Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 007

Wakatizamana tena na tena. Masimba hakuwa mjinga katika kile ambacho kilikuwa kikitokea pale. Muda wote alimuangalia yule msichana akikitafuta kile ambacho kilifichwa upande wa pili. Alikitafuta kile ambacho kingempa picha huyu alikuwa nani. Macho pekee ya mwanadada yule hayakuweza kumpa jibu la kwamba huyu alikuwa nani. Jicho legevu kama mtu alieupoteza usingizi kwa muda mrefu halikuweza kumpa majibu alioyataka. Kwa jicho la mwanamke huyu hata jasusi ama mpelelezi wa kiwango cha aina yoyote asingeweza kuligundua hilo. Akakumbuka kuwa kulikuwa na watu wengine, watu ambao walikuwa wakimuandama kila hatua. Aliwatambua na kuwajua, alihitaji kuutafuta ukweli kutoka kwa hawa na yule mwanamke alievaa mavazi ya kutamanisha. Alitaka kujua kama kunakujuana, kutambuana na hata kufahamiana. Alitaka kuifanyakazi kwa kutumia akili zake. Macho yake yakatembea taratibu yakizibwa na gazeti. Muda wote alihitaji kupata ujumbe kutoka kwa wenzake wakimjulisha kuhusu huyu mwanamke. Lakini hilo halikuwezekana kwa wakati ule, si kuwezekana kwa kuwa hawawezi, la hasha! Hata vijana hawakuwa wamemjua huyu mwanamke. Akatulia na kutulia tena, punde konda akatangaza kituo kinachofuata. Akili yake ikachemka kwa haraka, kilikuwa kipimo sahihi cha kugundua kama yule mwanamke ni abiria ama alikuwa mmoja kati yao. Akainuka naye akijiandaa kushuka.. macho yake muda wote yalikuwa machoni kwa watu ambao waliambatana naye, kuambatana kwa maana ya kumfuatilia. Bado alikikosa kile ambacho alikuwa akikitafuta. Bado hakufanikiwa kugundua kama walikuwa wakifahamiana ama lah. Akatembea akisogea mlangoni. Alikuwa makini kwa kila hatua, mikono yake ilikuwa tayari kuifanya kazi kama ingebidi. Daladala ikasimama kituo cha kinondoni mkwajuni. Masimba akashuka akiwa pamoja na abiria wawili watatu. Baada ya kushuka hakutaka kuangalia nyuma. Alitembea akiingia hapq na kutokea pale. Safari yake Hiyo ikaishia Eneo la kinondoni studio. Licha ya kutambua kuwa alikuwa akifuatiliwa tokea pale magomeni, cha kushangaza hakuwaona tena watu wale. Alitumia mbinu zake zote lakini bado hakufanikiwa kugundua chochote. Akatembea sasa akiivuka barabara fulani katika mitaa ile ya kinondoni, wakati anakikaribia kituo fulani cha teksi, mara akaisikia sauti ya mtu ikimuita, sauti ambayo ilikuwa ngeni kwake. Akaipuuza kama hakuwa amesikia. Lakini kwa mara nyingine sauti ile ilikuwa ikimuita tena. Sasa alionekana mtu yule akimuita tena huku akimfuata kule alipokuwa akielekea. Ilikuwa sauti ya mwanamke, sauti ya mtu ambaye hakuwahi kumuona achilia mbali kuisikia sauti ile. Akajipa kazi ya kugeuka, ni kweli akageuka.. macho yake yakamuona mtu, mtu yule yule ambaye alipanda pale kwenye daladala, mtu yule yule ambaye alimuacha ndani ya daladala. Lakini sasa alikuwa akimuita tena kwa jina lake, jina ambalo halitumii sana. Hakuuficha mshangao, hakuuficha kwa mtu kama yeye kugundua. Amenijulia wapi? Kwa nini anifuate mpaka huku? Nini anakitaka kwangu? Alijiuliza maswali mengi huku akisimama kumsubiri mwanamke yule.

Mwanamke yule akatembea kwa mwendo ule ule wa kuogopa kuikanyaga ardhi. Bado masimba alikuwa akipata kukitafuta kile ambacho alikikosa kule alipotoka. Bado mwanamke yule hakuonyesha uhatari na vilevile hakuonyesha kama alikuwa ni mtu wa misukosuko. Wakakutana na kwa mara ya kwanza wakishikana mikono. Wakasalimiana wakiangaliana. Masimba alimuangalia machoni kwa muda mrefu akikitaka kile ambacho alikihisi. Lakini bado huyu hakuonyesha kama ni mmoja kati ya hao. Bado jicho lake legevu lilitengeneza urembo wa kumvutia mwanaume yoyote lijali. Akataka kusema kitu, lakini kabla hajafanya hivyo akausikia mlio wa simu yake. Akaichomoa kutoka mfukoni na kukutana na kiboksi cha Ujumbe mfupi wa maneno, kuonyesha kuna ujumbe umetumwa. Kidole kikashuka na kuruhusu ujumbe ule kufunguka.

"Ni mmoja wao kuwa makini." Ulisomeka ujumbe ule. Ujumbe uliomfanya atabasamu na kucheka. Kwa mara ya kwanza alikuwa amekutana na mtu ambaye amefanikiwa kuyarahai macho yake. "Ni Mmoja Kati yao" neno lile likajirudia kichwani. Akahamisha macho kwa mwanamke huyu. Bado akakutana na jicho legevu, jicho ambalo liliuficha uhalisia wa kikazi.

"Nadhani hatutaweza kuongea kwa sasa. Chukua mawasiliano yangu nitafute saa mbili usiku. Bila shaka unanifahamu sana hivyo na mimi nataka nikufahamu." Aliongea Masimba huku akitoa business card yake na kumkabidhi mwanamke yule, huku akiondoka katika eneo hilo.

*********

Alishuka na kuingia nyumbani kwake. Akili yake ilikuwa imevurugwa kutokana na mambo kuonekana kuharibika mapema sana. Kitendo cha kuingia kwa masimba katika sakata hili, hakikuwa kitu kizuri kwake na kwa wengine. Hakutakiwa masimba kuijua hii mipango. Lakini kuuawa kwa Asteria wakati akitaka kuonana na masimba kumeharibu kila kitu. Kifo cha Asteria ndicho kikichomuibua masimba. Kutoweka kwa simu ya marehemu na mazungumzo yale, alihisi masimba atakuwa amegundua kuwa yeye ni mshirika wa Mpango ule. Teddy alijikuta kichwa chake kikiwa kizito. Teddy alijikuta katika wakati ambao hakuwahi kuwa nao. Akaelekea chumbani kwao, akaongoza mpaka sehemu anapoweka bastola yake. Akafungua na kuichukua kisha kuishika mkononi. Aliitizama huku akiwaza. Alikuwa tayari kumuua Masimba iwapo atagundua kama anaijua siri yao. Alikuwa tayari kumuua mpenzi wake kwa sababu ya pesa. Akasimama akiiangalia bastola. Hapo akakumbuka penzi lao lilipoanzia. Alikumbuka mengi.. moyo ukakosa ujasiri. Muda ule ule akahisi mikono ikimshika kiunoni kisha sauti nzito ikasikika. "Usiogope Mpenzi Nakupenda Sana... ilikuwa sauti ya Masimba. Teddy hakutegemea, hata alipogeuka na macho yao kukutana.. Hakuweza tena kumuangalia MASIMBA..
 
Asante ibra. Jf raha kwa kweli.unaingia hadithi hii unatoka hadithi nyengine
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 008

Usiogope nakupenda sana mpenzi. Ilikuwa sauti ya masimba, sauti ambayo ilitokea nyuma yake.hakuwa amejiandaa na hilo, hakuwa amelitegemea lile la masimba kuwepo pale ndani. Hili likamnyong'onyeza. Akatamani kuongea kitu lakini maneno hayakutoka. Hakujua muda ambao masimba alifika nyumbani, hakutegemea uwepo wake hapo, na hata pale alipokumbuka kitendo alichokifanya, alichoka kwa kuwa alitambua kuwa masimba alikuwa amekishuhudia kitendo kile. Akaiona akili yake ikishindwa kumsaidia katika kulitatua hili ambalo lilikuwa mwisho wake. Hata pale mikono ya masimba ilipokuwa akipapasa kiuno chake, bado Teddy hakuweza kumjibu. Bado bastola yake ilikuwa mkononi, bado hasira zilionekana usoni, na hata dhamira ya mauaji ilijengeka kupitia macho yake. Hakuweza tena kumuangalia masimba, hakuweza tena kuuinua uso wake kumtizama. Alitazama pembeni na alikuwa ameinamia chini. Mwili ulikuwa unatetemeka, alijikuta kwenye wakati mgumu kupambana na moyo wake. Moyo uliojaa mapenZi juu ya masimba, moyo ambao haukuwahi kumpenda mwingine zaidi ya huyu mwanaume. Mwanaume ambaye alichukua asilimia mia moja katika moyo wake? Ni vipi ataweza kuitumia bastola kumlenga huyu mwanaume? Ni vipi angeweza kukiruhusu kidole chake kutekenya kitufe kuruhusu risasi imuue Masimba? Ni vipi pale atakapoiona Risasi ikimtupa masimba chini huku damu zikisambaa? Hapo akauona ugumu, ugumu wa kufanya kile ambacho alitaka kukifanya, lakini vilevile aliyafikiria mabilioni ya shilingi. Kwa mara nyingine akakiona kichwa chake kikitaka kupasuka. Lakini mpapaso wa mikono ya masimba ukamfanya teddy aachie mguno. Mpapaso ambao ulipanda mpaka kwenye kifua chake kilichobeba viazi vidogo. Mikono hiyo ikatulia hapo kwa muda ikitomasa na kuchezea kwa ustadi mkubwa. Hilo likaanza kumlegeza teddy, likamuacha teddy akisinzia na kulegea. Masimba akamgeuza na kufanya wote watazamane. Watazamane katika namna ya kuhitajiana. Jicho lilikuwa usingizini na hata midomo ikawa tayari kupokea zawadi. Wakatizamana zaidi, muda huu nguo zilikuwa zikitupwa chini baada ya kuvuliwa. Bastola ilianguka pasipo hata teddy kugundua. Alikuwa akihema kama mwizi, alikuwa akihema kama ametoka kukimbia mbio ndefu. Hakuwa teddy yule aliekuwa ameapa kumpoteza masimba. Hakuwa teddy yule mwenye uwezo wa kunyoosha mkono kumuua masimba. Huyu alikuwa kondoo, kondoo anayetii mamlaka ya bwana. Akasogezwa kitandani, hata yeye mwenyewe akasogea, akakalishwa kitandani, hata mwenyewe akakaa, na hata kulala, akalala huku macho yake yakiwa yamefumbwa na kufumbika. Midomo bado ilihitaji kupokea kitu, kitu ambacho kingeianzisha safari nyingine. Ilikuwa hivyo.

*****
Alishtuliwa na mlio wa simu yake, akaupeleka mkono pembeni yake ambapo alikuwa amelala masimba. Lakini akashangaa kutokuwepo kwake. Bado simu yake iliita, lakini aliendelea kuipuuza. Sasa alikuwa akiinuka kutoka pale kitandani na kuelekea kule sebuleni. Akalifunua pazia akidhani atakutana na masimba hapo, lakini hapakuwa na mtu. Hilo likamshangaza tena na tena. Haikuwa kawaida ya masimba kumuacha kitandani. Wakati akiendelea kuumizwa na hilo bado simu chumbani iliendelea kuita. Safari hii mpigaji alikuwa akipiga kwa mara ya tatu. Akakata shauri kurudi chumbani kwenda kuipokea simu hiyo. Akazivuta hatua zake taratibu akiwa mtupu kama alivyozaliwa.akasogea na kuingia chumbani huku mawazo yakiwa ni wapi alipoelekea masimba. Akaifikia simu na kuichukua, macho yakatua juu ya kioo.. akakutana na jina la mtu alieufanya moyo wake upige kwa haraka. Jimmy Lambert ndiye aliekuwa akiipiga simu. Akakipeleka kidole chake na kupokea simu.

"Jimmy." Aliita tedy kwa sauti ndogo yenye kuonyesha uchovu.

"Vipi umelala au?" Lilikuwa swali kutoka kwa Jimmy.

"Yeah! Nilikuwa nimelala, kuna lolote? Alijibu kisha kuuliza.

"Naomba Uje Tegeta muda mfupi ujao, kuna mtu nataka mkutane, mfahamiane na mtambuane. Tumeona tukutafutie mtu wa kusaidiana naye." Alijibu Jimmy kisha akakata simu bila kusubiri jibu kutoka kwa Teddy. Hilo la kutafutwa kwa mtu likaupa mashaka moyo wake. Ni kweli pesa alizitaka na kuzihitaji. Ni kweli anampenda masimba kuliko maelezo. Lakini hata kama atamuua masimba, wapo wanaume wengine ambao watamuoa. Kinachotakiwa ni kupanga njia ipi sahihi ya kumuua. Kwa mara nyingine roho yake, akili yake ilikuwa tayari tena kumuua masimba. Alikuwa amedhamilia na alikuwa ameamua kumpoteza. Alichokifanya ni kujiandaa kwa safari ya kuelekea huko tegeta huku akiwa na nguvu na maamuzi sahihi.

Wakati yeye akitoka na kulifunga geti, masimba alikuwa nyumba ya tatu kutoka pale. Alikuwa amesimama hapo kwa muda mrefu akitizama kila kitu ambacho kiliendelea pale. Muda mfupi akamuona mpenzi wake akilifunga geti na baada ya hapo akamuona akiondoka pale kwa kutembea kwa miguu. Bado alitulia akiendelea kuangalia kila kitu ambacho kilikuwa kikitendeka pale. Bado mpenzi wake aliendelea kutembea akielekea kituo cha daladala. Hilo pia lilimpa nafasi ya kumfuatilia pasipokuonekana. Simu ilikuwa sikioni akiwasiliana na vijana wake, alikuwa akiwaeleza kila kitu cha kufanya. Aliwaaachia wao kazi ya kumfuatilia Teddy. Alichokuwa akipokea ni maelezo ya nini kinaendelea katika hilo.

******
Teddy alitembea mpaka kituo cha daladala, alipofika hapo akatulia akiangaza macho yake huku na huko. Alikuwa ametulia kwa muda akitizama kila mienendo ya watu. Alikuwa na hisia za kufuatiliwa, lakini kila alipopitisha macho yake sehemu zote, hakuweza kumuona mtu ambaye labda angepata mashaka naye. Baada ya kuhakikisha hilo, akaingia kwenye daladala na muda mfupi gari likaondoka likielekea Tegeta. Ilikuwa safari ambayo kwake ilikuwa muhimu sana. Walikuwa na mzigo wa mamilioni ya shilingi lakini bado haikuwezekana kuuza kutokana na matukio haya yanayoendelea kutokea hakuwa tayari kuiacha pesa ile kwa sababu ya mwanaume. Moyoni alijisemea kwamba labda angekuwa mama yake ndipo angefanya hivyo. Wakati akiwaza hakujua kwamba kuna watu walikuwa siti ya nyuma yake wakimtizama. Walikuwa vijana wawili wadogo kiumri, vijana ambao kwa kuwaona ungedhani labda ni wanafunzi wa sekondary. Lakini haikuwa hivyo, hawa walikuwa vijana kutoka kitengo nyeti katika nchi hii. Walikuwa wakiendelea kuzungumza hili na lile, huku mara moja moja wakimtupia jicho mwanadada huyu. Kilikuwa kitu kizuri sana kumfuatilia mtu ambaye hajui kuwa anafuatiliwa. Gari ilipofika tegeta kwa ndevu vijana wale wakasimama tayari kwa kushuka. Hata teddy naye alikuwa akishuka hapo. Alitangulia yeye kushuka, kisha wakafuatia wao kushuka. Baada yakushuka vijana wale wakangoza kuelekea barabara fulani. Hata teddy alikuwa nyuma yao akifuata barabara ile. Hakujua kuwa waliombele yake hawakuwa mabishoo kama alivyodhania, bali walikuwa makachero wakifuatilia kila hatua yake na kila kitu anachokifanya.

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom