Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Ni vema kwa wanachama na wapenzi wa cdm kumshukuru sana slaa, kwa alivyoweza kufanikiwa kukipandisha hadhi na umaarufu chama hicho. Aidha ni vema wakajua kuwa in long run, slaa anapaswa kukaa pembeni kwa sustainability ya chama hicho.
 
Wewe waberoya unaonyesha kuwa na uwezo mzuri sana wa kupandikiza propaganda za
udini dhidi ya DR SLAA na dhidi ya CHADEMA na ndio maana umeng'ang'ania sana hii hoja ovu
dhidi ya DR SLAA.

Hili swala la DR SLAA limezungumziwa na watu wengi kwa mapana na marefu kiasi cha
kushangaza mtu mwenye uwezo wa kutoa hoja kwa mtiririko mzuri kama wako, bado
anaweza akawa bado amekengeuka na kuendelea kushikia bango upuuzi huu.

Ntakuuliza maswali kadhaa.
Kwa kumpinga DR SLAA kutokana na imani yake, je inamaanisha kwamba waislamu hawako tayari
kuona nchi hii ikiongozwa na wakiristo? ndio, je vipi wakirsto nao wakianza kuongea hadharani kwamba
wasingependa kuona muislamu akiongoza nchi hii? kumbuka vihere here kama vyenu vikizidi sana
vinaweza kusababisha watu wakaachana na misingi yao ya kuangalia, kuchambua na kuamua mambo
ili kuenda sawa na misingi iliyoshamiri katika jamii.

Hii nchi sio ya kiislamu, kwa hiyo ni makosa kabisa kwa kikundi chochote kukaa na kufikiria juu ya
namna ya kuwafurahisha, kuwainua, waislamu kwa misingi ya kisiasa, na hii sio kwa waislamu tu
bali pia wakirsto na dini nyingine yoyote ile. Hivyo ni makosa kabisa kwa mfano, kwa CHADEMA kuwa
na agenda ama mkakati wa kichama wa kujisafisha dhidi ya uchafu wa udini wanaotupiwa,

Nchi hii ina watu wenye imani za dini tofauti tofauti, wote tunalazimika kuheshimu hilo, na
haitakiwi kumbagua mtu yeyote kutokana na imani yake, Hivyo Waberoya, CCM, pamoja na waislam
wachache waliokengekuka mkae mkijua kwamba mnachokifanya dhidi ya DR SLAA ni ubaguzi ambao
haujawahi kuonekana wakati wowote katika historia ya nchi yetu, mnamkataa mtu asitumie haki
yake ya kikatiba ya kuwa kiongozi kwa sababu ya dini yake.

Hivyo, Kama wewe waberoya umeona kwamba Dini ya DR SLAA ni tatizo kwa chadema, unatakiwa
kwa nguvu zako zote upaze sauti kwa watanzania na kuwaeleza kwamba propaganda za kidini dhidi
ya CHADEMA ni uovu usio na mantiki, na wote wanaotapakaza uchafu huu ilitakikana wachukuliwe
hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.

Hivyo waberoya, hapa unaadress an informed audience, nenda misikitini ukawaeleze wanachokifanya
waislamu ni jambo la dhihaka, aibu, la kijinga, kinyume cha katiba, ni ukosefu wa utu na staa,ni
kinyume cha misingi ambayo mwalimu nyerere alijitahidi kuijenga katika nchi yetu mpaka siku
anakwenda kaburini. uwaeleze kwamba wasiwasikilize wote wanaopita uko na kusambaza propaganda
hizi ovu dhidi ya usalama, mila, desturi na ustaarabu wa kitanzania.

Uwaeleze kwamba CHADEMA wapo pale kwa ajili ya kupigania maendeleo ya taifa hili bila ubaguzi
wa aina yoyote ile, na wanafanya hivyo kwa sababu wanadhani kwamba CCM imeshindwa, wawapime
katika hayo, kama wanaona CCM wanaweza basi wawaunge mkono kama wanaona CHADEMA wataweza
basi wawaunge mkono na wakati wote si katika misingi ya dini katika namna yoyote ile.

Nenda Waberoya.
 
Wabe,
Nilitamani ungenijibu nilichokuuliza hapo juu, anyway tusonge mbele..
Ukiweza nisaidie hili;..
1. UNA UFAHAMU WA KITU PROPAGANDA?
2. JE UNADHANI IKITOKEA AKAWEKWA MGOMBE MWISLAM HUKO CDM, JE CCM NA BAKWATA WATASIFU?
3. UNAKUMBUKA WALICHOFANYIWA CUF 2000?
Kaka ninayo mengi ya kuuliza,na ninawasiwasi huwezi/unaweza kunitosheleza.. LAKINI PIA MAWAZO YAKO NAYAHESHIMU NA NIYAKUJENGA,INGAWA NI NGUMU SANA KUTOSHELEZA MATAKWA YA CCM,CHAMA KINACHOAMINI KILIUNDWA KUTAWALA MILELE..
Mwisho naomba nikuachie hii,; JE UNAFIKIRI MUNGU ANAWEZA KUKUBALI MATAKWA YA IBILISI ETI NAYE ATAWALE WALAU DAKIKA MOJA MUNGU AKIWA BENCH?
Wakondya!
 
Yaani mtu aliyewafanya wakubalike zaidi na kupata kura zaidi na kuwa chama cha kitaifa zaidi ndio aondolewe? Well.. itakuwa ni kufanya mambo kinyume nyume. Wenzenu wameondoa watu waliokiletea chama matatizo siyo waliokijenga. Sasa pendekezo kuwa Dr. Slaa aondoke kwa sababu ni tatizo - ni gumu kuliwekea msingi kwa sababu itabidi uangalie namba na kulinganisha namba uweze kusema kuwa Dr. Slaa ni tatizo.

Kama Chadema inataka ife kwa haraka na ikose hata nafasi ya pili 2015 basi ifanye hili unalopendekeza. Ukiniuliza mimi Dr. Slaa anahitaji kuwa mwenyekiti kabisa wa Chadema tena mtendaji. Na I have to admit it kwa sababu nilimuunga mkono na ninaamini kabisa kuwa Tanzania inahitaji mtu kama yeye kulipeleka taifa kunakotakiwa.

Slaa si kweli ndiye ameipa chadema kura nyingi ama amewawezesha kukubalika, kwa hali iliyokuwepo hata wangemsimamisha Zitto/Kitila angevuna kura nyingi kuliko hizo za Slaa.

Ukweli halisia ya kwanini wapinzani wamepata kura nyingi ama majimbo mengi,mnauzunguka ama hamtaki kuusikia kwa sababu zisioeleweka.

Ukweli ni kwa sababu wananchi walitegemea makubwa sana mwaka 2005 kutoka kwa JK, naye akawakatisha tamaa kabisa kwa kushindwa kutekeleza hata vitu vya msingi kabisa.

CCM, wanajaribu kujishebedua tu eti kwa kujivua gamba wakati wanafahamu kabisa ulemevu ulipo, na ndio maana utaona wazugazuga tu kwa kubadilisha hiki na kuweka kile. Wala mambo ya dowans, richmond si sababu ya kutosha yani ya kwamba kulipelekea ccm kupoteza mwelekeo ktk uchaguzi uliopita.

Sababu kuu, ni JK mwenyewe kushindwa kukidhi mambo ya msingi kabisa kama Rais wa nchi na hiyo ndo sababu kuu.

Ukitaka kuona kama CHADEMA si lolote , ccm wafumbe macho tu waweke mgombea wa urais anayekubalika uone chadema itakovyo sita kukubalika.
 
Waberoya,

Usiwe na wasiwasi, kitu chochote kinapokua kwa kasi lazima kiwe na challenges na CHADEMA ndiyo ipo kwenye hiki kipindi cha mpito. (kutoka wabunge 4 hadi 26 ni zaidi ya 600%).

Na ndiyo maana zinaanzishwa hoja toka kwa watawala kukififisha na wanajua fika kwamba DR. Slaa ni tatizo / Kizingiti kikubwa sana kwao na ndiyo maama wamefikia uamuzi mgumu wa kujivua gamba, wakitafuta kujiosha katika macho ya wananchi baada ya kupoteza imani kwao.

Ukimwondoa DR. Slaa kwenye uongozi kwa hoja ya udini, litakuja la ukabila kwamba CHADEMA ni chama cha Wachaga huku unamlenga Mbowe. Baada ya hilo litaibuka na lingine kuwa CHADEMA ni chama cha wasomi tu na mengine mengi tu as long as CHADEMA inakubalika kwa wananchi.

Cha msingi hapa ni CHADEMA wakitumia wabunge na madiwani wao kuwaelimisha wananchi waelewe kwamba hizo ni propaganda, uzuri wananchi wanachotaka ni maendeleo hawataki kusikia chochote kuhusu dini, dhana ya udini ipo ndani ya watawala na baadhi ya watu wanaotumiwa na watawala kupandikiza hoja hii na zingine kuuwa upinzani ili watawale milele.
 
Kwanza ni vema ufahamu CHADEMA haiigi na haitkaa iige kile CCM wamefanya kujiita kuvua gamba

Pili kama unadhani Dr. Slaa amepoteza turufu za CDM kwa background yake basi you are living out of the real world...

Wajinga tu ndio waliobaki na agenda zenu za kipuuzi za udini....you loosers.....

Na tatu CDM ndio kimbilio la wale wanaotimuliwa CCM wengi tu wapo CDM baada ya kukosa waliyokuwa wanayataka CCM kama nakosea naomba nisahihishwe na wala sitashangaa hayo magamba/makapi yakitimkia CDM.
 
Wabe unachotaka ni kwamba cdm wamuweke katibu mkuu muislamu au ni kwamba dr. Slaa (Phd) hafai? fafanua tafadhali
 
Ro salaleee kaka Wabe!....Hivi unawezatuwekea hapa ushahidi ambao tutaona waislaam wote wa Tanzania kuwa hawaipendi CDM?
Hivi ulishaongea na waislaam mmoja mmoja kuzunguka Tanzania yote na wakakuambia hawaitaki CDM? Au na wewe ndiyo walewale mliolishwa sumu za udini na wewe ukaziweka akilini?....kwa taharifa yako waislaam wengi sana wanaipenda CDM....na sasa waliowengi wameshafahamu kuwa NENO UDINI ni propaganda za CCM na watu kama wewe kaka Wabe. Kuhusu Dr Slaa kuwa mgombea urais wakati amewahi kuwa padre....hiyo nayo haiingii akilini hata kidogo. Maana hata huko Haiti mwanamziki mstaafu alipojitokeza kugombania kiti cha urais alikumbana na propaganda kama hizi ambazo leo mnamvika Dr Slaa na chama chake....lakini mwisho wa siku wananchi wa Haiti wakapuuza mapropaganda yote na wakaamua kumchagua mwanamziki mstaafu kuwa ndiye rais wao na hatimae ameshinda urais.
Mwisho kumbuka hata kule Kenya,Malawi,Egypti,Zambia,Botswana,Tunis, Ivory coast na Libya kulikuwa na watu wabishi na wapropaganda kama wewe....lakini mwisho wa siku woooote walizolewa na kimbunga kikali cha demokrasia ya NGUVU YA UMMA. Tafakari kaka....
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
Nadhani Chadema watakuwa wanakosea sana kumuondoa Dr. Slaa kwa vile Waislamu (wachahche) hawamtaki. Hapo watakuwa wanaingiza misingi ya udini katika siasa. Ninaaamini kuwa CDM inatetea maslahi ya Watanzania wote bila kujali dini, rangi au kabila. Jambo hili linatakiwa lifahamike kwa kila Mtanzania, aidha awe Mkristo, Muislam, Budha n.k. n.k.. Ina maana kuwa kiongozi mwingine atakayechukua nafasi ya Slaa itabidi naye awe Muislamu tu? Atawekwa hapo kwa misingi ya dini au uwezo wake wa kisiasa?
 
Slaa si kweli ndiye ameipa chadema kura nyingi ama amewawezesha kukubalika, kwa hali iliyokuwepo hata wangemsimamisha Zitto/Kitila angevuna kura nyingi kuliko hizo za Slaa.

Ukweli halisia ya kwanini wapinzani wamepata kura nyingi ama majimbo mengi,mnauzunguka ama hamtaki kuusikia kwa sababu zisioeleweka.

Ukweli ni kwa sababu wananchi walitegemea makubwa sana mwaka 2005 kutoka kwa JK, naye akawakatisha tamaa kabisa kwa kushindwa kutekeleza hata vitu vya msingi kabisa.

CCM, wanajaribu kujishebedua tu eti kwa kujivua gamba wakati wanafahamu kabisa ulemevu ulipo, na ndio maana utaona wazugazuga tu kwa kubadilisha hiki na kuweka kile. Wala mambo ya dowans, richmond si sababu ya kutosha yani ya kwamba kulipelekea ccm kupoteza mwelekeo ktk uchaguzi uliopita.

Sababu kuu, ni JK mwenyewe kushindwa kukidhi mambo ya msingi kabisa kama Rais wa nchi na hiyo ndo sababu kuu.

Ukitaka kuona kama CHADEMA si lolote , ccm wafumbe macho tu waweke mgombea wa urais anayekubalika uone chadema itakovyo sita kukubalika.
Kwa minajili ya mjadala, ni nani huko CCM anayekubalika ki hivyo?
 
Sasa baada ya JK kuwa-let down,kwanini wasingeamua kumpigia kura Mrema,au Prof Lipumba au Dr Mvungi au Dovutwa? Ah siasa nazo bana!
Slaa si kweli ndiye ameipa chadema kura nyingi ama amewawezesha kukubalika, kwa hali iliyokuwepo hata wangemsimamisha Zitto/Kitila angevuna kura nyingi kuliko hizo za Slaa.

Ukweli halisia ya kwanini wapinzani wamepata kura nyingi ama majimbo mengi,mnauzunguka ama hamtaki kuusikia kwa sababu zisioeleweka.

Ukweli ni kwa sababu wananchi walitegemea makubwa sana mwaka 2005 kutoka kwa JK, naye akawakatisha tamaa kabisa kwa kushindwa kutekeleza hata vitu vya msingi kabisa.

CCM, wanajaribu kujishebedua tu eti kwa kujivua gamba wakati wanafahamu kabisa ulemevu ulipo, na ndio maana utaona wazugazuga tu kwa kubadilisha hiki na kuweka kile. Wala mambo ya dowans, richmond si sababu ya kutosha yani ya kwamba kulipelekea ccm kupoteza mwelekeo ktk uchaguzi uliopita.

Sababu kuu, ni JK mwenyewe kushindwa kukidhi mambo ya msingi kabisa kama Rais wa nchi na hiyo ndo sababu kuu.

Ukitaka kuona kama CHADEMA si lolote , ccm wafumbe macho tu waweke mgombea wa urais anayekubalika uone chadema itakovyo sita kukubalika.
 
Na tatu CDM ndio kimbilio la wale wanaotimuliwa CCM wengi tu wapo CDM baada ya kukosa waliyokuwa wanayataka CCM kama nakosea naomba nisahihishwe na wala sitashangaa hayo magamba/makapi yakitimkia CDM.

Kuna watu wamefukuzwa CCM? Mimi nadhani ni re-shuffle ya kawaida tu - recycling CCM style.
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

waislamu wasioitaka chadema eti tu kwa sababu dr ni mkristo ni wale tu waliokubali, kutiwa ujinga na propaganda za udini za ccm, au wale ambao wanafaidika moja moja kwa ccm kuwa madarakani, kwa hiyo waache waendelee kutoitaka, kuna mabo ya muhimu zaidi ya kushughulikia kuliko ku deal na watu wa aina hiyo.
 
Nadhani Chadema watakuwa wanakosea sana kumuondoa Dr. Slaa kwa vile Waislamu (wachahche) hawamtaki. Hapo watakuwa wanaingiza misingi ya udini katika siasa. Ninaaamini kuwa CDM inatetea maslahi ya Watanzania wote bila kujali dini, rangi au kabila. Jambo hili linatakiwa lifahamike kwa kila Mtanzania, aidha awe Mkristo, Muislam, Budha n.k. n.k.. Ina maana kuwa kiongozi mwingine atakayechukua nafasi ya Slaa itabidi naye awe Muislamu tu? Atawekwa hapo kwa misingi ya dini au uwezo wake wa kisiasa?

Ukifuatilia michango ya watu kwenye thread hii, sio vigumu kuona jinsi UKRISTO ulivyo kwenye Chadema. Watu wanatetea Chadema sio kama chama cha siasa ila kama dini na Slaa Padre wao! Hivyo ni vigumu kuona kasoro kwa 'nabii' wao!
Wabe anasema Slaa ni DIVISIVE person kutokana historia yake.
Bila kuleta utani hapa, HAKUNA muislam mwenye akili timamu na imani yake akaimba kwaya moja na Wana CHADEMA wa humu!
NI vigumu kwa Chadema kushinda kwa mazingira ambapo ina alienate zaidi ya 50% ya wapiga kura. Kuamini kuwa Chadema itashinda tuu bila kujivua gamba la udini ni UJINGA! Swallow it men, hata kama chungu!
 
Dr Slaa ana UDINI gani? Hivi kweli angekuwa mdini angeuacha upadre ambao alikuwa anaelekea kuwa Askofu? Makatibu Wakuu wengi wa TEC wamekuwa Maaskofu. Au ni yaleyale ya Mrema na NCCR mwaka 1995 yanataka kuanza?
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

My friend there is nothing you can do to control political prejudices. Ilianza na Ukabila/Ukanda ikaisha, tulipompumzisha Mbowe wamekuja na UDINI. Hakuna hoja katika kumtoa Dr Slaa. Ukweli uko wazi huwezi kulinganisha hali ya CDM na CCM au Makamba na Slaa.

Nina maana chochote kitakachofanyika hali itarudi kule kule. Na CCM na vibaraka wako wapo kutengeneza mazingira hatarishi kwa wapinzani wa KWELI.

Maoni CDM iendelee kuelimisha watanzania kwa nguvu zaidi. walionunuliwa kama hawa "waislam uchwara" wataelimishwa na waislamu wenzao kuwa wanatumiwa na CCM kama magogo ya chooni. Na hali imekuwa hiyo toka zamani za uhuru.

SLAA NI RAIS WA KIZAZI HIKI NA KIJACHO. hakuna jinsi.
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

That is being addressed by the coming in oof Prof Safari, ondoa shaka ya hilo.
 
Waberoya,

Mkuu Umetoa mawazo yako.nadhani suala la kumuondoa Dr.Slaa ni tofauti na la CCM kujivua gamba.CCM kulikuwana ufisadi na ombwe la fikra
(ingawa bado upo tena hatari zaidi kwa ma-pro walioteuliwa) katika uongozi wao,kitu ambacho wamekiri na ni kitu cha kweli ingawa sioni mantiki yao ya kujivua gamba kwa maana ya aina ya uongozi waliouweka.Wamejivua Gamba wakabaki uchi,hawataweza kutembea sasa

Back to the issue,Tuhuma za udini na ukabila hazina ukweli wala mantiki yoyote,inaonekana kwenye hoja yako na au kama kwa uhakika CHADEMA itaamua kutekeleza uliyosema basi CHADEMA itakuwa imebariki Ukabila na udini.Itakuwa sasa imevaa gamba la udini na ukabila philosophically.Ni hayo tu otherwise,good day!!!
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

kwa vile unafikiri waislam hawawataki chadema, na unafikiri chanzo ni dr wa ukweli. ulikuwa unashaurije?
 
Mkuu wewe umeona mbali sana!! Huyu mtu Slaa inabidi aondoke,, hakuna jinsi, na baadaye Mbowe ili Chama kiwe safi kabisa.

Yaah ni kweli kabisa Analytical...halafu pia aondoke Mnyika,Lema,Lisu,Mdee nk....halafu Uenyekiti tumpe zitto..ukatibu Shibuda...makamu mwenyekiti...tumsajili makamba senior si ameachwa ktk usajili...na makamu Katibu mkuu tumrudishe Shitambala...hapo vipi?
 
Back
Top Bottom