Riwaya: Nitakupata tu

[20:20, 10/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 012

Wakati masimba akishuka eneo la Ngamia Pub, macho yake yalikuwa yakiangaza huku na kule kuangalia nani na nini walikuwa wakimtiza. Kila aliemuona alikuwa kwenye mambo yake, hakuna ambaye alikuwa akimtizama. Hilo halikumfanya ajiamini kabisa, bado akatembea akiangalia huku na huko. Hata pale macho yake yalipomuona mwanamke mrembo alieketi pembeni, bado masimba hakuvutika kumtizama. Macho yake yalikuwa yakitizama upande mwingine kabisa. Hakutazama huko kwa makusudi, bali alikuwa akimtizama mtu ambaye alikuwa akimfananisha. Alifanana kabisa na mpenzi wake, alifanana kabisa na teddy. Akahitaji kufanya kitu ambacho kingemuaminisha kwamba mtu yule alikuwa mpenzi wake. Kengele ya tahadhali ikagonga kichwani pale alipowaona watu watatu wengine wakimtizama. Tabasamu mubashara likachomoka usoni kwake, halikuwa tabasamu la kufurahi wala kuwavutia wasichana waliojazana pembeni. Hili lilikuwa tabasamu la kukubali kile ambacho alikiwaza. Kile ambacho alijua lazima kitendwe na yule mwanamke. Alitambua baada ya kuwasiliana na kumwambia sehemu ambayo wangekutana, ni lazima naye angeisambaza taarifa ile. Hilo aliliamini na hapa alikuwa akilithibitisha. Vichwa vitano vilivyokaa sehemu tofauti vilikuwa vikimtizama yeye. Vikimuangalia na hata kumshuti basi wangefanya hivyo. Akaendelea kusogea akimuangalia yule mtu anayefanana na mpenzi wake. Ni kweli alikuwa teddy, ni kweli alikuwa yeye! Kwa nini yeye? Kwa nini hapa muda huu? Yupo kwenye hili? Hilo likamshangaza tena na tena. Lakini kwakuwa alikuwa na watu wake eneo lile, alijua kila kitu kingewekwa wazi, ingawa hakupewa taarifa ya uwepo wa Teddy, hilo halikumsumbua kwa kuwa alimjua teddy. Aliutambua uwezo wake wakijasusi, alitambua uwezo wake wakujibadilisha. Hilo halikumfanya Awalaumu vijana wake.

Akaifikia meza ambayo ilikaa mwanamke yule. Hakusubiri kukaribishwa, bali alivuta kiti na kukaa.

"Bila shaka sikatazwi kukaa hapa!" Aliongea huku akimtupia mwanamke yule jicho. Bado akakutana na jicho lile lile la ulaghai, jicho ambalo bado liliendelea kumdanganya Masimba. Jicho la usingizi, jicho la kuvutia na hata kubadilisha mtazamo wa watoto wakiume.

Kabla hajajibu, akaliachia tabasamu, tabasamu ambalo liliendelea kuufanya uso wake ung'are na uzuri kuongezeka.

"Sio hapa tu, hata nyumbani, tena chumbani kabisa ungekaribishwa." Akajibu mwanamke yule akiendelea kutabasamu.

"Kumbe hata chumbani nakaribishwa, kwanini tumekuja hapa? Akauliza masimba huku macho yake yakiendelea kutembea usoni kwa mwanamke huyu. Kuna kitu alikuwa akikitafuta, lakini usoni kwa mwanamke huyu bado hapakuonekana kile ambacho alikuwa akikitafuta. Sura ya mwanamke huyu ilipambwa na uzuri wa haja, uzuri wa kuvutia na kuwavutia wengi.

"Nimekuita hapa ili tufahamiane, pia kuna mawili matatu nahitaji tuongee!" Baada ya maneno hayo, mwanamke yule akaonekana kuwa tofauti, safari hii hapakuwa na tabasamu wala mbwembwe. Uso wake ulikuwa uso wa kazi. Hilo likamfanya Masimba naye abadilike. Lakini ubadilikaji wake haukuwa ubadilikaji ule. Huu ulikuwa ubadilikaji wa kuiteka akili ya mwanamke yule. Wakatizamana kwa muda kila mmoja akitafuta kilichopo ndani ya mwenzake.

"Naitwa Mwamvita Rajabu, ni ndugu wa binti alieuawa juzi usiku. Nimekuja hapa jijini leo asubuhi kufuatilia kile ambacho kimesababisha kifo cha ndugu yangu." Aliongea mwanamke yule huku akiendelea kuivaa sura ya Huzuni. Licha ya sura hiyo lakini kwa Masimba bado sura ile haikuwa katika huzuni hiyo, bali ilikuwa katika huzuni ya kulazimishwa.

'"Wewe ni Polisi, afisa usalama ama? Na kwa nini umeniona mimi pekee ndiye wakuongea nawe? Sasa aliuliza masimba safari hii ikiwa makini kumuangalia mwanamke yule usoni. Bado sura yake iliendelea kuwa na huzuni, lakini kitu kingine mwanamke yule alikuwa kimya akionyesha kupatwa na huzuni zaidi. Kwa jasusi aina ya masimba hakuwa mgeni wa mbinu zile, hakuwa mgeni kwa kuwa alijua mwanamke yule hakuwa na jibu kwa wakati ule. Ukimya wake haukusababishwa na huzuni bali swali aliloulizwa halikuwa na majibu. Safari hii mwanamke yule akainua uso wake na kumwangalia masimba. Hata macho yao yalipokutana, safari hii Masimba alikiona kile ambacho alikuwa akikitafuta. Macho yao yalikuwa yakielezana kwamba wote ni watu katika fani moja. Wote walikuwa majasusi wa kiwango cha hali ya juu.

"Nadhani umenitambua sasa, nadhani ulichokuwa unakitafuta umekiona." Akaongea mwanamke yule akiendelea kumuangalia masimba.

Tabasamu likachanua usoni, tabasamu ambalo lilifuatiwa na kicheko. Hakikuwa kicheko cha furaha, hiki kilikuwa kicheko cha ushindi. Ni rahisi kumuua adui unayemjua kuliko usiemjua. Kitendo cha mwanamke huyu kuongea kile alichokuwa anakitafuta kikampa kuamini kwamba hata huyu ni mmoja wao.

"Yeah! Nimekiona na nimepata majibu. Lakini bado hujaniambia wewe ni nani? Na umeniita hapa kutaka nikujue ama kuniambia ulichoniitia? Safari hii masimba aliongea kwa ukali huku macho yako ya kibadilika.

"Hupaswi kujua masimba, hupaswi kunijua. Lakini nakuomba uachane na hili ulilolianzisha. Hutafika popote masimba." Safari hii aliongea akichezesha midomo.

"Bahati mbaya aliekuelekeza kwangu amekosea. Kamwambia mimi huwa sitishwi na wala siogopagi. Sitaacha na sitarajii kuacha, lakini nadhani leo kuna kitu umesikia. Basi ile ni kazi yangu mimi." Alijibu masimba kwa kejeli. Alishajua adui zake washakuwa waoga, wameshaanza kumhofia. MASIMBA akasimama na kuanza kuondoka eneo lile. Alimuacha mwanamke yule akijisonya, akitamani kumlipua.. lakini haikuwa amri kwa siku hiyo.
[16:28, 13/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 013

Akamuangalia masimba alipokuwa akiondoka katika eneo lile, akatamani kuichomoa bastola yake ili ikiwezekana airuhusu risasi, lakini hakutaka kufanya hivyo kwa kuamini kuwa masimba hawezi kuwa pale peke yake. Akashuhudia akitembea na kupotelea katika upeo wake. Kuondoka kwa masimba kukampa nguvu ya kuamini kuwa masimba hakuwa mtu wa kutishwa. Aliamini hilo baada ya maneno yake. Akatamani kusimama kuwapa ishara watu wake ambao walikuwa katika maeneo tofauti. Lakini bado alisita akiamini kuna macho yapo mahali yakimtizama kwa kila alichokuwa akikitenda. Akajipa uvumilivu huku akishusha kinywaji kinywani. Masimba baada ya kuachana na mwanamke yule alitembea akitoka eneo la pub ile. Macho yake bado yalikuwa yakiangaza kuhakikisha kama kwelu mwanamke aliyekaa pembeni kabisa mwa Pub ile alikuwa Mpenzi wake. Lakini safari hii macho yake hayakumuona Teddy, hayakumuona mwanamke ambaye alidhani ni Mpenzi wake, bali yalimuona mtu mwingine, tena mwanamke harafu alikuwa amevaa mavazi kama yale yale aliokuwa amevaa Teddy. Hilo likampa tafsiri kwamba ulikuwa mchezo, ulikuwa mchezo ambao ulichezwa kwa kipindi kile. Ni kweli mwanzo alimuona Teddy, nikweli alikuwa na uhakika huo, lakini cha ajabu safari hii alikuwa akimuona mwanamke mwingine, mwenye sura nyingine, lakini alievaa mavazi yanayofanana na yale aliovaa Mpenzi wake. Lakini huyu hakuwa teddy! Mshangao kilikuwa kitu cha kwanza kutokea usoni kwake. Akaona ni wakati wakuondoka hapo kwa kuwa alikuwa akihitaji kwenda kuongea na Mama wa Marehemu Asteria, sambamba na dada yake. Akatoka akaelekea sehemu ambayo aliipaki gari yake. Alitembea macho yake yakiangalia kila kitu, hatua kadhaa kabla ya kufika kwenye maegesho ya magari akakiona kivuli, kivuli kuonyesha uwepo wa mtu karibu na alipoipaki gari yake. Kengele za hatari zikagonga kichwani kwake, hakujua kwa nini lakini alijikuta akiushusha mkono wake pale alipohifadhi bastola yake. Hakutaka kukiamini kile alichokiona. Akaendelea kutembea akikiangalia kile kivuli.. lakini kabla hajagundua chochote akausikia mlipuko mkubwa, mlipuko ambao ulisababisha hata yeye kutupwa pembeni kabisa na kuanguka mfano wa furushi. Gari yake na magari mengine yalikuwa yakiwaka moto kuonyesha kuwa alitegewa bomu kwenye gari yake. Eneo lote la mjimwema likawa katika taharuki, watu walikuwa wakikimbia huku na huko kila mmoja akipigania kuiokoa nafsi yake. Sehemu yote ikageuka vilio, iligeuka somalia kwa muda mfupi. Pale alipoangukia masimba ndio kwanza alikuwa akirudiwa na akili zake, alikuwa akifumbua macho huku akijaribu kuvuta kumbukumbu. Kumbukumbu ambayo haikuwezekana kurudi kutokana na mkanganyiko na vilio vya watu. Akatambaa na tumbo mpaka pembeni kidogo. Muda mfupi alikuwa akisimama huku akishuhudia gari yake ikiteketea, gari ambayo alipewa kama zawadi na mwanamke mmoja hivi baada ya kumfanyia kazi yake ipaswavyo.

Bado hakuamini kama amesalimika... akaituliza akili yake, alitaka kuirudisha kumbukumbu kabla ya mlipuko ule. Kivuli cha mtu kilikuwa kitu pekee alichokiona. Kivuli ambacho hakufanikiwa kumuona mhusika halisi wa kivuli kile. Kwa mara ya kwanza akashukuru. Ilikuwa ni lazima aondoke pale, ilikuwa ni lazima apotee hapo, akaipima nguvu katika mwili wake. Alipoiona inatosha akaanza kupiga hatua huku hisia kuwa teddy alikuwa mmoja kati ya wapangaji washambulie lile. Akatembea akijichanganya na watu waliokuwa wakipita katika eneo hilo wakikimbia. Naye alikuwa akikimbia sambamba nao, ni wakati akikimbia ndipo alipomuona tena Teddy akitokea upande ule ambao alikiona kivuli kabla ya mlipuko.. Hata yeye alikuwa akikimbia, hata yeye alionyesha kufadhaika, Alionyesha kutafuta kitu, hakuwa teddy yule kiburi, hakuwa teddy yule gaidi na mwenye usiri. Huyu alikuwa teddy aliechanganyikiwa. Hili likamvutia Masimba kulitizima. Lakini wakati hilo halijafika popote akaishuhudia gari ikisimama pale alipokuwa amesimama teddy. Gari iliposimama milango ikafunguliwa, teddy akaingia kisha gari kuwashwa. Kilikuwa kitendo kilichofanyika kwa sekunde mbili, kitendo ambacho kilimfanya masimba aduwae. Kitendo ambacho kilimpa picha na kumuaminisha kuwa teddy hakuwa Teddy yule walioanzana akiwa ndio kwanya yupo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi. Hakuwa Teddy Yule wa Ifakara, hakuwa Teddy yule mwenye kutangaza mapenzi ya kweli. Huyu sio teddy yule anayetoka Idara ya usalama wa Taifa, hakuwa teddy yule alietoka urusi katika mafunzo ya juu ya Ujasusi. Huyu alikuwa Teddy Muuaji, teddy msaliti. "NITAKUPATA TU" Ndio kauli pekee aliotamka wakati gari ile ikimpita kwa mwendo wa kasi.

*********

Palikuwa na ukimya wa ajabu, ukimya ambao kwa mbali ulikuwa ukiondolewa na mbwa waliokuwa wakibweka. Alikuwa hapo kwa minajili ya kuongea na dada wa marehemu Asteria. Alitembea kama kama kawaida akielekea mlangoni mwa nyumba ile. Muda wote macho yake yaliozoea giza yalikuwa yakiangaza huku na huko. Akaufikia mlango, akasimama kwa muda kisha akaanza kuangalia eneo lote, alipoona hakuna mtu wa kumtilia mashaka, akaugonda mlango kwa mara ya kwanza, hakujibiwa, kwa mara ya pili hapakuwa na majibu tena.. alipogonga kwa mara ya tatu, akasikia nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni, wakati akiusubiri mlango ufunguliwe akashangaa kumuona mtoto mdogo akilia kwa ndani. Hilo hakulitarajia, mkono wake ukashuka na kuichomoa bastola.. kabla hajaingia mlango ukafunguliwa kisha sura ya mtoto mdogo wa miaka kumi alietapakaa damu mwili mzima akatokea. Masimba hakutaka kuuliza, akamuweka mtoto pembeni kisha kuingia ndani, sebuleni akapokelewa na damu iliosambaa kila sehemu, huku miili ya watu wawili ikiwa imelala ikionyesha haina uhai. Masimba akaisogelea miili iliokuwa imelala katikati ya damu. Godfrey Maboba akiwa na mkewe Irene Charles walikuwa wamelala katikati ya dimbwi la damu wakiwa maiti. Walikuwa wamepigwa risasi vifuani mwao. Masimba akainama kwa uangalifu, akawaangalia marehemu. Bado walikuwa wa moto kuonyesha hawakuawa muda mfupi uliopita. Wakati ameinama hapi akakisikia kitu mfano wa chafya, kitu ambacho kilitokea dirishani. Aliujua mlio ule, aliujua haukuwa mlio mwingine bali wa bastola. Masimba akawahi kuchupa huku akisahau uwepo wa mtoto wa marehemu. Wakati anatua nyuma ya kiti pale sebuleni, akajikuta akitua sambamba na mwili wa Mtoto Yule ukiwa hauna Uhai....

MASIMBA AKAISHIWA NGUVU
 
[11:50, 19/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 014

Alikuwa akiitizama maiti ya mtoto yule. Mwili wake ulikuwa na matundu mawili ya risasi maeneo ya kifuani. Alikuwa amelala huku damu zikishuka taratibu ba kuanza kuilowesha sakafu. Masimba akaduwaa kwa muda wa sekunde tano akishindwa kuamini kile anakitizama. Mtoto asiye na hatia alikuwa ameuawa kifo kibaya, kifo ambacho hakupaswa kuuawa hivyo. Hakuwahi kulia na hakuwa mtu wa kulia katika maisha yake, lakini mwili wa mtoto huyu ulimliza na kumuumiza. Macho yake yalikuwa yamemtazama yeye kana kwamba yalikuwa yakimuuliza. Yakimuuliza ni lipi kosa lake ambalo amelitenda mpakq kuuawa, alikuwa akimuukiza kwa nini alimuachia mpaka risasi zile zikapenya? Masimba chozi likadondoka, kiganja cha mkono kikayafunika macho ya mtoto yule. Ndio kwanza akakumbuka kuwa alikuwa mbele ya maiti watatu, mbele ya maiti ya Godfrey Maboba mkewe pamoja na mtoto wao. Mikoni ikawa inamtetemeka huku hasira juu ya watu wale zikipanda. Ni wakati akiendelea kuangalia hapo akashuhudia mlango ukipigwa teke kisha watu zaidi ya kumi wenye silaha nzito wakaingia. Walikuwa ni askari wa kikosi maalum (special forces) askari ambao walikuwa na mafunzo ya kupambana na watu wa aina yoyote. Bunduki zao zilikuwa mbele zikimtizama Masimba. Hawakuonekana kuwa na utani, hawakuonekana kuwa ni wenye masihara. Walionekana walikuwa tayari kufanya chochote. Amri ikatolewa ya kumtaka masimba kutupa silaha yake chini. Hilo masimba akalitii, alilitii huku akili yake akifanyakazi ya zaida. Alijua kikosi hiki kimekuja hapa kwa sababu ya kumuangamiza. Ulikuwa ni mpango ambao umepangwa makusudi kwa sababu ya kumkwamisha. Mpango ambao ulitengenezwa mahususi na mtu mzito katika serikali. Special forces hawawezi kuja sehemu kirahisi, special forces hawawezi kutumwa kwenda kumkamata mtu mmoja. Hata kama mtu mwenyewe ni yeye, special forces hutumika katika sehemu ngumu ambazo sio za kawaida. Sasa nani ambaye ametoa orders ya wao kuja hapa katika jumba hili? Kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, alitambua kuwa lazima ameuziwa kesi ya mauaji. Akaitupa bastola yake chini. Kiongozi wa kikosi kile ambaye alikuwa na cheo cha Luteni Kanali akasogea pale aliposimama masimba. Bado bunduki zilimtizama yeye, bado bunduki zilikuwa zikicheza na mikono yake na hata uelekeo wa macho yake. Kiongozi wa kikosi kile maalum akasogea. Akasogea tena na tena, sasa alikuwa akitizama uso kwa macho na masimba. Punde mkono wa kiongozi yule ukazama mfukoni na kuibuka na pingu. "Wanataka wanifunge pingu? Lilikuwa swali la kwanza kujiuliza. Lakini kabla hajakaa sawa akakisikia kitu kizito kikitua kisogoni. Akaliona giza likiingia machoni mwake, akataka kujizuia asianguke, lakini haikuwa hivyo, muda mfupi alikuwa yupo chini. Hakujua tena kilichoendelea.

*******

Alihisi maumivu makali kichwani hasa upande wa kisogoni. Maumivu makali sana ambayo yalikifanya kichwa chake kionekane kizito. Akataka kuuasogeza mkono wake aguse sehemu ile, lakini alijikuta akishindwa, hakushindwa kwa kuwa mikono haikuwa na nguvu, bali alishindwa kwa kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa pingu. Hilo likamfanya atulie kwanza kuiruhusu akili yake ifanye kazi. Akavuta kumbukumbu ya nini ambacho kimetokea kabla ya kufikishwa pale. Akajaribu kwa muda lakini hakuweza kwa wakati ule. Hakutaka kushindwa katika hilo, akaendelea kukumbuka, punde taswira ya picha ya mtoto mwenye matundu mawili ya risasi ukiwa umelala sakafuni, ikamjia usoni. Taswira ambayo ilimkumbusha mengi sana. Kifo cha Asteria, kifo cha mwamvua, kifo cha dada wa asteria, mumewe pamoja na mwanawe. Maiti za watu wote watano zilikuwa zikipita kichwani mwake. "TEDDY nitakupata tu. Risasi yangu kutoka kwenye bastola yangu lazima ikifumue kichwa chako. Aliwaza huku sauti ya marehemu Asteria Ikiendelea kujirudia. Hapo akakumbuka pale alipowaona Askari wa kikosi maalum wakiingia. Akakumbuka wakati akitizamana na yule Luteni Kanali. Kufikia hapi akakumbuka kila kitu. Akatambua kwa nini yuko pale. Kwa mara ya kwanza akafumbua macho, cha kwanza kukiona baada ya kufumbua ni uzuri wa chumba alichomo. Kilikuwa chumba kizuri sana, chumba chenye upana wa kutosha. Kilikuwa na dirisha kubwa la kioo, dirisha ambalo halikuwa linaonyesha nje. Akageuza shingo akiendelea kukichunguza chumba kile. Macho yake yakanasa kitu mfano wa flash kikiwa kimewekwa juu ya Dirisha. Hakikuwa kitu kigeni kwa mpelelezi kama yeye. Alitambua kuwa zilikuwa camera ambayo ilikuwa ikichukua picha kutoka mle chumbani na kurusha sehemu fulani katika jengo lile. Bado akaendelea kuangalia tena na tena kujua jengo aliyomo liko sehemu gani. Haikuchukua muda kugundua kuwa alikuwa katika chumba cha siri ndani Ya Makao Makuu Ya idara ya usalama wa taifa yaliyopo Kijitonyama. Kwa nini ameletwa hapa? Ina maana hata hawa wenzake wanaamini kwamba amefanya mauaji? Hilo likamchanganya, hilo likamfanya atamani kuonana na kiongozi wake. Lakini hata kama angeonana naye angemwambia nini wakati kazi hii alikuwa akiifanya kwa siri bila kuihusisha Idara? Hapo akauona ugumu, hapo akaiona hatari ya kushtakiwa na kupewa kesi ya mauaji. Akatulia akifikiria nini akifanye.

Dakika kumi baadae akauona mlango ukifunguliwa, kisha watu watatu wakaingia. Hawakuwa wageni kwake. Bali uingiaji wa watu hawa ulizidi kumtia hofu na kumtisha zaidi. Sekunde mbili alikuwa akiangalia na Mkurugenzi Wa idara ya usalama wa Taifa Kanali Godliving Kimaro pamoja na maafisa wawili wa ngazi za juu wa Polisi.

"Masimba Muuaji umezinduka? Lilikuwa swali kutoka kwa mzee yule ambaye hakuonyesha kutokuwa na utani. Masimba bado alikuwa ametulia, bado alikuwa akihisi yupo katika ndoto. Alishakuwa masimba muuaji, alishakuwa msaliti. Kama bosi wake mkuu naye anaamini ni Muuaji, nani ambaye atamuamini? Wakati akiwaza hilo sauti ya mkurugenzi Ikamzindua kutoka huko.

"Licha ya taifa kupoteza pesa nyingi kukusomesha katika mataifa mbalimbali, lakini leo umeamua kuisaliti nchi yako, umeamua kuisaliti nchi kwa sababu ya kuwatetea wauza madawa ya kulevya. Unaua watu kwa sababu ya kuahidiwa fedha? Umeitia aibu System nzima, umeitia aibu Idara hii. Mtu ambaye unategemewa kama wewe leo unafanya huu upuzi? Kuanzia leo idara inakufukuza kazi na utakabiliwa na kesu ya mauaji na pia utaishi katika kizuizi mpaka ukweli wa hili utakapo kuwa mwingine."

Yalikuwa maneno ambayo yaliusisimua mwili wa masimba, sio mwili tu bali hata moyo na roho yake. Alitambua jimmy Lambert na washirika wake walikuwa wamemuwahi. Walikuwa wamemuwahi na kummaliza kabisa. Macho yake ya kazi yakamtizama mzee kimaro usoni. Sasa walikuwa wakiangaliana kwa muda. Macho yao pekee ndio yalikuwa yakiongea. Masimba akamlazimisha mzee aendelee kumtizama. Wakatizamana tena na tena. Kisha Bila kuongea kitu mzee kimaro akabonyeza kitufe fulani mle ndani, sehemu nne zikafunguka kisha wakaonekana watu wanne wakiingia.

TUKUTANE KESHO
[11:51, 21/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 015

Walikuwa watu watatu, watu ambao hawakuonekana kuwa na masihara yoyote. Bado masimba hakuwa akiamini. Akili yake haikuwa ikikubaliana na kile kinachoendelea pale. Hakuamini kama idara aliyoifanyia kazi inaweza kuja kudanganyika kwa urahisi kiasi kile. Walikuwa wakimjua vizuri katika majukumu mazito yote aliyowahi kushiriki, alinusurika mara tatu katika matukio ya hatari. Lakini leo hii alikuwa amewekwa kizuizini. Tena akipewa kesi ya kuhusika na mauaji ya Godfrey Maboba na familia yake. Idara kubwa yenye wajuzi wa hali ya juu katika masuala ya ujasusi leo ilikuwa ikidanganywa na watu. Watu ambao wanaiharibu jamii ya Tanzania kwa kuuza madawa ya kulevya. Yalikuwa mawazo na fikra zilizozidi kuipandisha hasira. Akaziangalia pingu ambazo ziliifunga mikono yake. Alizitazama kwa muda bila kuongea kitu. Kwa mara nyingine akainua kichwa chake na kumuangalia Mkurugenzi Mr Godliving Kimaro. Aliyagandisha macho yake usoni na kutaka kuongea kitu. Lakini machozi yake yakashuka mashavuni pasipo kutarajia.. hilo halikutarajiwa na wote waliokuwepo pale, kwa mara ya kwanza toka amjue Masimba ndio alikuwa akilishuhudia chozi lake. Ndio alikuwa akimuona Masimba akilia. Bado macho yake yalikuwa usoni kwa Chief. Lakini haukupita muda mrefu watu wale wakamuinua juu na kuanza kumkokota kutoka ndani ya chumba kile. Bado macho yake yalikuwa kwa Chief, aliendelea kumuangalia mpaka alipotelewa kabisa ndani ya Chumba kile. Safari yao ikaishia kwenye gari moja ambayo ilikuwa imepaki nje. Kufika pale mlango ukafunguliwa kisha ishara ya kimtaka aingie ikifuatia. Bastola zilikuwa zikimtizama huku wanaume waliovalia suti nyeupe wakiwa makini naye. Hakubisha na hakutaka kufanya rabsha yoyote. Akatii na kuingia ndani ya gari. Aliwekwa katikati huku bado midomo ya bastola ilimtizama. Watu waliomuweka hawakujishughulisha naye, hawakuwa wakiongea chochote. Walikuwa watu wa kazi, watu ambao kukuondoa kwao ni suala la kawaida. Hawakuwa wao tu, ndani kulikuwa na watu wengine wanne ambao nao walikuwa ni mfano wa hawa watatu. Hapo bado akauona ugumu wa kulianzisha. Hakutaka kufanya mapema kiasi kwa kuogopa kuharibu mipango yake. Akaendelea kutulia, punde akamuona mmoja akiishika mikono yake, ufunguo ukapita, punde pingu zikajiachia. "Usione tunakufungua ukajaribu kuleta ujanja. Ukifanya hivyo risasi itakuwa halali kichwani kwako." Alinguruma mmoja kati ya watu wale. Masimba hakuwa amemsikia, mawazo yake hayakuwa pale, alikuwa akimuwaza Teddy, alikuwa akimuwaza mwanamke huyu, mwanamke ambaye alitokea kuchukua sehemu kubwa katika maisha yake. Alimpenda Teddy, alimuamuni na kumheshimu. Hakuwahi kuwaza kama itakuwepo siku teddy angekuwa mnyama. Hakuwahi kuwaza kama angeweza kuja kumgeuka. Hakuwa na mashaka juu ya kukamatwa kwake, alitambua kinachofanywa ni kushurutishwa ili ataje wapi alipoyapeleka madawa ambayo ameyachukua kwa Jimmy. Bado aliendelea kukaa kimya huku gari ikiendelea kutembea. Alikuwa tayari kumuua mtu yoyote. Bado sauti ya Asteria ilikuwa ikijirudia kichwani mwake. Asteria binti mzuri, binti ambaye amekufa akiuomba msaada kutoka kwake, hata pale alipoukimbuka mwili wa mtoto yule alihisi kuwa na deni kubwa. Alitaka kumtafuta mwamvita, alitamani kuonana naye kwa vyovyote. Lakini kwa muda ule haikuwezekana tena. Lakini alitamani na aliipenda staili ya mwanamke yule. Punde akasikia kitu kama mfano wa geti likifunguliwa. Sekunde kumi baadae gari ilikuwa ikisimama. Milango ikafunguliwa kisha Masimba akatakiwa ashuke. Akatii huku midomo ya bastola na mitutu kutoka kwa walinzi wa Jumba lile ikimsindikiza.

***********

Alikuwa amelala kitandani akiitizama picha ambayo walipiga na masimba mwanzoni mwa mahusiano yao. Ilikuwa picha ambayo ilimkumbushe mengi sana katika maisha yake. Ilikuwa siku ya kwanza kukutana kwao, ilikuwa siku ambayo Teddy alikuwa amepata pass maalum. Akaitizama picha ile kwa muda mrefu sana. Alikuwa akiuvuta muda kumsubiri masimba. Bado moyo wake ulikuwa ukipambana na mapenzi, bado moyo wake haukutaka umuache masimba. Ni kweli aliitaka pesa, ni kweli aliipenda pesa, lakini pesa hii haiwezi kusababisha akamuacha masimba. Akaiweka ile picha pembeni na kuchukua nyingine. Hii ni picha ambayo ndio ilikuwa na kumbukumbu mbaya na nzuri kwake. Ilikuwa picha iliopigwa nchini Urusi wakiwa sambamba na wapelelezi wa shirika la kijasusu la Nchi hiyo, FSB zamani likijulikana kama KGB. ni picha ambayo walikuwa katika oparesheni moja katika mji moja katika nchi ya Syria. Ni misheni hiyo ambayo kama sio umakini na uwezo wa masimba basi angerudi jina. Lilikuwa tukio baya kukumbukwa lakini ni Masimba huyu huyu aliejitolea kuhatarisha maisha yake sababu yake. Kumbukumbu ya tukio nzima ilikuwa ikijirudia. Ni wakati akiliwaza hilo ndio mawazo yake yalipopitea baada ya kuusikia mchakato wa viatu vya mtu. Akajiinua kitandani mkononi akiwa ameikamita bastola yake. Akatembea akihisi labda alikuwa masimba, lakini utofauti wa siku ile ndio ulimpa wasiwasi wa kuhisi labda mtu huyu hakuwa masimba. Siku zote alitambua masimba hakuwa akiingia kwa kupitia mlangoni. Akaendelea kutembea akielekea kwa nje. Hakupitia mlango wa kawaida bali aliamua kutumia mlango wa siri ambao huwa unatokea moja kwa moja mpaka nje. Macho yake yalikuwa yakipita na kuingia hapa na kutokea pale. Muda wote masikio yake yalikuwa yamesimama mithiri ya sungura akitaka kunasa hiki na kile. Dakika mbili alikuwa nje ya nyumba yao akiangaza huku na huko. Palikuwa na giza sambamba na miti ambayo iliizunguka nyumba yote na kutengeneza kivuli. Akatulia kwanza akiangaza macho yake huku na kule. Punde akamuona mtu akichupa kutoka kwenye mmoja kati ya miti ile na kutumbukia kwa ndani. Mwili ukamsisimka. Japokuwa palikuwa na giza lakini mtu yule hakuwa Masimba kutokana na umbo lake. Akaipa muda akili yake kuwaza na kulitafuta jibu. Alikuwa nani katika nyumba yao na alikuwa akitaka nini? Hakuweza kupata jibu kwa wakati ule, lakini kwa mbali alianza kuhisi kuwa wenzake walikuwa wakimgeuka. Ingawa hayakuwa mawazo ya asilimia mia, lakini hakuna mtu mwingine ambaye angeweza kufika pale. Akaendelea kutulia akitizama zaidi na zaidi, kwa mara nyingine akamuona mtu wa pili naye akichupa na kutua ndani. Huyu wa pili alimsisimua zaidi kutokana na muonekano wake. Alikuwa ni mwanamke, tena mwanamke mwenye ujuzi.

Teddy hakutaka kusubiri, sekunde ile ile akarudi ndani kwa kupitia mlango ule ule wa siri. Muda wote alikuwa akijiuliza juu ya watu hawa. Akatokea kwa ndani kisha kutulia.. aliangaza macho kwa muda punde akakiona kama kivuli kimepita hatua hamsini kutoka pale alipotulia, sekunde ile ile akakiona kivuli cha pili pili kikipita. Muda ule ule akawaona watu walewale wawili wakichupa kutoka nje ya nyumba yao. Teddy akaduwaa. Kuduwaa kwake sio kuduwaa bure lakini alitambua watu hawa walitumwa na Jimmy kumchunguza yeye ama wametumwa na Idara ya Usalama wa Taifa kunfuatilia. Wazo la idara ya usalama hakuwa na mashaka nalo, lakini kuhusu Jimmy alikuwa na Uhakika nalo kwa kuwa ni siku hii mchana ambayo walimtishia kwa bastola, na sasa walituma watu ambao hakujua ni kina nani na wamekuja pale kwa sababu gani.

KESHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom