Riwaya: See Me (Nione)

Riwaya: See Me (Nione)

Ndiy hii natunga mpk mwisho kbs see me afu inbk ile hii mpk mwish naiachia ndo maan bad nk naiandaa kuandaa kaz 2 so mchez
 
SEE ME

(THE FINAL CHAPTER)
SEHEMU YA 44/50


“ Ma..ma yako ni nani?”. Jeradi akamuuliza mage ambaye muda wote amekodoa macho kwa mama yake juliana, jeradi akahisi yuko kwenye ndoto nzito ambayo anatamani ashtuke na kukuta siyo kweli anachosikia na kukiona, wakaanza kukokotwa kuingizwa ndani ya jengo hilo, ambalo wageni wanakaa katika giza ambako taa haiwaki kabisa ila watekwaji wanakaa katika mwanga mkali wa taa zilizokuwa zinawaka katika jengo, wakakokotwa na kuingizwa ndani wote kwa pamoja na wakatizam kule kwenye giza ambako wanunuzi ndiko walipo, ambao hata wao kwa asilimia kubwa sura zao hawafamiani, na kma mtu alipendezwa na mtu basi aliwasha taa ya bluu ambayo ilikuwa inawaka katika kifungo cha nguo yake ambayo lilikuwa ni koti lenye kishikizo chenye mwanga hafifu na kila mtu alikuwa na rangi yake ambayo ndiyo ilikuwa ikishindanishwa katika bei ya ununuzi wa watu hao lakini bluu ilikuwa maalumu zaidi..
Juliana alihisi kama ubaridi moyoni mwake akaanza kutetemeka huku roho na moyo wa huruma ukimvaa mwilini mwake, akaanza kujutia makosa yake aliyoyafanya miaka mingi iliyopita, macho yake yote yalikuwa kwa mtoto wake mage ambaye muda huo alikuwa mjamzito tena tumbo lake lilikuwa tayari lishaanza kuchomoka, akawa anameza mate huku akionekana kuogopa zaidi kwa kile kitakachoendelea ndani ya hilo jengo. Akaja mtu mwenye kipaza sauti mkononi mwake na uso wake ulikuwa umefunikwa na kinyago akasalimia kwa kuinama kidogo kama watu wa mashorati, au kung fu kisha, akaweka kipaza sauti mdomoni mwake sehemu ya kuongelea na kuongea kwa lugha ya kiswahili, ambayo kwa watu wa nchi za jerani walikuwa wanapata tafsiri kupitia headphone walizokuwa wamevaa masikioni mwao.
“ Nashukuru tumekutana tena baada ya miezi sita kupita mmekuwa wateja wetu waaminifu sana ndani ya miaka kumi toka bishara hii kuanzishwa na umoja wa afrika mashariki”. Akazungumza na kufanya jeradi kukunja ndita baada ya kugundua kuwa umoja wa nchi za kiafrika ndiyo zinaongoza biashara hii haramu.
“ Tunafanya hivi kuendesha serikali zetu na familia zetu, afrika siyo masikini ina utajiri wa kutosha na huu pia ni utajiri”. Akazungumza na kufanya vibopa kucheka kwa sauti,.
“ Tuanze biashara”. Akazungumza na wakaja watu wenye vinyago pia wakiwa na namba kwenye tisheti zao na kila mtu akasimama kwa mtekwaji mmoja mmoja,.
“ tunaanza na namba 6 nani anamtaka”. Akazungumza huku akimtizama namba 6 alikuwa ni mtoto mdogo wa kike umri kama miaka 18.
“ huyu bado mbichi mbichi ni wewe tu unataka figo lake, au unataka moyo wake, au unamtaka kimapenzi, au kushoot filamu za ngono”. Akazungumza huku akimtizama msichana yule ambaye ameshalia mpaka machozi kumkauka, taa ikawaka ya kifungo na dau kubwa likatangazwa na yule jamaa mwenye kipaza sauti, na msichana huyo akatolewa katika foleni hiyo ya mauzo na kukokotwa kwenda upande mwengine.
“ kuna wa ngono hapa wakucheza filamu za ngono “. Jamaa akazungumza na wakasogezwa wadada wengine mbele wanne na biashara ikaendelea kufanyika ya kuwanunua ili wakashoot filamu za ngono, alimaarufu kama XXX
“ Aya wa viungo wanakuja”.akazungumza na mstari wa jeradi ukafatia wakiwa wanaume washoka na wadada wenye afya zaidi na jamaa akaanza kuzungumza kama kawaida yake.
“ Namba 40 tulimpima maumbile yake ya mbele ana inchi zaidi 7”. Jamaa huyo akazungumza huku akimtizama mwanamume mmoja ambaye alikuwa ni pande la mtu, taa zaidi ya 8 zikawaka huku kila mmoja akimtaka mwanamume huyo ambaye walimuhitaji kwa kiungo chake au katika mambo ya ushoga.
“ waooh dau naweka kubwa”. Akatangaza dau kubwa na mtu mfupi alokuwa miungoni mwa hao wanunuzi akashinda kumpata mwanamume huyo, biashara iakendelea ya kuuza watu na viungo vyao.
“ huyu mpaka sasa anafigo moja pekee, moja lilikwisha toka na ni mtu mwenye afya nzuri zaidi”. Jamaa akazungumza na kumtizama jeradi aliyemkazia macho, taa ya kijani ikawaka na akanunuliwa na mwanamke na yeye akatolewa eneo hilo huku jeradi akitizama kule kwenye giza asifanikiwe. Kuwaona don john wala juliana.
“Wenye mimba wako 8 hawa bana hela zao ni kubwa maana unanunua mama na mtoto”. Jamaa akazungumza na kina mage wakasogezwa mbele na wenzake, taa za kutosha zikawaka bila hata ya jamaa kutangaza dau, wakaanza kucheka wao kwa wao na kila mtu akaweka pesa kubwa kumpata mtu aliyemtaka,Mage akawa anagombaniwa na watu zaidi ya wawili ghafla taa moja ikawaka na kutangaza dau kubwa ambalo kila mtu alizima taa yake na kuguna,huyo mwanamke akaoneka ndiye aliyenunuliwa kwa pesa kubwa zaidi kuliko ata figo zilizochukuliwa muda ulopita..
Biashara ikaendela na walonunuliwa wakatolewa eneo ilo na kupelekwa maeneo mengine kabisa ya sehemu iyo kwa ajili ya wanunuzi kuwachukua.
“ Ni lazima nimtoe mtoto wangu eneo hili”. Juliana akajisemea kimoyo moyo huku akiwaza kutokutoa dau hilo alilotangaza moyo wake ulikuwa mgumu katika utoaji wa pesa,lakini alijikuta sasa akiwa mwepesi moyoni mwake na roho ya huruma kumuingia ili tu amtoe binti yake..

AFRIKA YA KUSINI.

Gari ikazima njiani huku nikiwa sielewi niko maeneo gani katika nchi hiyo ya afrika ya kusini, nikamtizmaa tylat ambaye naye amenikodolea macho huku akionekana kuwa na hofu moyoni mwake.
“ tuko town” nikazungumza baada ya kuona miji kwa mbele ikiwa imepangika vyema na majengo makubwa ya kuvutia.
“ Inabidi tupate simu”. Nikazungumza na kuanza kutizama tizam ndani ya hilo gari bila kuona chochote, bahati nzuri nilifankikwa kuona raba ambazo kwa upande wangu sikuwa na viatu kwani vyangu nilimpa msichana huyo ambaye alivaa na vilimkaa vyema, nikavitizama na kuona vikinipwaya kidgo, sikuwa na cha kufanya nikavaa viatu ivyo, na nikaona pesa kwenye droo ya gari ilo kukiwa na noti za afrika kusini na sarafu, nikatabasamu baada ya kuona kibanda cha telephone kikiwa pembeni ya barabara,
“ Tutoke nje kuna simu pale”. Nikazungumza na tylat na akakubaliana na mimi tukatoka nje na kuelekea ndani ya kibanda icho chenye simu, nikatia sarafu kwenye kijishimo hukj tylat akibonyeza namba anazozijua mwenyewe na simu ikaanza kuita na kupokelewa sauti ya mwanamume ikasikika.
“ Hallo”.
“ snake ni mimi”. Binti akazungumza kwa kingereza na nikamuelewa.
“ Madaaaam huko wapi?”. Sauti hiyo ikasikika na kwa haraka nikakwapua simu na kuiweka sikioni.
“ Niko naye mimi, mleteni mwanamke wangu nami nitawakabidhi huyu binti”. Nikazungumza kwa sauti yenye msisitizo.
“ okay mko wapi?”. Akazungumza na nikaanza kutizma tizma majengo na vibao kama nitapata jina lolote
“ Sijuhi tulipo”. Nikazungumza kwa msisitizo
“ okay kuweni na simu yenu tuwafatilie”.
“ hatuna simu namuhitaji mwanamke wagu leo leo na usafiri wa kunipereka mpaka tanzania”. Nikazungumza
“ sawa tupe ushirikiano wako tutakupa ndege ambayo inaondoka leo na abiria kuelekea tanzania huyo binti awe mzima, wataalamu wangu wanakuja huko mlipo”. Akazungmza na nikatizama ile simu na kuivunja ikapoteza mawasiliano baada ya kuvuta nyaya zake kwa nguvu mpaka kukatika, eneo hakukuwa na watu saana maana ndiyo ilikuwa mwanzo wa mji ambao huko mbele yetu.
“ sasa tutawapataje”.
“ Tutapiga tena simu bado sarafu ninazo”. Nikazungumza na nikarudi ndani ya lile gari ambalo mwanzo kulikuwa na kanzu nyeupe nikaichukua na nikaivaa ilikuwa kubwa kuniliko mimi, nikamtizma yule binti na kuona naye akiwa amechoka choka.
“ Tutoke ili eneo”. Nikazungumza na tukaanza kutembea kuingia ndani ya mji huo.

SEE ME
THE FINAL CHAPTER
( leo saa 4 usiku mzigoo huu unaisha)
 
SEE ME

THE LAST CHAPTER
SEHEMU YA 45,46,47,48,49,50(THE FINAL EPISODE)

( ASENTENI WOTE, NA MNISAMEHE KWA NILIYOWAKERA ILA HII LIKIZO NAITUMIA VIZURI, NA NYIE)......

NB ( Ni story ya kufikirika tu haina uhalisia wowote ule na maisha halisi)

MWISHO……..

SEHEMU YA 45…

Tukaendelea kutembea na kuingia ndani ya jiji hilo ambalo hatukujua ni jiji gani hapo nchini afrika ya kusini, lilikuwa limechangamka kama mitaa ya kariakaoo jijini dar es salaam tanzania.
“ nasikia njaa”. Tyalt akazungumza na kuegemea ukuta, tulikuwa katikati ya majengo mawili makubwa ambayo katikati yake kulikuwa na kichochoro ambacho ukutani kumepigwa stika za kihuni na matusi ambayo yalitukana raia wa kigeni, kabla sijamjibu nikaona vijana wanne wakija kule tulipo, walionekana kama ni mateja.
“ Unajua ki afrika kusini?”. Nikamuuliza ila akatingisha kichwa kuwa hajui chochote.
“ Tulia”. Nikazungumza na kuwatizama wale vijana kwa macho ya kuibia ibia, wakatufikia na nyuso zao ni kweli walionekana na mateja wa madawa na bangi.
Wakazungumza kiafrika ya kusini, hakuna mmoja wetu aliyeelewa wanasem nini ila nahisi walishangaa muonekano wetu maana tulikuwa tumechakaa, wote wakatoa macho baada ya kumuona tylat vizuri walitambua ni msanii mkubwa duniani. Wakanong’onezana kisha wakasogea taratibu na mmoja wapo akanisogelea mpaka kwenye sikio lake na kuweka mdomo wake.
“ Umemtoa wapi?”. Akazungumza kwa kingereza
“ Nani?”. Nikamuuliza
“ Huyo mtoto uliyenaye ili ni dili maana dau kubwa la pesa limetangazwa tunaomba tujumuike wote kumrejesha”. Akzungumza na nikatambua wanahisi nimempata na nataka kumrejesha kwa watu wake kwahiyo nishirikiane nao ili nikipata pesa basi na wenyewe wapate.
“ Siwezi wapatia”. Nikazungumza.
“ uko peke yako sisi tupo wanne pili nimegundua wewe siyo mzaliwa wa hapa kwahiyo sitokuwa na huruma na wewe tutakuua na kukukata kata mapanga kama yule NACY B aliyemuua mwenzake”. Akazungumza na sikumuelewa kuhusu Nacy B ndiyo nani na kafanya nini?
“ mnahitaji tugawane kiasi gani”.
“ owah kwani we huoni television pesa iliyotangazwa ni zaidi ya dola milioni miatano”. Akazungumza kwa msisitizo
“ inaonekana mmechoka sana”. Akazungumza na kumsogelea tylat ambaye anatetemeka nikamuwahi kumshika mkono wake na kumzuia.
“ Ni mtu wangu ukienda kinyume na hili dili nalikata maana mimi najua mawasiliano ya kumpata na kumpereka walipo”.
“ hahah namba ziko hewani, kila mtu anazo”. Akazungumza na nikambana mkono kwa nguvu mpaka wenzake wakasogea na akawazuia kwa mkono.
“ tutagawana dola mililoni mia kila mmoja”. Nikazungumza na akatingisha kichwa huku akitabasamu
“ We ni jasiri lakini muoga”. Akazungumza na akajirekebisha
“ ili afike salama kuna watu lazima tuwakwepe”. Nikazungum a
“ na kama mtaniua au kunigeuka hatofika salama maana watu hao mimi ndiyo nawajua wakoje”. Nikazungumza na wakanong’onezana na nikaona wakirudisha silaha zao kwenye viuno vyao kwani niliwaona wakichomoa silaha na walitaka kunidhulu au kuniua kabisa.
“ Tufate”. Akazungumza yule jamaa na nikamkonyeza yule binti kuwa inatupasa tuwafate kwa sasa maana sikuwa na nguvu kabisa za kupambana nao nilikuwa nimechoka na mwili ulikuwa umekosa maji hadi chakula.
**************>>>*********

“ Umeninunua we shetani, ungeniacha huko huko nikafie huko huko sihitaji kuwa na wewe shetani”. Mage akafoka huku akimtizama mama yake juliana ambaye ndiye aliyemnunua mage.
“ Nisamehe mwanangu nimekuleta hapa pumzika kwanza na utapata kila kitu unachotaka”.
“ sihitaji kuishi na wewe wala kula chochote kile, wewe ni shetani mama”. Mage akazungumza na kusimama toka kitandani huku mishipa ikiwa imemtoka na hasira kumpanda
“ Nisamehe”. Juliana akazungumza kwa sauti ya utulivu, kabla ajafanya kitu mage akashika tumbo lake huku akihisi maumivu makali ya uchungu, juliana akataka kumshika ila mage akajaribu kumpush ila akashindwa, uchungu ukaanza kumshika mkoja ukamtoka wa kutosha kwenye uchi wake,
“ Ooh shit napigia daktari chapu”. Juliana akazungumza na kuchukua simu yake na kupigia majopo ya madaktari wa familia ya marehemu mr solo.
“ Mje nyumbani kuna mjamzito kashikwa na uchungu”. Akzungumza
“ sijuhi ana miezi mingapi?”. Juliana akazungumza huku moyo wake ukianza kupata hofu jinsi anavyomuona mage anavyougulia maumivu pale chini.
“ mage ina miezi miangapi nambiye tafadhali”. Akzungumza kwa upole
“ saba”. Mage akazungumza na juliana akamwambia daktari kwenye simu.
“ kwahiyo ni njiti, sawa tunamleta”. Juliana akazungumza na kukata simu kisha walinzi wakaja na kumtoa mage nje na kumuingiza kwenye gari kumuwaisha hospitali..
*******

“ Siwezi kufa kizembe”. Jeradi akazungumza huku akitizama anavyotaka kuchomwa sindano ya nusu kaputi ili viungo vyake vya ndani vitolewe na kuuzwa, akamtizama daktari anayekuja na sindano ya nusu kaputi, akajilegeza zaidi mwili wake kuonekana kuwa bado amelala, yule daktari akafika na kuandaa sindano yake vizuri kisha akashika dripu lililoisha maji na kutaka kuweka ile dawa ya nusu kaputi ili iingie taratibu kwenye mirija waliyokuwa wameipereka kwenye mwili wa jeradi,kwa kasi ya ajabu jeradi akamuwahi dokta na kuchukua ile sindano kisha kumtoboa nayo shingoni, hukua kichukua mirija ya dripu na kumbana nayo shingoni kisha akaanza kumnyiga kwa nguvu na kufanya dokta kuanza kupepesuka kuzuia roho yake isiende akawa anajaribu kujitoa ila anashindwa kwani alikabwa kisawa sawa, ndani ya dakika 2 dokta pumzi zake zikakata na kupoteza maisha kisha jeradi akabadili zile nguo na kuvaa yeye zile za udaktari kisha mtu wake akamlaza kwenye kitanda taratibu akaanza kutoka ndani ya chumba icho huku usoni akiwa na barakoa ya bluu ya kidaktari. Akazidi kutembea kwenye korido hiyo ndefu ambayo imejaa vyumba vingi vya upasuaji na pia kulikuwa na camera ambazo alijua zinamtizama kwahiyo alikuwa makini kutembea taratibu na asijulikane mapema maana kiumbo waliendana kabisa na yule daktari.
“ Naenda wapi”?. Akajiuliza baada ya kuona ngazi zikielekea chini kwenye jengo ilo ambalo lilionekana ni hospitali kubwa.
“ hii hospitali gani?. Akajiuliza huku akiendelea kutembea akapishana na mfanyakazi wa kike.
“ samahani”. Jeradi akazungumza
“ Ndiyo dokta pius”. Yule mfanyakazi akazungumza na kumfanya jeradi atizame kwenye kifua upande wa kushoto na kukuta jina likiwa limeandikwa dokta piusi kwenye mfuko wa juu ya kifua wa vazi ilo.
“ siko sawa unawez nisaidia kutoka nje”. Jeradi akazungumza na yule mfanyakazi akakunja uso kidogo na akaanza kumtizama jeradi juu mpaka chini, alimshtukia siyo dokta pius mwenyewe, yule dada akaanza kurudi nyuma baada ya kuona damu zikitoka usawa wa tumboni upande wa figo ambapo jeradi ndipo kuna kidonda chake, jeradi akajitizama na kuona damu zikivuja, kwa haraka akamuwahi yule mwanamke na kumbana mdomo wake kisha kuanza kumvuta na kumbana kwenye ukuta,huku akikwepa camera ambazo ziko huko chini ya hiyo hosptali.
“ Nitakuua kama kimya”. Akazungumza na kumbana kwa nguvu dada yule.
“ s..awa”. Akazungumza kwa tabu.
“ hii hosptali gani”? Jeradi akazungumza kwa msisitizo na sauti nzito na msichana huyo akamjibu na kufanya jeradi kutumbua macho ya mshangao kwani hosptali hiyo ndiyo hospitali kubwa TANZANIA na ndiyo yenye madaktari bingwa toka ndani na nje ya nchi.
“ Una uhakika hii ni hiyo hosptali”. Akamuuliza na kumbana
“ ndiyo kak…a niache sitoambia mtu”.
“ Huku ni wapi?”.
“ Chini kabisa ya hosptali yani chini”.
“ hii biashara inafanyika huku serikali inajua”.
“ ndiyo kaka”. Akazumgumza
“ Nitoe nje”.
“ Huwezi toka nje mpaka muda wa kutoka nje ufike labda tu itokee dharula ndiyo tunatoka”. Akazungumza na akatizama juu na nikaona alamu za moto pamoja na switch yake.
“ kwanini mnateka watu “.?
“ kaka”. Akazungumza kwa upole na kumtizama jeradi ambaye akamlegezea na kuacha kumkaba,
“ Njia ya kutoka ni ipi”.
“ kama unata kubinya hizo alamu njia ya kutoka iwa zinajifunguwa kawa dakika tano pekee kuna milango ya dharula miwili tu mmoja huko chini huku, na mwengine haujulikanigi wapi hupo ila nasikia upo mwengine”.
Akazungumza na jeradi akamtizama kwa umakini dada huyo
“ wewe ni mpelelezi hapa”. Jeradi akazungumza na kumfanya binti huyo kutumbua macho kwani siri yake imefichuka ya miaka mingi na akajiuliza huyu mtu amejuaje.
“ hapana kaka”.
“ Unaonyesha uogopi, unajilazimisha kuniogopa, wewe bila shaka ni mpelelezi”. Jeradi akazungumza
“ Uuh ndiyo raisi waliyemuua miaka iliyopita alinituama ni peleleze hii hoaptali alihisi kuna kazi haramu zinaendelea na mpaka leo naendelea na kazi yangu umejuaje?”.
“ tutakutana mungu akipenda”. Jeradi akazungumza na kwa haraka akabinya alamu ambazo zilianza kuwaka taa nyakundu ma kupiga honi ya moto.
“ Uko chini ya nani kwa sasa”.
“ Siwezi kwambia”. Akazungumza kwa kujihamini
“ Wewe ndiye shahidi ambaye nilikuwa natafuta muda mrefu sana kupata ushahidi ili kuifunga hosptali hii ya yule nyamela wewe ndiye shahidi wangu”. Akzungumza na kumkabidhi kadi yenye namba zake, jeradi akaichukua
“ pita kushoto mlango utakuwa wazi na muda so mrefu utajifunga maana kuna mitambo inascan kama kweli kuna moto au laha”.
“ Hakuna watu”.
“ hizo njia ni za siri we nenda uone ukitoka ndiyo utashtuka huko wapi”. Yule binti akazungumza na jeradi kwa haraka akampiga ngumi ya uso iliyomzimisha yule msichana na kumdondosha kama mzigo, ilikuwa ni ngumi ya kushtukiza tena bila huruma jaradi akaanza kukimbia kwa haraka na kutoka eneo hilo, akafata njia aliyoelekezwa na akatoka mpaka nje ya jengo ilo huku camera zikimnasa na mlango ukajifunga kiotomatiki akiwa tayari nje ya hosiptali hiyo.
“ BONDE LA MTO MSIMBAZI”. Jeradi akazungumza baada ya kuona ndipo alipotokea na akatizama mlango alotokea akaona ni jengo tu la kawaida kama gofu ambalo alijamalizia kujengwa huku pembezoni mwake kukiwa na uoto wa asili ulozunguka eneo hilo la mto msimbazi, akatizama jengo ilo na kugundua ni gofu tu ambalo limetelekzwa.
“ kwahiyo hospitali imefika mpaka huku au??”. Akawaza.
“ imechimbwa chini chini imefikia hadi huku ina maana ina ukubwa kiasi gani na je watu hawajuhi chochote kile”. Akawaza na kuanza kuvua zile nguo za udaktr na kuziwek pembeni, kwa kuzifunika funika na nyasi zile za uoto wa asili iliyoota eneo hilo na miti pamoja na mboga mboga wanazolima watu, eneo hilo liloonekana kama kichaka tu kutokana na uoto wa asili ulokuwa eneo hilo.
************ **********
AFRIKA YA KUSINI

“ badilini nguo”. Wale jamaa wakazungumza na kunirushia nguo mimi na Tyalt tukatizaman kisha wakatoka nje mana tulikuwa ndani ya godauni lao ambalo lilikuwa limejaa mabaki,ya marijuana na chupa nyingi za pombe kali toka kampuni mbalimbali za pombe,
“ nakujua vizuri vaa”. Nikazungumza kwani kama ni kumuona nishamuona umbo lake lote, akatizama suruali aliyopewa na sweta lenye kofia juu, hakuvaa nguo hizo zaidi akazichukua na kisha kuanza kuzitizama.
“Nakupisha”.Nikazungumza na Kuondoka ndani humo kisha nikaelekea kwenye kona moja wapo ili niweze kuvaa nguo nilizopewa macho yakanitoka baada ya kuona kwenye ukuta kuna picha za watu walopigwa X yaani alama nyekundu, nikasogea kwa umakini na kuona watu kama wanne wakiwa wote wana alama X huku mtu mmoja pekee akiwa bado hajapigwa alama hiyo, nikasogea kwa ukaribu zaidi na kushtuka baada ya kuona picha ya DON JOHN, Mshangao mkubwa ukanipata na kuhisi naota ndoto na siyo kweli mzee huyo hakuwa don john, lakini sivyo alikuwa ni yeye mwenyewe.
“ Unatizama nini?”. Sauti ikasikika nyuma yangu nikageuka na kumuona yule jamaa aliyekuwa anaongea na mimi kule nje, akanisogelea kwa ukaribu kisha na yeye akatizama ile picha ya don john na akatabasamu.
“ Unatoka tanzania vipi ushamuona huyo mtu,”.? Akaniuliza na kufanya nitafakari kidogo.
“ Umejuaje me mtanzania”?.
“ Hahha kwasababu na mimi ni mtanzania”. Jamaa akazungumza kwa lugha fasaha ya kiswahili na kufanya nifarijike kidogo ko kuona ndugu yangu katika nchi hizo za watu.
“ Simfahamu”. Nikazungumza
“ huyo ndiye anayeendesha kila kitu tanzania na raisi anayeongoza nchi kwa sasa hana cha kufanya maana Taifa linadaiwa pesa kubwa, na halina uwezo wa kulipa kwahiyo huyo mtu kupitia biashara zake ndiyo anaongoza kila kitu na analipa deni la taifa yeye”.
“ Na huku anafanya nini”?
“ Ni adui yangu”. Jamaa akazungumza kwa sauti nzito na kutoa pakti ya sigara mfukoni na kuchukua kiberiti cha gas kisha akatoa sigara au bangi na kuweka mdomoni kisha akawasha na kuanza kuvuta mapafu ya kutosha.
“ Adui yangu namba moja”. Akazungumza tena na kutabasamu kisha akatizama picha ya don john kwa macho makali, moyoni nikazidi kufarijika zaidi kwa kuwa tayari nimepata mtu mwengine ambaye ni adui wa DON JOHN mtu ambaye nahitaji anieleze ukweli wote kuhusu mimi na familia yangu na pacha wangu AMIDU.
Ghafla majibishano ya risasi yakaanza kusikika nje, kwa haraka jamaa akaemda kuchungulia dirishani kwa umakini na kisha akatoa bastola yake na yeye na kuiweka standby.
“ Unajua kutumia”?. Akaniuliza nikatingisha kichwa kuwa najua akataka kunipa ila akasita.
“ Mchukue binti pita naye mtoke kwenye ule mlango”. Akazungumza na kunionyesha mlango uliopo mbele yetu, nikatoka haraka kwenye hiyo kona na kwenda kumfata tylat ambaye alikuwa ameziba masikio yake,huku akitetemeka, nikamshika mkono na tukaanza kuelekea kule kwenye mlango wa pili wa godauni hilo huku wale jamaa wakitufata nyuma na wakabaki wawili ambaoa wanaendelea kushambuliana na watu ambao siwafahamu.
“ hawa ni watu wanaomtaka huyo dada”. Yule jamaa akazungumza na tukaendelea kutembea, tukafungua mlango na kukutana na gari pembeni, jamaa akafungua mlango na akaingia na sisi na wenzake pia tukafatia huku wale wawili wakibaki kule kwenye majibishano ya risasi.
“ Unaacha wenzako”?
“ hatuwaachi ila hapa ndo tunawafata”. Jamaa akazungumza na kumeza mate kisha akapangua gia na kugeuza gari na kulitoa kwa kasi huku tukivaa mikanda ya gari hilo lenye siti tata za nyuma, akalizungusha upande wa pili wa godauni hilo na kulitoa kwa kasi kuelekea kule kwenye mashambulizi ya risasi,kisha wakafungua mlango ubavuni kwangu na wale jamaa wawili kwa haraka wakaingia baada ya jamaa kusimamisha gari hilo, mmoja alikuwa amejeruhiwa na risasi mguuni, wakafunga mlango huku risasi zaikitufata na kugonga kwenye gari hilo bila kutupata wahusika, nikatizama vizuri na kumuona yule mtu mfupi aliyenipokea mimi na diana kule uwanja wa ndege na tuakenda kupewa kazi hii, jamaa akavuta mafuta na kuliondoa gari kwa kasi kutoka eneo hilo…

***********************
( Itaendeleaaa)LOADING 46


SEE ME

SEHEMU YA 46…..

Sauti ya mtoto ikasikika baada tu ya kutoka kwenye tumbo la mama mjamzito wa miezi saba pekee na siyo tisa kama ilivyo kwa binadamu.
“ Mzuri”. Daktari akazungumza na kutenganisha kitovu kisha akamchukua na kumuweka kwenye mashine maalumu ambayo akizaliwa mtoto njiti basi atakaa kwa muda fulani kisha kumtoa.
“ kwa mara ya kwanza toka nizaliwe naona mtoto njiti mwenye afya na uzuri wa kuvutia kama tu yule mwenye miezi 9”. Dokta akazungumza huku akimtizama mama wa mtoto ambaye mpaka sasa hajielewi.
“ Kuweni naye makini” Dokta akazungumza kisha akatoa gloves za mkononi na kumkabidhi nesi na kisha akavua na koti lake na kumkabidhi nesi.
“ nitarudi”. Akazungumza na kutoka nje na kukutana na juliana.
“ Nahitaji kumuona mjukuu wangu”. Akazungumza huku uso ukiwa na bashasha.
“ Ni wewe mtupu juliana yani uso wako kabisa”. Dokta akzungumza na kufanya juliana machozi kuanza kumtoka kwa wingi machoni mwake.
“ Una maanisha nafananae”.
“ Sana tu yani amekuzaa, binti yako sijuhi nani yako huyu, amekuzaa kabisa mtoto wa kike mzuri kama wewe”. Dokta akzungumza na kumfanya juliana azidi kutokwa na machozi.
“ utamuona kama ndani ya dakika 20 hivi”.
Furaha aliyokuwa nayo juliana haikuweza kijificha kabisa katika usoni mwake,
“ wanamsafisha dakika tano utaenda muona mzazi” . Dokta akzungumza
“ Nashukuru dokta”. Juliana akazungumza kwa furaha

