Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 004

Aliondoka kwa kupitia mlango wa nyumba ile. Kichwa chake kilishavurugwa kama sio kuvurugikiwa. Hakuamini kama tukio la kuuawa kwa mwanamke yule lingeyavumbua mambo makubwa kama yale tena kwa muda mfupi. Lakini ni nani waliomuua Rafiki huyu wa Teddy? Kwa nini wamuue? Au waliniona nikiondoka nyumbani wakaamua kunifuatilia? Kama walinifuatilia kwa nyuma ni vipi damu ilikuwa imeganda kuonyesha mauaji yalifanyika muda mrefu kidogo? Maswali hayo yakampa hamu ya kumchunguza mkewe, sio mkewe tu bali hata na Jimmy. Kwani aliondoka nyumbani akiwa peke yake, hakuona kitu chochote kilichompa wasiwasi kama alikuwa akifuatiliwa, sasa ilikuwaje kufika tu nyumbani kwa mtu aliekuwa akimuhitaji amkute ameuawa? Hilo likampa kile ambacho hakuwahi kukiwaza, tukio la coco beach lilibeba tukio zima la kuuawa kwa mwanamke huyu. Akatambua kuwa alitakiwa kuwa makini, alitambua kama atakwenda ndivyo sivyo basi anaweza asiimalize kazi hii. Alijua kama mkewe ni mshirika wa Jimmy na kama ni kweli ni yule aliemuona coco beach, basi alijua kuwa lazima atakuwa akitembea na macho ya watu kila mahali. Akairudia gari yake kwa kutokea uelekeo tofauti, baada ya kuikuta gari yake akawasha kitufe fulani cha kucheki usalama, aliporidhika muda mfupi alikuwa barabarani akielekea nyumbani kwake huku akiubeba utulivu wa Hali ya Juu. Hakutaka kumpa mashaka mpenzi wake, alitaka kumchunguza chini kwa chini. Muda mfupi alikuwa akiingiza gari ndani ya geti la nyumba yake. Akashuka na kurudi getini tena, baada ya kulifunga akaongoza kuingia ndani. Ile anaufungua mlango akapokewa na macho ya Teddy yakimtizama katika namna ya kuvutia. Yalikuwa macho malegevu, macho yanayohitaji kitu fulani. Masimba alilijua hilo, lakini hakutaka litendeke. Akapiga hatua mbili tatu mpaka aliposimama mwandani wake. Akamkumbatia kwa upendo wa hali ya juu. Walibaki wamesimama katika kumbatio lile, kumbatio ambalo lilidumu kwa muda wa dakika mbili. Kila mmoja akiliwaza lake. Punde walikuwa wakiachiana lakini huku wakiwa wanatizama.. kila mmoja alikuwa akimuangalia mwenzake kwa upendo. Lakini upendo ambao haukubeba maana nzima ya kutizamana kwao. Kwa mbali Masimba alikigundua kile ambacho kilifichika katika mtizamano ule. Kulikuwa na wasiwasi Machoni kwa mpenzi wake. Hakusubiri zaidi kumuangalia, aliushika mkono wake na kuelekea naye chumbani, hapo wakapokewa na kitanda, kitanda ambacho leo hili kilichelewa kuupumzisha mwili wa Masimba. Akaendelea kupiga hatua kuelekea pale kitandani. Alipofika alimlaza teddy kisha naye akayatoa mavazi yake kisha kujilaza kando ya Teddy. Wakauvuta usingizi kwa muda, usingizi ambao haukua rahisi kwa masimba. Sauti ya mwanamke alieuawa usiku wa juzi bado iliendelea kusikika masikioni mwake, bado hakujua kwa nini ilikuwa vile, bado hakujua wauaji walikuwa na lengo gani. Akapanga siku inayofuata kuelekea nyumbani kwa marehemu. Alitaka kwenda kupeleleza na kujua nini ambacho kipo nyuma. Alitaka kuujua ukweli juu ya kifo cha Asteria, alitaka kujua kuna uhusiano gani na Jimmy. Akaivuta shuka usoni, kisha kuutafuta usingizi.

*******

"Lazima Tumuue." Ilisikika sauti kutoka ndani ya chumba fulani. "Hawezi kucheza na sisi, hata hao waliomtuma tutawamaliza kabla ya jua la kesho kutwa." Aliendelea kuunguruma mwanaume yule. Alikuwa mwanaume wa makamo, mweusi na mwenyekitambi ambacho kilimfanya aonekane kama mkurugenzi au waziri katika wizara fulani. Ukimuondoa mwanaume huyo pembeni alikaa Jimmy na kushoto kwake alikaa mwanaume mwingine ambaye muda wote alikuwa kimya. Kilikuwa kikao ambacho hakikuwa rasmi. Kikaa ambacho kiliitishwa na watu watatu baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa vijana wao wawili. Hilo liliwapa mashaka makubwa sana, mashaka ambayo hapo mwanzo hawakuwa nayo. Ukweli waliujua na walimjua muuaji. Licha ya kumjua muuaji lakini hawakuwaza kama lingefika huko. Hawakujua kama Masimba angeanza kwa kuwatia Hasara, hawakujua kama wangewapoteza watu wao ambao walikuwa ni msaada mkubwa kwao, kwa mara ya kwanza wakajikuta wakikijutia kitendo cha kumuua Asteria Mbele ya Masimba. Walijua kitendo hicho ndicho kilichosababisha yote ambayo yalitokea usiku wa jana. Kila mmoja akatulia akihitaji kuipa utulivu akili yake ili kupata majibu sahihi juu ya kudili na mtu huyu ambaye ameonekana kuwa kikwazo kwao. Hakuna ambaye aliinua mdomo ama kuufumbua kuzungumza na mtu mwingine. Walinyamaza kumsubiri mtu ambaye ndie mtu wa mipango, walikuwa wakimsubiri Teddy Kupata majibu ya kipi ambacho kilitokea na kipi ambacho kifanyike. Kila mmoja NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 003

********

Namba ya Mwisho kumpigia marehemu ilikuwa namba ya Mpenzi wake. Hilo likamsisimua mwili wake, ile hisia kwamba mpenzi wake ndiye aliemuona kule coco beach sasa ilikuwa imeupata ushahidi wake. Lakini bado kichwa chake kilikuwa kizito kupindukia kuamini kwamba Teddy ni Mhusika katika tukio la kuuawa kwa mwanamke yule. Hilo halikumpa mashaka zaidi lakini alijiuliza ni vipi ameweza kufanya hilo wakati alikuwa naye ndani kwa kipindi chote. Ni katika kuyawaza hayo ndipo akaikumbuka siku iliopita pale alipoagwa na Teddy kuwa anakwenda kwao na hatarudi kwa siku hiyo. Kulikumbuka hilo kulizidi kuusisimua Mwili wake. Alitanbua kuna kila dalili za mpenzi wake kuhusika na kifo cha mwanamke yule. Lakini alijiuliza sababu za kumuua mwanamke mbele yake kulikuwa na maana gani kwake? Walikuwa wakimpa ujumbe gani kwake. Hapo akaipata hamu ya kuendelea kuichunguza simu ya marehemu Asteria. Jina la pili kukutana nalo ni la Mtu ambaye aliambiwa amchunguze. Lilikuwa jina la Jimmy Lambert. Alikuwa mmoja kati ya watu waliowasiliana na Asteria Muda Mfupi kabla ya kifo chake. Kila alichokuwa akikiona kilikuwa kama ndoto asioiamini. Kwa nini jina la Teddy kisha Jimmy? Teddy yupo wapi katika hili? Ana husika vipi katika kifo cha mwanamke huyu? Yalikuwa maswali mazito sana, maswali ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati ule. Hakuwa na jibu kwa wakati ule lakini ilikuwa lazima kulitafuta jibu kabla hakujapambazuka. Aliinuka na kuvirudisha vitu vyake sehemu yake, alipohakikisha kila kitu kipo sawa akaanza kutembea kuelekea nje ya nyumba yake. Hakupata hamu ya kulala kwa wakati ule. Uhusiano wa kifo cha mwanamke yule na urafiki wa Jimmy na Teddy kilikuwa kitu kilichomtia shaka na kuvuruga kichwa chake. Safari hii hakutaka kutumia usafiri wa kukodi, aliamua kutumia gari yake mwenyewe. Alikuwa amekata shauri ya kuelekea magomeni Mikumi nyumbani kwa rafiki wa mpenzi wake. Alitambua huko anaweza akaupata Ukweli kuhusu mauaji ya Binti yule na Uhusiano uliokuwepo kati ya Jimmy na Teddy. Kwa kuwa barabara haikuwa na magari, hapakuwa na ugumu wowote. Aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida huku akiwa makini kuangalia kama alikuwa akifuatiliwa. Lakini hapakuwa na kitu chochote kilichomtia wasiwasi. Baada ya muda alikuwa akiegesha gari umbali mfupi kutoka iliponyumba ananyoishi Rafiki wa mpenzi wake. Ilikuwa nyumba kubwa ya vyumba sita, sebule, choo sambamba na jiko. Hakuwa akiishi na mtu kutoka na mumewe kutokuwepo hapa nchini. Masimba alishuka na kuufunga mlango wa gari kisha akaongoza kuelekea getini kwa nyumba ile. Giza lilikuwa limechukua sehemu kubwa huku ukimya nao ukitawala kuonyesha kwamba watu wengi walikuwa wameshalala. Alitembea taratibu huku akiwa makini na kila kitu, alipolifikia geti akataka kuligonga lakini akagundua kuwa lilikuwa wazi. Hilo likamstaabisha, tokea amfahamu mwanamke huyu hakuwahi kumuona ama kukuta geti hili likiwa wazi. Kitendo cha leo kilimstaabisha sana. Akakata shauri aingie pasipokuligonga geti. Akalisukuma taratibu na kuzama ndani. Hapo pia akashangazwa kwa ukimya ambao aliukuta ndani. Taa zote zilikuwa zikiwaka, mlango wazi lakini hakukuwa na sauti yoyote kuashiria kama kulikuwa na mtu ama lah. Hilo likampa machale, akajivuta zaidi kuufuata mlango.. akaukuta ni kweli ulikuwa uko wazi. Akaingia na kusogea ndani, bado alipokewa na ukimya. Ukimya ambao hakuwahi kukutana nao katika jumba lile. Ukimya uliomfanya aichomoe bastola yake na kuishikilia mkononi. Akatembea kwa makini huku macho yake yakicheza pande zote. Bado hakuiona dalili ya kuwepo kwa mtu. Akaendelea kutembea huku umakini ukiongezeka. Akatokea sebuleni, kutokea sebuleni tu akahisi mwili ukisisimka.. sebule ilikuwa ilikuwa imevurugwa na vitu kutupwa huku na huko..

Akaikamata bastola yake vizuri kisha akaanza kusogea mbele zaidi na zaidi. Hatua saba mbele akaiona michirizi ya damu. Umakini ukaongezeka zaidi na Zaidi. Akatembea mdomo wa bastola ukitangulia. Alikuwa akitembea kuifuata michirizi ile ya damu. Alikuwa amejiweka tayari kwa kila kitu. Akaendelea kuifuatilia michirizi ile nyuma nyuma, mbele kidogo Akaiona ikiwa imeishia mlangoni mwa chumba fulani mle ndani. Hapo akasimama kwanza, baada ya hapo akausukuma mlango kisha kujitoma ndani. Hapo akajikuta akitizamana na Mwili wa Rafiki Wa Teddy Ukiwa umelala chini huku damu zikionekana kutuama. Akatembea mpaka pale ulipo mwili wa dada yule. Hakuonekana kuwa na uhai, hakuonekana kama alikuwa hai. Masimba akautazama mwili wa mwanadada yule kwa muda wa kama sekunde tano bila kufanya lolote. Kichwa chake kilikuwa kimevurugika, asteria, na sasa alikuwa ameuawa mwanamke huyu. Kipi kipo nyuma katika mauaji haya? Bado alitaka kujua kiundani zaidi, wakati akiwa bado ameduwaa asijue nini anatakiwa kufanya, akaisikia miguu ya watu ikitembea kisha minong'ono ikafuatia. Akatulia tuli huku mdomo wa bastola akiuelekeza mlangoni. Bado hatua za miguu na minong'ono ikaendelea kusikika, Sasa zilikuwa sasa hatua zile zilikuwa zikiukaribia mlango ule, punde akakiona kitasa kikitikiswa, wakati huo huo mlango ukasukumwa.. hakusubiri chochote kitokee, hakusubiri chochote kivuruge plani yake, mlio mdogo mfano wa chafya ukasikika, bastola ikakohoa mara mbili.. Hapakuwa na kelele. Ilikuwa miguno tu, miguno ilioambatana na kutambarajika kwa watu. Masimba akaurudia umakini wake, akatembea mpaka pale ilipolala ile miili ya watu wale wawili, akainama na kuigeuza miili. Zilikuwa sura ngeni machoni, hakuwahi kuwaona popote watu hawa. Alichokifanya nikuwapekua watu wale nakuchukua kila alichokiona kinafaa, kisha akatoweka eneo lile kwa kupitia mlango wa nyuma wa nyumba Ile. alikuwa akiitizama saa yake. Muda ulikuwa muda ulikuwa ukienda bila kumuona Teddy, kila mmoja akashangazwa na kitu kile, kila mmoja lishangazwa na kuchelewa kufika kwa Teddy, mmoja akaona aipige namba yake japo kumuuliza. Lakini kinyume chake namba haikuwa inapatikana. Hilo likawashangaza wote, liliwashangaza kwa kuwa taarifa alikuwa nayo na aliahidi kufika hapo katika muda husika. Lakini muda huu alikuwa hapatikani kabisa. Kila mmoja akasonya, akasonya huku akitukana matusi ya nguoni.

*****
Wakati akisubiriwa kule na watu wake, teddy alionekana akiingia katika maeneo ya nyumba ya rafiki yake. Ni ile nyumba ya rafiki yake alieuawa jana.aliukuta umati wa watu umezunguka eneo lote huku polisi wakiwa wamezungusha utepe kuonyesha kuwa hapakutakiwa mtu kupita hapo. Alipenya katikati ya watu mpaka karibu kabisa na waliposimama askari wa usalama. Akawasogelea kisha kuongea nao mawili matatu, wakaonekana askari wale wakimruhusu kupita kuingia ndani ya nyumba ya Rafiki yake. Alitembea bila kuonyesha wasiwasi wowote mpaka sebuleni ambapo aliwakuta wataalam wa picha wakiendelea kupiga picha mbali mbali, pia walikuwepo wanausalama kadhaa wakitizama hiki na kile, akawapita na kuelekea kule ambapo ilielekea michirizi ya damu. Akatembea akiangalia hiki na kile. Hatua tano akamuona mtu ameinama akiichunguza miili ya watu wawili ambao walikuwa wamelala katikati ya damu. Alimtambua mtu huyo na alimjua. Alikuwa mpenzi wake. Alikuwa masimba akiitizama miili ya wanaume wawili aliowauaa Jana. Akataka kusimama lakini alijikuta akiendelea kutembea baada ya masimba kugeuka na macho yao kukutana.
 
Stori nzuri lakini weka mpangilio mzuri wa aya ili kutomchosha msomaji.
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 005

Alitaka kusimama asiendelee na safari yakuelekea pale alipochuchumaa Masimba. Kitendo cha kumkuta mpenzi wake kulimpa picha mbili tofauti. Picha ambazo hazikuonyesha kumfurahisha yeye. Hata masimba alipogeuka na macho yao kukutana, bado alitembea na bado alikuwa akimuangalia kwa mashaka. Hata masimba alikitambua kitendo kile, lakini hakutaka kumshtua, hakutaka kumuonyesha kama anajua kitu. Baada ya Teddy kusogea pale, kwa mara ya pili masimba akainua uso na macho yake kumtizama Teddy. Alimuangalia kwa muda kisha kurudisha macho yake kwenye mwili wa Marehemu, alimuona jinsi alivyolala uso wake ukiwa umekunjamana kutokana na maumivu ambayo aliyapata wakati anauawa. Kila alipokuwa akimuangalia marehemu ndipo hasira juu ya mpenzi wake ziliongezeka. Alitambua kuuawa kwa mwanamke huyu ilikuwa ni kuzibwa mdomo juu ya kitu fulani ambacho hata yeye alihisi kuwa labda utakuwa ule mzigo. Kwa mara nyingine akajiapiza kuyafikia makazi ya Jimmy Lambert. Matundu mawili ya risasi kifuani na mawili shingoni ikikuwa ni kithibisho kuwa marehemu huyu hakutakiwa kuachwa hai. Baada ya kuridhika na kile alichokifanya pale akainuka, akaongea mawili matatu na mpenzi wake, alipomuacha hapo akaongea na wana usalama kisha akaondoka maeneo yale kuelekea nyumbani kwa Marehemu Esteria. Kwa kuwa hapakuwa mbali na eneo ambalo alikuwepo, masimba hakuona tatizo kutembea kwa miguu.. alitembea huku sura ya wasiwasi ilionyesha mpenzi wake ikijirudia. Hakuwa na wasiwasi pale alipotembea hapa na kutokea pale. Hakuwa na mashaka kuwa anafuatiliwa kwa kuwa walikuwepo vijana ambao walikuwa wakimfuatilia kwa nyuma kuangalia nani ambaye alikuwa nyuma yake. Bado alitambua mkewe alikuwa nyuma ya matukio haya, alijua Teddy alikuwa katika hili. Hilo lilimpa matumaini ya kugundua kuhusu mzigo uliokamatwa, na hata kuugundua ukweli mwingine ambao umefichwa kwa njia moja ama nyingine. Akaifikia nyumba ya marehemu Asteria. Askari walikuwa wengi wakilinda eneo lote. Kila mmoja alikuwa makini kwa kila hatua. Masimba akawafikia na kuongea nao mawili matatu, punde alikuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya nyumba ile iliojaa waombolezaji. Kila mtu alionekana ni mwenye uchungu sana. Kila mmoja alikuwa akilia kwa uchungu wa hali ya juu. Hilo likampa Masimba wakati mgumu. Wakati wakupata maelezo kutoka kwa ndugu wa marehemu Asteria. Alitembea macho yakitizama kila sura ya mtu aliekuwepo pale, siku zote alitambua kuwapo katika tukio lile na umati wa watu kiasi kile, ni njia moja wapo ya kuweza kumtambua ama kumshuku kwa macho, vile tu hisia zake zitakavyo. Kila sura ilionyesha majonzi, kila mmoja alionyesha kuumizwa na kifo cha Asteria. Hilo likamfanya masimba aikumbuke sauti ya msichana yule wakati alipokuwa akimuita. Hapo akahisi kitu kikimkaba kwenye koo. Kwa nini hakusimama kumsaidia binti huyu anayeonyesha kupendwa na watu? Alipewa kazi ya kuchunguza mzigo uliokamatwa, mzigo ambao haijulikani kama ni wote ambao umekamatwa. Lakini sasa alikuwa amebeba uchunguzi wa vifo vya watu wengine wawili. Vifo ambavyo vinaonyesha kuwepo na uhusiano wa kupotea kwa mzigo ambao alipewa kazi ya kuuchunguza. Alitembea kwa utulivu mpaka sehemu moja ambayo walikaa wakina mama wengi wakionyesha kumshika mama mmoja ambaye alionekana hajiwezi kwa kilio. Baada ya kufika hapo akaongea na dada mmoja ambaye alifanana sawia na marehemu Asteria.

"Wamemuua mdogo wangu, wamemuaa kwa sababu ya uaminifu wake kazini!" Alianza kuongea dada yule huku akiangua kilio.

"Najua una uchungu, najua unaumia, lakini hatuna lakufanya kwa kuwa limeshatokea. Naomba ufute machozi kwa kuwa niko hapa kwa kazi yakutaka kujua nani wapi nyuma ya kifo hiki. Futa machozi. Kisha nataka unijibu maswali kwa uchache. Aliongea masimba huku sasa akitoa kijitabu kidogo.

"Tunaweza kuanza mazungumzo.. nataka kujua kila kitu unachokijua wewe kuhusu marehemu.' Akaongea masimba huku akijiandaa.
Dada wa Asteria alimuangalia Masimba, kisha kwa sauti ya upole akaanza kumueleza.

"Asteria ni Mdogo wangu na mimi ndio msiri wake. Hakuwa akinificha chochote katika maisha yake. Wiki mbili zilizopita alinipigia simu akiniambia kwamba kuna kitu anataka kunieleza, lakini kitu chenyewe ni Cha hatari na hatuwezi kuzungumza kwenye simu. Baada ya kuniambia hivyo nilimshauri aje nyumbani anieleze kisha tuangalie hatua za kuchukua. Kweli Asteria alikuja siku ya pili yake usiku, tena akiwa katika mavazi ya ajabuajabu ambayo yalifunika mpaka uso wake. Ki ukweli aina ile ya mavazi na uingiaji wake ndani, ulinifanya nihisi kuwa kweli mdogo wangu alikuwa katika hatari. Basi sikutaka kumhoji kuhusu yale mavazi na hata uingiaji wake, nilimtaka aniambie tatizo lake. Ndipo hapo aliponieleza kuwa kuna watu matajiri wanataka wasaidiwe kuingiza madawa ya kulevya yenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Lakini sasa wanataka wawasaidie kuingizwa na kama yakifanikiwa Basi kila mmoja katika kitengo chao angepewa shilingi milioni mia tano. Na wenzake wotw wamekubali na anayesubiriwa ni yeye. Baada ya maelezo hayo nikamwambia wewe unaamua nini? Akasema yeye hayupo tayari, na aliongeza kuwa alitaka kukutana na mpelelezi aitwaye masimba amueleze hicho kitu kwa kuwa kulikuwa na mtu wake wa karibu anashirikiana na mtu anayeitwa Jimmy pamoja na viongozi wa serikali. Siku ambayo aliondoka hapa kumfuata Huyo mpelelezi, mdogo wangu hakurudi Tena akiwa hai. Amerudi akiwa marehemu." Alimaliza kuongea yule dada wa marehemu huku akiangua tena kilio.

Mishipa ya hasira na uchungu ilikuwa usoni kwa masimba. Kumbe marehemu alikuwa akimtafuta yeye, kumbe marehemu alikufa akitaka kuikabidhi siri mikononi mwake. Kwa nini hakusimama kumsikiliza. Masimba akatulia akifikiria kwa uchungu. TEDDY mpenzi wake alikuwa akihusika katika kifo cha Asteria. Akainuka akitaka kuondoka lakini akashikwa bega. Alipoinua kichwa alikutana na sura ya mama mzaZi Wa Asterina, akimuangalia kwa macho makali, macho ambayo hayakuonyesha woga. Wakaangaliana tena na tena.. Mama akataka kuongea kitu lakini sauti haikutoka.

*********

Walikaa kwa muda mrefu wakiisubiri simu kutoka kwa Teddy. Lakini bado simu yake haikuwa ikipatikana. Kila mmoja alikuwa akichanganywa na Ukimya ule. Lakini wakati wakiendelea kusubiri wakauona mlango ukifunguliwa. Teddy alikuwa akiingia akionekana hana tabasamu lake. Kila mmoja akabaki ameduwaa akimuangalia mwanadada huyu usoni.

"Kuna watu wawili wanatakiwa kufa". Akaongea Tedy kisha ukimya na hamaniko kutoka kwa watu wale likionekana. Kila mmoja alikuwa amekanganywa na maneno ya Teddy. Huna ambaye aliinua kinywa chake kuongea chochote. Mshangao bado uliwazubaisha. Wakiwa bado katika hilo teddy akaingeza.

"Hili Suala lipo mikononi mwa Idara ya Usalama wa Taifa. Vijana wanafanyakazi kubwa sana kutokana na vifo hivi. Masimba amelishikia bango hili suala na muda sio mrefu tunaweza kuumbuka." Teddy akaeleza mienendo yote ya masimba, mazungumzo yake na ndugu wa asteria. Na kuhusu watu wao waliouawa usiku wa kuamkia leo na kutoweka kwa Simu zao. "Sasa ni lazima mama wa Asteria na dada yake wauawe katika njia yoyote. Tukiwaachia hapa kisha wakakutana tena Na masimba kamwe hatutaweza kupona. Ni lazima wafe na ikibidi Hata Masimba Naye atawafuata...
 
sijui kwa nn wauaji wanakua na roho ngumu kuua kwao kama kuchinja kuku tu
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 006

Lazima tuwaondoe duniani, na ikibidi hata masimba atawafuata huko huko kuzimu. Hili suala bado gumu sana. Kukutana kwa masimba na wenzetu kule coco beach, kutoweka simu ya Marehemu Asteria pamoja na simu za vijana wetu, ni moja kati ya vitu hatari sana. Ninachoamini mimi Dada wa marehemu Asteria kuna kitu atakuwa anakijua kuhusu kifo cha mdogo wake, nilazima asteria alimpa siri kuhusu sisi. Kwa hiyo ilikujiweka katika mazingira sahihi nilazima tuwaondoe hawa watu. Nina amini hata masimba kuna kitu amekigundua kwangu, nadhani hata pale coco beach aliniona ndio maana hawakukaa sana. Sasa ni wajibu wetu kufanya kile ambacho kitatuweka salama zaidi. Kwani hata watu wa Idara ya Usalama Wa Taifa wamecharuka katika hili, nahawa ndio wanaompa nguvu huyu mwanaume, kwahiyo kwangu mimi nimemaliza na hii ndio mipango yangu." Aliongea Teddy kwa kirefu huku akiwaangalia wanaume wale wa tatu kwa zamu.

Kila mmoja alionekana yupo mbali kimawazo, kila mmoja alionekana akitafakari kuhusu jambo hili. Ukimya ukachukua nafasi katika eneo la chumba chote. Ni kweli hakikuwa kitu kidogo, lakini licha ua ukubwa wa kitu hiki hauwezi kuzuia mapambano. Mapambano sababu ya kupigania mamilioni yao ya Shilingi. Walikuwa tayari kumuua mtu yoyote kwa sababu ya pesa. Kila mmoja alikuwa akiutafakari ujumbe ulioletwa pale. Walihitajika kuawa watu wawili, na ikibidi watu watatu. Watu ambao watawafanya wao waishi kwa usalama zaidi. Watu ambao watakifanya kitendawili cha mzigo wao kubaki katika usiri nzito. Lakini watamuuaje masimba? Nani atainua bastola na kulenga kichwa ama kifua cha masimba? Hayo yalikuwa maswali ambayo yalikuwa yakipita vichwani mwao. Bado ukimya ulitawala na bado hapakuwa ni mtu wa kuzungumza. Kama Idara ya usalama imecharuka nini hatima yao katika hili. Walijua hapakuwa panahitajika nguvu, wakajua kutumia nguvu nikutafuta kushindwa katika hili pambano. Kila mmoja alitaka kuwa huru katika hilo. Kama simu za vijana wale zimetoweka, na simu zenyewe zilikuwa na mawasiliano walioyafanya na vijana hawa, nini ambacho kingewaponyesha.. hapo ndio walipouona Umuhimu wa kumuondoa Masimba kwanza kabla ya dada na mama wa Asteria. Kwa mara ya kwanza Jimmy aliamua kusimama kuzungumza kuhusu hilo. Kila mmoja alikuwa akimtizama akisubiria kusikia kile alichotaka kukizungumza.

******
Baada ya kumaliza kuongea na mama wa Asteria sambamba na dada yake, masimba akaona ni muda wa kuelekea nyumbani kwake huku akifikiria ni kipi ambacho atakifanya kuhusu mpenzi wake. Hakutaka kukurupuka katika hilo lakini kule kuambiwa na dada wa asteria kuhusu ukaribu wake na mmoja ya watu wenye mzigo huo, kulizidi kuitoa picha kuwa bado Teddy ni mhusika katika matukio yote ya mauaji. Ukianzia kuikuta mamba yake kuwa namba ya mwisho kuwasiliana na marehemu Asteria, kumuona coco beach usiku ule, kuonyesha wasiwasi alipomkuta akikagua miili ya watu wale mawili ni matukio ambayo yalimuaminisha na kuzifanya hisia zake kuwa sahihi. Licha ya kutembea pasipo na tahadhali, lakini bado alitanbua kuwa alikuwa na vijana wake wakimuangalia kila hatua. Alitambua umuhimu wa vijana wake. Wakati anataka kutokea kituo cha magomeni Hospital, akavutiwa na kitu fulani ambacho alikiona upande wa pili wa barabara. Licha ya kitu hicho pia hata simu yake ilipokea ujumbe kutoka kwa vijana wake. "Kuna vichwa viwili Vimeunda Urafiki nawe" ulisomeka ujumbe huo. Haikuwa kazi ngumu kuijua maana halisi ya ujumbe ule. Hata macho yake yalipoangaza katika maeneo yale ni kweli yakakutana watu wawili ambao walikuwa katikati ya umati wa watu ambao walikuwa wakisubiri usafiri wa kuelekea makwao. Ingawa watu hawa walijichanganya na abiria, lakini bado muonekano wao ulikuwa ni wakipekee, bado hawakuonekana kutulia hasa machoni mwao. Kila wakati walikuwa wakimwangalia Masimba kwa namna fulani ya kipekee. Aina ambayo haiwezi kufichika machoni kwa watu wenye fani ya ujasusi. Watu wale wawili, wakike na kiume bado walisimama wakionekana wakisubiri kitu, hata pale magari yaliposimama bado hawakupanda, bado hawakuonyesha kama walihitaji kupanda. Masimba akatabasamu kisha kupiga hatua akielekea pale waliposimama. Alitembea sawa na watu wengine waliokuwa wakiivuka barabara. Hata walipofika kituoni, gari ya kwanza kusimama masimba akapanda akiwaacha watu hawa wakihamanika. Lakini bahati nzuri konda aliwaona na kumuomba dereva asimame. Ni wakati watu wale wakipanda ndipo masimba alipoisikia miluzi na mayowe kutoka nje, watu waliokuwa wakishangilia kitu walichokiona. Akaruhusu macho yake yaelekee huko. Hapo hata yeye akashikwa na butwaa la muda, butwaa huku macho yakivutika kwa kile kinachopita nje.

Alikuwa akitembea kama twiga nyikani, alikuwa akitembea kama anaiogopa ardhi. Miguu ilitua kwenye ardhi kanakwamba haitaki. Alitembea akijitupa huku na huko. Kivazi chake kifupi kilikuwa kikiwavuta na kuwakata shingo wanaume kwa wanawake. Hata alipokuja kuingia kwenye daladala bado masimba alikuwa akimtizama, bado alikuwa akimuangalia twiga huyu, twiga alietoroka mbugani na kuja mitaani. Binti alikuwa haonyeshi kujali, haonyeshi aibu na kingine hakuonyesha kwamba labda angemuonea yoyote aibu. Ndio kwanza alikuwa akijipinda na Kujigeuza. Alikuwa akijishika hapa na kujiachia hapa. Hata pale alipokuwa akimtizama alihisi alikuwa akitizamana na Heaven Sent, ama alikuwa akiitizama picha yake. Alikuwa mzuri, alikuwa ameumbwa na alikuwa akivutia hata kutizamwa. Ni hapo binti yule alipotupa macho yake usoni kwa Masimba. Hata masimba alipomtupia jicho na hata macho yao kukutana, Kuna kitu kilionekana machoni kwa mwanamke yule. Kitu ambacho hakikuwa kigeni wala kipya machoni kwa Masimba.

WAKATIZAMANA ZAIDI NA ZAIDI..

KESHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom