Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Mimi ni muislamu tena jina langu ni Mohamedi. Naipenda Chadema kuliko chama chochote tangu nimeanza kufuatilia siasa na kuwa mwanachama wa chama hicho.

Hawa wanaotoa majibu ya jumla ya kukihusisha chadema na propaganda chafu za udini eti waislamu wanaichukia chadema ni wajinga, wapumbavu na wavivu wa akili walio zama kwenye tope la upoyoyo na wanatengeza tatizo kwa waislam ambalo kwa muislamu yeyote mwenye mtima ulio timamu hawezi kuwasikiliza. Wanapokisema chadema kuwa ni cha wakristo mbona huwa hawatoi mbadala kuwa waislamu waende kwenye chama gani? Mufti anapopinga maandamano ya chadema yeye kwa fikra zake anajua kuwa waislamu wana hali nzuri kimaisha? Na kwa nini atusemee waislamu wote Tanzania juu ya mapenzi yetu kwa chama mtu anachokipenda? Mufti hakifikiri kwa niaba ya watanzania waislamu juu ya tukipendacho na lazima ajue JK hasakamwi kwa kuwa yeye ni muislamu bali kwa kushindwa kwake kiungozi na kuonyesha ombwe lililopelekea kujivua gamba.

Wavivu wa kufikiri na wanao ongozwa na mihemko ya udini kwa mtu ambae hawakuona udini wake alivyopambana bungeni na kutaja mafisadi wakristo na waislamu ni juha asiye ona kwa nini Slaa na chadema yake wanapaswa kuungwa mkono na mtanzania yeyote mpenda maendeleo.

Mjenzi wa udini tunamjua, binafsi kama muislamu naamini wapo waislamu wengine wenye mafungamano makubwa na watu wa dini nyingine hata kuoleana au kuwa ndugu wa damu, kwenye foleni ya maji hatuulizani dini zetu tuwamoja na tunashirikiane.
Niko tayari kupambana juu ya propaganda chafu za ccm juu ya udini, walisema cuf ni wadini leo wamegeukia chadema! Nyambafu.

Hapo nilipo highlight umepaona ? ww twakujua sana sio Godfrey Christian Gwakisa ww? acha kuwadanganya watu humu JF
 
Sifa moja kubwa kwa Waislamu na Uislam ni kutobadili msimamo kwa lile walilokwisha aminishwa kwamba ni kweli hata kama sio. Wanaweza kumkubali Dr Slaa kwa mashaka sana endapo tu atasilimu basi.
 
Wewe waberoya unaonyesha kuwa na uwezo mzuri sana wa kupandikiza propaganda za
udini dhidi ya DR SLAA na dhidi ya CHADEMA na ndio maana umeng'ang'ania sana hii hoja ovu
dhidi ya DR SLAA.

Hili swala la DR SLAA limezungumziwa na watu wengi kwa mapana na marefu kiasi cha
kushangaza mtu mwenye uwezo wa kutoa hoja kwa mtiririko mzuri kama wako, bado
anaweza akawa bado amekengeuka na kuendelea kushikia bango upuuzi huu.

Ntakuuliza maswali kadhaa.
Kwa kumpinga DR SLAA kutokana na imani yake, je inamaanisha kwamba waislamu hawako tayari
kuona nchi hii ikiongozwa na wakiristo? ndio, je vipi wakirsto nao wakianza kuongea hadharani kwamba
wasingependa kuona muislamu akiongoza nchi hii? kumbuka vihere here kama vyenu vikizidi sana
vinaweza kusababisha watu wakaachana na misingi yao ya kuangalia, kuchambua na kuamua mambo
ili kuenda sawa na misingi iliyoshamiri katika jamii.

Hii nchi sio ya kiislamu, kwa hiyo ni makosa kabisa kwa kikundi chochote kukaa na kufikiria juu ya
namna ya kuwafurahisha, kuwainua, waislamu kwa misingi ya kisiasa, na hii sio kwa waislamu tu
bali pia wakirsto na dini nyingine yoyote ile. Hivyo ni makosa kabisa kwa mfano, kwa CHADEMA kuwa
na agenda ama mkakati wa kichama wa kujisafisha dhidi ya uchafu wa udini wanaotupiwa,

Nchi hii ina watu wenye imani za dini tofauti tofauti, wote tunalazimika kuheshimu hilo, na
haitakiwi kumbagua mtu yeyote kutokana na imani yake, Hivyo Waberoya, CCM, pamoja na waislam
wachache waliokengekuka mkae mkijua kwamba mnachokifanya dhidi ya DR SLAA ni ubaguzi ambao
haujawahi kuonekana wakati wowote katika historia ya nchi yetu, mnamkataa mtu asitumie haki
yake ya kikatiba ya kuwa kiongozi kwa sababu ya dini yake.

Hivyo, Kama wewe waberoya umeona kwamba Dini ya DR SLAA ni tatizo kwa chadema, unatakiwa
kwa nguvu zako zote upaze sauti kwa watanzania na kuwaeleza kwamba propaganda za kidini dhidi
ya CHADEMA ni uovu usio na mantiki, na wote wanaotapakaza uchafu huu ilitakikana wachukuliwe
hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.

Hivyo waberoya, hapa unaadress an informed audience, nenda misikitini ukawaeleze wanachokifanya
waislamu ni jambo la dhihaka, aibu, la kijinga, kinyume cha katiba, ni ukosefu wa utu na staa,ni
kinyume cha misingi ambayo mwalimu nyerere alijitahidi kuijenga katika nchi yetu mpaka siku
anakwenda kaburini. uwaeleze kwamba wasiwasikilize wote wanaopita uko na kusambaza propaganda
hizi ovu dhidi ya usalama, mila, desturi na ustaarabu wa kitanzania.

Uwaeleze kwamba CHADEMA wapo pale kwa ajili ya kupigania maendeleo ya taifa hili bila ubaguzi
wa aina yoyote ile, na wanafanya hivyo kwa sababu wanadhani kwamba CCM imeshindwa, wawapime
katika hayo, kama wanaona CCM wanaweza basi wawaunge mkono kama wanaona CHADEMA wataweza
basi wawaunge mkono na wakati wote si katika misingi ya dini katika namna yoyote ile.

Nenda Waberoya.

well said brother
 
mwalimu wake alipata shida sana kwa mtu huyu, hajui hata baadhi ya maneno kama sifa, kupanda na kushuka ajui hata kwa kushindwa ccm walitumia udini ili kukimaliza cdm kumbe walijiua wenyewe baada ya kushindwa dhamila yao leo je umewauliza kama magamba meusi ya udini wameyakwangua ? au baadaye yataoza na kuwanukia
 
Well....This is interesting.

In my opinion, a good reader should have the following qualities

1. Honesty

Leaders have to be honest.Common sense, if you ask me and I see it on Dr Slaa.

2. Responsibility

If you are going to make decisions, then you should take responsibility for the decisions that you make. Good leaders don’t pass the buck or blame other people – they deal with situations that arise and take responsibility for the results. Oh, and if you delegate a responsibility to someone under your charge and they screw it up, then it is YOU who have screwed up. That’s what leadership and responsibility is all about. Well, you will be my witness, Tanzania Leaders don't take responsibilities of their action. But frankly speaking, Dr Slaa is responsible on many aspect....He exposed most of the awful activities done by our government and his stand has never been shaken

3. Confidence

You have to believe in yourself. Dr Slaa is extremely confident


4. Enthusiasm

How do you make someone do something that they don’t want to do? Enthusiasm! Get psyched about the task that you’re assigning.

5. Reliability

Saying that you’re going to do something means that you will actually have to do it. Nobody likes an unreliable person, even if they’re not a leader. After your first time going back on your word, people just aren’t going to trust you anymore. I guarantee that Dr Slaa has been reliable since he joined CDM

6. Patience

Don’t underestimate the importance of patience. If you explain a task or situation to you charge and they don’t understand, then clarify it for them. It’s not their fault that they don’t understand your instructions – it’s YOUR fault. In short, He is never In hurry to react on objections.

7.Determination

This pretty much amounts to “finish what you start.” See tasks through to the bitter end, and keep your charges motivated to continue. I bet you, if it wasnt for uchakachuaji, Dr slaa would be our president since Nov 2010.

8. Loyalty

This is something that you expect of your charges. It is also something that your charges expect from you. The first time that you stab your charges in the back will also be the last. Just give an example if possible of when Dr Slaa was not royal to CDM and common Mwananchi

9. Courage

This could be the most important of the list, since it encompasses so much. As a leader, you must have courage in order to be decisive. You can’t be afraid of failure, or else you will not be able to function as a leader. Have the courage to stick to your convictions or go with a gut instinct. Well, you might be my witness, the courage of Dr Slaa is not comparable to Any of the 2010 presidential candidates.

Last but most Important.

If a Leader has the above qualities, for me it doesn’t matter whether he/she is a Moslem, Christian or non believer, I will surely vote for him/her.


‘Kiongozi yeyote, Awe Muislamu,Mkiristo au asiye na dini anaweza kuongoza vizuri kama atatanguliza maslahi ya wote na kusahau dini yake.Siamini Kama CDM wakiweka muislamu wanaweza kuondoa propaganda za CCM kwamba CDM ni wadini. Believe me, hii ni tactic tu ya CCM kukiua CDM, but kama CDM watakuwa makini na kuendelea na uzi ule ule, CCM wataanguka. Siamini kama kweli ndani ya CDM hakuna waislamu......Maandamano na vifo vya Arusha vinadhihirisha hilo ’
 
Mkuu Mkandara,

Wazo lako ni zuri sana lakini bado napata tabu kuamini kuwa solution hii itafaa...

-Hakuna guarantee kama CDM wakiongea na waislamu basi watapata kuungwa mkono unless wakubaliane na matakwa yao.
-Kama tunakubaliana kuwa matatizo ya waislamu ni wao wenyewe na kwa kushirikiana na chama tawala then tuna uhakika gani kama CDM ndio wanaweza kuwa solution kwa kuzungumza nao?
-Tusisahau kwamba hii chuki dhidi ya CDM ni kwa sababu Rais aliyepo madarakani ni mwislamu lakini kama ingekuwa vinginevyo basi hakuna muislamu ambaye angekuwa anangaika kuponda CDM kuwa ni chama cha maaskofu! CCM wakimsimamisha mkristo hadithi ya BAKWATA itabadilika for sure.....

Mimi binafsi sioni suluhisho zaidi ya kuzidi kuwaelimisha watanzania na kuwaamsha kupambana na matatizo yanayowakabili bila kujali dini na makabila yao kwani at the end of the day matatizo hayabagui.
Mkuu wangu labda hujui kuhusiana na Bakwata.. Bakwata imekuwa nyuma ya CCM toka Nyerere, Mwinyi, Mkapa na sasa hivi JK sii kwa sababu wao ni Waislaam ila ni sehemu au tawi la chama hicho kama kilivyo chama cha wanawake UWT.. Hivi hujiulizi kwa nini chombo cha Unoja wa Wanawake nchini kiwe chini ya bendera ya Chama tawala! - hii haikupi shida wewe kuelewa?

Matukio mengi ambayo Waislaam wenyewe wanayalalamikia yametokea ktk vipindi vya viongozi wote hawa..Na sii kwamba Dr.Slaa anakwenda kuonana na Waislaam ili wamkubali bali kuonyesha Courage ya kuwa face wananchi wake ktk maswala magumu na kuonyesha msimamo wake na wa chama - Period.. Sasa kama leo hawezi ni lini ataweza kuyazungumzia kama atapewa dhamana kubwa zaidi...

Kuna mchangiaji hapo nyuma kasema kitu Enthusiasm, na nadhani Dr.Slaa hashindwi kabisa kuwavutia Waislaam na kama kweli hawezi au fikra za kwamba hata kama akiwaona hatakubalika then ni dhahiri tukubaliane kwamba Dr. Slaa ana mapungufu - FAHAI.. Hafai kwa sababu anahofia kutoungwa mkono na Waislaam with no reason, au yaonyesha hakubaliani na madai yao kwanza...Na pili kutokubaliwa kwake kawaona au hakuwaona, ina maana hakubaliki na kundi moja la Jumuiya yetu eitherway...Halafu inachekesha sana mnaposema ati ni kundi dogo tu la waislaam wasiomkubali Dr.Slaa hali mnahofia yeye kukutana na Waislaam hatakubalika.. Kuna kipi kilichojificha hapa?

Kisha mkuu wangu tuzungumzie vitu kwa uwazi na kutokuwa na nidhamu ya woga.. Haya maswala ya dini ni muhimu sana ktk siasa za Tanzania...Hadi leo hii hatufahamu jinsi ya kudeal na Ukabila, Udini na hata rangi zetu kiasi kwamba swala la Uuwiano limetanda ktk ngazi zote za kiutawala hata kama hazina maana..Mimi najua kwa uhakika JK alitakiwa kuonyesha msimamo wake na kanisa ili apate (baraka zao) kukubaliwa mwaka 2010 na alifanya hivyo ndio maana akaitwa - Chaguo la Mungu - Na hata uchaguzi ulopita Kard. Pengo alimwambia wazi kuwa kama anataka kura za Wakristu ni lazima amwone yeye..This tells a lot jinsi dini ilivyokuwa na nguvu ktk siasa za Tanzania.

Na sisi wenyewe tumo...Wadanganyika siku zote macho yao hutazama list ya viongozi wetu serikalini, ktk mashirika na ajira mbali mbali kwa dini zao, jinsia na makabila yao, na hata Wazanzibar kuhesabu nafasi walizopewa kushiriki ndani ya serikali ya Muungano imekuwa ni issue kubwa sana ya kumchagua kiongozi yeyote na usipofanya hivyo utaitwa Mkabila, mdini na kadhalika..Uchaguzi wa Mukama kuwa katibu wa CCM tayari umeshakuwa mazungumzo makubwa ya dini na kabila yake kuunganisha na CV yake hivyo tusidanganyane hapa jamani.

Hizi habari za watu kusema hawajali kama rais ni Muislaam au Mkristu maadam ana deliver ni UONGO mtupu...we all say that lakini ukisoma hoja za watu hapa JF utajua ukweli ni upi..Hadithi zote za kisiasa nchini zinahusiana na uuwiano wa viongozi ngazi zote za kiutawala kuwa ndio haki ya msingi ktk kuondoa tabaka za Udini, Ukabila na kadhalika..Most Tanzanian would rather have the balance in appointments than who are represented..kwa sababu hawaamini Mkristu anaweza kusimamia maslahi ya Waislaam au Mbara kusimamia maslahi ya Wazanzibar, wanaume kusimamia maslahi ya wanawake na kadhalika..Haya mambo sii ya mzaha hata kidogo pamoja na kwamba mimi binafsi nayapinga sana lakini haya mambo yapo sana na yana apply ktk siasa za Tanzania vibaya sana. That is - REALITY!

Na kama Chadema na Dr.Slaa wanafiiria kwamba waislaam wataweza kumwelewa yeye kutokana na sera za chama basi afahamu kwamba Udini ni zaidi ya akili ya mtu kufikiria straight..Na sababu hasa ya Chadema kukutana na Waislaam ni kutokana na pandikizi la Udini ambalo hata siku moja haina aibu wala logic isipokuwa ni chuki inayotokana na Uadui wa kiroho..Jamani mwee tunapozungumzia tactics za CCM tujiulize, leo hii CUF wako wapi? bado tu hatujajifunza kutoka kwao..Na bahati mbaya sana ndugu zangu Tanzania tayari Udini umeshapandikizwa na kilichobakia ni kutokea yale ya Tegeta au Rwanda huku CCM ikinyooshea mkono vyama vya upinzani kuwa ndio sababu..WE must stop mapema tukiwa na muda na nafasi ya kufanya hivyo..

Na maajabu sana napowasoma watu wanaandika ati SIFA ya Waislaam ni kutobadilisha msimamo hadi mtu asilimu dini..sijui sifa hii wameipata wapi ikiwa waislaam walimkubali Nyerere pasipo kubadilisha dini yake..Kwa nini iwe vigumu kwa Dr.Slaa kuwaface waislaam kama alivyoweza Nyerere?.. Binafsi nina hakika na ugumu mkubwa kuamini kama ingekuwa kinyume wakristu wangempokea Muislaam bila kubatizwa vile vile, hivyo maoni ya mtu sii lazima yawe na ukweli..
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.
Ndg YANGU wABE kujivua magamba hakuwezi kumfanya nyoka akawa njusi!!!!! Siri za watu wako zote zipo nje, hivi sasa wanatapatapa!!!!!!! Nyota ya Dr wa ukweli Slaa ndio kwanza inachomoza, wacha kusema eti atakumbukwa. Mbona yupo tuu, mwendo mdundo baba haturudi nyuma. Wadanganye wajinga hakuna kilicho badilika ni ufisadi na chakachua tuu ghiliba za SISIEMU!!!!!!
 
HUYU NDIYE WABEROYA WA MASLAHI NA UANACHAMA WAKE KISIASA NCHINI

Ni bwana mmoja mwenye kubenda saana kubeba simu kati ya tatu hadi tano hivi. Yupo pale Haidery Plaza nyuma kidogo ya kituo cha mafuta pale Posta Mpya Dar.

Nadhani ni mmojawapo Watanzawanachama maslahi wachache tulionao hapa nchini. Kwa mara ya mwisho, wakati wa utawala wa Benjamin William Mkapa (Rais aliyemuona kwa picha ya Ukristo zaidi ya Utanzania wake) alikua ni mwana-CUF.

Sina uhakika kama kule Buguruni aliaga kabla ya kujiunga Chimwaga. Ki-Umri ni rika tu na Zitto ila kampita kidogo. Na hiyo ndiyo maana hayupo kwenye UVCCM ila moyoni huwa aamini kuwa kama li-King-Maker vile kisiasa akiwa nyuma ya pazia wakati ukweli wa mambo ni kwamba Political Base and Impetus zote ni za kufikirika tu angani.

Gari lake wakati wote ni kama nyumba na vikolombwezo kibao ndani, huvaa cheni ya dhahabu na kuachia vifungo vya shati hadi ya tatu na kuvaa casual siku zote. Ni swahiba mkubwa pia wa RA na EL huyu bwana.

Pindi tu CCM kilipobahatika kumpata Rais mpya Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia walikua na rapport / ushikaji mzuri tu huku mitaani, ndipo mwenzetu tukamuona kageuka rangi ya majani ya mgomba kutoka kwenye ile rangi ya zambarau na kauli mbiu 'Haki na Usawa kwa Wote'. Ki-akili zinachaji vizuri tu kulingana na kazi zake za kusukuma kalamu na hizo nyinginezo lakini shule bado haijamkubali saana vile.

Kwa sasa enyi mnaomsoma, kwenye koo yake kuna ka-upepo wa 'sisi-CDM' katika wiki za hivi karibuni. Lakini kabla ya hapo amekua tu ni mtu wa kubeba bango la NON-ALIGNED POLITICS / KUCHEZA UKATI WAKATI WOTE HATA KWENYE KUKOSOA hapa jukwaani. Hili la 'Sisi-CDM' aliyoanza nayo majuzi ni katika kile anachoamini (bila tathmini ya kisayansi) kwamba ndani ya CHADEMA kuna mtu mmoja tu mwenye uwezo kiuongozi ni rafiki yake wa tangu katikati ya miaka ya 90 Zitto Kabwe - wengine wooote mle aonavyo yeye ni wasindikizaji tu.

Huyu bwana ni miongoni mwao VISHOKA VYA SIASA; nyundo na komleo mkononi. Kati ya kazi wanaojipa moyo nayo hivi sasa ni kwamba CHADEMA is simply up-for-take kiulaini hivyo tu na bwana Zitto si kwa maendeleo ya CDM yenyewe bali ni kwa sababu tu ya kitu wanachokiita kwenye vikao vyao vya hiari pale Rose Garden katika kukisaidia CCM-Ufisadi kufanya 'POTENTIAL FURTHER DAMAGE CONTROL' ili kukidhibiti CDM na timu zima chini ya Dr Slaa kabla ya 2015.

Hakika hii kazi anayojipa huyu ndugu kiukweli inahitaji moyo wa ki-uendawazimu hivi, ujana wa sungura na utafiti wa kisayansi ili aweze kuikamilisha walau kwa miaka 10 ijayo.

Huyu Waberoya aka ... laiti angelitibu magonjwa haya kwanza basi ni mtu ambaye anaweza akawa very resourceful baada ya kujitambua kwanza kwa yeye yu nani na angependa kuhesabiwa kusimamia nini katika jamii kwa miguu yake mwenyewe badala ya huu upigaji-debe sugu kwa wengine tena tu. Magonjwa yake huyu bwana, mbali na kuwa GREEN SNAKE IN THE GRASS kwa wapiganaji wapenda mabadiliko ya kweli ni pamoja na ugonjwa wa

1. widespread procristination (jambo linalofanya vijitenda vingi vya aina hii kurundikana na kulala mezani kwake muda wote na kumpunguzia ufanisi),

2. wishfull-thinking (inayomfanya afanane na fisi kutegemea mkono wa binadamu kudondoka ili azma yake ya kutenga karamu itimie), self-agrandisement (kule kujipa ukuu asiyokua nayo kama vile kuwa msemaji wa Waislamu- CCM BAKWATA huku akiamini kuwazungumzia Waislamu wa Tanzania nzima) and

3. fallacious conclusions (jambo linalomfanya afanane na washauri wa Gbagbo kwamba anapendwa sana na kwamba wala asijiuzulu, mpaka pale picha inapomalizikia kwa kuopolewa kwao na bosi wao wakiwa so desparate kutoka chini ya ardhi kama nyoka aina ya nyamwiru).

Ni ushauri wa bure kwa Waberoya pamoja na Mr Mak, Malecela wa huko Ughaibuni kwamba wakati CDM sikuzote kinathamini sana mawazo ya kukosolewa ili kujiimarisha zaidi, hili la Zitto Zuberi Kabwe kuwa mgombea wa CHADEMA eti kwa kuwa mmemvisha kanzu ya Uislamu BAKWATA-CCM badala ya kujivalia tu Utanzania ni kule kwenu nyinyi kummaliza kabisasa huyu kijana mbaye hivi sasa sifa zake kisia iko ICU kwenye tathmini ya wananchi - huku nyinyi wajiaminisha kumsaidia kitu.

Sana sana hebu kakisaidie kwanza hiki chama chenu CCM kipate ujasiri wa kujivua gamba la katiba dhalimu kwa kuunga mkono kwa dhati kuundwa kwa katiba mpya yenye wananchi kushika ushukani, ufisadi wa kitaasisi kwa kufanya sweeping internal party constitutional review, na uchakachuaji chaguzi zetu nchini kila mara kwa kudhamini hoja ya tume huru ya uchaguzi na mgombea binafsi.

Ndio, Waberoya katumie muda wako kumweleza Zitto kwamba kupenda kule vya CCM na huku vya CDM mwenzetu atapasuka msamba; maadui pande zote mbili wakija kuungana ... asiombe!!!!!!!!!!!! Pia Waberoya kamwambi rafiki yako JK kwamba lilikaribia saana kuvuliwa lilikua ni lake mwenyewe kuwatema maswahiba CCM. Lakini hata kabla ya kumaliza kulivua akaliongezea tu gamba lingine zitto la kundi la pili la mawakala wa wale wale maswahiba wake ambao hivi sasa kuku kwa mrija Magogoni huku wakigongana Tano za ki-Jah people kula kunywa.

Sasa swali lililoko vichwani mwa kila Mtanzania ni kwamba baada ya JK kushindwa kulivua gamba lake mwenyewe chamani (kutokuwaachia wana CCM wenyewe kuchagua maafisa wapya badala ya kuteuliwa na yule yule mtuhumiwa namba moja wa Watanzania), je CCM chenyewe kinapanga kujivulia lini gamba lake?????????? Je, chama hiki kina ujasiri wa kutosha kweli kujivua jumla gamba kimfumo badala ya kisura????????????

Watanzania vita mbeeeeeeeeeelleeeeeeeee zaidi dhidi ya ufisdi, mawakala na taasisi-fadhili zake zote nchini!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wabe, mie nakushukuru kwa mawazo yako. Yapo mambo mengi ambayo ya msingi umegusia. Mtu ukiambiwa mwizi ni vema ukajiangalia pengine huwa unachukua vitu vyako kwa staili ya wizi. Ni vema chadema ikajitahidi kuonyesha na kuondoa hisia za udini walizopakwa na ccm wakati wa uchaguzi na hata kuprove ccm ndio wadini. Nilifurahi sana ktk bunge lililopita ktk timu ya slaa, hamad na zito. Nawaheshimu sana hawa watatu na mchango wao utakumbukwa daima.
 
1.Eti dr.Slah aondoke ili kuiga upuuzi wa ccm wa ''KUJIVUA GAMBA''.
2.Eti dr.Slah aondoke kwa sababu chama kitaitwa cha kidini kama kitaongozwa na mtu mwenye dini.
3.Eti mtu akiwa maarufu hapaswi kuongoza chama kwani anaweza kupoteza umaarufu wake.
4.Eti kwa kuwa watu wasio na logic wanaweza tu kumpinga basi yapaswa tumuondoe mapema bila logic.
TUPENDE KUFIKIRI TUSIENDESHWE NA KUWAZA
 
aliyeanzisha thread hii hapa ni mtu hatari, asiyefikiri vizuri.
Anapenda tu naye asikike.
Yapaswa apuuzwe
 
Mkuu wangu unafikiria kisomi sana, jaribu kufikiria kama Mtanzania aliyekosa tumaini la kupona isipokuwa kwa kwenda Loliondo, na imani hiyo imekubalika hadi viongozi wasomi wenye ma Phd..

Waislaam wengi hawana imani na Dr.Slaa kwa sababu wanaamini system nzima ya Utawala wa Tanzania inatawaliwa na kanisa...Sasa ni bora kwao kuwa na Muislaam ndani ya hilo kanisa kuliko kuwa na Mkristu tena Padre, hivyo ni jukumu la Dr.Slaa kuwahakikishia hakuna kitu kama hicho na kama kipo yeye atakikomesha..hapo tena wakiendelea kutomuamini basi wana lao jambo.. elewa tu kwamba asilimia 80 ya Watanzania ni kabuntas na shule zetu za kata tunazojisifia nazo dhidi ya madrasa..
Waelimisheni hao ndugu Mkandara.Hivi kweli JK ni mkristo na mawaziri wake ni wakristo?Si walikuwa wakienda kufuturu ikulu kipindi cha mfungo wa ramadhani tena JK akiwa nje ya nchi?Kuna mtu alisema TZ ina mfumo Islam?
Huo mfumo kristo ndio unaowapatia viongozi waislam wenye kutawala kikristo?
Waache ujinge,wajiunge na watanzania wenzao kujenga Taifa.
 
CDM walipofanya maandamano kanda ya ziwa waliungwa mkono na wananchi wengi, si kwasababu ya Slaa au Halima Mdee ni kwa ujumbe'message' iliyogusa maisha ya wananchi, umeme, kupanda gharama za maisha, Katiba na Dowans. Wananchi hawakuona tofauti zao zaidi ya shida zao za pamoja. Hiki ndicho CDM wanapaswa kuendelea nacho sehemu zote nchini ikiwa ni pamoja na sehemu ambazo hawafiki(pwani na kusini). Mwisho wa siku wananchi watajua ni nani yupo nao na ni akina nani wanawadangaya.

Thamani ya kitu ipo machoni na mioyoni mwa watu, CDM wasimamie thamani hizo na kuzibainisha kwa mifano kama ilivyokuwa Halamashauri ya Karatu ambayo kila mtu aliisifu na kuipenda chini ya Slaa. Hakuna sababu ya kwenda na upepo kwani hawa watu wanaoeneza udini ni wafanyakazi, walikuwepo CCM wakati wa Mkapa, wakahamia CUF na sasa hatujui wamerudi CCM au wameajiriwa na mafisadi. Nawahakikishieni wapo waislam wanaochukizwa sana na hili kundi na ni wengi bahati mbaya hawana vipaza sauti.Ni makosa kufikiri kikundi cha watu wachache au wa mtaa fulani ni jamii nzima.

Waislamu wampinga Mufti kuibeba CCM
Tanzania Daima Alhamisi 14 2011

na Abdallah Khamis, Dodoma,

UMOJA wa Kiislamu (Istiqama) Mkoa wa Dares Salaam, umemtaka Sheikh Mkuu nchini, Mufti Shaaban bin Simba, kuacha kuvishambulia vyama vya siasa vinavyoikosoa serikali na badala yake ashughulikie masuala yanayohusu maslahi na matakwa ya Waislamu hasa katika kipindi hiki cha vuguvugu la madai ya Katiba mpya. Msimamo huo ulitolewa jana na Sheikh Yasin Bahama, kwa niaba ya umoja huo wa mringano wa Kiislamu, wakati akitoa tamko kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na nafasi ya Waislamu katika mchakato huo.

Tamko hilo limekuja ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu Mufti Simba ayalaumu maandamano yaliyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mikoa ya Kanda ya Ziwa akisema yanahatarisha amani ya nchi.
Ajenda ya maandamano hayo ilikuwa ni kuishinikiza serikali kuchukua hatua za dharura za kulinusuru taifa liondokane na maisha magumu hasa baada ya kupanda kwa bei za vyakula, bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo umeme, gesi na mafuta. Sheikh Bahama alisema mufti kama kiongozi wa waislamu wote nchini anapaswa ahakikishe kuwa katiba ijayo inawapa Waislamu fursa na haki za kutosha ikiwa ni pamoja na kuwa na Mahakama ya Kadhi.

"Haya maisha magumu tunayapata wote sasa wanapotokea watu wanaishinikiza serikali ili hali iwe nafuu halafu anatokea mtu anawapinga (Mufti), kwa kweli ni jambo la kushangaza," alisema.
Sisi kama Waislamu hatuoni tatizo lolote linalofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kuwa ni chama cha siasa cha upinzani, na lengo la vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali kwa kuwa ni haki yao kisheria. Tunawasihi Waislamu wote kwa pamoja tuhakikishe Katiba mpya inakuwa na Mahakama ya Kadhi. ….tushughulike na kudai haki zetu ziingie kwenye Katiba. Tuachane na kutetea CCM na serikali yake, tuachane na kushambulia vyama vya siasa kwani vipo kwa mujibu wa sheria", alisema Sheikh Bahama.

Walisisitiza kuwa suala la kuwa na Katiba mpya ni muhimu kuliko kuangalia ni chama gani kinaongoza nchi kwa wakati huu, kwani chama kinachoongoza sasa kitafika mwisho wake lakini kama Katiba itakuwa mbovu basi haki na maslahi ya Mwislamu vitaendelea kudhulumiwa siku zote.
Alisema kuwa Waislamu wana madai mengi na ya msingi wanayopaswa kuhakikisha wanatimiziwa kuliko kuangalia kwanini serikali ya CCM inasemwa. Waliwataka viongozi wote wa kidini nchini kuachana na masuala ya kisiasa na badala yake wawaongoze watu wao katika kufanya mema kwa ajili ya mwenyezi Mungu.


My take:
Kauli ya mtu mmoja au kikundi cha watu isichukuliwe kama kauli ya jamii hadi itakapothibitishwa bila mashaka. Kuchukua kauli ya John kama ya wakristo au Hussein kama ya waislam ni ku 'marginalize' hata wale wasiokubaliana na hayo.Hili ni tatizo hapa JF na linaumiza 'hurt' CDM kwa namna fulani. Fikiri.

Pili, watu wanaguswa na thamani ya kile unachokisimamia kama walivyosema hao waislam kuwa shida zote CDM inazosimamia ni za watu wote bila kuchagua. CDM wasimamie thamani hizo zaidi.
Kuanza kuongea na makundi fulani ni kuyapa makundi hayo nguvu isiyostahiki na kujiona yanaweza huku mamilioni wanasahaulika. Nadhani ni vema kuwasiliana na wananchi kila kona ya nchi kuliko kuwasiliana na kikundi.


blank.gif
blank.gif
blank.gif

blank.gif
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.

Umehitimisha bla bla zako kwa kujihami na kujionesha wazi kuwa hujiamini,umesema utatukanwa,km hoja yako ni ya msingi kwa nini uhofie kutukanwa?WEWE NI NABII? Unaitabiria chadema kifo ushindwe.Je! unauhakika kuwa wewe huna tongo tongo?wewe mwenye upendo wa kinafiki na mawazo ya kinafiki upotee gizani na na ushauri wako wa kinafiki,na ilaaniwe njia ya ufahamu iliyoingiza mawazo haya ktk ubongo wako.
 
Lazima ifike muda tusiogope kukosoa kwa gharama za kutukanwa na wasiojua hali halisi ya nchi hii ilipo na tunapoenda. Hapa chini natoa sababu za kupinga au kutokukubaliana na hoja za Slaa na chama chake kutaja mafisadi

1. Criminalised society

Ukiwa na taifa ambalo secretary, messenger, polisi ,manesi na wote wenye vipato vya chini mishahara yao haikidhi mahitaji yao na bado wanaishi vizuri ni ishara tosha ya kuwa hiyo jamii/society ina matatizo

Ni jambo lisilopingika na ukweli kila mtu anaujua kuwa watu wengi asilimia zaidi ya tisini ya watanzania ni mafisadi na ii ni kutokana na mfumo ambao Tanzania ulipitia miaka zaidi ya 20 iliyopita.

Nchi hapo kwanza iliongozwa na aliye msafi Nyerere, akamwachia Mwinyi ambaye akaruhusu uchafu wa pili kuwa mkubwa zaidi ya ule wa kwanza. Watu walitegemea viongozi wangechukua hatua juu yaw ala rushwa hali haikuwa hivyo kuanzia Mwinyi mpaka Kikwete! People are tired their only consolation ni kuiba na kuwa mafisadi…Leo hii graduates wakiwa mashahidi ni msemo wa kawaida ‘kupiga' kuwa una piga mahali…unafisadi ndio unatoka kimaisha!! That's why I am saying we are living in criminalized society. Kuwa kama msafi ni wewe na Mungu wako mnajua na sio kusema Fulani msafi. Kwenye middle class ufisadi ni SIFA, kwenye lower class ufisadi ni ubaya since they don't have opportunity to do the same!!

2. Je wachafu wengine wamepona?

Kauli mbiu ya chadema ilitakiwa iwe ccm wote wachafu na kuonyesha watanzania ni jinsi gani na kwa nini wanasema hivyo. Kutaja baadhi ya watu ni ishara ya uvuvuzela kuwa chadema sasa haina umakini wakutambua alama za nyakati na wakati. Mwembe yanga ilikuwa zama zingine na sasa ni zama zingine, nitaeleza chini ni kwanini na sema hivi.

Kutaja baadhi ya watu globally unawaweka mafisadi wengine mahali pazuri pa kuonekana wazuri katika jamii. Mbaya zaidi maeneo wanayotoka hao watu ambao wengi ni kipenzi cha watu wao chadema wameishanunua mgogoro mwingine.

Kwa sisi wengine tunajiuliza is this priority? Kwa hali ya sasa ya kukijenga chama toka ngazi ya mtaa mpaka taifa? Hii ni mizizi ya chadema nchini au chaos ya chadema nchini?

3. Uniting CCM which was supposed to crack

Siku za hivi karibuni imeonekana wazi kabisa CCM inataka kubomoka kutokana na makundi mengi sana ambayo sina haja ya kuyaeleza

Tafiti zinaonyesha kuwa watu wa aina moja wanaokabiliwa na shinda za aina moja huwa wanapenda kuwa pamoja. This is nature and I can describe this further..it is nature!

Chadema inapaswa kutambua kuwa kuwataja watu kama akina Sumaye, Magufuli ambao kwa namna moja au nyingine walionekana threat ndio mwanzo wa hawa watu kuungana! EL or RA can just ring to Sumaye na kumpa pole…that is a starting point.

Tulitegemea kuwa karibu na uchaguzi kuna kundi ambalo lingejimega kutoka CCM aidha wakaja chadema ( kama wasafi) au wakaenda kwingine, ili lingekidhoofisha CCM to the large extent.

Kumeguka kwa CCM kunakotarajiwa ambako kumekuja zaidi baada ya wao kusema ‘kujivua gamba' hakutaweza kutokea kwani kwa sasa CCM wataugana zaidi na kuwa kitu kimoja , umoja ambo ni threat. Is not possible ukawaweka mawaziri wakuu wa zamani watatu waunde kundi moja na kusematunashinda kwa nguvu ya wananchi , ili hali hawa jamaa huko kwao wana nguvu sana.

Kuna tofauti gani ya UVCCM chairman na Dr.Slaa?

Je common sense au analysis kama hizi ziko wapi chadema?

4. So what? Was it right time?

So what? Wakijua kuwa kumbe waliotajwa ni watu wengine ambao hata hawako serikalini so what?? So what tulipiga kelele za list of shame miaka 6 iliyopita, tulichoona ni bado wako mtaani, bado wana wafuasi (kusupport point ya kwanza), bado wana nguvu, walishinda majimbo yao bila kuchakachua.

Leo hii mmeingiza majaji kuwa ni mafisadi, mmeshindwa kuwataja ni majaji gani? Mmeshindwa, ili hali tunategemea haki ipatikane huko?

Kama chadema inaaminisha umma kuwa hata mamjaji ni wachafu..maana yake ni nini? Was it necessary kuwasema sasa? Hali kwa sasa itapatikana wapi? Je Mtikila alishinda kesi ya mgombea binafsi wapi? Why generalize majaji?? Kuwa wote ni wachafu..Is this was your only wisdom? Yes ni kweli kabisa ni wachafu..my question is was it right time?

5. Chadema's mission

Ni kujenga chama kutoka ngazi ya mtaa na sio kuzunguka nchi nzima na kumaliza hela ya ruzuku . ili hali mikoani wanakufa. CCM wamajijenga ilo linajulikana

Guys, it just need three solid years to spread chadema calmly, friendly nchi nzima, kila kona , kila shule, kila kanisa na msikiti!!! Just spread good news that chadema will and can give you good life!! Semeni sera zenu

Mkijenga chama kuanzia ngazi ya mtaa au nyumba tano tano ndani ya miaka mitatu ijayo. muda uliobaki mngeanza operations zenu kama ile operation sangara! Wakati chama kina mizizi STOP THIS RUBBISH! Waberoya is saying stop this nonsense!!

Your mission should be

1. Jenga mizizi ya chama kuanzia nyumba tano tano
2. Piganieni tume huru ya uchaguzi ambayo HAMSEMI NA MKO KIMYA NA Kama uchaguzi uliopita mtaingia 2015 election na same Lewis makame na mtashtuka tu kuwa tume si huru wakati mmeshindwa!!! This is sick!!

6. If CCM said the same what is new?

Moja ya vitu walichofanikiwa CCM ni kupokonya hoja zote za CDM na kuzifanya zao.Juzi CCM wamesema wanajivua gamba, hata kama ni uongo kwa mtu wa kawaida leo HII anajua kumbe mission ya chadema na walichofanya CCM ni kile kile hawawataki mafisadi. CCM wameanza katika hili kama wiki moja tu iliyopita leo hii CDM wanasema karibu same theme ya CCM!!!! Think! Think! Think! Where is your political tactics??

Kwa sababu society ya Tanzania inapenda umbea.majungu na habari za kusikia KWANI HAYA NDIYO FARAJA YAO KWENYE DHIKI ZAO BASI NA NYIE ILI MUONEKANE WAZURI NI KUSEMA UDAKU NA UMBEYA ILI MMPENDEKE; kusema kile kitu ambacho wengi watakifurahia-tofauti ya chadema na shigongo ni ipi??!! Lakini kesho CCM wakisema zuri kwa watu walewale wanabadilika that makes point yangu namba 5 muhimu sana kuliko chochote mnachofanya hivi sasa!


7. STOP DECEIVING PEOPLE
Kuwadanganya watu kuwa katiba inaweza kubadilishwa within the next two years is a lie and you must stop? Stick on making a new election committee!!! Acheni kudanganya watu

8. Slaa's Frustration
Alifikiri atakuwa rais maskini kaukosa, alifikiri atapendeka kila kona, maskini jamii Fulani zin mkataa! Je kuongeza idadi ya mafisadi kwenye list yako ni kuonyesha haumchukii Kikwete? ( siri hii), na ni kuonyesha your neutrality in issues?

9. Is this all?

Kama kutaja mafisaid ndio priority ya chadema is this all?? Je mmemaliza wote? Wako wapi akina Nimrod Mkono? Is he clean au kwa sababu ni mwana sheria? Je mmewataja akina Lawrance Masha>akina Ridhwan kikwete? Yuko wapi Houseboy wa Makamba na housegirls wa majumbani mwetu? Au wizi ukifanywa na watu wa chini sio wizi na ukifanywa na viongozi ndio wizi? Je viongozi wanatoka wapi? Ni lini Slaa atajua kuwa ni system ambayo ina fuga wezi na wako millions!?

10. Kuchoma moto vibaka

Nataka uvute pumzi na kushusha taratibu1 Ikiwa sisi woote humu hatupendi kuona vibaka wakichomwa moto, na Slaa na wanasheria wengine watakubaliana na mimi.

Je kuna tofauti gani ya kumtaja Fulani ni mwizi publicly na kumchoma moto kibaka? Kumtaja mtu hadharani kuwa mwizi sio kuchukua sheria mkononi! Mkisema majaji ni walewale,je si mna-promote watu kuchukua sheria mkononi? Mbowe atapona? Aliyekopa hela za viinua mgongo na akashindwa kurudisha


Chadema semeni lingine move zenu bado hazija ni convince mimi, na sitawapa nchi hii mpaka nimeridhika mnafanya mambo kiakili na si kukurupuka!

Mwisho; hii ni mwisho kuwasadia kufanya siasa za nyakati, wakati na mkakati! Will not teach you again as you are cheating people again!

You are not helping society at all just seducing them because they love to hear that!!

 
First,they dont have to waste their time to convince you.Second,a long article with virtually no alternative to what Chadema have done so far.Third,two wrongs do not make a right.Kwa vile ufisadi unaanza kuonekana kama sehemu ya maisha ya kila Mtnzania si sababu ya kuuachia uendelee.Hata malaria imekuwepo miaka nenda miaka rudi na takriban kila mkazi wa ukanda wa joto ameshawahi kuumwa malaria lakini mapambano bado yanaendelea.Finally,who gave you the mandate to talk on behalf of the society?It's doesnt need a genius to figure it out that Tanzania would have been witnessing mfululizo maandamano against Chadema/Slaa had the society been against Dkt Slaa's seduction.Unfortunately for you,kinachojiri ni kinyume chake.Acha kutukana akili ya Watanzania.Hawahitaji kutongozwa na Dokta Slaa kukubaliana na anachosema.

Sorry,it's you who are cheating on yourself lakini you end up accusing Dkt Slaa.Why fix if it's not broken?Wanaohitaji ushauri-japo wa wa ovyo ovyo-ni hao wanaojivua magamba.
 
do not generalise that every person in tz is connected to ufisadi! this is a phenomenon commonly accepted and practiced by ccm! kild our everything! a national of 42 mln of no even a bank!NUTS!
 
unapaparuka tu badala ya kusoma taarifa vizuri watuma taarifa wamesema DR Slaa amesema wana CCM na chama ni mfu kinahitaji kunq'olewa wakatoa na mifano ya watu wengine ambao wanatakiwa pia wajitoe magamba unakuja na stori ndefu na chuki yako kwa DR Slaa kila mtu anakujua unachuki binafsi
Hivi ulitaka Dr Slaa aingie kwenye ushindani akijua kwamba atashindwa una inda weye mara kwa mara unaongea sana DR Slaa kugombea uraisi unaumia sana unasababu zako ambazo hutaki kuzisema au unatumwa ukidhani utaweza kumchafua kila mara umepiga mweleka kugombea kwake kumeleta manufaa kwa chama chake hata kama wewe hujawa convinced haituhusu sisi hayo ni matatizo yako
Umeambiwa watakuwa TBR kwa wiki kwa maoni yako msomi mzima unadhani watakuwa wanacheza kiduku au watakuwa kwenye mission za kujenga chama
unabore sana kwa kuanzisha thread za mtu mmoja 24/7 kama vile unaandikia thesis michango yako ni personal attack you are simply a hater
 
Back
Top Bottom