AFRIKA KUSINI

“ Wapigie watu wako” . Jamaa akazungumza na kunikabadhi simu nikaipokea kisha nikamkabidhi tylat ambaye aliandika namba kisha kunikabidhi mimi, simu ikaita na nikaipokea na kuiweka sikioni.
“ weka loudspeakr” jamaa akazungumza na nikafanya hivyo.
“ Niko na binti yenu”. Nikazungumza kwa sauti nzito
“ mko maeneo gani maana tushafanya kila kitu juu yako mpaka kukuandalia ndege itakayokurudisha tanzania”. Sauti ikasikika upande wa pili wa simu.
“ nipo naye mjini, nahitaji twende mpaka uwanja wa ndege nikiwa na mtu wenu na nyie mkiwa na mtu wangu ili tuweze badirishana ila kwa sharti moja”. Nikazungumza kwa sauti nzito.
“ Muwe na parachuti mbili”. Nikazungumza na nikasikia jamaa akimeza mate yake.
“ siwezi wa hamini mnaweza niuza kwenye serikali ya tanzania”. Nikazungumza.
“ Hakuna shaka ila kumbuka ili uruke utahitaji kuteka ndege ili mlango ufunguliwe na ni haramu kwa kosa hilo”. Jamaa akazungumza
“ Mpaka nasema hivi siko peke yangu”. Nikazungumza na kuwatizama wale wahuni ambao walitingisha vichwa vyao.
“ muwe na pesa za kutosha”. Nikazungumza kwa msisitizo
“ Kuhusu pesa usijali ila jambo la kuruka halitowezekana”. Jamaa huyo akazungumza na yeye kwa msisitizo
“ kuna option nyengine mtafata tanzania”. Nikazungumza
“ okay nimekuelwa mtaruka”.
“ parachuti tunahitaji zaidi ya sita”. Nikazungumza ila yule jamaa akatingisha kichwa na kunionyesha vidole vitatu
“ tunahitaji tatu”. Nikazungumza
“ sawa kuhusu pasipoti msijali tushamaliza kila kitu maana sisi tuna uwezo wa kwenda kokote kule” . Akazungumza
“ leo usiku ndege inaondoka na tumekutafuta sana ili tukambie”. Jamaa huyo akazungumza
“ Tunakutana wapi?”.
“ uwanja wa ndege”. Nikazungumza
“ ndege inaondoka saa 2 usiku”.
“ tutakuwa hapo saa moja”. Nikazungumza
“ mpe simu huyo msichana”. Nikazungumza
Kama sekunde kadhaa wakamkabidhi simu diana niliweza sikia sauti yake mwanzoni akisem staki ila aliposikia ni mimi alichukua kwa haraka.
“ Randy uko salama”.
“ ndiyo niko poa vipi ujaumia popote”.
“ Eeh”. Akazungumza na kuanza kulia kitendo kilichoumiza sana moyo wangu.
“ mpe jamaa simu”. Nikazungumza na akamkabidhi jamaa simu.
“ Kuna jambo moja mnaweza nifanyia, najua ninyi ni watu wenye akili nyingi kuhusu ujasusi, huyo binti ana kifaa mwili mwake naombeni mkitoe sasa hivi”.
“ Usijali tushamtoa zamani sana maana ilikuwa inaonyesha alipo na kidogo ilipukie kwenye mwili wake”. Jamaa akazungumza.
“ ohh shit”. Yule jamaa alonipa simu akazungumza na kwa haraka akaichukua na kutoa betri kisha laini na kuivunja vunja kisha kutupa chini vipande vipande vyake.
“ walikuwa wanahack simu watufatilie ndiyo maana jamaa alikuwa anaongea sana ili adukue simu”. Yule jamaa akazungumza na kunikazia macho kisha akawatizama wenzake.
“ mkipata hizo hela ni wakati sasa wa kuanzisha familia zenu,acheni pombe, acheni uhalifu kabisa na ishini kwa amani na familia zenu mimi nitarudi tanzania kwa jambo moja tu, kisasi changu lazima kitimie kwa don john, ishini kwa amani ndugu zangu sitokuwa na ninyi tena, nilioambana sana kupata pasipoti ila ilishindikana”. Jamaa akazungumza kwa sauti ya utulivu sana na kuwatizama wenzake ambao walionekana kusikitika, wakanyanyuka na kumfata kisha kuanza kumkumbatia mmoja mmoja.
“ Twende wote kaka huwezi muua mwenyewe”.
“ hapana lazima tumeua watu wengi sana huyu niachieni mimi”. Akazungumza
“ kaka huwezi tuacha hivi sisi ni ndugu”. Jamaa mmoja wapo akazungumza na wakaanza kuzungumza kiafrika kusini huku wakilia kwa uchungu na kukumbatiana, mpaka sasa sikujua don john alimfanya nini huyo jamaa.
Nikajikuta chuki dhidi ya nyamela huyo ikiongezeka nikawatizama jinsi wanavyolia kwa uchungu huku bastola ikiwa mezani kwa umakini sana nikaichukua na kuitia kiunoni huku nikiomba mungu wasiikumbuke kabisa, tylat aliniona kwa kitendo kile nilichokifanya nikatizama saa ya ukutani nakuona ni saa 10 za jioni na usiku wa leo ndiyo ilinipasa niondoke nchini humo na kuelekea tanzania,na huku tulikuwa mafichoni baada ya kufukuzwa kule tulipokuwa na wale jamaa wanaomtaka huyu binti.
“ kwa ninachokifanya kweli amidu na mage watakuwa salama”. Nikawaza huku nikitamani kumpereka tylat kwa wale watekaji
“ mmh hawawezi wauua lazima watakuwa salama”. Nikawaza
“ lazima nimuokoe kwanza diana wale hawawezi kufa “.
“ uuh nitawapataje sasa kama nikimrudisha huyu kwa wenzake”. Nikazidi kufikiria na kuhusu kuchanganyikiwa
“ kwa sasa lazima nifocus na jambo lilioko mbele yangu”. Nikazungumza na wale jamaa wakaleta nyama toka kwenye friji na chupa kadhaa za pombe
“ karibuni”. Wakazungumza na wakaanza kula nyama ile kubwa ambayo sikujua ata ni mnyama gani wakawa wanakula huku kila mmoja akiwa katika furaha na mara kadhaa wakitukana tukana matusi.
Wakapiga na pombe huku nikiwakazia macho hakuna aliyelewa hata mmoja inaonekana walikuwa nguli wa pombe watu waliobobea, masaa yakazidi kukimbia nikajikuta napitiwa na usingizi, kwenye sofa
******
KITU chenye ncha kali kikapita kwenye mgongo wangu na kufanya nitake kukurupuka ila nikazuiliwa.
“ Tulia una kifaa”. Sauti ya yule jamaa ikasikika na kufanya nikunje ndita kwani sikumbuki lini niliwekwa kifaa icho.
“ ichi ndiyo kilifanya wale jamaa wajue uko wapi na waje kutushambulia hauko makini”. Jamaa akazungumza na kukizim kisha kukikanyaga kilikuwa ni kama kadi ya kumbukumbu zile za kwenye simu.
“ hawako mbali huenda wako karibu yetu,”.
“ Muda umefika twendeni uwanja wa ndege”. Jamaa akazungumza na ghafla bovu la machozi na hewa chafu likatupwa ndani humo, hewa hiyo yenye gasi chafu ikaanza kutoka kwa wingi na kutufanya tuanze kukohaoa mithili ya mtu mwenye TB
“ oooh shiti wako wengi Ramsey”.
“ Wamezingira jumba zima”.
“ TUMEKWISHA”. Nikazungumza.

********************
Next episodes 47’48,49,50 The last chapter of SEE ME


ENJOY
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom