Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu
Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

MJkuu Waberoya , nakubaliana kwa kiasi tu na observations zako kwa CDM, chama kikubwa cha upinzani nchini.
Jukwaa kubwa la kisiasa kwa CDM ni katika mapungufu ya CCM kama chama tawala,zaidi ya hapo CDM haina objective politics, haina manifesto inayoeleweka.
Kila mtu anaweza kulaumu na kutoa kinadharia alternative scenarios iwe kwenye uchumi , utawala na vinginevyo.
The day of reckoning for CDM ni hii hali ya CCM "kujivua gamba" kwa amani na utulivu.
This is a master stroke ambayo hata CDM hawakuitegemea.
Katika vyama vyote vya upinzani theme ya "kujivua gamba" ni lazima itaambatana na fujo na watu kuunda splinter party groups.
Wapende wasipende lawama za CDM na vyama vingime vimeisaidia sana CCM kufika hapo ilipo.
Na hii ndiyo democratic multi party politics.
Hivi tunavyoongea mlengo wa kisiasa wa Chadema haujulikani vijijini wala msimamo wake rasmi-ukiacha lawama kwa kila jambo kwa CCM -liwe jema au vinginevyo.
CDM inabidi na wao waelewe kuwa kinachopendwa na wananchi ni matazamio yao ya baadaye. In the mean time CCM wanafanya vema kuwakaba koo mafisadi hivyo kuwanyima hewa ya kisiasa CDM
 
The real victims hapa ni sisi watanzania, siasa zetu zimeelekeza sana kwenye scaremonger tactics from both political parties truth be said. Hizi tabia za kukemea ufisadi au uongozi kupitia vyombo vya dini, in the process vina-mobilize followers, agitators being religious priests.

Once a church priest condemns the government or the president, his statement is left to many interpretition. Why now considering the president is a muslim. Why then do we have political parties what is their role?. This is where trouble begins if the muslim community interpret the statement as being an act of religious hatred of course they would defend the government. In the process it is us Tanzanian who suffer if the accusation had solid evidence.

Political parties are there to critisize the government, but if parties allow religious groups to condemn on their behalf. The party is indirectly associated with that group, we can not deny the fact CDM were the first to reject the new constitution bill, why the heck did the church had to follow, are they in politics too.

It is those kind of acts that people link CDM with christianity groups and muslims with CCM, something which is not real to most of us in JF. But remember most of us have some sort of education what about my uncle who has a simple mind, surely he is bound to be one of those who is moblized by this religious groups participatory.

Its about time the political parties stopped inflaming the prejudice and passions of poor people for their political gain. As it demonstrates there is no real desire for change from this politics but a few preveleged people fighting for the big prize at the cost of our peace and social change.
 
Huwezi kuzuia propaganda. Na sidhani kama chadema wanaweza kupoteza muda kujadlili propaganda badala ya kuconcetrate kwenye national issues
<br />
<br />
Yes, kama vile vurugu na maandamano "ya nchi nzima". Point!!
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.

Pure gibberish. The only positive thing about it is that you had the sense to write this mindless mumbo jumbo at all. You indeed seem to be a "brave" man!
 
Mkumbo mbaya sana, defencive mechanism mbaya kabisa!

Tofauti na wengi mlivyoichukulia post yangu, iko wazi na anayetaka kuelewa ataelewa tu, sijajua negativity imetoka wapi na kwa nini.

Mlio-comment vibaya humu mtagundua ukisoma tena nilikuwa na maana gani!

All I mean is that democracy is not always good in democracy people can say 2+2=5! while in reality is 4. Slaa hana udini, hana tatizo background yake ndiyo inatafutwa na imeishatafutwa na ndiyo kwa namna moja au nyingine inakiua auitakiua chadema.

This is just a piece of advice, sijasema Slaa ana ubaya wowote ule

Nimesema neno risk kwani ni pana sana.
 
Too sad for you my dear! kama ukaribu wangu na Zito ndio unaofanya CDM kichukiwa na unakosa hoja ya kukiokoa kwa sababu ya uhusiano wangu na Zito sawa! umenifanya nicheke, umeenda mbali na hoja, I am not hero, I am not intellectual hayo umenipa wewe na ulinipa wewe!

JIBU HOJA, KATAA kuwa Slaa asiondoke na sema nini wafanye! kwa nini mko kwenye gari mnajua kabisa haliendi popote bali ni kupiga resi tu na makonda kusema linaenda na bado liko stendi?

Huyo Zito wala hafai kuwa katibu mkuu wa chadema, wala sijui na sina ukaribu naye..we are connected with Zitto kwa mawazo yake na itikadi zake na si vinginevyo

Haya waislamu hawakitaki CDM unasema nini?

Conclusion zako kwenye post mbili zimenifanya nikuweke kwenye -ignore list, umeandika kama una uhakika kabisa! my God! namna hiyo unaweza kumgomnaisha mama yako na baba yako, ukimuona mama anaongea na mzee fulani utatoa conclusiona na kumweleza baba! childish, watu wanashindana kwa hoja na si kusingiziana vitu ambavyo personally unajua si kweli na kama unaamini umekosea!

poor MTM!

Ukikua utaacha.....unasumbuliwa na utoto na ufinyu wa mawazo na kutokujua kujenga hoja ila mtaalamu wa uzushi
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.

[I]Waberoya again!

Ukiona maada ngumu kama hizi ambazo hazieleweki kirahisi basi huwa nawaza mto hoja yukoje! Genius!

Ukiona maada mpaka akina mwanakijiji hawaielewi kirahisi basi ni ngumu sana kwa ubongo wa kawaida kuielewa!

Ukiona maada kama hizi ambazo pro-chadema wengi wanaishia kutukana na kutokusoma content basi taifa hili lina matatizo

Maada hii ni ngumu sana, ni kama vile chakula kigumu kwa chadema aidha kusuka au kunyoa, nilivyoelewa ni hivi

1. Pamoja na uzuri wa Slaa shutuma za udini walizorusha kwake zinaonekana kuaminika
2. Mafanikio ya slaa ya zamani siyo kipimo cha mafanikio ya kesho upepo unabadilika
3. Chadema ikubali

a) kutatua matatizo ya udini kwa vitendo
b) kumuondoa Slaa
c) Kikubali kufa

This is purely risk analysis , ndipo ambapo huwa namuogopa sana huyu Waberoya

Who is s/he? hemaphrodite??

Waberoya hands up!! fuxcxx you!
[/I]
 
Muasisi wa Udini TZ ni CCM,Imekuwa ikitumia Dini kupakazia chama chochote kinachoonekana kuwa tishio walianza na Nccr-mageuzi,TLP na juzi-juzi CUF hivyo usishangae kuona CDM wanasingiziwa zengwe kama hili yote hayo ni uongo wa CCM

Unajua kuwa unamsapoti Wabe?
Kama vyama ulivyovitaja vilidhoofishwa na hizo propaganda kwa nyakati tofauti kumbe tuna uhakika kuwa Chadema watadhoofishwa pia kwa hizo propaganda ama vinginevyo ikiwa hawatopuuzia ushauri huo wa bure.
Ni lazima kwa kutumia historia hiyo wajifunze kujilinda dhidi silaha hiyo kali ya Ccm ambayo imekwishafanya mauaji kadhaa...
 
Kama Dr. Slaa hangekuwa mgombea wa CDM, basi CDM ingebaki kwenye nafasi ya tatu (CCM, CUF then CDM) kama ilivyokuwa hapo nyuma.

Na zaidi ni kwamba kiukweli CDM ndicho chama namba wani kwa Watanzania kwa sasa. CCM is morally dead.
 
Mkandara,

..MOU ilisainiwa 1992 wakati Alhaji Mwinyi akiwa Raisi.

..pia Bakwata walikuwa wanashiriki kama observers wakati wa mchakato wa MOU.

..ninachojiuliza mimi ni kwanini Waislamu hawajiungi pamoja na kuandika MOU baina yao na serikali ili nao wapate kurudishiwa mali zao zilizochukuliwa na serikali?

..maadamu umesema unafahamu baadhi ya wanaharakati naomba uwaulize hili swali linalotutatiza baadhi yetu, kwamba Waislamu wanaishia kulalamika[since 1992] kwenye mihadhara bila ya wao kuandaa MOU baina yao na serikali.
Mkuu nashukuru kwa kunijuza kuhusu lini makubaliano ya MoU yalifanyika na hakika ndicho kinachowapa hofu sana Waislaam wa Tanzania (wanaharakati) na sii Bakwata..Na nitashukuru sana kama utanipa majina ya viongozi wa Bakwata waliohudhuria, bila shaka Sheikh Mkuu marehemu Hemed bin Jumaa wa Tanga alikuwa mshirika kubwa sana wa serikali ya CCM.

Kumbuka nawazungumzia zaidi wanaharakati Waislaam ambao wamejazwa ujinga na hawa viongozi wa CCM pamoja na Bakwata ktk kampeni hizi za kuivunja Chadema na kumchafua Dr. Slaa. Elewa kwamba Bakwata ni chombo cha CCM na wanafanya mambo mengi kwa maslahi ya chama zaidi ya Waislaam wenyewe kiasi kwamba Waislaam wanashindwa kuwauliza Bakwata maswali magumu wala kuwapinga..

Kama unakumbuka mimi binafsi nimewahi kuhoji Uislaam wa Mwinyi na nadhani kama unakumbuka navyopinga Bakwata na Mwinyi hasa baada ya Waislaam kuanzisha chombo chao kikiitwa Balukta kikiwa pinzani na Bakwata miaka hiyo hiyo ya makubaliano ya MoU...

Umeniuliza kwa nini Waislaam hawajiungi pamoja kupata makubaliano kama ya Wakristu, mkuu wangu hili haliwezekani chini ya Bakwata kwa sababu ni chombo cha CCM na hawapo hapo kwa maslahi ya Waislaam na kibaya zaidi Waislaam hawana kiungo chochote zaidi ya Bakwata kinachojulikana kama mwakilishi wao ila zipo NGos ambazo haziwakilishi Waislaam wote ila kujishughulisha na huduma ndogo ndogo kulingana na uwezo wao mdogo..Kinachofunga kazi ni hiyo imani ya kwamba CCM inatawaliwa na kanisa hivyo kila watakachojaribu kitapigwa chini.. Pengine wamejaribu na wameshindwa hivyo malalamishi haya sii tu yako magazetini ila wameisha kataliwa..

Kwa hiyo hofu hii ya kutokubaliwa ama kutotambuliwa isipokuwa kwa kupitia viongozi waliopandikizwa ndio hofu ya watu kama mimi na Waioslaam wengine ambao tunajua fika kwamba Mufti na viongozi wengine kama yule Mtangazaji wa kipindi cha kiislaam ktk TV wapo ktk payroll ya chama na wamekusudia kuupotosha Umma..
Je, Dr.Slaa na viongozi wengine watawasaidia vipi waislaam hata kama kusema ukweli kama alivyouliza Mwanakijiji ktk mada moja ya mahusiano baina ya Waislaam na CCM..

Mzee Mwanakijiji,
Umeniuliza swali zuri sana kuhusu Dr.Slaa kama hakubaliani na matakwa ya Waislaam kuna haja gani ya yeye kukutana nao... Hakika akifanya hivyo na kuwajulisha wazi kwamba hakubaliani na matakwa yao with reason behind zenye kuridhisha, bila shaka Waislaam watajua kwa uhakika where he stand badala ya kujificha nyuma ya pazia hali yeye anagombea Urais wa nchi..Na kibaya zaidi ni kuwaahidi Waislaam kama JK hali akijua haiwezekani..

Hata mimi hapa leo hii Dr.Slaa akisema hakubaliani a OIC na akanipa sababu, nitazipima hizo sababu, akisema hakubaliani na Mahakama ya Kadhi pia nitamsikiliza sababu zake lakini kama hizo sababu zitahusu Ukristu wake nitashindwa kumwelewa na pengine kukubaliana na hao wanaharakati kwa sababu dini ni haki ya kila Mtanzania kuabudu anachokiamini na haki hiyo haiwezi kuzuiliwa na katiba ile ile inayowaruhusu wengine kufanya ibada zao..

Wahindi Masingasinga na mabaniani wanachoma maiti na hatuwakatazi ingawa ktk utamaduni na dini zetu hiyo ni kufuru na hakuna sheria moja kwa sote..Sisi tunakula ng'ombe wakati hao wahindi hawali nyama ya Ng'ombe, kwao ni haramu..hivyo ni lazima Dr.Slaa awe mkweli na awape sababu za kuridhisha waislaam kwa nini anapingana nao.

Kuhusu ni kina nani anatakiwa kukutana nao? - Hii sidhani kama ni hoja hata kidogo kwa sababu kinachotakiwa kwa Waislaam ni kujua msimamo wake kuhusiana na hofu ya Waislaam. Anaweza kujibu maswali kutokana na hoja za watu ktk magazeti, mitanmdao na kadhalika au kujibu maswali kulingana na atakavyoulizwa na hao anaokutana nao maada jibu lake lina represent Waislaam wote.. Muhimu ni ile message yake imetoka huru na wazi kwa wananchi na huo ndio msimamo wake au wa Chadema..

Na mwisho kabisa mkuu wangu nina hakika maswala mengi ya Waislaam yanapingwa na CCM wenyewe.. Na ndio maana nikakubaliana nawe ulipouliza ni lini Waislaam wamekuwa marafiki na CCM?..Kama sikosei nimesikia swala la Mahakama ya kadhi lilipingwa na uongozi wa CCM hata kabla halijafika kujadiliwa na sababu zilikuwa za kikatiba kwa tafsiri ya nchi kutokuwa na dini na sii watu wake kuruhusiwa kuabudu dini zao. Binafsi nadhani nina sababu bora zaidi ya uongozi wa CCM ambao unawapiga tobo na magoli ya kisigino.

Sasa ile ruksa ya kuabudu ikageuka kuwa swala la Kitaifa japokuwa linawahusu waislaam na ibada yao. CCM ndio walipinga pia OIC na CCM ndio walioweka makubaliano ya MoU chini ya uongozi wa Al Hajj Mwinyi - Muislaam akiwa rais wa nchi na cha kushangaza waislaam wengi wanaamini ilikuwa wakati wa Mkapa.. na ndivyo nilivyoelezwa nilipokuwa Bongo.

Kwa hiyo mkuu wangu Waislaam hawako well informed, wanaburuzwa ovyo na hili la Mwinyi kuweka makubaliano na kanisa Katoliki litawamaliza kabisa..Na hakika kama Dr. Slaa ataliweka wazi hiyo chuki yao itageukia CCM kwani Siasa ni mchezo mchafu sana na Dr. Slaa anazo point safi sana kutoka ubao huu kuwawezesha hata wao kupata makubaliano kama alivyo suggest Jokakuu badala ya kuwaacha pasipo tumaini...

Kuna watu wamezungumzia matatizo ya Umeme kuwa ni yakitaifa lakini kwa uhakika zaidi maswala ya Richmond na Dowans yanahusu zaidi mkoa wa Dar es Salaam na sii Mwanza, Mtwara, Mbeya wala Musoma ila wananchi wanachukizwa na vitendo vya viongozi wetu kufisadi kodi zao kwa kuingia mikataba feki..

Tusichoke kuumiza vichwa vyetu kwa kufikiria kwamba ni tatizo la kitaifa tu ndilo lenye nguvu ya Kijamii, hapana mkuu wangu kwani kuuawa kwa Albino huko Shinyanga na Mbeya ni tatizo la nchi nzima, Kukeketwa kwa wanawake mikoa ya ziwa na kanda za juu, au kuuawa kwa watu huko Tegeta ni swala la nchi nzima ikiwa serikali inashindwa kusimamia majukumu waliyokabidhiwa hata iwe toka kitongoji kimoja..

Hivyo hivyo kuonewa kwa Waislaam na CCM iwe ni tatizo la Taifa zima kwani wao ni sehemu ya wananchi wanaounda Taifa hili..hakuna swala lolote la kijumla ni jumuiya zetu zinapodhurika ndivyo tunavyokemea uongozi uliopo madarakani...Kukemea na kulaani Mauaji ya Mwembechai ni jukumu letu sote Watanzania sii swala la waislaam pekee..
 
Mzee Mwanakijiji,
Umeniuliza swali zuri sana kuhusu Dr.Slaa kama hakubaliani na matakwa ya Waislaam kuna haja gani ya yeye kukutana nao...

Nadhani swali langu lilikuwa more rhetorical na kwa kwa kweli mzee mwenzangu sikulimaanisha hivyo ulivyouliza. Nilichosema kuwa tuseme Dr. Slaa amekutana na kundi la Waislamu - siyo kwamba akatae kukutana nao kabla ya kuzungumza kwa sababu ya kutofautiana. Tuseme Chadema kama chama ina msimamo kuhusu mambo mbalimbali. Dr. Slaa anaenda kukutana na jamii ya Waislamu na kusikiliza na kucompromise na kushindwa kucompromise mambo fulani kwa sababu ni position ya Chama - siyo position yake.

Huo msimamo wa chama ukaonekana kuwa hauwafurahishi kundi hilo la Waislamu kwani wanaona hautetei maslahi yao. Hapo anafanya nini? Point yangu ni kuwa kama kuna watu ambao wanaamini kuwa bila kupewa x, y basi mtu hakubaliki ni vigumu sana kuwaridhisha. Binafsi ningependa kujua kuwa ni compromise gani ambazo zinaweza kufanyika kuwaridhisha hawa waislamu wa kundi hili?

Kuhusu kina anani anatakiwa kukutana nao hii sio hoja hata kidogo kwa sababu kinachotakiwa ni kujua msimamo wake kuhusiana na hofu ya Waislaam.

Hili ndilo swali ambalo ni gumu wakati mwingine. Mtu anaposema "waislamu" huwa tunazungumza kama ni kundi moja linalofanana kwa kila kitu wakati mimi na wewe ni mashahidi kuwa ni kundi ambalo lina maslahi mengi zaidi ya yale ya "waislamu" tu. Kwanza ni kwa sababu hata ndani ya Uislamu wenyewe nchini si wote wanakubaliana - wale wa EAMWS (WARSHA) na wale wa BAKWATA N.K Kimsingi ni kuwa ili kuweza kuwafikia wengi zaidi itabidi akutane na makundi mbalimbali ya Waislamu unless Waislamu kwanza wakikaa pamoja na kuwa na msimamo mmoja. Hii inaelezea kwanini licha ya kukutana na viongozi wa Waislamu mwezi Septemba bado haikuridhisha kwa sababu labda hakukutana na wale ambao watu waliona anapaswa kukutana nao hasa.

Na mwisho kabisa mkuu wangu nia hakika maswala mengi ya Waislaam yanapingwa na CCM wenyewe.. Na ndio maana nikakubaliana nawe ulipouliza ni lini Waislaam wamekuwa marafiki na CCM?..Kama sikosei nimesikia swala la Mahakama ya kadhi lilipingwa na uongozi wa CCM hata kabla halijafika kujadiliwa na sababu zilikuwa za kikatiba kwa tafsiri ya nchi kutokuwa na dini na sii watu wake kuruhusiwa kuabudu dini zao.

Very tue kwa sababu naamini siku moja kuna mtu atawauliza tu kwanini wanaiunga mkono CCM. Kwa sababu kila nikifiria naona kuwa Waislamu na watanzania wengine walikuwa na nafasi nzuri ya kujiletea mabadiliko mwaka jana lakini yakawa deferred.

Kwa hiyo mkuu wangu Waislaam hawako well informed, wanaburuzwa ovyo na hili la Mwinyi kuweka makubaliano na kanisa Katoliki litawamaliza kabisa..Na hakika chuki yao itageukia CCM kwani Siasa ni mchezo mchafu sana na Dr. Slaa anazo point safi sana kutoka ubao huu kuwawezesha hata wao kupata makubaliano kama alivyo suggest Jokakuu badala ya kuwaacha pasipo tumaini...

Hivyo hivyo kuonewa kwa Waislaam na CCM iwe ni tatizo la Taifa zima kwani wao ni sehemu ya wananchi wanaounda Taifa hili..hakuna swala lolote la kijumla ni jumuiya zetu zinapodhurika ndivyo tunavyokemea uongozi uliopo madarakani...

Mkandara, mimi naamini kabisa kuwa hata yale mambo ya "waislamu" yakikubaliwa - na mimi sina tatizo hata kidogo tutakuja kuona kuwa wala siyo matatizo hasa ya Waislamu, kwani matatizo yao ni laye yale ya watanzania - kama unavyosema mara nyingi. Kwa sababu kama ingekuwa ni matatizo ya kidini tu Misri kusingekuwa na mvurugano, wala Iran, wala Syria, wala Jordan, wala Tunisia kwa sababu kwa nchi hizo mfumo unaotawala si "mfumo Kristo". Binafsi natamani kwenye Katiba Mpya tuyaingize mambo yale ambayo yana maslahi kwa Waislamu na nadhani hapo yatalazimisha wote tuangalie mambo yanayotuhusu sote kwa pamoja.

Kwa sababu wakishapewa mahakama ya Kadhi
Wakishapewa kujiunga na OIC
Wakishapewa mashule yaliyotaifishwa
n.k

Kinabakia nini isipokuwa matatizo yale yale yanayowagusa wananchi wengine? Ndio maana wakati mwingine nafikiria kutotatua matatizo ya Waislamu ni mbinu ya CCM kuendelea kuwashikia waislamu kitu cha kuwabembelezea au kuwaringishia bila kuwapa.

Chadema upande mwingine walipoteza nafasi nzuri ya kuweza kupenya na kugusa mioyo ya Waislamu. Nakumbuka kuna mapendekezo kadhaa niliyatoa (privately) ambayo kama wangeyakubali kwenye Ilani yao na kuyasimamia yangegawanya kura za Waislamu lakini nadhani hawakuwa tayari kufanya hivyo.
 
Viongozi wote wa CDM na wanachama wao popote pale walipo ni kujitahidi kuwaambia Watanzania kwamba CDM si chama cha kidini na pia kuna wanachama waislamu wengi tu na hata viongozi ndani ya chama hicho. Kule Kigoma ambako Zitto ni mwakilishi wao asilimia kubwa ya wakazi wa kule kama sikosei ni Waislamu. Sasa kama waliweza kuzikubali sera za CDM kama zilivyouzwa kwao na Zitto na hatimaye kumchagua basi popote pale Tanzania CDM wakiziuza sera zao vizuri wanaweza kabisa kukubalika miongoni mwa Watanzania waislamu walio wengi bila kujali propaganda chafu zinazofanywa na CCM za kudai kwamba CDM ni chama cha kidini.

I support this.

Ni hapa tu juzi tarehe 1 April,2011 MWANAZUONI MAHIRI NA MSOMI MAARUFU TANZANIA PROF.ABDULLA SAFARI ALIJIUNGA NA CDM. PROF.SAFARI SI MKRISTO NI MWISLAMU SAAFI.Kwa maneno yake mwenyewe amethibitisha KUWA CDM HAKUNA UDINI,UKABILA WALA UKASKAZINI. Kabla hajachukua uamzi wa kuhamia CDM amechunguza mambo hayo yote kwa UMAKINI MKUBWA UKIZINGATIA KUWA YEYE NI MWANASHERIA ALIYEBOBEA NA MWANASIASA mahiri na amekuja ku-CONCLUDE KUWA YOTE HAYO NI PROPAGANDA ZA CCM TU KUJARIBU KUKIPAKA MATOPE CHAMA CHA CDM.

Kwa hiyo hili swala la UDINI linapikwa na CCM tu ili kujaribu kuwaaminisha Wa-tz kuwa CDM kuna udini. CCM NI NYOKA MWENYE SUMU KALI AMBAYE AKISHAKUTEMEA HIYO SUMU USIPOKUWA MAKINI UNAPOFUKA MOJA KWA MOJA. Ukisoma hizi sentensi 2 hapa chini ndipo unaweza kujua CCM ni chama cha namna gani!!!Endelea:

  1. Mwaka 2000 wakti wa Uchaguzi Mkuu CCM WALITUMIA PROPAGANDA HII HIII KUJARIBU KUISAMBARATISHA C.U.F. wakti huo CUF ikionekana kuwa na nguvu ya upinzani. CCM HAWA HAWA WAKADAI KUWA CUF NI CHAMA CHA UDINI(UISLAMU)KWA HIYO WATU WASIKIUNGE MKONO!!!!LEO CCM HAWAHAWA WAMEUNGANA NA CUF KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA KULE VISIWANI!!!!TUWAELEWEJE CCM?????????
  2. Mwaka jana 2010 wakti wa Uchaguzi Mkuu baada ya KUONA CDM WAMEKUJA NA NGUVU KUBWA WAKIONGOZWA NA DR.W.SLAA kama mgombea wa Urais CCM wakaanza tena PROPAGANDA ZILE ZILE ZA UDINI! Kuwa CDM NI CHAMA CHA KIDINI(UKRISTO) KWASABABU DR.SLAA alikuwa Padre kwa hiyo watu wasiipigie CDM kura. Huu ni UNAFIKI NA UONGO MKUBWA SANA UNAOFANYWA NA CCM KUJARIBU KUWAHADAA WA-TZ ILI WASIWEZE KUCHAGUA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI VYENYE MWELEKEO WA KUMKOMBOA MTANZANIA.
Kwa hiyo CCM wanataka kutuambia kuwa siku ambayo kutatokea Chama chenye mgomboe mpagani asiyekuwa na dini(kama alivyo Kingunge Ngombare Mwiru) CCM watadai kuwa WATU WASIJIUNGE NACHO MAANA NI CHAMA CHA KIPAGANI!!!!!!!!!!

Ama kweli CCM ni chama cha majuha watupu!!!Pambaf kabisa.


 
Mimi ni muislamu tena jina langu ni Mohamedi. Naipenda Chadema kuliko chama chochote tangu nimeanza kufuatilia siasa na kuwa mwanachama wa chama hicho.

Hawa wanaotoa majibu ya jumla ya kukihusisha chadema na propaganda chafu za udini eti waislamu wanaichukia chadema ni wajinga, wapumbavu na wavivu wa akili walio zama kwenye tope la upoyoyo na wanatengeza tatizo kwa waislam ambalo kwa muislamu yeyote mwenye mtima ulio timamu hawezi kuwasikiliza. Wanapokisema chadema kuwa ni cha wakristo mbona huwa hawatoi mbadala kuwa waislamu waende kwenye chama gani? Mufti anapopinga maandamano ya chadema yeye kwa fikra zake anajua kuwa waislamu wana hali nzuri kimaisha? Na kwa nini atusemee waislamu wote Tanzania juu ya mapenzi yetu kwa chama mtu anachokipenda? Mufti hakifikiri kwa niaba ya watanzania waislamu juu ya tukipendacho na lazima ajue JK hasakamwi kwa kuwa yeye ni muislamu bali kwa kushindwa kwake kiungozi na kuonyesha ombwe lililopelekea kujivua gamba.

Wavivu wa kufikiri na wanao ongozwa na mihemko ya udini kwa mtu ambae hawakuona udini wake alivyopambana bungeni na kutaja mafisadi wakristo na waislamu ni juha asiye ona kwa nini Slaa na chadema yake wanapaswa kuungwa mkono na mtanzania yeyote mpenda maendeleo.

Mjenzi wa udini tunamjua, binafsi kama muislamu naamini wapo waislamu wengine wenye mafungamano makubwa na watu wa dini nyingine hata kuoleana au kuwa ndugu wa damu, kwenye foleni ya maji hatuulizani dini zetu tuwamoja na tunashirikiane.
Niko tayari kupambana juu ya propaganda chafu za ccm juu ya udini, walisema cuf ni wadini leo wamegeukia chadema! Nyambafu.

Nyerere aliposema nchi inakosa wasomi akumanisha watu weliofika chuo au maprofesa kama wengi walivyomuelewa vibaya, ila alimanisha people who can think critically like you, big up.
 
Mzee Mwanakijiji,
Nadhani swali langu lilikuwa more rhetorical na kwa kwa kweli mzee mwenzangu sikulimaanisha hivyo ulivyouliza. Nilichosema kuwa tuseme Dr. Slaa amekutana na kundi la Waislamu - siyo kwamba akatae kukutana nao kabla ya kuzungumza kwa sababu ya kutofautiana. Tuseme Chadema kama chama ina msimamo kuhusu mambo mbalimbali. Dr. Slaa anaenda kukutana na jamii ya Waislamu na kusikiliza na kucompromise na kushindwa kucompromise mambo fulani kwa sababu ni position ya Chama - siyo position yake.

Huo msimamo wa chama ukaonekana kuwa hauwafurahishi kundi hilo la Waislamu kwani wanaona hautetei maslahi yao. Hapo anafanya nini? Point yangu ni kuwa kama kuna watu ambao wanaamini kuwa bila kupewa x, y basi mtu hakubaliki ni vigumu sana kuwaridhisha. Binafsi ningependa kujua kuwa ni compromise gani ambazo zinaweza kufanyika kuwaridhisha hawa waislamu wa kundi hili?
sijui kama nilikosea ktk majibu yangu hapo nyuma lakini nadhani nimesema hivi?.. Kujibu kwake maswali ya Waislaam kutaondoa dukuduku za hao wanaompiga vita kwa sababu atakuwa kasema ukweli wake.. Yeye anagombea uongozi na haya ndio anaweza kuyafanya na haya hawezi kuyafanya iwe msimamo wake au wa chama kwani ndani ya chama kimoja inawezekana wagombea wawili wakatofautiana pia juu ya swala hili.. Hii itawasaidia wengi Waislaam ndani ya Chadema kujua nini msimamo wa chama na upi msimamo wake yeye dhidi ya kina Mbowe, Zitto au mgombea mwingine yeyote wa kiti hicho...

Na sisemei kwamba ni lazima akubaliane na Waislaam kwani hata mimi sikubaliani na wanaharakati ktk baadhi ya madai yao na ninazo sababu za kutokubaliana nao.. Wapo Waislaam wanaoniunga mkono na wapo wasioniunga mkono ila ujumbe wa msimamo wangu uko wazi kabisa na why nakiunga mkono Chadema nje ya maswala ya dini..
Hili ndilo swali ambalo ni gumu wakati mwingine. Mtu anaposema "waislamu" huwa tunazungumza kama ni kundi moja linalofanana kwa kila kitu wakati mimi na wewe ni mashahidi kuwa ni kundi ambalo lina maslahi mengi zaidi ya yale ya "waislamu" tu. Kwanza ni kwa sababu hata ndani ya Uislamu wenyewe nchini si wote wanakubaliana - wale wa EAMWS (WARSHA) na wale wa BAKWATA N.K Kimsingi ni kuwa ili kuweza kuwafikia wengi zaidi itabidi akutane na makundi mbalimbali ya Waislamu unless Waislamu kwanza wakikaa pamoja na kuwa na msimamo mmoja. Hii inaelezea kwanini licha ya kukutana na viongozi wa Waislamu mwezi Septemba bado haikuridhisha kwa sababu labda hakukutana na wale ambao watu waliona anapaswa kukutana nao hasa.
Mkuu wangu hapa hakuna ugumu wowote kwani tunapozungumzia Wakristu tunazungumzia jumuiya yote ya Wakristu hata kama wanatofautiana ktk ibada zao isipokuwa hili ni swala la Waislaam wote kulingana na maagizo ya Kuran..Kukubaliana na kutokubaliana ni hulka ya binadamu hata katiba yenyewe sii mambo yote tunakubaliana ila tunatazama haki. kama kweli kuna haki ya Waislaam imepotea na wanayo haki ya kushiriki ktk maendeleo yao sidhani kama kunahitajika dhehebu na ndio maana hili swala la udini ukilitazama sana ni baina ya Waislaam Sunni na Katoliki lakini limejumuisha madhehebu yote toka pande mbili..
Mkandara, mimi naamini kabisa kuwa hata yale mambo ya "waislamu" yakikubaliwa - na mimi sina tatizo hata kidogo tutakuja kuona kuwa wala siyo matatizo hasa ya Waislamu, kwani matatizo yao ni laye yale ya watanzania - kama unavyosema mara nyingi. Kwa sababu kama ingekuwa ni matatizo ya kidini tu Misri kusingekuwa na mvurugano, wala Iran, wala Syria, wala Jordan, wala Tunisia kwa sababu kwa nchi hizo mfumo unaotawala si "mfumo Kristo". Binafsi natamani kwenye Katiba Mpya tuyaingize mambo yale ambayo yana maslahi kwa Waislamu na nadhani hapo yatalazimisha wote tuangalie mambo yanayotuhusu sote kwa pamoja.

Kwa sababu wakishapewa mahakama ya Kadhi
Wakishapewa kujiunga na OIC
Wakishapewa mashule yaliyotaifishwa
n.k

Kinabakia nini isipokuwa matatizo yale yale yanayowagusa wananchi wengine? Ndio maana wakati mwingine nafikiria kutotatua matatizo ya Waislamu ni mbinu ya CCM kuendelea kuwashikia waislamu kitu cha kuwabembelezea au kuwaringishia bila kuwapa.

Chadema upande mwingine walipoteza nafasi nzuri ya kuweza kupenya na kugusa mioyo ya Waislamu. Nakumbuka kuna mapendekezo kadhaa niliyatoa (privately) ambayo kama wangeyakubali kwenye Ilani yao na kuyasimamia yangegawanya kura za Waislamu lakini nadhani hawakuwa tayari kufanya hivyo.
Mkuu hapa umemaliza kabisa na ndivyo navyofikiria mimi kwa nini Chadema na Dr.Slaa wasitumie mwanya huu kujikombea masifa kwa kuwa wawazi.. Ila hilo la Mahakama ya kadhi mkuu wangu siko nawe kabisa kwa sababu mimi naamini dini haifundishi kuchukua baadhi ya sheria na kuzitumia ukaacha vipengele muhimu zaidi vinavyosababisha madhara hayo. Kuruhusu mahakama ya kadhi ni sawa na kugawa vyandarua vya mbu kupambana na Malaria, ukashindwa kudhibiti na kukomesha nazalio ya mbu wenyewe...

Kitu kimoja tu nimalizie kusema kwamba - Mimi binafsi madai mengi ya Waislaam sikubaliani nayo kabisa kwa sababu naamini adui wa Waislaam ni Waislaam wenyewe ndani ya chama CCM na Bakwata...
Mara nyingi hujiuliza hili la kuwepo Bakwata kikitumiwa na chama kuwadhibiti Waislaam kiaina, kina mahusiano zaidi na serikali kuliko waislaam wenyewe na mara nyingi sana kipo kisiasa zaidi ya kidini... WHY?
Hili swali hujiuliza sana na mara zote huwa sipati jibu kwani hata kama Waislaam hawakitaki bado serikali itashinikiza kuwepo kwake kama wawakilishi wa Waislaam - Why in the hell has it got to do with the Government.

Utafiti unatakiwa kufanyika na pengine Dr Slaa au Chadema wanaweza kuwa waokozi wa Waislaam Tanzania kwani haina mantiki kabisa chombo cha Waislaam kuwa cha kisiasa bdabi ya chama tawala ni kama vile Umoja wa Wanawake CCM au Umoja wa vijana CCM inatisha mkuu wangu....
 
Mkuu Mkandara,

Wazo lako ni zuri sana lakini bado napata tabu kuamini kuwa solution hii itafaa...

-Hakuna guarantee kama CDM wakiongea na waislamu basi watapata kuungwa mkono unless wakubaliane na matakwa yao.
-Kama tunakubaliana kuwa matatizo ya waislamu ni wao wenyewe na kwa kushirikiana na chama tawala then tuna uhakika gani kama CDM ndio wanaweza kuwa solution kwa kuzungumza nao?
-Tusisahau kwamba hii chuki dhidi ya CDM ni kwa sababu Rais aliyepo madarakani ni mwislamu lakini kama ingekuwa vinginevyo basi hakuna muislamu ambaye angekuwa anangaika kuponda CDM kuwa ni chama cha maaskofu! CCM wakimsimamisha mkristo hadithi ya BAKWATA itabadilika for sure.....

Mimi binafsi sioni suluhisho zaidi ya kuzidi kuwaelimisha watanzania na kuwaamsha kupambana na matatizo yanayowakabili bila kujali dini na makabila yao kwani at the end of the day matatizo hayabagui.
 
Mkitaka CHADEMA isahaulike, na upinzani upotee TZ muondoeni Dr. Slaa. Nami nawakimbia siku hiyo hiyo!
 
Mkitaka CHADEMA isahaulike, na upinzani upotee TZ muondoeni Dr. Slaa. Nami nawakimbia siku hiyo hiyo!

Duh, ww ndio hamnazo kabisa unafuata mtu au hoja ? kama ni hoja ina maana yoyote atakae kuwepo ! kama unafuata mtu hapo sawa
 
Mkuu Mkandara,

Wazo lako ni zuri sana lakini bado napata tabu kuamini kuwa solution hii itafaa...

-Hakuna guarantee kama CDM wakiongea na waislamu basi watapata kuungwa mkono unless wakubaliane na matakwa yao.
-Kama tunakubaliana kuwa matatizo ya waislamu ni wao wenyewe na kwa kushirikiana na chama tawala then tuna uhakika gani kama CDM ndio wanaweza kuwa solution kwa kuzungumza nao?
-Tusisahau kwamba hii chuki dhidi ya CDM ni kwa sababu Rais aliyepo madarakani ni mwislamu lakini kama ingekuwa vinginevyo basi hakuna muislamu ambaye angekuwa anangaika kuponda CDM kuwa ni chama cha maaskofu! CCM wakimsimamisha mkristo hadithi ya BAKWATA itabadilika for sure.....

Mimi binafsi sioni suluhisho zaidi ya kuzidi kuwaelimisha watanzania na kuwaamsha kupambana na matatizo yanayowakabili bila kujali dini na makabila yao kwani at the end of the day matatizo hayabagui.

CDM wajivue gamba la udini + ukabila, hilo ndilo linalotakiwa kufanywa, ni dhahiri wao wameisha jionyesha wako upande gani bana
 
Back
Top Bottom