifa yoyote ameipata”
akasema Nawal na kupewa
simu akampigia Habiba
“Mama Habiba habari za
huko? Akauliza Nawal
“Huku naendelea
vizuri.Vipi wewe uko salama
huko Dar es salaam?akauliza
Habiba
“Niko salama mama
usihofu.Nimekupigia kujua
kama kuna taarifa mpya
umeipata lakini vile vile nataka
kukufahamisha kwamba bado
hatujampata
Assad.Tumewakamata watu
wake wakatuonyesha maficho
yake tulipomfuata tumekuta
kahama na hatujui amejificha
wapi,tunaendelea kumsaka”
akasema Nawal
“Nawal kumpata Assad ni
lazima.Fanyeni kila muwezalo
kuhakikisha anapatikana
kwani taarifa niliyoipata ni
kwamba tayari Sattar
amekwisha ondoka Marekani
saa mbili za asubuhi kwa saa
za Marekani kuelekea
Tanzania akiwa na kirusi hicho
na mtu anayemtegemea
kumpa msaada ni Assad hivyo
mkimpata Assad mtakuwa na
uhakika mkubwa wa kumpata
Sattar na kirusi” akasema
Habiba
“Sattar ameondoka
Marekani na ndege gani?
Akauliza Nawal
“Sifahamu ni ndege gani
amepanda kwani nimepata
taarifa ya jumla kwamba tayari
amekwisha ondoka Marekani
na yuko angani hivi sasa
akielekea Tanzania.Fanyeni
kila juhudi kuhakikisha
mnampata Assad kabla Sattar
hajakanyaga ardhi ya
Tanzania” akasema Habiba
“Ahsante sana mama kwa
taarifa hiyo.Una taarifa zozote
kuhusu Mathew Mulumbi?
“Hapana sina taarifa
zozote hadi sasa kumuhusu
Mathew” akasema Habiba
“Mama
nakushukuru.Nitakujulisha
tena pale tutakapokuwa
tumefanikiwa kumpata Assad”
akasema Nawal na kuagana na
Habiba akawageukia akina
Ruby
“Kwa mujibu wa Habiba
Jawad,tayari Sattar amekwisha
ondoka Marekani akiwa na
kirusi na yuko angani hivi sasa
anakuja Tanzania.Tunahitaji
kumtafuta Assad kwa namna
yoyote ile na kujua mahala
alipo kwani ni yeye ambaye
anategemewa kumsaidia Sattar
katika kukisambaza kirusi
hicho” akasema Nawal
“Kuna kitu nimekumbuka
ambacho kinaweza kutusaidia
sana kumpata Assad” akasema
Gosu Gosu
“Umekumbuka nini Gosu
Gosu?akauliza Ruby
“Mathew alipokuja
kuonana nasi na kutueleza
kuhusiana na mambo
yanayofanywa na IS hapa
nchini alitoa angalizo kwamba
tuwe makini tunapomfuatilia
Assad na watu wake kwani
wanapata msaada mkubwa
kutoka kwa vikosi vya
Marekani.Alikwenda mbali
zaidi akasema kwamba kila
siku Assad anapokwenda
katika nyumba ile walimokuwa
wakiishi akina Marwan
husindikizwa na gari la doria la
vikosi vya Marekani hivyo
naamini lazima watakuwa
wanafahamu mahala alipo
Assad hivi sasa” akasema Gosu
Gosu na Ruby akajipiga
kichwani
“Ni kweli Mathew alitoa
angalizo hilo.Kwa nini
nikasahau maelekezo haya?
Hivi sasa tungekuwa mbali
sana katika kumsaka
Assad.Ahsante Gosu Gosu kwa
kukumbuka” akasema Ruby
“Kwa sasa baada ya kupata
picha kuwa Assad anasaidiwa
na vikosi vya Marekani nini
kinafuata? Ruby akauliza
“Kuna kitu kimoja
ninakifikiria” akasema Nawal
“Marekani lazima
wachukue tahadhari kubwa
katika kukisafirisha kirusi
hicho na kuhakikisha kinafika
salama Tanzania hivyo
naamimi lazima Sattar
atakuwa anakuja na ndege
maalum ambayo haitaweza
kutua sehemu yoyote ile zaidi
ya hapa Dar es salaam.Na hapa
Dar e salaam atakuwa
anasubiriwa na Assad ambaye
tayari tumefahamu anasaidiwa
na vilkosi vya Marekani
vilivyopo hapa nchini.Kitu
ambacho tunapaswa kujua je
vikosi vya Marekani vinatumia
kiwanja gani cha ndege hapa
Dar es salaam? Naamini
lazima ndege zao zinaingia na
kutoka kila siku hivyo
tukifahamu ni uwanja gani wa
ndege wanautumia tutakuwa
tumempata Sattar” akasema
Nawal
“Nawal yuko sahihi.Kwani
hapa Dar es salaam kuna
viwanja vingapi vya ndege?
akauliza Gosu Gosu
“Kiwanja kikubwa ni cha
Julius Nyerere ambacho toka
zilipoanza vurugu kilifungwa”
akasema Ruby
“Kama hakuna kiwanja
kingine basi lazima ndege za
jeshi la Marekani zinatua
katika uwanja huo ambao sasa
uko chini ya vikosi vya jeshi na
nina uhakika hata ndege hiyo
inayomleta Sattar na kirusi
lazima itatua katika uwanja
huo” akasema Nawal.Ruby
akabofya kompyuta yake
haraka haraka halafu akasema
“Kutoka Washington hadi
Dar es salaam ni mwendo wa
kama saa ishirini.Hivi sasa ni
saa tano na dakika ishirini na
saba ambayo ni sawa na saa
tisa za alasiri Washington
hivyo kama ndege hiyo
imeondoka Marekani saa mbili
asubuhi ya leo tunategemea
itafika hapa Tanzania kuanzia
saa sita za mchana
kesho.Kama wote
tunakubaliana basi macho yetu
tuyaelekeze uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere kujua kila
kinachoendelea pale” akasema
Ruby
“Uwanja wa ndege
unalindwa na vikosi vya
jeshi,tutawezaje kupenyeza
watu wetu ndani ya uwanja
kujua kinachoendelea?akauliza
Nawal
“Litakuwa ni zoezi la
kimya kimya.Jambo zuri ni
kwamba taasisi zote za serikali
mifumo yao imeunganishwa
na SNSA kwa siri hivyo
tunaweza kuingia katika
mfumo wa taasisi yoyote ya
serikali muda wowote.Kuna
kamera zaidi ya mia tatu
katika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere tutatumia
kamera hizo kufuatila kila
kinachoendelea pale uwanjani
vile vile tutatumia pia na drone
zetu kufuatilia” akasema Ruby
na kuanza kucheza na
kompyuta yake kama vile ana
vidole nane katika kila
mkono.Baada ya muda mfupi
tayari alikwisha ingia katika
mfumo wa uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere na kamera
zikaanza kuonekana.Ruby
akamtaka Gosu Gosu
kuwakusanya wafanyakazi
wote katika sehemu ya
kukutania pale kunapokuwa
na jambo la muhimu la
kuwaeleza
“Habari za saa hizi ndugu
zangu” akasema Ruby
“Kutwa nzima ya leo
tulikuwa na zoezi la kufuatilia
maficho ya Assad
Ismail.Tunashukuru Mungu
kwamba watu wetu wote
wamerejea salama katika zoezi
hilo la hatari.Assad alifahamu
kuwa lazima tutamfuata pale
ndiyo maana yeye na watu
wake wakatega lile bomu
ambalo halikuleta madhara
kwa watu wetu.Bado suala la
Assad liko mezani na ni
kipaumbele
kikubwa.Tunaendelea
kumsaka kwa kila namna
tuwezavyo na lazima tumpate”
akasema Ruby na kubonyeza
kitanza mbali na katika runiga
kubwa ikaonekana picha ya
Sattar
“Anaitwa Sattar Sayf Al
Din. Anatoka kundi la kigaidi
la IS na anakuja Tanzania”
“Anakuja kufanya nini
Tanzania?mmoja wa
wafanyakazi akauliza
“Bado hatufahamu
anakuja kufanya nini lakini
huyu ana mahusiano na Assad
Ismail hivyo basi huyu ndiye
atakayetuongoza kujua mahala
alipo Assad.Sattar anatokea
Marekani kwa ndege maalum
na tunahisi anaweza akatua
katika kiwanja cha ndege cha
kimataifa cha Julius
Nyerere.Mtu huyu ni hatari
sana na nitawaeleza hapo
baadae kwa nini ni mtu
hatari.Kwa hiyo kuanzia sasa
tunajielekeza katika uwanja wa
ndege wa kimatafa wa Julius
Nyerere ambako tunahisi
ndiko Sattar
atashukia.Kuanzia sasa
tufuatilie kamera zote na kujua
kila kinachoendelea pale
uwanjani.Tufahamu kama
kuna ndege zozote zinatua pale
na zinatokea wapi na zimekuja
kufanya nini kwani uwanja
umefungwa na uko chini ya
uangalizi wa vikosi vya
jeshi.Tunategemea kuanzia
kesho mchana Sattar anaweza
akatua hapa nchini hivyo basi
tuyaelekeze macho yetu
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere.Hayo ndiyo niliyonayo
kwa sasa”akasema Ruby na
kuondoka na Gosu Gosu
“Gosu Gosu mchukue
Nawal mkapumzike hadi
asubuhi.Mimi nitaendelea
kusimamia shughuli zote za
hapa” akasema Ruby
Gosu Gosu na Nawal
wakaondoka kuelekea katika
makazi ya Gosu Gosu
kupumzika
VICTORIA – SHELI SHELI
Saa nane za usiku mlango
wa chumba walimo akina
Mathew ukafunguliwa
wakaingia walinzi
wanne.Tayari akina Mathew
alikuwa wamepitiwa na
usingizi.Mathew akaamshwa
na kutolewa mle ndani
akapelekwa katika chumba
Fulani ambako alimkuta
Jeffrey.
“Abu Zalawi tumekuondoa
usingizini lakini ni kwa jambo
la muhimu” akasema Jeffrey
“Tumepewa maelekezo
kwamba wewe na wale
wanasayansi kesho
mtapelekwa Marekani kwa
ndege maalum” akasema
Jeffrey na kumpa Mathew
maelekezo ya namna mpango
utakavyokuwa
“Abu Zalawi sisi
tumemaliza kwa upande wetu
ahsante sana kwa ushirikiano
wako .Nakutakia kila la heri
katika jukumu zito ulilopewa”
akasema Jeffrey
“Nashukuru sana Jeffrey
na ninawaahidi kwamba
nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha ninafanikisha
kupata kile nilichotumwa
nikafanye nchini Iran”
akasema Mathew na kuagana
na Jeffrey akarejeshwa tena
katika kile chumba chao
“Hawa jamaa walikuwa
wanataka nini? akauliza Yasser
baada ya Mathew kurejea
“Bado wanaendelea
kunihoji wakidhani labda
nimebadili msimamo
wangu.Wameniambia
nitafakari hadi kesho kabla
sijakutana na mateso ambayo
sijawahi kuyaona”
akadanganya Mathew
“Abu Zalawi chochote
unachokifahamu usiwaeleze
hawa jamaa.Hata ukiwaeleza
chochote hawatakuacha
salama.Usifanye nao
makubaliano yoyote makatili
hawa” akasema Yasser
“Niko tayari kufa lakini si
kuwaeleza chochote
Marekani.Msihofu ndugu
zangu hawawezi kupata
chochote kutoka kwangu”
akasema Mathew
wakampongeza kisha kila
mmoja akaenda kulala katika
godoro lake
“Mpaka hapa nilipofika
nimefanya vizuri.Hawa jamaa
tayari wameniamini na hicho
ndicho hasa kitu kikubwa
kwani hawa ndio
watakaonisaidia niaminiwe na
mamlaka za Iran.Ninaingia
katika sehemu ngumu sana ya
misheni hii.Namuomba
Mungu anisimamie” akawaza
Mathew
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 8
Saa mbili za asubuhi
mlango wa chumba
ulifunguliwa akina Mathew
wakaamriwa kusimama halafu
kila mmoja akafungwa pingu
na kuvishwa mfuko kichwani
kisha wakatolewa ndani ya kile
chumba
“Mnakwenda
kutuua?akauliza Yasser lakini
hakuna aliyemjibu
“Tungeomba mtupatie
nafasi ya dakika chache tusali
kabla ya kuuawa” akasema
Sajid Hassim
Waliingizwa katika gari
mlango ukafungwa
wakaondoka.Ndani ya lile gari
ambalo hawakulijua ni la aina
gani kulikuwa na watu wanne
wenye silaha wakiwalinda.
Baada ya dakika kadhaa
gari lile likasimama mlango wa
nyuma ukafunguliwa
wakashushwa halafu taratibu
walianza kupandishwa ngazi
na kuingia katika ndege.Kila
mmoja akakalishwa katika kiti
chake na kufungwa pingu
miguu na mikono
zilizounganishwa na mnyororo
mrefu.Dakika chache baadae
ndege ikapaa na ilipokaa sawa
angani mifuko waliyofunikiwa
kichwani ikatolewa.Ndani ya
ndege kulikuwa na walinzi
wanne waliokuwa na silaha.
Ndege iliendelea kupasua
anga huku akina Mathew
wakikirimiwa kwa vinywaji na
vitafunwa
“Kazi inaanzia hapa”
akawaza Mathew na kumuita
mmoja wa walinzi
akamwambia anahitaji
akajisaidie.Mlinzi Yule
akafungua mahala minyororo
ile ilipofungwa kisha
akampeleka Mathew
chooni.Akamfungulia mlango
Mathe akaingia kisha mlinzi
Yule akasimama kwa nje
akimsubiri.Mathew akapapasa
mahala alipoelekezwa akakuta
kuna funguo ya kufungulia zile
pingu.Haraka haraka
akafungua pingu za mikono
halafu akafungua za miguu
akawa huru.Akasimama
pembeni ya mlango
Zilipita dakika tano Yule
mlinzi akagonga mlango na
kumuuliza Mathew kama
amekwisha maliza
kujisaidia.Mara akasikia sauti
ya muanguko wa kitu
akafungua mlango haraka
haraka kuchungulia lakini
kitendo cha kuchungulia
akajikuta akipigwa kichwa
kizito halafu akadakwa na
kuvutwa ndani.Mathew
akamuongeza kichwa kingine
na ngumu za mfululizo Yule
mlinzi akaanguka chini
“Sihitaji kumchunguza
kama bado ana
fahamu.Ninaiamini mikono
yangu,haijawahi kukosea”
akawaza Mathew akamsachi
Yule jamaa na kuchukua
bunduki yake pamoja na
bastora akavaa fulana ya
kujikinga na risasi aliyokuwa
ameivaa Yule
mlinzi.Akamfunga Yule mlinzi
kwa pingu halafu akafungua
mlango taratibu akachungulia
nje hakukuwa na mtu maeneo
yale ya karibu akatoka na
kuanza kutembea kwa
kunyata.Alijitokeza katika
chumba walimokuwamo wale
wanasayansi ambao wote
walipatwa na mstuko mkubwa
baada ya kumuona Mathew
akiwa na bunduki na
bastora.Haraka haraka
akamfuata Yasser akamfungua
pingu za mikono na miguu
akawa huru akampa bunduki
halafu akamfungua Muharrem
Idris na kumtaka aendelee
kuwafungua wenzake.Mathew
akanyata kuelekea katika
chumba ambacho walinzi wale
walikuwa wamekaa
wakizungumza huku wakipata
kinywaji.Hawakuwa na
wasiwasi wowote wakiamini
mwenzao alikuwa katika
chumba cha wafungwa
akiendelea na zamu ya
ulinzi.Mathew akachungulia
katika kioo akawaona namna
walivyokaa halafu taratibu
akakishika kitasa akakinyonga
kikafunguka na kwa kasi ya
umeme akajitoma ndani ya
kile chumba cha
walinzi.Walipatwa na mstuko
mkubwa
“Wote simameni taratibu
huku kila mmoja mikono yake
ikiwa juu !! Mathew
akaamuru.Taratibu walinzi
wale wakaanza kuinuka
taratibu na ghafla mlinzi
mmoja akashusha mkono
akataka kuchomoa bastora
yake lakini kabla hajaifikia
risasi zikasikika na Yule mlinzi
akaanguka chini.Nyuma ya
Mathew alikuwa amesimama
Yasser akiwa na bunduki
inayofuka moshi.Ndiye
aliyemmaliza Yule mlinzi
Walinzi wale
wakachukuliwa wote na
kufungwa pingu .
“Tunatakiwa kuidhibiti
ndege na kuibadili uelekeo
wake ! akasema Mathew
“Abu Zalawi kuna jambo
ambalo hatukuwa
tumekueleza.Sisi wote hapa ni
wanajeshi na miongoni mwetu
Abdul Razaq ni rubani wa
ndege hivyo hakuna kitu cha
kusubiri twende haraka
tukawadhibiti wale marubani !
akasema Yasser kisha
wakatoka katika chumba kile
wakaanza kunyata kuelekea
katika chumba cha
marubani.Mlango wa chumba
cha marubani ulikuwa
umefungwa kwa ndani.Bila
kupoteza muda Yasser
akamimina risasi katika kitasa
na kukisambaratisha Mathew
akaurukia teke mlango
ukafunguka wakaingia ndani
ya chumba kile cha marubani
.Mathew akawataka wasimame
na watoke katika viti vyao
marubani wale wakatii kisha
Abdu Razaq na Tayeb Burhan
wakashika hatamu na kuanza
kuiongoza ndege .Kitu cha
kwanza walichokifanya ni
kuzima kifaa kinachowezesha
ndege kuonekana na
kufuatiliwa katika rada.
“Abdu badili uelekeo wa
ndege tunakwenda nyumbani !
akasema Yasser kwa furaha
kubwa.
“Mafuta yaliyopo
yanaweza kutufikisha
Iran?Mathew akauliza
“Ndiyo.Mafuta yanatosha
kutufikisha nyumbani.Ahsante
Abu Zalawi” akajibu Abdu
Razaq
“Vipi kuhusu
mimi?Nitakubaliwa kuingia
Iran kutokana na historia
yangu ya ugaidi?akauliza
Mathew
“Abu Zalawi wewe ni
shujaa na unastahili sifa
kubwa.Ni wewe uliyesababisha
haya yote yakawezekana.Ni
wewe uliyesababisha leo hii
tunarejea tena
nyumbani.Utapokelewa kwa
mikono miwili Abu Zalawi
usihofu” akasema Yasser na
kumkumbatia Mathew kwa
furaha kubwa kisha akaungana
na wenzake kuimba kwa
furaha wimbo wa taifa la Iran.
MPENDWA
MSOMAJI,TAYARI MATHEW
MULUMBI ANAELEKEA
NCHINI IRAN JE
ATAFANIKIWA KUINGIA
SALAMA NCHINI HUMO ?
SATTAR YUKO ANGANI
ANAELEKEA DAR ES
SALAAM JE RUBY NA
WENZAKE WATAFANIKIWA
KUMPATA NA KUZUIA
KIRUSI KISISAMBAE?
MPENDWA MSOMAJI
USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
Daa, methew anaingia Iran sasa, kazi ndo imeanza
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 1
Tangu kulipopambazuka,tayari
SNSA walianza kufuatilia
kilichokuwa kinaendelea
katika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere.Hii ni baada ya
kuhisi kuwa Sattar Sayf Al Din
ambaye anatumwa Tanzania
kusambaza virusi angeweza
kushukia katika uwanja
huo.Tayari walikwisha jiunga
na mfumo wa ulinzi wa
uwanjani hapo na walikuwa
wanafuatilia kamera zote
kufahamu kilichokuwa
kinaendelea.Uwanja wa Julius
Nyerere bado ulikuendelea
kufungwa na ulikuwa chini ya
uangalizi wa vikosi vya jeshi la
Tanzania.
Asubuhi hii jiji la Dar es
salaam lilikuwa shwari na
hakukuripotiwa matukio
yoyote ya vurugu.Maduka na
masoko yalianza kufunguliwa
ili kuwawezesha wananchi
kujipatia mahitaji
muhimu,wananchi wengine
waliokuwa wamekimbilia
katika makambi maalum
yaliyotengwa kwa ajili ya
kuwahifadhi watu waliokimbia
mapigano,walianza kurejea
katika majumba yao kufanya
usafi na kuhifadhi mali
zao.Taratibu hali ya maisha
katika jiji la Dar es salaam
ilianza kurejea kuwa ya
kawaida lakini bado doria za
vikosi vya ulinzi na usalama
ziliendelea katika mitaa mbali
mbali ya jiji ili kuhakikisha
hakuna vurugu zozote
zinazoendelea kutokea.
Saa moja na dakika kumi
na saba,Gosu Gosu na Nawal
waliwasili ofisi kuu SNSA na
moja kwa moja wakaelekea
ofisini kwa Ruby na kumkuta
akiendelea na kazi
“Tayari kazi imekwisha
anza.Tumeanza kufuatilia kila
kinachoendelea uwanjani hapo
toka saa kumi na mbili za
asubuhi na mpaka sasa hakuna
chochote
tulichokipata.Zimetua
helkopta mbili za jeshi na
ndege moja ya jeshi la
Tanzania.Tunaendelea
kufuatilia kwani kama
nilivyosema jana kuna
uwezekano mkubwa Sattar
Sayf Al Din akaingia hapa
nchini kuanzia saa sita za
mchana wa leo” akasema Ruby
“Nina mashaka kidogo.Ni
vipi kama Sattar atatumia
ndege ya kawaida ya abiria na
akaenda kutua katika uwanja
wa kimataifa wa Kilimanjaro
au hata Nairobi halafu akaja
Dar es salaam kwa gari ?
Akauliza Gosu Gosu
“Hilo haliwezekani”
akasema Nawal
“Kirusi hicho ni hatari
sana na hawawezi kutumia
ndege ya abiria
kusafirishia.Lazima watatumia
ndege maalum kuhakikisha
kinafika kikiwa salama hivyo
kwa vyovyote vile lazima
watatumia uwanja huu wa
Julius Nyerere” akasema
Nawal
“Tuendelee kufuatilia na
kama hatutapata chochote
tutatafuta namna nyingine ya
kuweza kumpata Sattar lakini
kwa siku ya leo kwa namna
yoyote ile lazima tuhakikishe
tumekipata kirusi hicho”
akasema Ruby wakaendelea
kufuatilia kamera zile za
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere katika runinga kubwa
wakiwa ofisini kwa Ruby
“Nawal unaonaje
ukimpigia simu Habiba Jawad
ukamuuliza kama amepata
taarifa zozote za kuhusu Sattar
Sayf Al Din pamoja na
Mathew? Akauliza Ruby na
kumpatia Nawal simu
akampigia Habiba Jawad
“Mama Habiba”akasema
Nawal baada ya Habiba
kupokea simu
“Nawal unaendeleaje?
Akauliza Habiba
“Niko salama kabisa
mama.Kwa ujumla jiji la Dar
es salaam liko salama.Hakuna
matukio ya vurugu japo
hakuna uhakika kama vurugu
zimekwisha au vipi lakini hadi
sasa jiji ni salama kabisa.Kuna
taarifa yoyote mpya
huko?Nawal akauliza
“Kwa sasa bado sijapata
taarifa yoyote mpya.Bado
taarifa niliyonayo ni ile ile
kwamba Sattar Sayf Al Din
amekwisha ondoka Marekani
akielekea Tanzania.Kuna
mipango yoyote mnayo ya
kujua mahala atakapofikia
huyu mtu? Akauliza Habiba
“Ndiyo mama.Kwa sasa
tunaendelea kufuatilia katika
uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Nyerere hapa Dar es
salaam ambako tuna uhakika
ndiko atatua.Tunategemea
kuanzia saa sita mchana wa leo
awe amewasili hapa Dar es
salaam kutokana na muda
alioondoka
Marekani.Nitakujulisha kile
tutakachokipata” akasema
Nawal
“Nawal narudia tena
kukusisitiza kwamba kwa
namna yoyote ile lazima
muhakikishe Sattar
anakamatwa kirusi
hakisambazwi nchini
Tanzania.Umenielewa Nawal?
“Nimekuelewa
mama,tunafanya kila
tuwezalo.Kuna taarifa zooze
umepata kuhusu Mathew
Mulumbi? Nawal akauliza
“Hapana.Bado sijapata
taarifa zozote.Msihofu kuhusu
Mathew atakuwa salama japo
atakumbana na magumu
mengi lakini ninao uhakika
mkubwa atayashinda yote na
atamaliza misheni
yake.Tuendelee kumuombea ili
awe salama.Kwa sasa
jielekezeni zaidi katika kirusi
hicho na mimi kila nikipata
taarifa yoyote ambayo naamini
inaweza kuwa na msaada
kwenu nitawajulisha haraka
sana” akasema Habiba
“Mama wewe
unafahamiana na viongozi
wote wakuu wa IS.Kwa nini
usiwasiliane nao wakueleze
mahala alipo Assad ili
iturahishishie kumpata Sattar
Sayf Al Din endapo hatatumia
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere?akauliza Nawal
“Mimi ni mfadhili wao tu
na si sehemu yao ya uongozi
hivyo kuna mambo mengine
ambayo hawawezi
kuniambia.Hata hivyo
nitajitahidi kutafuta taarifa za
namna ya kuweza kumpata
huyo Assad na nikifanikiwa
nitawajulisha” akasema
Habiba na kuagana na Nawal
“Kama mlivyosikia hakuna
jipya kutoka kwa
Habiba.Tuendelee na mipango
yetu tuliyoipanga” akasema
Nawal
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Taarifa za kupotea kwa
ndege iliyowabeba Mathew
Mulumbi mtuhumiwa wa
Ugaidi aliyelipua ubalozi wa
Marekani nchini
Tanzania,pamoja na raia sita
wa Iran waliokuwa
wanashikiliwa Mateka na
Marekani kwa muda
mrefu,zilipokelewa kwa
mstuko nchini
Marekani.Haraka haraka
juhudi za kuitafuta ndege hiyo
zikaanza.Kitu cha kwanza
walichokihisi ni kwamba
yawezekana ndege hiyo
imeanguka katika bahari ya
Hindi.
Taarifa hiyo ya kupotea
kwa ndege,zikamfikia Rais
William Washington wa
Marekani ambaye bila
kupoteza muda akampigia
simu makamu wake Mark
Piller
“Mheshimiwa Rais”
akasema Mark Piller baada ya
kupokea simu
“Mark nimejulishwa
kuhusu kupotea kwa ndege
yetu iliyokuwa inamleta
mtuhumiwa wa shambulio la
ugaidi katika ubalozi wetu
jijini Dar es salaam.Kuna
chochote unaweza ukaniambia
kuhusiana na tukio hilo?
Akauliza Rais William
“Ndiyo mheshimiwa Rais.
Ndege hiyo haijapotea bali kwa
sasa imebadili uelekeo na
kuelekea chini Iran. Hii ni
katika ule mpango niliokueleza
kwamba tunataka kumtumia
Abu Zalawi kuingia nchini
Iran.Usihofu mheshimiwa Rais
kila kitu kimepangwa kwa
umakini mkubwa sana”
akasema Mark Piller
“Mark una uhakika hiki
mnachokifanya kitafanikiwa?
akauliza Rais William
“Naomba uniamini
mheshimiwa Rais.Mpango huu
utafanikiwa na utakuwa na
manufaa makubwa sana
kwetu.Usiwe na hofu
mheshimiwa Rais tuko makini
sanana tumejipanga vizuri”
akajibu Mark
“Mark jitahidini sana
kufanya kila linalowezekana
kuhakikisha kwamba jambo
hili haligeuki na kuwa mzigo
kwetu.Endapo huyo gaidi
mnayemtumia akigundulika
mtakuwa mmeivua nguo nchi
yetu”
“Usiwe na shaka
mheshimiwa Rais.Tunaamini
Abu Zalawi ataifanya vyema
kazi anayotumwa kwenda
kuifanya kule Iran” akajibu
Mark Piller
“Vipi kuhusu kile kirusi?
Tayari kimefika Tanzania?
Akauliza Rais William
“Kwa taarifa nilizonazo ni
kwamba Sattar Sayf Al Din
anakaribia kufika Tanzania na
atakapofika tutajulishwa na
watu wetu kule.Kila kitu
kitakwenda sawa mheshimiwa
Rais”
“Mark narudia tena kutoa
angalizo kwamba kila hatua za
tahadhari lazima zichukuliwe
kuwalinda watu wetu kule
Tanzania.Sitaki kupoteza hata
raia mmoja wa Marekani
katika suala hili” akasema Rais
William
“Mheshimiwa Rais
naendelea kukusisitiza
kwamba hutakiwi kuonyesha
kama unafahamu chochote
kuhusiana na haya mambo
niliyokueleza.Yote
unayoyafahamu endelea
kuyafanya siri kubwa ambayo
hata mke wako
asiifahamu”akasema Mark
Piller
“Nitafanya hivyo Mark”
akajibu Rais William na
kuagana na Mark Piller
ambaye naye alimpigia simu
David Walker kiongozi wa
kikundi kile ambacho kimejipa
jina la The great 20 au kwa
kifupi G20.
“David nimetoka
kuzungumza na Rais muda
mfupi uliopita kuhusiana na
kupotea kwa ndege yetu”
“Anasemaje Rais? Akauliza
David
“Hafahamu chochote.Yeye
na wenzake wanachoamini ni
kwamba yawezekana ndege
imeangukia baharini”
“Safi sana.Mark mpango
unakwenda vizuri sana na hivi
tuzungumzavyo tayari ndege
hiyo inaelekea
Iran.Tunafuatilia na
tunaendelea kukujulisha kila
kitakachojiri” akasema David
Walker na kuagana na Mark
kwani alikuwa na safari ya
kuelekea kwa Jason
Washington mkurugenzi wa
CIA.Hakupoteza muda akatoka
kuelekea katika gari lake
akaondoka kuelekea nyumbani
kwa mkurugenzi wa
CIA.Tayari mida hiyo ilikaribia
saa kumi za usiku kwa saa za
Marekani.
David alifika nyumbani
kwa Jason Washington
akakaribishwa ndani na
walinzi wa Jason.Alipelekwa
moja kwa moja katika ofisi ya
Jason akaingia na kumkuta
akizungumza na mtu
simuni.Jason akamfanyia
ishara aketi na asubiri amalize
mazungumzo na Yule mtu
simuni.Baada ya dakika moja
Jason akaagana na Yule
aliyekuwa akizungumza naye
simuni akamgeukia David
“Karibu David” akasema
Jason
“Jason nikuonapo katika
sura hiyo najua kuna jambo
haliko sawa” akasema David
“Ni kweli David.Jana
kijana wangu alichukua gari la
mama yake bila ruhusa
akaenda nalo katika sherehe ya
kuzaliwa mmoja wa marafiki
zake na wakati wakirudi
amegonga gari lingine”
akasema Jason
“Ameumia? David akauliza
“Hapana hajaumia”
akajibu Jason
“Usijali Jason hayo ni
mambo ya kawaida kwa vijana
wetu yatakwisha tu.Kitu
kikubwa hajaumia katika ajali
hiyo” akasema David Walker
“Tuachane na hayo
David.Twende moja kwa moja
katika kile kilichokuleta hapa
alfajiri hii” akasema Jason
“Jason kuna jambo
limenileta hapa tulijadili mimi
na wewe ambalo ni la muhimu
sana katika ule mpango wetu
unaoendelea”
“Ndiyo David.Jambo gani
hilo? Kwanza kabla ya yote
nataka niwape hongera sana
kwa namna mlivyo ratibu
mpango huu kiasi cha
kutotiliwa shaka hata kidogo
kama ni mpango
uliotengenezwa.Hivi sasa
tayari utafutaji wa ndege hiyo
iliyopotea umeanza na wote
wanaamini yawezekana ikawa
imepata hitilafu ikaanguka na
kuzama katika bahari ya
Hindi.Una jambo gani
muhimu la kuongezea katika
mpango huu David? Akauliza
Jason
“Mpango kama unavyoona
unakwenda vizuri sana na tuna
uhakika mkubwa kwamba Abu
Zalawi ataingia nchini
Iran.Hata hivyo kuna jambo
ninalifikiria la muhimu sana
ambalo hatukulitilia maanani
hapo kabla”
“Ndiyo nakusikiliza David”
akasema Jason
“Uhakika wa Abu Zalawi
kuingia nchini Iran ni
mkubwa.Hatukutegeneza
mpango wowote wa kumsaidia
Abu Zalawi akiwa nchini
Iran.Akiwa kule kuna mambo
ambayo atayahitaji kama vile
mawasiliano,usafiri nk hivyo
lazima awepo mtu wa
kumsaidia kuyapata haya kwa
siri bila mtu huyo kujulikana”
akasema David
“Hilo ni wazo zuri sana
David lakini hatuna watu wetu
kule Tehran.Endapo
tungekuwa na watu wetu kule
ingekuwa rahisi kumpa Abu
Zalawi msaada muda wowote
atakaouhitaji”akasema Jason
“Ni kweli sisi hatuna watu
wetu Tehran lakini tunao
wenzetu wa Mossad.Wao wana
majasusi wao nchini
Iran.Tunaweza kuzungumza
nao ili majasusi hao waweze
kumsaidia Abu Zalawi.Abu ni
mgeni wa jiji la Tehran na
kama angeweza kumpata
mwenyeji ambaye angemsaidia
katika kufanikisha baadhi ya
mambo ingemrahisishia sana
shughuli yake.Unaonaje wazo
hilo la kuwaomba msaada
Mossad? akauliza David.Jason
akainamisha kichwa akafikiri
kidogo halafu akasema
“Ninakubaliana na wazo
lako David lakini sina uhakika
kama Mossad wanaweza
kukubali kutusaidia katika
operesheni hii.Kuna msuguano
ulitokea hapa kati kati baina
yetu hivyo basi mahusiano
yetu na Mossad si mazuri kwa
sasa” akasema Jason
“Jason kwa namna yoyote
ile lazima tumsaidie Abu
Zalawi kule Iran.Hatuna
majasusi wetu Iran na
hatuwezi kuingiza majasusi
wetu kule lakini Israel ambao
ni washirika wetu wakubwa
wana majasusi wao Iran
ambao tunaweza kuwatumia
kumpa msaada Abu Zalawi ili
aweze kukamilisha jukumu
tulilomtuma kule” akasema
David
“David kuna jambo
lilitokea na kuzorotesha
mahusiano yetu na
Mossad.Kuna wakati walihitaji
kufahamu mahala alipo
Ammar Nazari na wakaomba
msaaada kwetu lakini sikuwa
tayari kuwasaidia kuwapa
taarifa za mahala alipo Ammar
Nazari kwa kuwa tulikuwa na
mtu wetu katika kundi hilo
aliyekuw akatika operesheni
maalum.Baada ya kuwakatalia
kuwapa taarifa za mahala alipo
Ammar,Mossad walifanya
jitihada zao wenyewe na
kufanikiwa kufahamu mahala
anapojificha Ammar na
wakamuua kwa bomu.Toka
wakati huo mahusiano yetu
nao si mazuri” akasema Jason
“Pamoja na mashirikiano
kutokuwa mazuri lakini si
vibaya kama
tukiwajaribu.Endapo
watakataa kutusaidia
tutaangalia washirika wetu
wengine.Tunao washirika
kadhaa wanaoweza kutusaidia
lakini tunapenda kufanya kazi
na Mossad kwa kuwa majasusi
wake wana umahiri mkubwa
sana.Jaribu kuwasiliana na
mkurugenzi wa Mossad ili
tuone kama wanaweza
kutusaidia” akashauri
David.Kwa kufuata ushauri wa
David,Jason akachukua simu
na kumpigia Moshe Levine
mkurugenzi wa Mossad
“Jason habari za
siku?akauliza Moshe Levine
mkurugenzi wa Mossad baada
ya kupokea simu
“Huku tunaendelea vyema
kabisa”akajibu Jason
“Nafuarhi kusikia
hivyo.Poleni kwa shambulio la
Dar es salaam” akasema
Moshe
“Ahsante Moshe.Samahani
kwa kupiga muda huu lakini
nimekupigia kukuomba
msaada wako.Nafahamu
hatuna mashirikiano mazuri
kwa siku za hivi karibuni lakini
CIA na Mossad tumekuwa
marafiki na kushirikiana kwa
muda mrefu hivyo nashauri
tusahau yale yaliyopita na
tuanze tena mashirikiano
mapya baina yetu” akasema
Jason
“Nini unahitaji Jason?
Akauliza Moshe
“Nafahamu unao watu
wako jijini Tehran”
“Ndiyo ninao watu watu
wangu Tehran” akasema Jason
“Nahitaji msaada wako
Moshe.Kuna operesheni
kubwa sana tunaiendesha kule
Tehran.Kuna mtu wetu
tumemtuma huko katika
misheni ya muhimu
sana.Ninahitaji watu wako
kule Tehran wamsaidie huyo
mtu wetu aweze kufanikisha
misheni yake” akasema Jason
“Jason unaweza
ukanifafanulia ni operesheni
gani inaendelea huko Iran?
Akauliza Moshe na Jason
akamueleza Moshe kuhusiana
na misheni ile wanayotaka
kuifanya nchini Iran.
“Jason kwanza nashukuru
kwa kuniamini na kunieleza
kuhusiana na mpango wenu
unaoendelea nchini
Iran.Mossad tuna watu wetu
Tehran na hakuna tatizo katika
kumsaidia huyo mtu wenu
kufanikisha misheni
mliyomtuma kwani misheni
hiyo ni muhimu pia kwa taifa
la Israel kwani tumekuwa
tukipokea vitisho vingi kutoka
Iran.Hata hivyo kuna
tatizo”akasema Moshe
“Tatizo gani Moshe?
akauliza Jason
“Sina hakika kama huyu
mtu mnayemtumia katika
operesheni hiyo Abu Zalawi
mnamfahamu vyema”
akasema Moshe.Jason
akamtazama David
“Kuna nini kuhusu Abu
Zalawi? Akauliza Jason
“Huyu mtu mnamfahamu
vyema?
“Moshe unaonyesha wasi
wasi mkubwa.Unamfahamu
Abu Zalawi? Akauliza Jason
“Ndiyo
Jason.Ninamfahamu Abu
Zalawi kiundani ndiyo maana
ninasema kuna tatizo” akajibu
Moshe na Jason akashusha
pumzi
“Kabla sijawaeleza
chochote, ilikuaje mkachagua
kumtuma Abu Zalawi kazi hii
nyeti? Akauliza Moshe
“Tulihitaji mtu ambaye ni
Gaidi kwa ajili ya kazi hii na
tulipompata Abu Zalawi
ilitulazimu kwanza
kujiridhisha kama anafaa
tukampa mtihani akaufaulu
vizuri ndipo tulipomtuma
kwenda Iran.Kuna tatizo gani
kuhusu huyu mtu?akauliza
Jason
“Nina wasiwasi
mnamtumia mtu ambaye
hamumfahamu vyema na
ndiyo maana nasema lipo
tatizo.Abu Zalawi si gaidi kama
mlivyojulishwa”akasema
Moshe Levine
“Si gaidi? Ki vipi Moshe?
Akauliza Jason akionekana
kustuka kidogo
“Jina lake halisi ni Mathew
Mulumbi.Ni jasusi anatokea
Tanzania” akasema Moshe na
nusura simu imponyoke Jason
kwa mstuko alioupata
“Sijakuelewa Moshe
unachokizungumza” akasema
Jason
“Huyu mtu
mnayemfahamu kama Abu
Zalawi jina lake halisi ni
Mathew Mulumbi na ni jasusi
anayetokea Tanzania” akasema
Moshe Levine na kumsimulia
Jason kila kitu kuhusu Mathew
Mulumbi toka alivyovamia
ubalozi wa Israel jijini Nairobi
na kumtorosha Edger kaka na
hadi walivyofanikiwa
kumkamata na kumfunga kwa
miaka mitatu nchini
Israel.Jason akahisi kuanza
kuloa jasho.Moshe akaendelea
“Kwa muda mrefu
tumekuwa tukimtafuta
mfadhili mkuu wa vikundi vya
wanamgambo wanaopambana
na Israel ambaye anafahamika
kama Habiba Jawad.Mathew
naye alikuwa katika mpango
huo akatushawishi tuungane
naye katika kumsaka Habiba
na ndipo tulipokuja na
mpango wa kumuunganisha
Mathew na Ammar Nazari
kiongozi wa kundi la Ammar
Nazari Brigades aliyekuwa
anashikiliwa gerezani na
ambaye kundi lake lilikuwa
linafadhiliwa na Habiba.Hapo
ndipo jina la Abu Zalawi
lilipoanza.Hili ni jina ambalo
tulimpa alitumie kwa ajili ya
kujenga ukaribu na Ammar
Nazari na vile vile tukamuweka
katika mtandao wetu kama
mtu tunayemtafuta.Mathew
alifanikiwa kumtorosha Abu
Zalawi gerezani na kujiunga
naye na baada ya hapo
hatukuwahi kupata mrejesho
wowote kutoka kwake hadi
tulipofanikiwa kumuua
Ammar.Mathew aliibuka tena
na tayari alikwisha onana na
Habiba Jawad ambaye
alimtuma kuja Israel
kumchukua mwanae Edger
Kaka tuliyekuwa
tunamshikilia.Tulimkabidhi
mwili wa Edger Kaka akapotea
na hatukupata tena mrejesho
kutoka kwake hadi tulipopata
taarifa kuwa amehusika katika
shambulio la bomu katika
ubalozi wa Marekani jijini Dar
es salaam.Yawezekana hayo
yote hamkuwa mkiyafahamu
kuhusu huyu jamaa
mnayemtumia katika hiyo
misheni yenu muhimu sana”
akasema Moshe.Jason akavuta
pumzi ndefu kisha akasema
“Moshe umetufumbua
macho.Ni kweli hatukuwa na
taarifa zozote za kuhusiana na
huyu mtu.Tunachokifahamu
sisi ni kwamba anaitwa Abu
Zalawi raia wa Saudi
Arabia.Nimestuka kusikia
kwamba jina lake ni Mathew
Mulumbi na ni raia wa
Tanzania.Moshe ahsante sana
kwa taarifa hii ambayo
imenichanganya
sana.Ninaomba nikupigie
baadae kidogo” akasema Jason
na kukata simu akatazamana
na David
“David nini hiki
kinachoendelea? akauliza
Jason na kumpa David
maelezo yote aliyopewa na
Moshe Levine mkurugenzi wa
Mossad.
“Kweli hii ni taarifa ya
kustusha mno.Hakuna mtu
yeyote aliyefahamu kitu kama
hiki.Tumeletewa huyu mtu na
Habiba ambaye tunamuamini
na tumeshirikiana naye kwa
muda na akatupa taarifa zake
kuwa ni gaidi na anaitwa Abu
Zalawi.Tunamuamini Habiba
Jawad hivyo hakuna aliyekuwa
na wasiwasi hata kidogo
kuhusiana na mtu aliyetuletea”
akasema David Walker ukapita
ukimya mfupi halafu Jason
akasema
“Habiba ametuchezea
mchezo mbaya sana ! akasema
Jason kwa hasira
“Ni jambo la kustusha
mno”
“Baada ya kulifahamu
jambo hili nini tunafanya
David? akauliza Jason
“Imekuwa bahati mbaya
sana tumelifahamu jambo hili
katikati ya misheni na wakati
ambao tayari Abu anaelekea
Iran na hatuna namna tena ya
kuweza kumzuia asiendelee na
misheni hii.Jason kwa sasa
sina hakika kama kuna kitu
tunachoweza
kukifanya.Tumuache tu
aendelee na misheni yetu tena
kama ni jasusi itakuwa vizuri
zaidi kwani atafanya kazi kwa
ufanisi mkubwa sana”
akasema David Walker
“David,mtu huyu kama
alivyosema Moshe tumekosea
sana kumpa misheni kubwa
kama hii.Tulipaswa
kumchimba Abu Zalawi
mapema na kumfahamu
kiundani kabla ya kumtuma
kazi.Tulikosea mno” akasema
Jason
“Ni kweli Jason.Nikiri
tulikosea sana kutokufanya
uchunguzi wa kina kuhusu
Abu Zalawi kabla ya
kumkabidhi misheni hii lakini
hii ilisababishwa na imani
kubwa tuliyo nayo kwa Habiba
Jawad.Tuliamini mtu
aliyetuletea hana tatizo lolote
kwani amekuwa akitusaidia
kupata watu kwa ajili ya
shughuli mbali mbali na
hakujawahi kutokea tatizo
lolote hadi sasa.Ushauri wangu
tumuache Abu Zalawi aendelee
na misheni hii kwani tayari
amekwisha piga hatua kubwa”
akasema David Walker
“Hapana David hatuwezi
kumuacha akaendelea na
misheni hii na wala misheni
yenyewe haipaswi
kuendelea.Tunasimamisha kila
kitu ! akasema Jason na
kumfanya David apatwe na
mshangao
“Jason wewe ni mkuu
wangu na ndiye mwenye
maamuzi ya mwisho
kuhusiana na misheni zote
tunazozifanya lakini katika hili
siwezi kukubaliana nawe hata
kidogo.Tumekwisha tumia
gharama kubwa sana kwa ajili
ya kuandaa operesheni hii na
tayari tumefika nusu yake
hatuwezi kuishia hapa.Lazima
tuendelee hadi pale
tutakapotimiza lengo
letu.Kumbuka damu za watu
zimemwagika kwa sababu ya
misheni hii,hatuwezi kuishia
hapa! Tumekaribia sana kufika
pale ambapo tumekuwa
tunapatafuta kwa miaka
mingi” akasema David
“David nakubaliana nawe
kwamba imetugharimu fedha
na damu kuandaa misheni hii
lakini hatuwezi kuendelea
nayo tena.Madhara yake ni
makubwa sana kama
ikiendelea ukilinganisha na
gharama ambazo
tumetumia.Huyu jamaa
ambaye tayari tumefahamu
anaitwa Mathew Mulumbi ni
mtanzania.Hamuoni hatari
iliyopo kuendelea kumtumia?
Ni vipi kama tayari anafahamu
mambo tuliyoyafanya kule
Tanzania? Sikuwepo wakati
mkizungumza naye lakini
nataka nifahamu kutoka
kwako kwani ni wewe
uliyeongoza mahojiano naye
kuna chochote mlimwambia
kuhusiana na kile
tulichokifanya Tanzania?
Akauliza Jason na David
akaanza kukumbuka.
“Eneo la Afrika Mashariki
hivi sasa liko katika
machafuko makubwa sana ya
kidini.Kinachoendelea kule ni
moja ya mipango yetu na kwa
kuwatumia IS tumeweza
kufanikisha kuibuka kwa
machafuko makubwa sana ya
kidini ambayo yamepelekea
Marekani kupeleka vikosi
vyake.Hapa unaweza ukaona
ni namna gani Marekani
inafaidika kutokana na
makundi ya
kigaidi.Tumewatumia IS
kutengeneza vurugu zile na
sasa Marekani inafaidika kwa
mafuta mengi kutoka
Uganda.Meli za Marekani
zimepanga foleni zinapishana
kujaza mafuta ,akiba yetu ya
mafuta inaongezeka.Hii yote
ni kazi ya timu hii unayoiona
humu ndani na ni mfano wa
mafanikio makubwa ambayo
yanapatikana kwa
kuwatumia magaidi”
Sura ya David walker
ikabadilika baada ya kumbu
kumbu hii kumjia.
“Kuna kitu umekikumbuka
David?akauliza Jason
“Ndiyo Jason.Kuna kitu
nimekikumbuka.Katika
mazungumzo yetu tulimueleza
Abu Zalawi kila kitu
tunachokifanya bila kumficha
tukiamini yeye ni gaidi na ni
raia wa Saudi
Arabia.Hatukujua kama ni
jasusi tena raia wa
Tanzania.Tulifanya kosa”
akasema David na ukimya
ukapita
“Mlimweleza chochote
kuhusiana na mpango wa
kusambaza kirusi Tanzania?
Akauliza Jason
“Hapana mpango huo
umekuja baada ya yeye
kuondoka
Marekani.Hafahamu chochote
kuhusu mpango huo lakini
anachokifahamu ni kuwa,sisi
tukiwatumia magaidi wa IS
tumechochea vurugu za kidini
zilizotokea Tanzania kwa lengo
la kujipatia mafuta.Nilikuwa
mjinga sana kumweleza jambo
hili ! akasema David kwa
masikitiko
“David nadhani sasa
umeona wewe mwenyewe kwa
nini ninasema misheni hii
lazima isimamishwe haraka
sana bila kujali utekelezaji
wake umefika hatua gani.Abu
Zalawi au Mathew Mulumbi
kama anavyojulikana hapaswi
kuendelea na misheni
hii.Tayari anafahamu kuwa ni
sisi tulio nyuma ya machafuko
yale yaliyotokea Tanzania
lakini bado akakubali kufanya
kazi tuliyomtuma akaifanye
hudhani kuna kitu huyu jamaa
anapanga kukifanya? Kwa
mujibu wa Moshe huyu ni
mmoja wa majasusi hatari
kabisa na kwa miaka mitatu
alikuwa katika mateso makali
na hakuwahi kufungua mdomo
wake kusema
chochote.Japokuwa amekubali
kuifanya kazi yetu kama vile
hakuna chochote kilichotokea
lakini hatuwezi kujua moyoni
mwake nini
anakiwaza.Tumefanya kosa
kubwa sana David” akasema
Jason
“Yote haya ameyataka
Habiba Jawad.Yeye ndiye
aliyemleta huyu mtu na
akatuaminisha kwamba ni mtu
sahihi anayeweza kuifanya
operesheni hiyo kwa
ukamilifu.Kwa nini
akamchagua Abu Zalawi?
Hapo ndipo tunapaswa
kuanzia” akasema David
“Unadhani Habiba Jawad
alimfahamu Abu Zalawi ni
nani lakini bado makusidi
kabisa akaa mua kumleta
kwetu tumtumie? Akauliza
Jason
“Ninahisi hivyo.Alimleta
kwetu mtu ambaye naamini
alimfahamu fika ni nani na
ninahisi alifanya hivyo kwa
sababu maalum ambayo
hatuijui”
“Tumeshirikiana na
Habiba Jawa kwa muda mrefu
toka mume wake alipofariki na
tumemuwezesha kuwa na
utajiri mkubwa mno,unadhani
anaweza kuwa na mpango
wowote wa siri dhidi yetu?
Akauliza Jason
“Tutamfanyia uchunguzi
kulifahamu hilo lakini kwa
sasa ni kutafakari kuhusu
hatua za haraka za kuchukua
kuhusiana na misheni hii na
huyu jamaa Abu Zalawi”
akasema David
“Kama nilivyosema awali
kwamba kwa namna yoyote ile
Abu Zalawi hapaswi kuendelea
na misheni hii nyeti”akasema
Jason
“Hivi sasa naamini Abu
atakuwa njiani akielekea
Iran.Ndege aliyomo imepotea
haionekani na hatuna namna
ya kuweza kumpata hadi
atakapokuwa ameingia
Iran,ndiyo maana nilishauri
kwamba aendelee na misheni
yake kama kawaida na kama
tukif……..”
“David huyu mtu hapaswi
kuendelea na misheni yetu
yoyote.Huyu mtu ni bomu na
siku moja atatulipukia.Tayari
anafahamu sisi ndiyo sababu
ya mamia ya watu kupoteza
maisha Tanzania na
yawezekana miongoni mwa
waliofariki ni ndugu
zake,unadhani akisikia tena
kitakachotokea Tanzania
baada ya kirusi kusambazwa
nini atatufanya? Ni wazi
anaweza akageuka na kuwa
adui yetu mkubwa.Huyu mtu
tayari amekuwa mzigo kwetu
na kitu pekee ambacho
tunapaswa kukifanya kwa sasa
ni kutafuta namna ya kumuua
kabla hajaanza kufanya
chochote nchini Iran” akasema
Jason
“Tuliwaomba msaada
Mossad ili majasusi wao
walioko nchini Iran wamsaidie
Abu Zalawi tunaweza kubadili
badala ya kumsaidia mpango
uwe ni kumuua” akasema
David
“Nadhani itatulazimu
kufanya hivyo.Japo nakubali
tumefika hatua nzuri lakini
mtu tuliyemtumia si mtu
sahihi na hatuwezi kuendelea
naye.Tunapaswa kummaliza
haraka sana kisha tutaanza
kujipanga tena upya namna
nyingine.Vile vile
tumchunguze Habiba Jawad
tujue kama alimfahamu Abu
Zalawi ni nani lakini bado
akamleta kwetu ili
tumtumie.Tuchunguze
mahusiano yao.Habiba
anapaswa ahojiwe kwa kina
kuhusiana na huyu jamaa”
akasema Jason halafu
akachukua simu na kumpigia
Moshe Levine mkurugenzi wa
Mossad
“Moshe nimekupigia tena
kuomba msaada wako.Kwanza
ninakushukuru kwa
kutufumbua macho kuhusu
Abu Zalawi.Hatukuwa
tukimfahamu ni nani huyu
mtu na baada ya kumfahamu
tumeamua kukatisha misheni
tuliyomtuma akaifanye Iran”
akasema Jason Washington
“Ni maamuzi mazuri
mmeyafanya Jason,kwani
huyu jamaa si mtu sahihi kwa
misheni hii na hata sisi mpaka
leo hii tunajilaumu mno kwa
kuamua kushirikiana
naye.Ameturejesha nyuma
mno katika jitihada zetu za
kumsaka Habiba
Jawad.Tulidiriki hata
kumuachia Ammar Nazari
ambaye ni mtu hatari sana kwa
Israel tukitegemea kupata
matokeo lakini hatujapata
chochote mpaka sasa.Huyu
mtu anatakiwa aondolewe
haraka iwezekanavyo !
akasema Moshe Levine
“Ndiyo maana
nimekupigia Moshe ili
kukuomba tushirikiane tuweze
kuumuondoa Abu Zalawi
haraka sana kabla hajafanya
chochote nchini Iran” akasema
Jason
“Nina watu wangu jijini
Tehran ambao wakatekelea
mpango huo wa kumuua Abu
Zalawi lakini kuna kitu
tutakihitaji kutoka kwenu CIA”
akasema Moshe Levine
“Nini unakihitaji Moshe?
Akauliza Jason
“Ninataka kupata taarifa
za mahala alipo Habiba
Jawad”akasema Moshe
“Habiba Jawad? Akauliza
Jason kwa mshangao
“Ndiyo.Tutahitaji kujua
mahala alipo” akajibu Moshe
“Hatuna taarifa zozote za
kumuhusu Habiba Jawad”
akasema Jason
“Jason nimewaambia
hivyo kwa sababu nafahamu
mnazo taarifa za kumuhusu
Habiba Jawad.Tunafahamu
Abu Zalawi amekutana na
Habiba Jawad na kama
mmeweza kukutana na Abu
Zalawi mkamtuma katika
misheni yenu lazima
mnafahamu alipo Habiba
Jawad.Tunamuhitaji sana
Habiba Jawad hivyo tupeni
taarifa za mahala alipo na sisi
tuwatumie watu wetu
kumuondoa Abu Zalawi”
akasema Moshe Levine.
“Moshe nitakupigia
baadae kidogo tuzungumze
kuhusu suala hili” akasema
Jason Washington na kukata
simu akapiga meza kwa hasira
“Aaaaghh !! akasema kwa
hasira
“Mossad wanataka tuwape
taarifa za Habiba Jawad ndipo
watusaidie kumuonda Abu
Zalawi! Akasema Jason
“Wamefahamuje kama
tunafahamu alipo Habiba
Jawad?akauliza David
“Ni kwa sababu ya Abu
Zalawi.Wanafahamu amekuwa
akishirikiana na Habiba Jawad
hivyo basi kitendo cha sisi
kumtumia katika misheni yetu
kinawafanya waamini kwamba
tunafahamu mahala alipo
Habiba Jawad.David jambo
hili linazidi kuwa kubwa”
akasema Jason
“Jason kwa namna yoyote
ile hatuwezi kuwapa Mossad
taarifa za Habiba
Jawad.Hawapaswi kufahamu
kama tumekuwa tukishirikiana
naye.Hii ni siri yetu kubwa
ambayo hata Rais wetu haijui
hivyo hatuwezi kuianika kwa
mtu mwingine yeyote hasa
hasa Mossad” akasema David
“Lakini tunahitaji
kumuondoa Abu Zalawi
haraka sana na ni Mossad
pekee wanaoweza kutusaidia
katika hilo kwani tayari wanao
majasusi wao jijini
Tehran.David tukubali
Mossad wametubana katika
kona.Tunahitaji kuzungumza
nao vizuri katika jambo
hili.Tukichelewa tunaweza
kumkosa Abu Zalawi kwani
tayari tumekiwsha
mtengenezea mazingira
mazuri ya kuweza kupokelewa
bila tatizo nchini Iran na
anaweza akageuka kuwa
mwiba kwetu na
kutuchoma.Hatupaswi kumpa
nafasi lazima tuhakikishe
anauawa haraka sana
ikiwezekana kabla
hajakanyaga ardhi ya
Iran.Sidhani kama kuna haja
ya kubishana na
Mossad.Hakuna sababu ya
kumficha Habiba Jawad kwani
ni yeye ndiye aliyesababisha
haya yote yakatokea” akasema
Jason
“Habiba ni mtu
anayefahamu mambo yetu
mengi kwani tumeanza
kushirikiana naye kwa muda
mrefu.Ni mtu ambaye
hatuwezi kumtoa kirahisi kwa
Mossad.Lakini kwa kuwa na
sisi tunahitaji msaada wao basi
tunaweza kufanya kitu
kimoja.Tukubaliane nao
kwamba wamuue Abu Zalawi
na sisi tumuue Habiba
Jawad.Tunao uwezo wa
kumpata Habiba na kumuua
hivyo tufanye kazi hiyo sisi
wenyewe ili wasije
wakagundua mashirikiano
yetu na Habiba” akasema
David.
“Hilo ni wazo zuri David”
akasema Jason kwa sauti
ndogo kisha ukimya ukapita
“Lakini kwa nini tumuue
Habiba Jawad? Amekuwa nasi
kwa muda mrefu na
ametusaidia mambo mengi.Je
hatumuhitaji tena? Akauliza
David
“Habiba Jawad ndiye
aliyetufikisha hapa
tulipofika.Ametufanya
tukaingia katika misheni
ambayo ni sawa na kujifunga
kitanzi shingoni sisi wenyewe
baada ya kumleta kwetu Abu
Zalawi ambaye si gaidi bali ni
jasusi.Naamini hakufanya hivi
kwa bahati mbaya nahisi kuna
jambo wanalipanga kati yake
na Abu Zalawi hivyo lazima
tuwaondoe wote mara moja ili
tuendelee kuwa
salama.Nakuhakikishia David
bila kuwaondoa watu hawa
wawili hatutakuwa
salama.Usihofu kuhusu utajiri
tuliomuwezesha
Habiba,tutatafuta mtu
mwingine wa kumuwezesha na
akatufanyia kazi nzuri kuliko
hata Habiba” akasema Jason
lakini David alionekana
kuzama katika lindi la
mawazo.
“Jason nadhani suala hili
lifike kwanza kwa G20 ili
yafanyike maamuzi.Hili jambo
ni kubwa mno hatuwezi
kufanya maamuzi sisi wawili
pekee wakati tunao wenzetu
wengine.Ikiwezekana kura
inaweza kupigwa kuamua
jambo hili.Nitawakusanya
ndani ya muda mfupi asubuhi
ya leo kisha nitaliwasilisha
kwao jambo hili watalitafakari
na kulifanyia maamuzi na
pengine wanaweza wakawa na
mawazo mengine mazuri
zaidi” akasema David
“Sawa David nenda
kakutane na wajumbe hao
mzungumze na jibu lipatikane
haraka sana ili tujue namna ya
kulishughulikia jambo
hili”akasema Jason na David
akaondoka kwenda kufanya
maandalizi ya kukutana na
wajumbe wa kikundi chao cha
G20 kwa ajili ya kulijadili
suala lile nyeti lililojitokeza
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Bado macho ya SNSA
yalielekezwa katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere wakiendelea kufuatilia
kila kinachoendelea pale
uwanjani.Ilipofika saa sita na
dakika saba yakasikika
maongezi kati ya rubani wa
ndege na waongoza ndege wa
uwanja wa Julius
Nyerere.Ilikuwa ni ndege ya
jeshi la Marekani ikiomba
kutua katika uwanja huo ikiwa
imeleta mahitaji mbalimbali
kwa ajili ya vikosi vya jeshi la
Marekani vilivyoko Tanzania.
Dakika chache baadae
ndege ya jeshi la Marekani
ikatua.
“Yawezekana ndege
iliyoleta kirusi ni hii kwani
imefika kwa muda ule ule
ambao tulitarajia ndege
iliyombeba Sattar ingewasili”
akasema Gosu Gosu
“Tuendelee kufuatilia
tutajua kama ni hii” akasema
Ruby akionekana kuwa na
wasiwasi
Dakika chache toka
kuwasili kwa ndege ile
ukawasili msafara wa magari
ya vikosi vya jeshi la Marekani
vilivyopo Tanzania na kazi ya
upakuzi wa mizigo katika
ndege ile ikaanza.
“Inaonekana ni mizigo ya
kawaida inayohusiana na
wanajeshi” akasema Gosu
Gosu
“Tuendelee kuchunguza”
akasema Ruby wakati mizigo
ikipakuliwa kutoka ndegeni na
kuingizwa katika magari
“Hakuna dalili zozote za
kuwepo Sattar au kirusi katika
ndege hii ya mizigo” akasema
Gosu Gosu lakini hakuna
aliyemjibu watu wote
waliyaelekeza macho yao
katika kamera wakifuatilia kile
kilichokuwa kinaendelea pale
uwanjani.Mizigo iliyokuwa
katika ndege ile ilimalizika na
magari yakajipanga kwa ajili
ya kuondoka.Kiongozi wa
msafara ule akatoa maelekezo
na magari yakaanza kuondoka.
“Hakuna kirusi katika
ndege hii.Hawa watu
wametuc………….” Akasema
Gosu Gosu na Nawal
akamkatisha
“Subiri kwanza Gosu
Gosu.Kuna magari manne
yamebaki uwanjani.Mnadhani
kwa nini yamebaki? Akauliza
Nawal
“Ni kwa sababu bado kuna
kitu wanakisubiri.Yawezekana
wanamsubiri Sattar Sayf Al
Din” akasema Nawal
“Nawal yuko sahihi.Hawa
jamaa wanaonekana kuna kitu
wanakisubiri.Tuendelee
kuwafuatilia tujue kile
wanachokisubiri” akasema
Ruby
“Lakini mbona hakuna
dalili zozote za kuwepo Assad
Ismail hapa
uwanjani?Tulielezwa kwamba
yeye ndiye atampokea Sattar
Sayf Al Din” akasema Gosu
Gosu
“Relax Gosu Gosu”
akasema Ruby
Magari manne ya vikosi
vya jeshi la Marekani
yaliendelea kubaki pale
uwanjani na kwa namna
walivyokaa walionekana kuna
kitu wanakisubiri.
Dakika ishirini baadae
yakasikika mazungumzo kati
ya waongoza ndege wa uwanja
wa Julius Nyerere na Rubani
aliyekuwa akiomba kutua
katika uwanja huo wa ndege
“Hii lazima itakuwa
yenyewe ! akasema Nawal
Dakika chache baadae
ndege ikatua na magari yale ya
jeshi la Marekani yaliyokuwa
yamebaki yakisubiri yakaanza
kuijongelea ndege ile.
“Hii si ndege ya jeshi la
Marekani.Hii ni ndege
inayotumiwa na CIA kupeleka
maafisa wake sehemu mbali
mbali duniani”akasema Nawal
baada ya ndege ile kutua.
“Hii inatupa uhakika
kwamba ndege hii yawezekana
ndiyo imeleta kirusi”akasema
Ruby
Magari yale yalisogelea
ndege ile ambayo mlango wake
ulifunguliwa na baadhi ya
maafisa wa jeshi wakaingia
ndani.Baada ya muda
wakatoka wakiwa
wameongozana na mtu mmoja
aliyebeba masanduku
mawili.Wote mle ndani sura
zao zikaonyesha mabadiliko
baada ya kumshuhudia Yule
mtu aliyekuwa amebeba
masanduku mawili akiwa
ameongozana na maafisa wa
jeshi la Marekani kuwa ni
Sattar Sayf Al Din
“Hatimaye kirusi kimefika
Tanzania” akasema Nawal
Sattar Sayf Al Din
aliongozwa hadi katika
mojawapo ya magari yale na
kuondoka pale uwanjani.
“Nini kinafuata baada ya
kujiridhisha kuwa Sattar
ameingia nchini na muda
wowote wanaweza
wakasambaza kirusi?akauliza
Gosu Gosu
“Huyu Sattar Sayf Al Din
ni mtu ambaye lazima
watamchunga sana kwani
amebeba kitu hatari mno hivyo
basi nina uhakika
watampeleka katika sehemu
maalum watamlinda hadi
watakapomkabidhi kwa Assad
Ismail kwa ajili ya kuanza kazi
ya usambazaji wa kirusi”
akasema Nawal
“Sattar yuko katika
mikono ya vikosi vya Marekani
na yawezekana akapelekwa
katika kambi yao akahifadhiwa
huko na itatuwia ugumu kwetu
kuweza kumpata.Lazima tuje
na mpango kabambe wa
kutuwezesha kuingia katika
kambi ya jeshi la Marekani na
hatimaye kumfikia Sattar na
kuchukua kirusi” akasema
Ruby
“Nina wazo” akasema
Nawal
“Ninyi mna mawasiliano
ya karibu na Rais wa
Tanzania? Akauliza Nawal
“Ndiyo tuna ukaribu
mkubwa na Rais” akajibu
Ruby
“Vizuri.Basi italazimu
kumshirikisha Rais katika
jambo hili” akasema Nawal
“Hapana hatuwezi
kumshirikisha Rais katika
hatua hii.Ni mapema
mno.Tutamjulisha Rais baada
ya kukipata kirusi” akasema
Ruby
“Ruby nisikilizeni”
akasema Nawal
“Tayari tuna uhakika
kwamba Sattar Sayf Al Din
ameingia hapa nchini na
tumemuona akiwa na
masanduku mawili ambayo
tunaamini kirusi kimo ndani
yake.Ili tuweze kujua nyendo
zote za Sattar na mipango yake
yote ya kukisambaza kirusi
hicho ikiwa ni pamoja na kujua
mahala alipo Assad Ismail
lazima kuingia katika vikosi
vya Marekani .Kwa ninyi
itakuwa vigumu kwa sababu si
wamarekani lakini mimi ni
mmarekani hivyo inaweza
kuwa rahisi kwangu.Tufanye
hivi,tuonane na Rais na
aelezwe kila kitu kuhusiana na
kirusi hicho na kitu ambacho
tutamtaka akifanye ni kumuita
kamanda wa vikosi vya
Marekani vilivyoko hapa
nchini na atanikabidhi mimi
kwake akidai kwamba
nimeokolewa na vikosi vya
Tanzania kutoka katika
mikono ya
watekaji.Nitajitambulisha
kama mpiga picha wa
kujitegemea niliyekuja
kutembea Tanzania na
nikajikuta nimekwama katikati
ya machafuko nikatekwa hadi
nilipookolewa na vikosi vya
jeshi la Tanzania nikapelekwa
Dar es salaam.Nikisha
kabidhiwa kwao naamini
watanipeleka katika kambi yao
ambako nitaanza kufanya
uchunguzi kuhusiana na
mahala alipo Sattar na kujua
mipango yote ya kuhusiana na
usambazaji wa kirusi huku
nikiendelea kuwasiliana nanyi”
akasema Nawal
“Nawal huo ni mpango wa
hatari sana” akasema Ruby
“Ni kweli ni mpango wa
hatari sana lakini lazima
tuufanye kwani ndio pekee
utakaotuwezesha kukifuatilia
kirusi na kuzuia mpango wa
kukisambaza” akasema Nawal
“Gosu Gosu una ushauri
gani?Ruby akauliza
“Mimi naona wazo la
Nawal ni zuri tulifanyie kazi ili
aweze kuingia katika kambi ya
vikosi vya Marekani
kumfuatilia Sattar,lakini nina
hofu endapo Rais akifahamu
kuwa Marekani wako nyuma
ya haya yote yanayoendelea
hapa nchini anaweza
akapandwa na hasira na
kuvitaka vikosi vya Marekani
vindoke haraka sana na hivyo
tukashindwa kukamilisha
operesheni yetu” akasema
Gosu Gosu
“Anachokisema Gosu Gosu
ni kitu cha kweli.Tunapaswa
kuwa makini sana
tunapoamua kumueleza Rais
kuhusu jambo hili.Nashauri
tumuombe Rais akukutanishe
na mkuu wa vikosi vya
Marekani hapa nchini bila
kumueleza chochote
kuhusiana na operesheni
wanayoiendesha Marekani
hapa nchini hadi hapo
tutakapokuwa tumepata
taarifa za kutosha” akasema
Ruby wakajadiliana kwa muda
wakakubaliana halafu Ruby
akampigia simu Dr Fabian
Kelelo akamuomba waonane
kwa ajili ya suala muhimu na
Dr Fabian akamtaka aende
ikulu.
Kutoka ofisi kuu za SNSA
hadi ikulu si mbali hivyo
iliwachukua dakika kama kumi
kufika ikulu
“Ruby karibu
sana.Mnaendeleaje huko
katika idara yenu?akauliza Dr
Fabian baada ya akina Ruby
kuwasili
“Tunaendelea vyema
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby na kunyamaza kidogo
halafu akasema
“Mheshimiwa Rais huyu
anaitwa Chloe Bennet
anatokea Marekani” akasema
Ruby na Nawal akasimama
akaenda kumpa mkono Rais
“Karibu sana Tanzania
Chloe” akasema Dr Fabian
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akasema
Nawal
“Mheshimiwa Rais Chloe
yuko hapa kwa jambo
mahsusi.Kuna misheni
muhimu anasaidiana nasi”
akasema Ruby
“Naweza kufahamu ni
misheni gani inayoendelea kati
yenu na Chloe? Akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninaomba nisikwambie kwa
sasa hadi hapo tutakapokuwa
tumeikamilisha misheni hiyo”
“Ruby hapo ndipo huwa
unaniudhi.Kila mara
ninapokuuliza kinachoendelea
SNSA jibu lako limekuwa hilo
hilo moja kwamba huwezi
kunieleza kwa sasa hadi hapo
baadae?Kwa nini hutaki
kuniweka wazi mambo gani
yanayoendelea SNSA? Kuna
ugumu gani kunieleza kile
mnachokifuatilia? Don’t you
trust me? Akauliza Dr Fabian
kwa sauti ya ukali kidogo
“Ninakuamini
mheshimiwa Rais” akajibu
Ruby
“Kama unaniamini kwa
nini unasita kunieleza ukweli
wa kile kinachoendelea
SNSA?Kwa nini unafanya
siri?akaendelea kuuliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninakuomba unipe muda
kidogo tu halafu nitakuja
kwako na kukueleza kila
kitu.Ni mambo mazito
kidogo.Kwa mchana huu
nimekuja kwako kuomba
msaada” akasema Ruby.Dr
Fabian akachukua kitambaa
akafuta jasho usoni halafu
akasema
“Ruby naomba nikuweke
wazi kwamba sijapendezwa na
tabia hii ya kunificha mambo
yanayoendelea katika idara
yako.Usisahau kwamba mimi
ndiye mkuu wa SNSA hivyo
napaswa kufahamu kila
kinachoendelea katika idara
hiyo.Nini unataka
nikusaidie?akauliza Dr Fabian
“Ninahitaji huyu
mwenzangu haa Chloe
aunganishwe na vikosi vya
jeshi la Marekani vilivyoko
hapa nchini.kuna misheni ya
muhimu sana tunataka
kuifanya”akasema Ruby
“Ruby unanipa wakati
mgumu sana.Hutaki kunieleza
chochote kinachoendelea na
wakati huo huo unataka
nimuunganishe mwenzako na
vikosi vya Marekani vilivyoko
hapa nchini.Kuna nini
mnataka kukichunguza?
Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
naomba uniwie radhi tena
katika jambo hilo” akasema
Ruby na Rais akagonga meza
kwa hasira
“Ruby nimechoka
nawe.Ninawezaje kukusaidia
bila kujua kile mnachotaka
kukifanya kwa vikosi vya
Marekani vilivyoko hapa
nchini.Unachotaka nikifanye
kinaweza kuharibu mahusiano
mazuri yaliyopo baina yetu na
Marekani.Tunauheshimu sana
mchango wao mkubwa
walioutoa.Mara tu vurugu
zilipoibuka ni Marekani
waliotuma vikosi vyao kwa
haraka sana kuja nchini
kushirikiana na vikosi
vyetu.Unaponitaka
nishirikiane nanyi kuweka
pandikizi katika vikosi vya
Marekani lazima unipe sababu
ya msingi ya kufanya hivyo na
kama utaendelea na majibu
yako ya kunieleza baadae
sintakuwa na msaada
kwako.Nitakuachia ufanye kazi
zako wewe mwenyewe !
akafoka Dr Fabian
“Ruby kuna nini?akauliza
Nawal ambaye hakufahamu
kile walichokuwa
wakikizungumza Dr Fabian na
Ruby.
“Rais anahitaji kufahamu
dhumuni la kutaka uingie
katika vikosi vya Marekani”
akasema Ruby
“Hakuna namna Ruby
mueleze ukweli” akasema
Nawal.Ruby akafungua mkoba
wake akatoa faili akalifunua na
kutoa picha moja akampatia
Rais
“Anaitwa Sattar Sayf Al
Din.Huyu anatokea kundi la
kigaidi la IS na yuko hapa
nchini” akasema Nawal na
kufungua picha za video
akamuonyesha Rais namna
Sattar alivyokuwa akishuka
katika ndege
“Sijakuelewa
Ruby.Umesema huyu mtu
anatokea kundi la IS lakini
hapa ninamuona akishuka
katika ndege akiwa
ameongozana na maafisa
kutoka jeshi la
Marekani.Sielewi
kinachoendelea hapa !
akasema Dr Fabian
“Ndiyo maana
nikakuomba mheshimiwa Rais
nipe muda kwani jambo hili ni
kubwa na yawezekana
nikikueleza leo hii usinielewe”
akasema Ruby
“Make me understand !
akasema kwa ukali Dr Fabian
halafu ukapita ukimya mfupi
“I’m sorry Ruby
nimeshindwa kujizuia
kukasirika lakini ninahitaji
sana kujua kile kinachoendelea
hivi sasa.Kama huyu mtu ni
gaidi kwa nini yuko na vikosi
vya Marekani? Amekamatwa?
Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais mtu
huyu kama nilivyokueleza ni
gaidi na amekuja hapa nchini
kwa ajili ya kutekeleza
shambulio la
kigaidi.Mheshimiwa Rais
masanduku mawili
uliyomuona ameyabeba wakati
akishuka ndegeni yana kirusi
ambacho amekuja
kukisambaza hapa nchini”
“Kirusi? ! DrFabian
akastuka
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Kirusi cha aina gani
hicho? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
naomba na mimi nizungumze
kidogo.Kama Ruby
alivyonitambulisha kwako
ninaitwa Chloe Bennet
ninatokea shirika la ujasusi la
Marekani CIA.Tulipata taarifa
za kuwepo kwa shambulio la
kirusi hapa nchini Tanzania
ambalo linategemewa
kufanywa na kikundi cha
kigaidi cha IS.Mtu ambaye
umeonyeshwa na Ruby muda
mfupi uliopita ni kweli
amekuja hapa nchini kwa ajili
ya kutekeleza shambulio
hilo.Kwa ufupi tu ni kwamba
kirusi hicho ambacho
kinatazamiwa kusambazwa ni
kirusi hatari cha maangamizi
makubwa na kinachoua ndani
ya muda mfupi na husambaa
kwa njia ya hewa.Mheshimiwa
Rais mimi na wenzangu akina
Ruby tunataka kuzuia
shambulio hilo lisitokee lakini
kwa bahati mbaya mtu ambaye
amekuja kufanya shambulio
hilo anapata hifadhi katika
kambi ya vikosi vya jeshi la
Marekani ndiyo maana
tumekuja kwako kuomba
msaada wako ninataka
uniunganishe na kamanda
mkuu wa vikosi vya Marekani
vilivyoko hapa nchini ili
niweze kuingia katika kambi
hiyo kufanya uchunguzi huku
nikiwasiliana na wenzangu na
kujua mipango yote
inayopangwa kuhusiana na
usambazaji wa kirusi hicho”
akasema Nawal
“Mnazidi
kunichanganya.Nataka kujua
nani hasa anayetaka
kusambaza kirusi hicho?Ni
gaidi huyu mliyenionyesha au
ni wanajeshi wa Marekani?
Akauliza Dr Fabian
“Kirusi kimepangwa
kusambazwa na Sattar ambaye
ni gaidi kutoka kundi la kigaidi
la IS lakini anapata msaada
kutoka kwa vikosi vya
Marekani vilivyoko hapa
nchini na ndiyo maana
umeona katika video
tulizochukua kutoka uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere
Sattar akipokewa na maafisa
kutoka vikosi vya jeshi la
Marekani walioko hapa
nchini” akajibu Nawal
“Nini hasa sababu ya
kutaka kusambaza virusi
hivyo?akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais suala
hili ni pana sana na ndiyo
maana ninaendelea kusisitiza
nipe muda nitakuja kwako na
maelezo kamili ya kila
kinachoendelea hapa nchini
lakini kwa leo ninataka
unisaidie hicho
tulichokuomba.Ninataka
kumpandikiza Chloe katika
kambi ya vikosi vya Marekani
ili aweze kuchunguza na kujua
mahala alipo Sattar na kirusi
alichokuja nacho” akasema
Ruby
“Ruby ninashindwa
nifan…..” akasema Dr Fabian
lakini Ruby akamkatisha
“Mheshimiwa Rais
ninaomba uniamini katika
hili.Najua kuna mambo mengi
bado uko gizani na nitakuja
hapa kwako kukueleza kila kitu
lakini naomba kama hujawahi
kuniamini basi niamini katika
hili.Nchi iko katika hatari
kubwa na ndiyo maana mimi
na wenzangu tumeamua
kufanya jambo hili la hatari
kubwa kwa ajili ya kuiepusha
nchi na hatari
iliyopo.Tunakuomba sana
msaada wako mheshimiwa
Rais” akasema Ruby
“Nini unataka
nikifanye?akauliza Dr Fabian
baada ya kutafakari kwa
muda,Ruby akamuelekeza
namna walivyoupanga mpango
ule na kitu gani anatakiwa
kufanya Dr Fabian.
Baada ya kupewa
maelekezo ya kile
anachotakiwa kukifanya bila
kupoteza muda Dr Fabian
akachukua simu akampigia
simu waziri wa ulinzi na
kumpa maelekezo kwamba
anamuhitaji mkuu wa vikosi
vya Marekani vilivyoko nchini
Tanzania haraka sana pale
ikulu ana mazungumzo naye.
DAKIKA ISHIRINI BAADAE
Helkopta ya jeshi la
Marekani iliyombeba Jeneral
William Marshall mkuu wa
vikosi vya jeshi la Marekani
vilivyoko nchini
Tanzania,ilitua katika viwanja
vya ikulu jijini Dare s
salaam.Hii ni kufuatia ombi la
Rais la kutaka kuonana na
mkuu huyo.
Jenerali William akashuka
katika helkopta akapokewa na
walinzi wa Rais
wakamuongoza kuelekea
ndani kwa ajili ya kukutana na
Rais.Akiwa amevaa sare za
jeshi la Marekani alikaribishwa
sebuleni na baada ya dakika
kadhaa rais Dr Fabian
akajitokeza akiwa
ameongozana na
Nawal.William akasimama na
kutoa salamu ya kijeshi kwa
Rais kisha Rais akampa mkono
na kumkaribisha.
“Ahsante sana kwa kufika
kwa haraka Jenerali William
baada ya kupokea wito wangu”
akasema Dr Fabian
“Nimeelekezwa na waziri
wa ulinzi wa Tanzania ambaye
tunawasiliana mara kwa mara
kwamba unanihitaji mara
moja hivyo nikalazimika
kuacha kila nilichokuwa
nakifanya nije nikusikilize
mheshimiwa Rais” akasema
Jenerali William
“Karibu sana Jenerali
William.Kwanza kabisa
ninataka kujua maendeleo ya
vikosi vya Marekani hapa
nchini.Mnaendeleaje na
majukumu yenu?
“Tunaendelea vizuri sana
mheshimiwa Rais
tukishirikiana na vikosi vya
Tanzania na kwa kiasi kikubwa
ninaweza kusema kwamba
tumefanikiwa kudhibiti
vurugu.Kwa sasa tunaendelea
na doria za ardhini na angani
kuhakikisha hakuna tena
makundi yoyote yanayoleta
uvunjifu wa amani” akasema
William
“Tunawashukuru sana
William kwa kazi kubwa
mliyoifanya ya kuhakikisha
amani inarejea nchini.Hata
hivyo kuna jambo lingine
nimekuitia hapa mchana huu”
akasema DrFabian na
kumgeukia Nawal
“Anaitwa Chloe Bennet ni
raia wa Marekani ambaye
anajishughulisha na upigaji wa
picha na wakati machafuko
yalipoanza alikuwa katika
mbuga ya Serengeti akipiga
picha na akajikuta akinasa kati
kati ya mapigano.Alitekwa na
kundi la vijana akashikiliwa
yeye na wenzake wanne raia
wa Kenya hadi jana
walipokombolewa na vikosi
vya jeshi na kuletwa hapa Dar
es salaam.Nimekuita ili
nimkabidhi kwako uhakikishe
usalama wake kwa wakati huu
ambapo hakuna
ubalozi.Nilitaka kumsafirisha
kurejea Marekani lakini Chloe
akaniomba aendelee kubaki
Tanzania kwani anategemea
kuendelea na zoezi lake la
upigaji wa picha pale vurugu
zitakapokuwa
zimemalizika.Ninamkabidhi
kwako uhakikishe anakuwa
salama na pale vurugu
zitakapokuwa zimemalizika
basi ataendelea na kazi zake”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninakushukuru sana kwa
msaada mkubwa uliomsaidia
huyu mwenzetu nakuahidi
atakuwa salama katika
usimamizi wangu hadi pale
vurugu zitakapokoma kabisa”
akasema William
“Chloe nakutakia
mapumziko mema na pale
utakapokuwa tayari kwenda
kuendelea na shughuli zako za
upigaji picha njoo uniage
tafadhali na ninakuhakikishia
kwamba vifaa vyako vyote
vilivyopotea nitavigharamia
utapata vipya” akasema Dr
Fabian Nawal akasimama
akamfuata
“Nakushukuru sana
mheshimiwa Rais kwa msaada
mkubwa
ulionipatia.Ninakuhakikishia
kwamba nitakapokuwa tayari
kwenda kuendelea na shughuli
zangu nitakuja kukuaga”
akasema Nawal akimshukuru
Rais halafu akaenda
kusalimiana na William Rais
akawaaga wakaondoka
kuelekea katika helkopta ya
jeshi la Marekani wakaingia
helkopta ikapaa na kuondoka
maeneo ya ikulu.Dr Fabian
akamfuata Ruby aliyekuwa
katika sebule nyingine
“Tayari nimetekeleza
ulivyoniomba na mwenzako
amekwisha ondoka na mkuu
wa vikosi vya Marekani
vilivyoko hapa Tanzania.Ruby
mna uhakika na hiki
mnachotaka
kukifanya?Akauliza Dr Fabian
“Ninakushukuru sana
mheshimiwa Rais kwa
kutusaidia jambo hili.Hii ni
njia pekee ya kutuwezesha
kuingia katika kambi ya jeshi
la Marekani na kumfuatilia
Sattar na kuzuia mpango wa
kusambaza kirusi hapa
Tanzania” akasema Ruby
“Ruby nataka kufahamu
kwa kina kuhusiana na hiki
kirusi.Mna hakika kweli kuna
kirusi kinataka kusambazwa
hapa nchini? Akauliza Dr
Fabian
“Kirusi kipo kweli
mheshimiwa Rais na
tunaendelea kukifuatilia ili
kuzuia mpango wa
kukisambaza” akajibu Ruby
“Ruby hili si jambo la
kufanyia mchezo.Kama una
uhakika kuna kirusi hatari
ambacho kinaweza
kusababisha maangamizi
makubwa hapa nchini
tunatakiwa kuanza kujiandaa
ili pale mpango wenu wa
kuzuia kisisambazwe
ukishindwa kufanikiwa tuwe
na uhakika wa kuwakinga watu
wetu” akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais kwa
sasa suala hili litabaki siri yetu
na hatakiwi mtu mwingine
yeyote kufahamu kwani
inaweza kuzuka taharuki
kubwa na kuvuruga uchunguzi
wetu.Ninakuhakikishia
mheshimiwa Rais kwamba
tutafanya kila lililo ndani ya
uwezo wetu kuhakikisha kirusi
hicho hakisambazwi hapa
Tanzania” akasema Ruby
“Ruby ninataka kufahamu
je vikosi vya Marekani
vinahusika katika jambo hili?
Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais kama
nilivyokueleza awali kwamba
hili ni jambo pana lakini
nitakuja kukueleza kila
kitu.Naomba nipe muda
ninakuahidi nitakuja nikiwa na
maelezo ya kutosha kuhusiana
na jambo hili” akasema Ruby
lakini Dr Fabian akaonekana
bado ana wasiwasi
mwingi.Baada ya ukimya
mfupi akasema
“Ruby umenitaka
nikuamini katika suala hili na
mimi ninalazimika kufanya
hivyo lakini tambua ya
kwamba maisha ya watanzania
yako mikononi mwako hivyo
kwa namna yoyote ile mpango
huo wa kusambaza kirusi
katika ardhi yetu haupaswi
kufanikiwa.Umenielewa
Ruby?akauliza Dr Fabian
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais”akajibu
Ruby huku Dr Fabian
akimtazama kwa wasiwasi
“Ruby please swear to me
that you won’t let them win !
akasema Dr Fabian.Ruby
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Mr President I swear I
wont let them win ! akasema
Ruby
“Ahsante sana kwa
kunihakikishia hilo
Ruby.Narudia tena
kukusisitiza kwamba maisha
ya watanzania yapo mikononi
mwako.Kama kuna msaada
wowote utauhitaji muda
wowote hata kama ni vikosi
vya jeshi nitaarifu na mimi
nitakusaidia”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais nitafanya
hivyo” akasema Ruby kisha
akaagana na Dr Fabian
akaondoka kurejea katika ofisi
zao
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 2
Helkopta iliyowabeba
akina Nawal ilitua katika
kambi ya jeshi ya vikosi vya
Marekani iliyopo kandoni mwa
bahari.Kulikuwa na kambi
mbili za vikosi vya Marekani
jijini Dar es salaam,kambi
moja kubwa ikiwa katika
uwanja wa Uhuru ambako
ndiko vifaa vyote vilikuwa
vinahifadhiwa na kambi
nyingine ilikuwa ufukweni
mwa bahari ya Hindi.
Jenerali William alianza
kushuka katika helkopta
halafu akafuatiwa na Nawal
wakaongozana kuelekea katika
kontena lenye rangi nyeupe
ambalo lilikuwa linatumiwa
kama ofisi ya Jenerali
William.Ndani ya kontena lile
kulikuwa na ubaridi wa
kutosha kutokana na kiyoyozi.
“Chloe karibu sana.Hii ni
ofisi yangu” akasema Jenerali
William na kumkaribisha
Nawal katika chumba cha
kupumzikia.
“Pole sana Chloe kwa
masahibu yote yaliyokukuta”
“Ahsante sana Jeneral
nimekwisha poa” akajibu
Nawal na mara wakaingia
watu wawili na Jenerali
William akamtambulisha
Nawal kwao halafu
akamuomba aendelee
kupumzika kwani alikuwa na
mazungumzo na watu wale
walioingia mle ofisini.Jenerali
William alitoka na wale
wanajeshi wawili Nawal naye
akasimama na kutoka ndani ya
kile chumba akachungulia nje
akamuona Jenerali William na
wale jamaa wakielekea sehemu
nyingine.Haraka haraka
akarejea katika kile chumba
cha mapumziko na kuchukua
simu aliyopewa SNSA
akampigia Ruby
“Nawal ! akasema Ruby
baada ya kupokea simu
“Ruby tayari nimekwisha
ingia katika kambi yao iliyoko
ufukweni mwa bahari.Kwa
sasa niko katika ofisi ya
Jenerali Wiliam Marshall”
akasema Nawal
“Safi sana Nawal.Una
nafasi ya kufanya chochote
kwa muda huu?
“Jeneral William ametoka
na sifahamu atachukua muda
gani kurejea,ninataka kutega
kamera”
“Sawa Nawal.Hakikisha
unatega kamera na kifaa cha
kunasa sauti katika ofisi hiyo
ili tuweze kunasa mazungumzo
na kufuatilia kila
kinachoendelea hapo ofisini”
akasema Ruby
“Ninataka nijitahidi
nitumie nafasi hii ndogo
niweze kutekeleza hilo”
akasema Nawal na kukata
simu akafungua begi lake dogo
la mgongoni alilokuwa nalo
akatoa vifaa fulani ambavyo ni
kamera ya siri na kifaa kingine
cha kunasa maongezi.Akaenda
tena kuchungulia katika
dirisha kama kuna mtu
anaelekea upande ule lakini
hakukuwa na mtu yeyote
aliyekuwa anaelekea pande
zile.Haraka haraka akaelekea
katika mlango uliokuwa
umefungwa akausogelea akiwa
amevaa glovu mkononi
akakiminya kitasa mlango
ukafunguka akaingia ndani ya
ofisi.Mezani kulikuwa na kibao
Gen.William Marshall.
“Hii ndiyo ofisi yake”
akawaza Nawal kisha akatega
kifaa cha kunasa mazungumzo
chini ya meza,halafu akatega
na kamera ya siri katika kabati
la vitabu.Wakati akiendelea na
kutega kamera ile ya siri mara
akasikia vishindo vya mtu
haraka haraka akaenda
kujificha chini ya meza.Mlango
wa ofisi ya Jenerali Willium
ukagongwa Nawal mwili
ukamtetemeka.Mtu aliyegonga
mlango akakiminya kitasa na
kuufungua mlango
akachungulia ndani halafu
akaufunga mlango ule
akaondoka zake.Haraka
haraka Nawal akamalizia
kutega kamera ile ya siri halafu
akatoka kwa tahadhari kubwa
akarejea mahala ambako
aliachwa apumzike.Akachukua
simu na kumpigia simu Ruby
akamjulisha kwamba tayari
amekwisha tega kamera na kile
kifaa cha kunasa
maongezi.Tayari Ruby
alikwisha anza kupata picha za
kamera kutoka katika ile
kamera aliyoitega Nawal.
Dakika tano toka Nawal
atoke katika ofisi ya Jenerali
William akasikia vishindo vya
hatua za mtu na akajitokeza
Jenerali William
“Samahani Chloe kwa
kukuacha peke yako” akasema
Jenerali William na kuketi
sofani
“Bila samahani Jenerali
William” akasema Nawal
“Mimi ndiye mkuu wa
vikosi vyote vya Marekani
vilivyopo hapa Tanzania hivyo
ninakuwa na mambo mengi ya
kushughulikia” akasema
Jenerali William
“Kwa kuwa hapa kambini
ni sehemu yenye shughuli
nyingi,utapelekwa katika
nyumba ninakoishi mimi na
utaishi nasi hapo hadi pale
mambo yatakapotulia.Ubalozi
wetu hapa Dar es salaam
umelipuliwa hivyo sina
sehemu nyingine ya
kukupeleka zaidi ya mahala
ninapoishi.Usihofu ni sehemu
salama sana” akasema Jenerali
William
“Ninashukuru sana
Jenerali William kwa msaada
huu mkubwa” akasema Nawal
na Jeneral William akasimama
“Pale kambini utapatiwa
kila utakachokihitaji.Mimi
nitakuja jioni baada ya
kumaliza shughuli zangu na
tutapata wasaa wa
kuzungumza zaidi” akasema
Jenerali William akamuaga
Nawal akaondoka.
Dakika chache baada ya
Jenerali William kuondoka
akaingia mwanajeshi mmoja
akajitamblisha kwa Nawal
kwamba ametumwa na
Jenerali William kumpeleka
mahala anakoishi.Nawal
akavaa begi lake la mgongoni
kisha akaongozana na Yule
mwanajeshi hadi katika gari la
jeshi akaingia wakaondoka
kuelekea anakoishi Jenerali
William
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 3
Nawal alifikishwa katika
makazi ya maofisa wa vikosi
vya Marekani waliokuwa
wakiishi katika mojawapo ya
nyumba za wageni muhimu wa
serikali.Alipokewa na
wahudumu ambao ni
wanajeshi pia na tayari taarifa
zake walikwisha zipata hivyo
basi wakamuhudumia kwa
chakula halafu akaenda
kupumzika.Ilikuwa ni nyumba
ya kifahari sana.Nawal
akasimama dirishani
akatazama nje kulikuwa na
ulinzi mkali karibu kila kona
ya jumba lile kulikuwa na
mlinzi mwenye silaha,juu ya
paa vile vile kulikuwa na
wanajeshi wakilinda na katika
geti la kuingilia ndani ya
nyumba ile kulikuwa na ulinzi
mkali na kila gari lililoingia
lilikaguliwa kama limebeba
mlipuko
“Jumba la kifahari sana
hili na lenye ulinzi mkali mno
hata hivyo ulinzi huu hauwezi
kunizuia kutekeleza jukumu
langu.Lazima tukimbizane na
muda na kuhakikisha
tunafahamu mahala kilipo
kirusi.Mpaka mapambazuko
ya kesho lazima tayari tuwe na
kirusi mkononi” akawaza
Nawal halafu akachukua simu
na kumpigia Ruby akamjulisha
kuwa tayari amefika katika
makazi ya maofisa wa jeshi la
Marekani.
“Tumekuwa tunafuatilia
ile kamera uliyoifunga katika
ofisi ya Jenerali William lakini
toka wakati ule hajarejea
katika ofisi yake.Tunaendelea
kumfuatilia na kama kuna kitu
chochote tutakipata
nitakujulisha mara
moja.Hakikisha unachunguza
kila kinachoendelea katika
nyumba hiyo na kama
ikiwezekana tega kamera na
kifaa cha kunasa maongezi ili
tujue William anawasiliana na
nani na wanaongea nini.Nina
uhakika mkubwa lazima
anafahamu kinachoendelea
kuhusiana na kirusi
alichokileta Sattar”
“Sawa nitajitahidi kufanya
hivyo Ruby” akasema Nawal
“Kumbuka kuwa makini
sana kwani wakikugundua hao
jamaa lazima watakuua” Ruby
akasisitiza
“Ninalifahamu hilo Ruby
na mpaka hapa bado hakuna
tatizo lolote” akasema Nawal
“Kwa kutumia simu yako
tayari tumefahamu mahala
ulipo hivyo tunarusha drone
yetu mahala hapo ili
kuichunguza zaidi na kujua
kila kinachoendelea kwa nje”
akasema Ruby na kuagana na
Nawal.
TEHRAN - IRAN
Zimekwisha pita saa tisa
toka Mathew Mulumbi na
wenzake sita walipoiteka
ndege iliyokuwa inawapeleka
nchini Marekani.Ndani ya
ndege ilikuwa ni furaha
tupu.Raia wale wa Iran
waliimba na kucheza kwa
furaha wakifurahia kurejea
nyumbani baada ya miaka
kadhaa ya kuishi katika mateso
makubwa.Ilikuwa ni kama
muujiza kwao pale ndege
ilipobadili uelekeo na kuelekea
nchini Iran.Hawakutegemea
kama jambo hili
lingewezekana siku moja
waweze kurejea nyumbani.
Wakati ndege ikiendelea
kupasua anga kuelekea nchini
Iran,Mathew akachukua zamu
ya kuwalinda mateka wao
waliokuwa wamefungwa pingu
zile ambazo Mathew na
wenzake walikuwa
wamefungwa.
“Mnatupeleka
wapi?akauliza mmoja wa
mateka ambaye ni rubani wa
ndege
“Mnakwenda nchini Iran
ambako mtakabidhiwa kwa
mamlaka husika na
yawezekana hamtaweza
kuziona tena familia zenu”
akasema Mathew huku
akiichezea bastora
yake.Mmoja wa wale marubani
akainamisha kichwa na
kumwaga machozi
“Tafadhali msitupeleke
Iran watatuua.Uhasama wa
Iran na Marekani ni mkubwa
na watu wale ni makatili
wanaweza kubwa watatukata
vichwa ! akasema mmoja wa
walinzi wale
“Taifa lenu ndiyo taifa
katili kabisa duniani kuliko
yote.Hawa raia wa Iran ambao
bado hawaamini kama
wanarejea tena nyumbani
kwao walikamatwa na
kufungwa bila kuwa na
hatia.Wameteswa sana na
kilichokuwa kinafuata ni
kupelekwa Marekani
kuuawa.Huu ni ukatili
uliopitiliza.Machafuko
yanayoendelea eneo la Afrika
Mashariki hivi sasa ni nchi
yenu ndiyo imeyaratibu kwa
lengo la kujipatia mafuta
kutoka Uganda.Wakati damu
ya watu ikimwagika kila
uchao,tani na tani za mafuta
zinamiminika Marekani.Huu
ni zaidi ya ukatili.Marekani na
wamarekani wanastahili
adhabu kali ! akasema Mathew
kwa ukali
“Wewe ni gaidi na
umelipua ubalozi wa Marekani
jijini Dar es salaam unadhani
kwa hiki ulichokifanya
utakuwa salama? Akauliza
mmoja wa walinzi akimtazama
Mathew kwa hasira
“Nakuhakikishia
hautakuwa salama.Marekani
haijawahi kushindwa na gaidi
yeyote.Utasakwa kwa maisha
yako yote hadi tuhakikishe
umekamatwa na kupata
adhabu unayostahili kwa
unyama ulioufanya ! akasema
yulemlinzi lakini Mathew
hakumjibu kitu
Ndege ilikaribia kuingia
katika anga la Iran na Abdu
Razaq aliyekuwa anaiongoza
ndege ile akawaita wenzake na
kuwajulisha kuwa wanakaribia
kuingia katika anga la
Iran.Abdu Razaq akabonyeza
kifaa ambacho walikizima pale
walipobadili uelekeo wa ndege
ambacho kingewawezesha
kuwasiliana na waongoza
ndege na vile vile kuonekana
katika rada za Iran.
Ndege iliingia katika anga
la Iran na kuanza kuonekana
katika rada za Iran. Abdu
Razaq akajitambulisha kuwa
wao ni raia wa Iran lakini
walikuwa na ndege ya
Marekani.Halikuwa jambo
jepesi kuwaamini na ndani ya
muda mfupi wakajikuta
wamezingirwa na ndege nane
na kivita za Iran
zikiwasindikiza kuelekea
katika uwanja wa ndege wa
kijeshi jijini Tehran.
Kwa kufuata maelekezo
waliyopewa na waongoza
ndege Abdu Razaq aliiongoza
ndege hadi katika uwanja wa
kijeshi uliopo nje kidogo ya jiji
la Tehran huku ikiendelea
kusindikizwa na ndege za
kivita za Iran.Mara tu ndege ile
iliposimama ilizingirwa na
wanajeshi wenye silaha.Abdu
Razaq na wenzake
wakakumbatiana kwa furaha
baada ya ndege
kusimama.Walikuwa
nyumbani.Wote kwa pamoja
wakamshukuru Mathew kwa
ujasiri wake uliosababisha wao
wakawa huru tena.
Mlango wa ndege
ukafunguliwa na Yasser Wazir
akawa ni mtu wa kwanza
kushuka ndegeni.Akashuka
ngazi haraka haraka na
kukanyaga ardhi akainama
akasujudu.Wenzake nao
wakashuka na kufanya kama
alivyofanya Yasser.Uwanjani
pale alikuwepo Meja Jenerali
Farhad Karvan mkuu wa
majeshi wa Iran ambaye alifika
kuwapokea raia wale wa Iran
ambao waliaminika tayari
wamekwisha uawa.Ulikuwa ni
mshangao kwa wote
waliokuwepo pale uwanjani
baada ya kuwaona tena
wenzao wakishuka ndegeni
wote wakiwa hai japo
walikuwa wamedhoofika
sana.Meja Jenerali Farhad
akawakaribisha tena
nyumbani
Wakati salamu zikiendelea
katika mlango wa ndege
akajitokeza Mathew Mulumbi
na kuwafanya watu wote
wageuke kumtazama.
“Na Yule ni nani?akauliza
Meja Jenerali Farhad Karvan
“Yule ni mtu muhimu
sana.Anaitwa Abu Zalawi
ndiye ametuwezesha
tukanyage tena katika ardhi ya
nyumbani” akasema Yasser
Wazir
“Huyu mbona kama……”
akasema Meja Jenerali Farhad
baada ya kumtazama Mathew
kwa makini lakini Yasser
akamkatisha
“Anaitwa Abu Zalawi ndiye
aliyelipua ubalozi wa Marekani
jijini Dar es salaam.Huyu
ndiye aliyepambana na
kuhakikisha tunafanikiwa
kuidhibiti ndege na kuibadili
uelekeo kuja
nyumbani.Naweza kusema
kwamba bila yeye
tusingefanikiwa kukanyaga
tena ardhi ya nyumbani
tulikuwa tunaelekea
kuuawa.Ndani ya ndege kuna
walinzi tumewashikilia mateka
ambao wote ni raia wa
Marekani ” akasema Yasser.
Meja Jenerali Farhad
akatoa maelekezo Mathew
Mulumbi akachukuliwa
akaingizwa katika gari na
kuondolewa haraka pale
uwanjani.Farhad akiwa
ameongozana na Yasser
wakaingia ndegeni na
kuwashuhudia wale mateka
waliokuwa wamefungwa
pingu.Akatoa maelekezo na
mateka wale wakafunguliwa
pingu kisha wakashushwa
ndegeni na kuingizwa katika
gari la jeshi na kupelekewa
mahala alikoelekeza.Yasser na
wenzake nao pia wakaingizwa
katika gari maalum na
kupelekwa kwanza katika
hospitali ya jeshi kwa ajili ya
kuchuguzwa afya zao kabla ya
kuruhusiwa kukutana na
familia zao.Hakuna aliyejua
mahala alikopelekwa Mathew
Mulumbi japo Meja Jenerali
Farhad aliwahakikishia
kwamba amepelekwa sehemu
salama
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Kitendo cha Abdu Razaq
kuwasha tena kifaa
kilichowawezesha kuwasiliana
na waongoza ndege wa Iran na
vile vile kuiwezesha ndege
kuanza kuonekana katika rada
kiliwawezesha mamlaka za
Marekani waliokuwa
wakiitafuta ndege hiyo kuiona
na kufuatilia uelekeo wake na
wakagundua ilikuwa inaelekea
nchini Iran
Taarifa hiyo ya ndege
iliyopotea kuonekana ikielekea
nchini Iran iliwafikia G20
wakiwa katika kikao cha
kujadili mapendekezo ya mkuu
wa CIA Jason Washington ya
kutaka Abu Zalawi auawe
baada ya kujulikana kuwa si
gaidi bali ni jasusi akitokea
Tanzania na si Saudi Arabia
kama walivyoelezwa na Habiba
Jawad.Kikao kilikuwa kizito na
kilichukua muda mrefu
kutokana na wengi wa
wajumbe kutokukubaliana na
wazo la kutaka kumuua
Mathew Mulumbi kabla
hajamaliza kazi aliyotumwa
kuifanya.
David Walker aliyepigiwa
simu na Jason Washington
kumjulisha kwamba ndege
tayari imeingia katika anga la
Iran,aliwapa wenzake taarifa
zile.
“Hizi si taarifa za kustusha
wala kushangaza kwani
tulitegemea jambo hilo
kutokea kutokana na mipango
mizuri tuliyokuwa tumeiweka.
Suala mezani bado ni
kuhusiana na Abu Zalawi
ambaye limetolewa pendekezo
la kuuawa baada ya kujulikana
kuwa si gaidi kama
tulivyoaminishwa na Habiba
Jawad.Tunatakiwa kupata
muafaka katika jambo hili
haraka” akasema David
Walker
“Binafsi baada ya
kuwasikiliza kwa muda mrefu
sijaona bado sababu ya msingi
ya kutaka kumuua Abu Zalawi
hata kama tumegundua si
gaidi.Mpaka hatua hii
hajaonyesha dalili zozote
mbaya na amevumilia mateso
makali kwa ajili ya kuitekeleza
misheni hii
aliyopewa.Nashauri tumuache
aendelee na misheni yake
kwani mahala alipofika ni
muhimu sana.Pale
atakapokuwa amekamilisha
misheni yake ndipo tumuue
lakini kwa sasa tutafanya kosa
kubwa kumuua” akasema
Willie Simmons ambaye
alikuwa kimya kwa muda
mrefu wa kikao kile.Wajumbe
wengine wakaonekana
kumuunga mkono
“Kuna tatizo hapa ambalo
wengi hamtaki kuliona.Huyu
Abu Zalawi au Mathew
Mulumbi ambaye tumemtuma
akatekeleze kazi yetu nchini
Iran anatokea Tanzania na
tayari anafahamu kuwa ni sisi
tunaohusika na vurugu zile za
kidini zilizotokea nchini
Tanzania kwa lengo la
kuchukua mafuta kutoka
nchini Uganda.Kama
mtakumbuka wakati
tunamueleza kuhusu sisi
tulimueleza sehemu mbali
mbali ambazo tumetengeneza
machafuko na mojawapo ikiwa
ni Tanzania.Kwa namna
yoyote ile huyu mtu lazima
atakuwa na hasira na
sisi.Hatuwezi kujua moyoni
mwake anawaza nini lakini
Abu Zalawi ni mtu hatari sana
kuendelea kumtumia kwa sasa
katika misheni zetu” akasema
David walker
“Amefikaje kwa Habiba
Jawad hadi wakajenga
mashirikiano ya karibu?
Yawezekana akawa
amebadilika kutoka kuwa
jasusi hadi kuwa gaidi hivyo
hatakuwa na madhara yoyote
kwetu hata kama akifahamu
siri zetu” akasema Eric Wood.
“Niliwaeleza awali kwa
kirefu namna Mossad
walivyombadili Mathew
Mulumbi kutoka kwenye
ujasusi hadi kuwa gaidi Abu
Zalawi na lengo kubwa likiwa
ni kumuua Habiba Jawad
ambaye hadi leo hii Mossad
hawajui kama tunashirikiana
naye.Swali la kujiuliza hapa ni
je kama aliandaliwa kwa ajili
ya kumuua Habiba Jawad kwa
nini baada ya kuonana naye
hakufanya hivyo na badala
yake akaanza kushirikiana
naye? Kuna nini kati ya Abu
Zalawi na Habiba Jawad hadi
akaamua kumleta kwetu mtu
huyu ili tumtumie?
Tukiangalia mtiririko huo wote
tunaona ni namna gani
misheni yetu ilivyoingia
dosari.Hata kama
tukikubaliana kwamba
tumuache amalizie misheni
tuliyomtuma tutakuwa
tunajidanganya tu kwani
hatujui kuna nini kati yake na
Habiba Jawad? Upo
uwezekano mkubwa huyu
jamaa akabadilika na kuwa
mwiba kwetu ndiyo maana
lazima tumuwahi kumuua
kabla hajafanya chochote
nchini Iran” David Walker
akaendelea kuwashawishi
wenzake wakubali mpango wa
kumuua Mathew Mulumbi
“Vipi kuhusu Mossad
ambao wanataka tuwape
taarifa za mahala alipo Habiba
Jawad? Akauliza Michael
Torres.
“Hatutaweza kuwapa
taarifa za mahala alipo Habiba
Jawad badala yake Habiba
tutamuua sisi wenyewe baada
ya kumuhoji kujua kuhusu
Mathew Mulumbi.Ni yeye
ambaye ametufikisha hapa
tulipofika hivyo si mtu ambaye
tunaweza kumuanini na
kuendelea kushirikiana naye
tena.Lazima tumuue lakini
tutafanya hivyo pale tu
ambako Mossad watafanikiwa
kumuua Mathew Mulumbi”
akasema David Walker.
Baada ya mjadala mzito
hatimaye wakafikia
makubaliano ya kumuua
haraka Mathew Mulumbi kwa
kuwatumia majasusi wa
Mossad walioko nchini
Iran.Baada ya kumaliza kikao
kile David Walker akaondoka
kwenda kuonana na
mkurugenzi mkuu wa CIA
Jason Washington
“Dah ! siamini kama
misheni ambayo tumetumia
gharama kubwa ya fedha na
damu kumwagika imeishia
sehemu nzuri kiasi hiki.Tayari
Abu Zalawi amekwisha ingia
nchini Iran kwa ajili ya
kuianza kazi
tuliyomtuma.Itatuchukua
muda mrefu kuandaa tena
operesheni nyingine na kufikia
hatua kubwa kama hii ya
kupandikiza mtu nchini
Iran.Tulifanya makosa sisi
wenyewe hatukuwa makini
toka mwanzo na zoezi hili hadi
tukajikuta tukimtumia mtu
ambaye si sahihi.Imeniuma
sana kwani hivi sasa Abu
Zalawi tayari amekwisha ingia
nchini Iran.Kuna wakati
ninasikia sauti ambayo
inakataa tusifanye hiki
tunachotaka lakini ninaisikia
tena sauti nyingine ikinionya
kuwa Abu Zalawi ni mtu hatari
sana kwetu ambaye anapaswa
kudhibitiwa haraka sana.Ngoja
tukubali kushindwa na
tujipange vizuri zaidi ili
misheni ijayo iwe na mafanikio
makubwa” akaendelea kuwaza
David.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom