[20:20, 10/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 012
Wakati masimba akishuka eneo la Ngamia Pub, macho yake yalikuwa yakiangaza huku na kule kuangalia nani na nini walikuwa wakimtiza. Kila aliemuona alikuwa kwenye mambo yake, hakuna ambaye alikuwa akimtizama. Hilo halikumfanya ajiamini kabisa, bado akatembea akiangalia huku na huko. Hata pale macho yake yalipomuona mwanamke mrembo alieketi pembeni, bado masimba hakuvutika kumtizama. Macho yake yalikuwa yakitizama upande mwingine kabisa. Hakutazama huko kwa makusudi, bali alikuwa akimtizama mtu ambaye alikuwa akimfananisha. Alifanana kabisa na mpenzi wake, alifanana kabisa na teddy. Akahitaji kufanya kitu ambacho kingemuaminisha kwamba mtu yule alikuwa mpenzi wake. Kengele ya tahadhali ikagonga kichwani pale alipowaona watu watatu wengine wakimtizama. Tabasamu mubashara likachomoka usoni kwake, halikuwa tabasamu la kufurahi wala kuwavutia wasichana waliojazana pembeni. Hili lilikuwa tabasamu la kukubali kile ambacho alikiwaza. Kile ambacho alijua lazima kitendwe na yule mwanamke. Alitambua baada ya kuwasiliana na kumwambia sehemu ambayo wangekutana, ni lazima naye angeisambaza taarifa ile. Hilo aliliamini na hapa alikuwa akilithibitisha. Vichwa vitano vilivyokaa sehemu tofauti vilikuwa vikimtizama yeye. Vikimuangalia na hata kumshuti basi wangefanya hivyo. Akaendelea kusogea akimuangalia yule mtu anayefanana na mpenzi wake. Ni kweli alikuwa teddy, ni kweli alikuwa yeye! Kwa nini yeye? Kwa nini hapa muda huu? Yupo kwenye hili? Hilo likamshangaza tena na tena. Lakini kwakuwa alikuwa na watu wake eneo lile, alijua kila kitu kingewekwa wazi, ingawa hakupewa taarifa ya uwepo wa Teddy, hilo halikumsumbua kwa kuwa alimjua teddy. Aliutambua uwezo wake wakijasusi, alitambua uwezo wake wakujibadilisha. Hilo halikumfanya Awalaumu vijana wake.
Akaifikia meza ambayo ilikaa mwanamke yule. Hakusubiri kukaribishwa, bali alivuta kiti na kukaa.
"Bila shaka sikatazwi kukaa hapa!" Aliongea huku akimtupia mwanamke yule jicho. Bado akakutana na jicho lile lile la ulaghai, jicho ambalo bado liliendelea kumdanganya Masimba. Jicho la usingizi, jicho la kuvutia na hata kubadilisha mtazamo wa watoto wakiume.
Kabla hajajibu, akaliachia tabasamu, tabasamu ambalo liliendelea kuufanya uso wake ung'are na uzuri kuongezeka.
"Sio hapa tu, hata nyumbani, tena chumbani kabisa ungekaribishwa." Akajibu mwanamke yule akiendelea kutabasamu.
"Kumbe hata chumbani nakaribishwa, kwanini tumekuja hapa? Akauliza masimba huku macho yake yakiendelea kutembea usoni kwa mwanamke huyu. Kuna kitu alikuwa akikitafuta, lakini usoni kwa mwanamke huyu bado hapakuonekana kile ambacho alikuwa akikitafuta. Sura ya mwanamke huyu ilipambwa na uzuri wa haja, uzuri wa kuvutia na kuwavutia wengi.
"Nimekuita hapa ili tufahamiane, pia kuna mawili matatu nahitaji tuongee!" Baada ya maneno hayo, mwanamke yule akaonekana kuwa tofauti, safari hii hapakuwa na tabasamu wala mbwembwe. Uso wake ulikuwa uso wa kazi. Hilo likamfanya Masimba naye abadilike. Lakini ubadilikaji wake haukuwa ubadilikaji ule. Huu ulikuwa ubadilikaji wa kuiteka akili ya mwanamke yule. Wakatizamana kwa muda kila mmoja akitafuta kilichopo ndani ya mwenzake.
"Naitwa Mwamvita Rajabu, ni ndugu wa binti alieuawa juzi usiku. Nimekuja hapa jijini leo asubuhi kufuatilia kile ambacho kimesababisha kifo cha ndugu yangu." Aliongea mwanamke yule huku akiendelea kuivaa sura ya Huzuni. Licha ya sura hiyo lakini kwa Masimba bado sura ile haikuwa katika huzuni hiyo, bali ilikuwa katika huzuni ya kulazimishwa.
'"Wewe ni Polisi, afisa usalama ama? Na kwa nini umeniona mimi pekee ndiye wakuongea nawe? Sasa aliuliza masimba safari hii ikiwa makini kumuangalia mwanamke yule usoni. Bado sura yake iliendelea kuwa na huzuni, lakini kitu kingine mwanamke yule alikuwa kimya akionyesha kupatwa na huzuni zaidi. Kwa jasusi aina ya masimba hakuwa mgeni wa mbinu zile, hakuwa mgeni kwa kuwa alijua mwanamke yule hakuwa na jibu kwa wakati ule. Ukimya wake haukusababishwa na huzuni bali swali aliloulizwa halikuwa na majibu. Safari hii mwanamke yule akainua uso wake na kumwangalia masimba. Hata macho yao yalipokutana, safari hii Masimba alikiona kile ambacho alikuwa akikitafuta. Macho yao yalikuwa yakielezana kwamba wote ni watu katika fani moja. Wote walikuwa majasusi wa kiwango cha hali ya juu.
"Nadhani umenitambua sasa, nadhani ulichokuwa unakitafuta umekiona." Akaongea mwanamke yule akiendelea kumuangalia masimba.
Tabasamu likachanua usoni, tabasamu ambalo lilifuatiwa na kicheko. Hakikuwa kicheko cha furaha, hiki kilikuwa kicheko cha ushindi. Ni rahisi kumuua adui unayemjua kuliko usiemjua. Kitendo cha mwanamke huyu kuongea kile alichokuwa anakitafuta kikampa kuamini kwamba hata huyu ni mmoja wao.
"Yeah! Nimekiona na nimepata majibu. Lakini bado hujaniambia wewe ni nani? Na umeniita hapa kutaka nikujue ama kuniambia ulichoniitia? Safari hii masimba aliongea kwa ukali huku macho yako ya kibadilika.
"Hupaswi kujua masimba, hupaswi kunijua. Lakini nakuomba uachane na hili ulilolianzisha. Hutafika popote masimba." Safari hii aliongea akichezesha midomo.
"Bahati mbaya aliekuelekeza kwangu amekosea. Kamwambia mimi huwa sitishwi na wala siogopagi. Sitaacha na sitarajii kuacha, lakini nadhani leo kuna kitu umesikia. Basi ile ni kazi yangu mimi." Alijibu masimba kwa kejeli. Alishajua adui zake washakuwa waoga, wameshaanza kumhofia. MASIMBA akasimama na kuanza kuondoka eneo lile. Alimuacha mwanamke yule akijisonya, akitamani kumlipua.. lakini haikuwa amri kwa siku hiyo.
[16:28, 13/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 013
Akamuangalia masimba alipokuwa akiondoka katika eneo lile, akatamani kuichomoa bastola yake ili ikiwezekana airuhusu risasi, lakini hakutaka kufanya hivyo kwa kuamini kuwa masimba hawezi kuwa pale peke yake. Akashuhudia akitembea na kupotelea katika upeo wake. Kuondoka kwa masimba kukampa nguvu ya kuamini kuwa masimba hakuwa mtu wa kutishwa. Aliamini hilo baada ya maneno yake. Akatamani kusimama kuwapa ishara watu wake ambao walikuwa katika maeneo tofauti. Lakini bado alisita akiamini kuna macho yapo mahali yakimtizama kwa kila alichokuwa akikitenda. Akajipa uvumilivu huku akishusha kinywaji kinywani. Masimba baada ya kuachana na mwanamke yule alitembea akitoka eneo la pub ile. Macho yake bado yalikuwa yakiangaza kuhakikisha kama kwelu mwanamke aliyekaa pembeni kabisa mwa Pub ile alikuwa Mpenzi wake. Lakini safari hii macho yake hayakumuona Teddy, hayakumuona mwanamke ambaye alidhani ni Mpenzi wake, bali yalimuona mtu mwingine, tena mwanamke harafu alikuwa amevaa mavazi kama yale yale aliokuwa amevaa Teddy. Hilo likampa tafsiri kwamba ulikuwa mchezo, ulikuwa mchezo ambao ulichezwa kwa kipindi kile. Ni kweli mwanzo alimuona Teddy, nikweli alikuwa na uhakika huo, lakini cha ajabu safari hii alikuwa akimuona mwanamke mwingine, mwenye sura nyingine, lakini alievaa mavazi yanayofanana na yale aliovaa Mpenzi wake. Lakini huyu hakuwa teddy! Mshangao kilikuwa kitu cha kwanza kutokea usoni kwake. Akaona ni wakati wakuondoka hapo kwa kuwa alikuwa akihitaji kwenda kuongea na Mama wa Marehemu Asteria, sambamba na dada yake. Akatoka akaelekea sehemu ambayo aliipaki gari yake. Alitembea macho yake yakiangalia kila kitu, hatua kadhaa kabla ya kufika kwenye maegesho ya magari akakiona kivuli, kivuli kuonyesha uwepo wa mtu karibu na alipoipaki gari yake. Kengele za hatari zikagonga kichwani kwake, hakujua kwa nini lakini alijikuta akiushusha mkono wake pale alipohifadhi bastola yake. Hakutaka kukiamini kile alichokiona. Akaendelea kutembea akikiangalia kile kivuli.. lakini kabla hajagundua chochote akausikia mlipuko mkubwa, mlipuko ambao ulisababisha hata yeye kutupwa pembeni kabisa na kuanguka mfano wa furushi. Gari yake na magari mengine yalikuwa yakiwaka moto kuonyesha kuwa alitegewa bomu kwenye gari yake. Eneo lote la mjimwema likawa katika taharuki, watu walikuwa wakikimbia huku na huko kila mmoja akipigania kuiokoa nafsi yake. Sehemu yote ikageuka vilio, iligeuka somalia kwa muda mfupi. Pale alipoangukia masimba ndio kwanza alikuwa akirudiwa na akili zake, alikuwa akifumbua macho huku akijaribu kuvuta kumbukumbu. Kumbukumbu ambayo haikuwezekana kurudi kutokana na mkanganyiko na vilio vya watu. Akatambaa na tumbo mpaka pembeni kidogo. Muda mfupi alikuwa akisimama huku akishuhudia gari yake ikiteketea, gari ambayo alipewa kama zawadi na mwanamke mmoja hivi baada ya kumfanyia kazi yake ipaswavyo.
Bado hakuamini kama amesalimika... akaituliza akili yake, alitaka kuirudisha kumbukumbu kabla ya mlipuko ule. Kivuli cha mtu kilikuwa kitu pekee alichokiona. Kivuli ambacho hakufanikiwa kumuona mhusika halisi wa kivuli kile. Kwa mara ya kwanza akashukuru. Ilikuwa ni lazima aondoke pale, ilikuwa ni lazima apotee hapo, akaipima nguvu katika mwili wake. Alipoiona inatosha akaanza kupiga hatua huku hisia kuwa teddy alikuwa mmoja kati ya wapangaji washambulie lile. Akatembea akijichanganya na watu waliokuwa wakipita katika eneo hilo wakikimbia. Naye alikuwa akikimbia sambamba nao, ni wakati akikimbia ndipo alipomuona tena Teddy akitokea upande ule ambao alikiona kivuli kabla ya mlipuko.. Hata yeye alikuwa akikimbia, hata yeye alionyesha kufadhaika, Alionyesha kutafuta kitu, hakuwa teddy yule kiburi, hakuwa teddy yule gaidi na mwenye usiri. Huyu alikuwa teddy aliechanganyikiwa. Hili likamvutia Masimba kulitizima. Lakini wakati hilo halijafika popote akaishuhudia gari ikisimama pale alipokuwa amesimama teddy. Gari iliposimama milango ikafunguliwa, teddy akaingia kisha gari kuwashwa. Kilikuwa kitendo kilichofanyika kwa sekunde mbili, kitendo ambacho kilimfanya masimba aduwae. Kitendo ambacho kilimpa picha na kumuaminisha kuwa teddy hakuwa Teddy yule walioanzana akiwa ndio kwanya yupo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi. Hakuwa Teddy Yule wa Ifakara, hakuwa Teddy yule mwenye kutangaza mapenzi ya kweli. Huyu sio teddy yule anayetoka Idara ya usalama wa Taifa, hakuwa teddy yule alietoka urusi katika mafunzo ya juu ya Ujasusi. Huyu alikuwa Teddy Muuaji, teddy msaliti. "NITAKUPATA TU" Ndio kauli pekee aliotamka wakati gari ile ikimpita kwa mwendo wa kasi.
*********
Palikuwa na ukimya wa ajabu, ukimya ambao kwa mbali ulikuwa ukiondolewa na mbwa waliokuwa wakibweka. Alikuwa hapo kwa minajili ya kuongea na dada wa marehemu Asteria. Alitembea kama kama kawaida akielekea mlangoni mwa nyumba ile. Muda wote macho yake yaliozoea giza yalikuwa yakiangaza huku na huko. Akaufikia mlango, akasimama kwa muda kisha akaanza kuangalia eneo lote, alipoona hakuna mtu wa kumtilia mashaka, akaugonda mlango kwa mara ya kwanza, hakujibiwa, kwa mara ya pili hapakuwa na majibu tena.. alipogonga kwa mara ya tatu, akasikia nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni, wakati akiusubiri mlango ufunguliwe akashangaa kumuona mtoto mdogo akilia kwa ndani. Hilo hakulitarajia, mkono wake ukashuka na kuichomoa bastola.. kabla hajaingia mlango ukafunguliwa kisha sura ya mtoto mdogo wa miaka kumi alietapakaa damu mwili mzima akatokea. Masimba hakutaka kuuliza, akamuweka mtoto pembeni kisha kuingia ndani, sebuleni akapokelewa na damu iliosambaa kila sehemu, huku miili ya watu wawili ikiwa imelala ikionyesha haina uhai. Masimba akaisogelea miili iliokuwa imelala katikati ya damu. Godfrey Maboba akiwa na mkewe Irene Charles walikuwa wamelala katikati ya dimbwi la damu wakiwa maiti. Walikuwa wamepigwa risasi vifuani mwao. Masimba akainama kwa uangalifu, akawaangalia marehemu. Bado walikuwa wa moto kuonyesha hawakuawa muda mfupi uliopita. Wakati ameinama hapi akakisikia kitu mfano wa chafya, kitu ambacho kilitokea dirishani. Aliujua mlio ule, aliujua haukuwa mlio mwingine bali wa bastola. Masimba akawahi kuchupa huku akisahau uwepo wa mtoto wa marehemu. Wakati anatua nyuma ya kiti pale sebuleni, akajikuta akitua sambamba na mwili wa Mtoto Yule ukiwa hauna Uhai....
MASIMBA AKAISHIWA NGUVU