Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Mzee Mwanakijiji,
Mkuu hilo la Dr.Slaa kukutana na viongozi wa kiislaam na kuwahakikishia ama kuwatoa hofu hiyo sikumbuki kulisikia na ndio swali kubwa nilokuwa nikikabiriana nalo Bongo hasa nilipokuwa ktk vijiwe vyetu vya K. Tea shop..Waislaam wengi walitaka kujua Dr.Slaa ana msimamo gani kutokana na tuhuma zinazotolewa kwa sababu muda wote mashambulizi yanatoka Upande wa CCM na Masheikh hali Dr.Slaa na Chadema wamekaa kimya..

Sasa kama Dr.Slaa amewahi kukutana na Masheikh naomba unipe siku na mahala na alikutana na kina nani na mazungumzo yalihusu vitu gani haswa..Unajua unapogombania Urais ni muhimu sana kutembelea makundi ya watu kama hawa hasa wale wanaokupiga vita na utegemee maswali magumu ambayo yanaweza hata kukebehi imani yako..

Dr. Slaa anatakiwa kujijenga zaidi kisiasa na atakapoweza kukabili swala hili basi bila shaka atakuwa ni kiongozi tunayemhitaji nchini, kiongozi asieyona aibu wala kuhofia kukabiliana na changamoto hizi za Udini au Ukabila..Na hakika JK pamoja na mengi alojaribu kuyafanya udhaifu wake mkubwa upo ktk kukabiliana na maswala magumu ambayo kashindwa kabisa kuyafuatilia wala kuyapatia jibu...

Tanzania leo inapwaya ktk makusanyo ya kodi na inapwaya ktk matumizi makubwa ya serikali - na yote haya yametokana na udhaifu wa kiongozi mwenyewe kushindwa kukabiliana na matatizo hata iwe kwa kukemea madudu ya washirika wake.

Hii ilikuwa ni mwishoni mwa Septemba (kati ya Sept 29, na 30) makao makuu ya Chadema:

slaa-1.jpg
 
Mkandara kwa mara nyingine umerudisha taste kwenye JF, I strong admire the articulation of your point, that shows maturity and braveness. Kudo mzee.

Politics ni kama mchezo, and sometime you have to play dirty to win. Hakuna swala la unfair kwenye politics, CDM needs to learn that. CCM will use every tactics kushinda mchezo, they will lie, steal and everything in between ili washinde. Na mchezo wa kuifunga CDM na Roma umefanikiwa kwa asilimia kubwa sana. CCM won that battle and CDM wanashindwa kutafuta methodology ya kusawazisha.

Kuwasaidia wale wengi ambao wanaangalia CCM katika national level, ambapo siasa bado nichanga sana nitawapa mfano wa Marekani. Mwaka 1960 John F. Kennedy alikuwa mgombea kupitia chama cha democratic na Richard Nixon alikuwa mgombea kwa Republican. Ikumbukwe ya kwamba Evangelical Church ni maarufu sana kusini mwa America, na JFK alikuwa ni mkatoliki, hivyo Republican walitumia njia chafu kwamba ukimchangua JFK maanayake Papa na Kanisa katoliki wataongoza America. Na swala hilo liingia vichwani kwa waamerica walio wengi. JFK baada ya kuona kwamba vita hii inamzidi aliamua kuchukua risky direction ya kufanya mdahalo na mapadri wa Evangelical church maharufu kama Houston Ministerial Association. In the end it pays off, this is what he said "I am not the Catholic candidate for President. I am the Democratic Party's candidate for President who also happens to be a Catholic. I do not speak for my Church on public matters — and the Church does not speak for me."

Alichofanya JFK ni kuondoa hofu kwa watu kwamba yeye ni mroma lakini ataingia madarakani kutetea haki za wamarekani wote kwa sheria ya katiba ya marekani. Nimeeleza hichi kisa sababu kinashaabiana na njia wanayotumia CCM na kukaa kimya hakuisaidii CDM bali kunaiweka pahala pagumu.

Mchezo uliobaki ni kwa CDM na DR. Slaa kufanya mdahalo na Mashehe, Maimamu na mamufti wa Tanzania. Mdahalo ambao CDM itawaruhusu mashehe wazungumze hofu zao na mashaka yao na CDM itazijibu. Hii itapunguza makali.... I know it's a hard choice, lakini leaders need to make tough choices na hiyo ndio tofauti ya JK and Obama, tough choices. Sasa kama Slaa anataka kuwa among the great leader this is an opportunity kuprove kwamba he can meet the challenge bar.

CDM wanatakiwa watembelee mikoa ya Kusini na zanzibar, sio kwa kufanya maandamano bali kuongea na hawa mashekhe kwa karibu. You don't cure ugonjwa kwa kukataa dawa, unakunywa hata kama ni chungu.....
Nakubaliana na hoja,hata Obama alikwenda kuwatembelea ma evangelical kama kina Billy Graham na wengieneo ili kuwatoa ile hofu kuwa ni muislam nk.
Sijui walichoongea,hata hivyo sidhani kama sisi wabongo tunaweza kufanya hivyo,sanasana bongo pesa ndo huzungumza zaidi.Sijui nia halisi ya hao masheick,kama ulivyosema inawezekana wanatumiwa kisiasa.Kwa misingi hiyo,inawezekana pia rushwa imetumika towards hao viongozi wa kidini.Tulishuhudia sakata la Mtikila na RA,na ndio maana nahisi mazingira hayo hayo yamejenga huu msimamo wenye hila za kidini.
Kusema eti CHADEMA imuondoe Dr Slaa ndiyo kuchochea udini zaidi,yani ni kumwaga fuel on fire ukitegemea unaizima.
Kama mnakubali kuwa nchi yetu huwa inaendeshwa kwa hila za kidini,then ina maana mnataka favoratism ya kidini iendelee kwenye siasa.Maamuzi yoyote ya kujenga chuki kwasababu tu mtu ni muumini wa dini yatofauti hayajengi bali yatazidi kubomoa.
Wengine mnaotoa ushauri sijui nia yenu haswa,however,ushauri ungeukuwa umetolewa kwa chama cha CHADEMA kufanya mabadiliko ya kimfumo,maybe wengi wetu tungeelewa zaidi,lakini hili la kusema eti kumwondoa Slaa kutaijenga CHADEMA zaidi kwangu mimi ni pointless.
Na wakristo nao wakianza kuhoji waislam waliokwenda Hija,ama wale wenye sifa za Usheick nk kuwa hawafai kuongoza mtasemaje?
 
Nafikiri ni vizuri ukafanya utafiti ukajua ni mali ngapi za wakristu zimerudishwa mikononi mwao ni ngapi au ni asilimia ngapi na zilizopo kwenye mikono ya serikali bado ni asilimia ngapi.

Lakini pia kwa uelewa wangu mali nyingi zilizorejeshwa mikononi mwa kanisa ni kanisa lililoingia kwenye gharama ili kutoa fidia kwa serikali. Kama wamerejeshewa shule basi kwanza ni kanisa lilijenga shule nyingine na kupewa shule yake ya zamani iliyotaifishwa na serikali.

Mali nyingi za waislamu ziko mikononi mwa CCM kwani zilitaifishwa na TANU na siyo serikali iliyokuwa inaongozwa na TANU. Pia hebu tupeni "Orodha" ni mali zipi za waislamu ambazo bado zinashikiliwa na serikali kama siyo CCM!!
Mkuu wangu hata sikuelewi kabisa unaposema mali za Waislaam zimeshikiliwa na CCM sio serikali... Kisha unasema mali za Wakristu zilichukuliwa na serikali na kurudishiwa na serikali ila za Waislaam zimechukuliwa na TANU, sijui ni wakati gani unazungumzia haya... yaani hapa hata sikuelewi kabisa..TANU au CCM nani na serikali nani..
 
Hoja ya Weboyra inayodai kuwa Waislam hawaipendi au hawaitaki Chadema ni hoja isiyo na nguvu katika jamii yetu. Chadema ilipoanzishwa, haikuwa na mandate ya kupendwa au kukubalika na dini fulani. Na wala chadema haikuanzishwa msikitini, na wala chadema haiwezi kwenda kuhubiri makanisani au kutoa mihadhara misikitini kwa sababu hiyo siyo sehemu yake.

Katika utawala wa sheria na ukuaji wa demokrasia, huwezi kumlazimisha mtu au kikundi fulani kukipenda chama chako. Sera za chama ndiyo shughuli zake hapa, mtu akipenda sera za chama naamini atasukumwa na hizo sera kujiunga na chama no matter is muslim, christian, buddha or pagan.

Sina hakika kama kweli waislam hawaipendi Chadema, mambo ambayo Chadema inapigania kama vile maisha bora, kupinga rushwa, ufisadi na kuendeleza uwajibikaji, kuwepo uwazi kwenye mikataba ya serikali n.k ni mambo ambayo yanamgusa kila mtanzania bila kujali dini, kabila, jinsia. Kuwepo kundi ndogo ambalo CCM wamekuwa wakiwatumia kwa propaganda za kidini hakuwezi kuwakilisha jamii nzima ya dini inayohusika.

Hata huko Misri ambapo majority ni waislam wakati wanafanya yale mageuzi Tahriri square, walisema yale mageuzi ni ya wananchi wote (waislam na wakristo). walikataa kabisa ajenda ya Muslim Brotherhood walipotaka ku-take advantage ya yale mageuzi.
Kama kuna watu au kikundi hakiko comfortable na chama fulani, kinaweza kuanzisha chama chake au kujiunga na vyama vingine kama NRA. Katiba ya JMT inawaruhusu kuanzisha chama cha siasa iwapo watafuata sheria. Hatutaki kikundi fulani kuja kuamulia jamii fulani nini cha kufanya au chama gani kujiunga. Walijaribu kipindi fulani lakini hawakufaulu, hii ni Tanzania tofauti.
 
mkuu wangu hata sikuelewi kabisa unaposema mali za waislaam zimeshikiliwa na ccm sio serikali... Kisha unasema mali za wakristu zilichukuliwa na serikali na kurudishiwa na serikali ila za waislaam zimechukuliwa na tanu, sijui ni wakati gani unazungumzia haya... Yaani hapa hata sikuelewi kabisa..tanu au ccm nani na serikali nani..
pole!!
 
Hii ilikuwa ni mwishoni mwa Septemba (kati ya Sept 29, na 30) makao makuu ya Chadema:

View attachment 27153
Alikutana na kina nani maanake navyojua mimi Pinda ndiye alikwisha kutana na baraza la Waislaam waliochaguliwa kukutana naye na wakampaka kishenzi kiasi kwamba watu kama Othman Matata waliondolewa ktk kundi la watu waliokwenda kumwona..Ningependa sana kumsikia Dr.Slaa mwenyewe akinieleza haya na ingekuwa vizuri zaidi kama makutano haya yangekuwa live on TV ili ushahidi uwepo wazi...

Nilipokuwa Bongo nimekutana na wanaharakati wengi wa Kiislaam pamoja na Masheikh ambao wanamkataa kabisa Dr.Slaa kwa sababu wamepandikizwa chuki kwa vibahasha vya CCM na nimepata habari zaidi kwamba sio tu Masheikh ila hata viongozi wa kikristu wamechukua vibahasha ili kueneza Udini..

Hivyo mkuu wangu msifanye mzaha kabisa na jinsi CCM walivyojipanga kumwondoa Dr.Slaa katika picha kama walivyojaribu kwa Mbowe na kifo cha Chacha Wangwe.. hawa jamaa wako tayari kuyaondoa maisha ya mtu ili mradi kujenga hoja..Wangwe aliuawa, aliyemuua wanasema ni Mbowe, huyo Mbowe asifunguliwe mashtaka wala asifungwe na yule aliyesababisha kifo - tunaambiwa ni comandoo, kapigwa kifungo kifupi... hivi kweli a case of murder kwa Tanzania nayoijua mimi mtu anaweza kutoka kirahisi namna hii..CHUNGUZENI...CCM walimdhania Mbowe kuwa mgombea wa CDM 2010, lakini CDM was one step ahead of CCM on that..
 
Mkandara, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kwa angle ambayo umekuja nayo; na hii inahusu Mtazamo ambao umejengeka kwa muda mrefu na ambao umejengwa kwa muda mrefu. Hata hivyo tatizo linabakia pale pale, kama tukikubaliana na Waberoya kuwa Dr. Slaa aondoke kwa sababu Ukatoliki wake ni tatizo kwa Waislamu ambao wanahusisha Ukatoliki huo na Uongozi wa Kanisa Katoliki je, Mkatoliki yeyote ataweza kuwa na nafasi ya uongozi ndani ya Chadema? Siyo hivyo tu itakuwaje kama Mch. Manase au Msigwa wakitaka kugombea nafasi za uongozi ndani ya Chadema, je wakataliwe kwa sababu wao ni wachungaji?

Sijui mimi Wilson Mukama wa CCM ni dhehebu gani, tuchukulie kuwa Mkatoliki je anastahili kuwa katika nafasi hiyo? au atatumiwa na Kanisa Katoliki ndani ya CCM? Au kwa vile hajawahi kusomea Upadre?

Mimi nadhani tuwe waangalifu katika msingi tunaotaka kuweka, kama kuna tatizo la utendaji ambalo liko bayana ambalo Dr. Slaa anahusishwa nalo ni lazima achukuliwe hatua na kama ni tatizo la udini - sema kwa mfano kama Katibu Mkuu amekuwa akiwabagua Waislamu, akiwanyima nafasi, n.k n.k na ikathibitishwa hivyo basi atakuwa ni mdini na hana nafasi ya uongozi. Lakini kusema mtu aache kuwa kiongozi wa Chadema kwa sababu aliwahi kuwa Padre au kwa sababu ni Mkatoliki tunaingia kwenye eneo baya sana ambalo sijui tutatokaje?

Unafikiri Dr. Slaa aondolewe Ukatibu Mkuu kwa sababu baadhi ya Waislamu inadaiwa wana matatizo na Ukatoliki wake au historia yake ya kuwa aliwahi kuwa Padre?

A false start is worse than a bad start.

Hatuwezi kujenga hoja kama hoja zetu tumezijenga kwenye mchanga. Hatuwezi kumhukumu mtu kwa historia ya utumishi wake. Kwamba Slaa alikuwa Padri, haina tofauti kama Kikwete alikuwa katibu wa TANU Masasi at some point in his career. Only that at some point in their lives..they decided differently. Kumnyima mtu fursa ya uongozi kwa sababu ya imani yake..that will be the turning point in the history of our country.

Mimi naona kama baadhi ya viongozi wa kiislamu na mashekhe wangekuwa objective tungekubali kwamba wana legitimate fear dhidi ya Slaa na 'mfumo kristo' as they call it. Lakini inaonekana support yao kwa JK ni simply kwa sababu ni 'mwenzetu'. Ndo maana mwanakijiji ameuliza mara nyingi humu: Urafiki wa viongozi na baadhi ya waislamu na CCM ulianza lini?? kipindi cha Nyerere, Mwinyi, Mkapa au JK? na kama wanalaumu kwamba wametengwa na kuonekana second class, je ni kipi kimebadilika leo hii? waone kwamba whoever is critical of JK is against their interests also?? After all we have had CCM kama chama tawala kwa miaka yote. Je sera za chama dhidi ya waislamu zimebadilika? Ukiondoa miwani yako kidogo tuu utagundua kwamba hawa wote wanaolalamikia system ni waganga njaa tuu.

Mfano ukienda nchi nyingine utakuta watu wanalalamikia udini kwa sababu wanatengwa hawapati fursa kwenye uongozi na mambo mengine katika nchi. Nenda Sudan, Egypt, Mauritania utaliona hili. Lakini hivi kweli Tanzania unaweza kuilinganisha na Sudan? Kwa kipi? Nani ameshauawa kwa kuabudu dini yake?? Leo hii Raisi wetu, Makamu wa Rais, Jaji Mkuu, Mkuu wa Intelligence, plethora of Ministers, Directors nk..ni waumini wa dini ya kiislamu. Wana nafasi nyeti ambazo zina-determine mwelekeo wa kila siku wa taifa letu. Sasa jamani kipi kifanyike zaidi ya hili? I sometime feel kwamba watu wanaolalamika kila siku..hawalitakii mema hili taifa letu! Tunalalamika kwamba Tanzania inatawaliwa na mfumo 'kristo' lakini ni akina nani wanaoongoza huo mfumo? Tangu uhuru huu mfumo umeongozwa na wakristo na waislamu. Hivi ni kitu gani kifanyike hawa wanaolalamikia mfumo kristo waone kwamba they are also INCHARGE??

Mi nasema if thats what will please some of these people. Kikwete appoint baraza lote la mawaziri waislam. Some of us..hilo halitusumbui kabisa. We believe in the old adage 'let who is able, serve'.

Inasikitisha sana kuona mtu kama Dr. Slaa is being hated and villified simply because of who he is! Ni kitu kibaya sana. Muhukumuni Slaa kwa matendo yake na wala si kwa pua yake, dini yake, urefu wake wala unene wake! At the end of the day na yeye ni binadamu kama mimi na wewe..ukimchoma msumari anatoka damu. Same I would condemn yeyote ambaye atamhukumu Kikwete kwa sababu ya imani yake. Muhukumini Kikwete kwa rekodi yake ya uongozi. Basi.
 
tenda wema wende zako!

katika watu ambao ni tishio kwa ccm na mafisadi ni dr w. Slaa, ninaamini baada ya nyerere mtanzania makini na kiongozi imara anayemfuatia mwalimu ni dr slaa. Zengwe la dr slaa limefanya think tanks wote tunaowamni tanaznia kujitambua mfano ulimwengu, shivji, lwaitama, maprof, madr kibao, lakini zaidi na kubwa ni jinsi dr slaa alivyoingia vichwani na miyoni mwa watanzania.

Wabe slaa ni moto mbaya na wewe unajua fika, chachu ya slaa chadema inatisha, ni rais aliyeporwa ushindi, ninachomlaumu slaa ni walk the talk -manake angeamua kusimamia haki kwa vielelezo vya kura alizoibiwa basi ccm ingekuwa kama ivory cost leo.

Ccm mshukuruni sana slaa vinginevyo mngeng'oka kwa nguvu ya umma trust me.

Dr slaa is our hero and our only man.
 
A false start is worse than a bad start.

Hatuwezi kujenga hoja kama hoja zetu tumezijenga kwenye mchanga. Hatuwezi kumhukumu mtu kwa historia ya utumishi wake. Kwamba Slaa alikuwa Padri, haina tofauti kama Kikwete alikuwa katibu wa TANU Masasi at some point in his career. Only that at some point in their lives..they decided differently. Kumnyima mtu fursa ya uongozi kwa sababu ya imani yake..that will be the turning point in the history of our country.

Mimi naona kama baadhi ya viongozi wa kiislamu na mashekhe wangekuwa objective tungekubali kwamba wana legitimate fear dhidi ya Slaa na 'mfumo kristo' as they call it. Lakini inaonekana support yao kwa JK ni simply kwa sababu ni 'mwenzetu'. Ndo maana mwanakijiji ameuliza mara nyingi humu: Urafiki wa viongozi na baadhi ya waislamu na CCM ulianza lini?? kipindi cha Nyerere, Mwinyi, Mkapa au JK? na kama wanalaumu kwamba wametengwa na kuonekana second class, je ni kipi kimebadilika leo hii? waone kwamba whoever is critical of JK is against their interests also?? After all we have had CCM kama chama tawala kwa miaka yote. Je sera za chama dhidi ya waislamu zimebadilika? Ukiondoa miwani yako kidogo tuu utagundua kwamba hawa wote wanaolalamikia system ni waganga njaa tuu.

Mfano ukienda nchi nyingine utakuta watu wanalalamikia udini kwa sababu wanatengwa hawapati fursa kwenye uongozi na mambo mengine katika nchi. Nenda Sudan, Egypt, Mauritania utaliona hili. Lakini hivi kweli Tanzania unaweza kuilinganisha na Sudan? Kwa kipi? Nani ameshauawa kwa kuabudu dini yake?? Leo hii Raisi wetu, Makamu wa Rais, Jaji Mkuu, Mkuu wa Intelligence, plethora of Ministers, Directors nk..ni waumini wa dini ya kiislamu. Wana nafasi nyeti ambazo zina-determine mwelekeo wa kila siku wa taifa letu. Sasa jamani kipi kifanyike zaidi ya hili? I sometime feel kwamba watu wanaolalamika kila siku..hawalitakii mema hili taifa letu! Tunalalamika kwamba Tanzania inatawaliwa na mfumo 'kristo' lakini ni akina nani wanaoongoza huo mfumo? Tangu uhuru huu mfumo umeongozwa na wakristo na waislamu. Hivi ni kitu gani kifanyike hawa wanaolalamikia mfumo kristo waone kwamba they are also INCHARGE??

Mi nasema if thats what will please some of these people. Kikwete appoint baraza lote la mawaziri waislam. Some of us..hilo halitusumbui kabisa. We believe in the old adage 'let who is able, serve'.

Inasikitisha sana kuona mtu kama Dr. Slaa is being hated and villified simply because of who he is! Ni kitu kibaya sana. Muhukumuni Slaa kwa matendo yake na wala si kwa pua yake, dini yake, urefu wake wala unene wake! At the end of the day na yeye ni binadamu kama mimi na wewe..ukimchoma msumari anatoka damu. Same I would condemn yeyote ambaye atamhukumu Kikwete kwa sababu ya imani yake. Muhukumini Kikwete kwa rekodi yake ya uongozi. Basi.
Mkuu wangu unafikiria kisomi sana, jaribu kufikiria kama Mtanzania aliyekosa tumaini la kupona isipokuwa kwa kwenda Loliondo, na imani hiyo imekubalika hadi viongozi wasomi wenye ma Phd..

Waislaam wengi hawana imani na Dr.Slaa kwa sababu wanaamini system nzima ya Utawala wa Tanzania inatawaliwa na kanisa...Sasa ni bora kwao kuwa na Muislaam ndani ya hilo kanisa kuliko kuwa na Mkristu tena Padre, hivyo ni jukumu la Dr.Slaa kuwahakikishia hakuna kitu kama hicho na kama kipo yeye atakikomesha..hapo tena wakiendelea kutomuamini basi wana lao jambo.. elewa tu kwamba asilimia 80 ya Watanzania ni kabuntas na shule zetu za kata tunazojisifia nazo dhidi ya madrasa..
 
kwanza hizo unazoita tuhuma kwa dr wewe binafsi unakubali ni za kweli au propaganda chafu? Tuanzie kuweka msingi hapo wabe.

Huu ushauri ni wa kumshauri mtoto wa chekechea! Tumekushtukia kuwa umetumwa2ewe ! Hatudanganyiki! Ccm wangeondoa kwanza *k, Shein, Bilal, na kupangua safu ya wizara ya mambo ya ndani na Polisi.
 
Mtanganyika, umetumia mfano mzuri sana; na umeonesha jinsi gani Wamarekani walivyokuwa prejudicial dhidi ya Wakatoliki - of course na kwenye kuna historia yake. Dr. Slaa aliyasema hayo yote unayoyasema, na alikutana na viongozi wa dini ya Kiislamu na dini zote, na kwenye ule mdahalo maarufu alisema mambo hayo hayo alipoulizwa kuhusu Ukatoliki wake. "Mimi nitakuwa Rais wa Watanzania wote" alisema. Au alitakiwa kukana imani yake na kusema "kuanzia sasa mimi ni Muislamu" ndio watu wangekubali kuwa anafaa?

Mwanakijiji,

Kinachoendelea ndani ya CCM ni kujaribu strategy inayoitwa "shoot everythich that is moving". So, wameshaona kwamba Bakwata na makongamano mengine sijui mashekhe wa Tanga wana wasupport CCM. Na ili CDM wawe chama cha wote ni lazima wabattle hisi false accusations. Kama vile CCM wanavyopanga team ya kubattle true accusations zinazousu chama chao, then CDM need to do the same.

2011-2015 is four years battle ambapo only brave fighters can last. Nadhani ni wazi kwamba Dr slaa anaweza kufanya makongamano kadhaa na waislam. Mfano, Dr.Slaa anaweza kukutana na Young educated Muslim ambao wako na views toward Tanzania development less than muslim development. Hapa akawaambia kwamba majority of Tanzania have the same problem as you, they don't have sustainable energy, they can't afford three meals a day. This is our battle and not Roman battle neither Saudi Battle, This is Tanzanian battle. I believe this young mind will pass the idea to another. Remember you don't build a tower top bottom, you build bottom up.
 
Mkuu Mkandara,

Hayo mengine yote mbona yamekuwepo. OIC sio suala la leo na limekuwa likiendelea kuzungumzika. Hili suala la Mahakama ya Kadhi ni kosa la CCM kudandia gari kwa mbele. 'Mchovu' Mrema katika kuhangaika kutafuta umaarufu alilichomeka kwenye ajenda zake kwamba akiingia madarakani atawapa Waislamu Mahakama ya Kadhi. CCM kwa 'ulevi' wao wa madaraka wakakurupuka na kuliweka kwenye ajenda zao. Sasa linawatafuna. Kwa nini watu wasianzishe Mahakama yao ya Kadhi? Wache waanzishe. Kuna haja gani ya Mahakama hiyo kuingia kwenye mfumo wa Kimahakama na Serikali kubeba gharama? CCM wanapaswa kubanwa kuhusu hili. Waliamua kujitafutia umaarufu wa haraka haraka sasa linawatafuna.

Mkuu Mkandara labda hili la Maaskofu kukemea ndio linaweza kuwa jipya. Lakini mahali tulipokuwa tumefikia ni pabaya. Nchi hii ilikuwa inakwenda wapi? Wakati wa Mzee Mwinyi alipojaribu kuipeleka nchi 'harijojo' Mwalimu alikuwepo na aliweza kukemea. Sehemu ya Utawala wa Mkapa, mwalimu alikuwepo, we Mwenyewe umeona baada ya Mwalimu kuondoka Mkapa alikotupeleka. Kama watu ambao walitakiwa kumkemea JK na jamaa zake kwa mambo ya kipuuzi waliamua kunyamaza kimya ungetegemea na Maaskofu wanyamaze? Hivi unadhani hao Maaskofu hawajui kuwa MOU inawafaidisha wao na kwa hiyo wangetakiwa kunyamaza. Udini wa sasa (sio wa OIC wala Mahakama ya Kadhi) wa kumuona Slaa kama alama ya Ukristo ndio utakaotutoa damu. JK kwa makusudi amekuwa akiongea hadharani kwa kulalamika! Hivi wananchi wanalalamika! Rais analalamika! Tena analalamika kwa kuzua mambo, udini, uhaini. Inafika mahali najiuliza kama JK anajua kuwa yeye ni Rais!

Tuyapime wanayoyasema Maaskofu kama yana harufu ya udini (contents) na si Majoho yao (Cover Page). Hivi Kauli zote za Pengo, Mokiwa wanazotoa unaweza kuzifananisha na zile za kusema JK anachukiwa kwa sababu ni Mwislamu!!!!!! Hivi Maaskofu waache kukemea Serikali ya Kifisadi kwa sababu waislamu watakuja juu ili kumuepusha Fisadi ambaye ni muislamu mwenzao.! Kama ni hivyo basi safari ya kumtafuta Mungu ni ngumu! Na inawezekana kabisa sisi waislamu na wakristo misahafu yetu tunailewa kinyume! Labda mafisadi ndio watauona ufalme wa Mungu na Wakristo itakuwa ngumu kuuona ufalme huo kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

Mkuu Mkandara hayo magamba ya nyoka wanayojivua Dodoma wakati wao ni binadamu sio kitu ambacho wamekifanya kutoka mioyo yao. Ni wewe, mimi, Slaa, Maaskofu kauli zetu zimesikika nyikani. Umesahau kama hawa hawa walisema zile ni 'ajali za kisiasa' si hawa hawa ndio waliosema, hawaijui DOWANZI! Wadwanzi!

Mkuu wangu nakuomba unisome tena kupata kunielewa...

tatizo la Dr.Slaa sii kuwa katibu mkuu wa chama CDM hata kidogo ila ni nafasi ya Urais aliyogombea na ifahamike kwamba hili kundi dogo unalolisema ndilo linalotupa shida wote hapa kwani Uongo ukizungumzwa sana hufikia kuaminika..

Sijui kama wewe unaandika Ukiwa kama Muislaam/Mkristu au unaandika tu kwa sababu wewe ni Mtanzania mzalendo wa nafsi yako, lakini nakuomba sana jaribu kukaa na Waislaam ukayasikia malalamiko yao baada ya Udini na tofauti hizi za kijamii kuwa ndio msingi wa ujenzi wa maendeleo ya Mtanzania..

Mimi nimekosana na marafiki zangu Waislaam kwa sababu ya CDM na wengine wamesema hata nikifa hawatanizika, sasa habari kama hizi siwezi kuzichukulia dharau pasipo kupima nini wa wanafikiria na jinsi gani wao wasivyomwamini Dr.Slaa ambaye binafsi naamini kabisa UWT umefanya kazi kubwa sana kumpaka tope ili kuondoa nguvu ya CDM..

Na yote niliyoyaandika hapo juu yametokana na utafiti wangu binafsi nilipokuwa Bongo, kupima na kutafuta kuona athari ya Ukabila na Udini imefikia wapi..Sasa kama wewe huamini mkuu wa ngu hilo juu yako lakini Udini upo Tanzania na hakika nchi yetu inaelekea ktk mgawanyiko mkubwa sana na hatma ya yote haya ni nchi kugawanyika na istawalike..

Kuna makundi ya Kidini, Kikabila kisasa na yapo makundi ya walionacho na wasionacho Kiuchumi na wote hawa wana hasira na maisha... Hizi tofauti kama tusipozibaini leo na kuzifanyia kazi ndani ya katiba mpya au mapema zaidi basi ITAKULA KWETU sote..

Ebu jiulize kwa nini issue ndogo kama ya Libya imetugawa ktk makundi ya kiimani hata ktk kushabikia, pamoja na kwamba hatujui ukweli na uhalisia wa vita yao. Kwa nini wakristu na wenye makabila tofauti na JK wanaona poa tu akitajwa kwa kabila lake na dini yake lakini sivyo wanaposikia Dr.Slaa akitajwa hivyo.. Waislaam wanambeza DR.Slaa kwa dini yake lakini inawauma wanaposikia maneno haya yakizungumziwa JK..Leo kateuliwa Mukama watu wanataka kujua ni kabila gani hali tayari wamekwisha ijua dini yake kuwa ndio mjumuiko wa CV yake kumwezesha uongoza..

Mkuu Udini upo na kwa bahati mbaya gap inazidi kukua kama ilivyo kiuchumi.. Mauaji ya Tegeta ni shara tosha ya kuonyesha kwamba vita vipo karibu sana iwe kwa kupitia Umaskini au dini na hakika tusiposimamisha sheria, basi kilichobakia tumwombe Mungu atunusuru..
UDUNI UPO Tanzania tena kwa sana mkuu wangu..
 
Mnaposema uislam hawaipenda CDM sio kweli ni baadhi ya Viongozi nafikiri walipewa kitu kidogo na CCM,mwaka 2005 viongozi hao hao walisema Kikwete kuwa ni changuo la kanisa na wakamtaa wakamkumbatia Lipumba iweje leo wakionyeshee kidole CDM ni chama cha kidini?Baadhi wa sisi maamuma hatuwahelewi?
 
Mkuu Mkandara,

Hayo mengine yote mbona yamekuwepo. OIC sio suala la leo na limekuwa likiendelea kuzungumzika. Hili suala la Mahakama ya Kadhi ni kosa la CCM kudandia gari kwa mbele. 'Mchovu' Mrema katika kuhangaika kutafuta umaarufu alilichomeka kwenye ajenda zake kwamba akiingia madarakani atawapa Waislamu Mahakama ya Kadhi. CCM kwa 'ulevi' wao wa madaraka wakakurupuka na kuliweka kwenye ajenda zao. Sasa linawatafuna. Kwa nini watu wasianzishe Mahakama yao ya Kadhi? Wache waanzishe. Kuna haja gani ya Mahakama hiyo kuingia kwenye mfumo wa Kimahakama na Serikali kubeba gharama? CCM wanapaswa kubanwa kuhusu hili. Waliamua kujitafutia umaarufu wa haraka haraka sasa linawatafuna.

Mkuu Mkandara labda hili la Maaskofu kukemea ndio linaweza kuwa jipya. Lakini mahali tulipokuwa tumefikia ni pabaya. Nchi hii ilikuwa inakwenda wapi? Wakati wa Mzee Mwinyi alipojaribu kuipeleka nchi 'harijojo' Mwalimu alikuwepo na aliweza kukemea. Sehemu ya Utawala wa Mkapa, mwalimu alikuwepo, we Mwenyewe umeona baada ya Mwalimu kuondoka Mkapa alikotupeleka. Kama watu ambao walitakiwa kumkemea JK na jamaa zake kwa mambo ya kipuuzi waliamua kunyamaza kimya ungetegemea na Maaskofu wanyamaze? Hivi unadhani hao Maaskofu hawajui kuwa MOU inawafaidisha wao na kwa hiyo wangetakiwa kunyamaza. Udini wa sasa (sio wa OIC wala Mahakama ya Kadhi) wa kumuona Slaa kama alama ya Ukristo ndio utakaotutoa damu. JK kwa makusudi amekuwa akiongea hadharani kwa kulalamika! Hivi wananchi wanalalamika! Rais analalamika! Tena analalamika kwa kuzua mambo, udini, uhaini. Inafika mahali najiuliza kama JK anajua kuwa yeye ni Rais!

Tuyapime wanayoyasema Maaskofu kama yana harufu ya udini (contents) na si Majoho yao (Cover Page). Hivi Kauli zote za Pengo, Mokiwa wanazotoa unaweza kuzifananisha na zile za kusema JK anachukiwa kwa sababu ni Mwislamu!!!!!! Hivi Maaskofu waache kukemea Serikali ya Kifisadi kwa sababu waislamu watakuja juu ili kumuepusha Fisadi ambaye ni muislamu mwenzao.! Kama ni hivyo basi safari ya kumtafuta Mungu ni ngumu! Na inawezekana kabisa sisi waislamu na wakristo misahafu yetu tunailewa kinyume! Labda mafisadi ndio watauona ufalme wa Mungu na Wakristo itakuwa ngumu kuuona ufalme huo kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

Mkuu Mkandara hayo magamba ya nyoka wanayojivua Dodoma wakati wao ni binadamu sio kitu ambacho wamekifanya kutoka mioyo yao. Ni wewe, mimi, Slaa, Maaskofu kauli zetu zimesikika nyikani. Umesahau kama hawa hawa walisema zile ni 'ajali za kisiasa' si hawa hawa ndio waliosema, hawaijui DOWANZI! Wadwanzi!
Mkuu wangu labda nirudie tena kujieleza wazi na kukusahihisha..

1.Swala la Mahakama ya Kadhi ni ibada ya Waislaam na ni muhimu kwao kama wanavyolitambua wao.. Na Mrema alifanya alichoagizwa na Waislaam hata iwe kutafuta umaarufu lakini aliwakilisha na ndio maana Mrema alikubalika kwao wakati huo.

2. Swala la OIC ni muhimu kwa Waislaam vile vile wala sii swala la CCM isipokuwa Waislaam walilipeleka kwa CCM kwa sababu ndio wao walikuwa na wanaendelea kuongoza, hivyo ahadi za JK zilitokana na ombi la Zanzibar kwa Waislaam. Hapa Canada Qubec ni member wa French countries union hali states nyinginezo ni member wa Commonwealth.... iweje kwetu iwe shida pale bara ni member wa Commonwealth tunawavuta na Wazanzibar lakini hairuhusiwi kwa Zanzibar kujiunga na chombo chao hata kama ni cha kidini..

3.Swala la MoU ni swala jpya kwa Waislaam baada ya wao kushindwa kupata waliyoyataka kwa miaka yamewezekana kwa Wakristu hivyo ile dhana ya nchi kutawaliwa na kanisa ndio imepata mafuta ya kuchochea..

Kumbuka tu kwamba mimi ni Muislaam na sikubaliani na mahakama ya kadhi kwa sababu zangu ambazo hata Dr.Slaa kama anapinga anaweza kuchukua mtazamo wangu. Mimi napinga mahakama ya kadhi kwa sababu inachukuliwa sheria dhaifu ndani ya Uislaam na kuachwa sheria kubwa zaidi ambayo ndiyo ibada kubwa ya Muislaam. kwa mfano, Mwanamme anapozini njea ya ndoa yake (kabla ya kumpata hata mtoto nje ya ndoa) Hukumu yao wahusika wote ni Kifo... Je kwa nini Waislaam na Masheikh wasiombe hukumu hii mbele ya mahakama ya kadhi ili kuwahukumu watoto ambao kidini hawamo ktk urithi..kwa nini wasiwahukumu waislaam wenyewe waliotenda mabaya kwanza..

Kama tutazuia uzinifu bila shaka hao watoto wa nje ya ndoa hawatakuwepo, hivyo hukumu ya mirathi itakuwa rahisi zaidi...na zaidi ya hapo ndoa nyingi nchini zinavunjika kwa sababu ya uzinifu, mwanamme kapata bibie mwingine au mwanamke kapata Kapela na wanataka kumwagana, hivyo kidini wanaotakiwa kuhukumiwa kwanza ni hawa wazinifu ndani ya ndoa kabla hujaigawa mali ya mwanamke/ au mwanamme alivunja ndoa yake kwa uzinifu. Uzinifu pekee unakuondoa ktk Uislaam na ndio maana hukumu ya watu hawa ni kifo je kweli Watanzania Waislaam wako tayari kupokea hukumu ya kwanza kubwa kuliko mahakama ya kadhi?

Sasa maadam hatuwezi kuchukua hatua hii kali kabisa na tumeshindwa kuisimamia dini na maadili yake sioni sababu ya kuwa na mahakama ya kadhi kuhukumu mirathi na taraka ambazo zimevunja miiko na maadili ya Uislaam to begin with..

Swala la OIC bila shaka hili halina tatizo na sidhani kama Dr.Slaa au Chadema wanalipinga kwani ni haki ya Waislaam au chombo chochote cha kimataifa kinacholenga kuwaendeleza watu wake....Yapo Mabenki ya kikristu, wahindi na zipo NGO za kina Agha Khan ambazo zinaendeleza jumuiya zao, iweje hili la Waislaam liwe na pingamizi toka kwa Wakristu na sii watu wengine?..

Kuhusiana na MoU, waislaam wanataka uhalali na usawa ktk huduma zinazopatikana, kwani makubaliano baina ya serikali na kanisa ilikuwa ni swala la Kikatiba....kuhakikisha mali za watu wote zilizokuwa zimetaifishwa zinarudishwa kwa wenyewe na sio kikundi kimoja cha kanisa au viongozi kuchukua mali za Umma na kuzifanya zao..Huu ni uhuni ambao Chadema wanatakiwa kuupiga vita hata kama inawahusu ktk imani zao za dini..

Mbali na hapo navyosikia mkataba huo hauwezi kuvunjika kama Mkapa alivyouza Bulyanhulu na madini yake hata kama hatutakubaliana na mkataba ule.. mwisho wa siku tutapelekwa ICC na hakika Kanisa katoliki litatufilisi.. Why in the hell Mkapa alifanya hivyo kama sii Udini na kwa nini viongozi wa kikristu hawakudai mali kwa niaba ya Watanzania wote isipokuwa kanisa lao tu.. hapa walikuwa wakifikiria kweli maslahi ya Waislaam? noo sidhani hivyo udini unatafsirika vile vile..

Mkuu tusiwe na Nidhamu ya woga kuogopa viongozi wetu wa dini wanapokosea jambo au kuunga mkono hoja bila kufikiria upande wa pili watalichukulia vipi swala hilo ikiwa kweli tunadai sisi ni wamoja na hatuna Udini..Nitawakemea siku zote viongozi wa dini na serikali wanapopoteza mwelekeo wa nchi na hakika Nyerere aliyafanya yote haya kwa nia njema ya kuunda Taifa la Watanzania, ila leo baada ya kurudisha Ukoloni mamboleo (Ubepari) ndio matatizo ya Udini na Ubinafsi yanajitokeza..
 
At least nao thread inaendelea kwa hoja maridhawa

Guys, kwa wasioelewa msimamo wangu ni kuwa

Naamini CDM haina udini na ya kuwa CCM ndio imeleta hizo propaganda, hizi propaganda haijalishi nani kazileta zipo zinaishi na zina leta damage. what to do?
 
Sidhani kama kichwa cha habari kinaendana vema na "illogical" issues ambazo unadhani zinapaswa kulazimisha kuondolewa kwa Dr. Slaa. Hiyo unayoita risk assessment inapaswa kuangalia risk ya kufanya badiliko, na kama hiyo risk inaweza kuwa acceptable, transferred au kuwa na alternative. Ni wazi kuwa kukataa kufanya mabadiliko nayo ni available alternative!!

Ukianza kutumia illogical reasons, utapenda Dr. Slaa aondolewe kwa kukaidi amri zisizo halali zinazotoka kwa mamlaka halali, utasema aliacha upadri, utasema hana mke. Ukitaka kutumia logic utagundua kuwa mambo kama maendeleo, amani, uhuru, demokrasia, elimu na afya ndio mambo yaliyo muhimu kabisa kwa taifa hili.

Kila badiliko lifanywe kwa kuangalia ni nini lengo na lazima lengo liende ktk kuboresha!!
 
At least nao thread inaendelea kwa hoja maridhawa

Guys, kwa wasioelewa msimamo wangu ni kuwa

Naamini CDM haina udini na ya kuwa CCM ndio imeleta hizo propaganda, hizi propaganda haijalishi nani kazileta zipo zinaishi na zina leta damage. what to do?

Viongozi wote wa CDM na wanachama wao popote pale walipo ni kujitahidi kuwaambia Watanzania kwamba CDM si chama cha kidini na pia kuna wanachama waislamu wengi tu na hata viongozi ndani ya chama hicho. Kule Kigoma ambako Zitto ni mwakilishi wao asilimia kubwa ya wakazi wa kule kama sikosei ni Waislamu. Sasa kama waliweza kuzikubali sera za CDM kama zilivyouzwa kwao na Zitto na hatimaye kumchagua basi popote pale Tanzania CDM wakiziuza sera zao vizuri wanaweza kabisa kukubalika miongoni mwa Watanzania waislamu walio wengi bila kujali propaganda chafu zinazofanywa na CCM za kudai kwamba CDM ni chama cha kidini.
 
Now this is very right and logical question! Zile hadithi ulilenga mengine mkuu,umewahi kumtuhumu dr slaa kuwa ndie anaempiga vita zitto! Hoja zako zina rangi nyingi! Kama ni mafanikio umefanikiwa kupasua watu vichwa humu toka jana.Wabe bana!
 
Viongozi wote wa CDM na wanachama wao popote pale walipo ni kujitahidi kuwaambia Watanzania kwamba CDM si chama cha kidini na pia kuna wanachama waislamu wengi tu na hata viongozi ndani ya chama hicho. Kule Kigoma ambako Zitto ni mwakilishi wao asilimia kubwa ya wakazi wa kule kama sikosei ni Waislamu. Sasa kama waliweza kuzikubali sera za CDM kama zilivyouzwa kwao na Zitto na hatimaye kumchagua basi popote pale Tanzania CDM wakiziuza sera zao vizuri wanaweza kabisa kukubalika miongoni mwa Watanzania waislamu walio wengi bila kujali propaganda chafu zinazofanywa na CCM za kudai kwamba CDM ni chama cha kidini.
Mkuu maneno yako ni sawa kabisa lakini lazima ukumbuke kwamba hata sisi Chadema hatuwezi kumkubali mtu ambaye tunafikiria ni Fisadi hata kama sii fisadi na hana sababu ya yeye kujiaminisha kwetu..

Lowassa anakubalika sana huko nyanda za juu na wapo watu wengi sana wanamkubali na hawaamini kuwa ni fisadi ila tajiri kwa uwezo wake mwenyewe lakini haina maana Tanzania nzima watamkubali hivyo hata Zitto na watu wengine ndani ya Chadema kuwa Waislaam bado zipo tuhuma dhidi yao kama vile tunavyokituhumu chama kizima cha CCM pamoja na kwamba sii viongozi wote ni Mafisadi..Wapo wanaojulikana na ukaribu wa baadhi ya mafisadi kumewaweka hata wao ktk nafasi za kuogopwa.

Kibaya zaidi mkubwa wangu fikirieni kama asilimia 80 ya Watanzania waliosoma shule za kata na madrasa ambao ndio kesho wapiga kura na ndio wenye wasiwasi sana kwani hawana tumaini jipya...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Alikutana na kina nani maanake navyojua mimi Pinda ndiye alikwisha kutana na baraza la Waislaam waliochaguliwa kukutana naye na wakampaka kishenzi kiasi kwamba watu kama Othman Matata waliondolewa ktk kundi la watu waliokwenda kumwona..Ningependa sana kumsikia Dr.Slaa mwenyewe akinieleza haya na ingekuwa vizuri zaidi kama makutano haya yangekuwa live on TV ili ushahidi uwepo wazi...
.

mzee hicho ndicho nilichokuwa nahofia; kukutana kwake na viongozi wa dini (wakiwemo Waislamu) haikuwa siri, ilitangazwa hadharani na kwenye vyombo vya habari (kama picha inavyoonesha). Ila sasa yawezekena hakukutana na wale ambao watu fulani wangeridhika. Sasa hapo tena siyio suala la viongozi wa Waislamu bali aina fulani ya viongozi hao. Kama angekutana na kina Matata wangekuja viongozi wengine (BAKWATA kwa mfano) ambao wangelalamika kuwa Dr. Slaa akutana na viongozi wenye "msimamo mkali" na hivyo Waislamu "wengine" wakasema hawakubaliani nao.

Kwa jinsi ninavyoona, sijui ni kwa namna gani Dr. Slaa anaweza akawaridhisha waislamu wote kwa kuzungumza nao na hata akifanya hivyo inaonekana inakuwa implied kwamba akubaliane nao hata kama dhamira yake au ukweli wake unamfanya asikubaliane nao. Kwa mfano, hivi wakikaa kuzungumza naye na Dr. Slaa akisema hoja ya OIC na Mahakama ya Kadhi haiendani na ajenda ya Chadema si itaonekana Chadema ni kinyume na Waislamu? Kwa hiyo, ni wazi kwamba ili akubaliwe ni lazima akubali hayo.

Baada ya kusoma haya na mimi naweza kuona kile ambacho Waberoya anakisema, labda ni kweli Dr. Slaa aondoke kwenye uongozi na asije kugombea nafasi yoyote hasa kama ya Urais ili Chadema iweze kukubalika na Waislamu.

- Hata hivyo, itakuwaje kama Chadema - minus Dr. Slaa- bado haitakuwa na ajenda maalum kwa Waislamu?
- Itakuwaje kama vyama vyote vya siasa vikawa na ajenda maalum kwa ajili ya Waislamu na zikawa zinavutia, ni kitu gani Waislamu wataangalia katika kuchagua chama kinachowafaa? Sema vyama vyote viwe na ajenda ya Tanzania kujiunga OIC, kugharimia Mahakama ya Kadhi, Kuwa na affirmative action ya kupendelea Waislamu kwenye ajira na elimu? What would be the tie breaker?

Najaribu kuelewa zaidi kama Tatizo ni Chadema kama chama au tatizo ni Dr. Slaa kama mtu aliyewahi kuwa Padre na kutaka kugombea Urais maana kama ni hilo la pili - kwa kweli sioni msingi wake ni nini? Kama Watanzania wanataka waliowahi kuwa viongozi wa kidini wasigombee nafasi ya kisiasa ni vizuri iwekwe kwenye sheria ili kuwazuia wachungaji, mashehe au mapadre kugombea nafasi za kisiasa. Maana kama tunakubali wanagombea Udiwani, Ubunge (tena kwa miaka 15) halafu tuje kukataa wanapotaka kugombea Urais nadhani wenye matatizo ni sisi wananchi.
 
Back
Top Bottom