FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,231
- 4,387
STORY: SIKU ZA GIZA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: +255621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA KWANZA
DARK DAYS
INTRO.
USIKU:
INASIKIKA SAUTI YENYE MSISIMKO MKALI NDANI YAKE IKIWA INANENA KWA HISIA.
“Uhalisia wa maisha haupo kwenye kuyatafuta maisha bali ukweli wa maisha upo kwenye kuyaishi maisha yenyewe. Sasa unayaishi vipi maisha kama haukufanikiwa kuyatafuta maisha? Ni swali ambalo hata mimi siyajui majibu yake.
Lakini maisha yako ni wajibu wa nani? Wewe? Aliye kuumba? Aliye kuzaa? Anayekupenda ama atakaye kupumzisha kaburini siku ambayo mwili wako utakuwa zawadi kwa wadudu waishio ardhini? Ukweli ni kwamba huenda hakuna binadamu ambaye anaweza kukupatia jibu la maswali kama haya, hapo ndipo unaingia mfumo halisi wa maisha.
Maisha ni nini? Kwanini tunaishi? Kuna umuhimu wa kuishi au tunaishi kwa sababu hatuna namna nyingine ya kufanya? Maswali mengi kuhusu maisha hata mimi yalinifanya kuwaza mengi kuhusu uhalali wangu wa kuwepo hapa duniani. Najua huenda utahisi nimechanganyikiwa kwa kuweza kujiuliza maswali kama haya, lakini kuna umuhimu gani wa kuwa hai kama haujui hata kuhusu maisha ambayo unayaishi wewe mwenyewe? Kwamba unasindikiza watu wengine? Kwangu ni hapana, naweza kukiri kwamba huenda nilizaliwa kwa bahati mbaya ila ninaishi kwa makusudi ndiyo maana nataka kujua kuhusu uhalali wa maisha yangu.
Dunia na maisha ni vitu ambavyo vinaenda sambamba ila sio kitu kimoja japo najua watu wengi huwa wanachanganya haya mambo wakihisi ni kitu kimoja. Dunia ni sehemu ambayo wewe na viumbe vyote vilivyothibitishwa kuwa hai na kutokuwa hai vinaishi ila maisha ni kile ambacho kinatokea kila siku kwa hao viumbe. Sasa hawa viumbe wanafanya nini kwenye dunia ya namna hii? Binadamu aliumbwa, akaletwa duniani, jukumu la muumba liliishia hapo japo aliwakumbusha jambo moja ambalo ni mhimu kuhusu dunia na maisha ya hao viumbe.
Aliwahakikishia kwamba kwanza ili viumbe viishi ni lazima kuwe na utaratibu na mwongozo ambao utawafanya wanadamu waweze kuishi kwa utaratibu maalumu na sio kila mtu kujiamulia mambo ambayo anataka kuyafanya yeye kama yeye. Huo ukawa mwanzo wa kuanzishwa kwa sheria na taratibu rasmi ambazo zimekuwa miongozo ya mwanadamu na namna ya kuyaishi maisha yake kwa karne na karne sasa tangu uwepo wa mwanadamu kuwahi kuandikwa.
Kupitia hilo dunia ikafanikiwa kupata kitu kinaitwa SHERIA, sheria zikatengenezwa kuweza kurahisisha namna ya watu kuishi hivyo tukapata UONGOZI. Uongozi haukuja tu hivi hivi, kukawa na namna sahihi ya kuweza kuwapata viongozi duniani ambayo ikatuletea janga la dunia linaitwa SIASA na hapa ndipo dunia ikaingia kwenye hatari kubwa ya kuleta mambo ambayo huenda mwanadamu hakutakiwa kuyafanya ama kuwa nayo kwenye maisha yake.
Ubepari ukawa sehemu sahihi ya kuzinadi siasa, kuhoji kwa watu kukasababisha kuletewa tatizo jipya ndani ya siasa wakaliita DEMOKRASIA, kitu ambacho kwenye uhalisia wa maisha hakipo bali ni wazo ambalo lilianzishwa kwa ajili ya kuweza kumuendesha binadamu na kuhakikisha anajihisi kuwa sehemu ya maamuzi ndani ya UTAWALA WA KISIASA. DEMOKRASIA ikayaleta mambo ambayo hayakutarajiwa, siasa ikitumika kama chombo cha kukamilishia yote hayo.
Zikazaliwa nguvu ambazo zikashika dola, watu hao wakasahau kama walipata nafasi kwa matakwa ya wananchi wa mahali husika. Watu wakaamua kujimilikisha mataifa na dola za sehemu mbalimbali, watu wakaanza kuandamana wakipinga yote ambayo yanatokea, watu wakagoma kuendelea kuwa sehemu za mataifa yao. Hofu ikatanda kupitia watu kuuawa, watu kupotezwa na wale ambao walikuwa na nguvu ndio wakawa sehemu sahihi ya kuweza kufanya maamuzi yale ambayo waliyataka wao.
Dunia ikaingia kwenye kiza kinene, dunia ikahadaiwa na uongo wa kwamba maamuzi yanapaswa kufanywa na watu wachache kwa sababu wengi wataleta mkanganyiko kwenye maamuzi. Dunia ikawa ya watu wachache na kila ambaye alionekana kuwa sehemu ya kuwapinga watu hao basi maisha yake hayakuwa marefu na hata kama yangekuwa marefu basi ni yale ya mateso. SIKU ZA GIZA zikajichanua kama maji ya barafu ambalo limepigwa na jua la mchana utosini, hata ile nuru ndogo ambayo ilikuwa imeanza kuchanua ikawa imepotea jumla.
Sasa kwanini MUNGU aliwaacha watu wake wateseke? Hilo ni swali ambalo hata mimi sina jibu lake lakini ukweli ni kwamba SIKU ZA GIZA hazikuwa njema, zilikuwa zinatisha sio tu kwa kuziona bali hata kwa kusimuliwa tu. Lakini je hizo siku zilidumu au zitadumu milele? DARK DAYS.
SINA HATIA
GEREZANI
“Baba Vivian!” ilisikika sauti moja ambayo ilikuwa inasikika vyema kutoka kwa mwanamke ambaye alikuwa anamuita mume wake.
“Naam mke wangu!”
“Leo sitaki kula chakula mwenyewe, nimekusubiri kwa muda mrefu mbona sikuoni mume wangu!”
“Hahaha mwanamke unapenda kudeka wewe utadhani kwenu ulizaliwa wa mwisho. Namalizia mazoezi ndani ya dakika tano mumeo atakuwa mezani kukulisha chakula mke wangu”
“Sawa baba, ufanye haraka nakusubiri kwa hamu kubwa huku” mke wa yule mwanaume ambaye hakuwa anaonekana bado maana alikuwa anajibu kutokea ndani, alirudi zake kwenye nyumba kubwa baada ya kuridhishwa na majibu ya mumewe.
Yule bwana alitumia muda wa dakika zake nne kuweza kukamilisha kile ambacho alikuwa anakifanya alicho kiita mazoezi kisha akabeba taulo dogo akiwa anajifuta futa usoni na kuanza kuelekea kwenye nyumba kubwa kutoka kwenye nyumba ndogo ambayo ilikuwa pembeni na ndiyo alikuwa akiitumia kama sehemu ya mazoezi. Alikuwa nyumbani kwake hivyo hakuwa na wasiwasi, mlango ulikuwa wazi hivyo akaingia bila hofu akiwa anaendelea kujifuta usoni huku akiwa na tabasamu la kwenda kumfurahisha mkewe. Alibaki ameganda kwanza kwani hakuwa anaamini kama macho yake yalikuwa sawa ama ni yeye mwenyewe tu alikuwa na mawenge yake. Alijifuta tena usoni kwa mara nyingine kabla ya kuangalia kile ambacho hakuamini kukiona kwa mara ya kwanza mbele yake.
Mbele ya macho yake alikuwa anauona mwili wa mke wake, mwanamke wa ndoto zake na mwanamke ambaye aliwahi kumpenda kuliko hata alivyo jipenda yeye. Afadhali kama angekuwa amejilaza, haikuwa hivyo kwani ule mwili ulilala ukiwa hauna uhai, ni damu tu ambayo bado ilikuwa inaendelea kutoka ambayo ilikuwa inazidi kutapakaa chini. Bado nafsi yake ilikuwa inagoma kukubaliana na ule ukweli ambao ulikuwa mbele yake, hakuamini kama mke wake anaweza kumuacha kirahisi namna ile hivyo akajifuta tena na kusogea ile sehemu.
Alipiga goti na kumgusa mkewe shingoni na puani, hakuwa na uhai mwanamke yule. Bado akiwa yupo kwenye simanzi ndipo akakumbuka kuhusu Vivian, bintie wa pekee, alinyanyuka na kutaka kuanza kuondoka ila alisita, alisita baada ya kutambua nyuma yake kulikuwa na mtu. Aligeuka kifua kikiwa kimevimba, kuvimba kwa kifua chake kulisababishwa na hasira ambayo alikuwa nayo ndani yake, alitamani kufanya mambo ya kutisha kwa muda ule ila hakuwa na ule uwezo wa kutekeleza yale yote kwani alikuwa akitazamana na bastola kutoka kwa mtu ambaye aliufunika uso wake vyema huku akiwa na miwani myeusi hivyo hakufanikiwa kuona hata rangi ya macho yake.
“Ndugu yangu kwanza naweza kusema mimi ni moja kati ya mashabiki zako wakubwa kwenye hii nchi, umekuwa mwanasheria nguli kwa miaka kadhaa, umeshinda kesi nyingi ndani na nje ya taifa hili hali ambayo imekufanya kuwa kipenzi cha kila mtu. Kila ambaye anaisoma sheria anatamani kuwa kama wewe, kila kijana ukimuuliza nani anakusukuma wewe kuweza kuipenda sheria basi jina la kwanza linakuja lako. Sio rahisi kwenye zama hizi mtu kuwa na nguvu ya msukumo mkubwa namna hiyo hususani kwa vijana ambao wana ujuaji mwingi ndani yao lakini wewe umeweza, sitaki kuwa mnafiki kwa hili una heshima yangu kubwa.
Lakini kama unavyo tambua kwenye ulimwengu wa kisasa, watu wa aina yako huwa wanaanza kuwa hatari pale ambapo wanaanza kuwafurahisha zaidi wananchi. Ukiegamia upande huo ambao wewe upo mwisho wa siku unajikuta unaanza kwenda kinyume na utaratibu ambao umewekwa na wakubwa na hii ndiyo sababu ambayo imenifanya mimi kuwepo hapa muda huu. Najua unatambua nini kinaendelea ila tangu mwanzo ulitakiwa kufikiria haya mambo kabla ya kuyatenda kwanza, wakati unapambana kuwafurahisha raia ambao huwa wanakushangilia kwenye mitandao, ulipaswa kujiwazia kwamba utafika wakati ambao mambo yanaweza kuwa magumu na utakuwa mwenyewe na hao ambao huwa unaona wanakushangilia na kukupatia kiburi hutawaona tena. Angalia sasa madhara yake ambayo umeyapata saivi hapa, mkeo amekufa na ni hatihati kumpata binti yako mpendwa kwa sababu ulipenda zaidi umaarufu kuliko misingi ambayo imewekwa na wakubwa” kauli ya kumzungumzia mtoto wake ilimkera na kumuumiza, aliukunja uso wake macho yakiwa yanazidi kuwa mekundu lakini bwana yule alimpatia ishara ya kutoongea kwakuwa hakuwa amemaliza kumpatia maelekezo ambayo alitakiwa kuyapata.
“Naweza kukuhakikishia binti yako bado ni mzima wa afya na yupo hai ila hayupo hapa maana ametolewa na watu wangu na hapa ndipo unaingia wewe. Tumemuua mke wako lakini lengo kubwa ni wewe, ulitakiwa kufa lakini kama ukifa kwa kuuawa kutakuwa na maneno mengi ambayo yanaweza kuanza kutuharibia kwenye mataifa mengine hivyo hatupo tayari kuweza kuingia huko. Maana yangu ni kwamba kuanzia muda huu unatakiwa wewe ndiye ujulikane kama ulimuua mkeo” yule bwana alimrushia ile bastola ambayo alikuwa ameishika kwa gloves zake na kumtaka mwanasheria aweze kuibeba.
“Hiyo ndiyo bastola ambayo imetumika kumuulia mkeo, natambua sio rahisi kwa wewe kuweza kuishika na kuweza kuifanyia kazi hasa ukiwa kwenye hali kama hiyo ila hauna namna nyingine ya kufanya kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuweza kumfanya mwanao kuwa salama, kama hautaweza kufanya hivyo utaletewa maiti ya mwanao ndani ya nusu saa ijayo ila huwezi kuruhusu hilo litokee kwani wote tunajua kwa jinsi unavyo mpenda yule mtoto. Kwahiyo jambo ambalo unatakiwa kulifanya ili mwanao aendelee kuwa hai ni wewe kuibeba hiyo silaha kisha muda mfupi baadae polisi watafika hapa kwa sababu wameshapewa taarifa ya hili tukio, watakukamata na wakienda kupima alama za vidole itaonekana wewe ndiye ambaye umehusika na mauaji ya mkeo hivyo hakuna ambaye atakuelewa kwa lolote ambalo utakuja kuliongea tena hapo baadae. Na jambo jingine ukipelekwa mahakamani unatakiwa kukubali kwa kila ambacho utatuhumiwa kujihusisha nacho. Hiyo ndiyo njia pekee ya wewe kumuokoa mwanao, najua una maswali mengi kuhusu mimi, nani kanituma hapa, haya mambo mlengo wake mkubwa ni upi! Kwa sasa sina muda wa kukujibu ila kuna siku utakuja kutambua kila ambacho kinaendelea mwanasheria. Mimi nakutakia utekelezaji mwema” ilikuwa kama hadithi ambayo haikuwa na ukweli ndani yake ila ndio ulikuwa ukweli wenyewe, hata yeye hakuwa anaamini kama kweli yale mambo yalikuwa yanatokea. Bado alikuwa amepigwa na bumbuwazi, akili yake ilisafiri kwenda na kurudi akijaribu kung’amua jambo ila hakuelewa kama ilikuwa ndoto ama kweli, kwake ile ilikuwa ni kama dharau ya hali ya juu kufanyiwa ule ushenzi na yule bwana hivyo aliinama na kuibeba ile bastola akajaribu kumpiga risasi bwana yule kwa nyuma ila alitambua hakukuwa na risasi ndani yake. Alipiga kelele kwa sauti kubwa hasa baada ya kugundua tayari alikuwa ameishika ile bastola, alirudi kwenye mwili wa mke wake akapiga goti na kuanza kulia kwa sauti kali ambayo ilikuwa na maumivu ndani yake. Akiwa anaendelea na zoezi lile, ilisikika milio ya gari za polisi nje ya nyumba yake, alikaa chini na kuanza kucheka kwa sauti kama mtu ambaye hakuwa sawa kiakili. Dunia haikuwa sehemu sahihi kwake, mwanasheria aliivaa kesi ya kuhusika na mauaji ya mkewe wa ndoa ambaye alimpenda kupita maelezo.
SIMULIZI HII IMEACHIWA RASMI NA KWA SASA UNAWEZA KUIPATA YOTE MWANZO MPAKA MWISHO KWA SHILINGI 5000 TU.
Lipia 5000 yako kwa hizi namba hapa chini uweze kuisoma yote mapema na haraka zaidi upate maandishi Bora sana kutoka kwa mwandishi wako FEBIANI BABUYA. 👇
0621567672 (HALOPESA).... WhatsApp
0745982347 (M-PESA)
0714581046 (TIGO-PESA)
0689440143 (AIRTEL MONEY)
36316279 (LIPA NAMBA (M-PESA) inapokea mitandao yote)