Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 4
“Imekuwa vyema umefika
kwa wakati David kwani
tunakwenda kuonana na
makamu wa Rais amenitaka
nifike ofisini kwake” akasema
Jason Washington mkurugenzi
mkuu wa CIA baada ya David
Walker kufika ofisini kwake.
Bila kupoteza muda
wakaingia katika gari la Jason
na kuondoka kwenda kuonana
na Mark Piller makamu wa
Rais
“Nini kimejiri huko katika
kikao? Akauliza Jason na
David akamweleza kila kitu
walichokubaliana katika kikao
“Vizuri sana.Nilimdokeza
Mark Piller kuhusiana na
mpango wetu wa kumuondoa
Abu Zalawi.Mark amestushwa
sana na jambo hili ndiyo
maana amenitaka nikaonanye
naye kwani tusingeweza
kuzungumza kwa kirefu katika
simu.Haamini kile
nilichomweleza kuhusu Abu
Zalawi” akasema Jason
Washington
“Suala hili la Abu Zalawi
linaumiza vichwa sana.Kila
mtu anashangaa kuhusu
jambo hili limetokeaje?
“Hatuna wa kumlaumu
katika hili David.Tumekosea
sisi wenyewe na lazima
tuchukue hatua za haraka sana
kuhakikisha jambo hili
halitakuwa na madhara
kwetu.Kama tungechukua
tahadhari mapema haya yote
yasingetoke ana misheni
ingeendelea kama kawaida”
akasema Jason
“Kuna kitu nimekuwa
najiuliza vipi kuhusu wale
jamaa wanasayansi tuliokuwa
tunawashikilia kwa muda
mrefu? Tunakubali
tumewapoteza?akauliza David
na Jason akatikisa kichwa
akisikitika
“Watu wale japo
hawajatupa taarifa tulizokuwa
tunazihitaji lakini ni watu wa
muhimu sana kwa Iran.Katika
hili tumewapa Iran ushindi
mwepesi lakini lazima
tuhakikishe nao pia wanauawa
pamoja na Abu Zalawi.”
akasema Jason
Walifika katika ofisi ya
makamu wa Rais ambaye
alikuwa anawasubiri na bila
kupoteza muda wakaingia
katika chumba cha maongezi
ya faragha na kikao kikaanza.
“Jason nimevuruga ratiba
yangu ya siku ya leo ili niweze
kuzungumza nanyi.Nataka
kufahamu kwa kina kuhusiana
na hiki kinachoendelea”
akasema makamu wa Rais
Mark Piller
Jason akamuelezea Mark
Piller kila kitu hadi
walipogundua kuhusu Abu
Zalawi kuwa si gaidi bali ni
jasusi pamoja na maamuzi
waliyoyachukua ya kumuua
“Jason jambo hili
limetokeaje? Kwa nini
haukufanyika uchunguzi wa
kina kuhusiana na huyu mtu
Abu Zalawi hadi tumefika hapa
tulpofika? Akauliza Mark Piller
“Katika hili Mark hatuna
wa kumlaumu mtu bali
tunapaswa kujilaumu sisi
wenyewe.Tulifanya uzembe wa
kutokufanya uchunguzi wa
kina kuhusiana na Abu Zalawi”
akasema Jason
“Lakini yote haya
ameyasababisha Habiba
Jawad ambaye tulimuamini
kwa asilimia mia moja na
hivyo tukamuamini yule mtu
aliyetuletea.Hata mara moja
hajawahi kutuangusha na
katika kila operesheni
tuliyomshirikisha hakujawahi
kutokea matatizo.Hii ni mara
ya kwanza Habiba anatufanyia
kitu cha namna hii” akasema
David Walker
“Mnadhani Habiba
alikuwa na lengo lake binafsi la
kumleta kwetu Abu
Zalawi?akaliza Mark Piller
“Hatuna uhakika bado
ndiyo maana tunataka
kulifanyia uchunguzi suala hilo
lakini wakati uchunguzi huo
ukiendelea tunataka
kumuondoa kwanza Abu
Zalawi pamoja na wale
wanasayansi tuliokuwa
tunawashikilia” akasema
Jason.Baada ya tafakari ya
muda mfupi Mark akauliza
“Kutakuwa na athari gani
kama tukimuacha Abu Zalawi
akaendelea na misheni lakini
tukimfuatilia kwa ukaribu
mkubwa kujua kila
anachokifanya kwa kuwatumia
hao majasusi wa Mossad
ambao mnataka kuwatumia
kumuua?akauliza Mark Piller
na Jason akampa maelezo
aliyopewa na Moshe Levine
mkuu wa Mossad kuhusu Abu
Zalawi na Mark akazidi
kuchoka.
“Mark hatuna namna
lazima tumuondoe Abu Zalawi
haraka sana ili kujihakikishia
usalama wetu.Endapo
tukishindwa kumuondoa Abu
haraka itatugharimu baadae”
akasema Jason.Waliendelea na
majadiliano kwa muda halafu
Mark Piller akasema
“Jason na David
nimekubalianba na
mapendekezo yenu juu ya
suala hili lakini nina
ushauri.Hatuwezi kumuua
Habiba Jawad nchini kwao
Saudi Arabia.Habiba Jawad
ana ukaribu mkubwa na
mfalme wa Saudi Arabia
ambaye ni mshirika mkubwa
wa Marekani hivyo lazima
tujihadhari tusivuruge
mahusiano mazuri kati yetu na
serikali ya Saudi
Arabia.Habiba aitwe Marekani
na akifika huku ndipo
atakapouawa” akashauri Mark
Piller
“Ushauri mzuri
tutauzingatia” akasema Jason
“Angalizo.Habiba asiuawe
kama Mossad hawajamuua
Abu Zalawi.Pale ambapo Abu
Zalawi atakuwa ameuawa
ndipo Habiba auawe kwani
tunaweza kumuua Habiba
halafu Mossad wakashindwa
kumuua Abu Zalawi.Kama
kuna jambo wawili hawa
wanalipanga lazima
tuwaondoe wote wawili
akiondolewa mmoja na
mwingine akabaki hatutakuwa
tumefanya kitu” akasisitiza
Mark Piller.Baada ya
majadiliano Jason na David
wakaondoka .Mark Piller
hakupoteza muda akainua
simu na kumpigia Rais
William Washington
“Mheshimiwa Rais nahitaji
kukuona sasa hivi” akasema
Mark
“Njoo ofisini” akajibu Rais
William na Mark Piller
akatoka ofisini kwake kuelekea
ofisini kwa Rais.
“Mark mpango wenu
unakwenda
vizuri.Nimefurahishwa na
taarifa nilizozipata kwamba
ndege ile iliyopotea
imeonekana ikielekea nchini
Iran” akasema Rais William
baada ya Mark kufika ofisini
kwake
“Mheshimiwa Rais ni
kweli mpango umekwenda
vizuri sana na hivi
tuzungumzavyo tayari mtu
wetu amekwisha kanyaga
ardhi ya Iran” akasema Mark
Piller
“Vipi mna mawasiliano
naye baada ya kuwasili Iran?
Akauliza Rais William
“Mheshimiwa Rais
mpango wetu wa kwanza
ulikuwa ni kumuingiza Abu
Zalawi nchini Iran na mpango
huo umefanikiwa vizuri lakini
kuna tatizo limejitokeza”
akasema Mark Piller na sura
ya Rais William aikabadilika
“Kumetokea tatizo gani
tena” akauliza William
“Baada ya Abu Zalawi
kufika salama Iran tulihitaji
kumpa msaada na kwa vile
hatuna wetu wetu kule Iran
ilitulazimu kuomba msaada
kutoka kwa wenzetu wa
Mossad ambao wana majasusi
wao Iran na hapo ndipo
lilipoibuka jambo ambalo
hatukuwa tukilifahamu”
akasema Mark Piler na
kumueleza Rais William kila
kitu walichokifahamu kutoka
kwa Mossad kuhusiana na Abu
Zalawi.Zilikuwa ni taarifa
zilizomstua sana William
“Mark kwa nini haya yote
yametokea?Kwa nini
hamkuchukua tahadhari
mapema kuhakikisha
mnamfahamu vyema mtu
ambaye mnataka kumtumia
katika misheni kubwa kama
hii? Akauliza William
“Mheshimiwa Rais katika
hilo tunakiri tulikosea na
ndiyo maana tunataka
kuchukua hatua za haraka za
kurekebisha kwa kumuondoa
Abu Zalawi haraka sana kabla
hajaendelea na misheni
aliyotumwa nchini Iran”
“Kumuua Abu Zalawi ni
suluhisho la jambo
hili?akauliza William
akionekana kukasirika
“Mheshimiwa Rais huyu
mtu ni hatari kwetu kama
tukiendelea kumuacha
hai.Tayari anafahamu kila kitu
kuhusu sisi na baya zaidi
anafahamu ni sisi tulio nyuma
ya kile kilichotokea Tanzania
na Afrika mashariki na
anafahamu kwa nini tulifanya
vile….”
“Pamoja na kufahamu !
akasema kwa ukali Rais
William na kumkatisha Mark
Piller
“Pamoja na kufahamu
hayo yote lakini bado Abu
Zalawi au vyovyote vile
anavyofahamika amekubali
kuifanya kazi aliyotumwa na
kwa sasa tayari amefika nchini
Iran.Anafahamu kabisa
kwamba kazi aliyotumwa
kuifanya Iran ni kazi ya hatari
kubwa na kama akijulikana
kuwa ni pandikizi la Marekani
anaweza akauawa muda
wowote ule lakini bado yuko
tayari kufanya.Kumuua Abu
Zalawi ni kosa kubwaMark !
akasema Rais William
“Mheshimiwa Rais pamoja
na Abu Zalawi kukubali
kuifanya kazi aliyotumwa
aifanye lakini hakuna anayejua
moyoni mwake nini
anakiwaza,hatujui ana
mipango gani dhidi yetu.Kwa
taarifa tuliyoipata kutoka kwa
Mossad ni kwamba Abu Zalawi
ameyatoa maisha yake katika
kupambana na ugaidi hasa
kundi la IS linaloendelea
kuotesha mizizi katika eneo la
Afrika Mashariki.Abu Zalawi
ni bilionea na ana familia
inaishi Paris Ufaransa lakini
ameacha hivyo vyote
akajielekeza katika kupamba
na na magaidi.Jaribu kupata
picha mtu kama huyu anakuja
kugundua kwamba
tunashirikiana na magaidi wa
IS na kibaya zaidi kuchochea
machafuko katika nchi
anakotoka na kusababisha vifo
vya watu na sisi tukiendelea
kubeba tani na tani za mafuta
unadhani mtu kama huyu
atafanya nini?Lazima atakuwa
na chuki kubwa sana dhidi
yetu na hatujui nini
anakifikiria lakini ni wazi
jambo hili hataweza
kulivumilia” akasema Mark
Piller
“Mark nimekuelewa lakini
maamuzi ya kumuua mtu
kama huyu si sahihi.Mtu kama
huyu bado anaweza akawa
upande wetu.Tunaweza
kuzungumza naye na
kumfanya atuelewe na hata
kama alikuwa na kitu moyoni
mwake tukakiondoa.Sisi ni
taifa kubwa na hatuwezi
kukubali kushindwa kirahisi
namna hii.Hebu fikiria
Mark,nini kingine mtakifanya
kitakachowawezesha
kupandikiza mtu nchini Iran?
Kwa kuwatumia wale mateka
wa Iran imekuwa rahisi kwetu
kuweza kupenyeza mtu ndani
ya Iran na kama mkiharibu
msheni hii itachukua miaka
mingi kuweza kufanikisha
jambo kama hili na pengine
lisiwezekane tena.Kwa kuwa
tayari Abu Zalawi amekwisha
ingia Iran,itafutwe namna ya
kuzungumza naye na
kumuweka sawa aendelee na
jukumu lake badala ya
kufikiria kumuua” akasema
Rais William
“Mheshimiwa Rais…..”
Mark Piller akataka kusema
kitu lakini Rais William
akamzuia
“Mark sitaki kuendelea na
mjadala huu.Hatuwezi kuipa
Iran ushindi kirahisi namna
hii lazima kwa namna yoyote
ile misheni hii iendelee.Iran ni
taifa tishio kwa Marekani kwa
sasa na lazima tufahamu
uwezo wake wa silaha hivyo
lazima misheni iendelee.Abu
Zalawi hapaswi kuuawa !
akasema kwa sauti ya msisitizo
kisha wakabaki wanatazamana
“Mheshimiwa Rais sidhani
kama unaiona hatari iliyoko
mbele yetu kama tukiendelea
kumtumia huyu Abu Zalawi !
akasema Mark
“Mark sijali chochote,
ninachohitaji ni Abu Zalawi
aendelee na misheni
aliyotumwa nchini
Iran.Endapo Abu akiuawa na
misheni ikashindwa kuendelea
ninaapa nitakifuta hiki kikundi
chenu kwani hakitakuwa na
maana tena.Sijali kama
nitauawa ama nini kitatokea
lakini lazima nikifute !
akasema Rais William
“Mheshimiwa Rais
nilipokuja kukueleza
kuhusiana na kikundi hiki na
mambo yake nilikupa angalizo
kwamba unatakiwa usiri
mkubwa kwani Rais wa nchi
hapaswi kufahamu chochote
kuhusu uwepo wa kikundi
hiki.Utayaweka maisha yetu
sote katika hatari
kubwa.Nakuomba
mheshimiwa Rais usifikirie
kufanya hicho hicho
unachotaka kukifanya”
akasema Mark Piller
“Mark mimi siogopi
chochote na ninakuhakikishia
kwamba nitafanya hivyo na
wamarekani watajua kuwa
nchi yao inashirikiana na
magaidi”
“Mheshimiwa Rais !
akasema Mark
“Mark fanya
ninavyokuelekeza.Ukitaka
kundi lenu liendelee
kuwepo.Nataka Abu zalawi
aendelee na misheni yake
nchini Iran.Sitaki auawe.Fanya
kila linalowezekana
kuhakikisha misheni yake
inafanikiwa.Tunaihitaji sana
misheni hii ama sivyo Iran
itaendelea kutoa vitisho vya
kusishambulia Marekani!
Siwezi kuzivumilia kauli chafu
za vitisho zinazotolewa na Rais
wa Iran dhidi ya Marekani !
akasema Rais William
“Mheshimiwa Rais
kufanya hicho unachotaka
nikifanye ni usaliti mkubwa
kwa wenzangu na…..”
“Mark kumbuka kwamba
sisi ndio tunao ongoza nchi hii
na dhamana ya usalama wa
watu wetu tumeibeba sisi na
kwa sasa watu wetu wana hofu
kufuatia vitisho vya Iran kuwa
anao uwezo wa kuishambulia
na kuiharibu Marekani hivyo
basi lazima tufanye kila lililo
ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha tunaiweka nchi
yetu salama pamoja na watu
wake ndiyo maana ninasema
kwamba tunaihitaji sana
misheni hii kwa ajili ya
kufahamu wezo wa silaha za
Iran na baada ya hapo
tutaichakaza vibaya
sana.Ikitokea Iran
imeshambulia Marekani
watakaobeba mzigo wa
lawama ni sisi na si hao ambao
unaogopa kuwasaliti.Mark
fanya kila linalowezekana hata
kama ni kwa kuwasaliti
wenzako hakikisha Abu Zalawi
anakuwa salama na
anaendelea na misheni yake
nchini Iran.Vuruga mpango wa
kumuua ! akasema Rais
William na Mark Piller
akainamisha kichwa
akitafakari
“Umenielewa Mark
Piller?akauliza Rais William
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais.Nitafanya
kama ulivyoelekeza lakini
naomba ufahamu kwamba ni
jambo la hatari kubwa”
“Usihofu kuhusu hilo
Mark.Kama kuna hatari yoyote
unaihisi nijulishe na mimi
nitakulinda.Tunayafanya haya
kwa maslahi ya nchi yetu”
akasema Rais William na Mark
Piller akaondoka akarejea
ofisini kwake na kujiegemeza
kitini
“Hili jambo linaendelea
kubadilika kila wakati.Rais
anataka niwasaliti wenzangu
na kuvuruga mipango ya
kumuua Abu Zalawi ! akawaza
Mark
“Lakini ukilitazama jambo
hili kwa kina zaidi,Rais yuko
sahihi.Hatupaswi kumuua Abu
Zalawi badala yake tunapaswa
kufanya kila liwezekanalo
kumuweka upande wetu.Kwa
hiyo kwa mara ya kwanza
nitalazimika kuwasaliti
wenzangu na kuvuruga
mpango wa kumuua Abu
Zalawi.Kuna mtu mmoja tu
ambaye ninatakiwa
kuzungumza naye” akawaza na
kufungua mkoba wake akatoa
simu iliyokuwa na namba
kumi na mbili tu ambazo ni
namba za watu muhimu
akaelekeza kidole chake katika
namba ya sita ambayo ilikuwa
ni namba ya Habiba Jawad
akampigia baada ya sekunde
kadhaa simu ikapokelewa.
“Mark Piller ! akasema
Habiba Jawad akionekana
kushangaa
“Habiba Jawad
unaendeleaje? Akasema Mark
“Ninaendelea vizuri
Mark.Nimeshangaa kidogo leo
umenipigia simu.Sikutegemea
kabisa kupata simu yako”
akasema Habiba Jawad
“Habiba nimelazimika
kukupigia simu kuna mambo
ya muhimu sana ya
kuzungumza mimi nawe na
ninakuomba tafadhali yale
tutakayoyazungumza hapa
yawe ni baina yetu sisi
wawili.Mtu mwingine yeyote
kutoka G20 hatakiwi
kufahamu kama nimekupigia
simu.Umenielewa
Habiba?akauliza Mark Piller
“Nimekuelewa Mark.Nini
unataka kuzungumza
nami?akauliza Habiba
“Kwanza kabisa ninataka
kukupa taarifa kuwa mpango
wetu umekwenda vizuri na hivi
tuzungumzavyo tayari Abu
Zalawi amekwisha ingia nchini
Iran” akasema Mark Piller
“Hizo ni taarifa njema
sana.Nimefurahi kusikia
matokeo mazuri ya mpango
huu.Ninakuhakikishia Mark
kuwa kama tayari Abu
amefanikiwa kuingia nchini
Iran lazima atafanikisha kila
kitu alichotumwa
kukifanya.Kitu cha msingi kwa
sasa ni kujitahidi kutafuta
namna ya kuwasiliana naye na
kujua maendeleo yake”
akasema Habiba
“Tayari tumelifanya hilo
Habiba ila kuna tatizo
limejitokeza”
“Tatizo gani
Mark?akauliza Habiba
“Baada ya kuhakikisha
Abu Zalawi ameingia Iran
ilitulazimu kuomba msaada
kutoka kwa wenzetu wa
Mossad ambao wana watu wao
kule Iran kwa ajili ya kumpa
msaada na hapo ndipo
tulipofahamu kila kitu kuhusu
Abu Zalawi” akasema Mark na
kumueleza Habiba kila kitu
walichokigundua kuhusu Abu
Zalawi.Kupitia spika za simu
Habiba Jawad akasikika
akivuta pumzi ndefu
“Habiba unaweza
ukazungumza chochote
kuhusiana na jambo
hili?akauliza Mark
“Sina cha kuzungumza
Mark lakini kila kitu
mlichoelezwa kuhusu Abu
Zalawi ni cha kweli” akasema
Habiba na Mark Piller akahisi
mwili unamtetemeka
“Kwa nini Habiba kama
ulifahamu kuwa Abu Zalawi ni
jasusi tena anatokea Tanzania
ukamleta kwetu tukampa
misheni kubwa kama hii?
Akauliza Mark Piller
“Kwa sababu Abu Zalawi
ndiye pekee anayeweza
kuifanya kazi hii.Hakuna gaidi
ambaye ana uwezo wa kuingia
Iran na kufanya jambo la
hatari la kuichunguza Iran
zaidi ya Abu Zalawi.Mark hii si
misheni ya kigaidi hii ni
misheni ya kijasusi na mtu
niliyewaletea ndiye anayefaa”
akasema Habiba Jawad
“Habiba sisi tulihitaji gaidi
lakini wewe ukatuletea jasusi
tena anatokea Tanzania nchi
ambayo kwa kushirikiana na
magaidi wa IS tumechochea
machafuko ya kidini na
kusababisha waumini
kushambuliana na damu
nyingi kumwagika na kama
haitoshi bado tunaendelea na
mpango wa kusambaza kirusi
hatari kwa lengo la kuendelea
kuchota utajiri mkubwa ulioko
Afrika Mashariki.Kwa nini
ukatufanyia hivi? Akauliza
Mark
“Mark kama
nilivyokueleza kwamba huyu
ndiye mtu pekee anayefaa kwa
misheni hii” akajibu Habiba
“Habiba japokuwa una
uhakika kuwa mtu huyu ndiye
anayefaa lakini tayari ana
kasoro.Hatujui ni kitu gani
anakiwaza baada ya kugundua
kwamba sisi tuko nyuma ya
kile kinachoendelea Afrika
Mashariki.Hii ni kasoro kubwa
na tayari imetia doa misheni
nzima” akasema Mark
“Mark nataka
nikuhakikishie kwamba Abu
Zalawi hana tatizo lolote na
msiwe na wasiwasi wowote
naye.Anakwenda kutekeleza
kile alichotumwa kukifanya
Iran na uwezo wa kufanya
hivyo anao.Abu Zalawi japo ni
jasusi lakini nimembadilisha
na anafanya kazi
kwangu.Nimembadili kutoka
Jasusi kuwa Gaidi.Ni mimi
pekee anayenisikiliza kila
ninachomuelekeza kukifanya
kwani nimemfanya kuwa
mwanangu,amemuoa
mwanangu Najma hivyo Abu
Zalawi ni sehemu ya familia
yangu” akasema Habiba
“Habiba kama
nilivyokueleza kuwa tayari
misheni imeingia dosari.Baada
ya kugundua kuwa Abu Zalawi
si Yule uliyetuaminisha kuwa
ni gaidi bali ni jasusi tena
anatokea Tanzania,kuna
maamuzi yamefanyika”
akasema Mark Piller na
kunyamaza kidogo
“Mmefanya maamuzi gani
Mark?akauliza Habiba
“Tumekubaliana kumuua
Abu Zalawi na misheni
itakuwa imeishiahapo”
akasema Mark na ukimya
ukapita
“Mark Piller hilo ni kosa
kubwa sana ambalo mtalijutia
kwani hamtapata tena nafasi
nyingine ya kumuingiza mtu
wa kuwafanyia ujasusi nchini
Iran.Hii ni nafasi pekee
mmeipata na mkishindwa
kuitumia vyema ni juu yenu”
akasema Habiba
“Habiba misheni tayari
imevurugika na aliyeivuruga
misheni hii ni wewe kwa
kutuletea mtu ambaye hakuwa
sahihi kwa misheni
hii.Tulikuamini sana Habiba
na ndiyo maana hatukuwa na
wasi wasi wowote na Abu
Zalawi lakini baada ya
kumfahamu vyema Abu Zalawi
umevunja uaminifu na
maamuzi yaliyopitishwa ni
wewe kuuawa pia” akasema
Mark Piller na ukimya
ukawala.
“Mark ! akaita Habiba
Jawad
“Unasemaje Habiba?
“Mnakwenda kufanya kosa
kubwa sana kwa hiyo mipango
yenu mliyoipanga” akasema
Habiba
“Ninafahamu Habiba”
“Kwa nini ukanipigia
kunijulisha kuhusu mipango
yenu?akauliza Habiba
“Nimekupigia kwa sababu
baada ya kutafakari kwa kina
nimegundua kwamba
tutafanya kosa
kubwa.Tunaihitaji mno
misheni hii ifanikiwe hivyo
nimekupigia kuomba msaada
wako” akasema Mark na
ukimya ukatawala tena.Habiba
Jawad akavuta pumzi na
kusema
“Nini unahitaji tena
kutoka kwangu Mark wakati
tayari mmekwisha panga
mipango ya kuniua? Akauliza
Habiba
“Nimeamua kuwasaliti
wenzangu na kukueleza ukweli
kuhusu mipango yetu,kwanza
ili uchukue tahadhari na
kujificha na pili ni kutafuta
namna ya kumfikishia Abu
Zalawi taarifa za kumtaka
achukue tahadhari kwani kuna
watu wanaotaka
kumuua.Nataka Abu aendelee
na misheni hii hadi
atakapoikamilisha” akasema
Mark Piller
“Mark nimekuwa mtumwa
wenu kwa miaka
mingi,nimewafanyia kazi
nyingi kwa manufaa ya nchi
yenu lakini hata baada ya
kuwafanyia hayo yote
ninachoambulia ni kutaka
kuuawa.Mmenisikitisha sana
Mark”
“Habiba ndiyo maana
nimekupa siri hii ili uweze
kuchukua tahadhari na
ikiwezekana uondoke Saudi
Arabia ukajifiche mahala”
akasema Mark
“Siwezi kukimbia
Mark.Siwezi kukimbia.Kama
mnataka kuniua njooni
mtanikuta hapa ninawasubiri
lakini fahamuni ya kwamba
damu yangu haitawaacha
salama ! akasema Habiba
Jawad
“Habiba tafadhali naomba
tusilifanye jambo hili liwe
gumu.Wewe mwenyewe
unafahamu namna misheni hii
ilivyo muhimu.Wengine wote
hawalioni hilo lakini mimi
ninafahamu umuhimu
wake.Habiba tafadhali
nakuhitaji sana.Naomba
tushirikiane kuhakikisha
misheni hii inaendelea na
inafanikiwa.Naomba tafuta
namna ya kumlinda Abu
Zalawi dhidi ya wale wote
watakaotumwa kumuua na
aendelee na kazi aliyotumwa
kuifanya.Habiba nakuahidi
nitakulinda dhidi ya mipango
yoyote mibaya inayopangwa
juu yako” akasema Mark Piller
“Mark….. !
“Habiba tafadhali ! Sisi
nawe tumetoka mbali sana na
umetusaidia mambo mengi
naomba mashirikiano yetu
yaendelee kama kawaida na
ninakuahidi kukulinda hata
kama ni kwenda kinyume na
wenzangu wote niko tayari
kufanya hivyo.Tafadhali
Habiba” akasema Mark
“Mark nimekuelewa lakini
nataka kufahamu jambo
moja.Nataka kufahamu namna
mlivyopanga mipango ya
kutuua mimi na Abu Zalawi”
akasema Habiba na Mark
akamueleza mipango yote
namna ilivyopangwa ya
kuwaua yeye na Mathew
“Mark Piller unadhani nini
kitakutokea pale wenzako
watakapobaini kuwa
umewasaliti?akauliza Habiba
“Ninafahamu nitakuwa
matatizoni lakini niko tayari
kukabiliana na chochote
kitakachonitokea.Misheni hii
ni muhimu mno kwa nchi
yangu na kwa namna yoyote ile
lazima ifanikiwe” akasema
Mark Piller
“Sawa Mark
nimekuelewa.Nitashirikiana
nawe kuhakikisha misheni hii
inafanikiwa.Nitajitahidi
kuhakikisha Abu Zalawi
anapata taarifa mapema kabla
ya watu wa Mossad
hawajamfikia.Ninachotaka
ukifanye ni kuendelea kunipa
taarifa za mipango yenu yote
mnayoipanga ili na mimi
nitafute namna ya kumsaidia
Abu Zalawi” akasema Habiba
“Nitakujulisha kila kitu
Habiba Jawad lakini
nakuomba nawe uchukue
tahadhari kuanzia sasa.Pale
utakapoitwa uje Marekani toa
kisingizio kwamba hautaweza
kwa sasa kuna mambo ya
msingi unayashughulikia na
mimi nitaongeza
nguvu.Ongeza ulinzi na mtu
yeyote asiyefahamika
asikaribishwe katika makazi
yako” akasemaMark Piller
“Nakushukuru Mark.Mimi
nitahakikisha Abu Zalawi
anakuwa salama na
anaendelea na mipango yake
yote kama alivyotumwa nchini
Iran” akasema Habiba
wakaendelea na mazungumzo
kidogo wakapeana mikakati
namna watakavyokuwa
wakiwasiliana kwa siri kisha
wakaagana.
“Nilijua tu lazima
watagundua kuhusu Mathew
lakini sikutegemea iwe
mapema namna
hii.Nilifahamu
watakapogundua kuhusu
Mathew mzigo wote wa
lawama nitaubeba mimi na
nilikwisha jiandaa kwa jambo
hilo.Kwa sasa baada ya
kuifahamu mipango yao
natakiwa kuhakikisha Mathew
anakuwa salama ili aweze
kuikamilisha misheni yake”
akawaza Habiba Jawad na
kuchukua simu nyingine
akazitafuta namba Fulani na
kupiga kisha simu ikapokelewa
“Habiba” akasema mtu
aliyepokea simu upande wa
pili
“Vahid
unaendeleaje?akauliza Habiba
Jawad
“Siwezi kusema naendelea
vizuri Habiba.Bado kifo cha
mwanangu Najma
kinaniumiza mno.Ninajuta
kwa nini nilimruhusu aje
Riyadh.Kama ningeendelea
kukaa naye hapa Tehran
yasingemkuta haya
yaliyomkuta.Kwa ujumla bado
siko sawa na itanichukua
muda mrefu kulizoea jambo
hili” akasema Vahid Ghorbani
baba mzazi wa Najma.Vahid
na Habiba waliwahi kuwa na
mahusiano na wakamzaa
Najma lakini hawakufunga
ndoa na kila mmoja
akaendelea na maisha yake.
“Vahid suala hili
linatuumiza sote.Huwezi kujua
niko katika hali gani kwa sasa
baada ya kuwapoteza wanangu
wawili ndani ya kipindi
kifupi.Ni wakati mgumu sana
huu kwetu sote hivyo
tusaidiane kufarijiana badala
ya kulaumiana” akasema
Habiba
“Sikulaumu Habiba
nafahamu ulivyompenda
Najma.Tuachane na hayo vipi
maendeleo yako?
“Kama nilivyokwambia
Vahdi kwamba siko
sawa.Nimewapoteza watoto
wawili ndani ya kipindi kifupi
ni suala zito kulibeba lakini
ninajitahidi.Hata hivyo
sijakupigia simu kwa suala
hilo.Vahdi kuna jambo nataka
unisaidie”
“Sema chochote
Habiba.Unataka nikusaidie
nini?akauliza Vahid
“Kuna wanasayansi sita wa
Iran waliokuwa wamepotea
lakini leo hii wamerejea
nyumbani”akasema Habiba
“Nimepata taarifa hizo
kwamba wale watu wetu
waliokuwa wamepotea
wamerejea nyumbani leo hii
lakini haijatolewa taarifa rasmi
kwamba walikuwa wapi muda
huu wote” akasema Vahid
“Aliyewakomboa watu hao
na kuwarejesha nyumbani
anaitwa Abu Zalawi”
“Abu Zalawi?! Vahdi
akauliza
“Ndiyo.Anaitwa Abu
Zalawi”
“Ni mtu wa wapi huyo Abu
Zalawi?
“Ni Raia wa Saudi Arabia”
“Hatujafahamishwa jambo
hilo.Nini unataka nikusaidie
Habiba? Akauliza Vahid
“Ninataka ufanye kila lililo
ndani ya uwezo wako uweze
kuonana na huyu Abu Zalawi”
“Nionane na Abu Zalawi?
Vahid akauliza
“Ndiyo.Kuna ujumbe wa
muhimu sana ambao nataka
umfikishie”akasema Habiba
“Habiba sifahamu alipo
huyo Abu Zalawi na wala sijui
ni jinsi gani nitaweza
kumpata” akasema Vahid
“Vahid unatakiwa ufanye
kila linalowezekana
kuhakikisha unampata Abu
Zalawi”
“Habiba sidhani kama
mimi ni mtu sahihi wa
kukusaidia kwenye jambo hilo”
akasema Vahid
“Vahid ni muhimu sana
ukaonana na Abu Zalawi.Huyo
ndiye mume wa Najma”
“Mume wa Najma?! Vahidi
akastuka
“Ndiyo ni mume wa
Najma”
“Najma alikuwa na
mume?Kwa nini hujawahi
kuniambia jambo hili?
“Najma mwenyewe ndiye
aliyetaka iwe siri na
tusikujulishe.Kama
unavyofahamu kuwa Najma
hakuwahi kuwa na mpenzi
lakini alipokutana na Abu
Zalawi akajikuta akimpenda na
kufunga naye ndoa ya kimya
kimya na alitoa maelekezo ya
kutokufahamisha jambo
hili.Alitaka yeye mwenyewe
akujulishe pale atakapokuwa
tayari lakini kwa bahati mbaya
hakuwahi kufanya hivyo mauti
yakamkuta” akasema Habiba
“Habiba ulikosea sana
kukubali kunificha kuhusu
Najma kuolewa wakati mimi
ndiye baba yake
mzazi.Hukunitendea haki
katika hili”akasema Vahid
“Nakubali Vahid kwamba
nilikosea lakini nilifanya hivyo
kuheshimu matakwa ya
mtoto.Alitaka akueleze jambo
hili yeye mwenyewe muda
utakapofika.Tusameheane
katika hilo”
“Nilipokuja msibani kwa
nini huku nijlisha kuwa Najma
alikuwa na mume hadi leo hii?
“Nilikuwa
nimechanganyikiwa Vahid
ndiyo maana sikukueleza
chochote.Tafadhali naomba
sana unisamehe kwa hilo”
akajibu Habiba.Baada ya muda
Vahid akauliza
“Unataka kumfikishia
ujumbe gani huyo Abu
Zalawi?akauliza Vahid
“Nataka uonane naye ana
kwa ana na umpe simu
nizungumze naye”
“Habiba umenipa mtihani
mgumu sana.Kwanza ni nani
huyo Abu Zalawi?Kwa nini
yuko hapa? Akauliza Vahid
“Vahid naomba unisaidie
hilo ninalokuomba ni muhimu
sana”
“Habiba niko tayari
kukusaidia lakini lazima
nifahamu huyu mtu ni nani na
kwa nini yuko hapa Iran?
“Abu Zalawi anataka
kuuawa na Mossad hivyo
nataka niongee naye nimpe
angalizo awe makini” akasema
Habiba
“Anataka kuuawa na
Mossad?akauliza Vahid
“Ndiyo.Kuna majasusi
wanatumwa kuja Tehran kwa
lengo la kumuua.Anatakiwa
aipate haraka sana taarifa
hiyo”akasema Habiba
“Kwani huyu Abu Zalawi
ni nani hadi Mossad watake
kumuua? Akauliza Vahid
“Vahid nitakueleza kila
kitu hapo baadae kuhusiana na
Abu Zalawi lakini kwanza
naomba unisaidie kufanya kila
uwezalo uonane naye na
umpatie simu nizungumze
naye.Unaweza ukanisadia kwa
hilo? Akauliza Habiba
“Sawa Habiba.Nitajitahidi
kumtafuta huyo Abu Zalawi”
“Jitahidi Vahid wewe ni
mfanya biashara mkubwa
nchini Iran unafahamiana na
watu wengi hata viongozi wa
serikali naamini haitakuwa
kazi ngumu kwako kufahamu
mahala alipo Abu Zalawi”
akasema Habiba Jawad na
kuagana na Vahid.
******************
Baada ya kutoka
kuzungumza na makamu wa
Rais,Jason na David walirejea
katika ofisi ya Jason ambaye
bila kupoteza muda akampigia
simu Moshe Levine
mkurugenzi wa Mossad
“Jason Washington”
akasema Moshe baada ya
kupokea simu
“Habari za muda huu
Moshe.Nimekupigia kufuatia
mazungumzo yetu ya awali”
akasema Jason
“Ndiyo Jason.Umefikia
wapi kuhusiana na yale
tuliyoyazungumza?akauliza
Moshe Levine
“Kama nilivyokueleza
asubuhi kwamba tunataka
kumuua Abu Zalawi.Bado
mpango huo unaendelea na
kama nilivyokudokeza
tunataka kuwatumia watu
wako wa Mossad walioko
nchini Iran” akasema Jason
“Jason nina watu wangu
Tehran ambao wanaweza
wakaifanya hiyo kazi muda
wowote watakapopewa
maelekezo lakini nilitoa
masharti asubuhi ya kama
mkitaka tuwasaidie kumuua
Abu Zalawi basi na nyinyi
mtupe taarifa za mahala alipo
Habiba Jawad.Mmefikia wapi
katika suala hilo?akauliza
Moshe Levine
“Tumejadiliana na
tumekubaliana jambo
moja.Habiba Jawad tutamuua
sisi wenyewe pale ambapo
nanyi mtakuwa mmemuua
Abu Zalawi”
“Jason hatukukubaliana
hivyo.Ninataka mtupe taarifa
za mahala alipo Habiba Jawad
na tutamkamata sisi
wenyewe.Hatutaki kumuua
kuna mambo mengi tunahitaji
kuyafahamu kuhusiana na
mtandao wake kabla ya
kumuua hivyo tupeni taarifa za
mahala alipo sisi tutamkamata
hatuhitaji msaada wa kumuua”
akasema Moshe Levine
“Moshe sisi tuko tayari
kutoa aina yoyote ya
ushirikiano kwenu.Kama
hamtaki kumuua Habiba
hatuna tatizo na hilo.Sisi
tutamkamata Habiba na
tutamkabidhi kwenu lakini
lazima kwanza tuhakikishe
Abu Zalawi ameuawa ndipo
tutawakabidhi Habiba
Jawad.Tunakubaliana katika
hilo?akauliza Jason
“Jason tunamtaka Habiba
Jawad kwanza ndipo
tuwafanyie kazi yenu ! Kuna
ugumu gani wa kutupa taarifa
za mahala alipo Habiba ?
akauliza Moshe Levine
“Moshe sisi na ninyi ni
washirika wakubwa tena wa
miaka mingi tunapaswa
kuaminiana.Tuna sababu za
msingi kwa nini hatuwezi
kuwapa taarifa za mahala alipo
Habiba Jawad.Naomba
uniamini Moshe kwamba
tutamkabidhi kwenu Habiba
Jawad pale tutakapokuwa na
uhakika kwamba Abu Zalawi
ameuawa.Hivi tuzungumzavyo
tayari timu inaandaliwa kwa
ajili ya kwenda kumkamata
Habiba Jawad.Tutamuhifadhi
hadi pale ambapo mtakuwa
mmekamilisha zoezi la
kumuua Abu Zalawi”
“Jason kutakuwa na
ugumu katika jambo
hilo.Tupeni Habiba Jawad na
sisi tumuue Abu Zalawi”
“Moshe nakuhakikishia
kwamba hata dakika hii
mkimtaka Habiba Jawad
mtampata lakini hatuwezi
kumkabidhi Habiba kwenu
wakati bado hamjatekeleza
kazi yetu.Muondoeni Abu
Zalawi kwanza ili mumpate
Habiba
“Tufanye
hivi.Tudhihirishieni kwanza
kama kweli mnaye Habiba
Jawad na tutaelekeza apelekwe
katika ubalozi wenu Jerusalem
na baada ya kumuua Abu
Zalawi mtamkabidhi
kwetu.Tunakubaliana katika
hilo”
“Hakuna tatizo katika
hilo.Tutafanya hivyo”
“Vizuri.Nashukuru kama
tumekubaliana hivyo Jason
basi na sisi tunaanza mara
moja mpango wa kumuua Abu
Zalawi.Tutaendelea
kufahamishana kila hatua
tunayopiga” akasema Moshe
Levine wakaagana
“Mambo yanazidi kuwa
magumu David” Jason
akamwambia David na
kumuelezea kila kitu
walichozungmza na Moshe
Levine
“Nini maamuzi yako katika
jambo hili? akauliza David
Walker
“Hatuna ujanja lazima
tumkamate Habiba Jawad na
kumuandaa kwa ajili ya
kuwakabidhi Mossad pale
watakapokuwa wamemuua
Abu Zalawi”
“Jason huo ni mpango wa
hatari sana.Ni vipi kama
wakimchunguza na kugundua
kuwa tumekuwa
tunashirikiana naye?akauliza
David
“Tutamuweka Habiba
Jawad katika ubalozi wetu
jijini Jerusalem na baada ya
wao kumuua Abu Zalawi sisi
pia tutamuua Habiba Jawad
na kuwakabidhi maiti
yake.Hatuwezi kuwakabidhi
Habiba akiwa mzima”
akasema Jason wakaendelea
kujadiliana kuhusiana na
mpango ule halafu Jason
akainua simu na kumjulisha
Mark Piller kuhusu
mazungumzo yake na Moshe
Levine pamoja na mpango
waliouandaa.
Mark Piller baada ya
kumaliza maongezi na Jason
akampigia simu Habiba Jawad
“Mark karibu tena”
akasema Habiba
“Habiba nimerejea tena
kama nilivyokueleza awali
kwamba nitakuwa ninakupa
taarifa mipango yote
inayopangwa dhidi yako”
akasema Mark na kumueleza
Habiba kuhusiana na mpango
ule wa kutuma kikosi kwenda
kumteka na kumpeleka katika
ubalozi wa Marekani jijini
Jerusalem tayari kwa
kukabidhiwa kwa Mossad pale
watakapokuwa wamefanikisha
mpango wa kumuua Abu
Zalawi.
“Ahsante sana Mark Piller
kwa angalizo hilo.Tayari
nimekwisha anza taratibu za
kumtafuta Abu Zalawi na
kujua mahala alipo ili niweze
kumuonya kuhusiana na
mpango wa
kumuua.Nategemea kabla ya
watu hao wa CIA waliotumwa
kuja kunikamata hawajafika
hapa tayari nitakuwa
nimekwisha mpata Abu
Zalawi” akasema Habiba
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Kiza tayari kilikwishatanda
katika jiji la Dar es
salaam,Nawal alitoka
chumbani kwake na kwenda
kukaa sehemu ya kupumzikia
iliyo mbele ya nyumba ile
wanakoishi viongozi wa vikosi
vya jeshi la Marekani vilivyopo
Dar es salaam.Taa zilikuwa
zinawaka katika nyumba hii
kwani walikuwa wanatumia
jenereta .Ulinzi pia ulikuwa
mkali karibu kila pembe ya
nyumba hii kulikuwa na
walinzi.Akiwa amejipumzisha
mbele ya nyumba muhudumu
akamfuata na kumuuliza kama
angependa kutumia kinywaji
chochote na Nawal
akamuagiza amtengenezee
kahawa
“Nilipowasiliana na Ruby
saa kumi na mbili jioni,bado
Jenerali William hakuwa
amerejea ofisini kwake na hadi
giza limeingia hatujui mahala
alipo Sattar.Kwa namna yoyote
ile lazima usiku wa leo tujue
mahala kilipo
kirusi.Nitamvamia Jenerali
William usiku wa leo
chumbani kwake na lazima
ataeleza alipo Sattar na
kirusi.Kitu kikubwa
ninachohitaji kufahamu ni
watu wangapi wanaoishi ndani
ya nyumba hii ili nijue namna
ninavyoweza kukabiliana nao
na kama nikiona sintaweza
basi nitaomba msaada kutoka
SNSA.Nitakaa hapa hapa hadi
jenerali William atakaporejea”
akawaza Nawal na kutolewa
mawazoni baada ya kahawa
yake kuletwa.
“Ahsante sana.Jina lako
nani nimelisahau” akauliza
Nawal
“Naitwa Brenda”
“Ouh Brenda .Naitwa
Chloe” akasema Nawal na
kumtaka Yule muhudumu
kukaa kwa ajili ya
mazungumzo lakini Brenda
akamjulisha kwamba
watazungumza pale
atakapokuwa amekamilisha
majukumu yake
“Huyu Brenda anaweza
akanipa taarifa za kutosha
kuhusu mahala hapa.Ngoja
nimsubiri amalize majukumu
yake” akawaza Nawal
akiendelea kunywa kahawa
yake taratibu
Akiwa ameyaelekeza
macho yake katika geti mara
akawaona wanajeshi
waliokuwa wakilinda geti
wakiwa katika heka heka
akakaza macho zaidi ili kujua
kinachoendelea.Geti
likafunguliwa na gari nne
zikaingia mle ndani.Tatu
zikiwa ni gari za doria za jeshi
la Marekani na moja ikiwa ni
aina ya Prado.Kutoka katika
mojawapo ya gari akashuka
Jenerali William na na
makamanda wengine wawili
na kutoka katika ile Prado
wakashuka watu wanne ambao
hawakuwa wanajeshi.Nawal
alihisi mapigo ya moyo wake
yakibadilika na kwenda haraka
haraka baada ya kuziona sura
za wale jamaa walioshuka
katika Prado
“Sattar ! Assad ! akasema
kwa sauti ndogo ya mshangao
Jenerali William akiwa
ameongozana na wale jamaa
wengine wanne na wanajeshi
wawili wakaanza kupiga hatua
kuelekea ndani ya ile nyumba.
“Chloe ! akasema Jenerali
William baada ya kumkuta
Nawal amekaa nje
“Jenerali William”
akasema Nawal na kusimama
“Habari za toka
mchana?Umeshinda salama?
Akauliza Jenerali William
“Niko salama kabisa
Jenerali William.Nimepata
huduma nzuri”
“Nafurahi kusikia hivyo
Chloe.Hawa ni wenzangu Meja
Greg na Meja Thomas”
akasema Jenerali William na
kufanya utambulisho.
“Huyu ni mmarekani
mwenzetu ambaye alikuwa
hapa Tanzania katika shughuli
zake za upigaji picha lakini
alijikuta amenasa katika
machafuko na jana
amekombolewa na vikosi vya
jeshi la Tanzania akaletwa Dar
es salaam na leo mchana Rais
akanikabidhi.Chloe ataishi na
sisi hapa hadi pale hali ya
amani itakapokuwa nzuri”
akasema Jenerali William na
kumtaka Nawal waingie
ndani.Miguu ya Nawal ilikuwa
inagongana kwa kile
alichokuwa
amekishuhudia.Katika wale
watu walioongozana na
Jenerali William
aliwashuhudia kwa macho
watu wawili waliokuwa
wanawatafuta kwa jasho na
damu.Assad Ismail na Sattar
Sayf Al Din
“Siamini ninachokiona
huu ni kama muujiza
mkubwa.Watu wote hawa
wawili Assad na Satter wote
tunawatafuta kwa kila
namna.Hadi mwili wangu
unatetemeka sikuwa
nimelitegemea kabisa jambo
hili.Lakini mbona hawana yale
masanduku ya
kirusi?Wamekipeleka wapi?
Au tayari wamekwisha anza
kukisambaza?akajiuliza Nawal
“Usiku wa leo lazima kila
kirusi kipatikane.Wamejileta
wenyewe kwenye mdomo wa
Mamba na hawatatoka
salama” akawaza Nawal
Jenerali William
akamuelezea Brenda
kumpeleka Nawal katika
chumba maalum cha
mapumziko wakati yeye
akiendelea na mazungumzo na
wageni wake.Nawal hakwenda
katika chumba cha mapumziko
bali alielekea moja kwa moja
chumbani kwake na kitu cha
kwanza alichokifanya ni
kuishika simu akampigia Ruby
“Hallo Ruby ! akasema
Nawal
“Nawal kuna nini?Mbona
unahema haraka haraka
namna hiyo?Kuna tatizo?
akauliza Ruby
“Ruby wako hapa !
akasema Nawal
“Akina nani
Nawal?akauliza Ruby
“Assad na Sattar wote
wako hapa.Wamekuja na
Jenerali William” akasema
Nawal
“Nawal una uhakika ni
wenyewe?
“Nimewashuhudia mimi
mwenyewe kwa macho
yangu.Wamefika muda si
mrefu wakiwa wameongozana
na Jenerali William”
“Yale masanduku mawili
aliyoshuka nayo Sattar
ndegeni ambayo tunaamini
yana kirusi yameletwa
hapo?akauliza Ruby
“Hapana Ruby kirusi
hakipo hapa.Yawezekana kuna
mahala kimehifadhiwa au
yawezekana tayari kimekwisha
pelekwa kusambazwa”
akasema Nawal
“Hapana bado
hakijasambazwa kwani mtu
pekee aliyeletwa kuja
kusambaza kirusi hicho ni
Sattar Sayf Al Din.Kama
hayuko nacho hapo basi lazima
kirusi hicho kimehifadhiwa
sehemu Fulani wakisubiri
muda ufike
wakisambaze.Nawal usiku huu
wa leo lazima tuhakikishe
tunakipata kirusi hicho.Ni kufa
na kupona leo lazima nyumba
hiyo ivamiwe tuwachuku watu
hao wote waliomo katika hiyo
nyumba na watatuonyesha
mahala kilipo kirusi.Nawal
endelea kufuatilia watu hao
kama wataondoka au watalala
hapo wakati tunaandaa kikosi
kwa ajili ya kuvamia nyumba
hiyo.Kuanzia mchana wa leo
tumekuwa tukiichunguza
nyumba hiyo na kuona namna
walivyojipanga
kiulinzi.Makomando wetu
wako tayari na muda
utakapowadia watavamia
nyumba hiyo.Nawal
tunakutegemea sana uweze
kuwasaidia timu ya
makomando watakapofika
hapo” akasema Ruby
“Tayari nimekwisha
yasoma mazingira ya hapa na
ulinzi ulivyo hivyo hakuna
tatizo nitasaidiana na timu
itakayofika hapa” akasema
Nawal na kumpa Ruby
maelekezo kadhaa
Mara tu alipomaliza
kuzunguma na Nawal Ruby
akampigia Gosu Gosu
akamtaka afike ofisini kwake
mara moja akamueleza
kuhusiana na kile alichoelezwa
na Nawal
“Ruby mpaka hapo
naamini tayari tumekwisha
kipata kirusi.Usiku huu lazima
tuwapate hawa magaidi wote
pamoja na
kirusi.Nitaongozana na
makomando wetu
watakaokwenda kuvamia
nyumba hiyo” akasema Gosu
Gosu
“Hapana Gosu
Gosu.Tuwaache makomando
waende.Wewe utakuwa na kazi
ya kuwahoji akina Assad
kufahamu mahala kilipo kirusi
pale watakapokuwa
wameletwa hapa” akasema
Ruby
“Ruby kwa nini hutaki
nishiriki katika misheni siku
hizi? Kila ninapotaka kushiriki
katika misheni unanizuia.You
don’t trust me?akauliza Gosu
Gosu
“Si hivyo Gosu Gosu.Sitaki
kuyaweka hatarini maisha
yako wakati tayari tunacho
kikosi kinachoweza
kupambana .Kumbuka huko
wanakoenda kunalindwa na
wanajeshi wa Marekani ambao
wana mafunzo ya hali ya juu
hivyo itakuwa ni nusu
vita.Naamini kikosi chetu cha
makomando kina uwezo
mkubwa sana wa kuweza
kufanikisha misheni hii.Kama
nilivyokuahidi kwamba wewe
utafanya kazi ya kuwahoji
akina assad watakapoletwa
hapa” akasema Ruby
“Ruby imekuaje ukabadili
mawazo leo na unataka
niwahoji magaidi?akauliza
Gosu Gosu
“Kwa namna yoyote ile
tunahitaji kukipata kirusi
hivyo basi kila aina ya mbinu
lazima itumike wakati wa
kuwahoji magaidi hao ili
waweze kufunguka kirusi kiko
wapi”
“Sawa Ruby nitaifanya
kazi hiyo” akasema Gosu Gosu
kisha wakatoka kwenda
kuanza maandalizi kwa ajili ya
misheni ile
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 5
Kikosi cha makomando
tisa wa SNSA kilikaribia kufika
katika nyumba anakoishi
mkuu wa vikosi vya wanajeshi
wa Marekani walioko
Tanzania.Wakati kikosi hicho
kikiikaribia nyumba hiyo
wenzao waliokuwa katika
helkopta maalum
wanayoitumia katika
operesheni mbali mbali za
usiku tayari walikwisha fika
usawa wa ile nyumba na
walikuwa wanasubiri kupewa
taarifa kuwa kila kitu tayari ili
helkopta iweze kushuka chini
na kushusha kikosi cha
makomando ambacho
kitadhibiti eneo la juu la
nyumba ile.
Nawal ambaye alikuwa
ndani ya ile nyumba akapewa
taarifa kuhusu vikosi vile
kuikaribia nyumba ile.Bado
Jenerali William na akina
Assad walikuwa wanaendelea
na mazungumzo katika sebule
ya chini.
Nawal akatoka chumbani
kwake taratibu akaenda jikoni
ambako hakukuwa na mtu.Ni
sauti za maongezi ya akina
William ndizo zilisikika.Nawal
akiwa na vifaa vyake katika
begi akakata waya unaopeleka
umeme katika jiko kubwa la
kupikia halafu akafanya
utundu wa kuunganisha nyaya
na shoti kubwa ya umeme
ikatokea iliyosababisha
umeme kukatika ghafla jumba
lote likawa giza.Haraka haraka
akarejea chumbani kwake na
kuwajulisha akina Ruby
kwamba tayari umeme
umekatika.
Baada ya kupewa taarifa
ya umeme kukatika,helkopta
ya makomando ambayo
inatumia teknolojia ya hali ya
juu ambayo haina mlio ikaanza
kushuka taratibu na ilipofika
usawa Fulani makomando
wakaanza kushuka kwa
kutumia miavuli.Tayari
walikuwa wanafahamu upande
ule wa juu kulikuwa na
wadunguaji sita.Kutokana na
giza wadunguaji wale
hawakuweza kuwaona
makomando wa SNSA
walipokuwa wakishuka na
hawakuwa na wazo lolote la
kuvamiwa.Waliendelea
kuzungumza wakati wakisubiri
umeme uwake.
Makomando wa SNSA
wote walikuwa wamevaa
miwani ya kuwawezesha
kuona sehemu za giza na
waliweza kuwaona vizuri
namna wadunguaji wale
waliokuwa juu ya ile nyumba
walivyokaa na baada ya
kupewa amri risasi kama mvua
zilitoka katika bunduki zao
zilizofungwa viwambo vya
kuzuia sauti.Kufumba na
kufumbua wadunguaji wote
walikuwa chini.Makomando
wa SNSA wakatua taratibu na
kulidhibiti eneo la juu la
nyumba ile na kila mmoja
akachukua nafasi yake.Baada
ya kulidhibiti eneo la juu kazi
iliyoifuata ni kuwasafishia njia
kikosi cha chini ambao
walikuwa mita chache kutoka
katika jumba lile.Kwa msaada
wa miwani ile waliyokuwa
wameivaa ya kuona kwenye
giza makomando waliokuwa
wametawanyika katika sehemu
ya juu ya ile nyumba
wakajipanga tayari kwa ajili ya
kuanza kuwaondoa wanajeshi
waliokuwa wakilinda upande
wa chini.
Ndani ya nyumba bado
zoezi la kufuatilia chanzo cha
hitilafu iliyopelekea umeme
kukatika liliendelea.Wanajeshi
walikuwa wanapita chumba
kimoja kimoja
kuchunguza.Nawal akafungua
mlango wa chumba chake
akatoka na kuanza kushuka
chini akakutana na wanajeshi
wale waliokuwa wanafuatilia
kujua chanzo cha hitilafu ile ya
umeme.Wanajeshi wale
wakamtaka radhi kwa hitilafu
ile kutokea wakamuahidi kuwa
ndani ya muda mfupi umeme
utarejea.
Nawal akapita sebuleni
ambako Jenerali William na
akina Assad walikuwa
wanaendelea na
maongezi.Walikuwa
wanatumia taa maalum
inayotumia betri
“Chloe” akaita Jenerali
William baaada ya kumuona
Nawal akipita pale sebueleni
“Kumetokea hitilafu ya
umeme hapa ndani lakini
tatizo hilo linashughulikiwa na
muda si mrefu umeme
utarejea” akasema Jenerali
William
“Nimeshindwa kukaa
ndani kuna joto kali sana ngoja
nipunge upepo hapo nje hadi
umeme utakaporejea”
akasema Nawal na kutoka nje
akaenda kujibanza sehemu na
kutuma ujumbe kwa Ruby
akimjulisha kuwa Assad na
Sattar bado wapo mle ndani
akawahimiza kufanya hima
kwani tayari wamekwisha anza
kufuatilia kujua hitilafu ile ya
umeme imetokea wapi.
Mara tu baada ya Ruby
kupokea ujumbe ule kutoka
kwa Nawal,akampa taarifa
mkuu makomando waliokuwa
upande wa juu.Tayari kila
komando alikuwa amelenga
mwanajeshi na amri ikatolewa
ya kuwafagia.Mvua ya risasi
kutoka katika bunduki
zilizofungwa viwambo vya
sauti ikaanza kunyesha na
baada ya sekunde kadhaa
wanajeshi wote walikuwa
wakilinda sehemu ya chini ya
nyumba ile walikuwa
chini.Bila kukawia kikosi cha
makomando waliokuwa nje
kikafika kwa haraka na kuvuka
geti kisha wakachukua nafasi
ili kuhakikisha hakuna hatari
yoyote.Nawal akapewa
maelekezo kwamba aende
akaungane na kikosi kile cha
makomando akawafuata na
kujitambulisha kwao
akawajulisha kuwa watu
wanaowatafuta wapo sehemu
ya chini ya nyumba
ile.Makomando wale
wakajipanga vyema na kuanza
kusogelea mlango mkubwa wa
kuingilia ndani huku wale
waliokuwa upande wa juu wa
nyumba ile wakishuka chini
Wakati wakiendelea na
maongezi Jenerali William
akastushwa na mlio wa kitu
akawataka akina Assad
wanyamaze kimya
“Kuna nini
Jenerali?akauliza Assad na
Jenerali William akamfanyia
ishara ya kukaa kimya.Zilipita
sekunde kadhaa Jenerali
William akaupeleka mkono
wake wa kulia kifuani kwake
akabonyeza kidude katika
redio yake ya mawasiliano na
kuita
“Charles ! Charles !
Unanisoma?
Hakupata jibu lolote
“Alpha ! Alpha
unanisoma?akaita tena lakini
hakujibiwa.Akasimama na
kutoa bastora yake
“Kuna kitu hakiko sawa
hapa ! akasema akionekana
kuwa na wasiwasi
“Kuna nin……..” Assad
akataka kuuliza lakini sauti
kali ikawaamuru wasimame
kama walivyo.Walivamiwa na
watu waliokuwa wamefunika
nyuso zao.Kwa kasi ya aina
yake Assad akataka kuinyakua
bastora yake iliyokuwa mezani
lakini kabla mkono wake
haujaifikia akapigwa risasi ya
bega akaanguka chini..
“Wekeni silaha zenu chini
taratibu” Sauti ikawaamuru
Jenerali William na
Sattar.Taratibu Jenerali
William akaiweka bastora yake
chini,Sattar naye akachomoa
bastora yake na kuiweka chini
wakainua mikono juu.Haraka
haraka wakafungwa pingu na
kupandishwa sehemu ya juu ya
nyumba ile.Assad akapewa
huduma ya haraka ya kuzuia
damu kuvuja kwa wingi kisha
naye akafungwa pingu na
kupandishwa juu ambako
tayari helkopta ilikuwa imetua
akaingizwa katika helkopta
pamoja na akina
Sattar.Upekuzi uliendelea
ndani ya nyumba ile na baada
ya muda wanawake wawili
waliokuwa wahudumu
wakatolewa na kuingizwa
katika helkopta kisha ikapaa
na kuondoka.
Ruby na makomando
wengine wakaingia katika
magari yao mawili na
kuondoka eneo lile.
“Hii ni moja ya operesheni
tamu sana ambayo nimewahi
kushiriki.Wanajeshi wale
hawakujua kama wanaweza
kuvamiwa hivyo hawakuwa
wamejiandaa.Sifahamu
Marekani watatoa tamko gani
kesho asubuhi pale
watakapokuta miili ya
wanajeshi wao wakiwa
wameuawa.Lakini haya yote ni
malipo ya udhalimu wao.Usiku
wa leo hakuna kulala hadi
kirusi kipatikane.Haijalishi
damu kiasi gani itamwagika
lakini lazima kirusi kipatikane”
akawaza Nawal akiwa garini
wakielekea makao makuu ya
SNSA.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 6
Helikopta ilitua ofisi kuu
za SNSA ,mtu wa kwanza
kushushwa alikuwa Assad
aliyekuwa amepigwa risasi ya
bega akakimbizwa katika
kitengo cha afya ili kupatiwa
matibabu.Wakashushwa
Jenerali William na Sattar
wakiwa wamefungwa pingu na
kufunikwa na mifuko vichwani
Gosu Gosu akaelekeza
wapelekwe katika chumba cha
chini ya ardhi.Mwisho
wakashushwa wale wahudumu
wawili wakapelekwa katika
chumba kingine
“Ahsanteni sana kwa kazi
nzuri” akasema Ruby baada ya
kupewa taarifa ya namna
operesheni ile ilivyokwenda
“Makomando
wameimaliza kazi yao sasa
mpira umekuja kwetu”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu leo nakuachia
uhuru fanya kila uwezalo
kuwafungua hawa
watu.Kipaumbele cha kwanza
ni kujua mahala kilipo kirusi
na baada ya hapo tutaendelea
kuwahoji mambo mengine
yanayohusiana na machafuko
yaliyotokea lakini angalizo
Gosu Gosu jitahidi kudhibiti
hasira” akasema Ruby
“Usihofu Ruby kabla ya
mapambazuko lazima tuwe
tumekipata kirusi” akasema
Gosu Gosu na kumsubiri
Nawal ili kazi ya kuwahoji
watu wale waliokamatwa ianze
mara moja.
TEHRAN – IRAN
Saa nne za usiku kwa saa
za Iran,waziri wa ulinzi wa
Iran brigedi Jenerali Ahsan
Javad aliwasili katika makazi
ya bilionea Vahid
Ghorbani.Alipokewa na Vahid
mwenyewe na kumkaribisha
ndani.Vahid ni mmoja wa
wafanya biashara wakubwa na
wanaoheshimika sana nchini
Iran.
“Karibu sana Ahsan”
akasema Vahid
“Nashukuru Vahid na
samahani kwa kuchelewa
kuja.Nilikuwa na mambo
mengi sana siku ya leo”
akasema Brigedia Jenerali
Ahsan.
“Usijali
Ahsan.Ninafahamu majukumu
yako mengi” akasema Vahid na
baada ya maongezi mafupi ya
utangulizi Ahsan akasema
“Vahid nimepita kwako
mara moja kukusikilza kama
ulivyoniomba.Nikitoka hapa
kuna sehemu ninaelekea hivyo
sintachukua muda mrefu hapa
kwako” akasema Ahsan
“Ahsan nimekuita hapa
ninahitaji msaada wako”
“Unahitaji nikusaidie nini
Vahid?
“Kuna raia wetu
waliokuwa wamepotea
wamerejea leo” akasema Vahid
“Ndiyo wamerejea
leo.Umekuwa ni kama mujiza
kwetu kwani tayari tulikwisha
hisi wameuawa.Hatukuwa na
tegemeo la kuwaona tena
wakiwa hai.Tumefurahi sana
kuwaona tena ndugu zetu
wale” akasema Ahsan
“Kuna mtu mmoja alikuwa
ameongozana nao ambaye si
raia wa Iran anaitwa Abu
Zal…….” akasema Vahidi lakini
Ahsan akamkatisha
“Abu Zalawi.Kwa taarifa
tuliyoipata ni raia wa Saudi
Arabia na anajishughulisha na
ugaidi.Abu Zalawi ndiye
aliyelipua ubalozi wa Marekani
jijini Dar es salaam siku
chache zilizopita” akasema
Ahsan na kumstua sana Vahid
“Ni gaidi?! Vahid akauliza
kwa mshangao
“Ndiyo ni gaidi !
“Hii inashangaza”akasema
Vahid
“Ni jambo
linalomshangaza kila mtu
lakini tutawafanyia mahojiano
na kujua nini hasa kimetokea
hadi watu wetu wakajikuta
wakiwa na huyu gaidi”
akasema
“Nini mipango yenu
kuhusiana na huyu
mtu?Hamuoni kama anaweza
kuongeza matatizo na
Marekani endapo wakifahamu
kuwa mtu aliyelipua ubalozi
wake yuko hapa nchini kwetu?
Akauliza Vahid
“Kwa sasa ni mapema sana
kusema chochote kuhusu huyu
mtu hadi pale tutakapowahoji
watu wetu na kufahamu kwa
undani nini hasa kilichotokea
na imekuaje wakajikuta
wakiwa na huyu gaidi.Baada ya
hapo tutafanya maamuzi”
akasema Ahsan na ukimya
mfupi ukapita
“Mbona umeuliza kuhusu
huyu jamaa? Akauliza Ahsan
“Ahsan kuna jambo nataka
kuliomba.Yawezekana ni
jambo kubwa na
hukulitegemea lakini
nakuomba unisaidie”
“Sema unachohitaji Vahdi
nitakusaidia,wewe ni zaidi ya
rafiki” akasema Ahsan
“Ninataka kuonana na Abu
Zalawi” akasema Vahid na
mstuko mkubwa ukaonekana
usoni kwa Ahsan
“Unataka kuonana na Abu
Zalawi? Akauliza Ahsan akiwa
bado
anashangaa.Hakutegemea
kama Vahid angeweza
kumuomba kitu kama kile
“Ndiyo Ahsan ninataka
kuonana na Abu Zalawi”
Ahsan akavuta pumzi
ndefu na kuuliza
“Vahid mimi nawe
tumefahamiana muda mrefu
sana toka tukiwa vijana
wadogo masomoni na
tumeendelea kuwa marafiki
wakubwa hata sasa.Nini
sababu ya kutaka kuonana na
huyu mtu? Naomba unieleze
bila kunificha tafadhali”
akasema Ahsan
“Nilikueleza kuhusiana na
kifo cha mwanangu Najma”
“Ndiyo ulinieleza”
“Kuna jambo ambalo
sikuwa nikilifahamu
kuhusiana na Najma ambalo
nimelifahamu leo hii” akasema
Vahid na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Najma alikuwa ameolewa
lakini alifanya siri hakutaka
nifahamu”
“Alikuwa ameolewa?
“Ndiyo lakini kwa siri na
hakutaka nifahamu.Kwa
mujibu wa mama yake alitaka
kunipa taarifa hizo yeye
mwenyewe lakini hakufanya
hivyo hadi mauti
yalipomkuta.Kwa bahati
mbaya aliyekuwa mume wake
ni Abu Zalawi”
“Abu Zalawi?! Ahsan
akazidi kushangaa
“Ndiyo.Nimeambiwa
kwamba ndiye aliyekuwa
mume wa Najma”
“Najma ametoka wapi na
huyu gaidi? Binti yako alikuwa
ni msomi mzuri na mwenye
sura ya kimalaika
inawezekanaje hadi akajikuta
akiingia katika mahusiano na
huyu jamaa?akauliza Ahsan
“Ahsan hata mimi
sifahamu nini kilitokea lakini
nilichoelezwa ni hicho kwamba
aliolewa na Abu Zalawi”
akasema Vahid
“Vahid yawezekana si Abu
Zalawi huyu gaidi.Yawezekana
kuna Abu Zalawi mwingine”
akasema Ahsan
“Ahsan ninaomba msaada
wako niweze kuonana na huyu
Abu Zalawi na kuzungumza
naye japo kwa dakika tano tu
ili niweze kupata uhakika
kama kweli ni yeye aliyemuoa
mwanangu Najma” akasema
Vahid
“Sawa nitakusaidia
Vahid.Nilikueleza kuwa
nikitoka hapa ninaelekea
sehemu Fulani.Ninakwenda
kuwatembelea mashujaa wetu
waliorejea leo kujua
maendeleo yao na kwa kuwa
umeniomba basi baada ya
kutoka hapo hospitali
tutaelekea mahala
alikopelekwa Abu Zalawi
ukaonane naye” akasema
Ahsan.Hakukuwa na muda wa
kupoteza wakaingia katika gari
la Ahsan na kuondoka
kuelekea hospitali.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 7
Saa tano za usiku waziri
wa ulinzi wa Iran Brigedia
Jenerali Ahsan Javad aliwasili
katika hospitali ya jeshi
walikopelekwa Yasser Wazir
na wenzake baada ya kurejea
nyumbani wakitokea mahala
kusikojulikana.Mpaka muda
huu hawakuwa wamehojiwa
chochote kuhusiana na mahala
walikokuwa kwa muda wote
waliokuwa
wamepotea.Brigedia Jenerali
Ahsan Javad hakuwa peke
yake alikuwa ameongozana na
Sassan Mahmoud
anayeongoza wizara ya ujasusi
ya Iran MOIS na vile vile
alikuwa na Vahid Ghorbani
mfanyabiasha mkubwa nchini
Iran na rafiki yake wa karibu.
Waliwatembelea na
kukagua maendeleo ya akina
Yasser na kujiridhisha kuwa
wanapatiwa huduma ya afya ya
hali ya juu.Baada ya hapo
wakaondoka kuelekea mahala
alikopelekwa Abu
Zalawi.Baada ya mwendo wa
dakika kadhaa wakafika katika
nyumba moja kubwa yenye
ulinzi mkali inayotumiwa na
MOIS kwa shughuli zake na
kubwa zaidi ikiwa ni kuhifadhi
watu mbali mbali wanaohojiwa
na idara hiyo.
Geti la nyumba
likafunguliwa magari
yakaingia,milango
ikafunguliwa haraka haraka na
msimamizi mkuu wa nyumba
ile akatoka kuja kuwapokea
wageni akawakaribisha ndani
“Anaendeleaje mgeni
wetu? Akauliza Sassan
Mahmoud mkuu wa MOIS
“Anaendelea vizuri.Kabla
ya kumleta hapa tulimpeleka
kwanza katika hospitali yetu
akaangaliwa afya yake na
kupatiwa matibabu ndipo
tukamleta hapa.Anaendelea
vizuri” akasema Yule
msimamizi wa ile nyumba
kisha Ahsan akamtaka Sassan
wazungumze pembeni.Baada
ya mazungumzo yaliyochukua
dakika zipatazo tano Sassan
akamtaka Yule msimamizi wa
ile nyumba kuzima kamera
zote kwa muda halafu
akamtaka awapeleke katika
chumba alimowekwa Abu
Zalawi.Mlango wa chumba
ukafunguliwa wakaingia ndani
na kumkuta Mathew akiwa
amejilaza kitandani akiwa
amefungwa bandeji sehemu
mbali mbali za mwili wake
zilizokuwa na vidonda.Mathew
hakuwa na wasiwasi hata
chembe akainua kichwa chake
akawatazama watu wale
waliokuwa wanamtazama kwa
woga
“Abu Zalawi
unaendeleaje?akauliza Ahsan
“Ninaendelea vizuri”
akajibu Mathew
“Karibu sana Iran.Mimi
naitwa Brigedia Jenerali Ahsan
Javad waziri wa ulinzi wa
Iran.Nimekuja kukutazama
kujua maendeleo yako”
“Ahsante mheshimiwa
waziri ninaendelea vyema”
“Sawa Abu ninashukuru
kama unaendelea vyema.Mimi
nawe tutakuta tena pale afya
yako itakapokuwa imekaa
vizuri.Kwa sasa endelea
kupumzika na
ninakuhakikishia uko salama
hivyo siwe na hofu yoyote”
akasema Ahsan
“Nashukuru sana
mheshimiwa waziri” akasema
Mathew
“Kabla sijaondoka kuna
mtu ambaye anahitaji kuonana
nawe” akasema Ahsan na
Vahid akaitwa mle
chumbani.Watu wote
wakatoka na kuufunga mlango
akabaki Mathew na Vahid.
“Karibu” akasema Mathew
akimshangaa Vahid namna
alivyokuwa akimtazama
“Abu Zalawi” akasema
Vahid kwa sauti ndogo
“Ndiyo ni mimi
karibu.Wewe ni nani? Akauliza
Mathew ambaye aliinuka na
kukaa kitandani
“Naitwa Vahid Ghorbani”
“Karibu
Ghorbani.Nikusaidie nini?
Akauliza Mathew.Vahid akatoa
simu na kuzitafuta namba za
Habiba akapiga
“Kabla sijazungumza nawe
chochote kuna mtu ambaye
unatakiwa uzungumze naye
simuni” akasema Vahid na
kumpatia Mathew ile simu
“Hallow” ikasema sauti ya
mwanamke upande wa pili
sauti ambayo haikuwa ngeni
masikioni mwa Mathew
“Hallow” akasema Mathew
“Mathew
Mulumbi.Nimefurahi tena
kuisikia sauti
yako.Unazungumza na
Habiba” akasema Habiba
Jawad akitumia lugha ya
kiswahili
“Mama Habiba.! Akasema
Mathew naye akishangaa
“Mathew sina muda
mwingi wa kuzungumza
nawe.Kuna jambo ambalo
nataka nikufahamishe”
akasema Habiba
“Nakusikiliza mama”
“G2o tayari wamefahamu
kila kitu kuhusu wewe kuwa si
gaidi bali ni jasusi” akasema
Habiba na Mathew akastuka
sana
“wamefahamuje?akauliza
Mathew
“Wamepata taarifa zote
kutoka Mossad”
“Bastard ! akasema
Mathew kwa hasira
“Usihofu Mathew
japokuwa wamefahamu kila
kitu kuhusu wewe lakini kila
kitu kinaendelea kama
kawaida.Misheni yako
inaendelea kama kawaida
kwani tayari ndani ya G20
wamekwisha gawanyika.”
akasema Habiba na kumueleza
Mathew kila kitu
kinachoendelea
“Kwa hiyo Mathew
nimekupigia kukupa tahadhari
kuhusiana na mpango huu wa
kukuua kwa kuwatumia
majasusi wa Mossad” akasema
Habiba
“Mama nakushukuru sana
kwa kunipa tahadhari
kuhusiana na mpango huo wa
kuniua.Ninakuahidi sintaishia
njiani nitahakikisha
ninalimaliza hili kundi la G20”
“Nakutakia kila la heri
Mathew.Kila nitakapokuwa
nikipata taarifa zozote
nitajitahidi nikufikishie lakini
ukiona kimya kwa muda wa
wiki moja kuanzia sasa ujue
tayari nimekwisha kufa”
“Mama Habiba tafadhali
endel……….”
“Kwa heri Mathew.Kuwa
makini” akasema Habiba na
kukata simu.
“Tayari umeupata ujumbe
wako? Akauliza Vahid
“Ndiyo nimeupata
ninashukuru sana” akasema
Mathew na kumrejeshea Vahid
simu yake
“Abu Zalawi nimepewa
muda mfupi wa kuzungumza
nawe.Naamini mimi
hunifahamu na hujawahi
kuniona”
“Ni kweli sikufahamu”
akasema Mathew
“Mimi ni…………..”
akasema Vahid na kusita
“Karibu Iran Abu Zalawi”
akasema Vahid na kugonga
mlango ukafunguliwa Mathew
akabaki anashangaa
“Alitaka kunieleza nini
huyu jamaa halafu
akasita?akajiuliza Mathew na
kuinuka akaketi kitandani.
“Kazi imekuwa kubwa
zaidi ya nilivyodhani.Kama
hawa jamaa tayari
wamekwisha nifahamu mimi
ni nani na wanataka kuniua
natakiwa kutumia akili kubwa
ili waweze kuniamini tena.Kwa
namna yoyote ile lazima
nirejee tena Marekani
kumaliza kazi
niliyoianza.Siwezi kuishia
njiani lazima nifike mwisho na
kukifutilia mbali kikundi cha
G20.Namshukuru Habiba kwa
kunipa taarifa za mpango wao
wa kutaka kuniua.Nina
wasiwasi sana kama wakati
nitakapomaliza misheni yangu
Habiba ataendelea kuwa hai
kwani hawa jamaa tayari
wanadai amewasaliti.Naomba
Mungu amsaidie huyu mama
awe hai na ashuhudie kwa
macho yake namna kundi la
G20 linavyosambaratishwa”
akawaza Mathew
“Kama wanataka kuniua
mimi na kusitisha ile misheni
waliyonituma,ninapata picha
kwamba hata wale jamaa
niliowaokoa watakuwa
mashakani.Naamini nao pia
watakuwa katika mpango wa
kuuawa ili isijulikane kama
walikuwa wametekwa na
Marekani.Lazima niwasadie
kwani wale ndio kinga yangu”
akawaza Mathew
Baada ya kutoka katika
chumba cha Mathew,Vahid
alipelekwa katika gari ambako
Brigedia Jenerali Ahsan
alikuwa anamsubiri,kisha
wakaondoka
“Nimeshindwa
kumwambia Abu Zalawi kuwa
mimi ndiye baba yake
Najma.Nimejikuta nikimuonea
huruma ghafla Yule kijana
baada ya kumuona namna
mwili wake ulivyo na vidonda
vingi.Kwa nini kijana Yule
akaamua kujiingiza katika
masuala ya ugaidi.Kwa nini
Mossad wanataka
kumuua?Ninahitaji kupata
tena wasaa mwingine
nizungumze naye kwa kirefu
zaidi” akawaza Vahid wakiwa
garini baada ya kuondoka
mahala alikopelekwa Mathew
Wakati Ahsan na Vahid
wakiondoka katika nyumba
alikopelekwa Mathew,katika
moja ya mtaa jijini Tehran
watu watatu walikuwa
wamekaa juu ya nyumba
Fulani wakizungumza.Wawili
miongoni mwa watu hao
walikuwa majasusi kutoka
Mossad walioko jijini Tehran
“Nawaahidi hadi kufika
kesho mchana tayari nitakuwa
nimepata taarifa za mahala
alipo Abu Zalawi pamoja na
wale raia wengine waliokuwa
wamepotea” akasema Zana
Behnam ambaye anafanya kazi
katika wizara ya ujasusi na
usalama wa taifa ya Iran.
“Tunashukuru
Zana.Tunaamini
hautatuangusha” akasema
Avner jasusi kutoka Mossad
“Siwezi
kuwaangusha.Mimi nanyi
tumekwisha shirikiana katika
mambo mengi” akasema
Zana.Avner akatoa bahasha
kutoka katika mfuko wa koti
na kumpatia Zana
“Hiki ni nusu ya kiasi cha
fedha ulichokihitaji kwa ajili ya
kazi hii.Pale utakapokuwa
umekamilisha jukumu lako
basi utamaliziwa kiasi
kilichobaki” akasema Avner na
bila kuhesabu Zana akaiweka
bahasha mfukoni wakaagana
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
“Nawal hongera sana
umefanya kazi nzuri” akasema
Ruby baada ya Nawal kuwasili
na gari la makomando
“Ahsante Ruby lakini
tutapata muda wa
kuzungumza na kupongezana
hapo baadae kwa sasa
tunatakiwa kuitumia vyema
kila dakika tuliyonayo kabla ya
mapambazuko ili kufahamu
mahala kilipo kirusi na
kukichukua kwani ikifika
asubuhi itagundulika kile
tulichokifanya na yawezekana
tusikipate tena kirusi hicho
hivyo kufa au kupona lazima
usiku huu kirusi
kipatikane.Tunao watu
wanaofahamu mahala kirusi
kilipo hivyo hakuna kuwaonea
huruma lazima tutumie kila
mbinu hadi waonyeshe
walipokificha kirusi hicho”
akasema Nawal na mkuu wa
kikosi cha makomando
akatokea na kumkabidhi Ruby
vazi Fulani
“Hili ni moja ya vazi
tumelikuta katika nyumba ile
baada ya kufanya
upekuzi.Yapo mengine kumi
na sita na vazi hili ni maalum
kwa ajili ya kujikinga na hewa
ya sumu au maambukizi ya
virusi”akasema
“Washenzi hawa
walikwisha jiandaa kujikinga
na virusi wakati sisi
tukiteketea” akasema Ruby
“Mtu wa kwanza kumuhoji
ambaye anafahamu kilipo
kirusi ni Jenerali
William.Huyu nitamuhoji
mimi mwenyewe” akasema
Gosu Gosu kisha maandalizi
kwa ajili ya kuanza kumuhoji
Jenerali William
yakaanza.Maandalizi
yalipokamilika Jenerali
William akaingizwa katika
chumba maalum kwa ajili ya
mahojiano.Gosu Gosu Ruby na
Nawal walimtazama katika
kioo kikubwa wakiwa katika
chumba kingine .Gosu Gosu
akavuta pumzi ndefu na
kutoka ndani ya kile chumba
akaingia katka chumba cha
mahojiano akavuta kiti na
kuketi
“Habari yako Jenerali
William” akasema Gosu Gosu
lakini Jenerali William
hakujibu kitu akamtazama
Gosu Gosu kwa macho ya
dharau
“Naitwa Papi G0su
Gosu,ni mwanajeshi.Kwa
miaka zaidi ya ishrini nimeishi
msituni nikipigana vita hivyo
nataka tuzungumze kama
wanajeshi” akasema Gosu
Gosu na Jenerali William
akacheka kidogo
“Nini maana ya mchezo
huu mlioufanya?akauliza
Janerali William
“Huu ni mchezo wa kijinga
sana mmeufanya.Sisi tuko
hapa kwa ajili ya kuwasaidia
kutafuta amani katika nchi
yenu halafu ninyi mnatufanyia
hivi ! Ninawahakikishia
kwamba hiki mlichokifanya
kitakuwa na athari kubwa sana
kwenu.Hamtabaki salama hata
kidogo ! akasema Jenerali
William
“Huna hata aibu ya
kusema mmekuja kutusaidia !
Akasema Gosu Gosu
akionekana kuanza kupandwa
na hasira
“Ndiyo tumekuja
kukusaidieni kutafuta amani
baada ya kuanza kuuana
wenyewe kwa wenyewe lakini
malipo yake ndiyo
haya.Mnafanya jambo bay
asana kuteka na kuua walinda
amani ! akafoka Jenerali
William
“Jenerali William sisi si
watoto wadogo wa kushindwa
kutambua mambo.Karibu
vurugu nyingi zinazotokea
barani Afrika nchi
zilizoendelea zina mkono
wake.Mnatengeneza
machafuko kwa malengo
mnayoyajua wenyewe halafu
mnaleta vikosi vyenu mkijidai
mnakuja kutusaidia kutafuta
amani kumbe mna ajenda
zenu za siri.Tunafahamu kila
kitu mnachokifanya Afrika na
sasa mwisho wenu umefika !
akasema Gosu Gosu
“Sisi hatuna sababu yoyote
ya kuleta machafuko kwa bara
masikioni kama hili.Sisi ni
taifa kubwa lenye uchumi
mkubwa kuliko yote
duniani.Ni taifa lenye nguvu
kubwa kijeshi kuliko yote
duniani kwa nini tusumbuke
na watu masikini kama
waafrika? Hizo ni dhana
potofu mnazojenga kwamba
vikosi vya Marekani au nchi
nyingine kubwa vikija kulinda
amani Afrika vinakuwa na
ajenda zao za siri wakati si
kweli.Sisi ni taifa
linaloheshimu haki za
binadamu na hatuko tayari
kuona haki za binadamu
zikivunjwa na watu kuuawa
ndiyo maana tuko mstari wa
mbele katika kuhakikisha
tunapeleka vikosi vyetu haraka
sana sehemu yoyote ile
ambako kuna kuwa na
uvunjifu mkubwa wa haki za
binadamu.Tazama hivi majuzi
vurugu zilizotokea hapa nchini
kwenu mkaanza kuuana
wenyewe kwa wenyewe kwa
sababu ya dini hivyo kwa
sababu ya dini,tumeleta vikosi
vyetu kuja kuwasaidia kutafuta
amani !
“Mwongo mkubwa wewe !
akasema Gosu Gosu kwa ukali
huku akigonga meza
“Nilikwambia tunafahamu
kila kitu mlichokifanya na
mipango yenu yote
tunaifahamu hivyo usijaribu
kunidanganya.Unadhani
hatujui mnachokifanya kule
Tanga? Tunafahamu namna
mnavyopora tani na tani za
mafuta ya kutoka
Uganda.Tunafahamu
machafuko haya yote
yaliyotokea mmeyatengeneza
ninyi kwa ajili ya kujipatia
mafuta.Tunafahamu kila kitu
Jenerali na msituone tuko
kimya mkajua kuwa
hatufahamu chochote !
akasema Gosu Gosu kwa ukali
“Hiki ni kichekesho wewe
kijana.Marekani haina haja ya
kuja kuchukua mafuta huku
Afrika.Tuna akiba kubwa ya
mafuta na tunaendelea
kutengeneza mafuta ya
kutosha kutoka katika mimea
na tumewekeza sana katika
teknolojia rahisi ya
kutengeneza magari na
mitambo isiyotumia mafuta
mengi hivyo basi hatuna haja
na mafuta machafu kutoka
Uganda ! akasema Jenerali
William kwa dharau
“Gosu Gosu kompyuta
yetu inatuonyesha William
amepatwa na mstuko mkubwa
ulipomtajia suala hilo la
kuchukua mafuta kule
Tanga.Endelea kukazia hapo
hapo ! Ruby akamjulisha Gosu
Gosu kupitia kifaa alichokuwa
amekivaa sikioni.
“Tunafahamu kila kitu
Jenerali William kuhusiana na
mipango yenu yote
mnayoipanga na magaidi wa
IS.Bado muda kidogo tu dunia
yote itafahamu kila kitu
ambacho kinafanywa na taifa
lako kwa siri.Itakuwa ni aibu
kubwa kwa taifa kubwa kama
Marekani pale
tutakapoitangazia dunia
namna inavyozinyonya nchi
masikini ! akasema Gosu Gosu
na Jenerali William
akaonekana kupandwa na
hasira
“Huo ni upumbavu
mkubwa ! akahamaki Jenerali
William
“Marekani haiwezi
kushirikiana na magaidi wa IS
au kikundi chochote cha
kigaidi.Tumekuwa mstari wa
mbele katika kupambana
ugaidi duniani na katu
hatuwezi kushirikiana
nao.Hiki unachokitamka ni
kitu cha kijinga sana ! akasema
kwa ukali Jenerali William
huku akijaribu kuitikisa
mikono yake lakini ilikuwa
imefungwa barabara kwa
pingu zilizo katika kiti kile
maalum.
Gosu Gosu akalifungua
faili akatoa picha ya Assad
Ismail
“Unamfahamu huyu?
Akauliza Gosu Gosu
“Wewe kijana una
upungufu wa akili,maswali
gani hayo unaniuliza?
“Jenerali William hapa
hauna nguvu ya kufanya
chochote,tafadhali jibu kile
unachoulizwa kwa ufasaha”
akasema Gosu Gosu
“Kwa nini mmenileta hapa
ninyi watu wenye akili finyu?
Akafoka Jenerali William
“Sisi tuna akili finyu? Leo
utafahamu watu wenye akili
finyu ni watu wa aina gani !
akasema Gosu Gosu
“Unamfahamu huyu mtu
pichani? Gosu Gosu akauliza
“Simfahamu mtu huyu !
akajibu Jenerali William
“Hujawahi kumuona
sehemu yoyote? Akauliza Gosu
Gosu
“Nimekwambia sijawahi
kumuona na simfahamu !
akajibu Jenerali William
“Kama humfahamu
ninakufahamisha kuwa huyu
anaitwa Assad Ismail ni
kiongozi wa kundi la kigaidi la
IS ambaye ndiye
mnayemtumia katika
kuchochea vurugu za kidini
hapa nchini.Yeye na kundi lake
ndio wanaofanya mauaji ya
viongozi wa dini na
kushambulia nyumba za ibada
ili kujenga chuki miongoni
mwa waumini na kusababisha
washambuliane na kuuana”
akasema Gosu Gosu na sura ya
Jenerali William
ikabadilika.Gosu Gosu
hakumjali akatoa picha
nyingine
“Nafahamu hata
nikikuuliza huyu ni nani
utakana kumfahamu lakini
huyu anaitwa Sattar Sayf Al
Din.Naye vile vile ni mfuasi wa
IS” akasema Gosu
Gosu.Jenerali William alikosa
maneno ya kuongea akabaki
anaikodolea macho picha
ile.Gosu Gosu akatoa picha
nyingine akaiweka mezani.
“Picha hii ni ya mchana wa
leo.Hapa ni uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius
Nyerere Dar es salaam ambapo
Sattar aliwasili akitumia ndege
aina ya Gulfstream G650ER na
ndege hii hutumiwa na shirika
la ujasusi la Marekani CIA”
akasema Gosu Gosu na
kumtazama Jenerali William
ambaye macho yake
aliyaelekeza katika ile picha
mezani.Gosu Gosu akatoa
picha nyingine
“Hapa Sattar akishuka
ndegeni akiwa ameongozana
na wanajeshi wa
Marekani.Ukiitazama picha hii
Sattar ana masanduku
mawili.Tunafahamu
masanduku haya mawili yana
kirusi ndani yake ambacho
Sattar amekuja kukisambaza
hapa Tanzania”
“Sielewi
unachokizungumza wewe
kijana ! akafoka Jenerali
William
“Utanielewa tu Jenerali
William” akasema Gosu Gosu
“Marekani baada ya
kufanikiwa katika mpango
wake wa kuchukua mafuta ya
Uganda kupitia bandari ya
Tanga wana hofu kwamba
amani itarejea muda si mrefu
na vikosi vya Marekani
havitahitajika tena kuwepo
hapa Tanzania hivyo zoezi la
uchukuaji wa mafuta
litakoma.Mmetafuta namna ya
kuviwezesha vikosi vyenu
kuendelea kuwepo hapa nchini
kwa muda mrefu zaidi na
mmekuja na mpango wa
kusambaza kirusi hatari cha
maangamizi hapa Tanzania ili
muweze kuongeza vikosi
zaidi.Jenerali William sisi tuna
akili finyu kama ulivyosema
lakini tunafahamu kila kitu
kuhusiana na mipango yenu na
ninakuhakikishia kwamba
mipango yenu haitaweza
kufanikiwa” akasema Gosu
Gosu
“Huu ni upuuzi uliopitiliza
! akafoka Jenerali William
“Jenerali William kuna
kitu kimoja tu ambacho
ninataka kufahamu kutoka
kwako ambacho ndicho
kitakachokutoa salama humu
ndani.Nataka kujua kirusi hiki
alichokuja nacho Sattar kiko
wapi? Akauliza Gosu Gosu na
kumtazama Jenerali William
“Gosu Gosu usimuulize
tena swali lingine muache
kwanza atafakari njoo huku”
Ruby akamwambia Gosu Gosu
ambaye aliinuka
“Ninakuacha utafakari
baada ya muda nitarejea
tuendelee na mazungumzo
yetu.Nakupa angalizo Jenerali
William mimi ni mtu mbaya
mno na usiombe uingie katika
anga zangu ! Nitarejea baada
ya muda mfupi ! akasema
Gosu Gosu na kuchukua faili
lake akatoka ndani ya kile
chumba akaingia katika chmba
walichokuwamo akina Ruby
“Umemuanza vizuri na
kompyuta yetu hapa
inatuonyesha kwamba
amepatwa na mstuko
mkubwa.Hakutegemea kama
tungefahamu mipango yao ya
siri.Pamoja na hayo kuna
jambo lingine ambalo
tumelipata.Tumeifahamu
familia yake.Ana watoto wawili
wa kike ambao majina yao ni
Cynthia na Lisa.Vile vile ana
mke anaitwa Deborah”
akasema Ruby na kumpatia
Gosu Gosu picha za familia ya
Jenerali William
“Hii familia yake ni silaha
ya mwisho ambayo tutaitumia
katika kumfanya Jenerali
William afunguke endapo njia
nyingine za kumfungua
zitashindikana.Kabla ya
kurejea kumuhoji Jenerali
William tutamuhoji kwanza
Sattar na zoezi hili mtalifanya
wewe na Nawal.Wakati
mkiendelea kumuhoji Sattar
tutaendelea kumtesa Jenerali
William kwa kufungua muziki
mkubwa” akasema Ruby na
bila kupoteza muda Nawal na
Gosu Gosu wakaenda katika
chumba kingine cha
mahojiano alimo Sattar.Nawal
akavuta kiti akaketi Gosu Gosu
akasimama pembeni
“Sattar Sayf Al Din ndilo
jina lako? Akauliza Nawal
lakini Sattar hakujibu
kitu.Gosu Gosu ambaye
mikono yake ilikuwa myepesi
akakishika kichwa cha Sattar
na kukigongesha katika meza
mara mbili
“Ukiulizwa kitu unajibu
haraka ! akafoka Gosu Gosu
“Nakuuliza tena jina lako
ni Sattar Seyf Al Din? Akauliza
Nawal
“Ndiyo.Naitwa Sattar Sayf
Al Din”
“Umetokea nchi gani?
“Mimi ni raia wa Syria”
“Umeingia Tanzania
ukitokea Syria?akauliza Nawal
“Hapana nimetokea
Marekani”
“Umekuja kufanya nini
Tanzania? Akauliza Nawal na
Sattar akawa kimya
“Nakuuliza Sattar
Tanzania umekuja kufanya
nini? akauliza tena Nawal
lakini Sattar hakujibu
“Nawal hatuna muda wa
kupoteza na hawa watu !
akasema Gosu Gosu na
kwenda katika meza iliyokuwa
na vifaa mbali mbali
akachukua vifaa kadhaa na
kumfuata Sattar.Nawal naye
akasimama na kumsogelea
Sattar
“Sattar nakuuliza kwa
mara ya mwisho umekuja
kutafuta nini Tanzania?
Akauliza Nawal lakini Sattar
aliendelea kuwa kimya.Gosu
Gosu hakumkawiza akamnasa
kofi zito lililomfanya Sattar
aone nyota nyota halafu Nawal
akakikamata kichwa chake
akakigandamiza katika kiti
Gosu Gosu akaupanua mdomo
na kuingiza kifaa mdomoni na
kulishika jino moja akaling’oa
kwa nguvu damu zikaaza
kumwagika huku Sattar
akipiga makelele kwa
maumivu makali aliyoyapata.
“Leo tutaelewana !
akasema Gosu Gosu
“Sattar nakuuliza umekuja
kufanya nini Tanzania? Nataka
ujibu ama sivyo mateso haya
yataendelea na tutakuondoa
kiungo kimoja kimoja !
akasema Nawal lakini Sattar
aliendelea kupiga kelele.Nawal
akamfanyia ishara Gosu Gosu
wakamkamata tena na
kuondoa jino lingine Sattar
akapoteza fahamu.
“Ruby tunaomba watu wa
afya waje haraka humu ndani
wamuhudumie huyu mtu
atakapozinduka zoezi
litaendelea.Wakati
tunamsubiri tunarejea kwa
Jenerali William” akasema
Gosu Gosu kisha wakatoka
ndani ya kile chumba
wakaelekea katika chumba
alimo Jenerali William.Mara
tu Gosu Gosu alipoingia mle
ndani muziki
ukazimwa.Macho ya Jenerali
William yalikuwa yanatoa
machozi
“Kwa nini mnanifanyia
hivi?Nawaambia mmekosea
sana kunifanyia haya”
akasema Jenerali William
“Huu ni mwanzo tu
Jenerali William bado mengi
yanakuja.Marekani mlikuwa
mkiwakamata watuhumiwa wa
ugaidi na kuwapeleka katika
gereza la Guantanamo
kuwatesa na leo umefika
katika Guantanamo ya
Afrika.Utakutana na mateso
kama mliyokuwa mkiwatesa
wale magaidi hadi pale
utakapofunguka na kusema
ukweli” akasema Gosu Gosu
“Nani amewatuma
mnifanyie haya? Hiki
unachokifanya wewe kijana
kitakuwa na athari kubwa sana
kwa nchi yako ! akasema
Jenerali William
“William tunaanzia pale
tulipoishia katika awamu ya
kwanza.Ninataka kufahamu
kirusi alichokuja nacho Sattar
Sayf Al Din kiko wapi?
Akauliza Gosu Gosu
“Wewe kijana nimekwisha
kwambia una akili
pungufu.Sifahamu una
maanisha nini
unapozungumzia kirusi !
akafoka Jenerali William
“Sattar Al Din ambaye
hadi usiku huu ulikuwa naye
katika makazi yako ameleta
hapa nchini kirusi kwa lengo la
kukisambaza.Nataka
kufahamu kilipo kirusi hicho”
akasema Gosu Gosu
“Sifahamu chochote
kuhusiana na kirusi hicho
unachokizungumzia” akasema
Jenerali William
“Jenerali nitazame vizuri
nimechafuka damu.Nimetoka
kumuhoji Sattar Sayf Al Din
ambaye ameleta kirusi hapa
nchini na amekiri kukukabidhi
wewe kirusi hicho.Nataka
uniambie kilipo kirusi hicho”
akasema Gosu Gosu
“Sikuelewi unachokiongea
wewe kijana.Tafadhali naomba
mnifungue haraka sana kabla
ya vikosi vya Marekani
havijavamia mahala hapa !
akafoka Jenerali William
“Hakuna kikosi chochote
kitakachothubutu kufika
mahala hapa na
hawatafahamu kamwe kama
uko hapa hivyo juhudi za
kutoka hapa ni zako wewe
mwenyewe.Ninakuhakikishia
William kirusi tutakipata na
tutakwenda kukisambaza
Marekani” akasema Gosu Gosu
na kufungua faili lake akatoa
picha ya mke wa Jenerali
William akaiweka mezani
“Mkeo Deborah” akasema
Gosu Gosu na kutoa picha za
watoto wa William akaziweka
mezani
“Hiyo ni familia yako
ambayo nina uhakika
unaipenda kuliko kitu
chochote.Utajisikiaje pale
utakaposikia kuwa
wameathiriwa na kirusi hiki
ambacho mmekileta
mkisambaze hapa Tanzania?
Watoto hawa wadogo
watapoteza maisha na
watakufa kifo chenye mateso
makali.Hebu fikiria
mwanamke mrembo kama
huyu Debor…………….”
Akasema Gosu Gosu lakini
Jenerali William akatoa
ukelele wa hasira
“Aaagghhhh !! akapiga
kelele Jenerali William huku
akijitikisa katika kiti akijaribu
kutaka kuking’oa lakini
kilikuwa kiti imara
“Ninasema waacheni
familia yangu katika hili !
akafoka Jenerali William
“Ninarudia tena
kukuhakikishia Jenerali
William kwamba tutakipata
kirusi na baada ya kukipata
tutakirejesha Marekani
ambako tutakisambaza na
tunaanzia katika familia yako
na ukumbuke kwamba kirusi
hiki hakina tiba wala
kinga.Lakini usihofu nitakupa
simu utazungumza nao na
kuwaaga pale watakapokuwa
wameanza kuumwa” akasema
Gosu Gosu
“Nitakuua ! Nitakuua
mkiigusa familia yangu !
akafoka Jenerali William
“Huwezi kufanya chochote
Jenerali William.Kitu pekee
ambacho kinaweza kukusaidia
ni kutuonyesha mahala kilipo
kirusi hicho ili kujiokoa wewe
na familia yako ! akasema
Gosu Gosu na Jenerali William
akabaki kimya
“Jenerali William hakuna
faida yoyote kuendelea kuficha
kirusi hicho.Tuonyeshe
mahala kilipo tutakichukua na
kukihifadhi sehemu
salama.Hakuna
atakayefahamu kuhusu
mpango huo na nchi zetu
zitaendelea kuwa salama”
akasema Gosu Gosu
“Sifahamu chochote
kuhusu hicho kirusi
unachokizungumzia.Wewe ni
mwanajeshi wa aina gani
ambaye unashindwa
kunielewa?Nitazame macho
yangu kama ninakudanganya !
akafoka Jenerali William
“Gosu Gosu,Sattar
amezinduka” Ruby
akamfahamisha Gosu Gosu
“Ninakuja baada ya muda
mfupi na safari hii utanielewa
mimi ni mwanajeshi wa
namna gani ! akasema Gosu
Gosu na kutoka akaingia
katika chumba walimo akina
Ruby
“Gosu Gosu inakuaje
unashindwa kutumia nguvu
kumfungua huyu jamaa?Muda
unatukimbia na tunatakiwa
hadi mapambazuko tuwe
tumekwisha kipata kirusi”
akasema Nawal
“Huyu mtu ni mwanajeshi
na si kazi nyepesi kumfungua
mwanajeshi lakini nawaahidi
nitakaporejea tena anakwenda
kueleza ukweli” akasema Gosu
Gosu halafu akaongozana na
Nawal wakaelekea katika
chumba alimo Sattar.Tayari
alikwisha rejewa na fahamu na
alikuwa amefungwa katika
kiti.Baada ya kuingia wale
watu wa kitengo cha afya
wakatoka wakawaachia uwanja
akina Gosu Gosu.
“Sattar tumerejea tena.
Nakuhakikishia leo utapoteza
fahamu hata mara kumi hadi
utakapoamua kufunguka na
kutueleza
ukweli.Tumekuondoa meno
mawili tutaendelea kuyaondoa
moja baada ya lingine na kama
bado utakuwa kimya
tutaendelea na viungo
vingine.Ili mambo haya
yasiendelee tueleze kweli
tafadhali ! akasema
Nawal.Sattar mdomo wake
ulikuwa umevimba na bado
alionekana kuwa katika
maumivu makali.Gosu Gosu
akaenda kuchukua vifaa vile
vya kung’olea meno akaviweka
mezani.Nawal akachukua
picha moja akaiweka mezani
“Unaweza ukamtambua
huyu mtu pichani? Akauliza
Nawal.Sattar akaitazama picha
ile na kwa taabu akatamka
“Huyu ni mimi ! akajibu
kwa kiarabu
“Safi.Ahsante kwa kuamua
kutoa ushirikiano.Picha hii
ilipigwa mchana wa leo katika
uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Nyerere pale
ulipowasili.Sattar tunafahamu
katika masanduku haya mawili
ulibeba kirusi ambacho
umetumwa kuja kukisambaza
hapa Tanzania.Nataka
kufahamu kirusi hicho kiko
wapi?akauliza Nawal,Sattar
hakujibu akabaki kimya
“Sattar nahitaji majibu
ama sivyo zoezi litaanza upya !
akasema Nawal lakini bado
Sattar hakufumbua mdomo
wake.Nawal akasimama na
Gosu Gosu akashika tena vile
vifaa vyake
“Mara ya mwisho
nakuuliza kirusi kiko wapi?
Akauliza Nawal lakini Sattar
bado alikuwa kimya.Gosu
Gosu akamnasa makofi mawili
mazito halafu kichwa chake
kikagandamizwa katika kiti na
jino la tatu likang’olewa.Sauti
ya Sattar ilielekea kukauka
kutokana na kulia kwa
maumivu aliyoyapata.
“Kirusi kiko wapi Kirusi?
Akauliza Nawal.
“Nawal huyu bado
maumivu hayajamkolea !
akasema Gosu Gosu na
kushika tena vile vifaa vyake
lakini Sattar akatamka kitu
Nawal akamtaka Gosu Gosu
asubiri
“Unasemaje Sattar?
Akauliza Nawal
“Nitawaeleza ! akasema
Sattar.Gosu Gosu akachukua
pamba akamimina dawa
Fulani na kumuwekea Sattar
pale mahala alipong’oa jino na
baada ya sekunde kadhaa
damu ikaacha kutoka lakini
bado Sattar aliendelea kuhisi
maumivu makali mno.
“Kiko wapi kirusi?
Akauliza Nawal
“Nili…aaaghh
!akagugumia kwa maumivu
“Niliwakabidhi
wamarekani wakihifadhi hadi
kesho” akasema Sattar kwa
taabu.
“Unafahamu mahala kirusi
hicho kilipohifadhiwa?
Akauliza Nawal
“Sifahamu ! akajibu Sattar
“Sattar eleza ukweli ama
sivyo tutaendelea kukung’oa
jino moja baada ya lingine !
akafoka Nawal
“Nawaeleza ukweli
sifahamu wamekiweka wapi !
akasema Sattar
“Anasemaje huyu?
Akauliza Gosu Gosu ambaye
hakuelewa kile alichokisema
Nawal kwa kuwa hafahamu
lugha ya kiarabu
Nawal akamwambia Gosu
Gosu alichokisema Sattar
“Anaonekana anasema
ukweli.Endelea naye taratibu
aeleze mambo yote mimi ngoja
nikaendelee na Jenerali
William” akasema Gosu Gosu
na kutoka akarejea katika
chumba alichokuwamo
Jenerali William
“Jenerali William hii
nimekuja ni mara ya mwisho
nataka unieleze mahala kirusi
kilikofichwa !
“Nenda kuzimu Bazazi
wewe ! akafoka Jenerali
William na kumpandisha
hasira Gosu Gosu akamsogelea
na kumtandika ngumi mbili za
usoni na mdomo wa Jenerali
William ukajaa damu
“Unanipiga !! akasema
Jenerali William kwa ukali
“Muda wa mchezo
umepita William sasa ni kazi
moja tu.Aidha uonyeshe kilipo
kirusi au nikuharibu haribu na
kukuachia ulemavu wa
kudumu ! akasema Gosu Gosu
na Jenerali William
akamtemea mate yenye damu
“Kamwe huwezi kunitisha
nyani wewe ! akasema Jenerali
William na Gopsu Gosu
hakumjibu kitu akaanza
kumvurumishia makonde
mazito.Ndani ya sekunde
chache uso mweupe wa
Jenerali William ukabadilika
na kuwa
mwekundu,ulichafuka kwa
damu.
“Mimi ni muuaji lakini
wewe sintakuua ninataka
nikutese ili uwe
mfano.Nitakukata ulimi wako
hautaweza kuzungumza
tena,nitakuondoa vidole vyako
vya mikono na miguu na
hautaweza kuandika wala
kumsimulia mtu
kilichokupata.Utateseka na
utakufa taratibu.Kwa mara ya
mwisho wapi kilipo kirusi?
Akauliza Gosu Gosu lakini
Jenerali William hakujibu kitu.
Gosu Gosu akatoka na
kwenda kumchukua Sattar
aliyekuwa anahojiwa na Nawal
akaingia naye katika chumba
alimo Jenerali William ambaye
alistuka baada ya kuiona sura
ya Sattar ilivyobadilika.
“Gosu Gosu anataka
kufanya nini? Ruby akauliza
kwa wasi wasi
“Subiri tuone anachotaka
kukifanya” akajibu Nawal
“Japo ulikana
kutomfahamu lakini huyu ni
Sattar Sayf al Din ambaye
amekiri kuleta kirusi hapa
Tanzania na kuwakabidhi
ninyi mkakihifadhi.Nataka
kujua mahala kirusi hicho
kilipo ! akasema Gosu Gosu
lakini bado Jenerali William
aliendelea kubaki kimya
Ghafla Gosu Gosu kafanya
kitu ambacho hakuna
aliyekuwa
amekitegemea.Alichomoa
bastora yake kwa kasi ya ajabu
na kumtandika risasi Sattar
katika paji la uso akaanguka
sakafuni na kufariki .Jenerali
William akaingiwa na woga
mkubwa
“Nini umefanya hiki wewe
katili? Akauliza Jenerali
William sauti yake ikitetemeka
“Tumefika mwisho
William.Hatutaki mchezo
tena.Huyu ndiye aliyetumwa
kuja kusambaza kirusi hapa
Tanzania.Nimemuua na
hakuna tena mtu wa
kukisambaza kirusi
hicho.Huyu ndiye aliyekuwa
na maelekezo yote ya namna
ya kufanya.Una sekunde
thelathini za kuamua aidha
kuonyesha kilipo kirusi hicho
au kumfuata huyu shetani
mwenzako ! akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu what have you
done ?! Ruby akauliza na
kutaka kutoka ndani ya kile
chumba ili aweze kumfuata
Gosu Gosu katika chumba cha
mahojiano lakini Nawal
akamzuia
“Subiri kidogo Ruby.Kuna
kitu nimekiona ! akasema
Nawal
“Umeona nini?
“Subiri kidogo” akasema
Nawal akiwa ameyaelekeza
macho yake akimtazama
Jenerali William
“Mara ya mwisho William
wapi kilipo Kirusi? Akauliza
Gosu Gosu lakini Jenerali
William akabaki
akimtazama.Alionekana
kuchanganyikiwa.Gosu Gosu
akamnyooshea bastora
“Sekunde thelathini
zimekwisha.Kwa heri William”
akasema Gosu Gosu na
William akafumba
macho.Gosu Gosu akaachia
risasi mbili zilizopita pembeni
ya kichwa cha William
Sekunde kadhaa zikapita
William akafumbua
macho.Alikuwa anatokwa na
jasho usoni huku akihema
haraka haraka
“Nimetaka kukuonyesha
kwamba ninao uwezo wa
kukutoa roho yako muda
wowote William.Nimepitisha
risasi pembeni makusudi
kabisa lakini safari ijayo
sintakosa.Nitaingiza risasi kati
kati ya kichwa chako.Tuokoe
muda nataka unieleze kilipo
kirusi ! akasema Gosu Gosu na
Jenerali William akafumba
macho
“William uko tayari kufa
kwa ajili ya kulinda kirusi?
Hujui kamba kirusi hicho
kinaweza kuvuka mipaka na
kusambaa hadi nchini kwenu
Marekani na hata familia yako
inaweza kuathirika? Usiwe
mjinga kiasi hicho
William.Hawa waliokutuma
ufanye hivi ni kwa maslahi
yao.Tusaidiane kuokoa watu
wetu wasije
wakaangamia.Yawezekana
labda hujaelezwa kwa undani
kuhusiana na kirusi
hicho.Labda nikueleweshe
William kwamba kirusi hicho
ambacho hakina tiba wala
kinga kinasambaa kwa njia ya
hewa na endapo kikiachiwa
hapa Tanzania hakuna namna
ya kukizuia kisivuke mipaka ya
Tanzania na kusambaa katika
nchi jirani hatimaye bara zima
la Afrika na mwisho dunia
nzima.Hata Marekani lazima
kitafika.Utajisikiaje pale
ndugu zako watakapoanza
kuangamizwa na kirusi
ambacho umesaidia
kukisambaza? Akauliza Gosu
Gosu na kumtazama Jenerali
William
“Ninakupa nafasi nyingine
William ya kuweza kuiokoa
dunia dhidi ya maangamizi
makubwa yatakayotokea
endapo kirusi hicho
kitasambazwa.Nakubali
endapo kirusi hicho
kitasambaa mtafanikiwa
kutimiza lengo lenu kwani
mtaleta watu wenu wengi tu
kwa lengo la kuja kutoa
msaada kumbe mna ajenda ya
siri nyuma yake.Mtachukua
mali nyingi lakini damu za
wale watakaokuwa wamefariki
kutokana na kirusi hicho
hazitawaacha
salama.Zitawaandama usiku
na mchana.William sitaki
kuzungumza mambo mengi
nataka ukatuonyeshe mahala
kilipo kirusi ! akasema Gosu
Gosu.Jenerali William
akainamisha kichwa akafikiri
kwa muda halafu akainua
kichwa na kusema
“Nini mtakifanya endapo
nitawaonyesha mahala kilipo
kirusi hicho? Mtakwenda
kukisambaza Marekani kama
ulivyoniambia? Akauliza
Jenerali William
“Sisi si wakatili kama
ninyi.Hatutaweza
kukisambaza hicho kirusi
tutakihifadhi sehemu salama
ambako hakitakuwa tishio kwa
binadamu” akasema Gosu
Gosu
Jenerali Wiliam akafikiri
kwa muda halafu akasema
“Endapo nitawaonyesha
mahala kilipo kirusi hicho
kuna mambo mawili ninataka
tukubaliane” akasema Jenerali
William
“Nini unakitaka Jenerali
William? Akauliza Gosu Gosu
“Kwanza kabisa mtaniacha
huru na pili suala hili litabaki
kati yetu na hakuna
atakayefahamu kama kulikuwa
na mpango wowote wa
kusambaza kirusi hapa
Tanzania.Nataka tulimalize
suala hili kimya kimya
mchukue kirusi mkakihifadhi
sehemu salama na suala hili
lifike mwisho.Mko tayari kwa
hilo? Akauliza Jenerali
William na Gosu Gosu
akacheka kidogo
“Gosu Gosu mkubalie
hicho anachokitaka” Ruby
akampa maelekezo Gosu Gosu
“Nini ?! Gosu Gosu
akashangaa
“Ninahitaji kujadiliana na
wenzangu kuhusiana na suala
hili.Nitarejea ndani ya muda
mfupi” akasema Gosu Gosu na
kutoka mle ndani akawafuata
akina Ruby
“Ruby are you out of your
mind ?! akauliza Gosu Gosu
kwa ukali
“Gosu Gosu hatuna namna
ya kufanya zaidi ya
kukubaliana na ombi lake ili
tuweze kukipata kirusi
hicho.Tusiharibu mambo Gosu
Gosu nenda mle ndani
mwambie tunakubaliana na
matakwa yake na atuonyeshe
kilipo kirusi”
“Then we let him go?
Akauliza Gosu Gosu
“Ruby hawa watu ni
wanyama sana.Mambo
waliyoyafanya katika ardhi
yetu si ya
kibinadamu.Watanzania
wenzetu wengi wamepoteza
maisha kwa sababu ya watu
hawa.Hatuwezi kumuacha
akaenda hivi hivi” akasema
Gosu Gosu
“Anachokisema Gosu Gosu
kina msingi.Hatuwezi
kuwaacha watu hawa
wakaendelea kuifanya kile
wakitakacho lazima
wafundishwe adabu ! akasema
Nawal
“Nini mnashauri kifanyike
ili tukipate kirusi hicho?
Akauliza Ruby
“Tumkubalie ombi lake ili
atuonyeshe kilipo
kirusi.Tukisha kipata kirusi
hicho hatutamuacha salama !
Marekani lazima waondoke
hapa nchini kwa nguvu !
akasema Gosu Gosu
“Una maanisha tumuue
Jenerali Wiliam? Ruby
akauliza
“Hakuna haja ya
kumuonea huruma.Huyu
amekuwa akishirikiana na hata
kuwalinda watu wa IS
wanaochochea vurugu za
kidini hapa nchini na
kusababisha vifo vya watu
wengi.Lazima tupeleke vilio
pia Marekani kama wao
walivyosababisha vilio hapa
nchini” akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu tusipoteze
muda nenda kazungumze naye
na atuonyeshe kilipo kirusi na
baada ya kukipata tutajua nini
cha kufanya” akasema Ruby na
Gosu Gosu akarejea katika
chumba cha mahojiano alimo
Jenerali William.Sakafu ya
chumba kile ilikuwa
imetapakaa damu na Sattar
Sayf Al Din alikuwa amelalia
dimbwi la damu.
“Tumeyakubali yale
unayoyataka lakini
tutatekeleza pale
tutakapokuwa tumekipata
kirusi.Hivyo bila kupoteza
muda tuonyeshe mahala kilipo
kirusi hicho” akasema Gosu
Gosu
“Nitawapeleka mimi
mwenyewe mahala hapo”
“Wewe utabaki hapa na
sisi tutakwenda wenyewe
kukichukua kirusi hicho na
tutakapokihakiki kwamba ni
chenyewe ndipo
tutakapokuachia uende zako
lakini kabla ya kukitia kirusi
hicho mikononi mwetu
hautabandua mguu wako
ndani ya chumba hiki !
akasema Gosu Gosu
“Kirusi hicho kiko mahala
ambako ninyi hamuwezi
kuingia,kama kweli mnakitaka
niko tayari kwenda
kuwakabidhi”
“Mahala pekee ambako
hatuwezi kuingia ni mbinguni
anakoishi muumba wetu lakini
kwa hapa duniani sehemu
yoyote sisi tunaingia.Unadhani
ni Marekani pekee ambao mna
jeshi au makachero wenye
uwezo mkubwa? Hata sisi
tunao uwezo mkubwa sana wa
kufanya yale mnayoyafanya
ninyi na hata zaidi hivyo
tuelekeze mahala kirusi kilipo
na sisi tutakwenda
kukichukua” akasema Gosu
Gosu kwa kujiamini
“Kwa nini unashindwa
kunielewa? Kirusi hakiko baa
au shambani kiko sehemu
nyeti sana ambako ninyi
hamuwezi kufika” akasema
Jenerali William
“Kiko wapi? Tupe
maelekezo na sisi tutakwenda
kukichukua tena naomba
ufanye hivyo haraka kabla
sijabadilika.Nimekwisha
kwambia hautabandua mguu
wako humu ndani hadi pale
tutakapokipata kirusi na
kujiridhisha kuwa kweli ni
chenyewe ndipo
tutakapokuacha uende zako”
akasema Gosu Gosu
akimtazama William kwa
macho makali
“Kwa mara ya mwisho
wapi kilipo Kirusi? Akauliza
Gosu Gosu na kuupeleka
mkono wake ilipo bastora
“Kirusi kipo katika kambi
ndogo ya wanajeshi wa
Marekani iliyoko ufukweni”
akasema Jenerali William
“Kiko sehemu gani ndani
ya hiyo kambi? Gosu Gosu
akauliza
“Kuna kontena ambalo
hulitumia kwa ajili ya
kuhifadhi miili ya wanajeshi
wanapokuwa wamefariki
dunia na humo ndimo kilimo
kirusi” akasema Jenerali
William
Gosu Gosu akafungua
mlango akatoka na kuingia
katika chumba walimo akina
Ruby bila kuwasemesha
akachukua karatasi na kalamu
akarejea katika chumba cha
mahojiano na kuviweka
mezani.
“Nataka uchore ramani ya
namna ya kuweza kufika
katika hilo kontena lenye
kirusi” akasema Gosu Gosu na
kumfungua mkono wa kulia.
Jenerali William akaunyoosha
mkono halafu akaanza kuchora
ramani ya kambi ilivyo na
namna ya kuweza kufika
katika kontena ambalo
kumehifadhiwa kirusi.
“Ahsante kwa ushirikiano
wako.Utaendelea kubaki hapa
hapa hadi pale tutakapokipata
kirusi” akasema Gosu Gosu
“Mnajidanganya bure
hamtaweza kufika mahala
hapo” akasema Jenerali
William
“Na wewe maisha yako
yatakuwa yameishia humu
ndani ! akasema Gosu Gosu na
kutoka.
“Mambo yameiva !
akasema Gosu Gosu
“Tunakwenda kuvamia
kambi ya jeshi la Marekani hii
si operesheni rahisi hata
kidogo” akasema Ruby
“Ni operesheni nzito lakini
lazima ifanyike usiku huu na
lazima ifanikiwe kwa namna
yoyote ile ! Akasema Gosu
Gosu
“Nawal ulifanikiwa kuingia
katika kambi hiyo
anayoizungumzia William.Nini
ulikiona hapo?
“Ni kambi ndogo na haina
wanajeshi wengi hata vifaa
vilivyoko pale ni
vichache.Kambi yao kubwa iko
katika uwanja wa
Uhuru.Tusiogope jamani
tunaweza kuvamia kambi
hiyo”
“Ruby kwa nini tusiombe
msaada kutoka kwa Rais
atupatie vikosi vya jeshi?
Akauliza Gosu Gosu
“Operesheni hii ni ya
kimya kimya na hawapaswi
kujua nani
aliyewashambulia.Tukitumia
vikosi vya jeshi utakuwa ni
mgogoro mwingine
tumeuanzisha.Tunao
makomando wetu
tutawatumia wote na vile vile
tunao makachero.Hakuna
atakayebaki hapa leo wote
wanakwenda kupambana
kuhakikisha wanakipata kirusi
hicho.Wakusanye watu wote
niwajulishe kile
tunachokwenda kukifanya
usiku huu” akasema Ruby na
kabla Gosu Gosu hajatoka
Nawal akasema
“Nina wazo moja.Katika ile
nyumba alikokuwa akiishi
huyu Jenerali William
kulikuwa na gari la jeshi la
Marekani.Ninafikiria kwa nini
tusilichukue gari lile na
kulitumia katika operesheni
hii? Akasema Nawal
“Wazo zuri sana
Nawal.Gari hilo linaweza
kutusaidia kuingia katika hiyo
kambi wakidhani sisi ni
wenzao halafu tutawapa
shambulizi la kushtukiza na
watakapostuka wamevamiwa
tayari tutakuwa tumekipata
kirusi na kuondoka zetu”
akasema Gosu Gosu halafu
akatoka kwenda kuwakusanya
makomando na makachero
wengine wote wa SNSA kwa
ajili ya kupanga namna ya
kwenda kukichukua kirusi
katika kambi ndogo ya
wanajeshi wa Marekani.
Ilichukua saa mbili
kufanya maandalizi kwa ajili
ya operesheni ile ya kuvamia
kambi ya wanajeshi wa
Marekani.Baada ya Ruby
kujiridhisha kuwa kila kitu
kiko vizuri,akatoa ruhusa
safari ianze.Msafara wa magari
ya makomando na makachero
wa SNSA wakiongozwa na gari
la jeshi la Marekani ambalo
lilikwenda kuchukuliwa
mahala alikokuwa akiishi
Jenerali William,uliondoka
katika makao makuu ya SNSA
kuelekea katika kambi ndogo
ya jeshi la Marekani.Helkopta
maalum kwa ajili ya
operesheni za usiku nayo
haikubaki nyuma ilipaa angani
ikiwa na makomando kuelekea
katika kambi hiyo.
SAA MOJA BAADAE
Ukimya mkubwa ulitawala
katika ofisi kuu za SNSA.Ndani
ya chumba cha operesheni
walikuwemo Ruby,Nawal na
wafanyakazi wengine wa SNSA
wakifuatilia kwa karibu kile
kilichokuwa kinaendelea
katika operesheni ya kuvamia
kambi ndogo ya jeshi la
Marekani kwa ajili ya
kuchukua kirusi kilichokuwa
kimehifadhiwa hapo.Toka
kikosi cha SNSA kilivyofika
katika kambi hiyo na kuvamia
wakiwa na silaha nzito
walikuwa wakiwasiliana na
ofisi kuu kuwajulisha
kilichokuwa kinaendelea lakini
baada ya muda mapambano
yakawa makali na kilichobaki
kinasikika ni milio ya risasi na
sauti za maelekezo ya
viongozi.Mapambano yalikuwa
makali na hii iliwapa hofu
kubwa sana watu waliobaki
ofisi kuu za SNSA kuhusu
usalama wa wenzao.
Baada ya takribani saa
moja ikisikika milio ya risasi
na mabomu,hatimaye nyuso za
akina Ruby zikachanua kwa
tabasamu pale walipoisikia
sauti ya Gosu Gosu
akiwajulisha kuwa
wamefanikiwa kukipata kirusi.
“SNSA tumemaliza kazi na
tumekipata kirusi.Narudia
tena tumefanikiwa kukipata
kirusi” akasema Gosu Gosu na
watu wote waliokuwamo ndani
ya chumba kile wakashangilia
kwa nguvu.
“Mapigano yamemalizika?
Akauliza Ruby
“Hakuna kilichobaki
hapa.Tumeiteketeza kambi
yote.Hapa kinachoonekana
kwa sasa ni moto unaoendelea
kuwaka ! akasema Gosu Gosu
“Vipi kuhusu watu wetu
wako salama?
“Tumepoteza watu saba
lakini wote miili yao
inarejeshwa hakuna hata mwili
mmoja wa watu wetu uliobaki
hapa.Tayari vikosi vya ardhini
vimekwisha ondoka na sisi
tunaondoka sasa hivi na
helkopta tutazungumza
tukifika huko lakini kitengo
cha afya wajiandae kwani watu
wengi wameumia wengine
vibaya sana” akasema Gosu
Gosu
“Ahsante Gosu Gosu.Kazi
nzuri” akasema Ruby na
maandalizi ya kuwapokea
wenzao yakaanza mara moja.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 8
Helkopta ya SNSA ilitua
katika sehemu yake na mtu wa
kwanza kushuka alikuwa ni
Papi Gosu Gosu aliyekuwa
amebeba masanduku
mawili.Alikuwa ameloana
damu.Wafanyakazi wa SNSA
walikuwa wamejipanga tayari
kuwapokea
“Hongereni sana kwa kazi
hii kubwa” akasema Ruby na
kuyapokea yale masanduku
mawili kutoka kwa Gosu Gosu
“Ahsante sana
Ruby.Lilikuwa ni shambulio la
muda mfupi lakini kali sana !
akasema Gosu Gosu huku
majeruhi wakishushwa kutoka
katika ile helkopta na
kukimbizwa katika kitengo cha
afya kwa ajili ya kupatiwa
matibabu.
“Gosu Gosu umeumia sana
unatakiwa kwenda kupatiwa
huduma kwanza” akasema
Ruby na Gosu Gosu
akachukuliwa kwenda
kupatiwa matibabu.
Dakika chache baadae
msafara wa magari
ukawasili.Majeruhi
wakashushwa wakakimbizwa
kupatiwa matibabu na miili ya
wale waliopoteza maisha
ikapelekwa katika chumba
maalum kuhifadhiwa.Ruby
akawashukuru watu wote kwa
kazi kubwa waliyoifanya ya
kuhakikisha kirusi kile
kinapatikana.
Wakati majeruhi
wakiendelea kupatiwa
matibabu,Nawal akatumia
muda huo kuwasiliana na
Habiba Jawad kumjulisha
kuwa tayari wamekipata kirusi
“Hongera sana Nawal kwa
kazi nzuri mliyoifanya wewe
na wenzako.Sasa dunia iko
salama.Nimefurahi mno kwa
mpango huu mbaya wa
kusambaza kirusi kushindwa
kufanikiwa” akasema Habiba
“Kirusi hicho kiko wapi
kwa sasa? Akauliza Habiba
“Kiko hapa SNSA hii ni
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi.Utafanyika
utaratibu wa kukihifadhi
sehemu salama” akasema
Nawal
“Hongera sana Nawal kwa
kazi hii iliyotukuka
mliyoifanya” akasema Habiba
“Mama wewe ndiye
unayestahili hongera kwani
bila wewe jambo hili
lisngefanikiwa.Vipi kuhusu
Mathew Mulumbi una taarifa
zake zozote? Akauliza Nawal
na Habiba akasita kidogo
“Mama una taarifa zozote
za Mathew? Akauliza tena
Nawal
“Ndiyo Nawal.Tayari
Mathew yuko Tehran lakini
kuna tatizo limejitokeza”
akasema Habiba na kumueleza
Nawal kile kilichokuwa
kimetokea na hatua
alizochukua kwa ajili ya
kumsaidia Mathew asiuawe.
“Mama umenistua sana
kwa taarifa hii.Maisha ya
Mathew yako hatarini .Yuko
peke yake kule Tehran na
hawa jamaa wanaweza
wakamzidi nguvu
wakamuua.Mama nataka
niende huko Tehran haraka
sana kumsaidia Mathew”
akasema Nawal
“Unalosema ni jambo la
kweli Nawal,Mathew anahitaji
sana msaada.Hawa jamaa
watafanya kila mbinu
kuhakikisha wanamuua hasa
watakapopata taarifa kuwa
mpango wao wa kusambaza
kirusi Tanzania umeshindwa
kufanikiwa.Kwa kuwa hapo
umekamilisha kazi fanya
mpango uweze kuondoka mara
moja kuja hapa Riyadh ili
tupange namna ya kumsaidia
Mathew”
“Sawa mama nitafanya
mipango ya kuondoka huku
haraka na nitakujulisha”
akasema Nawal
“Kwa mara nyingine tena
Nawal hongereni sana kwa
kazi nzuri
mliyoifanya.Naamini
Marekani wakisikia mpango
wao umeshindwa kufanikiwa
watapasuka vichwa” akasema
Habiba na kuagana na Nawal
ambaye alirejea katika ofisi ya
Ruby na kumkuta Gosu Gosu
akiwa tayari amekwisha
gangwa jeraha lake la
shingoni.
“Pole sana Gosu Gosu”
akasema Nawal
“Ahsante Nawal.Ahsanteni
nyote kwa msaada wenu.Ule
mpango wako wa kutumia gari
lao ulisaidia sana kwani
walipoliona hawakuwa na wasi
wasi wakajua ni wenzao.Mara
tu walipofungua geti watu
wetu hawakupoteza muda
wakaanza mashambulizi na
hapo ndipo shughuli
ilipoanzia.Wengi wa wanajeshi
waliokuwepo kambini
walikuwa wamelala na
hawakutegemea kama
wangevamiwa na wengine
walikuwa wamekwenda
doria.Ninakiri wanajeshi wale
walikuwa wachache lakini
mahiri sana.Baada ya
kugundua wamevamiwa kwa
haraka sana wakajipanga na
tukaanza
kushambuliana.Wana mbinu
nyingi za kupigana lakini
nawasifu makomando wetu
nao wameiva barabara kwani
waliweza kukabiliana nao na
hatimaye tukalifikia lile
kontena lenye kirusi
tukalifungua na kukichukua na
hapo ndipo mapambano
yalipozidi kwani tayari watu
wetu kadhaa walikuwa
wameuawa.
Kitu cha kwanza
tulichokifanya baada ya
kuvamia kambi ile tuliilipua
nyumba iliyokuwa na mitambo
ya mawasiliano hivyo
hawakuweza kuwasiliana na
wenzao kuomba msaada.Hata
hivyo walijitahidi sana licha ya
uchache wao na kama
wangefanikiwa kuwajulisha
wenzao walioko katika kambi
kubwa uwanja wa uhuru sijui
kama tungetoka salama.Wale
jamaa wako vizuri katika vita”
akasema Gosu Gosu
“Poleni sana.Japokuwa
tumewapoteza wenzetu lakini
damu yao haijapotea
bure.Wamekufa kishujaa
wakilinda nchi yao na
wameokoa maisha ya wengi
ambao wangepoteza maisha
endapo kirusi hicho
kingesambazwa” akasema
Ruby
“Tayari tumekipata
kirusi.Nini kinafuata?
Tunakihifadhi wapi?
Mkumbuke vile vile kuwa
tumeiteketeza kambi yao yote
na hii haitakuwa taarifa njema
kwa Marekani” akasema Gosu
Gosu
“Ni wakati muafaka wa
kumjulisha Rais afahamu
kilichotokea na kile
kinachoendelea hapa nchini”
akasema Ruby
“Vipi kuhusu Jenerali
William? Akauliza Gosu Gosu
“Tulikubaliana
tutamuachia huru pale
tutakapokuwa tumekipata
kirusi na kwa kuwa tumekipata
lazima tuheshimu
makubaliano yetu na
tumuachie huru”akasema
Ruby
“Ruby niambie
humaanishi hicho
unachokisema ! akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu lazima
tuheshimu makubaliano yetu!
Akasema Ruby
“Ruby hawa watu si wa
kuonea huruma hata
kidogo.Hawa watu
wamesababisha ndugu zetu
wengi wakapoteza
maisha.Hatuwezi kumsamehe
mtu kama huyu.Kama
tusingekuwa na taarifa za
mpango wao wa kusambaza
kirusi hicho kingeanza
kusambazwa kesho na hakuna
anayejua yawezekana na sisi
tungekuwa miongoni mwa
wale ambao wangeathiriwa na
kirusi hicho.Mamia kama si
maelfu ya watu wengepoteza
maisha.Huyu ndiye ambaye
amekuwa akimlinda Assad
Ismail mchochezi mkubwa wa
machafuko yaliyopelekea watu
wengi kupoteza maisha.Katu
mtu kama huyu hatuwezi
kumuachia.Hastahili huruma
ya aina yoyote kwani yeye
hakuona huruma wakati watu
wetu wanauana” akasema
Gosu Gosu
“Gosu Gosu nadhani
tutalijadili jambo hili baada ya
kuzungumza kwanza na Rais”
akasema Ruby na kuchukua
simu akampigia Rais Dr
Fabian lakini akataarifiwa
kuwa simu ya Rais inatumika
ikamlazimu kusubiri
“Kuna jambo nataka
niwataarifu jamani” akasema
Nawal
“Nimezungumza na
Habiba Jawad
nikamfahamisha kuwa tayari
tumekipata kirusi” akasema
Nawal
“Ama kweli haya ni
maajabu.Ni vigumu kuamini
eti Habiba Jawad huyu
ambaye tunamfahamu
anafadhili makundi ya magaidi
ndiye ambaye ameokoa taifa
letu lisiingie katika
maangamizi makubwa.Bila
yeye tusingefahamu chochote
kuhusiana na hiki
kirusi.Nadhani hata hao
wamarekani wenyewe
watashangaa tumewezaje
kugundua mpango wao
uliokuiwa wa siri kubwa.
Tunapaswa kumshukuru sana
huyu mama” akasema Gosu
Gosu
“Uko sahihi Gosu
Gosu.Habiba Jawad pamoja na
mambo anayoyafanya lakini
kwa hili anastahili shukran
kwani bila yeye maelfu ya watu
wangeangamia” akasema Ruby
“Kuna jambo lingine
amenieleza Habiba la muhimu
sana.Amenipa taarifa kwamba
tayari Mathew Mulumbi
amekwisha ingia Iran”
“Oh thank you Lord !
akasema Ruby
“Tunamshukuru Mungu
kwa kumuwezesha Mathew
kuingia salama nchini Iran
lakini kuna tatizo
limejitokeza.Maisha ya
Mathew yako hatarini”
“Kivipi Nawal? Akauliza
Ruby kwa wasi wasi.Nawal
akawapa taarifa ile aliyopewa
na Habiba
“Bastard ! Gosu Gosu
akasema kwa hasira
“Japokuwa tayari Habiba
amekwisha muonya kuhusiana
na mpango wa kutaka kumuua
lakini baada ya kutafakari
nimeona bado maisha yake
yako hatarini.Wale jamaa
wanaweza wakamshinda
nguvu na kumuua kwani
Mathew yuko ugenini na hana
msaada wowote.Nimeamua
nitakwenda Iran kumsaidia
Mathew katika kufanikisha
misheni yake”
“Unataka kwenda Iran?
Akauliza Ruby
“Ndiyo.Nitapita kwanza
Saudi Arabia kisha nitaelekea
Iran.Nimeipenda sana
Tanzania na nilitamani
kuendelea kukaa hapa lakini
kwa hili lililojitokeza lazima
niondoke haraka sana kwenda
kumsaidia Mathew Mulumbi”
akasema Nawal na Ruby
akashusha pumzi
“Ni wazo zuri sana
Nawal.Kwa namna yoyote ile
lazima kwenda kumsaidia
Mathew ikiwezekana
kumuondoa asiendelee na hiyo
misheni yake kwani kirusi
tayari tumekipata na
tutaendelea kuwasaka wote
wanaohusika na vurugu hadi
tutakapohakikisha wote
wametiwa nguvuni.Tatizo ni
namna ya kupata usafiri wa
haraka wa kukupeleka Saudi
Arabia” akasema Gosu Gosu.
“Nadhani ……..” Ruby
akataka kuzungumza kitu
lakini akanyamaza baada ya
simu yake kuita.Alikuwa ni
Rais Dr Fabian
“Imekuwa vyema Rais
amepiga” akasema Ruby na
kuipokea simu
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby
“Ruby ulinipigia simu
lakini wakati unanipigia
nilikuwa nazugumza na mkuu
wa jeshi la polisi.Kuna tukio
baya limetokea usiku
huu.Moja ya kambi za
wanajeshi wa Marekani
walioko hapa Dar es salaam
imevamiwa na watu wasio
julikana usiku huu na
inasadikiwa wanajeshi wote
waliokuwepo kambini wakati
wa uvamizi huo wameuawa na
kambi yote kuteketezwa vibaya
sana kwa mabomu.Matukio
haya yanataka kukipasua
kichwa changu” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais
nilikupigia ninaomba kuonana
nawe”
“Usiku huu ?! akauliza Dr
Fabian
“Ndiyo mheshimiwa Rais
usiku huu.Ni muhimu sana”
“Haliwezi kusubiri hadi
kesho?
“Hapana mheshimiwa
Rais ni suala la kuzungumza
usiku huu huu” akasema Ruby
na Rais akakubali Ruby aende
ikulu kuonana naye usiku
ule.Aliingia katika gari lake
akiongozana na walinzi wake
kuelekea ikulu akiwaacha Gosu
Gosu na Nawal
Mara tu Ruby alipoondoka
Gosu Gosu akaenda katika
chumba alimo Jenerali
William.Ujio wa Gosu Gosu
ulimstua Jenerali William
“Nimerejea ! akasema
Gosu Gosu akimtazama
Jenerali William kwa macho
yaliyojaa hasira
“Tumepoteza watu saba
lakini kirusi tumekipata na
kambi yote
tumeiteketeza.Hakuna
mwanajeshi wako hata mmoja
aliyekuwapo kambini hapo
usiku huu aliyepona wote
tumewaua ! akasema Gosu
Gosu na Jenerali William
akapandwa na hasira
“Aaaagghhhh !! akasema
kwa hasira Jenerali William
huku akijaribu kujitikisa katika
kiti alichokuwa amefungwa.
“Hakuna unachoweza
kukifanya William ! Huu ni
mwisho wako ! akasema Gosu
Gosu
“Tuliweka makubaliano na
nimetimiza upande
wangu.Sasa ni upande wenu
nataka mniachie huru niende
zangu kama tulivyokuwa
tumekubaliana ! akasema
Jenerali William
“Siyo rahisi namna hiyo
kama unavyodhani
William.Itakuchukua miaka
kutoka humu na ikiwezekana
hautaweza tena kutoka”
akasema Gosu Gosu
“Tulikubaliana !! akafoka
Jenerali William
“Sikiliza Jenerali
William.Ninyi ni watu makatili
msio na hata chembe ya
huruma.Mmesababisha mamia
ya watanzania wameuana kwa
kujenga chuki baina yao.Kana
kwamba damu mliyoimwaga
haitoshi bado mkataka tena
kusambaza kirusi ambacho
kingesababisha maangamizi
makubwa.Mungu analipenda
taifa hili na mpango wenu
umeshindwa
kufanikiwa.Hatuwezi
kukuachia kirahisi namna hiyo
Jenerali William.Kwa sasa
endelea kupumzika
tutazungumza vizuri hapo
baadae hizi ni salamu tu
nimekufikishia” akasema Gosu
Gosu na kutoka
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 9
Ruby aliwasili ikulu na
kumkuta Dr Fabian
akimsubiri.
“Karibu Ruby” akasema Dr
Fabian huku akimimina
kinywaji katika glasi mbili
akampatia moja Ruby.
“Ruby wewe ni mtu
ambaye sikufichi
jambo.Nataka nikuweke wazi
kwamba sifikirii tena kuwania
urais kwa kipindi cha pili pale
kipindi changu cha kwanza
kitakapomalizika.Hii si kazi
nyepesi hata kidogo kuna
nyakati ninajuta kwa nini
niliingia katika siasa” akasema
Dr Fabian
“Dr Fabian hayo ni
masuala yako binafsi ambayo
sisi wengine hatustahili
kuyafahamu lakini kwa sasa
kwa kuwa bado umekalia kiti
cha urais basi jielekeze katika
kuwatumikia
watanzania.Simama imara
kuhakikisha nchi inakuwa
salama na maisha ya
watanzania yanarejea kuwa ya
kawaida” akasema Ruby
“Ninachokupenda Ruby ni
namna unavyoweza kunieleza
ukweli.Wengine hawawezi
kunitamkia maneno kama
haya uliyonitamkia.Ahsante
kwa kuwa mkweli kwangu na
nitayaheshimu mawazo yako”
akasema Dr Fabian na kunywa
funda la kinywaji
“Nimepigiwa simu usiku
huu na mkuu wa jeshi la polisi
akinijulisha kuwa kambi
ndogo ya wanajeshi wa
Marekani iliyoko kando mwa
bahari imevamiwa na watu
wasiojulikana waliokuwa
wamejihami kwa silaha nzito
na kuiteketeza kabisa pamoja
na kuua wanajeshi wote
waliokutwa hapo
kambini.Taarifa hiyo
imenichanganya sana kichwa
changu ! akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
tuliweke kwanza hilo pembeni
tutalizungumza baadae lakini
nimekuja kukupa taarifa ya
kile ambacho SNSA tumekuwa
tunakichunguza tukianzia
kwanza na vurugu zile kubwa
zilizopelekea umwagaji
mkubwa wa damu” akasema
Ruby na kunyamaza kidogo
“Toka vurugu zilipoanza
tulianza kuchunguza chanzo
chake tukijaribu
kuziunganisha na vurugu
zilizoanzia nchini Uganda
lakini napenda nikiri kwako
kwamba tulifika mahala
tukakutana na giza nene mbele
yetu.Hatukuwa na mwangaza
,tulikata tamaa.Mara akatokea
Mathew Mulumbi ambaye
ndiye aliyekuja kutufumbua
macho na kutupa mwangaza”
akasema Ruby na kunyamaza
baada ya sura ya Dr Fabian
kubadilika aliposikia jina la
Mathew Mulumbi likitajwa
“Mheshimiwa Rais najua
jina la Mathew linakuchefua
lakini naomba uvumilie kwani
litajitokeza mara nyingi katika
mazungumzo haya” akasema
Ruby
“Endelea usijali” akasema
Dr Fabian
“Mathew alikutana nasi,
mimi na Gosu Gosu na
akatufahamisha kwamba
amekuja nchini kwa misheni
maalum ila hakutueleza ni
misheni gani.Alichotueleza ni
kwamba vurugu zile
zilizotokea nchini na
kupelekea waumini wa dini
kushambuliana na kuuana zina
nguvu kubwa kutoka nje ya
nchi” akasema Ruby na
kumueleza Dr Fabian kila kitu
alichoelezwa na Mathew na
sura ya Dr Fabian ikabadilika
kwa mshangao mkubwa
alioupata.Ruby hakumjali
akaendelea
“Tulifuata maelekezo ya
Mathew na kuwakamata wale
magaidi wote isipokuwa Assad
Ismail ambaye ndiye
aliyekuwa kiongozi
wao.Wakati tukiendelea
kumsaka Assad tukampokea
mgeni anatokea Saudi Arabia
ambaye ni Yule Chloe
niliyekuja naye hapa jana
nikakuomba
utusaidiekumuunganisha na
mkuu wa vikosi vya Marekani
vilivyoko hapa nchini.Yule ni
Jasusi aliyekuwa anafanya kazi
na shirika la ujasusi la CIA
ambaye alikutana na Mathew
huko Palestina katika kikundi
kimoja cha wanamgambo
wanaopambana na serikali ya
Israel ambako Mathew alikuwa
amejiunga nao akiwa katika
misheni maalum” akanyamaza
Ruby baada ya Dr Fabian
kumfanyia ishara anyamaze
“Ruby mambo
unayonieleza ni mazito sana
lakini naona kama vile
unanieleza juu juu.Ninataka
unieleze kwa kina.Umesema
huyu Chloe ni jasusi ambaye
alikutana na Mathew huko
Palestina katika kikundi cha
wanamgambo.Mathew alikuwa
anafanya nini katika kikundi
hicho cha wanamgambo?
Ninataka kufahamu tafadhali”
akasema Dr Fabian
“Ili ulifahamu jambo hili
kwa undani zaidi nitakuanzia
mbali kidogo” akasema Ruby
na kuanza kumueleza Dr
Fabian namna Mathew
alivyopotea wakati wa
operesheni ya kubadilishana
mateka kati yao na magaidi wa
IS.Ruby alimueleza Dr Fabian
kila kitu toka Mathew
alipokamatwa na watu wa
Mossad na kufungwa kwa
miaka mitatu akiteswa na hadi
alipojiunga na kundi la Ammar
Nazari Brigades.Historia hii
yote alielezwa na Nawal
Ruby akaendelea kumpa
Rais maelezo ya kuhusiana na
safari ya Mathew hadi
alipokutana na Habiba Jawad
“Baada ya kufika kwa
Habiba Jawad misheni
ikabadilika na mipango ya
kumuua haikuendelea tena
badala yake akajiunga naye na
kuwa sehemu ya familia kwa
kumuoa mtoto wa Habiba”
“Dah ! Yaani akathubutu
kumuoa mtoto wa mtu
anayefadhili ugaidi duniani !
akasema Dr Fabian kwa
mshangao
“Wote tulistuka tulipopata
taarifa hizi lakini mstuko wetu
ni kwa sababu hatukuwa
tukimfahamu vyema Habiba
Jawad ni nani.Mathew alipata
bahati ya kumfahamu haraka
ndiyo maana akajiunga
naye.Nikukumbushe tu
mheshimiwa Rais kwamba
katika sakata lile la Melanie
David na James Kasai
wakishirikiana na magaidi wa
IS,ni Habiba Jawad ambaye
alimuwezesha Mathew
Mulumbi kulimaliza lile jambo
kwa kumpa taarifa muhimu
kuhusu James Kasai na
mipango yao yote” akasema
Ruby
“Are you sure? Akauliza Dr
Fabian
“100% Mr President”
akajibu Ruby
“Inashangaza sana.Kwa
nini akafanya hivyo wakati
yeye ndiye aliyekuwa
akiwafadhili magaidi wale?
“Baada ya kukamilisha
misheni ile Mathew Mulumbi
alirejea Saudi Arabia ambako
tayari alikwisha kuwa raia na
alijulikana kama Abu Zalawi
na safari hii ndipo
alipogundua siri kubwa
aliyokuwa nayo Habiba
Jawad” akasema Ruby na
kumueleza Dr Fabian
kuhusiana na kikundi
kinachojulikana kama G20
kilicho ndani ya shirika la
ujasusi la Marekani CIA
ambacho ndicho kinamtumia
Habiba Jawad katika kufadhili
makundi ya kigaidi.Mshangao
alioupata Dr Fabian ulikuwa
mkubwa
“Ruby hiki unachokisema
ni kitu kizito mno.Naomba
uongee vitu ambavyo una
uhakika navyo.Marekani
kamwe haiwezi kushirikiana
na magaidi wakati ni nchi
inayoongoza katika kupiga vita
ugaidi duniani.Inawezekanaje
wakaihadaa dunia kuwa wao ni
vinara katika kupambana na
ugaidi halafu wakageuka
upande wa pili na kushirikiana
nao? Ruby naomba uwe
makini mno na jambo hili”
akasema Dr Fabian
“Usihofu mheshimiwa
Rais,nina uhakika na hiki
ninachokueleza” akasema
Ruby
“Kikundi hicho cha G20”
Ruby akaendelea
“Kimekuwa kikishirikiana
na makundi mbali mbali ya
kigaidi katika mipango mbali
mbali duniani yenye maslahi
kwa nchi ya Marekani.Vurugu
za kidini zilizotokea katika
nchi za Afrika ya Mashariki
zikianzia Uganda na kusambaa
katika nchi nyingine Tanzania
na kidogo nchini Kenya ni
moja ya mikakati ya kikundi
hicho”
“What ?! akauliza Dr
Fabian
“Narudia tena
mheshimiwa Rais kwamba
vurugu hizi ambazo zimetokea
Afrika Mashariki na
kusababisha waumini wa dini
kushambuliana hazikuibuka
hivi hivi tu bali ni mipango ya
kundi hili la G20 wakiwatumia
magaidi wa IS katika
kuchochea vurugu hizo”
“That’s not true ! akasema
Dr Fabian na kusimama
“It is true Mr President !
akasema Ruby
“Wapi umeyatoa mambo
haya Ruby? Kwa Mathew
Mulumbi? Akauliza
“Mheshimiwa Rais
haijalishi taarifa hizi
tumezipata wapi lakini ni
taarifa za kweli kabisa na
ninaomba uniamini” akasema
Ruby
“Hata mwendawazimu
hawezi akakuamini Ruby kwa
taarifa hiyo.Nimekwisha
kutahadharisha kwamba
taarifa hizi unazopewa na
vyanzo vyako si taarifa sahihi
na zina lengo la kuleta
mgongano baina ya nchi zetu
na Marekani.Nchi ya Marekani
ni marafiki zetu wa muda
mrefu na wamekuwa
wakitusaidia sana na hata
machafuko haya yalipotokea ni
wao waliotuma majeshi yao
haraka kuja kutusaidia hakuna
nchi nyingine iliyofanya hivyo”
“Nalifahamu hilo
mheshimiwa Rais lakini
naomba utulie nimalizie kile
ambacho ninataka kukueleza”
akasema Ruby na Dr Fabian
akaketi.Ruby akamueleza kwa
kirefu kile walichokigundua
kutokana na vurugu zile za
kidini zilizopelekea mamia ya
watu kupoteza maisha.Dr
Fabian akabaki mdomo wazi
“Kwa hiyo mheshimiwa
Rais vurugu hizi zote
zilizotokea malengo yake ni
kujipatia mafuta ya Uganda na
ukitazama kwa makini
utaamini kile
ninachokwambia.Vurugu
zilianzia Uganda na zikafika
hadi hapa nchini na kwa hapa
nchini vurugu zilianzia jijini
Tanga.Kwa nini iwe Tanga na
si Kilimanjaro? Jibu ni jepesi
tu ni kwa sababu ili waweze
kuyapata mafuta ya Uganda
walilazimika kuudhibiti mji wa
Tanga kwani bomba la mafuta
linatoka Uganda na kuishia
Tanga na mara tu vurugu
zilipoanza Marekani ikatuma
vikosi vyake haraka sana kwa
lengo la kusaidia kurejesha
amani.Hivi sasa meli za
Marekani zinapanga foleni
zikijaza mafuta jijini Tanga”
akasema Ruby na ukimya
mfupi ukatanda mle ndani
“Ruby unachokizugumza
kinaweza kuwa kweli.Sasa
nimeanza kukuelewa” akasema
Dr Fabian
“Baada ya mpango wao wa
kuchukua mafuta
kufanikiwa,walihitaji kufanya
kitu ambacho kitavifanya
vikosi vya Marekani viwe na
sababu ya kuendelea kuwepo
hapa nchini kwa muda mrefu
zaidi na ndipo walipokuja na
mpango wa kusambaza kirusi
hatari cha maangamizi”
akasema Ruby na kumueleza
Rais kuhusiana na mpango ule
wa kusambaza kirusi hapa
Tanzania.Dr Fabian
akalazimika kufuta jasho
usoni.Ruby akatoa faili katika
mkoba wake akalifungua na
kutoa picha akampatia Rais
“Anaitwa Sattar Seyf Al
Din.Huyu ndiye aliyetumwa
kuja nchini kusambaza kirusi
hicho” akasema Ruby na
kutoa picha nyingine
“Hapa ni wakati akishuka
ndegeni katika uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere akiwa
ameambatana na wanajeshi wa
Marekani.Haya masanduku
mawili ndimo kilimo
kirusi”akasema Ruby.Dr
Fabian akazitazama picha zile
kisha akasema
“Hebu subiri kidogo
Ruby.Ninyi mlifahamuje kama
kuna mpango huo wa
kusambazwa kwa kirusi hapa
Tanzania na hadi mkafahamu
mtu anayetumwa kuja
kuifanya kazi hiyo? Akauliza
Dr Fabian
“Chloe alitumwa kuja
kutupa taarifa hiyo na Habiba
Jawad.Kikundi hicho cha G20
walimtaka Habiba awatafutie
mtu kutoka IS ambaye
watamtumia katika mpango
huo wa kusambaza kirusi hapa
Tanzania na akamtafuta Sattar
halafu akamtuma Chloe
kutuletea taarifa” Akasema
Ruby na kuendelea
kumsimulia Dr Fabian
kilichoendelea baada ya Sattar
kuwasili nchini na hadi
walivyotumia mbinu ya
kumkutanisha Nawal na
Jenerali William
“Tunashukuru Chloe
alipokewa vyema na Jenerali
William na akampeleka katika
makazi yake na saa mbili za
usiku akatupa taarifa kwamba
Jenerali William amefika
katika makazi hayo akiwa
ameongozana na Assad Ismali
tuliekuwa tukimtafuta kwa udi
na uvumba na vile vile alikuwa
ameongozana na Sattar Sayf Al
Din.Baada ya kupewa taarifa
hiyo tukaanza kujiandaa na
kutuma kikosi caha
makomando wetu wakavamia
nyumba hiyo na kuwakamata
Jenerali Wiliam,Sattar na
Assad lakini kirusi
kilikosekana.Tuliwafanyia
mahojiano na Jenerali Wiliam
akatuonyesha mahala kirusi
hicho kilipohifadhiwa ambako
ni katika kambi yao ndogo
iliyoko ufukweni mwa
bahari.Hatukuwa na namna
nyingine ya kufanya zaidi ya
kujipanga na kwenda kuivamia
kambi hiyo”
“Wait..! ni ninyi mliovamia
kambi ya wamarekani?
Akauliza DrFabian kwa
mshangao
“Ndiyo mhshimiwa Rais ni
sisi.Tumepoteza watu saba na
wengine wamejeruhiwa lakini
tumefanikiwa kukipata kirusi
ambacho kilitazamiwa kuanza
kusambazwa siku ya
kesho.Kwa sasa kirusi
kimehifadhiwa SNSA na nchi
iko salama” akasema Ruby na
ukimya ukatawala mle
ndani.Baada ya muda Dr
Fabian akasema
“Nimekosa maneno ya
kusema Ruby ! Sijui
nitawashukuru vipi kwa jambo
hili kubwa mlilolifanya la
kuiokoa nchi yetu kutoka
katika janga kubwa.Watu hawa
ni wanyama wakubwa
sikutegemea kabisa kama
wanaweza wakatufanyia kitu
kama hiki.Watu hawa ambao
tunawaheshimu kama rafiki
zetu kumbe wana sura mbili !
akasema Dr Fabian kwa hasira
“Kwa nini Habiba Jawad
anafanya haya kwa nchi yetu?
Akauliza Dr Fabian
“Ni kwa sababu amechoka
kufanya hiki anachokifanya na
kwa sasa anashirikiana na
Mathew kuweza kukiondoa
kikundi hicho cha G20
ambacho amekuwa akifanya
kazi kwa niaba yao” akasema
Ruby
“Hapo ndipo
mnaponichanganya.Mathew
Mulumbi anashikiliwa na
Marekani kwa kulipua ubalozi
wake hapa Dar es
salaam.Atafanikiwa vipi
kukiondoa kikundi hicho
wakati ana tuhuma za ugaidi?
Akauliza Dr Fabian
“Ule ulikuwa ni mpango
maalum uliopangwa na hao
G20” akasema Ruby
“Unataka kuniambia
kwamba wamelipua ubalozi
wao wenyewe? Akauliza Dr
Fabian
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Mpango huo uko hivi.Hivi
sasa Marekani na Iran hazina
maelewano mazuri na
zimekuwa zikitoleana kauli za
vitisho vya
kushambuliana.Marekani
wana hofu kwamba
yawezekana kweli Iran akawa
anamiliki silaha kali kama
inavyojitapa hivyo basi
wakaamua kuja na mpango
maalum wa kuweza kufahamu
kuhusu silaha za Iran”
akasema Ruby na kumweleza
Dr Fabian mpango wote wa
G20 kumuingiza Mathew
nchini Iran kuchunguza silaha
za Iran
“Hivi sasa Mathew yuko
nchini Iran tayari kabisa
kuanza kazi yake aliyotumwa”
akasema Ruby
“Ruby kila unavyozidi
kunieleza ninazidi
kuchoka.Mambo haya ni
makubwa mno.Mathew
Mulumbi ameingia katika
misheni ya hatari sana”
“Ni misheni ya hatari mno
na kama akifanikiwa kuimaliza
salama basi itakuwa na
mafanikio makubwa kwani
lazima atakiondoa kikundi cha
G20”
“Sikufahamu chochote
kilichokuwa kinaendelea
kuhusu Mathew ndiyo maana
nikatamka maneno mengi
mabaya na…”
“Usijilaumu mheshimiwa
Rais hukufahamu chochote
kilichokuwa kinaendelea ndiyo
maana nilikushauri kuwa
usizungumze maneno mabaya
kwani utafika wakati ambao
utajilaumu kwa maneno yako”
akasema Ruby na ukimya
ukatanda
“Kwa hiyo mheshimiwa
Rais hiyo kazi tuliyokuwa
tunaifanya ambayo kila
uliponiuliza nilikuomba unipe
muda zaidi ni hiyo niliyokuleza
na hapo ndipo tulipofika”
akasema Ruby
“Ruby narudia tena sioni
maneno mazuri ya
kuwashukuruni kwa jambo hili
kubwa mlilolifanya kwa taifa
letu na dunia nzima kwa
ujumla kwani endapo kirusi
hicho kingesambazwa hapa
Tanzani lazima kingesambaa
sehemu nyingine duniani”
“Mheshimiwa Rais pamoja
na mafanikio haya makubwa
tuliyoyapata lakini bado tuna
kazi kubwa mbele yetu.Bado
tunatakiwa kuufahamu
mtandao wote ambao
umeshiriki katika kuchochea
vurugu zilizotokea hapa nchini
na kuwakabidhi jeshi la polisi
kwa hatua zaidi za
kisheria.Tunaye Assad ambaye
tunaamini atatueleza kila kitu
kuhusu watu anaoshirikiana
nao.Jambo lingine tunacho
kirusi hatari ambacho
tunatakiwa kutafuta namna ya
kukihifadhi na jambo la
mwisho tumeua wanajeshi wa
Marekani walioko hapa nchini
na kwa hilo tumetengeneza
mgogoro na
Marekani.Tunahitaji msaada
wako katika hili kuihakikishia
serikali ya Marekani kwamba
kilichofanyika ni shambulio la
kigaidi”
“Hapana Ruby ! Hatuwezi
kuwaogopa.Ni wao walioanza
na sisi tunamaliza.Kuanzia
kesho nitawaondoa wanajeshi
wote wa Marekani hapa nchini
na nitawaeleza ukweli
watanzania na dunia
wafahamu ni kitu gani
ambacho Marekani imekuwa
inakifanya.Hili si suala la
kufumbia macho ! akasema
kwa ukali Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais wakati
wa kuwatangazia watanzania
na dunia juu ya jambo hili
bado.Ukifanya hivyo
utavuruga misheni ya Mathew
kule Iran.Tuvute subira kidogo
ili Mathew amalizie misheni
yake na kisha akakimalize kile
kikundi cha G20 na hapo
ndipo tutaitangazia dunia
mambo yote waliyokuwa
wanayafanya na hadi wakati
huo tutakuwa tumekamilisha
uchunguzi wetu kuwafahamu
watu walioshiriki katika
kuchochea machafuko”Ruby
akamshauri Rais ambaye
aliinama akafikiri halafu
akasema
“Wazo zuri Ruby lakini
hatuwezi kuendelea
kuwaruhusu Marekani
waendelee kuchukua tani na
tani za mafuta ya
Uganda.Lazima tuwaondoe
bila ya vurugu.Kuna njia
nyepesi ya kuweza kuwaondoa
hapa Afrika Mashariki.Watu
hawa wamekuja kwa ajili ya
mafuta hivyo basi pale
watakapoyakosa mafuta
hawatakuwa tena na ulazima
wa kuwepo hapa.Tutalipua
bomba la mafuta linalotoka
Uganda na hiyo itapelekea
mafuta kutokushuka tena
Tanga.Wakikosa mafuta
wataondoka zao” akasema Dr
Fabian.
“Hilo ni wazo zuri pia
mheshimiwa Rais.Tutajifanya
hatujui chochote kuhusiana na
mipango yao na hii itasaidia
kumpa Mathew nafasi ya
kuweza kukamilisha misheni
yake” akasema Ruby
Majadiliano yaliendelea
kwa zaidi ya saa moja
wakakubaliana mambo kadhaa
ya kufanya halafu Ruby
akasema
“Mheshimiwa Rais kuna
suala lingine ambalo ninahitaji
msaada wako”
“Sema Ruby nini
unahitaji?
“Mathew Mulumbi yuko
katika hatari kubwa ya
kuuawa” akasema Ruby na
kumueleza Dr Fabian
kuhusiana na mipango ya
kumuua Mathew.
“Endapo wakifanikiwa
mipango yao basi mpango wa
kukisambaratisha kikundi cha
G20 hautafanikiwa kwani
mpango huo unamuhiaji mno
Mathew.Kwa namna yoyote ile
lazima tumsaidie ili aweze
kuwa salama na afanikishe
misheni yake” akasema Ruby
“Kama waliomtuma
hawataki aendelee na misheni
waliyomtuma na wanataka
kumuua kuna ulazima gani wa
kumsaidia afanikishe misheni
aliyotumwa na hao jamaa?
Kitu cha msingi ni kumsaidia
atoke Iran na kurejea
nyumbani”Akasema Dr Fabian
“Kuna umuhimu mkubwa
wa Mathew kuendelea na
misheni yake na
atakapoikamilisha itakuwa ni
tiketi kwake ya kuingia tena
Marekani na hapo ndipo
atakapopata nafasi ya
kukimaliza kikundi cha
G20.Bila kukamilisha misheni
aliyotumwa hataweza kurejea
Marekani na G20 wataendelea
kuwa tishio duniani” akasema
Ruby
“Namna gani unataka
kumsaidia? Una mawasiliano
naye? Unafahamu mahala
alipo?Akauliza Dr Fabian
“Sina mawasiliano naye
lakini Habiba Jawad tayari
amekwisha wasiliana naye na
kumjulisha kuhusiana na
hatari inayomkabili.Pamoja na
kupewa taarifa za hatari hiyo
lakini Mathew yuko ugenini na
hana msaada wowote wale
jamaa wanaweza wakamzidi
nguvu na kumuua.Ikitokea
bahati mbaya Mathew
akauawa hizi juhudi zote
tulizofanya zitakuwa bure na
hawa jamaa wanaweza
wakajipanga na kurejea
kivingine.Baada ya kujadiliana
tumekubaliana kwamba Chloe
atakwenda Tehran kumsaidia
Mathew.Yeye itakuwa rahisi
kuingia nchini Iran kwa kuwa
ana uraia wa Saudi Arabia.Vile
vile Habiba Jawad
anafahamiana na watu
wanaoweza kumsaidia Chloe
kuingia kwa urahisi nchini
Iran”
“Kama mna uhakika
kwamba Chloe anaweza kuwa
na msaada mkubwa kwa
Mathew basi aende mara
moja” akasema Dr Fabian
“Kuna jambo
limetukwamisha.Namna
atakavyoweza kuondoka hapa
kwa haraka kuelekea Riyadh”
akasema Ruby na Dr Fabian
akainamisha kichwa na
kusema
“Hakuna tatizo la
usafiri.Kwa jambo muhimu
kama hili nitatoa hata ndege
ya Rais impeleke haraka huko
Riyadh.Lini anataka
kuondoka?
“Hata sasa hivi akipata
usafiri” akajibu Ruby
“Nitatoa maelekezo ndege
yangu iandaliwe ili aweze
kuondoka kesho asubuhi”
akasema Dr Fabian
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby
Tayari imekwisha timu saa
kumi za alfajiri,Ruby akaagana
na Rais akaondoka kurejea
ofisi za SNSA.
Baada ya Ruby kuondoka
Dr Fabian akamimina mvinyo
katika glasi akagugumia wote
“Mpaka sasa mwili
unanisisimka kwa mambo
aliyonieleza Ruby.Marekani
wamekuwa ni rafiki zetu kwa
muda mrefu na wamekuwa
wakitupa misaada mingi ya
kimaendeleo na vile vile ni
wachangiaji wa bajeti yetu ya
serikali lakini kumbe ni chui
mwenye ngozi ya
Kondoo.Imeniumiza sana kwa
kitendo hiki
walichotufanyia.Huu ni
uonevu na ukandamizaji
uliovuka mipaka.Kama vijana
wangu wasingesimama imara
na kupambana kuhakikisha
mipango yao
haifanikiwi,wangeweza
kusambaza kirusi hatari na
mamia ya watanzania
wangeangamia.Huu ni unyama
uliovuka kiwango! Akawaza Dr
Fabian akiwa ameikunja sura
yake kwa hasira akanywa
funda lingine la kinywaji
“Sasa ninaanza kupata
picha kumekuwa na magonjwa
mbali mbali yanaibuka zama
hizi bila kujua yametokea wapi
na mengine mpaka leo hii
hayana tiba,yawezekana virusi
vinavyoeneza magonjwa haya
vinatengenezwa na kuja
kusambazwa huku kisha
tunatumia gharama kubwa
kununua dawa.Dah ! Matukio
haya yamenifundisha jambo
kubwa sana.Ili kuepukana na
haya yote nchi zetu zinapaswa
kuachana kabisa na utegemezi
wa mataifa makubwa.Nchi
zetu za Afrika zinapaswa
kuanza kujitegemea zenyewe
bila kusubiri wafadhili.Kama
tukiendelea kutegemea
mataifa makubwa waje
watuletee maendeleo matokeo
yake ni kama haya
yaliyotupata ! akaendelea
kuwaza Dr Fabian halafu
akawasha simu yake aliyokuwa
ameizima ili azungumze na
Ruby akatoa maelekezo ndege
yake iandaliwe kwa ajili ya
safari ya nje ya nchi asubuhi
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 10
Ruby alirejea SNSA.Ulinzi
ulikuwa umeimarishwa sana.
“Vipi maendeleo ya hapa?
Akauliza Ruby
“Hapa kila kitu
kinaendelea vizuri.Vipi huko
utokako? Akauliza Gosu Gosu
na Ruby akawaeleza kila kitu
kilichojiri ikulu.
“Ahsante sana Ruby kwa
msaada huu mkubwa wa
kupatikana usafiri kwenda
Riyadh.Inapendeza kama Rais
mwenyewe amekubali kutoa
ndege yake kwa ajili ya
kunifikisha haraka Riyadh.Hii
ina maanisha kwamba
Tanzania inanituma kwenda
kumsaidia mtoto wao ambaye
ni Mathew Mulumbi na
ninawaahidi kwamba
nitafanya kila lililo ndani ya
uwezo wangu kuhakikisha
kwamba ninamsaidia Mathew
na misheni yake
inakamilika.Mathew atarejea
nyumbani akiwa mzima
kabisa” akasema Nawal
“Inakaribia saa kumi na
moja za Alfajiri,nendeni
mkapumzike kwa muda mfupi
kwani si muda mrefu
kutapambazuka” akasema
Ruby.GoSu Gosu akamchukua
Nawal wakaingia garini huku
wakisindikizwa na walinzi
kuelekea nyumbani kwa Gosu
Gosu kwa ajili ya mapumziko
mafupi kabla ya kuanza safari
kuelekea Riyadh.
“Gosu Gosu tukifika
nyumbani hakuna maongezi
mengi.Nataka tutumie muda
mfupi uliobaki kuagana kwani
yawezekana nisirejee tena
Tanzania.Ninafahamu
unachokitaka kwangu toka
nimefika” akasema Nawal
wakiwa ndani ya gari na
kumfanya Gosu Gosu
asisimkwe mwili kisha
akatabasamu.
Mara tu baada ya kufika
nyumbani, Gosu Gosu
hakutaka kusubiri.Bila kujali
maumivu aliyokuwa nayo
kutokana na majeraha
aliyoyapata,akambeba Nawal
na kupanda naye ngazi hadi
chumbani kwake ambako
hakukuwa na muda wa
kupoteza mpambano ukaanza
mara moja.Gosu Gosu
aliumiliki uwanja vilivyo.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 11
“Gosu Gosu ! Amka
kumekucha tayari” akasema
Nawal ambaye naye alistuliwa
na mlio wa simu ya Gosu Gosu
iliyokuwa ikiita mfululizo.Gosu
Gosu akakurupuka kutoka
usingizini na kuichukua simu
yake.Mpigaji alikuwa ni Ruby
“Ruby habari za asubuhi !
akasema Gosu Gosu kwa sauti
ya uchovu
“Nzuri Gosu Gosu,tayari
nimekwisha anza kupatwa na
wasiwasi.Si kawaida yako
kuchelewa kupokea simu
namna hii” akasema Nawal
“Ni uchovu wa
jana.Mambo
yanakwendaje?Uko salama?
Akauliza
“Huku shwari kabisa kila
kitu kinakwenda vizuri”
“Nawal anaendeleaje?
“Anaendelea vizuri.Ni
yeye aliyeniamsha nilikuwa
nimepitiwa na usingizi”
“GosuGosu ulikuwa
umelala na Nawal? Akauliza
Ruby na kumstua Gosu Gosu
“Oh no ! akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu nimetaarifiwa
na Rais kwamba ndege iko
tayari .Mwambie Nawal
ajiandae kwa ajili ya
safari.Ninakuja hapo
kuwapitia tuelekee uwanja wa
ndege” akasema Ruby na
kukata simu
“Sikutaka Ruby afahamu
kama nimelala na Nawal,hata
hivyo hakuna kilichoharibika”
akawaza Gosu Gosu na
kumfuata Nawal chumbani
kwake na kumkuta akitoka
kuoga.
“Ruby anasemaje?
Akauliza Nawal
“Ndege iko tayari
anatupitia muda si mrefu
tuelekee uwanja wa ndege”
akasema Gosu Gosu na
kumkumbatia Nawal
“Tafadhali fanya kila
uwezalo urejee Tanzania pindi
mtakapokuwa mmekamilisha
misheni yenu huko
Iran”akasema Gosu Gosu
“Nimekwisha kuahidi
Gosu Gosu kwamba nitarejea
Tanzania.Nimeipenda sana
nchi hii” akasema Nawal na
kuliachia taulo likaanguka
chini
“Mama yangu ! akawaza
Gosu Gosu baada ya
kuushuhudia mwili mwororo
wa Nawal
“Kama isingekuwa Ruby
anakuja ningeanzisha kipute
kingine hapa hapa.Lakini
ngoja tujiandae kwa safari”
akawaza Gosu Gosu
“Mbona unanitazama kwa
tamaa namna hiyo kama Fisi
mwenye njaa? Usijali nitarejea
Dar es salaam kwa ajili yako”
akasema Nawal na kumfuata
Gosu Gosu akambusu na
kumtaka akajiandae.
“I’m not handsome like
Mathew and others lakini nina
bahati ya kukutana na
kupendwa na warembo wenye
uzuri wa kimalaika” akawaza
Gosu Gosu akielekea
chumbani kwake kujiandaa.
Dakika kumi na tano
baadae Ruby akawasili na
hakukuwa na muda wa
kupoteza wakaingia garini
wakaondoka kuelekea uwanja
wa ndege wa Julius
Nyerere.Asubuhi hii hali ya jiji
la Dar ilikuwa shwari na
sehemu nyingi za jiji watu
tayari walianza kuendelea na
maisha yao ya kawaida licha ya
kuwa na hofu bado kuwa
machafuko yanaweza kuanza
tena.Vikosi vya jeshi na polisi
viliimarisha doria katika mitaa
mbali mbali
Walifika uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere ambako
Ruby alikutana na wasaidizi
wa Rais ambao tayari
walikwisha fika uwanjani pale
mapema wakawaongoza
kuelekea ndani ya uwanja hadi
katika ndege ya Rais.Kabla
hawajaingia ndegeni Ruby
akamuita pembeni Nawal
“Nawal ukifanikiwa
kuonana na Mathew mpe
barua hii”akasema Ruby huku
akilengwa na machozi
“Nitafikisha ujumbe wako
usijali” akasema Nawal na
kumkumbatia Ruby na Gosu
Gosu halafu akapanda
ndegeni.Mlango ukafungwa na
taratibu ndege ikaondoka
baada ya dakika chache ikapaa
kuelekea Riyadh
“Tumuombee Nawal afike
salama na amsaidie
Mathew.Sisi huku bado
tunaendelea na mchaka
mchaka wetu ! akasema Ruby
wakaingia garini na kuondoka
kurejea SNSA.
MPENZI MSOMAJI
- MPANGO WA
KUMUUA MATHEW
MULUMBI
UTAFANIKIWA?
- NAWAL ATAFANIKIWA
KUINGIA NCHINI
IRAN KUMUOKOA
MATHEW ?
- NINI KITAENDELEA
NCHINI TANZANIA
BAADA YA
WANAJESHI WA
MAREKANI KUUAWA
NA SNSA?
MAJIBU YA MASWALI HAYA
NA MENGINE MENGI
USIKOSE SEHEMU IJAYO YA
SIMULIZI HII.
TUNAPOKARIBIA KUFIKA
MWISHO WA SIMULIZI HII
NDEFU YA SIRI,JIANDAE
KWA BALAA LINGINE LA
MATHEW MULUMBI
KATIKA HADITHI MPYA
SCANDAL(KASHFA)
 
Siamini weekend inaisha hujatupia walau hata episode kadhaa.....mkuu tafadhali...
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 5 : EPISODE 11
“Gosu Gosu ! Amka
kumekucha tayari” akasema
Nawal ambaye naye alistuliwa
na mlio wa simu ya Gosu Gosu
iliyokuwa ikiita mfululizo.Gosu
Gosu akakurupuka kutoka
usingizini na kuichukua simu
yake.Mpigaji alikuwa ni Ruby
“Ruby habari za asubuhi !
akasema Gosu Gosu kwa sauti
ya uchovu
“Nzuri Gosu Gosu,tayari
nimekwisha anza kupatwa na
wasiwasi.Si kawaida yako
kuchelewa kupokea simu
namna hii” akasema Nawal
“Ni uchovu wa
jana.Mambo
yanakwendaje?Uko salama?
Akauliza
“Huku shwari kabisa kila
kitu kinakwenda vizuri”
“Nawal anaendeleaje?
“Anaendelea vizuri.Ni
yeye aliyeniamsha nilikuwa
nimepitiwa na usingizi”
“GosuGosu ulikuwa
umelala na Nawal? Akauliza
Ruby na kumstua Gosu Gosu
“Oh no ! akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu nimetaarifiwa
na Rais kwamba ndege iko
tayari .Mwambie Nawal
ajiandae kwa ajili ya
safari.Ninakuja hapo
kuwapitia tuelekee uwanja wa
ndege” akasema Ruby na
kukata simu
“Sikutaka Ruby afahamu
kama nimelala na Nawal,hata
hivyo hakuna kilichoharibika”
akawaza Gosu Gosu na
kumfuata Nawal chumbani
kwake na kumkuta akitoka
kuoga.
“Ruby anasemaje?
Akauliza Nawal
“Ndege iko tayari
anatupitia muda si mrefu
tuelekee uwanja wa ndege”
akasema Gosu Gosu na
kumkumbatia Nawal
“Tafadhali fanya kila
uwezalo urejee Tanzania pindi
mtakapokuwa mmekamilisha
misheni yenu huko
Iran”akasema Gosu Gosu
“Nimekwisha kuahidi
Gosu Gosu kwamba nitarejea
Tanzania.Nimeipenda sana
nchi hii” akasema Nawal na
kuliachia taulo likaanguka
chini
“Mama yangu ! akawaza
Gosu Gosu baada ya
kuushuhudia mwili mwororo
wa Nawal
“Kama isingekuwa Ruby
anakuja ningeanzisha kipute
kingine hapa hapa.Lakini
ngoja tujiandae kwa safari”
akawaza Gosu Gosu
“Mbona unanitazama kwa
tamaa namna hiyo kama Fisi
mwenye njaa? Usijali nitarejea
Dar es salaam kwa ajili yako”
akasema Nawal na kumfuata
Gosu Gosu akambusu na
kumtaka akajiandae.
“I’m not handsome like
Mathew and others lakini nina
bahati ya kukutana na
kupendwa na warembo wenye
uzuri wa kimalaika” akawaza
Gosu Gosu akielekea
chumbani kwake kujiandaa.
Dakika kumi na tano
baadae Ruby akawasili na
hakukuwa na muda wa
kupoteza wakaingia garini
wakaondoka kuelekea uwanja
wa ndege wa Julius
Nyerere.Asubuhi hii hali ya jiji
la Dar ilikuwa shwari na
sehemu nyingi za jiji watu
tayari walianza kuendelea na
maisha yao ya kawaida licha ya
kuwa na hofu bado kuwa
machafuko yanaweza kuanza
tena.Vikosi vya jeshi na polisi
viliimarisha doria katika mitaa
mbali mbali
Walifika uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere ambako
Ruby alikutana na wasaidizi
wa Rais ambao tayari
walikwisha fika uwanjani pale
mapema wakawaongoza
kuelekea ndani ya uwanja hadi
katika ndege ya Rais.Kabla
hawajaingia ndegeni Ruby
akamuita pembeni Nawal
“Nawal ukifanikiwa
kuonana na Mathew mpe
barua hii”akasema Ruby huku
akilengwa na machozi
“Nitafikisha ujumbe wako
usijali” akasema Nawal na
kumkumbatia Ruby na Gosu
Gosu halafu akapanda
ndegeni.Mlango ukafungwa na
taratibu ndege ikaondoka
baada ya dakika chache ikapaa
kuelekea Riyadh
“Tumuombee Nawal afike
salama na amsaidie
Mathew.Sisi huku bado
tunaendelea na mchaka
mchaka wetu ! akasema Ruby
wakaingia garini na kuondoka
kurejea SNSA.
MPENZI MSOMAJI
- MPANGO WA
KUMUUA MATHEW
MULUMBI
UTAFANIKIWA?
- NAWAL ATAFANIKIWA
KUINGIA NCHINI
IRAN KUMUOKOA
MATHEW ?
- NINI KITAENDELEA
NCHINI TANZANIA
BAADA YA
WANAJESHI WA
MAREKANI KUUAWA
NA SNSA?
MAJIBU YA MASWALI HAYA
NA MENGINE MENGI
USIKOSE SEHEMU IJAYO YA
SIMULIZI HII.
TUNAPOKARIBIA KUFIKA
MWISHO WA SIMULIZI HII
NDEFU YA SIRI,JIANDAE
KWA BALAA LINGINE LA
MATHEW MULUMBI
KATIKA HADITHI MPYA
SCANDAL(KASHFA)
Mkuu tuwekee mzigo tafadhal
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 24
Saa nne na nusu za
asubuhi msafara wa Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania uliwasili katika
kambi ya jeshi ya kikosi cha
operesheni maalum.Alishuka
garini na kupokewa na
waziri wa ulinzi na
kusalimiana na mku wa
majeshi na makamanda
wengine wakubwa wa jeshi
akiwamo Austin January
mkuu wa kikosi kile cha
operesheni maalum.Baada ya
Rais kuwasili ratiba
iliyopangwa kwa ajili ya
kuiaga miili ya wanajeshi
waliopoteza maisha katika
operesheni ya kuwakomboa
Coletha na Olivia
ikaanza.Viongozi wa dini
walianza kwa dua na sala
mbali mbali za kuwaombea
marehemu wale na ratiba
ikaendelea.Miili ya
wanajeshi wale ikaagwa na
Rais akaondoka kurejea
ikulu ambako alitarajiwa
kulihutubia taifa
“Ndugu watanzania
wenzangu ni siku nyingine
tena nimekuja mbele yenu
kuzungumza nanyi.Awali ya
yote narudia tena kuwapeni
pole wale wote mliofiwa na
wapendwa wenu katika
matukio ya kigaidi
yaliyotokea hapa
nchini.Tunawaombea
marehemu wote wapumzike
kwa amani Amina.
“Ndugu watanzania,nchi
yetu ambayo amani
imetamalaki,ilipatwa na
majanga ya mashambulio
mawili ya kigaidi,moja ni
bomu lililolipuliwa katika
hospitali ya Mtodora na
shambulio lingine ni
kutekwa kwa wanafunzi
sitini na sita katika shule ya
sekondari ya St
Getrude.Katika shambulio la
hospitali ya Mtodora
walifariki watu ishirini na
moja na wengine wengi
kujeruhiwa wengine vibaya
sana na katika wanafunzi
waliotekwa wameuawa
watoto wanne na
tukafanikiwa kuwakomboa
wanafunzi sitini na mbili na
walimu wao
watatu.Wanafunzi wote
waliokombolewa
watakabidhiwa kwa wazazi
wao kwa sasa wanaendelea
kupatiwa msaada wa
kisaikolojia ili kuwaweka
vizuri kwani kitendo
kilichowatokea
kimewasababishia mstuko
mkubwa.Kwa wale
waliouawa taratibu
zinafanywa ili miili yao
ikabidhiwe kwa familia zao
kwa ajili ya mazishi ambayo
yatagharamiwa na
serikali.Tunawapa pole sana
wote mliofiwa na watoto na
ndugu zenu katika
mashambulio haya
tunawaombea uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu.
“Ndugu watanzania
wenzangu magaidi
wanapofanya shambulio
mahali Fulani huwa na
sababu zao aidha kulipiza
kisasi au kulazimisha
wapewe au kutimiziwa
mambo Fulani yenye
manufaa kwao.Hapa kwetu
walifanya hivyo kuna mambo
walikuwa wanayahitaji na
wakafanya mashambulio
yale ili kushinikiza serikali
iwatimizie madai
yao.Serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania
haijawahi na haitafanya
makubaliano yoyote na
magaidi.Jukumu letu ni
kuhakikisha tunawafyekelea
mbali kila pale wanapojaribu
kujipenyeza nchini kwetu na
ndivyo tulivyofanya.Alasiri
ya jana majasusi wetu
wakishirikiana na kikosi cha
jeshi cha operesheni maalum
walifanikiwa kugundua
maficho ya magaidi hao
wakavamia na kuwakomboa
watoto sitini na mbili na
walimu wao watatu.Magaidi
wote waliokuwamo katika
nyumba hiyo
waliuawa.Hatuna huruma na
gaidi yeyote.Msako mkali
ulianza jana hiyo hiyo na
tayari tumefanikiwa
kuwakamata watu kadhaa
ambao wana mahusiano na
kikundi cha kigaidi cha IS na
tunaendelea kukamata
wengine hadi
tutakapohakikisha magaidi
wote wametiwa
mikononi.Nawaahidi
kwamba hakuna gaidi
atakayebaki,tutawakamata
wote na kuufyekelea mbali
mtandao wao wote hapa
nchini.
Usiku wa jana pia
kumetokea mapigano
makubwa kati ya kikosi
chetu cha operesheni
maalum na magaidi katika
mpaka wa Tanzania na
Kenya na katika mapigano
hayo makali tumewapoteza
vijana wetu kumi na tatu na
kuwasambaratisha magaidi
wote.Tunawaombea vijana
wetu hao mashujaa
wapumzike kwa amani
kwani wamemwaga damu
yao kwa kulipigania taifa lao
Ndugu watanzania
katika watu tuliowakamata
wakihusiana na mtandao wa
kigaidi wamo pia viongozi wa
serikali.Wapo baadhi ambao
tunawashikilia tunaendelea
kuwachunguza na pale
uchunguzi utakapokamilika
tutawafikisha
mahakamani.Katika sakata
hili pia tumegundua kwamba
kuna watu ambao si raia wa
nchi hii lakini wanaishi hapa
nchini na tayari wamekwisha
ingia hadi katika ngazi za
uongozi.Tunaanza kufanya
uhakiki wa viongozi wote wa
serikali kujiridhisha kama
kweli ni raia wa
Tanzania.Tumebaini mchezo
unaofanywa na watu
wasiotutakia mema wa
kupandikiza watu wao hapa
nchini toka wakiwa wadogo
kwa malengo ya kuwatumia
katika mipango yao na watu
hao wanaopandikizwa
wamediriki kushika hadi
nafasi za uongozi.Tutakuwa
makini katika mipaka yetu
kudhibiti wahamiaji haramu
ninatoa rai kwenu
watanzania wenzangu kama
unamfahamu mtu yeyote
ambaye si raia wa nchi hii
lakini anaishi hapa nchini
toa taarifa katika vyombo
husika ili aweze
kushughulikiwa haraka sana
kwani wengiwa magaidi
hawa ni wageni ambao
wamekuwa wakiishi hapa
nchini wakifadhiliwa na
wenyeji
Ndugu watanzania
matukio haya
yametufundisha kwamba upo
ulazima wa kuviongezea
nguvu kubwa vyombo vyetu
vinavyohusika katika
mapambano na ugaidi ili
viwe na uwezo mkubwa wa
kubaini matukio ya kigaidi
kabla hayajatokea na
kuyadhibiti.Hilo tutalifanya
haraka sana.Mwisho kabisa
nataka kuwajulisha kwamba
kuanzia leo hii nimelivunja
baraza langu la mawaziri
nitateua baraza jipya hapo
baadae.
Narudia tena wito wangu
wa kuwataka watanzania
tuwe wavumlivu na tuviache
vyombo vya ulinzi na
usalama vifanye kazi yake
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza
BAADA YA MWEZI MMOJA
Tayari umekwisha pita
mwezi mmoja toka
yalipofanyika mashambulio
ya kigaidi.Nchi imetulia na
wananchi wanaendelea na
maisha yao kama
kawaida.Rais Dr Evans
ameunda baraza jipya la
mawaziri.Baada ya uchuguzi
kukamilika aliyekuwa waziri
mkuu wa jamhuri ya
munganowa Tanzania na
wenzake sitini na saba
walifikishwa mahakamani
wakituhumiwa kwa makosa
ya ugaidi.Dr Olivia Themba
alikikabidhi serikalini kituo
cha utafiti wa magonjwa ya
binadamu na wanyama
ambacho alikijenga kwa
fedha kutoka kwa watu wa
IS na yeye akaanza ujenzi wa
hospitali kubwa ya
magonjwa ya moyo pembeni
kidogo ya kituo kile.
Mathew Mulumbi
alitafutwa bila mafanikio na
hakuna aliyefahamu yuko
wapi.Timu iliyotumwa
kumtafuta ilirejea bila ya
Mathew Mulumbi na kutoa
ripoti yake kwamba kuna
uwezekano mkubwa alifariki
na kuliwa na fisi kwani eneo
lilipotokea shambulio lile
kuna fisi wengi.Rais Dr
Evans alituma ujumbe
maalum kwenda Paris
Ufaransa kwa Peniela mke
wa Mathew kupeleka salamu
za pole kufuatia kifo cha
Mathew.Ujumbe ule
uliongozwa na Austin
January ambaye alikuwa na
Mathew eneo la tukio.Ruby
aliondoka nchini kwenda
kuendelea na shughuli zake
lakini Gosu Gosu aliombwa
na Peniela kubaki nchini
kuendelea kusimamia miradi
yote ya Mathew ombi ambalo
Gosu Gosu alilipokea kwa
mikono miwili.
Mahusiano kati ya Dr
Evans na Agrey Themba
yaliendelea baada ya Dr
Evans kueleza ukweli wa kile
kilichotokea na kumuomba
rafiki yake yule mkubwa
msamaha wakasameheana
na maisha yakaendelea
kama ilivyokuwa awali lakini
kilichotokea kilibaki kuwa
siri kati yao
Siku tatu baada ya
shambulio la mpakani
kutokea Devotha aliondoka
nchini kwa ndege akielekea
Dubai na hakuna mwenye
mawasiliano naye tena wala
kufahamu mahala alipo.
Idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi
iliimarishwa zaidi na Rais
aliamua kuitambulisha
rasmi idara hii kwa viongozi
wa juu wa serikali na ulinzi
ili wafahamu uwepo
wake.Kaiza alipewa
ukurugenzi wa idara hii.
TAMATI
MPENZI MSOMAJI HAPA
NI TAMATI YA SIMULZI
YA SIRI PART 1.USIKOSE
KUSOMA SIRI PART 2
YENYE KICHWA
MAISHA NA KIFO CHA
MELANIE CHUMA


Safi sana... Story Nzuri sana...

Chapter 1 Closed...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom